HUKUMU YA KATELINA KASENSE
The appellant was accorded the right to be heard, failed to object to the sale contract or raise forgery and death-date issues at the trial stage, and the respondent proved purchase and ownership of the disputed land through oral and documentary evidence. The appeal lacked merit and was dismissed.
Source-derived case information.
- Citation
- HUKUMU YA KATELINA KASENSE
- Parties
- Appellant: Ketelina Jackob Vundwe; Respondent: Elina Merry Kasense
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Land Appeal / Judgment on Appeal
- Outcome
- Appeal dismissed
- Legal Topics
- Sale of Land, Contract Validity, Forgery Allegations, Right to Be Heard, Burden of Proof
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Ketelina Jackob Vundwe
Appellant
Elina Merry Kasense
Respondent
Procedural Posture
Land Appeal / Judgment on Appeal
Legal Issues
- 1 Whether the sale contract for the disputed land was valid or forged
- 2 Whether the appellant was denied the right to be heard
- 3 Whether the respondent proved ownership of the disputed land
Ratio Decidendi
The appellant was accorded the right to be heard, failed to object to the sale contract or raise forgery and death-date issues at the trial stage, and the respondent proved purchase and ownership of the disputed land through oral and documentary evidence. The appeal lacked merit and was dismissed.
Court Disposition
Appeal dismissed
Orders
- Appeal dismissed without costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MASJALA NDOGO YA MBEYA MBEYA RUFAA YA ARDHI NA. 24233 YA 2023 REJEA YA KESI NA. 202409271000024233 (Inatokana na Maombi Na. 97 ya 2023 katika Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Mbeya) KETELINA JACKOB VUNDWE ……………………………..………….MRUFANI NA ELINA MERRY KASENSE …………………………..………………MRUFANIWA HUKUMU Tarehe 19/12/2024 na 13/3/2025 JAJI NONGWA. Elina Merry Kasense, alifungua mgogoro wa ardhi katika Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Mbeya (Baraza) ambayo ulisajiliwa kama Maombi Na. 97 ya 2023 dhidi ya mrufaniwa, akidai kuvamia eneo lenye ukubwa wa ekari moja na robo lililopo kitongoji cha Iwe Kijiji cha Isangala kata ya Iwindi ndani ya wilaya na mkoa wa Mbeya (eneo la mgogoro). Aliomba atangazwe mmiliki halali wa eneo la mgogoro, amri ya kumwondoa mrufaniwa, fidia ya usumbufu na gharama za kesi. Maelezo mafupi ya madai ni kuwa mrufani na mrufaniwa walikuwa wake wenza ambapo waliolewa na William Hayola Kasense kwa sasa 1 marehemu. Kwamba eneo la mgogoro alilipata mwaka 2023 kwa njia ya kununua kutoka kwa mrufani na mme wake kwa shilingi 2,000,000/=. Mauziano yalifanyika mbele ya viongozi wa Kijiji cha Isangala. Lakini ilipofika mwezi Octoba 2023 alipotaka Kwenda kulisafisha eneo la mgogoro alikuta mrufani amemkodisha Kamendu. Alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji na mkodishwaji kuliacha. Kwenye ushahidi mrufaniwa(SM1) alieleza namna alivyonunua eneo la mgogoro ambapo mkataba wa ununuzi ulitolewa kama kielelezo P1. Ushahidi wa SM1 uliungwa mkono na Mary Wlliam Kasense (SM2), Elia Ambonisye Kibona (SM3) ambao walishuhudia mauziano na Petrol William Hayola (SM4) ambaye alisema aliona wakati mrufaniwa anaoneshwa shamba. Kwenye utetezi wa maandishi, mrufani alikubali kumuuzia eneo mrufaniwa lakini alisema sio eneo lote na kwamba mkataba wa mauziano haukusema ukubwa wa eneo. Wakati wa kusikiliza mrufani alikuwa shahidi pekee, kwenye ushahidi wake alikataa kuuza eneo la mgogoro lakini alisema mrufaniwa alitoa hela za kumuuguza mme na walikubaliana atazirudisha. Baada ya kusikiliza pande zote, Baraza liliona kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa mrufaniwa alinunua eneo la mgogoro na mrufani alikubali hilo. Hivyo mrufaniwa alitangazwa mmiliki wa eneo la mgogoro. 