Bank ya Posta Tanzania Ltd Another vs Lameck Orgenes Lymo
The court found that the statutory notices required by law were duly served on the respondent, and the sale price was not below 25% of the market value. The tribunal erred in its evaluation of the evidence and misapplied the law regarding valuation and notice. The appeal was allowed, and the sale of the mortgaged...
Source-derived case information.
- Citation
- Bank ya Posta Tanzania Ltd Another vs Lameck Orgenes Lymo
- Parties
- Appellant: Benki ya Posta Tanzania; Appellant: Tulvin Investment (T) Ltd; Respondent: Lameck Orgenes Lymo; Respondent: Miraji Nyalandu
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2016
- Procedural Posture
- Land Appeal / Judgment on Appeal
- Outcome
- Appeal allowed
- Legal Topics
- Mortgage Enforcement, Auction Procedure, Notice Requirements, Valuation of Security, Appeal Procedure
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Benki ya Posta Tanzania
Appellant
Tulvin Investment (T) Ltd
Appellant
Lameck Orgenes Lymo
Respondent
Miraji Nyalandu
Respondent
Procedural Posture
Land Appeal / Judgment on Appeal
Legal Issues
- 1 Whether proper statutory notices were served before auction of mortgaged property
- 2 Whether the sale of the mortgaged property was conducted below market value in violation of the law
- 3 Whether the trial tribunal properly evaluated the evidence
Ratio Decidendi
The court found that the statutory notices required by law were duly served on the respondent, and the sale price was not below 25% of the market value. The tribunal erred in its evaluation of the evidence and misapplied the law regarding valuation and notice. The appeal was allowed, and the sale of the mortgaged property was upheld as lawful.
Court Disposition
Appeal allowed
Orders
- Decision of the District Land and Housing Tribunal set aside
- Sale of the mortgaged property upheld as lawful
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (MASIJALA NDOGO YA DODOMA) ILIYOPO DODOMA RUFAA YA ARDHI NO. 47 YA 2023 (AsHia shauri la Ardhi Na. 59 la 2017 Baraza la Ardhi na Nyumba la WHaya ya Singida) BENKI YA POSTA TANZANIA................................................. MRUFANI WA 1 TULVIN INVESTMENT (T) LTD............................................... MRUFANI WA 2 DHIDIYA LAMECK ORGENES LYMO.............................................. MRUFANIWA WA 1 MIRAJI NYALANDU......................................................... MRUFANIWA WA 2 HUKUMU Tarehe ya Amri ya mwisho: 30/7/2024 Tarehe ya Hukumu: 30/9/2024. KHALFAN, J. Lameck Orgenes Lymo, ambaye ni mrufaniwa wa kwanza, alifungua shauri katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Singida, akiomba stahiki kadhaa ikiwemo tamko la uuzwaji wa kipande cha ardhi, kiwanja namba 760 kitalu "S" kilichopo mtaa wa Minga Manispaa ya Singida (itarejewa kama ardhi yenye mgogoro) uliofanywa na mrufani wa 2 kwenda kwa mrufaniwa wa 2 ni batili, mrufaniwa wa 2 azuiwe kuendeleza ardhi yenye mgogoro, mrufaniwa wa 1 apewe muda wa kulipa salio la mkopo pamoja na gharama za shaurl. Kwa kifupi, kwa mujibu wa kumbukumbu za baraza, hakuna ubishi kwamba mnamo mwezi Machi 2016, mrufaniwa wa 1 aliomba na kupatiwa mkopo kutoka kwa mrufani wa 1 kiasi cha Tsh milioni 7 ambapo ardhi yenye mgogoro iliwekwa kama dhamana ya mkopo. Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo, mrufaniwa wa 1 alipaswa kurejesha kiasi cha shilingi 711,700/= kila mwezi mpaka pale ambapo mkopo wote utakapomalizika. Mrufaniwa wa 1 hakuweza kutekeleza wajibu wake wa kulipa mkopo husika jambo lililopelekea mrufani wa kwanza kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa mkataba wa mkopo ambapo ardhi yenye mgogoro iliuzwa kwa mrufaniwa wa 2 Hi kulipa deni la mkopo ambalo mrufaniwa wa 1 alikuwa akidaiwa. Katika hati ya utetezi iliyowasilishwa baraza la ardhi, mrufani wa 1 alidai kwamba taratibu zote za kuuza ardhi yenye mgogoro ambayo iliwekwa kama dhamana zilifuatwa ikiwa ni pamoja na kutoa notisi kwa mrufaniwa wa 1 ambaye hakulipa deni na hivyo kupelekea mrufani wa 2 kuuza ardhi husika kwa mnada wa hadhara ambayo ilinunuliwa na mrufaniwa wa 2. 2 Baada ya kusikiliza shauri pande zote, baraza lilijiridhisha kwamba uuzwaji wa ardhi ycnye mgogoro ulikuwa batili kwani haukufuata taratibu. Hivyo iliamuriwa kwamba mrufaniwa wa 1 aendelea kuwa mmiliki wa ardhi yenye mgogoro, mrufaniwa wa 1 alipe mkopo uliobakia kwa mrufani wa 1, mrufaniwa wa 2 arudishiwe kiasi cha pesa shilingi 6,500,000/=kutoka kwa mrufani wa 1 na mrufaniwa wa 1 alipwe gharama za shauri na mrufani wa 1. Mrufani wa 1 hakuridhika na uamuzi wa baraza. Hivyo, alifungua rufaa hii akiainisha sababu 2 kama ifuatavyo: 1. Kwamba mwenyekiti hakutathmini kwa umakini ushahidi uliotolewa. 2. Kwamba baraza HHkosea kusikiliza shauri biia kuwa na mam/aka kinyume cha sheria ya Mashauri ya Serikaii [sura ya 5 rejeo ia mwaka 2019]. Wakati rufaa hii ilipoitishwa kwa kusikilizwa, warufani waliwakilishwa na Bw. Emmanuel Mwakyembe, wakili msomi wa serikaii. Mrufaniwa wa 1 alijiwakilisha mwenyewe, mrufaniwa wa 2 hakutokea ingawa alipelekewa wito. Rufaa hii ilisikilizwa kwa njia ya maandishi. Katika hoja zake za maandishi, Bw. Mwakyembe aliomba kuondoa sababu ya pili ya rufaa. Akifafanua sababu ya kwanza ya rufaa, Bw. 3 Mwakyembe alieleza kwamba baraza lilishindwa kuchambua ushahidi uliotolewa. Alieleza kwamba baraza lilipotoka lilipoamua kwamba ardhi yenye mgogoro iliuzwa chini ya bei ya soko na kinyume cha kifungu cha 133(2) na kwa kuzingatia kielelezo Namba 4 ambacho ni hati ya kuthaminisha kiwanja iliyoonesha kwamba ardhi yenye mgogoro ilikuwa na thamani ya shilingi milioni 20. Alifanunua zaidi kwamba hakukuwa na ushahidi uliotolewa na mrufaniwa wa 1 kuonesha thamani ya sasa ya eneo la mgogoro kuthibitisha kwamba ardhi yenye mgogoro ilikuwa na thamani ya shilingi milioni 20. Alieleza kwamba baraza lilipotoka katika kutumia hati ya kuthaminisha eneo kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya uthaminishaji na usajili wa wathaminishaji. Alirejea shauri la mahakama hii la Access Bank Tanzania dhidi ya Mkandala Gabriel Mkandala na mwenzake, Rufaa ya Ardhi Namba 10 ya 2022. Bw. Mwakyembe alieleza zaidi kwamba baraza halikuzingatia ushahidi wa warufani kwamba katika mnada kilichouzwa ni kiwanja pekee na siyo mali nyingine kama ambavyo ilidaiwa na mrufaniwa wa 1. Alieleza zaidi kwamba hakukuwa na ushahidi wowote uliowasilishwa na mrufaniwa wa 1 kuonesha kama kulikuwa na maendelezo yeyote yaliyofanyika katika eneo la mgogoro. 4 Alifanunua zaidi kwamba baraza lilikosea lilipotamka kwamba mrufaniwa wa 1 hakupcwa notisi ya siku 60 na wala hakupewa notisi ya siku 14. Wakili alieleza kwamba SU2 alitoa ushahidi pamoja na vielelezo kuthibitisha kwamba mrufaniwa wa 1 alipcwa notisi ya kwanza mnamo tarehe 29/10/2016, kisha akapewa notisi ya pili 3/11/2016 na mnamo tarehe 19/12/2016, mrufaniwa wa 1 alipewa notisi ya siku 60 ambapo notisi hizo zilitolewa kama kielelezo DI. Bw. Mwakyembe pia alieleza kwamba warufani waliweza kuthibitisha kwamba mrufaniwa wa 1 alipewa notisi zote na hakutimiza wajibu wake wa kulipa deni husika. Aidha, wakili msomi