ocr tanzlii husna senkondo
The appellant was denied the right to be heard on her objection and request for recusal of the magistrate as raised in her letter dated 29/9/2023. The Primary Court and District Court erred by not ensuring both parties were given an opportunity to present and respond to these objections. This procedural irregularity...
Source-derived case information.
- Citation
- ocr tanzlii husna senkondo
- Parties
- Appellant: Husna Senkondo; Respondent: Shabani Eliah Mkongwe
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Civil Appeal (probate) / Judgment on Second Appeal
- Outcome
- Appeal allowed (on first ground only); matter remitted for hearing of objection.
- Legal Topics
- Right to Be Heard, Appointment of Administrator, Procedural Fairness, Family Law, Appeals Process
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Husna Senkondo
Appellant
Shabani Eliah Mkongwe
Respondent
Procedural Posture
Civil Appeal (probate) / Judgment on Second Appeal
Legal Issues
- 1 Whether the appellant was denied the right to be heard on her objection regarding the appointment of the administrator of the estate
- 2 Whether the lower courts erred in appointing the respondent as administrator without considering the appellant's objections
- 3 Whether the process for handling the appellant's letters of objection and recusal was procedurally fair
Ratio Decidendi
The appellant was denied the right to be heard on her objection and request for recusal of the magistrate as raised in her letter dated 29/9/2023. The Primary Court and District Court erred by not ensuring both parties were given an opportunity to present and respond to these objections. This procedural irregularity violated the appellant's constitutional right to be heard, warranting the setting aside of the lower courts' decisions and remitting the matter for proper hearing of the objections.
Court Disposition
Appeal allowed (on first ground only); matter remitted for hearing of objection.
Orders
- The appeal is allowed to the extent of the first ground regarding the right to be heard.
- The record of Probate Cause No. 1395/2023 is remitted to the Primary Court of Temeke for hearing of the objection raised in the letter dated 29/9/2023, with both parties to be given an opportunity to present and respond to the objection, and the proceedings to be properly recorded.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA MASJALA NDOGO YA MAHAKAMA KUU-TEMEKE KITUO JUMUISHI CHA UTOAJI HAKI RUFAA YA MADAI NA 000018510 YA MWAKA 2024 (Inayotokana na Rufaa ya Mirathi Na. 25959/2023, Mahakama ya WUaya ya Temeke na shauri fa Mirathi Na. 1395/2023Mahakama ya Mwanzo Temekd) KATI YA HUSNA SENKONDO (Mjane Na Mke wa Marehemu KADIRI ELIAH MKONGWE)....................................MLETA RUFAA DHIDI YA SHABANI ELIAH MKONGWE (Msimamizi wa Mirathi ya Marehemu KADIRI ELIAH MKONGWE) .................................................................................. MJIBU RUFAA HUKUMU Tarehe ya Amri ya mwisho: 25/10/2024 Tarehe ya Hukumu: 29/10/2024 S. D. Mwaipopo J Shauri hili la rufaa limefunguliwa na Bi Husna Senkondo (Mjane na Mke wa Marehemu Kadiri Eliah Mkongwe) ambaye ni Mleta rufaa dhidi ya Shaban Eliah Mkongwe (Msimamizi wa Mirathi ya marehemu Kadiri Eliah Mkongwe), kama Mpinga rufaa. Katika rufaa yake, Mleta rufaa anapinga Hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke katika Rufaa ya Mirathi Na. 25959/ 2023 (Mhe. M.X Sanga Hakimu Mkazi Mwandamizi) na Hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Temeke katika shauri la Mirathi Na. 1395/2023 (Mhe. N.G Kachua Hakimu Mkazi) iliyotolewa tarehe 3/10/ 2024. Maelezo mafupi ya shauri hili ni kwamba Mpinga rufaa alifungua Maombi ya kuteuliwa kuwa mismamizi wa Mirathi ya marehemu Kadiri Eliah Mkongwe kwenye Mahakama ya Mwanzo Temeke. Wakati wa usikilizaji wa shauri husika Mleta rufaa, alipinga maombi ya uteuzi wa usimamizi wa mirathi kupitia barua ya tarehe 20/9/2023 ambapo pingamizi hilo lilisikilizwa tarehe 29/9/2023 na lilitupiliwa mbali na Mahakama ya Mwanzo na hatimaye maombi ya uteuzi wa msimamizi wa mirathi kuendelea kusikilizwa na kutolewa uamuzi mnamo tarehe 3/10/2024, ambapo Mahakama ya Mwanzo ilimteua Bw. Shaban Eliah Kadiri Mkongwe, Mpinga rufaa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Eliah Kadiri Mkongwe. Aidha, siku hiyo ambayo pingamizi la awali lilisikilizwa yaani tarehe 29/9/2023, Mpinga rufaa aliandika barua nyingine iliyoelekezwa kwa Mhe. