LAMECK KIAGA
Procedural errors occurred in the lower courts, including failure to properly record and evaluate recusal grounds and failure to determine existence of a prima facie case before calling for defence, rendering the proceedings invalid and requiring a retrial.
Source-derived case information.
- Citation
- LAMECK KIAGA
- Parties
- Appellant: Lameck Kiaga; Respondent: Bulegwa Mihangwa; Respondent: Mondo Mihangwa; Respondent: Sangali Mihangwa
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2009
- Procedural Posture
- Criminal Appeal / Second Appeal Before High Court
- Outcome
- appeal allowed
- Legal Topics
- Judicial Bias, Prima Facie Case, Burden of Proof, Criminal Procedure
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Lameck Kiaga
Appellant
Bulegwa Mihangwa
Respondent
Mondo Mihangwa
Respondent
Sangali Mihangwa
Respondent
Procedural Posture
Criminal Appeal / Second Appeal Before High Court
Legal Issues
- 1 Whether the trial magistrate erred by refusing to recuse himself for alleged bias
- 2 Whether the lower courts properly evaluated evidence and determined existence of a prima facie case
- 3 Whether procedural errors in trial vitiated the proceedings
Ratio Decidendi
Procedural errors occurred in the lower courts, including failure to properly record and evaluate recusal grounds and failure to determine existence of a prima facie case before calling for defence, rendering the proceedings invalid and requiring a retrial.
Court Disposition
appeal allowed
Orders
- Proceedings of lower courts quashed and set aside
- Case to be retried before a different magistrate in the Primary Court at appellant's option
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MASJALA NDOGO YA SHINYANGA ILIYOPO SHINYANGA RUFAA YA JINAI NAMBA: 20240611200015985 (INAYOTAKA NA RUFAA YA JINAI NAMBA: 39925/ 2023, MBELE YA MAHAKAMA YA WILAYA KISHAPU, YENYE ASILI YAKE JINAI NAMBA 65/2023 MAHAKAMA YA MWANZO KISHAPU) LAMECK KIAGA .............................................................MRUFANI DHIDI YA 1. BULEGWA MIHANGWA 2. MONDO MIHANGWA .......................WARUFANIWA 3. SANGALI MIHANGWA HUKUMU TH 22 & 30 JULAI 2024 F.H. MAHIMBALI, JAJI Mrufani alifungua shauri la jinai mbele ya mahakama ya mwanzo akiwashitaki warufaniwa kwa kosa la kuharibu Mali kwa Makusudi K/F 326 (1) Kanuni ya Adhabu, Sura 16 Toleo la 2022. Ilielezwa kuwa 1 warufaniwa mnamo tarehe 16/7/2023 majira ya usiku katika kitongoji cha Mwasele B mji mdogo wa Mhunze Wilayani Kishapu, kwa makusudi na bila halali waliharibu mali ya mrufani kwa kukata miti ndani ya shamba la mrufani yenye thamani ya Tshs 11,050. Mahakama ya mwanzo baada ya kusikiliza shauri hilo, ilihitimisha kuwa shitaka dhidi ya warufaniwa halikuthibitishwa vilivyo. Mrufani alikata rufaa kwenda mahakama ya wilaya bila mafanikio. Akiwa hajaridhika na maamuzi ya mahakama ya wilaya amefika mbele ya mahakama hii akiwa na sababu nne za rufaa ambazo zimejikita kwenye malalamiko dhidi ya Mheshimiwa hakimu wa mahakama ya wilaya kutomtendea haki kwa kukataa kujitoa kusikiliza shauri lake licha ya kuwa alikua amemkataa na kwamba mahakama ya mwanzo haikutilia nguvu ushahidi uliokua umetolewa na mrufani kiasi cha kushindwa kuona hatia dhidi ya warufaniwa. Hoja hizo zilipingwa vikali katika majibu ya warufaniwa kwamba sababu za rufaa hazina mashiko na Mheshimiwa hakimu alikua sahihi katika kutekeleza majukumu yake. Wakati wa usikilizwaji wa shauri hili, mrufani na warufaniwa walifika mbele ya mahakama hii wao wenyewe bila uwakilishi. Akielezea sababu za rufaa, Mrufani alieleza mahakama hii kwamba hajaridhika na uamuzi wa Mahakama ya Wilaya kwa sababu zifuatazo; Sababu ya kwanza na ya pili zinahusu Hakimu husika kukataa kujitoa 2 katika kesi hata baada ya kutolea ufafanuzi ni jinsi gani alivyo na maslahi katika kesi hiyo lakini bado aling'ang'ania. Kwenye