MGAMBWA SADALA MCHIWA
- Citation
- MGAMBWA SADALA MCHIWA
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2024
- Posture
- Maombi Madogo Ya Jinai / Uamuzi Wa Maombi Ya Kuongezewa Muda Wa Kukata Rufaa
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2024
- Posture
- Maombi Madogo Ya Jinai / Uamuzi Wa Maombi Ya Kuongezewa Muda Wa Kukata Rufaa
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
The applicant demonstrated sufficient cause for delay, as he was in prison and dependent on prison officers for document preparation. The previous appeal was withdrawn due to defects. The court is satisfied that the reasons justify extension of time.
Court disposition
Application granted
Orders
- Applicant to file notice of intention to appeal within 10 days from the date of this ruling.
- Applicant to file appeal within 45 days from the date of this ruling.
02
Material facts
Parties
Mgambwa Sadala Mchiwa @ Mussa Sadala Mchiwa
Mleta MaombiJamhuri
Mjibu Maombi Counsel: Bi. Zubeda Lyaumi na Bi. Linda Mmbaga03
Procedural history
Posture
Maombi Madogo Ya Jinai / Uamuzi Wa Maombi Ya Kuongezewa Muda Wa Kukata Rufaa
04
Questions and positions
Legal issues
Whether the applicant has shown sufficient cause for extension of time to file notice of intention to appeal and appeal out of time
Party arguments
- Applicant
- Applicant relied on his affidavit and stated he was unable to file the appeal on time due to being in prison and dependent on prison officers for preparation of documents. The previous appeal was withdrawn due to procedural defects.
- Respondent
- State counsel supported the application, citing the applicant's dependence on prison authorities and the right to appeal as fundamental. The delay was justified by the circumstances outlined in the applicant's affidavit.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Section 361(2) of the Criminal Procedure Act [Cap 20 R.E. 2022]
Court may extend time to file appeal if sufficient cause is shown.
- 02
Karibu Textile Mills Limited v. Commissioner General, Tanzania Revenue Authority, Misc. Civil Application No. 192/20 of 2016, Court of Appeal of Tanzania (unreported)
Even if the application is unopposed, the court must be satisfied that sufficient cause exists.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
The applicant demonstrated sufficient cause for delay, as he was in prison and dependent on prison officers for document preparation. The previous appeal was withdrawn due to defects. The court is satisfied that the reasons justify extension of time.
Obiter and limits
- Right of appeal is fundamental and should be facilitated where justified.
Court disposition
Application granted
- Applicant to file notice of intention to appeal within 10 days from the date of this ruling.
- Applicant to file appeal within 45 days from the date of this ruling.
Source and reliance status
TANZLII · 1 January 2024
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 1 January 2024
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (MASIJALA NDOGO YA DODOMA)
ILIYOPO DODOMA MAOMBI MADOGO YA JINAI Na. 23808 YA 2024 (AsiHa shauri la Uhujumu Uchumi Namba 12 la 2023, Mahakama ya WHaya ya Manyoni)
MGAMBWA SADALA MCHIWA @ MUSSA SADALA MCHIWA........................................... MLETA MAOMBI
DHIDI YA JAMHURI........................................................................ MJIBU MAOMBI
