lububu
The respondent proved ownership of the disputed land to the required standard by showing continuous possession and use since 1974, and the appellant failed to prove any government order restoring pre-ujamaa land rights. The trial tribunal's decision was correct and is upheld.
Source-derived case information.
- Citation
- lububu
- Parties
- Appellant: Joseph Lububu; Respondent: Athuman Shabani
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 1974
- Procedural Posture
- Land Appeal / Judgment
- Outcome
- Appeal dismissed with costs
- Legal Topics
- Land Ownership, Burden of Proof, Village Land Allocation, Succession
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Joseph Lububu
Appellant
Athuman Shabani
Respondent
Procedural Posture
Land Appeal / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the respondent proved ownership of the disputed land to the required legal standard
- 2 Whether the trial tribunal erred in law and fact in its evaluation of evidence
Ratio Decidendi
The respondent proved ownership of the disputed land to the required standard by showing continuous possession and use since 1974, and the appellant failed to prove any government order restoring pre-ujamaa land rights. The trial tribunal's decision was correct and is upheld.
Court Disposition
Appeal dismissed with costs
Orders
- The decision of the District Land and Housing Tribunal is upheld
- Respondent remains the lawful owner of the disputed land
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MASIJALA NDOGO YA TABORA RUFAA YA ARDHI NA. 37 GF 2023 (Inatokana na Uamuzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Nzega kwenye Shauri la Maombi ya Ardhi Na. 19 ya 2023) JOSEPH LUBUBU............. .............. ...MRUFANI DHIDI YA ATHUMAN SHABANI......... ............................. ..........MJIBU RUFAA HUKUMU Tarehe ya amri ya mwisho: 23/07/2024 Tarehe ya hukumu: 29/08/2024 MANGO, J Rufaa hii inatokana na uamuzi wa baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Nzega kwenye Shauri la Maombi ya Ardhi Na. 19 la mwaka 2023. Kumbukumbu za Mahakama zinaonesha kwamba Mjibu rufaa alifungua shauri husika dhidi ya Mrufani kwenye baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Nzega akidai umiliki wa eneo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa ekari moja na nusu. Mjibu rufaa alidai eneo la mgogoro ni mali ya Marehemu baba yake, SHABANI KIDUMULA MAKWAYA ambaye alilipata wakati wa operesheni vijiji vya ujamaa mnamo mwaka 1974. Mrufani hakupinga kwamba eneo hilo alipewa SHABANI KIDUMULA MAKWAYA wakati wa operesheni vijiji vya ujamaa, isipokuwa anadai kuwa yeye allkuwa mmiiiki wa aWali wa eneo hilo kabla ya uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa. Anadai kwamba, baada ya kuisha kwa vijiji vya ujamaa watu walirejea kwenye maeneo yao ya asili hivyo umrniiiki wa eneo la mgogoro ulirejea kwake. Baada ya kusikiza wadaawa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Nzega liliona kwamba eneo la mgogoro ni mali ya Mjibu Rufaa na lilimtamka Mjibu Rufaa kuwa mmiliki halali wa eneo lenye mgogoro. Mrufani hakuridhika na uamuzi huo hivyo amekata rufaa mbele ya Mahakama hit akiwa na sababu za rufaa zifuatazo; 1. KWAMBA baraza la ardhi na nyumba wilaya limekosea kisheria na kiushahidi kwa kushindwa kuchambua ushahidi ulioletwa kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wowote wa maneno au wa maandishi ambao uliotolewa na Mjibu Rufaa mbele ya baraza ili kuthibitisha umrniiiki wake juu eneo lenye mgogoro. 2. KWAMBA ni makosa kwa baraza la ardhi na nyumba wilaya kufanya maamuzi kwa kuangalia ushahidi wa mashahidi tu bila uwepo wa ushahidi wa maamuzi ya serikali ya kijiji kuthibitisha kwamba u mill kish waji wa eneo la mgogoro kwa mjibu maombi ulifa nywa na chombo chenye mamlaka ya kufanya hivyo. 