ESTHER MEDARD HUKUMU
The appellant is a lawful wife and thus a legal heir, regardless of the date of marriage or when the property was acquired. The house in dispute forms part of the deceased's estate and should be distributed as inheritance. The appellant is entitled to half of the house as her share of inheritance, not as her...
Source-derived case information.
- Citation
- ESTHER MEDARD HUKUMU
- Parties
- Appellant: Esther Medadi; Respondent: Busapare Daudi Lubinza (msimamizi wa Mirathi ya Marehemu Denja Lubinza Busapare)
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2006
- Procedural Posture
- Land Appeal / Second Appeal From District Court Decision, Originating From Primary Court Probate Objection
- Outcome
- Appeal partly allowed
- Legal Topics
- Distribution of Deceased Estate, Spousal Inheritance Rights, Validity of Family Agreements, Probate Administration
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Esther Medadi
Appellant
Busapare Daudi Lubinza (msimamizi wa Mirathi ya Marehemu Denja Lubinza Busapare)
Respondent
Procedural Posture
Land Appeal / Second Appeal From District Court Decision, Originating From Primary Court Probate Objection
Legal Issues
- 1 Whether the appellant is entitled to the disputed house as her own property or as inheritance from the deceased husband
- 2 Whether the lower courts erred in evaluating the evidence regarding the date of marriage and ownership of the house
Ratio Decidendi
The appellant is a lawful wife and thus a legal heir, regardless of the date of marriage or when the property was acquired. The house in dispute forms part of the deceased's estate and should be distributed as inheritance. The appellant is entitled to half of the house as her share of inheritance, not as her exclusive property. The lower courts erred by treating the dispute as a matrimonial property division rather than a succession matter.
Court Disposition
Appeal partly allowed
Orders
- Appellant is entitled to half share of the disputed house as inheritance from the deceased husband.
- The other half share of the house is for the first wife and her children.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MASJALA NDOGO YA SHINYANGA ILIYOPO SHINYANGA RUFAA YA ARDHI NO.10734 /2024 (Inatokana na Uamuzi wa mahakama ya wilaya ya Shinyanga katika Rufaa Na. 12 /2023, yenye asili yake shauri la maombi ya Pingamizi Na. 2/2023 Mahakama ya Mwanzo Salawe) ESTHER MEDADI ...........................................................MRUFANI DHIDI BUSAPARE DAUDI LUBINZA ( msimamizi wa Mirathi ya Marehemu Denja Lubinza Busapare) ........................................MRUFANIWA HUKUMU TH 23 & 31 JULAI 2024 F.H. MAHIMBALI, JAJI Mrufani katika shauri hili alikua mke mdogo wa marehemu Denja Lubinza Busapare na kwamba Mrufaniwa aliteuliwa na mahakama ya mwanzo kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu tajwa. Ilielezwa kwamba mjibu rufaa baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi, alitimiza majukumu yake kwa kukusanya na kugawa mali za marehemu 1 kwa warithi akiwemo Mrufani. Ikumbukwe kuwa Mrufani aligoma kushiriki kwenye kikao cha ukoo ambacho kilimpendekeza Mrufaniwa kuwa msimamizi wa mirathi. Hata hivyo baada ya mahakama ya wilaya kusikiliza rufaa iliamua kwamba,mjibu rufaa alitimiza wajibu wake kama msimamizi wa mirathi na nyumba ambayo Mrufani alidai kwamba ni yake na si mali ya marehemu Denja Lubinza Busapare haikuthibitishwa na hivyo mahakama ya wilaya ikabariki maamuzi ya mahakama ya mwanzo. Mrufani hakuridhika na maamuzi hayo na hivyo kufika mbele ya Mahakama hii akiwa na sababu (2) za rufaa kama ifuatavyo: - 1. Kwamba, Mahakama ya mwanzo na mahakama ya wilaya zimekosea kisheria na kimantiki kwa kuzingatia ushahidi dhaifu wa Mrufaniwa kwamba Mrufani alioana na marehemu mwaka 2015 ambavyo si kweli kama ilivyorekodiwa kimakosa katika hukumu ya Mahakama ya mwanzo. 