JOSEPHAT SALIGE WANKA RUFAA KISWAHILI
The appeal was dismissed because the appellant failed to demonstrate any legal or procedural error by the lower courts. The revocation of the appellant as administrator was justified, the will was properly scrutinized as a legal issue, and all parties were accorded procedural fairness. Minor discrepancies in party...
Source-derived case information.
- Citation
- JOSEPHAT SALIGE WANKA RUFAA KISWAHILI
- Parties
- Appellant: Josephati Salige Wanka; Respondent: Aphayo Mgaya Wanka
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2024
- Procedural Posture
- Civil Appeal / Judgment on Second Appeal
- Outcome
- Appeal dismissed
- Legal Topics
- Revocation of Administrator of Estate, Validity of Will, Procedural Fairness in Appeals
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Josephati Salige Wanka
Appellant
Aphayo Mgaya Wanka
Respondent
Procedural Posture
Civil Appeal / Judgment on Second Appeal
Legal Issues
- 1 Whether the lower courts erred in revoking the appellant as administrator of the estate
- 2 Whether the will presented was valid and properly considered
- 3 Whether procedural fairness was accorded in the appellate process
Ratio Decidendi
The appeal was dismissed because the appellant failed to demonstrate any legal or procedural error by the lower courts. The revocation of the appellant as administrator was justified, the will was properly scrutinized as a legal issue, and all parties were accorded procedural fairness. Minor discrepancies in party names were clerical and did not affect the substance or outcome.
Court Disposition
Appeal dismissed
Orders
- Appeal is dismissed for lack of merit
- Decisions of the lower courts are upheld
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MASJALA NDOGO YA SHINYANGA ILIYOPO SHINYANGA RUFAA YA MADAI Na 21620 ya Mwaka 2024 (Imetokana na hukumu katika rufaa namba 16273 ya mwaka 2024 katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga mbele ya Mhe Y.Zahoro SRM tarehe 05/08/2024) JOSEPHATI SALIGE WANKA ………………………….....……..........MRUFANI DHIDI YA APHAYO MGAYA WANKA……….………….…………………..........MRUFANIWA HUKUMU Tarehe 1st & 31st Oktoba 2024 F.H. MAHIMBALI – JAJI Mrufani hakuridhika na maamuzi ya Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga katika rufaa namba 16273/2024 mbele ya Mhe. Zahoro SRM ya tarehe 05/08/2024. Katika shauri la msingi, Mrufaniwa aliweka pingamizi katika Mahakama ya Mwanzo Chibe akiomba mrufani atenguliwe kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu MGAYA WANKA MGAYA kwa sababu wosia uliowasilishwa mahakamani ni batili lakini pia ameshindwa kuwa mwaninifu na mkweli na ameshindwa kutekeleza majukumu kama msimamizi wa mirathi na baadae Mahakama ikaona kuna sababu ya msingi ya kumtengua mrufani kuwa msimamizi wa mirathi ya 1 marehemu na maamuzi hayo yaliungwa mkono na maamuzi ya Mahakama ya Wilaya. Mrufani hakuridhika na maamuzi hayo ya Mahakama ya Wilaya kubariki maamuzi ya mahakama ya mwanzo na hivyo kupelekea uzao wa rufaa hii. Katika kupinga uamuzi wa Mahakama ya wilaya, mleta rufaa amefika mbele ya Mahakama hii akiwa na sababu zifuatazo;- 1. Kwamba, Mh Hakimu alijielekeze vibaya kisheria na kimantiki kwa kutolea maamuzi sababu za rufaa ambazo hazikufafanuliwa na mrufani wakati wa kusikiliza shauri lake. 2. Kwamba, Mh Hakimu alijielekeza vibaya kisheria na kimantiki kwa kushindwa kumwelekeza mrufani afafanue sababu za rufaa na si hoja nyingine. 