alieleza kwamba baada ya kupewa notisi ya siku 60, mrufaniwa wa 1 alipewa notisi ya siku 14 ambayo ilitangazwa katika gazeti la Habari Leo la tarehe 14/5/2017 ambalo lilitolewa kama kielelezo D2. Kwamba baada ya notisi zote hizo, mrufaniwa wa 1 hakutimiza masharti ya mkopo kulikopelekea mrufani wa 2 kufanya mnada mnamo tarehe 21/5/2017 ambapo mrufaniwa wa 2 ndiye aliyeibuka mshindi wa mnada. Alifafanua kwamba ni msingi wa sheria kuwa pale ambapo mkopeshaji anapotekeleza mamlaka yake ya kuuza dhamana ya mkopo, mdai lazima athibitishe kwamba mnada uligubikwa na rushwa au hila la sivyo mahakama hairuhusiwi kuingilia uuzwaji wa dhamana ya mkopo. Alirejea uamuzi katika 5 shauri la Dcnki ya taifa ya Biashara dhldi ya Dar es Salaam Education & Stationery [1995] TLR 272. Bw. Mwakiyembe aliwasilisha kwamba mrufaniwa wa 2 alinunua ardhi yenye mgogoro bila hila na hivyo baraza lilipaswa kutamka kwamba mrufaniwa wa 2 ni mmiliki halali wa ardhi yenye mgogoro. Alirejea uamuzi katika shauri la Stanley Kalama Masiki dhidi ya Chihiyo Kuisia Nderingo Ngomuo [1981] TLR 143. Alitaka mahakama hii ambayo inasikiliza rufaa ya kwanza kuchambua na kuzingatia ushahidi uliotolewa. Wakili msomi alihitimisha kwa kuiomba mahakama itambue kuwa mnada ulifanyika kwa kufuata taratibu zote. Katika majibu yake, mrufaniwa wa 1 alieleza kwamba mwenyekiti wa baraza alichambua ushahidi uliotolewa kwa usahihi na alizingatia fomu ya uthaminishaji dhamana katika kuamua endapo ardhi yenye mgogoro iliuzwa katika bei halali. Mrufaniwa wa 1 alieleza kwamba kilichouzwa ni msingi wa vyumba 6 na tofali 5000 na kwamba mrufaniwa wa 2 alieleza kwamba alinunua zaidi ya ardhi. Mrufaniwa wa 1 aliongeza kwamba kwa mujibu wa kielelezo D2, vitu ambavyo vingeuzwa ni kiwanja pamoja na bidhaa za dukani. Hivyo, 6 haukuhitajika ushahldi wa zlada kuonesha kwamba kilichouzwa ni zaidi ya ardhi ycnyc mgogoro. Mrufaniwa wa 1 alidai kwamba baraza lilijiridhisha kwamba hakukuwa na notisi ya siku 14 wala notisi ya siku 60 zilizoeleza uuzwaji wa ardhi yenye mgogoro. Alirejea kifungu cha 132 (2) cha Sheria ya Ardhi ambacho kinaeleza kwamba endapo dhamana itauzwa kwa bei chini ya 25% basi mahakama inaweza kutengua mnada kama ambavyo ilifanyika katika shauri hili ambapo ardhi yenye mgogoro iliuzwa chini ya bei ya soko. Mrufaniwa wa 1 aliomba mahakama itamke kwamba notisi zote zilizotolewa na warufani kama vielelezo zilikuwa ni batili na hazikuzingatia sheria. Baada ya kupitia hoja za warufani na kumbukumbu za baraza, Mahakama ina jambo moja la kutatua ambalo ni kama baraza lilizingatia ushahidi uliotolewa na wadaawa ambapo kimsingi ndiyo hoja katika sababu ya kwanza ya rufaa hii. Katika uamuzi wake, mwenyekiti wa baraza alieleza katika ukurasa wa 5 kwamba ardhi yenye mgogoro ilikuwa na thamani ya shilingi milioni 20 kwa kuzingatia kielelezo D4 ambacho ni hati ya kudhaminisha ardhi yenye mgogoro. Baraza lilieleza zaidi kwamba wakati wa mauzo ya ardhi kulikuwa 7 /4 na tofali 5000 ambazo thamanl yakc ni shilingi 5,000,000 pamoja na msingi wa vyumba sita ambavyo vyote kwa pamoja viliuzwa kwa shilingi 6,500,000/=. Lakini pia baraza lilieleza wazi kwamba hakukuwa na notisi ya siku 60 iliyotolewa kwa mrufaniwa wa 1 wala notisi ya siku 14 kabla ya kufanywa kwa mnada. Nitaanza na madai ya kutokuwepo kwa notisi iliyotolewa kwa mrufaniwa kabla ya mauzo ya ardhi yenye mgogoro kuuzwa. Katika ushahidi wake alioutoa mbele ya baraza, mrufaniwa wa 1 anakiri kushindwa kulipa mkopo na kisha alipatiwa notisi ambazo alisaini mnamo tarehe 17/5/2017. Katika ushahidi wake, SU2 wa mrufani wa 