hadija damiana mchekula v mohamed sadiki mrope 2023 tzhc 23224 27 novemba 2023
Appellant demonstrated sufficient contribution to the Salasala house through domestic work and improvements, warranting an increased share of 30% rather than 5%. Other assets allegedly sold were not sufficiently proved and remain excluded from division.
Source-derived case information.
- Citation
- hadija damiana mchekula v mohamed sadiki mrope 2023 tzhc 23224 27 novemba 2023
- Parties
- Appellant: Hadija Damiana Mchekula; Respondent: Mohamed Sadiki Mrope
- Court
- TZHC
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Civil Appeal / Judgment
- Outcome
- appeal partially allowed
- Legal Topics
- Division of Matrimonial Property, Contribution of Spouses, Appeal From Lower Court, Proof of Contribution
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Hadija Damiana Mchekula
Appellant
Mohamed Sadiki Mrope
Respondent
Procedural Posture
Civil Appeal / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the lower court erred in assessing the appellant's contribution to acquisition of matrimonial property
- 2 Whether the division of matrimonial assets was fair and in accordance with the law
- 3 Whether the appellant was entitled to a greater share of the Salasala house
Ratio Decidendi
Appellant demonstrated sufficient contribution to the Salasala house through domestic work and improvements, warranting an increased share of 30% rather than 5%. Other assets allegedly sold were not sufficiently proved and remain excluded from division.
Court Disposition
appeal partially allowed
Orders
- Appellant awarded 30% share of Salasala house; respondent to receive 70% after sale or compensation based on valuation.
- Other orders of the district court remain.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MASJALA NDOGO YA TEMEKE (KITUO JUMUISHI CHA HAKI KATIKA MASUALA YA MIRATHI NA NDOA) ILIYOPO TEMEKE RUFAA YA MADAI NA. 9 YA 2023 (Inatokana na Shauri la Rufaa ya Talaka Na. 58 & 59 ya 2022 kutoka Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi Temeke) HADIJA DAMIANA MCHEKULA.......................................................... MRUFANI DHIDI YA MOHAMED SADIKI MROPE........................................................ MRUFANIWA HUKUMU 09 Oktoba & 27Novemba, 2023 BARTHY, J. Hadija Damiana Mchekula baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mirathi na Ndoa Temeke, katika shauri la Rufaa ya Talaka Na. 58 na 59 ya 2002, ameleta rufaa mbele ya mahakama hiii akiwa na sababu zifuatazo; 1. Kwamba, mahakama iiikosea kisheria na kimaeiezo kwa kutoa maamuzi biia kuzingatia Ushahidi unaothibitisha mchango wa mrufani na mrufaniwa katika upatikanaji wa nyumba Saiasa/a. 2. Kwamba, mahakama iiikosea kisheria na kimaeiezo kwa kutoa maamuzi pasipo kuzingatia Ushahidi unaothibitisha i kwamba mrufaniwa ndio amechangia kwa asi/imia kubwa katika upatikanaji wa nyumba hivyo kufikia maamuzi yasiyo sahihi. 