3. Kwamba, Mh Hakimu alijielekeza vibaya kisheria na kimantiki kwa kutoa hukumu ambayo wadaawa wake walikuwa ni tofauti na wadaawa katika mwenendo wa kesi Na. 202407091000016273 nakala ya tarehe 6/8/2024 4. Kwamba, Mh.Hakimu alijielekeza vibaya kisheria na kimantiki kwa kuchambua mwenyewe sababu za mrufani ambao hazikupingwa na mrufaniwa wakati wa kusikiliza rufaa hiyo. Hukumu hiyo inaonesha 2 kutumika kwa nguvu za mahakama na si ushaidi au uzito wa hoja za mrufaniwa alizozitoa wakati wa usikilizaji wa rufaa hiyo. 5. Kwamba, Mh. Hakimu alijielekeza vibaya kisheria na kimantiki kwa kutolea maamuzi suala la wosia ambalo halikuwa kwenye sababu za rufaa za mrufani na halikubishaniwa katika shauri la mirathi lililosikilizwa katika mahakama ya mwanzo Chibe. Rufaa ilisikilizwa kwa mawasilisho ya moja kwa moja Mahakamani na pande zote zilisimamia rufaa hii bila kuwa na uwakilishi. Kwa upande wa Mrufani, alieleza kwamba anaomba sababu zake za rufaa alizowasilisha katika rufaa hii zichukuliwe kama sehemu ya mawasilisho yake. Mrufani alianza kufafanua sababu ya kwanza, kwamba Mhe. Hakimu hakumpa kabisa nafasi ya kufafanua sababu zake za rufaa zote nne. Kwa kutokufafanuliwa kwake, zilitia dosari maamuzi ya Mahakama. Hivyo ilikiuka haki yake ya msingi ya kufafanua hoja moja baada ya nyingine. Kuhusiana na hoja namba mbili, ufafanuzi wake ni kuwa sababu zake ni nne tu na hakuna sababu ya wosia aliyozungumzia. Hivyo kwa hakimu kuibua hoja ngeni na hoja hiyo kuwa ndiyo ya msingi katika 3 kuendesha shauri hilo ambayo haikuwa imekatiwa rufaa iliathiri sana hukumu ya kesi husika. Kwenye sababu ya tatu, hoja yake ni kuwa majina ya wadaawa katika rufaa hiyo (Hukumu) inatofautiana na wadaawa halisi wa kesi husika. Kwamba katika mwenendo wa kesi, wadaawa walikuwa ni Joseph Salige Wanka na Mgaya Wanka Mgaya. Lakini hukumu ya wilayani ina majina ya Josephati Salige Wanka dhidi ya Alphayo Mgaya Wanka. Kwa tofauti hii ya majina, hukumu ina walakini. Kwa sababu hii, inatosha kabisa kubatilisha uamuzi. Kuhusu sababu na 4 ya rufaa; hoja ni kuwa ushahidi wake haukuwa wa mdomo bali wa nyaraka ambazo nazo zimeandaliwa na Mahakama. Kwamba ushahidi wake ulitegemea zaidi wadaawa katika shauri hili na kwenye ugawaji wa mali tumeshirikiana nao kwa upendo kabisa. Kimsingi badala ya mjibu rufaa kujibu hoja zake, Mahakama ndiyo ikawa wakili wake wa kumsemea na kwamba hiyo haikuwa sawa kabisa kisheria. Sababu na.5, hoja yake ni kuwa Hakimu alijielekeza vibaya kabisa katika shauri la wosia kwenye jambo ambalo hakulikatia rufaa na wala halikua sehemu ya mjadala wa kesi na mahakama kuipa uzito mkubwa. 