Download PDF

Tanzania Judgment

TANZLII

Maombi Madogo

On this page

Professional case brief

Research organized from the available case record

Source document

01

Holding and result

Extension of time granted due to credible system challenges and procedural illegality; applicant not at fault for delay or procedural error caused by language barrier and eCMS system.

Court disposition

application allowed

Orders

  • Each party to bear own costs
  • Applicant to file appeal within 21 days from date of order

02

Material facts

Parties

Flora Hera Sumaye

Applicant

Munna Singh Sohai

Respondent Counsel: Gladness Fungo

03

Procedural history

  1. Posture

    Miscellaneous Civil Application / Ruling on Extension of Time

04

Questions and positions

Legal issues

Party arguments

Applicant
Applicant claims inability to file appeal within time due to eCMS system requiring unavailable reference number and lack of assistance from court IT officer; further claims procedural illegality as new case was filed instead of rehearing as directed, and language barrier prevented understanding of court orders.
Respondent
Respondent admits eCMS required reference number but disputes lack of assistance, arguing applicant failed to attach supporting affidavit from IT officer; asserts applicant herself filed new case at primary court and cannot complain about procedural error.

05

Court’s reasoning

  1. 01

    John Chuwa v. Antony Ciza [1992] TLR 233

    Applicant facing registry challenges must attach affidavit from involved court officer to support claim.

  2. 02

    Interpretation of Laws Act, Section 84A; Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2021; Interpretation of Laws (use of English Language in Courts) Rules, G.N. 66/2022

    Court proceedings should be in Kiswahili, with English documents accompanied by Kiswahili translation.

06

Ratio, limits and disposition

Ratio decidendi

Extension of time granted due to credible system challenges and procedural illegality; applicant not at fault for delay or procedural error caused by language barrier and eCMS system.

Obiter and limits

  • Courts should ensure justice is accessible in language understood by litigants.
  • Implementation of eCMS system caused challenges for self-represented litigants.

Court disposition

application allowed

  • Each party to bear own costs
  • Applicant to file appeal within 21 days from date of order

Source and reliance status

TANZLII · 1 January 2019

This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.

Judgment reading view

Judgment text

The complete available source text.

Source document

TANZLII

Judgment· 1 January 2019

Maombi Madogo

MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (MASIJALA NDOGO IRINGA) ILIYOPO IRINGA. MAOMBI MADOGO YA MADAI NA. 5546 YA 2024 (Asilia Shauri la Rufaa ya Ndoa Na. 16/2023 la Mahakama ya WHaya ya I ringa mbe/e ya Mhe. E.A. Nsangalufu, HMM). FLORA HERA SUMAYE .............................................. MWOMBAJI

DHIDI YA MUNNA SINGH SOHAI ............................................. MJIBU MAOMBI

UAMUZI 22 & 25/3/2024 I.C. MUGETA, 3 : Shauri hili lina historia ndefu ambayo nitaifupisha. Kwa imani kuwa mwombaji na mjibu maombi walikuwa mke na mme, mwombaji alifungua shauri Mahakama ya Wilaya Iringa kuomba talaka. Baada ya kutoridhika na uamuzi wa Mahakama ya Wilaya, mwombaji alikata rufaa katika Mahakama hii, Rufaa ya Ndoa Na. 41/2019. Mahakama hii iliona makosa katika uendeshaji wa shauri la Ndoa Na. 1/2014 katika Mahakama ya Wilaya na kuamuru kesi hiyo isikilizwe upya mbele ya hakimu mwingine. Badala ya kurudi mahakama ya wilaya mwombaji alifungua kesi mpya katika Mahakama ya Mwanzo Iringa Mjini. Hakuridhika na uamuzi wa mahakama hiyo akakata rufaa Mahakama ya Wilaya ambako alishindwa tena katika Page 1 of 6 Rufaa ya Ndoa Na. 16/2023. Hukumu ilisomwa tarehe 30/10/2023. Sasa anaomba aongezewe muda aweze kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwa vile juhudi zake za kukata rufaa ndani ya muda zilikwamishwa na kuanza kwa mfumo mpya wa usajili wa mashauri wa eCMS. Kwamba ili aweze kufungua rufaa, mfumo ulihitaji namba maalum (reference number) ambayo ilikuwa haipatikani katika mfumo wa zamani na juhudi za kusaidiwa na Afisa TEHAMA wa Mahakama Kuu ziligonga mwamba. Mjibu maombi katika kiapo kinzani chake anakiri mfumo ulikuwa unahitaji "reference number" lakini hakubali kuwa mwombaji alishindwa kusaidiwa na Afisa TEHAMA kwa vile hajaambatanisha kiapo cha Afisa huyo kuunga mkono

