john cosmas matimila vs john csmas matimila msimamizi wa mirathi ya marehem cosmas paul matimila 2023 tzhclandd 16803 24 august 2023
The application for review was filed within the prescribed time, and the Tribunal erred in allowing execution of a judgment already set aside by the High Court. The Tribunal's orders were contrary to the High Court's directives and are therefore set aside.
Source-derived case information.
- Citation
- john cosmas matimila vs john csmas matimila msimamizi wa mirathi ya marehem cosmas paul matimila 2023 tzhclandd 16803 24 august 2023
- Parties
- Appellant: John Cosmas Matimila; Respondent: John Cosmas Matimila (Administrator of the estate of the late Cosmas Paul Matimila)
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 24 August 2023
- Procedural Posture
- Land Appeal / Judgment
- Outcome
- appeal allowed
- Legal Topics
- Appeal, Limitation of Time, Execution of Judgment, Review of Decisions
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
John Cosmas Matimila
Appellant
John Cosmas Matimila (Administrator of the estate of the late Cosmas Paul Matimila)
Respondent
Procedural Posture
Land Appeal / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the application for review was filed within the prescribed time
- 2 Whether the District Land and Housing Tribunal erred in allowing execution of a judgment already set aside
- 3 Whether the Tribunal erred in failing to comply with the High Court's orders
Ratio Decidendi
The application for review was filed within the prescribed time, and the Tribunal erred in allowing execution of a judgment already set aside by the High Court. The Tribunal's orders were contrary to the High Court's directives and are therefore set aside.
Court Disposition
appeal allowed
Orders
- The decision of the District Land and Housing Tribunal for Temeke in Misc. Application No. 32/2023 dated 07/06/2023 is set aside.
- The application for review No. 32/2023 was filed within time and must be heard within sixty days from the date of this judgment.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA ARDHI DAR ES SALAAM MAOMBI YA RUFAA NA. 247 YA 2023 BAINA YA JOHN COSMAS MATIMILA............................................................. MRUFANI DHIDI YA JOHN COSMAS MATIMILA (Msimamizi wa Mirathi ya Marehemu COSMAS PAUL MATIMILA).............................................. MRUFANIWA HUKUMU 19/07/2023 & 24/08/2023 K. MSAFIRI, J. Rufaa hii inatokana na Mrufani kutoridishwa na uamuzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Temeke, katika Maombi Madogo Na. 32 ya Mwaka 2023. Chimbuko la Maombi Madogo Na. 32 ya Mwaka 2023 ni Hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu mwenye Mamlaka ya Nyongeza (Extended Jurisdiction) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni/Kinondoni, katika Rufaa ya Ardhi No. 100/2022. Rufaa hiyo iliwasilishwa Mahakamani hapo ambapo John Cosmas Matimila (Mrufani wa sasa) pia alikuwa Mrufani, akiwasilisha rufaa dhidi ya John Cosmas Matimila (Msimamizi wa Mirathi ya Marehemu Cosmas i Paul Matimila) (Mrufaniwa wa sasa) ambae pia alikuwa Mrufaniwa katika rufaa hiyo tajwa. Katika Rufaa hiyo, Mrufani alikuwa akipinga uamuzi uliotolewa na Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke, katika mashauri ya madai Maombi Na. 362/2021, na Maombi Na. 633/2021. Pia Mrufani alikuwa akipinga Mwenendo wa shauri na uamuzi wa Baraza la Kata Keko katika Shauri la Madai Na. 88/2015. Katika Rufaa Na. 100/2022 Mrufani aliiomba Mahakama kutengua na kufuta maamuzi tajwa hapo juu. Baada ya kusikilizwa pande zote mbili za madai, Mahakama chini ya Mhe. Hakimu Mkazi Mwenye Mamlaka ya Nyongeza, ilifuta