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo kuOmba Mhe. Kachua aliyekuwa akisikiliza shauri husika kujitoa kwenye shauri hilo kwa maslahi ya haki na sababu nyinginezo ambazo alizianisha katika barua husika. Kadhalika, kupitia barua hiyo aliwasilisha hoja nyinginezo mbalimbali zinazohusiana na kupinga mirathi ya marehemu Kadiri Eliah Mkongwe. Kwa mujibu wa rekodi ya Mwenendo wa Mahakama ya Mwanzo, barua husika ilipokelewa na Mahakama ya Mwanzo mnamo tarehe 2/10/2024 na kumfikia Mhe. Kachua aliyesikiliza shauri husika tarehe 3/10/2024 baada ya uamuzi wa uteuzi kuwa umeshasomwa. Aidha, kufuatia ombi la hakimu kujitoa lililowasilishwa na Mleta rufaa, Mahakama ya Mwanzo baada ya kuipitia barua husika ilimuelimisha Mleta rufaa kuondoa pingamizi lake la Hakimu kujitoa pamoja na msimamizi wa mirathi ambapo Hakimu aliendelea kusikiliza shauri hilo, kutoa amri stahiki na kulipangia tarehe nyingine. Kufuatia uamuzi huo Mleta rufaa alifungua Rufaa ya Mirathi Na. 25959/ 2023, katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi - Temeke akipinga Uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo ya Temeke, shauri la Mirathi Na. 1395 la Mwaka 2023 mbele ya Hakimu Kachua, uamuzi wa tarehe 3-10-2023. Mahakama ya Wilaya baada ya kusikiliza hoja za rufaa iliitupilia mbali rufaa husika bila gharama. Mleta rufaa hakuridhishwa na Hukumu ya Mahakama ya Wilaya na hivyo alikata rufaa Mahakama Kuu kwa kuzingatia hoja zifuatazo: 1. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea Kisheria na Kimantiki kwa kutozingatia kuwa Mahakama ya Mwanzo hapa Kituo Jumuishi cha Mahakama imekosea kisheria na kimantiki kwa kutoa uamuzi wa kumteua Mjibu Rufaa kuwa Msimamizi wa Mirathi ya marehemu KADIRI ELIAH MKONGWE bila ya kutoa nafasi ya kuzingatia na kusikiliza pingamizi la Mleta Rufaa la tarehe 20/09/2023. 2. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea Kisheria na Kimantiki kwa kutozingatia kuwa Mahakama ya Mwanzo hapa Kituo Jumuishi cha Mahakama imekosea kisheria na kimantiki kwa kutoa uamuzi wa kumteua Mjibu Rufaa kuwa Msimamizi wa Mirathi ya marehemu KADIRI ELIAH MKONGWE bila ya kuzingatia kuwa na kusikiiiza lalamiko la Mleta Rufaa kuwa Mjibu Rufaa si mtu sahihi kusimamia mirathi ya marehemu mume wake kwani Mjibu Rufaa alishiriki kumnyang'anya Mleta Rufaa cheti cha kifo, kadi ya NSSF, kadi za benki za mume wake na simu mbili na kuwachukua watoto 3. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea Kisheria na Kimantiki kwa kutozingatia kuwa Mahakama ya Mwanzo hapa Kituo Jumuishi cha Mahakama imekosea kisheria na kimantiki kwa kutoa uamuzi wa kumteua Mjibu Rufaa kuwa Msimamizi wa Mirathi ya marehemu KADIRI ELIAH MKONGWE bila ya kuzingatia na kusikiliza lalamiko la Mleta Rufaa kuwa Mleta Rufaa ambaye ni Mjane na Mke wa marehemu hakushirikishwa na wala hakuwahi na pia hajawahi kuweka sahihi kwenye muhktasari wa kikao chochote cha marehemu mume wake kutokana na mgogoro uliokuwepo na uliosababishwa na Mjibu Rufaa. 4. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea kisheria na kimantiki kwa kusema kuwa Mleta Rufaa hakuleta ushahidi wa kuhusu mtoto NADYA kuwa sio wa marehemu bila ya kuzingatia kuwa Mleta Rufaa hakupewa nafasi ya kusilizwa lalamiko lake na kueleza kuwa mtoto NADYA si miongoni mwa warithi wa marehemu mume wake na hatambuliki na pia hakuna ushahidi wa cheti cha kuzaliwa na vipimo vya DNA kuthibitisha kuwa ni mtoto wa marehemu. 5. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea Kisheria na Kimantiki kwa kukubaliana na Uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo ya Temeke ya Kumteua Mjibu Rufaa kuwa Msimamizi wa Mirathi bila ya kuzingatia kuwa yeye Mleta Rufaa akiwa ni mjane, mrithi na mke wa marehemu ana maslahi mapana na mail za marehemu mume wake hivyo ana ana nafasi kubwa ya kusimamia mali za mume wake 6. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea Kisheria na Kimantiki kwa kusema kuwa Marehemu KADIRI ELIAH MKONGWE alikuwa na wake wa ndoa watatu bila ya kuzingatia marehemu ameacha mke moja tu wa ndoa ambae ni HUSNA SENKONDO kwa ndoa halali iliyofungwa tarehe 27-11-2009. Hivyo Mleta Rufaa ameiomba Mahakama hii impatie nafuu zifuatazo: 1. Rufaa hii ikubaliwe; 2. Hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama-Temeke katika shauri la Rufaa ya Mirathi na. 25959 la Mwaka 2023, Hukumu ya tarehe 18/ 07/ 2024 mbele ya Mhe. Hakimu Mkazi Manfred Sanga ifutwe na itupiliwe mbali; 3. Hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama cha Temeke katika Shauri la Mirathi Na. 1395 la Mwaka 2023 hukumu ya tarehe 3-10- 2023 mbele ya Mheshimiwa Hakimu Kachua ifutwe na itupiliwe mbali; 4. Mahakama hii tukufu itamke ya kwamba Mleta Rufaa Husna Senkondo ambaye ni Mjane na Mke wa marehemu ndiye mtu sahihi kusimamia mirathi ya mume wake Kadiri Eliah Mkongwe 5. Nafuu nyinginezo ambazo Mahakama hii tukufu itaona inafaa kuzitoa Usikilizwaji wa rufaa hii uliendelea kwa utaratibu wa hoja za maandishi kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Mahakama. Mrufani aliwakilishwa na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) na Mrufaniwa aliwakilishwa na Wakili msomi Frank Mwampamba. Akiwasilisha hoja za maandishi za kuunga mkono rufaa yake Mrufani alianza kwa kuweka kumbukumbu sawa kuwa mnamo tarehe 3/10 / 2024, Mahakama ya Mwanzo ilitoa uamuzi wa shauri na. 1395 pamoja na amri mbalimbali zifuatazo: -Msimamizi wa Mirathi ajaze na 5 ya mali za marehemu Fomu na 6 ya mgawanyo wa mirathi ya marehemu Shauri kwa kuwaislisha mrejesho tarehe 6/12/2024 Ameendelea kueleza kuwa kutokana na maamuzi hayo yeye kama mke wa mjane Eliah Kadiri Mkongwe hakupewa nafasi ya kusikilizwa pingamizi lake la kumkataa msimamizi wa mirathi wakati shauri hilo likiendelea hivyo aliamua kukata rufaa katika Mahakama ya Wilaya akipinga uamuzi huo kupitia shauri na. 25959/2024 ambapo mnamo tarehe 18/7/2024 Mahakama ilitupilia mbali rufaa yake kwa gharama. Hivyo kufuatia uamuzi huo, Mleta rufaa alikata rufaa kwenye Mahakama hii akiwa na sababu sita za rufaa. Akiwasilisha kwenye hoja ya kwanza ya rufaa, Mleta rufaa ameeleza kuwa aliweka pingamizi la msimamizi wa mirathi kutokuteuliwa wakati shauri la mirathi likiendelea ambalo halikusikilizwa. Aliamua kuandika barua ya tarehe 29/9/2024 akiomba Hakimu anayesikiliza shauri hilo kujitoa pamoja na msimamizi wa mirathi. Kupitia barua hiyo pia aliainisha hoja mbalimbali za kupinga mirathi husika kuendelea hata hivyo licha ya kuwasilisha barua hiyo, Mahakama haikumsikiliza na badala yake iliendelea kumteua msimamizi wa mirathi jambo ambalo anaona lilimnyima haki yake ya kusikilizwa kwa mujibu wa Ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri Muungano ya Tanzania. Haki hii inampa fursa ya kusikilizwa na kupewa muda wa kutosha kuandaa kesi yake, mashahidi, kuuliza maswali ikiwemo kuwakilishwa. Aliirejesha Mahakama kwenye Rufaa ya madai na. 39/2019 ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo inasisitizia umuhimu wa haki ya mtu kusikilizwa. Kwa mujibu wa Ibara hii, ni hoja yake kuwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa barua yake ya tarehe 29.9.2024 hali iliyopelekea Mahakama kuendelea kuteua msimamizi wa mirathi asiye na maslahi ya mali ya marehemu pasipo na haki. Kuhusiana na hoja ya 2 na ya 5 ya rufaa, Mleta rufaa aliomba kuziwasilisha kwa pamoja ambapo alieleza Mahakama kuwa jukumu la Mahakama ni kuteua msimamizi wa mirathi mwenye maslahi na mali za marehemu na yeye kama mke wa marehemu ana maslahi. Alirejea kesi ya Seif Marare vs Mwadawa Saium (1985) TLR 253. Alieleza kuwa mleta rufaa si mtu sahihi kwakuwa alishiriki kumnyan'ganya watoto, kadi za benki na Nssf na simu mbili. Kwamba hakuwahi kushirikishwa kwenue kikao cha kuteua msimamizi wa mirathi na msimamizi wa mirathi alimuongeza mtoto Nadya kama mtoto wa marehemu bila ya kuwa na vithibitisho vyovyote. Alirejea kesi ya Msimamizi wa mirathi ya marehemu Ndakidemi dhidi ya kuthibitisha hoja kwamba yeye ana maslahi na mali za marehemu. Akiwasilisha hoja ya 3 ya rufaa, Mleta rufaa alieleza kuwa hajawahi kushirikishwa kwenye kikao cha familia cha kupendekeza msimamizi wa mirathi na hajawahi kuweka sahihi katika muhtasari wa kikao. Alirejea kesi ya Masubi Jacob dhidi ya Rosemary William. Ameeleza kuwa endapo angepewa nafasi ya kusikilizwa angeweza kutoa sababu zake za kumpinga msimamizi wa mirathi pamoja na mtoto Nadya. Zaidi barua yake ya malalamiko ya tarehe 29.9.2024 haikusikilizwa ambapo angetumia fusra hiyo