3. Kwamba, mahakama Hikosea kisheria na kimaelezo kwa kutoa mgao wa asilimte tano (5%) ikiwa ni gharama za ujenzi ambazo mrufani alltoa kwenye kujenga karo na kuweka Hpu (plaster) bite ya kuzingatia michango mingine ya kite siku ambayo mrufani aiitoa kwa mrufaniwa akiwa mke haiaii wa ndoa katika upatikanaji wa nyumba hiyo. 4. Kwamba, mahakama Hikosea kisheria na kimaeiezo kuamua kwamba mrufani apewe mgao wa asiiimia tano ikiwa ni fidia ya mrufani aiiyoitoa kwenye marekebisho ya nyumba pasipo kuzingatia mrufaniwa pia ameshauza mail nyingine ziiizo patikana kwenye ndoa bite kumshirikisha mrufaniwa. 5. Kwamba, mahakama Hikosea kisheria na kimaeiezo kwa kushindwa kutoiea maeiezo yeyote kuhusu maH nyingine ambazo waiichuma Pamoja na mrufaniwa, kuuza hizo maH pasipo kumshirikisha mrufani. 2 Hivyo basi, mrufani anaiomba mahakama hii kuamuru kwamba; rufaa hii ikubaliwe, mienendo ya shauri la mahakama ya mwanzo na wilaya ibatilishwe pamoja na hukumu na tuzo zake, mgao wa usawa utolewe, gharama za shauri hili itolewe na nafuu nyingine ambazo mahakama hii itaona busara na haki kutoa. Mahakama ilitoa amri kwamba shauri hili lisikilizwe kwa maandishi na pande zote ziliridhia amri hiyo na kuwasilisha majumuisho yao kwa wakati. Mrufani katika majumuisho yake makuu alichanganya sababu za rufaa ya 1 na 2 na kusema, katika ushahidi wake alioutoa katika shauri la Talaka Na. 350 ya 2021, aiiieleza mahakama kwamba walifunga ndoa 1990 na walifanikiwa kununua kiwanja na kujenga nyumba ambayo ipo Salasala, Dar es Salaam. Pia walinunua mashamba (1 Kerege Bagamoyo, 1 Bungu na Rufiji) pamoja na gari; kama ilivyoelezwa kwenye hukumu ya mahakama. Alisema pia upatikanaji wa nyumba hiyo ya Salasala ilikuwa katika kipindi cha ndoa na kulikuwa ha kuna ubishani kama inavyoonekana katika ukurasa wa 3 na 4 wa hukumu ya Mahakama ya Mwanzo. Pia mrufani aiiieleza mahakama walivyo shirikiana na mrufaniwa kupata mali hizo, na jinsi alivyotekeleza majukumu yake ya nyumbani kama mama. Sambamba na hayo alikuwa akifanya biashara ndogo ya 3 kuuza vitafunwa na hela aliyopata alimpatia mrufaniwa hadi wakanunua kiwanja na kujenga nyumba na wakati wa ujenzi alikuwa akisimamia, akichota maji kwa ajili ya ujenzi hivyo msingi wa upatikanaji wa nyumba hiyo uiitokana na jitihada zao wote wawili. Mrufani alidai kwamba, Mahakama ya Wilaya ilishindwa kuzingatia hoja kwamba alicheza hadi upatu na kumpa fedha mrufaniwa. Kuweka mkazo katika hoja hiyo, alitaja shauri la Sefu Ali Makamula v. Happvness Xavier Asmani, Rufaa ya Madai No. 20 ya 2023 ambao ilirejea shauri la Cleophas M. Matibaro v. Sophia Washusha, Rufaa ya Madai Na. 13 ya 2011 ambapo mahakama ilisema; "iazima kuwe na muunganiko kati ya makusanyo ya mail na majukumu ya pande katika ukusanyaji huo, hivyo kwa maii za ndoa katika kugawiwa iazima kuwe na maii ziiizo kusanywa na pande wakati wa ndoa yao" Ilikua rai ya mrufani kwamba mahakama ya Wilaya ilipaswa kuzingatia mchango wa pande zote katika kufanya mgawanyo na kuamuru asilimia 50 kwa kila pande. Katika hoja ya tatu mrufani aliomba iungane na hoja zilizopita. Alikazia kwa kueleza kuwa asilimia tano (5%) ilihesabika katika mchango wa kujenga karo la choo, kupiga plasta nyumba na kuunganisha umeme 4 nyumba nzima bila kuzingatia kwamba mshitakiwa alikuwa mke halali wa ndoa tangu 1990. Akikazia hoja zake alitaja Kifungu 114(1) cha Sheria