3. KWAMBA ni makosa kwa baraza la ardhi na nyumba wilaya kufanya maamuzi kuhusiana na umilikishwaji wa ardhi kwa kutegemea ushahidi wa mashahidi pekee bila kuona muhtasari wa kikao cha serikali ya kijiji kilichoruhusu au kuamua kuhusu umilikishwaji wa ardhi huslka. 4. KWAMBA baraza la ardhi na nyumba wilaya limekosea kisheria na kiushahidi kufanya maamuzi kwenye mgogoro wa ardhi husika bila 2 kuliunganisha baraza la kijiji ambalo lilimilikisha Mjibu rufaa ardhi husika. 5. KWAMBA baraza la ardhi na nyumba wilaya Ijmekosea kisheria na kiushahidi kumtamka Mjibu rufaa kuwa mmiliki wa eneo lenye mgogoro wakati Mjibu rufaa hakuweza kuthibitisha umiliki wake kwenye eneo husika. Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hii, Mrufani aliwakilishwa na Wakili msomi Emmanuel Musyani na Mjibu rufaa aliwakilishwa na Wakili msomi Edward Malando. Rufaa hii ilisikilizwa kwa njia ya maandishi. Kwenye maelezo yake ya kimaandishi, wakili wa Mrufani alielezea sababu moja tu ya rufaa inayohusu udhaifu wa ushahidi wa Mjibu rufaa kwenye kuthibitisha umiliki wake kwenye eneo husika. Wakili msomi alibainisha baadhi ya mambo yanayoonesha udhaifu kwenye ushahidi wa Mjibu Rufaa ambaye ndiye aliyekuwa mleta maombi mbele ya Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya. Kwa mujibu wa hoja za Wakili wa Mrufani, jambo la kwanza lenye kuonesha udhaifu kwenye kesi ya Mjibu rufaa ni kushindwa kuleta ushahidi kutoka kwenye Serikali ya Kijiji ambao unaoonesha kijiji kilimgawia ardhi husika Mjibu rufaa au baba yake. Wakili aliongeza kwamba, Mjibu rufaa hakuweza kuleta nyaraka yoydte kutoka Serikali ya Kijiji wala kumleta shahidi yoyote kutoka uongozi wa kijiji ambaye angeweza kuthibitisha umilikishwaji wa ardhi husika kwa mjibu rufaa au baba yake. Wakili wa Mrufani pia ameongelea udhaifu kwenye ushahidi wa Anthony John Msabil (SM2)? shahidi wa Mjibu Rufaa. Wakili ameeleza kuwa, kwa 3 mujibu wa ushahidi wake, shahidi huyu hakuwa anajua chochote kuhusu eneo la mgogoro. Wakili alimalizia kwa kukumbusha jukumu la kuthibitisha madai ni la mdaawa aliyefungua shauri mahakamani na kwamba lilikuwa jukumu la Mjibu rufaa kuleta ushahidi kuthibitisha madai yake juu ya umiliki wa ardhi husika. Na kwamba kama Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya lingeangalia kwa umakini ushahidi wa Mjibu rufaa lisingeweza kumtamka kuwa mmiliki wa eneo la mgogoro Akijibu hoja za Mrufani, wakili wa Mjibu rufaa alisisitiza kuwa suala la baba wa Mrufani kupewa eneo la mgogoro na serikali wakati wa operesheni vijiji sio bishaniwa. Wakili ameeleza kuwa suala hilo limethibitishwa na ushahidi wa Mjibu rufani na shahidi wake, pamoja na shahidi wa Mrufani Leonard Mshamindi. Wakili wa Mjibu rufani ameeleza kwamba kwa ushahidi wa namna hii, Mrufani hawezi kudai kwamba Mjibu rufaa hakuthibitisha umiliki wake kwenye eneo husika. Wakili ameongeza kwamba iwapo eneo husika lingekuwa ni la Mrufani basi angelidai katika kipindi cha mwaka 1974 hadi 2014 wakati eneo husika likitumiwa na baba na mama wa Mjibu rufaa. Wakili ameeleza zaidi kuwa hata kama Mjibu rufaa angekuwa ameingia kwenye eneo la mgogoro kwa uvamizi bado kwa muda aliokaa kwenye eneo husika Mjibu rufaa atakuwa amejipatia umiliki wa eneo husika kupitia matumizi ya muda mrefu ya ardhi husika. Wakili amehitimisha kwa kusema kwamba hoja za Mrufani hazina mashiko Mrufani hakuwa na majumuisho. 