pia kupinga mtoto Nadya ambaye uthibitisho wake wa DNA haukutolewa. Akihitimisha hoja ya sita ya rufaa, Mleta rufaa alieleza kuwa Mahakama ya Wiiaya ilikosea kuamua kuwa marehemu aliacha wake watatu wakati jambo hilo sio kweli kwakuwa aliacha mke mmoja ambaye nl yeye mwenyewe na walifunga ndoa tarehe 27/11/ 2009. Akiwasilisha hoja za kupinga rufaa, Mpinga rufani aliomba Mahakama hii ijielekeze kwenye Hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke 18/07/2024 na mwenendo wake, na taarifa zote za Mahakama ya awali. Amewasilisha kuwa kwa kiasi kikubwa hoja za mleta rufaa zinajikita katika hoja ya kutosikilizwa na kutolewa uamuzi wa pingamizi lake la awali. Alieleza kuwa, kwa upande wa Mrufaniwa wamejikita katika kupinga hoja zote kwa kuonesha kuwa hazina mashiko zaidi ya kuchelewesha haki kwa wanufaika wa mirathi ya marehemu. Aidha alieleza kuwa wanakubaliana na uamuzi na hukumu za Mahakama za chini na wanaomba rufaa hii itupiliwe mbali. Kuhusu hoja ya kwanza ya rufaa, Mrufaniwa aliwasilisha kuwa sababu hii ya rufaa haina mashiko kwakuwa pingamizi analolisemea mrufani aliwasilisha hoja yake kwenye Mahakama ya awali. akapewa nafasi ya kusikilizwa kikamilifu na uamuzi ulitolewa, aliirejesha Mahakama kwenye mwenendo wa shauri la Mahakama ambalo ndio chimbuko la Rufaa ya Mahakama ya Wilaya na kueleza kuwa rufaa hii ni kinyume kabisa na wasilisho la mrufani katika kutetea hoja yake ya kwanza. Kuhusu hoja ya kuwa Mrufaniwa, si mtu sahihi kwa kuwa alishiriki kumnyang'anya mrufani cheti cha kifo, kadi ya NSSF, kadi za benki za marehemu, simu mbili na kuchukua watoto, alieleza kuwa ni jambo ambalo linahitaji uthibitisho zaidi na anapaswa afuate utaratibu wa kisheria, kwakuwa Mahakama ya awali ilkuwa siyo mahali pake kuwasilisha masuala hayo. Aliirejesha Mahakama katika ukurasa wa Tatu (3) na wa Nne (4) wa barua husika ambao umeanisha malalamiko yake ikiwemo kunyan'ganywa . watoto wawili ambao ni Farida na Rahma Kadiri Mkongwe. Alimtaka mrufani kulipeleka suala hili katika mamlaka husika. Kuhusiana na hoja iliyopo katika barua hiyo aya ya Pili (2) amekubaliana na Mahakama ya awali ilivyoamua na kuwa Mrufani katika wasilisho lake amerejea Ibara ya 13 (6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na katika ukurasa wa 5 wa wasilisho lake amesema ameeleza kuwa malalmiko ya mrufani yalisikilizwa. Aliirejesha Mahakama kwenye ukurasa wa Nne (4) aya ya 2 Hukumu ya Mahakama ya Wilaya na kunukuu ifuatavyo: "Katika mwenendo wa Mahakama ya Mwanzo inaonyesha tarehe 20 mwezi wa 09 mwaka 2023 Mrufani aliwasilisha barua ya pingamizi. Mahakama Hisikiiiza pingamizi hiio na kutoa uamuzi hivyo haina shaka kuwa Mrufani na Mrufaniwa waiipewa haki ya kusikiiizwa kwa mujibu wa Ibara ya 13 (6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977". Mpinga rufani aliongeza kuwa; kutokana na nukuu hapo juu ni wazi kuwa haki ya kusikiiizwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 haikukiukwa na Mahakama ya Mwanzo kinyume na wasilisho la Mrufani. Hivyo hata kesi ya Rufaa ya Madai Na.39/2029 Mahakama ya Rufaa ya Tanzania iliyorejewa na Mrufani ambayo hata wadaawa1 hawajatajwa haiwezi kuwa sahihi kutumika kutetea sababu ya kwanza ya Rufaa. Ni wazi kuwa Aya ya nne (4) ya barua ya Mrufani inathibitisha wazi kuwa Mrufani alipewa fursa ya kusikilizwa baada ya pingamizf lake kukataliwa ndiyo akamua kuandika barua iliyorejewa hapo juu. Kuhusu kujitoa kwa hakimu alirejea Msimamo wake kuwa mrufani alitakiwa amwandikie hakimu anayesikiliza kesi na siyo kwa mfawidhi wake. Kuhusu hoja ya Pili (2) na ya Tano (5) ya Rufaa, alieleza hazina mashiko na wanaungana na Hukumu ya Mahakama ya Wilaya kwa kuungana na uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo kuwa ilizingatiwa kuwa mrufaniwa anayo maslahi juu ya mirathi ya marehemu, aliirejesha Mahakama kwenye kesi ya Jaqueline Tibamanya dhidi ya Maximilan Ponsian (PC) Civil Appeal no. 26 of 2022 High Court of Tanzania at Bukoba District Registry (Unreported) katika ukurasa wake wa 11 ambapo Mahakama ilieleza kuwa; "4 primary Court upon which jurisdiction in the administration of estates of the deceased's estates has been conferred may; I 1. Either of its own motion or on application by any person interested in the administration of the estates appoint one or more persons interested in