eston gabriel na wenzake 6 vs nashera hotel 2021 tzhcld 150 3 juni 2021
- Citation
- eston gabriel na wenzake 6 vs nashera hotel 2021 tzhcld 150 3 juni 2021
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2021
- Posture
- Maombi Ya Marejeo / Hukumu Ya Mwisho
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2021
- Posture
- Maombi Ya Marejeo / Hukumu Ya Mwisho
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
Waleta maombi hawakuachishwa kazi bali mikataba yao ya ajira ilifika ukomo wa muda waliokubaliana. Hakukuwa na matarajio ya kawaida ya kuongezewa mikataba na waleta maombi hawakuendelea na kazi baada ya mikataba kuisha. Hivyo, hawastahili mafao yoyote ya kuachishwa kazi na uamuzi wa Tume ni sahihi.
Court disposition
Maombi ya marejeo yanatupiliwa mbali kwa kukosa mashiko.
Orders
- Uamuzi wa Tume unaendelea
- Kila upande ujigharamie gharama zake za kuendesha shauri hili
02
Material facts
Parties
Eston Gabriel na Wenzake 6
Waleta Maombi Counsel: Boniface BasesaNashera Hotel
Mjibu Maombi Counsel: Baraka LweyekaAmounts and remedies
- Kiasi Kilichodaiwa Na Waleta Maombi: TZS 52,000,000
03
Procedural history
Posture
Maombi Ya Marejeo / Hukumu Ya Mwisho
04
Questions and positions
Legal issues
- 01
Iwapo waleta maombi walikuwa na matarajio ya kuongezewa mikataba ya ajira
- 02
Iwapo waleta maombi waliachishwa kazi au mikataba yao ilifika ukomo
- 03
Nafuu zipi zinazostahili kwa kila upande
Party arguments
- Applicant
- Waleta maombi walikuwa na mikataba ya muda maalum lakini walipaswa kupewa mikataba ya kudumu kwa kuwa kazi zao ni endelevu na hawakuwa katika kada ya uongozi. Walidai kuwa waliondolewa kazini bila kufuata utaratibu na hawakulipwa mafao ya kuachishwa kazi. Pia walidai fidia ya milioni 52 kwa kuachishwa kazi isivyo halali.
- Respondent
- Mjibu maombi alieleza kuwa waleta maombi walikuwa na mikataba ya muda maalum iliyofika ukomo tarehe 30/04/2017 na walitaarifiwa mapema. Hakukuwa na matarajio ya kuongezewa mikataba na hakuna ushahidi wa madai ya fidia. Kisheria, mwajiri si lazima kufuata taratibu za kuachisha kazi pale mkataba wa muda maalum unapofikia ukomo.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Kanuni ya 4(2) na (3) ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini, GN No. 42/2007
Mikataba ya muda maalum inaisha yenyewe muda uliokubaliwa unapofika, isipokuwa kama mkataba unasema vinginevyo au kuna matarajio ya kawaida ya kuongezewa mkataba.
- 02
YARA Tanzania Limited dhidi ya Charles Aloyce Msemwa na Wenzake 2, Kesi ya Biashara Na. 5 la 2013
Wadaawa wanafungwa na nyaraka zao walizowasilisha mahakamani (pleadings) na hawawezi kuwasilisha hoja nje ya nyaraka hizo.
- 03
Kifungu cha 36(a)(iii) Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya 2019
Kusitishwa kwa ajira kunajumuisha kushindwa kuongeza mkataba wa kipindi maalumu kama kulikuwa na matarajio ya kawaida ya kuongeza mkataba.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
Waleta maombi hawakuachishwa kazi bali mikataba yao ya ajira ilifika ukomo wa muda waliokubaliana. Hakukuwa na matarajio ya kawaida ya kuongezewa mikataba na waleta maombi hawakuendelea na kazi baada ya mikataba kuisha. Hivyo, hawastahili mafao yoyote ya kuachishwa kazi na uamuzi wa Tume ni sahihi.
Obiter and limits
- Hoja ya waleta maombi kupewa mikataba ya kudumu haikuwa sehemu ya hoja zilizowasilishwa kwenye kiapo chao wala mbele ya Tume, hivyo haiwezi kuzingatiwa.
Court disposition
Maombi ya marejeo yanatupiliwa mbali kwa kukosa mashiko.
