Laurent Sayida Doto
The High Court found that the respondent's evidence, corroborated by multiple witnesses and consistent with the history of land use, was more credible and reliable than the appellant's unsupported documentary evidence. The appellant failed to prove his claim to the required standard. The Tribunal did not err in its...
Source-derived case information.
- Citation
- Laurent Sayida Doto
- Parties
- Appellant: Laurent Sayida Doto; Respondent: Guhenga Sayida Doto
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Land Appeal / Judgment at High Court
- Outcome
- Appeal dismissed
- Legal Topics
- Burden of Proof, Admissibility of Evidence, Land Ownership Disputes, Documentary Evidence
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Laurent Sayida Doto
Appellant
Guhenga Sayida Doto
Respondent
Procedural Posture
Land Appeal / Judgment at High Court
Legal Issues
- 1 Whether the District Land and Housing Tribunal erred in law and fact by relying on the respondent's documentary evidence created 30 years after the alleged sale
- 2 Whether the Tribunal erred by disregarding the appellant's 1977 sale agreement
- 3 Whether the Tribunal failed to detect fraudulent conduct by the respondent
Ratio Decidendi
The High Court found that the respondent's evidence, corroborated by multiple witnesses and consistent with the history of land use, was more credible and reliable than the appellant's unsupported documentary evidence. The appellant failed to prove his claim to the required standard. The Tribunal did not err in its assessment of the evidence or in its decision.
Court Disposition
Appeal dismissed
Orders
- Appeal is dismissed for lack of merit
- Decision of the District Land and Housing Tribunal is upheld
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA YA TANZANIA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MASIJALA NDOGO YA SHINYANGA SHAURI LA RUFAA YA ARDHI NA. 17864 YA 2024 KATI YA LAURENT SAYIDA DOTO ...................................................................... MRUFANI DHIDI YA GUHENGA SAYIDA DOTO ................................................................. MRUFANIWA (INAYOTOKANA NA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WILAYA YA KISHAPU) (Mbele ya H. Hatson – Mwenyekiti) Tarehe 29/05/2024 katika SHAURI LA ARDHI ASILIA NA. 13 YA MWAKA 2024 HUKUMU Tarehe 20 Novemba na 6 Desemba 2024. Mbele ya F.H. Mahimbali, Jaji. Mrufani na mrufaniwa ni ndugu wa tumbo moja na baba mmoja. Ugomvi mkubwa baina yao ni juu ya umiliki wa jumla ya hekari 23 ambazo kila mmoja anadai ni mali yake. Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya 1 Kishapu mara baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili ilimpa ushindi Mrufaniwa hii ni kutokana na uzito wa ushahidi uliowasilishwa wakati wa usikilizaji wa shauri hilo amablo pia lilifunguliwa na Mrufaniwa. Maamuzi hayo hayakumfurahisha Mrufani hivyo kupelekea maamuzi hayo kupingwa katika Mahakama Kuu. Mrufani ameleta sababu tatu za rufaa ambazo ni: 1.Kwamba, Baraza la Wilaya lilikosea kisheria na kimwongozo lilipojikita na kuzingatia kielelezo cha Mrufaniwa katika kutoa uamuzi wake, kielelezo ambacho kilitengenezwa makusudi baada ya miaka thelasini. 2.Kwamba, Baraza la Wilaya lilikosea kisheria na kimwongozo lilipo shindwa kabisa kwa sababu anazozifahamu Mh.Mwenyekiti kuzingatia mkataba wa mauziano wa Mrufani na Ndugu Daud Zuberi wa mwaka 1977, kushindwa huko, kulipelekea kutoa uamuzi ambao siyo sahihi na wa haki. 3.Kwamba, Baraza la Wilaya lilikosea kisheria na kimwongozo liliposhindwa kubainisha hila za uongo za mrufaniwa. Mrufani alinunua ardhi gombaniwa mwaka 1977 na Mrufaniwa alidai alilinunua mwaka 1983, iweje leo eneo hilohilo liwe na mgogoro mwaka 2023 kama siyo 2 mbinu za kupora mali ya mrufani baada ya kutengeneza kielelezo cha kubumba-‘kuweka kumbukumbu ya kununuliana eneo’.Endapo Baraza lingebaini hila za Mrufaniwa, lisingetoa uamuzi lililoutoa kuhusiana na ardhi gombaniwa. Wakati wa usikilizaji wa rufaa hii, Mrufani alijiwakilisha mwenyewe ilihali Mrufaniwa aliwakilishwa na wakili msomi Bw. Frank Samweli ambaye aliipinga rufaa hii vikali kwa kukosa mashiko ya kimantiki na sheria hali kadhalika. Akielezea sababu zake za rufaa, Mrufani hakuwa na mengi zaidi ya kurejelea sababu zake za rufaa na kufafanua kuwa kielelezo cha mrufaniwa kilitengenezwa miaka 30 baada ya hayo yanayosemwa mauziano baina ya wawili hao (SM1 na SM2). Hoja ya mrufani ni kuwa kama mauziano yalifanyika mwaka 1983 kama Mrufaniwa (SM1) anavyodai, iweje kielelezo cha mauziano hayo yawe na tarehe ya mwaka 2023 (miaka 30) baadae? Lalamiko lake ni kuwa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya lilikosea kisheria kuipokea nyaraka hiyo kama kielelezo na hatimae kuipa uzito mkubwa wa kimaamuzi. 