2. Kwamba, Mahakama ya mwanzo na mahakama ya wilaya zimekosea kisheria na kimantiki kwa kutokuzingatia ushahidi wenye nguvu wa Mrufani ambao ni kielelezo ambacho ni makubaliano ya familia kati ya marehemu na Mrufani ambayo marehemu alimpatia/alimmilikisha Mrufani nyumba/kiwanja husika na kuthibitisha kwamba ni mali yake tangu mnamo tarehe 20/07/2004. 2 Hivyo Mrufani anaomba rufaa yake ikubaliwe na mamuzi ya mahakama ya wilaya na mwanzo yafutwe na kuwekwa kando. Rufaa hii ilisikilizwa kwa njia ya mawasilisho ya moja kwa moja kutoka kwa wadaawa wenyewe na kwamba kila pande ilisimamia rufaa yenyewe bila kuwa na wakili. Kwa upande wa Mrufani alieleza kwamba anapinga maamuzi ya mahakama ya wilaya ambayo kimsingi yanakubaliana na maamuzi ya mahakama ya mwanzo na kuomba sababu zake za rufaa kuwa sehemu ya mawasilisho katika rufaa hii. Hata hivyo Mrufani aliendelea kueleza kwamba alikuwa mke wa pili wa marehemu na ameishi naye wakati wote wa maisha yake na wala siyo hawala na kua marehemu alimgawia haki yake wakati wa uhai wake. Sambamba na hilo Mrufani alieleza kwamba anashangaa kuporwa mali alizopatiwa na marehemu enzi za uhai wake na msimamizi wa mirathi kudai hana haki na kuanza kumfukuza na baadae anaanza kutumia mali hizo kama mnufaika yeye mwenyewe wakati si sehemu ya warithi wa marehemu. Kwa upande wa Mrufaniwa alieleza kwamba anapinga rufaa na alikubali kwamba Mrufani aliolewa kwa marehemu mwaka 2015 na Marehemu Denja Lubinza Busapare alifariki mnamo tarehe 4/8/2019 na kuzikwa tarehe 5/8/2019. 3 Hata hivyo Mrufani aliendelea kueleza kwamba kwenye kikao cha wanandugu, wake wote wawili walikuwapo na kuulizwa waliachiwa nini na marehemu. Mke mkubwa alijibu kwa ufasaha kuhusu mali hizo. Hali kadhalika kwa Bi mdogo, nae alipoulizwa alizitaja mali alizozinunua kwa pamoja. Mrufaniwa aliendelea kueleza kwamba yeye kama msimamizi wa mirathi anao wajibu wa kugawa mali za marehemu licha ya kwamba mrufani amejichagulia mali za kurithi utafikiri ni mgawanyo wa mali za wanandoa walizochuma pamoja wakati ni mali za urithi. Hata hivyo Mrufaniwa alieleza kwamba katika kugawa mali za marehemu Mrufani amepatiwa mbuga hekari tatu za kulima, ng'ombe mmoja na pesa taslimu Tshs 300,000/= ambazo hataki kuzichukua na kuomba mahakama itoe muongozo mzuri kwenye hilo. Mwisho, Mrufani aliomba rufaa itupiliwe mbali kwa sababu haina mashiko kisheria. Hali kadhalika Mrufani kwenye nyongeza, aliendelea kusisitiza kuwa ni mke wa marehemu na hivyo ana haki na hapaswi kudhulumiwa na kuomba rufaa yake ikubaliwe. 4 Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili na kupitia kumbukumbu za Mahakama, Mahakama hii inajikita katika hoja moja kuu;- Je rufaa hii ina mashiko? Kabla ya kuanza kujibu sababu za rufaa, Mahakama hii itaongozwa na matakwa ya kisheria kwamba maamuzi ya mahakama mbili za chini yanapofanana (yaani mahakama iliyosikiliza kesi ya awali na iliyosikiliza rufaa kwa mara ya kwanza), basi Mahakama itakayosikiliza rufaa kwa mara ya pili, haiwezi kutengua maamuzi hayo, vinginevyo yawe yamefikiwa kimakosa na kupelekea haki kutokutendeka. Matakwa hayo yalielezwa katika shauri la Director of Public Prosecution dhidi ya Jaffari Mfaume Kawawa [1981] TLR 149, Musa Mwaikunda dhidi ya Jamhuri [2006] TLR 387 na Wankuru Mwita dhidi ya Jamhuri, Rufaa ya jinai Namba 2019 ya mwaka 2012(haijaripotiwa). Kwa kuanza na sababu ya kwanza ya rufaa, Mrufani alieleza kwamba Mahakama zilikosea kuzingatia ushahidi kwamba Mrufani alioana na marehemu mwaka 2015. Wakati huo upande wa Mrufaniwa akieleza kwamba mleta rufaa walioana na marehemu mwaka 2015 ni kutokana na ushahidi wa Mrufani na mashaidi wake. Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili na kumbukumbu za mahakama ni wazi kwamba wakati Mrufani anaulizwa 5 swali na Mrufaniwa, alisema aliolewa na marehemu mwaka 2015. Ushahidi ambao uliungwa mkono na Mrufaniwa na mashaidi wake ambao walieleza kwamba Mrufani aliolewa kwa marehemu mwaka 2015. Ni matakwa ya kisheria kwamba mdaawa mwenye ushahidi mzito kuliko wa mwingine ndiye anayepaswa kupewa ushindi. Matakwa hayo yameelezwa chini ya wa kanuni ya 6 ya kanuni za Ushahidi Mahakama za Mwanzo GN 22/ 1964 na katika shauri la HEMED SAID DHIDI YA MOHAMED MBILU [1984] TLR 113. Kutokana na maamuzi ya kesi tajwa hapo juu na ushahidi uliotolewa ni ukweli kwamba ushahidi wa mjibu rufaa ni mzito kuliko wa Mrufani kwa sababu unaonesha kwamba Mrufani aliolewa mwaka 2015 na siyo kwamba Mrufaniwa aliolewa mwaka 1998. Kwa kumalizia na sababu ya pili,kwamba Mahakama zilikosea kwa kutokuzingatia ushahidi wenye nguvu wa Mrufani ambao ni kielelezo ambacho ni makubaliano ya familia ya marehemu na Mrufaniwa ambapo marehemu alimmilikisha nyumba/kiwanja mwaka 2004. Mrufaniwa alisema kielelezo hicho hakina mashiko yoyote kwa sababu kiliandikwa kwamba alikabidhiwa nyumba mwaka 2004 wakati huo ushahidi unaonesha aliolewa kwa marehemu mwaka 2015, hivyo ni cha kutengeneza. 6 Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili na kumbukumbu za mahakama, ushahidi unaonesha mrufani aliolewa na marehemu mwaka 2015. Kielelezo A-1 hakikushuhudiwa na ndugu wa upande wa mrufani wala marehemu. Mbaya zaidi hata mwenyekiti wa kitongoji (SMII) alikiri kwamba alisimamia makabidhiano yasiyo halali ambayo hakujiridhisha mmiliki ni nani na ushahidi unaonesha Mrufani hakukitoa kielelezo hicho kwenye shauri la mirathi kwa sababu hakujua kama kipo. Hivyo kutokana na ushahidi huo ni kweli kwamba Mrufani aliolewa kwa marehemu mwaka 2015 na hivyo hakuna namna marehemu angeweza kumpa nyumba mwaka 2004 kama mke wake wakati hajaolewa kwake na hivyo kufanya kielelezo A-1 kuwa batili kama ambavyo ilithibitishwa na mwenyekiti wa kitongoji aliyeshuhudia makubalino hayo. Kwa msingi huo Mrufaniwa amethibitisha madai kwamba nyumba ni mali ya marehemu na siyo ya Mrufaniwa. Katika shauri la GENEROZA NDIMO dhidi ya BLASIDUS YOHANES KAPESI (1988) TLR 73 ilielezwa kwamba kila upande una wajibu wa kuthibitisha madai yake. Kutokana na ushahidi huo Mrufani ameweza kuthibitisha madai yake katika viwango toshelevu na katika ulinganifu wa minzani kama ilivyolezwa katika shauri la ANTHONY M.MASNGA 7 dhidi ya PENINA (MAMA MGESI) & LUCIA (MAMA ANNA), rufaa ya madai Namba .118 ya 2014 Mahakama ya rufaa (haijaripotiwa). Pamoja na hoja hizo hapo juu kushindwa, hata hivyo, hakuna ubishi kwamba Mrufani ni mke wa marehemu DENJA LUBINZA BUSAPALE. Mrufaniwa ambaye ni msimamizi wa mirathi amegawa mirathi ya marehemu kwa warithi akiwepo Mrufani, ambaye alipewa mbuga hekari tatu za kulima, ng'ombe mmoja na pesa taslimu tshs 300,000/= lakini amekataa kupokea mali hizo na hivyo mahakama hii kuona kwamba msimamizi ametimiza wajibu wake kwa kugawa mali kwa warithi kama ilivyoelekezwa kwenye kesi ya MONICA NYAMAKARE JIGAMBA dhidi ya MUGETA BWIRE BHAKOME na HAWA SALUMU MENGELE, maombi madogo ya madai Namba. 