4 Kwa sababu hizo, anaomba sana Mahakama hii ikubaliane na rufaa ili kufuta uamuzi wa Mahakama ya wilaya. Kwa upande wa mjibu rufaa alijibu hoja ya kwanza kwamba mrufani alipewa fursa nzuri kabisa ya kufafanua sababu zake za rufaa na hivyo anashangaa hapa anageuka. Kuhusu sababu ya pili, si ya kweli, maana kila mtu alipewa fursa kama alivyopatiwa hapa Mahakamani – leo. Hata hivyo hakumbuki kama kuna hoja yoyote iliachwa bila kufafanuliwa. Kwenye hoja ya majina ya wadaawa, anasema hajaona utata mkubwa. Maana majina halisi katika PC yalikuwa ni Josephat Salige Wanka dhidi ya Mgaya Wanka Mgaya ( Marehemu). Hivyo sioni kama ni shida ya msingi. Hali kadhalika kwenye hoja ya kwamba hakujibu hoja zake bali zilijibiwa na mahakama siyo kweli kabisa na alizijibu kwa ufasaha. Kuhusiana na hoja ya wosia kuwa ngeni, hiyo si kweli maana hoja hii ya wosia kwanza ni jambo la kisheria hivyo linawezaibuliwa wakati wowote ule. Hata hivyo suala hili pia limeshajitokeza sana hata PC kuhusiana na jambo hili na hivyo si jambo geni. 5 Kwa majibu haya, anaomba mahakama hii kutupilia mbali kabisa rufaa hii kwa gharama kwa sababu haina mashiko. Hata hivyo mrufaniwa alileza kuwa mrufani ni baba mkubwa na anataka pesa za marehemu zitumike hadi kujengea ndugu zake na yeye mwenyewe. Wao walio wengi wanahitaji fedha iliyobaki katika akaunti ya Mahakama itumike kuwasomesha na kitendo cha mrufani kutaka kutumia fedha kwa ajili ya manufaaa ya ndugu zake ni ufujaji wa dhahiri kabisa wa fedha za marehemu. Sambamba na hilo, aliendelea kueleza kwamba mrufani aachane tu na mirathi hii aendele na shughuli zake na huu wosia kiuhalisia ni wa dhulumati kabisa ndiyo maana waliupinga na kuukosoa. Kwanza wosia wenyewe ni mwandiko wa mrufani na rufaa hii itupiliwe mbali kwa kukosa mashiko. Hali kadhalika mrufani alieleza kwamba kwakuwa wosia haukupingwa si halali kuibiliwa sasa. Hata hivyo alileza kwamba yeye si mnufaika bali ni msimamizi tu wa mirathi. Alphayo ni mla unga na mvuta bangi na amekataa chuo na mrufani anasema yeye ni msimamizi wa wosia na kila kitu kimeelezwa bayana. 6 Hivyo mrufani anaomba Mahakama hii itengue usimamizi wa mirathi wa huyu mrufaniwa kwa kuwa eti ni mpuuzi kabisa si vema akaendelea kusimamia mirathi hii. Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili na kupitia kumbukumbu za Mahakama, Mahakama hii imejiuliza swali Je rufaa hii ina mashiko au la. Ni msimamo wa kisheria kwamba shauri la rufaa kwa mara ya pili, mahakama hiyo inayosikiliza rufaa ya pili haipaswi kwenda kinyume na maamuzi ya mahakama za chini zilizotoa maamuzi linganifu kwenye shauri husika labda tu kama kuna dosari za kisheria, mahakama yaweza kuingilia na kurekebisha kasoro hizo. Msimamo huo unasadifiwa kwenye maamuzi mbalimbali kama vile; Abdallahman Athuman v. Republic, Criminal Appeal No. 149 of 2014; Omari Mussa Juma v. Republic, Criminal Appeal No. 73 of 2005; 8 Josephat Shango v. Republic, Criminal Appeal No. 62 of 2012; and Yohana Dioniz and Another v. Republic, Criminal Appeals No. 114 and 115 of 2009(all unreported). Kabla ya kujibu hoja hizo Mahakama itajikita kwenye matakwa ya kisheria chini ya Kanuni ya 1 (2) cha Sheria ya Ushaidi Mahakama za Mwanzo GN No. 22 ya Mwaka 1964 kwamba mdaawa 7 anayeomba kupewa ushindi lazima athibitishe madai yake katika viwango toshelevu vya ulinganifu wa mizani. Matakwa hayo ya kisheria yalielezwa na mwandishi maarufu Sarkar, katika kitabu chake cha Sheria za Ushaidi Toleo la 18 kilichochapishwa na Lexis Nexis ukurasa wa 1896 (the legendary authors