ya Ndoa, Sura ya 29, Marejeo 2019 (Sheria ya Ndoa) kinachoeleza kwamba, baada ya mahakama kutoa talaka itakuwa na jukumu la kugawa mali zilizochumwa kwa jitihada za Pamoja wakati wa ndoa. Na Kifungu 114(2)(b) kinatambua jitihada za kila mmoja katika ugawaji wa mali. Kama ambavyo imesemwa katika kesi ya Tumaini M. Simoga v. Leonia Tumaini Baleqa, Rufaa ya Madai 117 ya 2022 katika ukurasa wa 11 na 13 mahakama ilisema kwamba, mchango wa mwanamke kwenye upatikanaji wa chumo la ndoa siyo lazima uwe mchango wa pesa au mchango unaoonekana wa mali au thamani. Mrufani aliendelea kujadil sababu ya 4 na 5 za rufaa na kueleza, mahakama ya wilaya haikutenda haki kwa kutoa mgao wa 5%. Alidai kuwa zipo mali kama shamba la Kerege na Bungu, na gari ambavyo vyote vimeuzwa na mrufaniwa wakati mgogoro bila kumshirikishwa. Hata alipokuwa mahakamani ya mwanzo, mrufaniwa hakubisha kwamba mali ziiikuwepo na mahakama haikutoa amri yeyote. Alileza zaidi kuwa, endapo mahakama ingezingatia hilo, basi ingetoa hata asilimia 100 kwa mrufani kufidia hilo. Hivyo kwa sababu tajwa hapo juu mrufani aliomba rufaa yake ikubaliwe. 5 Katika kujibu hoja hizo, mrufaniwa alijumuisha sababu za rufaa ya 1 na 2 kwa pamoja kwa kurejea Kifungu 110(1) na (2) cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 Marejeo ya Mwaka 2022 (Sheria ya Ushahidi), ambacho inabainisha kwamba yeyote anayeleta madai kwa lengo la kudai haki lazima athibitishe madai hayo. Alisisitiza mrufani ameshindwa kuthibitisha mail hizo zilipatikana akiwa ndani ya ndoa. Ambapo mrufaniwa alithibitisha kwamba alinunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo bila mchango wa mrufani. Pia maelezo ya mrufani kwamba alitimiza majukumu yake kama mama ni maelezo ambayo hayakuwasilishwa na mrufani katika ushahidi wake wa Mahakama ya Mwanzo ni maelezo ya kufikiriwa baada ya maamuzi hivyo hayana uzito katika rufaa ya pili. Mrufaniwa pia alirejea ushahidi wa mrufani alioutoa mahakama ya mwanzo kama inavyoonekana ukurasa wa 5, mstari wa 9 wa hukumu; kwamba mrufani alikiri mpaka anahamia katika nyumba hiyo ya Salasala hakuwahi kupokea hata shilingi 100 kutoka kwa mrufani. Hivyo alieleza kwa ushahidi huo unatosha kuonyesha kwamba mrufani hakuchangia chochote. Akijibu hoja ya 3 mrufaniwa alisema kwamba, mrufani alikuwa mke wa tangu mwaka 1990. Lakini hoja hiyo haikusemwa mbele ya mahakama ya mwanzo. Alikazia kwa kueleza kuwa mchago pekee uliowasilishwa ni 6 katika upatikanaji mali ilikuwa, ni maboresho na ujenzi wa karo. Alilejerea shauri la Bibie Mauridi v, Mohamed Ibrahimu [1989] TLR 162 ambapo mahakama ilitamka lazima kuwepo ushahidi wa kiwango cha mchango kabla ya kufanya mgawanyo wa mali za ndoa. Pia shughuli za nyumbani zitahesabika katika mchango wa upatikanaji wa mali hizo, lakini sio lazima iwe 50%. Mrufaniwa alieleza katika shauri hili mrufani hajawahi kutamka mchango wake mbele ya mahakama ya mwanzo. Hivyo hoja hii haiwezi kuletwa katika rufaa ya pili. Kuweka msisitizo alirejea shauri la Edward Mbele v. Magdalena Jackline Mbele, Rufaa ya Ndoa Na. 11 ya 2011, Mahakama Kuu Dodoma, ambayo ilinukuu shauri la Farida na mwenzake v. Domina Kagaruki, Rufaa