2 Mrufani hajakubaliana na hukumu ya Baraza, ameleta hati yake ya rufaa yenye sababu nne, nimelazimika kuzinukuu kama zilivyo kwenye mfumo was e-CMS. ‘1. Baraza la ardhi na nyumba la wilaya limekosea kisheria na kiukweli pale ilipompa ushindi mrufaniwa kwani sijawahi fanya mauziano yoyote ya shamba na mrufaniwa kitendo ambacho ni kinyume cha sheria, kwamba mkataba uliotumika kama ushahidi wa mnufaniwa katika Baraza la ardhi ni mkataba ambao siutambui sijawahi fanya mauziano hayo na mrufaniwa wala sijawahi kusaini huo mkataba ni mkataba uliotengenezwa na mrufaniwa na kugushi kuniwekea sahihi mwenyewe kwenye mkataba na kuandika jina langu mwenyewe mrufaniwa. 2. Kwamba Baraza la ardhi na nyumba la wilaya Mbeya limekosea kisheria na kiukweli pale ilipozingatia mkataba wa mrufaniwa ambao hauna ukweli ndani yake ni mkataba uliofanyika kinga ya kuzurumiwa shamba la mrufani kwani hata sahihi iliyopo ya muuzaji sio ya mrufani. 3. Baada ya kugundua kwamba kuna mkataba ambao mimi mrufani sijahusika kwenye mkataba huo nimepeleka lalamiko polisi kulalamikia mkataba uliofojiwa kwa maana ya kunisainia na kuandika jina langu kwenye mkataba bila idhini yangu kitendo ambacho ni kinyume cha sheria kumuandikia mtu jina na kumsainia, polisi tayari inafanya uchunguzi wa mkataba wa mrufaniwa alioutoa katika Baraza la 3 Ardhi kama ushahidi wake na ndio uliopelekea kupata ushindi mrufaniwa. 4. Kwamba Baraza la ardhi na nyumba la wilaya lilikosea kisheria na kiukweli pale ilipotamka kwenye maamuzi kwamba mrufani nimekili kwamba eneo la mgogoro nimemuuzia mrufaniwa, kitendo ambacho sio kweli sijawahi kumuuzia mrufaniwa eneo la mgogoro na sikutamka hivyo ilivyoandikwa kwenye maamuzi.’ Niweke wazi kuwa sababu zake za rufaa ambazo ziliwasilishwa kwenye mfumo wa e-CMS kama matakwa ya sheria yanavyotaka ni tofauti kidogo na zile zilizopo kwenye nakala ngumu. Lakini zina ufanano na hakuna aliyeathirika. Wakati wa kusikiliza rufaa, mrufani hakuwa na uwakilishi wa wakili, kwa upande wa mrufaniwa aliwakilishwa na wakili Bi. Pamela Kalala. Pande zote zilikubaliana rufaa isikilizwe kwa kuwasilisha hoja za maandishi na mahakama ilibariki ombi hilo. Hoja ziliwasilishwa kama ilivyoamriwa. Kwenye hoja zake, mrufani aliwasilisha kwa ujumla, hukutenganisha sababu zake za rufaa. Alieleza kuwa mkataba wa mauziano ulikuwa batili kwa sababu ulighushiwa, akidai kuwa uliandikwa na mrufaniwa kwa nia ovu. Alieleza kuwa baada ya kugundua kuna mkataba ambao yeye hautambui alitoa taarifa polisi na uchunguzi bado 4 unaendelea. Alienda mbali zaidi na kudai kwenye mkataba wa mauziano kuna wauzaji wawili, yaani William Hayola Kasense na yeye ambao walikuwa mume na mke lakini cha kushangaza sahihi za wauzaji zinafanana. Mrufani aliendelea kueleza kuwa hakupewa nafasi ya kuita mashahidi na kusikilizwa kinyume na haki za kibinadamu na kikatiba. Aliwasilisha kuwa tarehe ya mauziano kwenye