1 alitoa notisi kadhaa ambapo mrufani wa 1 alikiri kupokea notisi ya tarehe 19/12/2016 ambayo ilipokelewa kama kielelezo DI. Nimepitia notisi ya tarehe 19/12/2016 na kubaini kwamba ni notisi ya siku 60 ikimtaka mrufaniwa wa 1 kulipa deni lote ndani ya siku 60 kuanzia tarehe ya kupokea notisi husika. Hivyo, ni wazi kwamba mrufaniwa wa 1 alipewa notisi ya siku 60 na mwenyewe alikiri kupokea notisi husika. Hivyo, baraza halikuzingatia kipande hiki cha ushahidi ambacho kipo wazi. Endapo baraza lingezingatia kipande 8 hiki, lingekuwa na hitimisho kwamba mrufaniwa wa 1 alipewa notisi ya siku 60. Pia, baraza lilifikia hitimisho kwamba mrufani wa 1 hakutoa notisi ya siku 14 kabla ya mnada kufanyika. Mahakama hii haikubaliani na baraza kwa hitimisho hili kwani ushahidi upo wazi kwamba mrufani wa 1 alitoa notisi kupitia gazeti la Habari leo la tarehe 4/5/2017 ambalo lilipokelewa kama kielelezo D2. SU2 alitoa ushahidi wake kwamba baada ya tangazo kutolewa kwenye gazeti, mrufani wa 2 alifanya matangazo kwa siku 4 na kisha mnada ukafanyika tarehe 21/5/2017. Hivyo hakuna shaka kwa ushahidi uliotolewa kwamba notisi zote mbili zilitolewa kwa mujibu wa sheria. Suala la pili ni kwamba endapo ardhi yenye mgororo iliuzwa chini ya bei ya soko. Kama nilivyoeleza hapo awali, baraza lilifikia hitimisho kwamba ardhi yenye mgogoro iliuzwa chini ya bei ya soko kwa sababu nilizoeleza hapojuu. Mahakama hii imepitia kwa umakini fomu ya madai iliyowasilishwa katika baraza na mrufaniwa wa 1. Kwanza kabisa mrufaniwa wa 1 alieleza kwamba ardhi yenye mgogoro ina thamani ya shilingi milioni kumi. Lakini jambo la pili mrufaniwa wa 1 hakusema endapo katika eneo lenye mgogoro kulikuwa na tofali 5000 wala msingi wa vyumba sita. Hivyo, katika ushahidi 9 wake, mrufaniwa wa 1 alipodai kwamba kulikuwa na tofali 5000 ambazo thamani yake ilikuwa ni shilingi 5000,000/= hakukuwa na ushahidi wowote. Hata alipohojiwa juu ya madai ya msingi na tofali, mrufaniwa wa 1 alieleza, na nanukuu: "...sina risitiza gharama ya tofalina msingi..." Hivyo, kwa kipande cha ushahidi hapo juu, hakukuwa na uthibitisho wa bei ya tofali na hivyo baraza halikujielekeza vema kwenye ushahidi uliotolewa. Katika uamuzi wake, baraza lilizingatia kielelezo D4 ambacho ni hati ya kudhaminisha mkopo. Kwa mujibu wa hati hiyo, inaonesha ardhi iliyowekwa dhamana ina thamani ya shilingi milioni 20. Awali ya yote, hati siyo ripoti ya tathmini kwa mujibu wa sheria. Hivyo, haiwezi kutumika kama ripoti sahihi kuonesha thamani ya ardhi yenye mgogoro. Hata kama ingetumika kuonesha ardhi yenye mgogoro ina thamani ya shilingi milioni 20, hakuna ubishi kwamba ardhi yenye mgogoro iliuzwa kwa thamani ya shilingi 6,500,000/=. Kwa mujibu wa kifungu cha 133 (2) cha Sheria ya Ardhi kinaeleza kwamba dhamana itahesabika kuwa imeuzwa chini ya bei ya soko endapo itauzwa chini ya 25%. Katika shauri hili, kwa kuwa ardhi yenye mgogoro iliuzwa kwa kiasi cha shilingi 6,500,000/= na kwa kuzingatia thamani 10 inayodaiwa kwa mujibu wa kielelezo D4; basi ni dhahiri kwamba ardhi yenye mgogoro iliuzwa kwa 32% ambayo sio chini ya bei ya soko kwa mujibu wa kifungu cha 133(2) cha Sheria ya Ardhi. Hivyo, kutokana na mjadala mfupi hapo juu, mahakama hii inaona kuwa rufaa hii ina mashiko na inaruhusiwa. Maamuzi ya baraza yanatenguliwa na kuwekwa kando. Mahakama hii inaona kuwa mauzo ya ardhi yenye mgogoro yalizingatia sheria na kwamba mrufaniwa wa 2 alinunua kihalali ardhi yenye mgogoro. Kwa mazingira haya, kila upande utabeba gharama zake. Imeamriwa hivyo. Imetolewa Dodoma leo tarehe 30 Mwezi Septemba 2024. n