4 Nimezingatia hoja zilizoletwa na -panda zote mbili pamoja na kumbukumbu za mahakama ambazo ni mwenendo wa shauri kutoka Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya. Jambo kubwa linalobishaniwa kwenye rufaa hii ni iwapo Mjibu rufaa ambaye ndiye alikuwa Mleta Maombi mbele ya Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya amethibitlsha umiliki wa eneo husika kwa kiwango kilichowekwa na sheria ambacho ni urali wa mizania. Ushahidi uliopelekwa mbele ya Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya unaonesha kwamba, eneo husika ni sehemu za mali zilizoachwa na Marehemu Shabani Kidawale. Ushahidi unaothibitisha hilo unapatikana kutoka kwa mashahidi watatu waliotoa ushahidi wakati wa usikilizwaji wa shauri hili mbele ya Baraza la Ardhi na Nyumba. Ushahidi wa Mjibu Rufani ambaye alitoa ushahidi wake kama shahidi wa Mdai No.l unaonesha kwamba eneo husika limekuwa mali ya baba yake mnamo waka 1974 kupitia Operesheni Vijiji na kwamba wazazi wake wamelitumia eneo hilo hadi mwaka 2014 ndipo mgogoro ukaanza. Mgogoro ulianza mara tu baada ya kifo cha mama mzazi wa Mjibu Rufaa. Maelezo yanayofanana na ya Mjibu Rufaa yalitolewa na Mrufani, Joseph Lububu (SU1) na Shahidi wake Leonard Mshamindi (SU2). Kwa mujibu wa ushahidi wa Mrufani, hapingi kwamba eneo husika alipewa baba wa Mjibu Rufaa. Anaeleza wazi kama inavyoonekana kwenye ukurasa wa tisa wa mwenendo wa shauri uliochapwa kwamba Shabani alipewa eneo husika na Seri kali ya kijiji. Maelezo hayo yanaonekana kwenye ushahidi wa SU2 ukurasa wa 11 wa mwenendo wa shauri uliochapwa. Maelezo hayo yanathibitisha wazi kwamba eneo husika limekuwa likitumiwa na Shabani Kidawale na familia yake tangu mwaka 1974 hadi 2014 ulipoibuka mgogoro huu. Ni wazi pia, Mrufani anajarlbu kudai kurudishiwa eneo husika kwa madai kwamba lilikuwa eneo lake kabla ya operesheni vijijL Kwa mujibu wa maelezo ya Mrufani na SU2, ni kwamba baada ya kumalizlka kwa operesheni vijiji, watu waiiamuriwa na Serikali warudi kwenye maeneo yao. Kwa maana nyingine, Mrufani naye anajaribu kurudi kwenye eneo ambalo inadaiwa alikuwa akilimiliki kabla ya operesheni vijijL Sheria ya ushahidi, kupitia Kifungu 110(1) &(2) inampa jukumu anayeleta madai kuweza kuyathibitisha. Kwakuwa Mrufani ndiye aliyedai uwepo wa amri ya Serikali iliyowataka wananchi waliokuwa kwenye vijiji vya ujamaa kurudi kwenye maeneo yao ya awali, alipaswa kuthibitisha uwepo wa amri hiyo ambayo ndiyo inayojenga msingi wa madai yake dhidi ya Mjibu Rufaa. Kwa bahati mbaya, Mrufani hakuthibitisha uwepo wa amri hiyo ya serikali. Kimsingi, operesheni vijiji na vijiji vya ujamaa havikuwahi kufutwa Tanzania wala hakuna amri yoyote iliyowataka wananchi warudi kwenye maeneo yao waliyokuwa wakiishi kabla ya operesheni vijiji. Vijiji vya ujamaa Tanzania vilipoteza tu umaarufu wake kwa sababu ya changamoto mbalimbali. Hivyo kulazimisha mwananchi ambaye, hakuna ubishi kuwa alipewa ardhi na kijijj, kuhama eneo husika ili kumpisha aliyedaiwa kulitumia eneo husika kabla ya kuanzishwa kwa vijiji hakuwezi kubarikiwa na Mahakama hii. Swali muhimu nililojiuliza ni je kwa ushahidi huu, Mjibu Rufaa alifanikiwa kuthibitisha madai ya kwa kiwango cha urari wa mizania kama ilivyoelekezwa na Kifungu Na. 110(l)&(2) cha sharia ya Ushahidi, Sura ya 6 ya sharia za Tanzania kama ilivyorejewa mwaka 2022 na mashauri mbalimbali ikiwepo 6 shauri la Barelia Karangirangi dhidi ya Asteria Nyalambwa (Shauri la Madai la Rufani Na. 237 of 2015) [2019] TZCA 51 (1 April! 2019) Kwa kuzingatia ushahidi wa Mjibu Rufaa nilioueleza kwenye uamuzi huu, nakubaliana na Wakili wa Mjibu Rufaa kwamba Mjibu Rufaa amethibitisha kwa kiwango kinachotakiwa kisheria kwamba ardhi husika ni sehemu ya mirathi ya Marehemu Shabani Kidumula Makwaya. Kwa sababi hiyo sioni sababu yoyote ya kubadilisha maamuzi ya Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ambalo limemtamka Mjibu Rufaa ambaye ni msimamizi wa mirathi ya Marehemu Shabani Kidumula Makwaya kuwa mmiliki halali wa eneo bishaniwa. Hivyo, rufaa hii inatupiliwa mbali kwa gharama. Imetolewa leo tarehe 29 mwezi wa Nane mwaka 2024 JAJI