mkataba ni tarehe 22/4/2023 wakati muuzaji mmoja William Hayola Kasense alifariki tarehe 14/4/2023. Pia alisema Baraza lilikosea kusema yeye alikubali madai jambo ambalo hakulisema. Aliomba rufaa yake ikubaliwe kwa gharama. Akijibu hoja za mrufani, wakili Pamela alieleza kuwa mrufani ameshindwa kujikita kwenye sababu zake za rufaa kwa uwazi. Akijibu hoja ya suala la mkataba kuchunguzwa na polisi, wakili alisema suala hilo halikuibuliwa Baraza na hivyo kwa mjibu wa sheria isizingatiwe. Alirejea shauri la Ramadhani Msangi vs Sunna G. Mandara & Others, Land Appeal No. 39 of 2017 [2018] TZHCLandD 456 (3 August 2018; TanzLII) kuwa jambo ambalo halikuibuliwa kwenye madai na kujadiliwa na mahakama ya chini haliwezi kujadiliwa na mahakama ya rufaa. 5 Alieleza kuwa mkataba huo ulikuwa halali ambapo ulishuhudiwa na Aneth mtoto wa mrufani kama shahidi wa wauzaji. Aliongeza kuwa SM1, SM2, SM3 na SM4 walishuhudia mkataba. Zaidi kuwa mrufani hakupinga kuwepo mauziano, alirejea ukurasa wa 17 wa mwenendo wa Baraza. Kuhusu kutopewa nafasi ya kusikilizwa na kuita mashahidi, wakili Pamela alisema, kumbukumbu za mahakama hazipaswi kupuuzwa kirahisi, alirejea kesi ya Halfani Sudi na Abieza Chichili [1998] TLR 527. Aliongeza kuwa cheti cha kifo kuthibitisha William Hayola Kasense alifariki tarehe 14/4/2023 hakikutolewa na ukweli ni kuwa alifariki tarehe 21/5/2023 baada ya mkataba kufanyika. Aliendelea kueleza kuwa mrufani aliuza shamba lote lakini pia hata walipo jaribu kusuluhishwa, mrufani hakuwa tayari. Aliliomba rufaa itupiliwe mbali kwa gharama. Nimepitia maelezo ya maandishi ya pande zote mbili pamoja na kumbukumbu zote za rufaa, naona kuna hoja mbili za kutolea majibu. Moja, kama mrufani hakupewa haki ya kusikilizwa na Baraza, na mbili kama rufaa ina mashiko. Kwa kuanza hoja ya kwanza, haikuwa miongoni mwa sababu za rufaa zilizopo kwenye mfumo wa e-CMS bali kwenye nakala ngumu 6 iliyowasilishwa mahakamani. Bila kujali hilo, ni suala la kisheria na pande zote mbili zimepata wasaa wa kusikilizwa. Hivyo nitalijadili. Uvunjaji wa haki ya kusikilizwa si tu ukiukaji wa kanuni kuu ya haki asili bali pia ni kuvunjwa kwa dhamana ya kikatiba ya haki ya msingi ya kusikilizwa ambayo imejumuishwa chini ya Kifungu 13(6)(a) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Kunyimwa haki ya kusikilizwa katika mchakato wowote kunabatilisha mwenendo mzima. Mrufani kwenye hoja zake anasema hakupewa nafasi ya mashahidi wake kusikilizwa. Wakili Pamela alijibu kuwa alipewa nafasi ya kusikilizwa na kumbukumbu za mahakama hazipaswi kukosolewa. Nimepitia mwenendo mzima wa Baraza ambao unaonyesha mchakato mzima toka shauri kuwasilishwa Baraza hadi hukumu kusomwa. Nimeona kuwa wakati mrufaniwa anatoa ushahidi pamoja na mashahidi wake, mrufani alipewa haki ya kuwahoji wote yaani SM1, SM2, SM3 na SM4. Pia wakati vielelezo vinatolewa alipewa nafasi ya kupinga. Baadaya ya mrufaniwa kufunga ushahidi upande wake, mrufani alitoa ushahidi wake na kuliambia Baraza kuwa hakuwa na shahidi mwingine, hivyo anafunga utetezi. Hakuna sehemu kwenye mwenendo wa Baraza mrufani aliomba nafasi ya kuleta mashahidi akanyimwa. Kumbukumbu za Baraza zinayonesha kwamba mrufani alipewa haki ya kutoa ushahidi na kuleta 7 mashahidi. Ni sheria iliyo thabiti kwamba, kumbukumbu za mahakama/Baraza ni hati muhimu ambazo usahihi wake hauwezi