of Sarkar on Sarkar's Laws of Evidence, 18 Edn., M.C. Sarkar, S.C. Sarkar, and P.C. Sarkar, published by Lexis Nexis, katika ukurasa wa 1896) alieleza kwamba wajibu wa kuthibitisha madai ni kwa mdaawa anayeomba kupewa ushindi na si kwa mdaawa anayekana madai hayo. Halikadhalika pia, matakwa hayo yalielezwa katika shauri la ANTHONY M. MASANGA dhidi ya PENINA (MAMA MGESI) & LUCIA (MAMA ANNA), rufaa ya madai Namba .118 ya 2014 Mahakama ya Rufani ya Tanzania (haijaripotiwa). Katika kujibu sababu za rufaa ,Mahakama hii itajibu sababu moja baada ya nyingine. Kwa kuanza na sababu ya kwanza ya rufaa, kwamba, Mh Hakimu alijielekeze vibaya kisheria na kimantiki kwa kutolea maamuzi sababu za rufaa ambazo hazikufafanuliwa na mrufani wakati wa kusikilza shauri lake. 8 Mrufani alieleza hakuwepa nafasi ya kufafanua sababu zake za rufaa na hivyo kutia dosari katika maamuzi. Wakati huo mjibu rufaa akisema mrufani alipewa fursa nzuri kabisa ya kufafanua sababu zake za rufaa na hivyo anashangaa hapa anageuka. Mahakama hii imezingatia hoja zilizowasilishwa na wadaawa na kupitia kumbukumbu za mahakama cha chini na kubaini kwamba pande zote mbili zilipewa nafasi ya kufafanua sababu za rufaa lakini ushaidi wa mjibu rufaa ukawa mzito zaidi kuliko wa mrufani. Katika shauri la HEMEDI SAIDI vs MOHAMED MBILU (1984) TLR 113, Mahakama iliamua kwamba mdaawa mwenye ushaidi mzito na wa kuaminika unaothibitisha madai yake katika mizani na viwango toshelevu ndiye anapaswa kupewa ushindi. Aidha ni msimamo wa kisheria kwamba kumbukumbu za mahakama zinahesabika kuwa halali na halisi kwa namna zilivyo chukuliwa na kuhifadhiwa. Sitegemei kwa Mhe Hakimu kutenda kinyume na kiapo chake cha uhakimu ambacho kinamtaka kuwa mwadilifu na mwenye weledi mkubwa. Ikumbukwe kuwa uandishi wa mwenendo kwenye mashauri ni taaluma ya kipekee na inapaswa kuheshimiwa, siyo kila kitu anachoeleza mdai kinapaswa kunakiliwa bali hakimu au jaji hunakili vitu muhimu vitakavyomsaidia kufikia maamuzi ya haki, huo ni msimamo 9 katika shauri la; Halfani Sudi vs Abieza Chichili [1998] TLR 527 and Hellena Adam Elisha @ Hellen Silas Masui vs Yahaya Shabani & Another [2021] TZCA 669 (TANZLII). Kutokana na ufafanuzi huo, mahakama hii bila kuwa na wasiwasi inatamka kwamba wadaawa walipewa haki ya kusikilizwa na kufananua sababu za rufaa na ushaidi wa mjibu rufaa ulikuwa mzito zaidi kuliko wa mrufani na hivyo sababu ya kwanza ya rufaa haina mashiko na inatupiliwa mbali kwa mrufani kushindwa kuonyesha namna alivyonyimwa hiyo nafasi ya kufafanua hoja tajwa. Sababu ya pili ya rufaa kwamba, ni eti Mhe Hakimu alijielekeza vibaya kisheria na kimantiki kwa kushindwa kumwelekeza mrufani afafanue sababu za rufaa na si hoja nyingine. Mrufani alieleza kwamba Mahakama iishindwa kumuelekeza afafanue sababu za rufaa. Mjibu rufaa alipinga hoja hiyo akisema kila mtu alipewa fursa kama walivyopatiwa mbele ya mahakama hii na hakumbuki kama kuna hoja iliachwa bila kufafanuliwa. Kwa mjibu wa Ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na katika shauri la I.P.T.L. v . Standard Chartered Bank (Hong Kong) LTD, Civil Revision No.1 of 2009 (unreported) vinaeleza wazi kwamba hakuna 10 chombo chochote cha utoaji haki