- Uamuzi wa Tume unaendelea
- Kila upande ujigharamie gharama zake za kuendesha shauri hili
Source and reliance status
TANZLII · 1 January 2021
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 1 January 2021
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
DIVISHENI YA KAZI
ILIYOKETI MOROGORO MAOMBI YA MAREJEO NA. 50 YA 2019
BAINA YA ESTON GABRIEL NA WENZAKE 6............................................. WALETA MAOMBI NA NASHERA HOTEL............................................................................MJIBU MAOMBI
HUKUMU Tarehe ya mwisho ya Amri: 20/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 03/06/2021 A. E. MWIPOPO, J. ESTON GABRIEL, ARNOLD EMMANUEL, MARIAM GILBERT, MOSHI ABDALLAH, RASHID JUMANNE, KAMBI SAID na MARIA TESHA ambao ni Waleta Maombi katika shauri hili la Marejeo wamewasilisha shauri hili wakiomba Mahakama irekebishe Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi uliotolewa katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/88/17 wa Tarehe 29/10/ 2019. Waleta Maombi wanaomba yafuatayo: 1. Mahakama hii ikipendezwa iitishe kumbukumbu za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa ajili ya kurekebisha Tuzo ya Tume iliyotolewa Tarehe 29/10/2019 na Mh. Kayugwa, H, Muamuzi, ambayo Waleta Maombi waliipokea siku hiyo hiyo. i 2. Mahakama hii ikipendezwa itoe Amri ya kufuta Tuzo ya Tume kwa kuwa Muamuzi alikiuka Mamlaka yake ya kisheria na kulikuwa na makosa katika tuzo hiyo.
3. Nafuu yoyote ambayo Mahakama itapendezwa kutoa. Shauri hili lilikuwa linaungwa mkono na kiapo cha pamoja cha Waleta Maombi ambapo katika aya ya 6 ya kiapo walikuwa na hoja nne za kisheria zinazotokana na ushahidi. Hoja hizo ni kama zifuatazo:- i. Kwamba Muamuzi alikosea kisheria kuona kuwa Waleta Maombi hawakuachishwa kazi na Mjibu Maombi ila mikataba yao ilifika ukomo wa muda wakati baadhi ya Waleta Maombi hawakuwa na mikataba iliyoandikwa. ii. Kwamba Tuzo ya Tume ilitolewa kinyume na mamlaka ya Tume na ilikuwa na makosa. iii. Kwamba Muamuzi alikosea kushindwa kuzingatia kuwa Waleta Maombi waliachishwa kazi na Mjibu Maombi na kuwa hawakulipwa mafao ya kuachishwa kazi. iv. Kwamba Muamuzi alikosea kisheria kuwa kushindwa kuzingatia ushahidi uliotolewa na Waleta Maombi. Historia fupi ya shauri hili ni kuwa Waleta Maombi waliajiriwa na Mjibu Maombi katika nafasi mbalimbali na kwa Tarehe tofauti kuanzia 2 mwaka 2011 mpaka mwaka 2015 kwa mikataba ya muda maalum. Mnamo tarehe 30/04/2017 ajira ya Waleta Maombi ilifika ukomo na Mjibu Maombi aliwataarifu kuwa mikataba hiyo haitaongezwa kwa sababu ya muanguko wa kiuchumi (Financial crisses). Waleta Maombi hawakuridhika na uamuzi huo wa Mjibu Maombi, hivyo walifikisha mgogoro wao mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (hapa itajulikana kama Tume). Katika Uamuzi wake, Tume iliona kuwa mikataba ya Waleta Maombi ilifikia ukomo na