sababu ya tatu, hoja kubwa ni tafasiri ya Mahakama ya Wilaya katika ushahidi alioutoa Mahakamani kushindwa kutafisiriwa vizuri hivyo kutoa uamuzi usio sahihi kisheria. Mwisho kabisa, aliomba Mahakama hii iwaone warufaniwa wote ni wenye hatia kwa kosa walilotenda na kuwaadhibu ipasvyo. Kwa upande mwingine, Warufaniwa walieleza mahakama hii kuwa wanapinga rufaa hii kama ilivyowasilishwa. Na katika sababu ya kwanza ya rufaa, inakanushwa vikali kwa sababu vigezo vya kisheria kwa Mhe. Hakimu kujitoa katika kesi havikuwepo. Maana kisheria, siyo kila takwa la mdaawa kumkataa hakimu ni lazima likubaliwe. Kama mdaawa atatoa hoja ya kumkataa Hakimu, hakimu husika atajipima na kisha kuitolea uafafanuzi endapo hoja zina mashiko ya kisheria au laa. Katika kesi hii hapakuwapo na hoja yoyote. Lakini pia huo uswahiba wa Hakimu na warufaniwa haukuweza kutolewa ushahidi. Kuhusu sababu ya pili ya rufaa nayo haina mashiko kwa sababu hapakutolewa ushahidi wowote wa kuonyesha Hakimu alikua ana maslahi kwa mujibu wa ushahidi katika hoja hii. 3 Sababu ya tatu ya rufaa nayo haina mashiko kabisa kwa sababu kwa mujibu wa sheria, ushahidi uliochukuliwa ulitafsiriwa vizuri kabisa na hakimu. Hivyo hapakuwepo na kasoro yoyote ya tafsiri kama inavyodaiwa. Mwisho, Mrufaniwa wa kwanza aliomba mahakama hii kuiona rufaa hii haina mashiko, na iitupilie mbali. Mrufaniwa wa pili na tatu waliunga mkono hoja zilizoelezewa na mrufaniwa wa kwanza. Akihitimisha hoja zake, Mrufani aliendelea kusisitiza kuwa rufaa yake ina mashiko na hivyo ikubaliwe kwa kuwa warufaniwa walipewa ushindi isivyo halali kuhusiana na umiliki wa eneo hilo. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kwenye shauri hili la rufaa, wajibu wangu sasa ni kuamua rufaa. Na kwa dhati, hoja ya msingi ya kuamriwa ni iwapo rufaa hii ina mashiko. Ikumbukwe kuwa kwa hapa Mahakama Kuu, hii ni hatua ya pili ya rufaa baada ya Mahakama ya Wilaya kuisikiliza rufaa kwa mara ya kwanza dhidi ya uamuzi wa mahakama ya mwanzo. Hivyo, ni msimamo wa kisheria kwamba mahakama ya juu haiwezi kuingilia maamuzi mfanano ya mahakama mbili za chini vingenevyo kuwepo na dosari kubwa za kisheria ambazo zimepelekea maamuzi yasiwe ya haki. Tazama maamuzi katika shauri la Abdallahman Athuman v. 4 Republic, Criminal Appeal No. 149 of 2014; Omari Mussa Juma v. Republic, Criminal Appeal No. 73 of 2005; Josephat Shango v. Republic, Criminal Appeal No. 62 of 2012; and Yohana Dioniz and Another v. Republic, Criminal Appeals No. 114 and 115 of 2009 (all unreported). Katika shauri hili mrufani amemlalamikia hakimu wa mahakama ya wilaya kwa kushindwa kujitoa kusikiliza shauri lake kwa maelezo kuwa hakimu huyo ni swaiba na rafiki wa warufaniwa na kwamba alikua na masilahi. Kwa bahati mbaya mahakama ya wilaya haikueleza kwa kina ni sababu zipi mrufani zilimfanya amkatae mheshimiwa hakimu. Mahakama ilieleza tu kuwa ilipokea barua ya kuomba hakimu huyo ajitoe na baada ya hakimu kuipitia barua hiyo alieleza kuwa sababu zilizotolewa hazina mashiko na hivyo shauri liendelee. Kwa mwenendo wa shauri ulivyo, hauoneshi sababu za kukataliwa kwa hakimu. Utaratibu wa mahakama ni kwamba pale hakimu/Jaji anapotakiwa kujiondoa kusikiliza shauri, sababu za mdaawa huyo zitanakiliwa kwenye mwenendo wa shauri kisha upande mwingine utapewa pia fursa ya kuelezea, kisha mheshimiwa Hakimu atapima kama hoja zina mashiko au laa. Kwa maana nyingine hayo yanapaswa 5 kuonekena kwenye mwenendo wa shauri jambo ambalo halikufanyika katika shauri hili. Katika shauri la REGISTERED TRUSTEES OF SOCIAL ACTION TRUST FUND AND ANOTHER VS. HAPPY SAUSAGES LIMITED AND 11 OTHERS (2004) TLR 264, Mahakama ya Rufani Tanzania ilihitimisha kuwa itakua swala la ajabu sana kwa kila mtu akihisi kutotendewa haki anaomba hakimu ajitoe kwenye kusikiliza shauri. ” it is our considered view that it would be an abduction of judicial function