199/01 YA MWAKA 2019 Mahakama ya Rufani Tanzania ( haijaripotiwa) na IBRAHIMU KUSAGA dhidi ya EMMANUEL MWETA [1984] TZHC 8, ambapo Mahakama ziliamua kwamba wajibu wa kugawa mirathi ni wa msimamizi wa mirathi na siyo Mahakama. Hata hivyo katika kutimiza wajibu huo, Msimamizi wa mirathi anapaswa kugawa mali za mirathi kwa warithi/wategemezi wote wa marehemu wakati wa uhai wake. Aidha katika kutekeleza wajibu huo, Msimamizi wa Mirathi ni muhimu kufahamu kuwa mali zinazogawiwa kwa warithi ni zile tu ambazo marehemu alikua anazimiliki ndizo zitakua fungu la mirathi. 8 Endapo marehemu alikua Mwenza, jambo la msingi la kuzingatia ni nani walikua warithi/wategemezi wake wakati anafariki. Ni muhimu kutambua kuwa, kwa zama za sasa za maisha, kuwa tu mwenza au mtoto wa marehemu hakukupi haki ya moja kwa moja kuwa mtegemezi na hivyo kuwa mrithi. Mtu unaweza kuwa mwenza au mtoto wa marehemu lakini pekee haikupi haki ya utegemezi japo inakupa haki ya kurithi. Hivyo basi inapotokea marehemu ameacha warithi ambao ni tegemezi zaidi kwake kiwango chao cha urithi ni kikubwa kuliko pale mrithi anapokua anajimudu mwenyewe kimaisha, maana urithi si mgawanyo wa hisa au faida ya biashara kwa wanahisa bali ni mgawanyo wa mali za marehemu kwa warithi wake/wategemezi wake. Hivyo siyo kila mwenye nasaba na marehemu ni mrithi wake kisheria ila mwenza, watoto na katika mazingira ya kipekee wazazi, pale wanapokua ni tegemezi kabisa kwa marehemu. Kwenye shauri hili, ni wazi kuwa Mrufani akiwa Mke Mdogo alikua akiishi na marehemu katika makazi nje ya himaya ya nyumba ya Mke Mkubwa. Hoja kwamba hizo mali zote zilichumwa kabla ya Mke Mdogo (Mrufani) hajaolewa, haizuii yeye kuendelea kuishi katika nyumba hiyo kama Mrithi wa marehemu. Maana wakati wa mirathi si wakati wa kugawanya mali zilizochumwa kwa pamoja na wanandoa, bali kutambua ni mali zipi zilikua ni za marehemu ambazo zinapaswa kuwanufaisha 9 warithi wake kwa kuzingatia kiwango cha utegemezi na siyo kiwango cha kuchangia upatikanaji wake. Hivyo basi hoja kwamba hizo mali zilichumwa na marehemu wakati akiwa na Mke Mkubwa pekee hazimuondolei Mke Mdogo haki ya kurithi, kwani tunachotazama hapa siyo kuolewa lini na mlichuma nini bali je, wewe ni mwenza na mrithi/mtegemezi wa marehemu? Jambo hili wala halizingatii muda wa kua mwanandoa katika ndoa maana hapa hatushughuliki na mgogoro wa talaka na mgawanyo wa mali bali urithi wa mali za marehemu. Hitimisho langu katika hili, kwakua hakuna uthibitisho kuwa nyumba hiyo anayoitumia Mrufani (mke mdogo wa marehemu) ilikua ni miliki ya Mke Mkubwa bali ya marehemu Denja Busapere, hakuna sababu ya msingi ya kisheria ya kumpoka mali hiyo eti kwa kigezo kuwa ilichumwa/kupatikana kabla ya Mrufani kuolewa. Kisheria, kua mwenza tayari kunapelekea kuwa sehemu ya warithi halali wa marehemu bila kujali uliolewa lini, ispipokua tu pale ambapo itathibitika kua hata kwa kua mwenza au mtoto wa marehemu, haukua tegemezi kwa marehemu wakati wa uhai wake. Jambo ambalo si hoja katika shauri hii. Kwa sababu nilizoeleza hapo juu, Mahakama hii imeona kua kuna makosa yalifanywa na Mahakama za chini/Msimamizi wa mirathi ya kumuona Mrufani kama mke katika mgogoro wa ndoa unaohusisha mgawanyo wa mali zilizochumwa kwa pamoja badala ya mgawanyo wa 10 mali za marehemu kwa warithi wake ambapo mke ni sehemu ya warithi halali ya warithi pale Mume anapofariki kama ilivyo katika shauri hili. Hivyo basi, rufaa hii inaruhusiwa kwa kiasi nilichokieleza hapo juu kuhusiana na nyumba anayoishi Mrufani kwamba inapaswa kuwa sehemu ya urithi wake kutoka kwa marehemu mume wake kwa yeye kupata nusu ya asilimia ya nyumba hiyo maana yeye hakua mhamiaji/mpangaji kwa marehemu. Nusu ya mali hiyo itakua ni hisa ya Bi Mkubwa na wanawe. Uamuzi huu umetolewa leo na kusainiwa hapa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Shinyanga leo tarehe 31 Julai 2024. Haki ya rufaa iko wazi. F.H. Mahimbali Jaji. 11