ya Madai Na. 130 ya 2006 ilisema kwamba; "mahakama ya Rufaa haiwezi kuzingatia Ushahidi ambao haukutoiewa mahakama za chini". Hivyo aliweka mkazo kwa kusema mahakama hii isizingatie ushahidi huo na mgao wa 5% zilizotolewa na mahakama zilikuwa sawa. Katika hoja ya 4 na 5 za sababu ya rufaa, mrufani alisema alionyesha jinsi gani alizipata mali hizo; kama inavyoonyesha katika ukurasa wa 4 na 5 wa hukumu ya mahakama ya mwanzo. Aiitaja Kifungu cha 110(1) cha 7 Sheria za Ushahidi ambacho inatoa jukumu la kuthibitisha dai na mrufani ameshinda kuthibitisha dai lake. Pia kuhusu mali zilizouzwa, katika rufaa ya kwanza mahakama alitoa sababu mbili kama inavyoonyeshwa katika ukurasa wa 7 wa hukumu kwamba, kwakua mali hizo zimeuzwa haziwezi kuingizwa tena kwenye mgao na kurudia maamuzi ya shauri la Edward Mbele. Mrufaniwa aliomba mahakama hii itupilie mbali rufaa hii. Katika majibu ya nyongeza mrufani alikazia kwa kusema mchango wa mrufani unajionyesha katika mwenendo wa shauri, ingawa mrufani hakuchangia kununua kiwanja, lakini alisaidia katika upatikanaji wake kwa kufanya kazi za nyumbani na maboresho. Mrufaniwa alirejea kuweka mkazo katika hoja ambazo amezieleza hapo awali. Baada ya kupitia kwa kina hoja za pande zote mbili, mahakama hii itaangalia iwapo sababu za rufaa zina mashiko. Katika hoja hizo za rufaa, kimsingi sababu zote za rufaa zinajikita katika hoja moja. Hivyo hoja zote zitaunganishwa na kuwa hoja moja inayosema; je mahakama ilikoea kisheria na kimantiki kutozingatia mchango wa mrufani kakika upatikanaji wa mali za ndoa na hatimae kutoa mgao usio sawa? Nikijielekeza katika Kifungu cha 114(1) cha Sheria ya Ndoa, kinaeleza kwamba baada ya mahakama kutoa talaka itakuwa na jukumu la kugawa mali zilizochumwa kwa jitihada za pamoja au kwa kuagiza kuuzwa kwa 8 mail hizo na kugawanya mapato ya mail hizo zilizopatikana wakati wa ndoa kadri ya mchango wa kila mmoja. Na Kifungu 114(2)(b) cha Sheria ya Ndoa kinataka kuzingatia jitihada au mchango wa kila mmoja katika kutoa amri ya mgawanyo wa mali. Pia kifungu cha 114(3) kinaenda mbele zaidi kueleza kwamba, mali zile ambazo zilipatikana na kumilikiwa na upande mmoja kabla ya ndoa lakini ziliendelezwa au kuboreshwa wakati wa ndoa kwa nguvu za pamoja, nazo pia mahakama imepewa mamlaka kuona ni mali ya pamoja inayostahili kugawanywa. Kwa kuongozwa na vifungu hivyo, katika mwenendo wa shauri katika ya mahakama ya mwanzo ambayo ilisikiliza shauri hilo la msingi; unaonyesha kwamba mrufani alieleza mali walizochuma pamoja na mrufaniwa ni; kiwanja ambacho baadae ilijengwa nyumba, shamba lililopo Kerege-Bagamoyo na Bungu-Rufiji na gari. Kama inavyoonekana (ukurasa wa 4 wa hukumu ya mahakama ya mwanzo). Mrufani amekiri katika Ushahidi wake kuwa hakuchangia kununua kiwanja kwakuwa mrufaniwa hakumshirikisha. Lakini alieleza kuwa alichangia kwenye kumalizia ujenzi kama vile kupaka rangi, kujenga karo la maji taka, na alikuwa akimpatia pesa mrufaniwa ambaye alikuwa anapeleka kwa mafundi. 