kinapaswa kutoa maamuzi yanayoathiri haki za watu bila kuwasikiliza. Kutokana na mawasilisho ya pande zote mbili na kumbukumbu zilizomo katika jalada husika ni dhahiri kwamba mrufani ndiye aliyepeleka rufaa wilayani na hivyo siyo wajibu wa mahakama kumwelekeza namna gani afanunue sababu za rufaa bali ni kumpa haki ya kumsikiliza atoe ufafanuzi mwenyewe kwenye sababu za rufaa na si vinginevyo na haki hiyo ilifafanuliwa vilivyo na mahakama ya wilaya. Hivyo kwa kuzingatia ufafanuzi huo, mahakama hii inaona kwamba sababu ya pili ya rufaa haina mashiko pia inatupiliwa mbali kwa muktadha wa kukosa mashiko. Kwa sabubu ya tatu, kwamba Mh Hakimu alijielekeza vibaya kisheria na kimantiki kwa kuota hukumu ambayo wadaawa wake walikuwa ni tofauti na wadaawa katika mwenendo wa kesi Na. 202407091000016273 nakala ya tarehe 6/8/2024 Mrufani alieleza kwamba majina ya wadaawa katika rufaa hiyo (Hukumu) inatofautiana na wadaawa halisi. Alifafanua kua awali ilikuwa ni Josephati Salige Wanka dhidi ya Mgaya Wanka Mgaya. Lakini wilayani ikawa ni Josephat Salige Wanka dhidi ya Alphayo Mgaya Wanka na utofauti huo wa majina ni sababu tosha ya kubatilisha 11 maamuzi ya Mahakama hiyo. Mjibu rufaa, katika kujibu hoja hii, alieleza kwamba hakuna utata kuhusiana na majina ya wadaawa kwa sababu majina halisi katika Mahakama ya Mwanzo yalikuwa ni Josephat Salige Wanka dhidi ya Mgaya Wanka Mgaya ( Marehemu) na hivyo hakuna shida yoyote. Kwa mjibu wa Kanuni ya 9 (2) (e) ya Kanuni za Usimamizi wa Mirathi Mahakama ya Mwanzo, za Mwaka 1964, Nyongeza ya tano ya Sheria ya Mahakama za Mahakimu Sura 11 Marejeo mwaka 2019, Mahakama inapomtengua msimamizi wa mirathi, mahakama inaweza kumteua mrithi,mnufaika au mtu yeyote kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu. Kutokana na mawasilisho ya pande zote mbili na kurejea kumbukumbu za mahakama ya chini ni ukweli kwamba katika shauri la mahakama ya mwanzo mwombaji alikuwa Josephat Salige Wanka dhidi ya Mgaya Wanka Mgaya (marehemu) na hakuna ubishi pia kwamba mjibu rufaa (Alphayo Mgaya Wanka) alipeleka ombi la kumtengua mrufani na lilikubaliwa na mrufani akakata rufaa kwenda wilayani dhidi ya maamuzi hayo. Kwa msingi huo lazima majina katika mahakama ya wilaya yatofautiane na mahakama ya mwanzo kwa sababu mrufani 12 alitenguliwa na kuteuliwa mjibu rufaa (Alphayo Mgaya Wanka) na hivyo sababu yake ya rufaa inatupiliwa mbali na haina mashiko yoyote. Ikumbukwe pia kwamba wakati mrufani anafungua shauri mahakama ya mwanzo alifungua shauri lisilo na ubishani (Probate Cause not a suit). Kwa hivyo hapakuwepo na wadaawa wawili, lakini mara baada ya mjibu rufaa kumpinga na kuomba mahakama imtengue mrufani, shauri lilibadilika nakuwa shauri bishaniwa (contentious not a cause) ambalo lilipelekea wadaawa kubadilka. Katika mashauri ya mirathi ni kawaida sana hali hii kutokea na wala hakuna dosari kisheria. Hivyo sababu ya tatu ya mrufani haina mashiko. Aidha kuhusu kasoro za jina la mrufani kutosomeka Josephat Salige Wanka na badala yake kupata ubatizo wa jina la Josephati Salige Wanka. Ni kweli kua jina la Josephat Salige Wanka ni tofauti kisheria na jina la Josephati Salige Wanka na hivyo linaweza kumaanisha mtu mwingine kisheria. Hata hivyo, kila kesi huamuliwa kutokana na mazingira yake. Kwa mazingira ya kesi hii, kosa hilo halikusababishwa na mjibu rufaa au mrufani bali ni Mahakama yenyewe tena wakati wa kuandika hukumu. Kasoro hiyo naichukulia kama ni makosa tu ya uchapaji/uandishi ambayo nafuu yake kama kuna mtu ameathirika ni kuomba tu jina hilo lirekebishwe lakini siyo hoja eti hukumu hiyo ni batili. Huo ni upofu wa kufikiri. 