hivyo hawakuachishwa kazi. Waleta Maombi hawakuridhika na uamuzi wa Tume jambo lilopelekea kufunguliwa kwa shauri hili la marejeo hapa Mahakamani. Katika shauri hili, pande zote mbili zilikuwa zinawakilishwa ambapo Waleta Maombi waliwakilishwa na Bw. Boniface Basesa, Mwakilishi Binafsi, na Mjibu Maombi alikuwa anawakilishwa na Bw. Baraka Lweyeka, Wakili. Akifanya mawasilisho ya kuunga mkono marejeo, Mwakilishi wa Waleta Maombi alieleza kuwa Waleta Maombi walikuwa na Mkataba wa kazi wa mwaka mmoja mmoja, hivyo walikuwa na mkataba wa muda maalum. Waleta Maombi walitakiwa kupewa mkataba wa kudumu kwa sababu Waleta Maombi hawakuwa katika kada ya uongozi. Waleta Maombi walikuwa wameajiriwa katika nafasi za kutunza bustani, Mhasibu Msaidizi (Cashier), Mpishi na Uhudumu. Hivyo waleta maombi walitakuwa kupewa 3 mkataba wa kudumu lakini Tume haikukubaliani na hili. Kazi ya hoteli ni kazi endelevu na sio ya msimu hivyo Waleta Maombi walipaswa wapewe mikataba wa kudumu. Mwakilishi Binafsi aliendelea kueleza kuwa barua ya taarifa ya kutoongeza mkataba iliwataarifu kuwa sababu ya kuwaachisha kazi ni kuwa kipato cha Mjibu Maombi kimepungua. Lakini hakuna uthibisho uliotolewa kuhusu kupungua kwa kipato cha Mjibu Maombi. Katika ushahidi wake, shahidi wa Mjibu Maombi ambaye ni DW1 alieleza kuwa mikataba ya Waleta Maombi ilifika ukomo. Hii inaleta kupingana kwa maelezo ya Mjibu Maombi iwapo
sababu ya kuwaachisha kazi au kutoongezewa mikataba Waleta Maombi ni kupungua kwa kipato au kufikia ukomo kwa mikataba. Akiendelea na Mawasilisho, Mwakilishi wa Waleta Maombi alieleza kuwa hakuna utaratibu wowote uliofuatwa wa kupunguzwa kazi kwa Waleta Maombi. Chama cha Wafanyakazi na waleta maombi hawakushirikishwa katika upunguzwaji huo. Mwakilishi alieleza ingawa katika fomu Na. 1 ya CMA Waleta Maombi hawakueleza mchanganuo wa maombi yao ya kulipwa milioni 26, lakini katika ushahidi wao walionesha kuwa madai yao ni milioni 52. Ushahidi huu hawakupingwa na Mjibu Maombi lakini tume haikutoa malipo hayo kwa 4 Waleta Maombi. Hivyo, Tume ilijielekeza vibaya kuona kuwa hakukuwa na mchanganuo wa madai ya Waleta Maombi. Hivyo, Mwakilishi wa Waleta Maombi aliomba Uamuzi wa Tume utupiliwe mbali kwa sababu Mjibu Maombi ameshindwa kuthibitisha kama uachishwaji kazi ulikuwa halali na Waleta Maombi walipwe milioni 52 kama fidia ya kuachishwa kazi isivyo halali. Akijibu mawasilisho ya Waleta Maombi, Wakili wa Mjibu Maombi alieleza kwa mawasilisho ya Waleta Maombi ambayo hayaendani na kiapo chao, hivyo aliomba mawasilisho hayo yasizingatiwe. Wakili alieleza kuwa Waleta Maombi walikuwa wameajiriwa kwa kipindi maalum na mikataba yao ya mwisho iliisha tarehe 30/04/2017. Kielelezo PD2 - kilikuwa ni barua za kuwataarifu kuwa mikataba inaisha kama kichwa cha barua hivyo kinavyoonesha. Kwa mujibu
wa Kanuni ya 4(2) ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007, mkataba wa kipindi Maalum unaisha pale muda maalum wa mkataba utakapoishia. Mikataba hiyo ilipokelewa kama kielelezo DI na vifungu vya mikataba vinaeleza kuhusu ukomo wa muda wa mikataba pamoja na utaratibu wa kuhuisha mikataba. Mtu anayetaka kuongeza mkataba ulitakiwa kutoa taarifa ya miezi miwili kabla ya mkataba husika 5 kuisha. Mjibu Maombi hajawahi kupokea taarifa ya kutaka kuhuisha mikataba toka kwa Waleta Maombi. Katika kuunga mkono hoja yake Wakili wa Mjibu Maombi alirejea kesi ya Rosanistika Siwema dhidi ya ADD International Tanzania, Marejeo Na. 498 ya 2019, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyoketi Dar Es Salaam, ambapo Mahakamani iliona kuwa pale mkataba wa kipindi maalumu ukifikia mwisho mwajiri hawajibiki kufuata taratibu