kukosolewa kirahisi. Rejea kesi ya Salehe Omary Ititi na Nina Hassan Kimaro, Civil Application No. 583 of 2021 [2023] TZCA 232 (9 May 2023; TanzLII). Kutokana na kile kinachoonekana kwenye mwenendo wa Baraza, mrufani alipewa haki zake zote muhimu katika mchakato mzima wa usikilizwaji. Hivyo hoja hii ambayo ni sababu ya pili kwenye nakala ngumu ya rufaa imekataliwa. Nikija katika hoja ya pili ambayo imebeba sababu zote za rufaa. Nitaongozwa na kanuni za kisheria zifuatazo, moja, wadaawa wanabanwa na yaliyomo katika nyaraka zao za shauri. Ni sheria kuwa pande zitahusishwa na maelezo yao ya maandishi na kwamba ushahidi wowote utakaotolewa na upande wowote ambao si wa kuunga mkono au unapingana na kile kilichoelezwa katika maelezo ya upande huo lazima upuuziliwe mbali. Rejea kesi ya Salim Said Mtomekela vs Mohamed Abdallah Mohamed, Civil Appeal No. 149 of 2019 [2023] TZCA 15 (15 Februari 2023; TanzLII). Mbili, ni kuhusiana na mzigo wa uthibitisho na kiwango cha kuthibitisha katika kesi za madai. Ni kanuni muhimu ya sheria kwamba, 8 katika kesi za madai, mzigo wa uthibitisho upo kwa upande unaodai jambo lolote linalomfaidi. Haya yameekekezwa katika kifungu cha 110 na 111 ya Sheria ya Ushahidi sura ya 6 Marejeo 2022. Mrufaniwa ambaye ndiye alipeleka kesi Baraza, alidai kuwa eneo la mgogoro alinunua kwa mrufani, aliweza kutoa mkataba wa mauziano ambao haukupingwa na mrufani. Ni sheria iliyo thabiti kwamba maudhui ya kielelezo kilichopokelewa bila upinzani kutoka upande mwingine, kinakuwa kimethibitishwa kikamilifu kutokana na kushindwa kuleta upinzani wakati kinakubaliwa kama ushahidi. Rejea kesi ya Eupharacie Mathew Rimisho t/a Emari Provision Store & Another vs Tema Enterprises Limited & Another, Civil Appeal No. 270 of 2018 [2023] TZCA 102 (13 March 2023; TanzLII). Kwenye hoja zake za maandishi mrufani amedai kuwa yeye hakufanya mkataba wowote na sahihi zilizopo zimeghushiwa. Wakili Pamela alikuwa sahihi alipojibu kuwa hoja hiyo haikuibuliwa wala kujadiliwa na Baraza. Wakati SM1 anatoa mkataba huo kama ushahidi, mrufani hakuweza kupinga hivyo uwepo wa mkataba huo pamoja na maelezo yake vilikubaliwa na mrufani. Pia alisema suala ya sahihi kughushiwa lilipelekwa polisi na uchunguzi unaendelea. Baada ya kupitia mwenendo wa Baraza nimeona hoja hiyo haikuibuliwa mbele ya Baraza 9 hivyo ni suala jipya katika hatua hii. Bila kuathiri yaliyo semwa hapo juu, hata kama sahihi zilikuwa zimeghushiwa kama inavyodaiwa, ilikuwa jukumu la mrufani kuchukua hatua haraka, kutumia njia nyingine kwa kutoa taarifa ya suala hilo kwa Polisi kwa sababu wakati wote, na kabla ya kuwasilisha jibu la maandishi la utetezi, mrufani alikuwa anajua kuwepo kwa mkataba uliokuwa umeunganishwa kwenye madai. Katika hali hii, kutokuchukua hatua kwa mrufani kutumia njia za haki za jinai kunaacha mengi ya kujiuliza. Kwa ufupi hakuna ushahidi wowote uliotolewa mbele ya Baraza kuhusiana na kughushiwa zahihi za mrufani kama anavyodai wala uwepo wa suala hilo katika vyombo vya kipolisi kulichunguza. Sambamba na hilo ni uwepo wa hoja kuwa mkataba ulisainiwa wakati muuzaji mmoja William Hayole Kasense amefariki. Kama nilivyojadili awali hoja hii pia haikuibuliwa Baraza na wala mrufani hakupeleka ushahidi wowote kuonyesha tarehe ambayo muuzaji daiwa alifariki ili kuleta mashaka kwenye mkataba huo wa mauziano yaani