the administration to be the administrator or administrators thereof, and in selecting such an administrator, shall unless for any reason it considers in expedient so to do having regard to any wishes which may have been expressed by the deceased; Pia alirejea shauri la Sekunda Mbwambo dhidi ya Rose Ramadhani [2004] TLR at page 439 kuwa; "4/7 administrator may be a widow/widows, parent or child of the deceased or any other dose relative; if such people are not available or if they found to be unfit in one way or another, the court has power to appoint any other person to discharge the duty." Mpinga rufaa alihitimisha kwa kueleza kuwa Mahakama ya Wilaya ilikuwa sahihi kuungana na Mahakama ya Mwanzo kumteua Mrufaniwa kuwa Msimamizi wa Mirathi ya marehemu mtajwa hapo juu kwakuwa alikuwa anakidhi matakwa yote kama yalivyoainishwa hapo juu kwenye nukuu za kesi ziliyorejewa kulingana na mazingira ya mirathi husika. Aliongeza kuwa Marehemu katika uhai wake alifunga ndoa na wake watatu tofauti. Mke wa kwanza alizaa naye mtoto mmoja, mke wa pili alizaa naye mtoto mmoja pia na mke wa tatu ndiye mrufani ambaye alizaa naye watoto wawili kwa hiyo kati ya watoto wa marehemu na warithi wapo watoto wawili wa mama tofauti ambao siyo watoto wa kuzaliwa wa Mrufani ambao bila shaka Mahakama ya awali iliona kuwa Mrufani hafai kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu kwasababu hatawatendea haki baadhi ya warithi wa marehemu ambao siyo watoto wake wa kuwazaa, wakiwemo wazazi wa marehemu, ndugu wa marehemu kwakuwa asili ya mirathi hii ni kiislamu na inahusisha watoto wa marehemu, ndugu, wazazi n.k hivyo Mrufaniwa ndiye mtu sahihi kuwa Msimamizi wa mirathi. Na pia katika mirathi ya marehemu kuna mali ambazo marehemu alichuma na wake zake wawili wa kwanza na wa pili ikiwepo Nyumba iliyopo Kimara ambayo mrufani kama mke wa tatu wa ndoa wa marehemu ameikuta hivyo anatakiwa kujua pamoja na yeye kuwa na mchango wa uchumaji mali na marehemu zipo mali ambazo marehemu alichuma na mke wa kwanza na wa pili hivyo kumfanya Mrufaniwa kuwa mtu sahihi kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Kadiri Eliah Mkongwe kwa maslahi ya haki kutendeka kulingana na asili ya mirathi yenyewe. Akiwasilisha juu ya aya ya 3 ya barua ya Mrufani iliyopo katika ukurasa wa Tatu (3) ,na Nne (4) aliijibu (3) kuwa hoja ya tatu (3) ya Rufaa haina mashiko kwa kiasi kikubwa kwakuwa kikao cha ukoo hakifanyi kazi ya kumteua' msimamizi wa mirathi bali ni Mahakama kama ilivyofanya Mahakama ya awali. Alizitaja kazi za kikao cha familia/ukoo ni kutoa taarifa kwa wana ukoo au familia wajue mchakato wa mirathi ya marehemu na ndicho chenye jukumu kukubaliana ni nani apendekezwe kuteuliwa na Mahakama kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu.Aliirejesha Mahakama katika aya ya mwisho katika ukurasa wa 9 na ya kwanza ukurasa wa 10 katika shauri la Jaqueline Tibamanya dhidi ya Maximilan Ponsian (PC) Civil Appeal no. 26 of 2022 High Court of Tanzania at Bukoba District Registry (unreported) na Muhtasari wa kikao unonesha mjane (mrufani alihudhuria siku ya kikao cha familia. Alisisitiza kupendekezwa kwake na familia kusimamia mirathi hii hakuna shida yeyote. Kuhusu sababu y Nne (4) ya rufaa, alieleza kuwa haina msingi wala mshiko yoyote hivyo aliomba itupiliwe mbali kwa gharama kwakuwa Hukumu ya Mahakama ya Wilaya ilikuwa sahihi. Alieleza kuwa Mrufani alishawasilisha lalamiko hilo kwenye mahakama ya Mwanzo na mtoto husika Nadya alishaondolewa kwenye warithi wa mirathi ya marehemu kwasababu tu ni mtoto wa । marehemu wa nje ya ndoa na kwa kuwa asili ya mirathi hii ni dini ya kiislamu pamoja na hoja kuwa kitanda hakizai haramu ni jambo la wazi la kubaguwa warithi wa marehemu. Huo ni ubaguzi na ni mila za kizamani kwasababu hakuna lengo au dhamira wazi iliyowekwa na marehemu kumzuia mtoto huyo asiwe mrithi wake. Aidha Mahakama ya Wilaya iliweka bayana kuwa wajibu wa kutambua warithi na kuwaweka katika urithi ni wa msimamizi wa mirathi na siyo Mahakama na hii inadhihirisha wazi kuwa Mrufani hafai kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemeu Kadiri Eliah Mkongwe kwakuwa alianza toka katika Mahakama ya awali kumkataa mtoto (Nadya) wa marehemu bila hata kuithibitishia Mahakama kuwa siyo mtoto wa marehemu jambo ambalo ni ubaguzi na halikubaliki. Akiwasilisha