za kumwachisha kazi mwajiriwa. Aidha katika kesi ya Doto Shabani Kuingwa dhidi ya CSI Engineering Company Ltd, Marejeo Na. 5 ya 2020, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyoketi Dar Es Salaam, Mahakama iliona kuwa mkataba wa kipindi maalum huwa unafikia ukomo pale tarehe ya mwisho wa mkataba itakapofika labda mkataba uwe unasema vinginevyo. Wakili alieleza ya kwamba masharti ya Mkataba wa ajira yanatakiwa yaheshimiwe kutoa sababu za kutongeza mkataba hakuleti athari yoyote. Habari za kuwa alipunguzwa kazini hazipo katika
ushahidi. Kifungu cha 36 cha Sheria cha Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 ya 2019 hakihusiani na mtu ambaye mkataba wake umefikia ukomo. Kuhusu madai ya milioni 26, Wakili wa Mjibu Maombi alieleza kuwa madai hayo hayakuwa na ushahidi wa kuyathibitisha. Pia Mjibu Maombi 6 hakuwa na wajibu wa kueleza kwa Waleta Maombi kuwa uchumi wake umepungua. Kwa sababu hiyo, Wakili alieleza kuwa maamuzi ya Tume yalikuwa sahihi na maombi haya ya marejeo yatupiliwe mbali. Akifanya mawasilisho ya nyongeza Mleta Mombi amerudia maelezo yake katika mawasilisho ya msingi (submission in chief). Baada ya kupokea mawasilisho ya pande zote mbili nimeona kuwa kuna haja ya kuongelea wasilisho la Wakili wa Mjibu Maombi kuwa mawasilisho ya Mwakilishi Binafsi wa Waleta Maombi yasizingatiwe kwa sababu amewasilisha maelezo ambayo hayaendani na kiapo chao. Nimeangalia mawasilisho hayo ya Waleta Maombi na kuona kuwa hoja waliyowasilisha kuwa walitakiwa kupewa mkataba wa kudumu kwa sababu hawakuwa katika kada ya uongozi na kuwa kazi ya hoteli ni kazi endelevu sio sehemu ya hoja za Waleta Maombi katika kiapo chao. Wadaawa huwa wanafungwa na nyaraka zao walizowasilisha Mahakamani (pleadings). Katika kesi ya YARA Tanzania Limited dhidi ya Charles Aloyce Msemwa na Wenzake 2, Kesi ya Biashara Na. 5 la 2013, Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, iliyokaa Dar Es Salaam, Mahakama ilieleza kwamba ni msimamo wa
kisheria kuwa wadaawa wanafungwa na nyaraka zao (pleadings) na hakuna mdaawa anayeruhusiwa kuwasilisha kesi yake kinyume na nyaraka alizowasilisha. 7 Aidha, hoja hiyo ya Waleta Maombi kupewa mikataba ya kudumu haikuwa mojawapo ya hoja zilizokuwa zinabishaniwa mbele ya Tume. Rekodi ya Tume inaonesha katika ukurasa wa 11 wa mwenendo uliochapwa wa Tume kuwa mojawapo ya hoja ambazo hazibishaniwi ni kwamba walalamikaji mbele ya Tume waliajiriwa kwa masharti ya mikataba ya muda maalum. Hivyo, Waleta Maombi wamekosea kuwasilisha hoja hiyo katika mawasilisho yao na hivyo sitaizingatia. Kwahiyo, hoja zinazobishaniwa ambazo zimebaki na Mahakama inatakiwa izitolee uamuzi ni mbili. Hoja hizo ni kama zifuatazo;- i) Iwapo kulikuwa na matarajio ya kuongezwa kwa muda wa mikataba ya ajira ya Waleta Maombi. ii) Ni nafuu zipi zinazostahili kwa kila upande? Kwa kuanza na hoja ya kwanza kama kulikuwapo na matarajio ya kawaida kwa waleta maombi kupatiwa mikataba mingine ya ajira, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya Sheria, kama Ilivyorejewa mwaka 2019, inaeleza katika kifungu cha 36(a) (iii) kuwa kusitishwa kwa ajira kunajumuisha kushindwa kuongeza mkataba wa kipindi maalumu katika masharti yaleyale au yanayofanana nayo kama kulikuwa na matarajio ya kawaida ya kuongeza mkataba. Kifungu hicho kinasomwa pamoja na Kanuni ya 4(2) na (3) ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini 8 (Kanuni za