13 Kuhusu sababu na 4 ya rufaa kwamba, Mhe. Hakimu alijielekeza vibaya kisheria na kimantiki kwa kuchambua mwenyewe sababu za mrufani ambao hazikupingwa na mrufaniwa wakati wa kusikiliza rufaa hiyo. Hukumu hiyo inaonesha kutumika kwa nguvu za mahakama na si ushaidi au uzito wa hoja za mrufaniwa alizozitoa wakati wa usikilizaji wa rufaa hiyo. Mrufani alieleza kwamba mahakama ya wilaya iligeuka kuwa wakili wa mjibu rufaa na kumsemea sababu zake za rufaa, jambo ambalo si sawa kisheria. Wakati huo mjibu rufaa akieleza kwamba mahakama haikumjibia sababu za rufaa bali alizijibu yeye mwenyewe kwa ufasaha. Mahakama hii imepitia hoja za pande zote mbili na kuonanisha na kumbukumbu za mwenendo na kugundua kwamba wadaawa walipewa nafasi na kueleza na kujibu sababu za rufaa na hakuna mahali kwenye kumbukumbu za mahakama zinaonesha kwamba mahakama ya wilaya iligeuka kuwa wakili na kumjibia mjibu rufaa sababu zake. Kumbukumbu za Mahakama ya Wilaya wakati wa usikilizaji wa rufaa inaonyesha mambo yafuatayo: 14 Your honor, I pray to submit as per his petition of appeal. Your honor the trial court in dealing with the objection against the appellant, the court was proper on that. In the second ground of appeal the appellant withdrew from doing his main obligation as administrator by being arrogant and started doing his work basing on some of beneficiaries and isolate others. Your honor, the appellant has given opportunity to bring witnesses and exhibits however has not done so. Your honor, on third ground of appeal, it is true that the appellant has not mentioned other properties of deceased including the motorcycle of the deceased which is in hands of my brother Abel. I have registration card of the said motorcycle. Your honor, I pray the primary court decision to be upheld as the previous administrator has failed to perform his duties and basing only to some beneficiary and ignore the rest and the said will to be cancelled as signed by beneficiaries including Abel, my brother, Josephat Salige Wanka, the 15 brother of the deceased and Nyamkwe, the brother of deceased who is beneficiary of the will. Your honor, the will does not bear the signature of the testator and not appointed the executor. Your I did not agree with will and no any record to prove that I was agreeing with stated will. Your honor, the will was not private as the son of the deceased, Abel has been a witness. I pray the will be cancelled and primary court’s decision to be set aside. Kwasababu ya ukweli huu wa kumbukumbu za mwenendo katika Mahakama ya Wilaya, sababu ya nne ya rufaa pia haina mashiko hivyo inatupiliwa mbali kwa kukosekana ushahidi wa kimwenendo huo. Kwa kumalizia na sababu ya tano ya rufaa, kwamba Mhe. Hakimu alielekeza vibaya kisheria na kimantiki kwa