267 Scaned
The parties reached a binding settlement allocating land with permanent crops to plaintiffs and developed two acres to defendants, with all claims withdrawn and each party bearing its own costs.
Source-derived case information.
- Citation
- 267 Scaned
- Parties
- Plaintiff: Juma Gome; Plaintiff: Pili Ally Gome (as administrator of the estate of the late Ally Gome); Defendant: Muria Tangwesi; Defendant: Swaumu Saidi Abdallah; Defendant: Maria Langwa; Defendant: Mfaume Rajabu Gome
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Land Civil Suit / Judgment on Settlement
- Outcome
- case settled by consent judgment
- Legal Topics
- Ownership Dispute, Settlement, Inheritance, Trespass, Damages
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Juma Gome
Plaintiff
Pili Ally Gome (as administrator of the estate of the late Ally Gome)
Plaintiff
Muria Tangwesi
Defendant
Swaumu Saidi Abdallah
Defendant
Maria Langwa
Defendant
Mfaume Rajabu Gome
Defendant
Procedural Posture
Land Civil Suit / Judgment on Settlement
Legal Issues
- 1 whether plaintiffs are lawful owners of the disputed land
- 2 whether defendants unlawfully entered and constructed on the land
- 3 entitlement to damages and injunctive relief
Ratio Decidendi
The parties reached a binding settlement allocating land with permanent crops to plaintiffs and developed two acres to defendants, with all claims withdrawn and each party bearing its own costs.
Court Disposition
case settled by consent judgment
Orders
- Land with permanent crops (mango, cashew, coconut) awarded to plaintiffs.
- Remaining land without permanent crops awarded to defendants.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA ARDHI DAR ES SALAAM SHAURI LA MADAI YA ARDHI NA. 267 YA 2023 JUMA GOME..................................................................... MDAI WA KWANZA PILI ALLY GOME(kama msimamizi Wa mirathi ya Marehemu ALLY GOME)............................... MDAI WA PILI DHIDI YA MURIA TANGWESI................................................. MDAIWA WA KWANZA SWAUMU SAIDI ABDALLAH........................................ MDAIWA WA PILI MARIA LANGWA...........................................................MDAIWA WA TATU MFAUME RAJABU GOME.............................................. MDAIWA WA NNE HUKUMU YA MARIDHIANO 11/10/2024 A, MSAFIRI, J, Wadai walifungua shauri hili dhidi ya wadaiwa tajwa hapo juu wakiwa na madai kwamba wao ni wamiliki halali wa eneo lenye mgogoro lenye ukubwa wa ekari Mia Nne na Hamsini (450) lililoko katika Kijiji cha Ndwati, Kata ya Gwata, Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mkoa wa Pwani. Walieleza kuwa eneo hilo awali lilimilikiwa na Baba mzazi wa wadai aitwae Gome ambae alifariki mwaka 1990 ambapo shamba hilo lilirithiwa na watoto wa marehemu ambao ni wadai tajwa. Wadai wanaeleza kuwa mnamo Mwaka i 2016, wadaiwa na 1, 2, na 3 walivamia eneo lenye mgogoro na kuanza ujenzi wa makazi ya kudumu pasipo na uhalali. Vilevile, Mdaiwa na. 4 anadai kuwa mmiliki wa eneo lenye mgogoro pasina uhalali wowote. Hivyo, wadai wanaomba Mahakama itoe hukumu na tuzo dhidi ya wadaiwa wote kama ifuatavyo; a. Itamkwe kuwa wadai ni wamiliki halali wa ardhi bishaniwa yenye ukubwa wa Ekari Mia Nne Hamsini (450) iliyopo Kijiji cha Ndwati Kata ya Gwata, Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mkoa wa Pwani. b. lamriwe kuwa wadaiwa, Wafanya kazi wao, warithi wao, madalali wao wazuiliwe kuingia katika Ardhi ya wadai. c. Amri ya kubomoa kwa nyumba iliyojengwa na mdaiwa wa 1, mdaiwa wa 2, na mdaiwa wa 3 kwenye ardhi ya wadai. d. Wadaiwa namba 1, 2, na 3 waamriwe kulipa gharama za uharibifu wa jumla kiasi cha Shilingi za kitanzania milioni mia tatu (300,000,000/=) kwa wadai kwa sababu ya ugumu na usumbufu ulisababishwa nao na familia zao kufuatiwa na uvamizi uliofanyika kwenye ardhi yenye mgogoro. e. Wadaiwa waamriwe kulipa gharama za shauri. f. Na nafuu zozote Mahakama hii tukufu itaona inafaa kutolewa. Wadaiwa wote nao waliwasilisha Hati za utetetezi wao Mahakamani ambao walikanusha madai ya Wadai na kuiomba Mahakama kutuplia mbali madai ya wadai. 