hoja yake. Sababu nyingine inayotolewa kuunga mkono maombi haya ni kuwepo makosa ya kisheria (illegality). Kwamba badala ya kusikiliza upya Shauri Na. 1/2014, Mahakama ya Wilaya Iringa, ilifunguliwa kesi mpya mahakama ya mwanzo kinyume na maelekezo ya mahakama hii kwamba kesi ya mahakama ya wilaya isikilizwe upya. Mjibu maombi anawakilishwa na msomi wakili Gladness Fungo ambaye alitoa hoja kuwa mwombaji ndiye alifungua kesi upya mahakama ya mwanzo hivyo hawezi tena kulalamika kuwa ilifunguliwa kimakosa. Page 2 of 6 Akijibu hoja hiyo mwombaji alisema hukumu ya mahakama iliandikwa kwa Kiingereza lugha asiyoielewa na alipoomba msaada wa kutafsiriwa ndipo aiielezwa kuwa anapaswa kufungua kesi mpya kwenye mahakama ya mwanzo, hivyo, kutofuata maeiekezo ya mahakama hii siyo kosa lake!! Alieza pia jinsi alivyofika kwenye mabanda ya wiki ya Sheria hapa Iringa kuomba msaada wa kufungua rufaa ambapo ilishindikana licha ya juhudi za Mhe. Rehema Mayagilo kujaribu kumsaidia na hatimaye kesi itifunguliwa tarehe 15/3/2024. Mam bo yaliyoibuliwa katika maombi haya yamenitafakarisha juu ya ugumu wa kufanya uamuzi wa haki na kutoa hukumu isiyo na lawama. Hakuna ubishi kuwa kuanza kwa matumizi ya mfumo wa eCMS kumeleta changamoto ambazo Mtanzania anayejisimamia kwenye kesi yake kama mwombaji atazipitia anapoutumia. Hivyo ni Dhahiri mwombaji alipitia changamoto hizo. Hata hivyo, mahakama hii

ilishaweka msimamo wa sheria kwamba mdaawa anayekumbana na changamoto za kimasjala katika kufungua kesi akitaja mtumishi wa mahakama aliyeshiriki kutanzua changamoto hiyo, sharti aambatanishe kiapo cha mtumishi huyo kuunga mkono hoja yake. Hii iiielezwa katika kesi ya John Chuwa v. Antony Ciza [1992] TLR 233. Mwombaji amemtaja Richard Mchaga Mleleu, kama Afisa Page 3 of 6 TEHAMA, aliyejaribu kumsaidia bila mafanikio lakini hakuambatanisha kiapo chake. Hivyo, kisheria hoja yake ina upungufu huo. Licha ya upungufu huo, hoja yake kwamba mfumo ulishindwa kutoa "reference number" haijapingwa na ninatambua ilikuwa mojawapo ya changamoto za mfumo wa eCMS ulipoanza kutumika rasmi mwezi Novemba, 2023. Kwa msingi huo sina sababu ya kutilia shaka maelezo ya mwombaji kuwa mfumo ulisababisha achelewe. Kuhusu alivyofika kwenye mabanda ya wiki ya Sheria, hoja hiyo haiko katika kiapo chake hivyo siwezi kuijadili japo ninaamini hasemi uongo. Ninahitimisha kwamba, sababu ya kucheleweshwa kufungua kesi kwa shida za mfumo ni ya msingi, nimeikubali. Nahamia kwenye hoja ya pili, kwamba kuna makosa kwenye mwenendo wa shauri hili. Ni kweli kwamba mahakama hii ilielekeza kesi ya wadaawa isikilizwe upya na mahakama ya wilaya. Ni kweli pia kuwa, mwombaji alifungua kesi mpya katika mahakama ya mwanzo badala ya kuendelea na kesi katika mahakama ya wilaya. Anadai sababu ya kukosea kwake ni kutofahamu