kuhusu hoja ya Sita (6) ya rufaa, Mpinga rufaa alieleza kuwa haina mashiko kwakuwa Hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke ilisema kuwa marehemu alioa wake watatu (3) tofauti ikiwa inarejea wasilisho la Wakili wa Mrufaniwa kama alivyowasilisha Mahakamani lakini kwakuwa hoja ya wake wa marehemu haikuwa sababu ya rufaa bishaniwa katika Mahakama ya Wilaya, Hakimu hakuitolea uamuzi. Hivyo alieleza kuwa, kwa kuwa jambo hili haiikutolewa uamuzi na Mahakama ya Wilaya na wala haikuwa hoja mojawapo ya mrufani katika Mahakama ya Wilaya inakuwa vigumu kwa Mahakama hii kuamua endapo Mahakama ilikuwa sahihi au vinginevyo kwakuwa Mahakama ya chini haikutolea uamuzi wowote juu ya hiio. Aidha, alieleza kuwa kwakuwa kwenye hatua ya rufaa wadaawa hawaruhuwi kuleta mambo mapya zaidi ya kukosoa yale yaliyopo kwenye hukumu au mwenendo wa Mahakama ya chini yake, sababu ya sita inakosa mashiko kwa jinsi hiyo kwakuwa Mahakama hii imefungwa mikono kuamua juu ya hilo. Akihitimisha wasilisho lake, Mrufaniwa aliiomba Mahakama hii itupilie mbali rufaa husika kwa kukosa mashiko. Baada ya kupitia hoja ya pande zote mbili swali la msingi ambalo Mahakama imejiuliza ni endapo rufaa hii ina mashiko. Katika kushughulikia rufaa hii Mahakama hii imezingatia msingi kwamba kama Mahakama ya pili ya rufaa inaweza kuingilia maamuzi ya Mahakama iliyosikiliza shauri endapo kuna kasoro. Rejea shauri la Bushangilangonga dhidi ya Mayanda Maige [2002] TLR 355. Aidha, Mahakama imezingatia kwamba ni sheria iliyojengeka kuwa Mahakama inapaswa kushughulikia hoja zote zinazoletwa mbele yake. Rejea shauri la: Malmo Montagekonsult AB Tanzania Branch dhidi ya Margret I Gama, Rufaa ya Madai Na. 86 of 2001 (haijaripotiwa); Simon Edson @ Makundi dhidi ya Republic (Criminal Appeal 5 of 2017) [2020] TZCA 1730 (18 August 2020) TANZLII; Nyakwama s/o Ondare @ Okware vs. Republic (Criminal Appeal No. 507 of 2019) [2021] TZCA 592 (21 October 2021) TANZLII na; Revocatus Mugisha dhidi ya Republic (Criminal Appeal No 200 of 2020) 2022 TZCA 63 (22 Februari 2022) TANZLII. Vilevile katika shauri la Zuberi Bakari Mwichikitu dhidi ya Selemani Bakari Mwichikiti, Civil Appeal No.91353/ 2023, Mahakama ya Rufaa, ilieleza kuwa Mahakama inayokaa kama ya rufaa haifungwi kushughulikia hoja zote za rufaa. Inaweza kuzichanganya zote kwa pamoja au ikazishughulikia kwa mpangilio: "An appellate court, however, is not bound to determine all grounds of appeal. It can determine a ground that disposes of the matter alone. It can also determine the groundsJointly or generally or in seriatim. Msimamo huu pia ulielezwa na Mahakama ya Rufaa ya Rufaa katika kesi ya Malmo Montagekonsult AB Tanzania Branch dhidi ya Margret Gama, (supra) kuwa Mahakama inaweza kushughulikia hoja zote za rufaa au hoja moja tu ambayo itaona inamaliza usikilizaji wa shauri. I "In the first place, an appellate court is not expected to answer the issues as framed at the trial. That is the role of the trial court. It is, however, expected to address the grounds ofappeal before it Eventhen, it does not have to deal seriatim with the grounds of appeal as listed in the memorandum of appeal. It may, ifconvenient, address the grounds generally or address the decisive ground ofappeal only or discuss each ground separately". Nikirudi kwenye shauri lililopo mbele yangu, Mleta rufaa amewasilisha hoja sita za rufaa, hata hivyo baada ya kuzipitia hoja hizo Mahakama imeamua kuanza na hoja ya kwanza ya rufaa inayosema kwamba; Mahakama ya Mwanzo iiikosea kisheria na kimantiki kwa kumteua Mjibu Rufaa kuwa Msimamizi wa Mirathi ya marehemu KADIRI ELIAH MKONGWE bila ya kutoa nafasi ya kuzingatia na kusikiliza pingamizi la Mleta Rufaa la tarehe 20/09/2023; Nimepitia hoja za mawasilisho za Mleta rufaa pamoja na rekodi za Mahakama ya Wilaya na kugundua kwamba hoja hii ya rufaa inarejea barua ya tarehe 20/9/2024 ambayo iliwasilisha pingamizi la awali kwenye uteuzi wa msimamizi wa mirathi. Vilevile nimepitia hoja za maandishi za Mleta rufaa na kuona kuwa hoja hii pia inarejea barua ya tarehe 29/9/2024 iiiyoelekezwa kwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo ikumuomba Hakimu anayesikiliza shauri husika kujitoa na pia ikimkataa Msimamizi wa mirathi. Katika kujirdhisha na hoja hii ya Mleta rufaa, Mahakama ilipitia pia mwenendo