na kuweka kando uamuzi na amri zote zilizotolewa na Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya Temeke katika mashauri yafuatayo; Shauri la Maombi Madogo Na. 362/2021, Shauri Na. 632/2021, Shauri Na. 633/2021 na shauri la Ukazaji Hukumu Misc. Civil Application No. 584 of 2020 ambapo mashauri haya yote yanawahusisha mrufani na mrufaniwa katika Rufaa ya sasa. Mahakama yenye Mamlaka ya Nyongeza pia ilitoa amri kuwa Mrufani anaongezewa muda wa siku 30 kuanzia siku ya hukumu ili afungue shauri la maombi ya kufanya marejeo ya Shauri Namba 88/0015 au 88/2015 iliyopo katika Baraza la Kata Keko. Hivyo katika Rufaa hiyo 2 Mrufani alishinda, na kupewa amri kufungua shauri la maombi ya Marejeo ya mwenendo na uamuzi wa Baraza la Kata Keko kwenye shauri tajwa hapo juu. Uamuzi wa Hakimu Mkazi mwenye Mamlaka ya Nyongeza Mhe. Kiswaga ulitolewa tarehe 11 Januari 2023. Kufuatia Amri hiyo, Mrufani aliwasilisha Maombi ya Marejeo Na. 32 ya 2023 mbele ya Baraza la Ardhi la Wilaya. Hata hivyo mjibu maombi (Mrufaniwa) aliibua pingamizi la awali kuwa maombi hayo yamepitwa na wakati. Alieleza kuwa katika Hukumu ya Hakimu Mkazi Mkuu mwenye Mamlaka ya Nyongeza iliyotolewa tarehe 11/01/2023, mleta maombi alipewa siku 30 ili kuleta maombi hayo lakini ameyaleta kwa kuchelewa kwa muda wa siku mbili zaidi. Baada ya kusikiliza pingamizi hilo la awali, Mwenyekiti aliesikiliza maombi hayo alikubali pingamizi hilo na kueleza kuwa mleta maombi alileta maombi yake tarehe 14/02/2023 ilhali alipaswa alete maombi hayo tarehe 11/02/2023. Mwenyekiti alikubali pingamizi hilo na kuamuru kuwa utekelezaji katika Maombi Madogo Na. 584 ya 2020 utaendelea. Uamuzi huo ulitolewa tarehe 07/06/2023. Mrufani hakuridhishwa na uamuzi huo na sasa amewasilisha Rufaa hii ikiwa na sababu tatu (3) kama inavyoelezwa hapa chini; 3 1. Kwamba, Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya lilikosea kisheria na kimantiki kutamka kuwa maombi ya mleta maombi yameletwa tarehe 14/02/2023 hivyo yamekuja nje ya muda wa siku 30. 2. Kwamba, Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya lilikosea kisheria na kimantiki kwa kukiuka amri ya Mahakama Kuu na kutamka kuwa utekelezaji wa Maombi Madogo Na. 584/2020 uendelee licha ya kuwa Mahakama Kuu ilifuta na kuweka kando nafuu zote zilizotolewa katika Maombi Namba 584/2020. 3. Kwamba, Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya lilikosea kisheria na kimantiki kwa kutoa amri ya utekelezaji wa maamuzi ambayo tayari Mahakama Kuu imetamka yana mapungufu mengi ya kisheria na yanahitaji kufanyiwa marejeo. Hivyo, mrufani anaiomba Mahakama hii itengue na kufuta uamuzi uliotolewa na Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke tarehe 07/6/2023. Pia Mrufani anaiomba Mahakama hii itoe tamko kwamba maombi ya mleta maombi yalikuja ndani ya muda na yanatakiwa kufanyiwa marejeo mbele ya Mhe. Mwenyekiti tofauti na Mhe. Chinyele. Rufaa hii ilisikilizwa kwa njia ya maandishi (written submissions), na pande zote mbili wamewasilisha hoja zao kwa muda uliopangwa. 4 Mahakama hii imezingatia hoja zote na itazifafanua wakati ikichambua sababu za Rufaa. Katika hoja zake za msingi, Mrufani alitetea sababu yake ya kwanza ya Rufaa kuwa, alipeleka maombi ya marejeo Namba 32/2023 katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya Temeke mnamo tarehe 10/2/2023, ikagongwa muhuri wa kupokelewa tarehe 10/2/2023 na ikapokelewa {admitted} siku hiyo ya tarehe 10/02/2023. Hivyo maombi hayo yalikuwa ndani ya muda. Katika uchambuzi wa sababu hii ya kwanza ya Rufaa, nimepitia kumbukumbu za Baraza la Nyumba la Wilaya na kubaini kuwa ni kweli mrufani (akiwa kama mleta maombi) aliwasilisha maombi yake