lugha ya kiingereza iliyotumiwa na mahakama hii katika hukumu yake hivyo alipotoshwa na aliyemtafsiria. Ni kweli hukumu ya mahakama hii katika rufaa ya Ndoa Na. 41/2019 imeandikwa kwa Kiingereza. Page 4 of 6 Kwa vile hakuna ushahidi kuwa mwombaji anafahamu lugha ya kiingereza, nimeridhika kwamba ni kweli alipotoshwa na aliyemtafsiria. Haki inataka asibebeshwe lawama kutokana na mfumo wa utoaji haki kutumia lugha isiyofahamika kwa wengi. Pengine wakati umefika wa mahakama katika ngazi zote kuhakikisha haki inawafikia wananchi kwa lugha wanayoielewa kwa kuzingatia kifungu cha 84A cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria [Sura ya 1] (The Interpretation of Laws Act) kinachosema lugha ya Mahakama ni Kiswahili tangu tarehe 15/4/2021 baada ya kurekebishwa na Sheria Na. 1/2021 [yaani, The Written Laws (Misecellaneous Amendments) Act, 2021] na utaratibu wa matumizi ya Kiingereza ukafafanuliwa na Jaji Mkuu kupitia Kanuni za Sheria ya Tafsiri ya Sheria Kuhusu Matumizi ya Lugha ya Kiingereza katika Mahakama Kwa Kuzingatia Mazingira Husika, TS No. 66/2022 (The Interpretation of Laws (use of English Language in Courts) (Circumstances and Conditions) Rules, G.N. 66/2022). Kanuni hizo zinaainisha mazingira ambapo nyaraka za kufungulia kesi, mwenendo wa kesi na hukumu vitakuwa kwa Kiingereza na kwamba vitatolewa pamoja na tafsiri ya Kiswahili chake. Kwa vile mahakama hii ilielekeza shauri la Ndoa Na.

1/2014, Mahakama ya Wilaya Iringa lisikilizwe upya badala yake ikafunguliwa kesi Page 5 of 6 mpya mahakama ya mwanzo, ni dhahiri kuna makosa ya kisheria (illegality) yanayotosheleza kuamua kwamba maombi haya yana mashiko ili Mahakama Kuu ichunguze uhalali wa kufungua kesi mpya kinyume na maelekezo yaliyotolewa. Kwa msingi wa niiiyoeleza, nimeridhika kwamba mwombaji alizuiliwa na mfumo kufungua rufaa ndani ya muda na kuna makosa ya kisheria katika mwenendo wa shauri linalolalamikiwa. Kwa mantiki hiyo, maombi haya nimeyakubali kila upande utabeba gharama zake. Rufaa ifunguliwe ndani ya siku 21 tangu tarehe ya amri hii. I.C. MUG ETA

JAJI 25 / 3/2024 Mahakama: Uamuzi huu umesomwa mbele ya wadaawa na Gladness Fungo, wakili wa mjibu maombi. Isw: I.C. MUGETA

JAJI 25 / 3/2024 Page 6 of 6

Source wording is retained. Consult the source document for its original formatting and pagination.

Authorities

Authorities used by the court

Cases, legislation, regulations, and constitutional provisions identified in the available record.

John Chuwa v. Antony Ciza [1992] TLR 233

Case cited

Interpretation of Laws Act

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2021

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Case-aware research

Ask AI about this case

The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.

About this LexChat collection

This page organizes the available case record for research. Verify quotations, current status, and subsequent treatment against the source document. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.

Legal information, not legal advice. Research summaries do not replace the judgment.