and an encouragement of spurious application for a judicial officer to adopt the approach then he/she should disqualify himself/herself whenever requested to do so on application of one of the parties on grounds of possible appearance of bias. A judicial officer should not automatically stand aside whenever requested to do so” Tazama pia shauri la: Senzo Maswi @Mwitsa and Another vs. Republic, Criminal Appeal No.518/2018, Issack Mwamasika and 2 Others vs. CRDB Bank Limited, Civil Revision No.6/2016. Kwasababu hizo ni wazi kwamba mheshimiwa hakimu alikosea kwa kushindwa kufuata utaratibu wa kusikiliza na kunukuu hoja za kujitoa kusikiliza shauri husika na kisha kujipima na kutoa uamuzi. 6 Aidha mrufani amelalamika kwa warufaniwa kuonekana hawana hatia ili hali mzania wa ushahidi wake ulikua mzito zaidi kuliko wa warufaniwa. Mahakama imetazama kumbukumbu za mahakama za chini wakati wa usikilizwaji wa shauri hii na kugundua kuwa mahakama ya mwanzo ilifanya makosa katika usikilizwaji wa shauri. Mahakama baada ya kupokea ushahidi wa mlalamikaji/mrufani haikuupima ushahidi huo ili kuona ni toshelevu kiasi gani kuwafanya warufaniwa kuweza kujitetea. Kwakuwa lilikua shauri la jinai ilikua ni lazima kuwepo na uamuzi wa iwapo washitakiwa walikua na kesi ya kujibu au hapana. Tazama F. 36 ya Kanuni za mwenendo wa Mashauri ya Jinai Mahakama za Mwanzo. Katika shauri la Director of Public Prosecution Vs Morgan Malik & Nyaisa Makori, Criminal Appeal No 133 of 2013 CAT- (haijaripotiwa ) Mahakama ilitoa tasfiri ya maana ya neno kesi ya kujibu ambapo ilisema “A prima facie case is made out if, unless shaken, it is sufficient to convict an accused person with the offence with which he is charged or kindred cognate minor one ..., the prosecution is expected to have proved all the ingredients of the offence or minor cognate one thereto beyond reasonable doubt. If there is a gap, it is wrong to call upon the accused 7 to give his defence so as to fill it in, as this would amount to shifting the burden of proof" Zaidi ya hayo katika shauri la; DPP vs Ernest Warioba Muhindi and Muhindi Ernest, Criminal Appeal No 126 of 2021, iliamriwa kuwa "...It is a trite law that prima facie case means a standard of proof whose evidence suffices to ground conviction if the accused does not offer explanation. See Patel vs Republic [1968] 1 EA 97. Further, it is a dear position of law that in assessing evidence at the prima facie stage, the court is not required to apply a fully-fledged analysis. This is what makes prima facie distinct from proof beyond reasonable doubt” Tazama pia shauri la Republic vs. KHeo Bakari KHeo and 6 others, Criminal Sessions Case No. 19 of 2011, na Republic vs Jonas Janies @Kombe, Criminal Sessions Case No. 18 of 2002, HC at Arusha. Kwa kusema hayo ilikua makosa kwa mahakama ya mwanzo kuchukua ushahidi wa utetezi pasipo kuamua iwapo washitakiwa walikua na kesi ya kujibu ili kuweza kujitetea. Dosari hizo zinabatilisha mwenendo mzima wa shauri na hivyo kufutwa wote. 8 Kwakua dosari hizi zipo zilizoanzia Mahakama ya Mwanzo na zile za Wilaya, kwa kufutwa mwenendo wote, maana yake ni kua shauri hili sasa likaanze upya katika Mahakama ya Mwanzo kwa hiari ya Mrufani (endapo ataona bado ana nia hiyo). Kutokana na dosari zilizoenekana katika uendeshaji wa shauri hili na makosa ya kisheria, inatamkwa kwamba rufaa imekubaliwa kwa maelekezo kuwa shauri hili likasikilizwe upya mbele ya Mhe. Hakimu mwingine katika mahakama ya mwanzo kwa kuzingatia matakwa ya sheria. Hayo ndio maamuzi ya mahakama. Uamuzi huu umetolewa leo na kusainiwa hapa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Shinyanga leo tarehe 30 Julai 2024. Haki ya rufaa kwenda Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa upande ambao haukuridhika na uamuzi huu kwa hoja za kisheria iko wazi. F.H. Mahimbali Jaji. 9 10