ya marejeo ambayo yalisajiliwa kama Maombi ya Marejeo Na. 32 ya 2023. Maombi hayo yalipokelewa na kusajiliwa tarehe 10/02/2023. Hii inathibitishwa na wito wa faragha {Chamber Summons} iliyowasilishwa kwenye Baraza la Ardhi Wilaya, ambayo inaonesha kuwa maombi hayo yalipokelewa na kupangwa kwa Mhe. A. Sosthenes mnamo tarehe 10/02/2023. Kwa muktadha huu, kwa kuwa amri ya Mahakama Kuu chini ya Hakimu Mkazi Mkuu mwenye Mamlaka ya Nyongeza ilitolewa tarehe 11 Januari 2023, basi ni dhahiri kuwa Maombi ya Marejeo Na. 32 ya 2023 5 yalikuwa ndani ya muda. Hivyo nakubaliana na sababu ya kwanza ya Rufaa. Sababu za pili na tatu za Rufaa ziliwasilishwa kwa pamoja (consolidated), na Mrufani. Alieleza kuwa, Hukumu ya Rufaa Na. 100/2022 iliyotolewa na Mahakama hii chini ya Hakimu mwenye Mamlaka ya Nyongeza ilifuta amri na uamuzi wote uliotolewa na Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Temeke. Mrufani alinukuu maamuzi yaliyofutwa kuwa ni Shauri la Maombi Madogo Namba 362/2021, Shauri Namba 632/2021, Shauri Namba 633/2021 na shauri la ukazaji Hukumu Misc. Civil Application No. 584 of 2020. Kwa msingi huo, Mrufani alieleza zaidi kuwa Baraza la Ardhi na Nyumba katika Shauri la Maombi Madogo Na. 32/2023 lilikosea kutoa amri kuwa utekelezaji katika Maombi Madogo Na. 584/2020 unaendelea ilhali tayari maamuzi katika shauri hiyo yalishafutwa na Mahakama ya juu. Akijibu sababu za pili na tatu za Rufaa, Mrufaniwa alieleza kuwa sababu hizi ni mpya na si haki kisheria kuziibua katika hatua hii ya rufaa wakati hakuziibua mbele ya Baraza la Ardhi la Temeke. Aliomba Mahakama izitupilie mbali hoja hizo. /Vfj L - 6 Baada ya kupitia hoja za pande zote zinazobishana, ninakubaliana na hoja za Mrufani kuwa ni sahihi kuwa Baraza la Ardhi Wilaya lilikosea kisheria katika uamuzi wake kwenye Maombi Madogo Na. 32 ya Mwaka 2023 ambapo Baraza lilitoa amri kuwa utekelezaji katika Maombi Madogo Na. 584 ya mwaka 2020 uendelee. Utekelezaji katika Maombi Madogo Na. 584/2020 hauwezi kuendelea/ kufanyika kwani Mahakama Kuu katika Rufaa ya Ardhi Na. 100/2022 chini ya Mamlaka ya Nyongeza, ilifutilia mbali na kuweka kando amri zilizotolewa katika Shauri Na. 584/2020. Pia Mahakama Kuu ilimruhusu Mrufani kufungua Shauri la Maombi ya Marejeo ya Shauri Na. 88/0015 au 88/2015 ambayo ndicho chanzo cha maombi ya kukazia Hukumu Na. 584 ya 2020. Hivyo Amri ya Baraza katika Maombi Madogo Na. 32 ya 2023 kuruhusu ukaziaji hukumu katika Maombi Madogo Na. 584/2020 haitekelezeki kwani maombi hayo hayapo tena kisheria mbele ya Baraza baada ya kufutwa na Mahakama Kuu. Kuhusu hoja za mrufaniwa kuwa sababu za pili na tatu za Rufaa zimeibua hoja mpya, sikubaliani nazo. Hii ni kwa sababu za pili na tatu ni hoja za kisheria {pointsoflaw} baada ya Baraza la Wilaya kukosea kisheria na kutoa amri ya kuendelea na utekelezaji wa maamuzi ambayo tayari 7 yamefutwa na Mahakama ya juu. Sababu za pili na tatu za Rufaa nazo zimekubaliwa. Kwa msingi huo, Mahakama hii inakubali na kuruhusu Rufaa hii. Pia inatengua na kufuta uamuzi uliotolewa na Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke katika Maombi Madogo Na.32 ya Mwaka 2023 ya tarehe 15/6/2023. Mahakama hii inatamka kuwa Maombi ya Marejeo Na. 32 ya 2023 yalikuwa ndani ya muda kisheria. Maombi hayo ya marejeo ya Shauri Namba 88/0015 au 88/2015 ya Baraza la Kata Keko yapangwe na kusikilizwa mbele ya Baraza la Wilaya, Temeke ndani ya muda wa miezi miwili (siku sitini) kuanzia tarehe ya Hukumu hii. Kwa kuwa mrufani na mrufaniwa ni ndugu (Baba mdogo na mtoto), Mahakama haitoi amri ya gharama. Kila upande ujigharamie wenyewe. Inaamriwa hivyo. Haki ya Rufaa imeelezwa bayana. A. MSAFIRI JAJI 24/8/2023 8