UAMUZI Tarehe ya amri ya mwisho: 26/9/2024 Tarehe ya uamuzi: 30/9/2024 KHALFAN, J. Mgambwa Sadala Mchiwa, mleta maombi katika shauri hili, ameleta maombi haya chini ya kifungu cha 361(2) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai [Sura ya 20 marejeo ya mwaka 2022]. Mleta maombi anaomba mahakama hii imuongezee muda zaidi ili aweze kuleta taarifa ya nia ya kuleta rufaa na rufaa nje ya muda dhidi ya hukumu ya mahakama ya wilaya ya Manyoni katika shauri la Uhujumu Uchumi namba 12 la mwaka 2023. Maombi haya yameambatishwa na kiapo cha mleta maombi. i Maombi haya yalipoitishwa kwa ajili ya kusikilizwa, mleta maombi alifika na hakuwa na uwakilishi wowote. Upande wa mjibu maombi uliwakilishwa na Bi. Zubeda Lyaumi na Bi. Linda Mmbaga, mawakili wasomi wa serikali. Alipopewa nafasi ya kufanya mawasilisho yake, mleta maombi aliomba mahakama izingatie kiapo chake kama sehemu ya mawasilisho yake. Hakuwa na jambo la ziada la kuieleza mahakama. Kwa upande wake, Bi. Lyaumi, wakili msomi wa serikali, aliunga mkono maombi haya. Aliieleza mahakama kwamba mleta maombi ana sababu ya msingi ambayo imeainishwa katika aya ya nne (4) ya kiapo chake. Alieleza kwamba, baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo, mleta maombi alikata rufaa katika mahakama hii. Alieleza zaidi kwamba, rufaa hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kusikilizwa mleta maombi aliomba kuondoa rufaa yake kwa kuwa ilikuwa na mapungufu
kadhaa. Alieleza kwamba, rufaa ya mleta maombi iliondolewa tarehe 22/4/2024. Alieleza kwamba kwa kuwa mleta maombi yupo gerezani ambapo hutegemea zaidi maafisa wa magereza katika kuandaa nyaraka kumepelekea mleta maombi kushindwa kuleta rufaa yake kwa wakati. Wakili 2 msomi wa serikali alieleza kwamba, rufaa ni haki ya kila mmoja ambaye hajaridhika na maamuzi ya mahakama. Hivyo, ili haki iweze kutendeka, mleta maombi aruhusiwe kuleta rufaa yake. Baada ya kupitia majumuisho ya pande zote mbili katika maombi haya, jambo la msingi ni endapo mleta maombi ametoa sababu za msingi katika maombi haya. Ingawa maombi haya hayakupingwa na mjibu maombi, mahakama bado ina jukumu la kupima endapo mleta maombi ana sababu za msingi. Msimamo huu ulielezwa katika shauri la Karibu Textile Mills Limited dhidi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania maombi madogo ya Madai Na. 192/20 ya 2016 Mahakama ya Rufaa ya Tanzania iliyoketi Dar es Salaam (haijaripotiwa). Kama ilivyoelezwa hapo awali, maombi haya yameletwa chini ya kifungu cha 361(2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai. Kifungu hicho kinaipa mahakama hii mamlaka ya kuongeza muda wa kukata rufaa pale ambapo sababu za msingi zinakuwa zimetolewa. Katika maombi haya ambapo kimsingi yaliungwa mkono na wakili msomi wa serikali, ni kwamba mara baada ya uamuzi wa mahakama ya Wilaya kutolewa, mleta maombi alifungua rufaa katika mahakama
hii, lakini rufaa hiyo iliondolewa na mleta maombi baada ya kuwa na dosari kadhaa. Alieleza kwamba mleta maombi yupo gerezani ambapo anategemea mamlaka ya gereza imsaidie kuandaa nyaraka zake kwa ajili ya rufaa jambo lililopelekea kuchelewa kufungua rufaa yake. Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili pamoja na kiapo cha mleta maombi, ni wazi kwamba mleta maombi ameweza kuainisha sababu za msingi za kuchelewa kwake kufungua rufaa kwa wakati. Katika shauri hili, imeelezwa wazi kwamba mleta maombi alifungua rufaa yake katika mahakama hii lakini ilionekana kuwa na dosari na hivyo kuondolewa tarehe 22/4/2024. Hata hivyo, nimezingatia kwamba mleta maombi yupo gerezani kunakomfanya awe tegemezi kwa maafisa wa magereza kuandaa nyaraka zake za rufaa. Kwa sababu hiyo, mahakama inaona maombi haya yana mashiko hivyo inayakubali. Mleta maombi alete taarifa ya nia ya kukata rufaa ndani ya siku 10 na rufaa ndani ya siku 45 kuanzia tarehe ya uamuzi huu. Imeamriwa hivyo. Imetolewa Dodoma leo tarehe 30 Mwezi Septemba, 2024. F. R. KHALFAN
JAJI 30/9/2024 4
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.