kielelezo P1. Pia ufanano wa sahihi mrufani hakuibua wala kuhoji ili Baraza liweze kuangalia na kulitatua kwa mjibu wa sheria. Kwa ujumla, maandishi au sahihi inaweza kuthibitishwa kwa kukubaliwa na mwandishi au kwa ushahidi wa shahidi au mashahidi ambao mbele yao 10 hati iliandikwa au kutiwa sahihi. Pia kuthibitishwa kwa maoni ya mtaalamu wa maandishi, ushahidi wa watu ambao wanajua maandishi ya mtu anayedaiwa kuandika maandishi fulani kama inavyotolewa chini ya vifungu vya 47 na 49 vya Sheria ya Ushahidi, na kupitia kulinganisha na Mahakama kwa maandishi yaliyofanywa mbele ya mahakama au kukubaliwa au kuthibitishwa kuwa ni maandishi au sahihi ya mtu huyo. Soma hukumu ya Mahakama ya Rufani kwenye kesi ya Ahmed Freight Limited Another vs Ecobank Tanzania Limited, Civil Appeal No. 182 of 2020) 2024 TZCA 172 (12 March 2024; TanzLII). Baada ya kumalizana na malalamiko ambayo yaliibuliwa na mrufani kwenye hoja zake za maandishi, nikiwa kama mahakama ya rufaa ya kwanza ninalo jukumu la kuangalia kama mrufaniwa alithibitisha madai yake ya kununua eneo la mgogoro. Kupitia ushahidi wake wa mdomo na kielelezo P1 ni kweli kuwa eneo la mgogoro alinunua kutoka kwa mrufani. Uwepo wa kuuziana hakukupingwa na mrufani kwenye majibu yake ya maandishi ambayo aliwasilisha Baraza tarehe 24/11/2023, isipokuwa yeye alisema hakuuza eneo lote, hivyo anabanwa na utetezi wake. Mrufaniwa aliwaleta mashahidi ambao walishuhudia mauziano baina ya mrufani na mrufaniwa ambao ni SM2 na SM3. Wao walisema walitia sahihi katika mkataba na ni kweli majina yao na sahihi 11 zinaonekana kwenye kielelezo P1. Pia SM4 alisema alishuhudia mrufaniwa akiwa anaoneshwa eneo walilouziana. Kuna hoja kutoka kwa mrufani kuwa kielelzo P1 hakisemi ukubwa wa eneo, nakubaliana naye lakini hili halimaanishi nakubaliana kwa kila kitu. Kwanza ushahidi wake unajikanganya na majibu yake ya utetezi. Kwenye utetezi wa maandishi alisema hakuuza shamba lote, kwenye ushahidi wa mdomo alisema hakuuza shamba bali walikubaliana mrufaniwa atoe hela za kumuuguza mme na atazirudisha. Alipohojiwa na wakili Pamela alisema aliuza nusu. Mkanganyiko huu unaenda kwenye kiini sha ushahidi wa mrufani. Ni kanuni ya sheria iliyo wazi kuwa kila shahidi anastahili kuaminiwa, na katika rufaa hii mrufaniwa na mashahidi wake walikuwa wakweli kwa sababu wote walikuwa sehemu ya mkataba wa mauziano, hivyo walijua ukubwa wa aneo ambalo lilikuwa linauzwa. Hakuna malalamiko kuwa mrufani alikuwa na ugomvi wowote na SM2, SM3 na SM4 mpaka wamgeuke. Pia kielelezo P1 kinaonesha shahidi wa wauzaji alikuwa ni Aneth William Kasense, lakini hakuitwa ili kutoa ushahidi kuhusiana na ukubwa wa eneo ambalo liliuzwa. Kitendo hiki kinaleta mashaka kuwa labda angekubaliana na ushahidi wa mrufaniwa kuwa eneo la ekari moja na robo ndilo liliuzwa na mrufani. 12 Kutokana na yaliyojadiliwa hapo juu, nakubaliana na hukumu ya Baraza kuwa mrufaniwa alithibitisha madai yake na sijaona sababu yoyote ya kutofautiana na hilo. Malalamiko yote yaliyoibuliwa dhidi ya hukumu ya Baraza ni yakufikirika. Mwisho rufaa hii haina mashiko na naitupilia mbali bila gharama kwani wadaawa walikuwa wake wenza. V.M. NONGWA JAJI 13/3/2025 Imesainiwa na kusomwa hapa Mbeya leo tarehe 13/3/2025 mbele ya Bi Pamela Kalala wakili wa Mrufaniwa na Mrufaniwa akiwepo bila uwepo wa Mrufani. V.M. NONGWA JAJI 13