kutolea maamuzi suala la wosia ambalo halikuwa kwenye sababu za rufaa za mrufani na halikubishaniwa katika shauri la mirathi lililosikilizwa katika mahakama ya mwanzo Chibe. Mrufani alieleza kwamba mahakama ya wilaya ilijadili hoja ya wosia na kuitolea maamuzi wakati haikuwa sababu ya rufaa na 16 haikubishaniwa katika mahakama ya mwanzo. Kwa upande wake, mjibu rufaa alisema hoja ya wosia si suala geni na ni jambo la kisheria hivyo linawezaibuliwa wakati wowote ule na suala hilo liliibuliwa mahakama ya mwanzo. Kutokana na mawasilisho na kurejea kumbukumbu za mahakama ni wazi kwamba mahakama katika ngazi ya rufaa lazima ipitie kumbukumbu zote za mahakama ya chini na kuangalia kama ushaidi ulizingatiwa na kunapokuwa na jambo ambalo ni la msingi na halijazungumziwa, mahakama inayosikiliza rufaa lazima iingilie kati kupitia ushaidi ili haki iweze kutendeka kama ilivyoelezwa kwenye kesi ya Paulina Samson Ndawanya vs Theresia Thomas Madaha,Civil Appeal No. 45 of 2017 CAT Mwanza. Aidha ni takwa la kisheria kwamba swala la kisheria linaweza kuibiliwa wakati wowote. Rejea maamuzi ya; A/S Noremco Construction vs Dar es Salaam Water and Sewage Authority (DAWASCO) Commercial Case No. 47 of 2009. Zaidi ya hayo, si kweli kama anavyoeleza mrufani kwamba hoja ya wosia haikua imeibuliwa kwenye rufaa, anasahau kuwa sababau moja wapo ya pingamizi mahakama ya mwanzo ilikua wosia kuwa siyo halali. Kwahivyo uamuzi wa mahakama ya mwanzo ulikua imegusia swala la 17 wosia na kuathiri pande zote. Kwa mantiki hiyo kwakuwa lilikua jambo la kisheria na kwakuwa liligusa maamuzi yaliyokatiwa rufaa ilikua lazima mahakama ya wilaya kulizungumzia kwa maslahi mapana ya pande zote mbili. Kwa msingi huo na kwa maslahi mapana ya haki ya shauri hili, swala la wosia ni hoja ya kisheria na mahakama ilitimiza wajibu wake wa kupitia ushaidi wa mahakama ya chini ili kujiridhisha na uhalali wa wosia huo na kutolea maamuzi suala hilo, hivyo sababu ya tano haina mashiko na inatupiliwa mbali. Sambamba na hayo, hoja ya kwamba mrufani ni mla unga na mvuta bangi na amekataa chuo, chokoraa na ni mpuuzi hafai kusimamia mirathi haijathibitishwa na mrufani ili ionekane ni sababu ya msingi ya kumtengua mrufani, badala yake huenda mrufani kwa mwamvuli wa kuwa Msimamizi wa Mirathi anataka kutumia mali za marehemu kwa ajili ya kuwajengea nyumba ndugu zake kwa kigezo kwamba anasimamia wosia wa marehemu ambao mahakama imeshautangaza kuwa batili. Niwarai mrufani na mrufaniwa kuwa linapokuja swala la usimamizi wa mirathi ni vyema wakashikamana ili kurahisisha mchakato kukamilika kwa wakati. Haileti afya kwa ndugu kugombania mali za marehemu tena kwa baba mkubwa kuonekana unakandamiza haki za Watoto wa 18 marehemu. Kwakuwa warithi halali ni Watoto wenyewe wa marehemu ni vyema wakasikilizwa wanataka nini. Kwa sababu nilizoeleza hapo juu, Mahakama hii inatupilia mbali rufaa hii kwa sababu haina mashiko na maamuzi ya Mahakama za chini yanaendelea kusimama kama yaliyoamriwa. Kutokana na shauri hili kuhusisha ndugu kila upande utabeba gharama zake. Hukumu hii imetolewa leo na kusainiwa hapa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Shinyanga tarehe 31 Oktoba 2024. F.H. Mahimbali Jaji. 19