wa shauri la Mahakama ya Mwanzo na kuona kuwa; Mleta rufaa aliandika barua mbili za mapingamizi zenye hoja mbalimbali za kuzingatiwa na Mahakama ya Mwanzo katika maombi ya mirathi ya bwana Eliya Kadiri Mkongwe, yaani barua ya tarehe 20/9/ 2023 iliyomkataa msimamizi wa mirathi na ya tarehe 29/9/2023 ambayo Mleta rufaa alimuomba Hakimu anayeendesha shauri husika kujitoa. Kwa mujibu wa rekodi ya Mwenendo wa Mahakama ya Mwanzo, hoja ya kupinga msimamizi wa mirathi iliyowasilishwa kwa barua ya tarehe 20/9/2023 ilisikilizwa mnamo tarehe 29/9/2023 na kutolewa uamuzi wake na hatimaye maombi ua uteuzi kusikiiizwa na kutolewa uamuzi mnamo tarehe 3/10/2023. Hata hivyo hoja za Mleta rufaa za kumkataa Hakimu zilizowasilishwa tarehe 29/ 9/2023 zilipokelewa na Mahakama ya Mwanzo mnamo tarehe 2/10/ 2024 na kwa mujibu wa rekodi ya mwenendo wa shauri, zilimfikia Mhe. Hakimu aliyekuwa akiendesha shauri husika tarehe 3/10/2023 saa 11.45 baada ya Hakimu kuwa ameshasoma uamuzi wa kuteua msimamizi wa mirathi. Baada ya kupokea barua husika, Hakimu aliyekuwa anasikiliza shauri husika la uteuzi wa msimamizi aliwasilisha jalada husika kwa Hakimu Mfawidhi kwa hatua zake, baada ya yeye mwenyewe kupitia hoja husika za Mleta rufaa na kuamua kuwa hakukuwa na sababu za msingi za yeye kujitoa. Sehemu ya mwenendo imenukuliwa kama ifuatavyo: Hakimu Mfawidhi nimepokea barua ya malalamiko kutoka kwa Bi Husna Senkondo ambaye ni Mke wa Marehemu katika mirathi hii akiomba niondolewe katika kusikiliza shauri hili. Nimesoma malalamiko yake nimeona hoja zote zilizoelezwa hazina msingi/uzito wa kufanya nijitoe katika shauri hili. Rekodi za Mahakama zinajieleza kwamba pingamizi lilisikilizwa na uamuzi ulitolewa...... Mnamo tarehe 12/10/ 2024 Mhe. Hakimu Mfawidhi alitoa amri ya Mhe. Kachua kuendelea kusikiliza shauri husika kwa maslahi ya haki kwakuwa tayari alikwishaelekezwa kuliendesha shauri husika. Mnamo tarehe 23/10/ 2024 Hakimu anayesikiliza shauri husika alipanga tarehe ya kusikiliza pingamizi hilo tarehe 9/11 /2023. Aidha, rekodi ya tarehe 9/11/2023 inaonesha kuwa pingamizi husika lilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa na wadaawa walikuwepo Mahakamani. Hata hivyo, rekodi ya Mahakama inaonesha kuwa siku husika, Mleta rufaa hakupewa nafasi ya kuwasilisha hoja zake za pingamizi zilizoanishwa kwenye barua ya tarehe 29/9/2023 ikiwemo hoja ya Hakimu kujitoa kwenye kesi. Badala yake rekodi ya Mahakama inaonesha kuwa Hakimu aliyekuwa anaendesha kesi alitoa uamuzi wake moja kwa moja baada ya kupitia pingamizi. Hata Mpinga rufaa hii hakupewa nafasi ya kuweka msimamo wake au majibu kwenye barua ya tarehe 29/9/ 2023. Rekodi husika inasoma kama ifuatavyo; Tarehe: 09/11/2023 Mbele ya: Mhe. N.G Kachua RM Mleta Pingamizi -Yupo Mjibu Pingamizi-Yupo Mahakama- Nimepitia pingamizi lililowasilishwa na Bi Husna Senkondo na sababu alizoeleza. Pingamizi hilo aliliwasilisha katika hatua za awali za kusikiliza maombi ya msimamizi wa mirathi na baada ya kuyasikiliza nilitoa maamuzi kwa sababu mleta pingamizi ni mtu ambaye hafahamu hana taaluma ya sheria na hana muwakilishi Mahakama imemuelimisha na ameondoa pingamizi lake. AMRI- -Msimamizi wa Mirathi ajaze na 5 ya mali za marehemu Fomu na 6 ya mgawanyo wa mirathi ya marehemu Shauri kwa kuwaislisha mrejesho tarehe 6/12/2024 Ni mtizamo wangu kwamba, barua anayoirejea Hakimu ambayo alisikiliza hoja ya msimamizi kujitoa ni tofauti na barua ya tarehe 29/ 9/2023 ambayo imenukuliwa kwenye hoja za maandishi za Mleta rufaa. Pili, utaratibu huu uliotumika wa kutosikiliza hoja zilizoanishwa kwenye barua ya tarehe!29/9/ 2024 haukuwa sahihi kwasababu hoja hizo hazikusikilizwa kwenye pingamizi la tarehe 20/9/ 2024 ambapo pande zote zilipewa nafasi ya kusikilizwa na kurekodiwa kwenye mwenendo wa shauri. Katika barua ya tarehe 20/9/2023 hakukuwa na hoja ya Hakimu kujitoa. Kwa upande wa barua ya tarehe 29/9/ 2023, pande zote mbili za kesi hawakupewa nafasi ya kusikilizwa hoja zao. Hivyo ninakubaliana na wasilisho la Mleta rufaa kuwa hakupewa haki ya kusikilizwa kwenye hoja zilizowasilishwa kwenye barua ya tarehe 29/9/2023 hususani hoja ya Hakimu kujitoa. Ilikuwa ni wajibu wa Hakimu Mkazi kuweka utaratibu wa kusikiliza hoja husika kwa kutoa fursa kwa Mleta rufaa kueleza sababu zake za Hakimu kujitoa pamoja na hoja nyinginezo