Utendaji Bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007 ambayo inaeleza kuwa, nanukuu:- "4(2) Pale ambapo mkataba utakuwa wa muda maalum, mkataba utakoma wenyewe wakati muda uliokubaliwa utakapoisha isipokuwa kama mkataba utaeleza vinginevyo. (3) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (2), mkataba wa muda maalum unaweza kuongezwa kwa matarajio kwamba mwajiriwa ataendelea kufanya kazi baada ya kukoma kwa mkataba wa muda maalum na mazingira yakiwa yanaruhusu kufanya hivyo." Hivyo, ill kuwe na matarajio ya kuongezwa kwa mkataba wa ajira wa muda maalum baada ya muda uliokubaliwa kuisha inatakiwa mkataba wenyewe useme hivyo au kwa mwajiriwa kuendelea kufanya kazi baada ya kukoma kwa mkataba huo. Katika maombi haya, Waleta Maombi walidai ya kwamba walikuwa na mikataba ya muda maalum hivyo walitegema kupatiwa mikataba ya kudumu kwa kuwa ajira zao zilikuwa za kudumu na sio za muda mfupi. Kwa upande mwingine Mjibu Maombi alieleza mikataba ilikuwa ni ya muda maalum hivyo ilikoma pale muda wake ulipokwisha. Mahakama hii baada ya kupitia kumbukumbu za Tume pamoja na mawasilisho ya pande zote mbili inaona kuwa hakuna ubishi ya kwamba Waleta Maombi walikuwa na mikataba ya muda maalumu kama inavyoungwa mkono na kielelezo DD1 - mikataba ya muda maalum. Ushahidi wa barua za kutoongeza mikataba - 9 kielelezo DD3 inaonesha kuwa Mjibu Maombi alitoa taarifa ya kutohuisha mikataba. Sababu ya kutoongeza mikataba
hiyo ni kutokana na changamoto ya biashara. Katika kesi ya Brenda Kasanda Ndassi dhidi ya Makafuli Motors Ltd, Marejeo. Na. 25 ya 2011, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyokaa Dar Es Salaam (haijaripotiwa), Mahakama ilikuwa na maoni kwamba mwajiri na mwajiriwa wanaongozwa na masharti waliyokubaliana yanayoongoza ajira. Na kuwa itakuwa ni hali ya vurugu iwapo waajiriwa na waajiri wataachwa huru kufanya kama wanavyopenda kuhusiana na masuala ya ajira. Katika shauri hili mikataba ya ajira - kielelezo DD1 na barua za kuongeza muda wa mikataba - kielelezo DD2 zinaonesha kuwa muda wa mikataba unaisha tarehe 30 Aprili, 2017. Pia Mjibu Maombi alitoa taarifa ya kutoongeza mikataba kama kielelezo DD3 kinavyoonesha. Hii iliondoa matarajio ya Waleta Maombi kuongezwa mikataba yao ya ajira baada ya muda wa mikataba kuisha. Aidha, ushahidi unaonesha kuwa Waleta Maombi hawakuendelea na kazi baada ya muda wao wa mikataba kuisha. Hivyo ni maoni yangu kuwa Waleta Maombi hawakuachishwa kazi bali mikataba yao ya ajira ilifika ukomo wa muda. Kwa sababu hiyo nakubaliana na Tume kuwa Waleta Maombi hawakuachishwa kazi na Mjibu Maombi. io Hoja ya mwisho ni nafuu zipi zinazostahili kwa kila upande? Katika mazingira haya ambapo mikataba ya ajira ya Waleta Maombi imekwisha yenyewe kutokana muda waliokubaliana kuisha ni wazi kuwa hawastahili kulipwa mafao yoyote ya kuachishwa kazi. Hivyo naona Uamuzi wa Tume ni sahihi na natupilia mbali (dismiss) shauri hili la marejeo kwa kukosa mashiko. Uamuzi wa Tume unaendelea. Kila upande unatakiwa ujigharamie gharama zake za kuendesha shauri hili. 03/06/2021 11
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.