9 Katika upatikanaji wa gari, mrufani alikiri hakuchangia pesa, lakini aiidai alichangia kwa njia ya mawazo {ukurasa wa 6 na 7 wa hukumu ya Mahakama ya Mwanzdy Mrufaniwa katika utetezi wake alisema kila mtu alikuwa alinunua mwenyewe mali zake. Ikiwemo shamba la kerege na Bungu {ukurasa wa SJ): Lakini baada ya mrufani kupinga hukumu ya Kadhi iliyomtaka amkabidhi shamba la Kerege, ndipo mrufaniwa alimpatia Tsh. 1,500,000/= Sambamba na hoja hizo za pande zote mbili, mahakama ya wilaya katika uamuzi wake kama inavyoonekana kwenye ukurasa wa 4 ilisema kwamba kitendo cha kupaka rangi, kuweka umeme, kujenga karo ni maboresho yanayostahili mgao katika nyumba na hivyo mrufani alipewa 5% za thamani ya nyumba hiyo. Pia mahakama ilitoa Tsh. 1,500,000 kwa mrufaniwa kama pesa ya kuanzia maisha. Mgao huo haukufuata ule yalifanyika kidini. Mahakama iiizingatia kuwa ndio chombo chenye mamlaka kisheria kutoa mgao wa mali baada ya kutamka kwamba ndoa baina ya wadaawa imevunjika. Kwa mali zinazodaiwa kuwa ziliuzwa mahakama ya wilaya aliona hakuna uthibitisho kwamba mali ziliuzwa bila ridhaa. Baada ya kupitia hoja za pande mbili pamoja na maamuzi ya mahakama mbili za chini; ili mahakama kufanya mgawanyo wa mali io zilizopatikana kwa pamoja kwa wanadoa, inazingatia uamuzi katika shauri la Bi Hawa Mohamed v. Ally Sefu [1983] TLR 32, ilitoa kanuni mbili za kuzingatia kwamba; "(i) Since the welfare of the family is an essential component of the economic activities ofa family man or woman it is proper to consider a contribution by a spouse to die welfare of the family as a contribution to the acquisition of matrimonial or family assets; (ii) the "joint efforts" and 'work towards the acquiring of the assets have to be construed as embracing the domestic "efforts'or "work" of husband and wife" Sheria inaelekeza kuangalia shughuli za kiuchumi za kila mwanandoa katika mchango wake wa upatikanaji wa mali za pamoja za ndoa ikiwepo kazi za nyumbani. Kwa kuangalia ushahidi uliotolewa mbeleya mahakama na upembuzi uliofanywa katika hukumu ya mahakama ya mwanzo, ni dhahiri kuwa haikuzingatia mchango wa kila mmoja katika upatikanaji mali hizo za ndoa. Lakini mahakama ya wilaya ilizingatia maboresho aliyofanya mrufani katika nyumba ambayo mchango mkubwa ulifanywa na mrufaniwa na kumpa mrufani 5% ya nyumba. Kwa mantiki kwamba mrufani alikiri ii hakuchangia katika ununuzi wa kiwanja ambacho baadae nyumba ilijengwa. Mahakama hii inazingatia kwamba, mrufani ambae alitimiza wajibu kama mke, pamoja na maboresho aliyothibitisha kufanya katika nyumba hiyo ni mchango tosha katika uendelezaji wa maii za ndoa. Katika kiini cha mgawanyo wa maii baada ya mahakama kutoa amri ya kwamba talaka itolwe, mchango wa kila upande unatakiwa uzingatiwe na mahakama. Ingawa mchango huo hauweki takwa la lazma la kugawa maii hizo sawa baina ya wadaawa. Kwakua hakuna ubishi kuwa mrufani anao mchango katika maii hizo za ndoa, hoja ya msingi ya kujadiliwa na mahakama hii ni kiasi gani wadaawa wanashahili mgao wa maii za ndoa. Mahakama hii inazingatia wadaawa wanapokuwa kwenye mahusiano ya ndoa ya muda mrefu, ni vigumu kuweka kumbukumbu za upatikanaji maii za ndoa au wakati mwingine uthibitisho wa maii alizochangia. Kwa kuzingatia kwamba katika nyakati hizo wadaawa kama wanandoa wanakuwa wameghubikwa upendo