zilizoanishwa kwenye barua husika bila ya kujali uzito wa hoja hizo na matokeo yake na pia kutoa fursa kwa mpinga rufaa kuwasilisha * c. * hoja zake za majibu badala ya Hakimu kuwasilisha hoja husika yeye mwenyewe na kutoa uamuzi yeye mwenyewe. Aidha, haikuwa sahihi kwa Hakimu kurekodi kwenye mwenendo kuwa Mleta rufaa ameelimishwa na kuondoa hoja yake. Swali la kujiuliza ni elimu gani aliyopewa na endapo alielewa kuweza kuondoa hoja zake kwa hiyari maana hakuna rekodi inayoonesha Mleta rufaa aliondoa hoja zake yeye mwenyewe. Ni mtazamo wangu kwamba jambo hili halikuwa sahihi kwakuwa utaratibu unahitaji linapotolewa pingamizi sharti pande zote za kesi wapewe nafasi ya kuwasilisha hoja zao moja kwa moja na kurekodiwa kwenye mwenendo wa shauri namna walivyotoa hoja zao na hata pindi pingamizi linapoondolewa na mleta pingamizi sharti rekodi husika ijieleze moja kwa moja na isiwe katika mfumo wa kutolewa taarifa. Mwenendo wa shauri hili unaonesha Hakimu aliliwasilisha pingamizi mwenyewe na kulishughulikia yeye mwenyewe kwa kulitolea taarifa. Katika kufikia uamuzi huu nimezingatia kuwa, pamoja na kwamba hoja ya rufaa inarejea barua ya tarehe 20/9/2024 ambayo ilisikilizwa, nimegundua kuwa ndani ya maelezo au hoja za maandishi za mleta rufaa zinarejea barua yake ya tarehe 29/9/2024 na hoja hizi pia ziliwasilishwa katika rufaa iliyoenda Mahakama ya Wilaya. Hivyo ni sehemu ya rekodi ya Mahakama ya Wilaya na Mpinga rufaa alipata fursa ya kujibu hoja husika. Aidha, ninakubaliana na wasilisho la mleta rufaa kuwa kitendo hicho kilimnyima fusra Mleta rufaa ya kusikilizwa hoja yake ya Hakimu kujitoa na hoja nyinginezo zilizoibuliwa kwenye barua husika bila ya kujali uzito wa hoja zilizowasilishwa hata kama zilikuwa na mashiko au hazikuwa na mashiko. Hivyo kwenda kinyume na matakwa ya haki ya kusikilizwa iliyoainishwa kwenye ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri Muungano wa Tanzania, 1977. Ninakubaliana na mrufani kuwa alinyimwa haki ya kusikilizwa pingamizi lake la tarehe 29/10/2023 wa mujibu wa Ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na ninaafiki kwamba kwamba Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya zilikosea kwenye eneo hili kwa kusema kuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo alikuwa sahihi kutosikiliza shauri hilo kwakuwa barua haikuelekezwa kwake na ilielekezwa kwa Mfawidhi. Hoja hii si sahihi kama ambavyo nimeeleza hapo juu. Bado Hakimu aliyesikiliza shauri alipaswa kutoa fursa ya pande za kesi kusikilizwa moja kwa moja kwenye hoja zilizoibuliwa. Hivyo ninakubaliana na hoja hii ya kwanza na inashinda kwa kiasi hiki, kwa kuzingatia uchambuzi wangu wa barua ya tarehe 29/9/2023. Hivyo nalirejesha jalada la Mahakama ya Mwanzo Temeke Hi Mleta rufaa akasikilizwe hoja yake ya Hakimu kujitoa na nyinginezo zilizoainishwa kwenye barua ya tarehe 29/9/2023 ambayo ilipokelewa na Mahakama husika mnamo tarehe 2/10/2023. Hii itatoa fursa baada ya maamuzi kutolewa, kwa upande ambao haujaridhika kukatia rufaa masuala ambayo tayari yalikwishashughulikiwa na Mahakama ya Mwanzo badala ya hoja mpya au mbichi kwenda kushughulikiwa kwenye Mahakama za juu zinazofuata za rufaa. Hoja hii ya kwanza kwa (kiasi hiki) inatosha kumaliza usikilizwaji wa rufaa hii. Hivyo baada ya kusikiliza pande zote za kesi ninatoa amri zifuatazo; a) Rufaa inakubaliwa kwa kuzingatia hoja ya kwanza inayohusiana na maelezo ya pingamizi lililowasilishwa kupitia barua ya tarehe 29/9/2023 kutosikilizwa; b) Ninarejesha jalada la shauri la Mirathi Na. 1395/2023 Mahakama ya Mwanzo Temeke ili pingamizi lililowekwa la Hakimu kujitoa kupitia barua ya tarehe 29/9/2024 iliyopokelewa tarehe 2/10/2024, likasikilizwe na pande zote za kesi wapewe fursa ya kuwasilisha hoja zao na kusikiiizwa juu ya pingamizi hilo ikiwemo kurekodiwa kikamilifu kwenye mwenendo wa shauri kwa namna watakavyowasilisha hoja zao. c) Kutegemea na Uamuzi utakaotolewa kwa kuzingatia kipengele (b) hapo juu, hoja nyinginezo zilizoibuliwa kwenye barua ya tarehe 29/9/2023 ziwekewe utaratibu wa kusikilizwa na pande zote wapewe nafasi ya kuziwasilisha na kuzijibu. d) Hakuna amri ya gharama kwa kuzingatia uasili wa shauri hili. Haki ya kukata rufaa imeelezwa. Imeamriwa hivyo. Imetolewa leo Temeke Tarehe 29 ya Mwezi wa Kumi Mwaka 2024 S. D. MWAIPOPO JAJI 29/10/2024