2 Baada ya kukamilika kwa hatua za awali za majibizano, na kongamano la awali kufanyika, shauri hili liliwasilishwa mbele ya Kituo cha Usulihishi cha Mahakama Kuu kwa hatua za usuluhishi. Usuluhishi ulifanyika kwa mafanikio mbele ya Mheshimiwa Angela Bahati Salema, Jaji /Msuluhishi na wadaawa walikubaliana kumaliza shauri hili kwa njia ya usluhishi na hivyo kusajili Amri ya Makubaliano ya Upatanisho ambayo ilisainiwa na pande zote mbele ya Msuluhishi mnamo tarehe 04/10/2024. Tarehe 11/10/2024, wadaawa walifika mbele ya Jaji mwendesha shauri (trial Judge) kwa minajili ya kurekodi/kusajili Tuzo ya Makubaliano kwa mujibu wa Kanuni ya VIII Kanuni Ndogo 33 (a) na 34 za Sheria ya Mwenendo wa Madai Sura ya 33, kama ilivyorejewa Mwaka 2019 (Order VIII Rule 33(a) and 34 of the Civil Procedure Code, Cap 33 R.E 2019 as amended by G.N. No 381 of 2019). Katika usajili wa Tuzo mbele ya Mahakama, wadaawa waliwakilishwa na mawakili kama ifuatavyo; Mlyambelele Ng'weli, Wakili wa Mdaiwa namba 4 ambae pia alikuwa akishika mikoba ya Augustino Ndomba, Wakili wa Wadai, na Jersey Kasambala, Wakili ambae alikuwa akishika mikoba ya Faraji Mangula, wakili wa wadaiwa namba l,2,na 3. Hivyo,pande zote mbili za wadaawa zimekubaliana kumaliza shauri hili, kwa njia ya upatanisho na kukubaliana yafuatayo:- 3 a. Kwamba, Eneo lenye mazao ya kudumu kama vile miembe, mikorosho na minazi itakuwa mali ya Wadai na Eneo jingine linalobakia ambalo halina mazao ya kudumu litakuwa mali ya wadaiwa. b. Kwamba, eneo ambalo wadaiwa wameliendeleza, wamejenga ambalo ni ekari mbili (2) litabakia kuwa mali yao halali. c. Kwamba, Wadai na Wadaiwa wanakubaliana kuheshimu, kufuata na kuzingatia Makubaliano na utaratibu wa Kijiji cha wafugaji Kigoda ya tarehel6/10/2023 kuhusiana na maeneo ya malisho ya mifugo, kutumia vyanzo vya maji kunyweshea mifugo. d. Kwamba Wadai na Wadaiwa wanakubaliana kwamba makubaliano haya yanukuliwe na iwe ndio makubaliano ya mwisho na kwamba hakutakuwa na makubaliano mengine yataingiwa au kuingiwa zaidi ya haya. e. Kwamba, Wadai na Wadaiwa wanakubaliana kuwa makubaliano haya yanukuliwe kuwa hukumu na tuzo katika shauri hili. f. Kwamba, wadaiwa wanakubaliana kuwa makabaliano haya yatatafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. HIVYO BASI, wadaawa wanaafiki na wanakubaliana na Mahakama inanukuu amri za makubaliano kama ifuatavyo; 1. Eneo lenye mazao ya kudumu kama vile miembe, mikorosho na minazi itakuwa mali ya wadai na eneo jingine linalobakia ambalo halina mazao ya kudumu litakuwa mali ya wadaiwa. 2. Eneo ambalo wadaiwa wameliendeleza, wamejenga ambalo ni ekari mbili (2) litabakia kuwa mali yao halali. . 4 3. Wadai na wadaiwa wanakubaliana kuheshimu, kufuata na kuzingatia Makubaliano na utaratibu wa Kijiji cha wafugaji Kigoda ya tarehe 16/10/2023 kuhusiana na maeneo ya malisho ya mifugo, kutumia vyanzo vya maji kunyweshea mifugo. 4. Makubaliano haya yamenukuliwa na Mahakama na ndio makubaliano ya mwisho na hakutakuwa na makubaliano mengine yataingiwa au kuingiwa zaidi ya haya. 5. Makubaliano haya yamenukuliwa kuwa hukumu na tuzo ya Makubaliano au maridhiano. 6. Madai yote ya Wadai yameondolewa kupitia Makubaliano na maridhiano baina ya wadaawa. 7. Kila Upande utabeba gharama zake katika hili shauri hili. 5