na huba, hivyo sio rahisi mara zote kuwa na kumbukumbu ya kila mchango aliotoa. Hoja kama hii ilielezwa vema katika shauri la Victoria Siqala v. Nolasco Kilasi, Rufaa ya Ndoa No. 1 of 2012, Mahakama Kuu Iringa, mbayo iliyonukuu shauri 12 la Anna Aloyce v. Zakaria Zebedavo Mgeta, Rufaa ya Ndoa Na. 1 of 2020, Mahakama Kuu Mwanza ambayo iliamuru haya kwa kunukuu; "Indeed, there is no fast and hard rule in deciding on the amount ofcontribution and division ofmatrimonial assets. Where the matrimonial assets were acquired during the happy days of subsistence of marriage and in the joint efforts of the spouses there is no need of requiring one spouse to give evidence to show the extent of her/his contribution..." Katika shauri hili waada wamekuwa katika ndoa kwa muda mrefu tango mwaka 1990. Mrufani akiwa na mchango wa shughuli za nyumbani alizofonya kwa takribani miaka 30. Ingawa mrufaniwa alidai hiyo ni hoja mpya ambayo haikuwahi kuibuliwa katika rufaa ya awali. Hoja hiyo haiondoi uhalisia kuwa wadaawa wamekua wanandoa kwa muda wote huo na mrufani ana mchango katika mali za ndoa. Ikiwemo kiwanja kilicho nununuliwa na mrufaniwa wakiwa ndani ya ndoa ni dhahiri kuwa kuna ushahidi mrufani alichangia kiuchumi kwa kufanya maboresho na kazi za nyumbani. Hivyo, mahakama hii kwakuzingatia michango ya pande zote mbili inampa mrufani 30% ya thamani ya nyumba ya Salasala. 13 Jambo la mwisho ambalo mahakama hii pia inapaswa kuangalia ni hoja ya mail zingine kuuzwa kabla ya kuvunjika kwa ndoa ya wadaawa iwapo zilikuwa ni mail za pamoja za ndoa. Kumbukumbu za Ushahidi ambazo zimetolewa mbele ya mahakama ya mwanzo hazina uthibitisho wa kutosha kubainisha mali hizo ziliuzwa kwa thamani gani na iwapo mrufani hakufaidika na mauzo ya mali hizo. Hivyo mahakama hii inaona kwamba mrufani alikuwa na wajibu kisheria kuthibitisha uwepo wa mali hizo, mchango wa kila mwanandoa katika upatikanaji wa mali hizo pamoja na thamani yake na kwa kiasi gani ziliuzwa. Kwakua mahakama hii inakaa katika rufaa ya pili, katika hoja hii haioni sababu ya kutengua maamuzi ya mahakama mbili za chini ambazo ziliamua kwa kuafikiana kuwa mali hizi hazikuthibitishwa. Kama ambavyo katika shauri la Amratlal Damodar na mwenzake v. A, H. Jariwalla [1980] TLR31, mahakama ilisisitiza kutoathiri maamuzi ya pamoja ya mahakama mbili za chini kama hakukukuwa na ukiukwaji wa sheria. Hivyo, hoja hii inakosa mashiko kisheria na kutupiliwa mbaii kwa kukosa uthibitisho wa mali za ndoa zilizouzwa wakati wa mgogoro wa ndoa. Hivyo basi, mahakama hii inaona rufaa hii kwa sehemu ina mashiko na hivyo inatengua sehemu ya hukumu ya mahakama ya wilaya kwenye kwa kuongeza asilimia ya mgawanyo wa mali na inatamka kwamba 14 mrufani apate mgao wa 30% ya nyumba ya Salasala kama mchango wake katika upatikanaji wa nyumba hiyo na mrufaniwa apate asilimia 70% baada ya nyumba hiyo kuuzwa au mrufaniwa kumfidia mrufani kiasi cha fedha kinacholingana na thamani hiyo; baada ya kufanyiwa tathmini. Amri nyingine zinaendelea kama ilivyo amriwa na mahakama ya wilaya. Kila pande utabeba binfasi gharama ya shauri. Imetolewa hapa Dar es salaam tarehe 27 ya Novemba, 2023. JAJI 15