3 Kwenye sababu yake ya pili, hoja ya mrufani ni kuwa tofauti na hicho kielelezo cha Mwaka 2023, yeye hati yake ya ununuzi wa eneo hilo ni ya mwaka 1977 kutoka kwa Bw. Daud Zuberi ambapo alilinunua kwa shilingi 500 za kitanzania mbele ya uongozi wa Katibu wa CCM – Tawi la Migunga Kishapu (U1). Iweje basi Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya kushindwa kuipa uzito ushahidi huu?, alihoji Bw. Laurent Sayida Doto – Mrufani. Katika hoja ya tatu ya rufaa, Mrufani anahoji iweje Baraza la Ardhi na Nyumba kushindwa kabisa kubaini njama za hila na uongo za Mrufaniwa kwa kutengeneza ushahidi wa mwaka 2023 na hatimae kuanzisha mgogoro huu wa umiliki ilihali yeye ana nyaraka za umiliki wa Mwaka 1977? Alihitimisha hoja hii kwa kusema hizo zilikua ni njama tu za nduguye - Mrufaniwa za kutaka kumdhulumu ardhi yake na Baraza la Wilaya bila ya utashi sahihi, lilikakubaliana na uongo huo. Kwasababu ya hoja hizi, Mrufani anaiomba Mahakama hii tukufu, iongozwe na utashi sahihi wa kisheria ili kufikia maamuzi ya haki na yaliyo sahihi kwa yeye kupewa ushindi, hukumu ya Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ibatilishwe, gharama zitozwe na Mahakama hii itoe amri nyingine stahiki kwa mujibu wa sheria ambazo ni sahihi, alihitimisha Bw. Laurent Sayida Doto. 4 Kwa upande wake Wakili Msomi Frank Samweli akipinga rufaa hii kwa niaba ya Mrufaniwa alisema hakubaliani na hoja zote zilizotolewa na kufafanuliwa na Mrufani wakati akielezea rufaa yake. Kwenye hoja ya kwanza ya rufaa, Wakili Samwel, alifafanua kuwa ni kweli kielelezo “M1” ni cha mwaka 2023 kikielezea ni vipi mauziano yaliyofanyika Mwaka 1983 kati ya Mrufaniwa na muuzaji wake (SM2) ambae ni Bw. Shilinde Simbi, hatimae kuwekewa maandishi mwaka 2023 ili tu kuondokana na usumbufu wa mara kwa mara kati ya Mrufani na Mrufaniwa ambao wamekua na malumbano yasiyoisha yanayohusiana na eneo hilo tokea mwaka 2018. Hivyo basi kutokana na kuepusha usumbufu kwa siku za usoni, aliamua kuyaweka mauziano hayo kwa njia ya maandishi sasa (mwaka 2023) ili kuweka kumbukumbu sawa na haikumaanisha kuwa ni mkataba mpya. Hivyo hapakuwapo na jambo lolote baya ndani yake na hayo yoye yanafafanuliwa kwa uzuri kabisa na ushahidi wa muuzaji mwenyewe (SM2) sambamba na ushahidi wa Mrufaniwa mwenyewe (SM1). Hivyo basi kielelezo hicho ni kuunga mkono tu ushahidi wa SM1 na SM2 ambao unafafanua ni veepe Mrufaniwa alipata eneo hilo wakati yeye akiwa amelipata mwaka 1975 kutoka kwa Masunga Masanja. 5 Pamoja na uwepo wa hati inayodhaniwa ni ya manunuzi ya shamba ya Mwaka 1977 ya Mrufani kutoka kwa Daudi Zuberi, kielelezo hicho kilikosa thamani mbele ya mauziano ya Mwaka 1983 kutokana na ushahidi uliowasilishwa wa pande zote mbili kuonekana ushahidi wa Mrufaniwa kuwa ni wenye nguvu na ushawishi zaidi ya ukweli kuliko ushahidi wa Mrufani kupitia kielelezo chake. Wakili Samweli alifafanua kuwa ukiachilia kilelezo hicho cha 1977 (U1), hapakuwapo shahidi yoyote aliyefika Mahakamani kuelezea namna alivyoshuhudia mauziano hayo. Kwa sababu hizo basi, Mwenyekiti hakua amekosea kabisa kuupuzia ushahidi huo maana haukua na thamani yoyote kisheria kwa kukosekana ushahidi wa kuunga mkono ushahidi huo wa maandishi tofauti na ilivyo kwa ushahidi wa Mrufaniwa. Akijibu hoja ya tatu ya rufaa, Msomi wa Sheria Bw. Samwel, aliieleza Mahakama kuwa hapakuwapo na uongo wala kughushi kwa nyaraka kwa upande wa mrufaniwa kwa jinsi ushahidi wa Mrufaniwa ulivyokuwa mnyoofu, wa uhakika na wenye kuaminika dhidi ya ushahidi wa mrufani. Kimsingi, katika mizania ya ushahidi wa pande zote mbili, ni ushahidi wa Mrufani ndiyo wenye mashaka zaidi kuliko ushahidi wa Mrufaniwa. Kwa kuzingatia ushahidi wa mashahidi SM1, SM2, SM3 na SM4 kwa pamoja, ni dhahiri kuwa kesi ya Mrufaniwa dhidi ya Mrufani ilikuwa imeelezwa bayana kwa ushahidi thabiti 6 na wa kuaminika kuliko ushahidi dhaifu wa Mrufani. Hivyo wakili Samwel alihitimisha kwa kuiomba Mahakama kupuuzia kabisa sababu hii ya rufaa na hivyo kwa ujumla wake kuitupilia mbali rufaa hii kwa gharama kwa kukosekana kwa mashiko ya kimantiki na kisheria. Mrufani katika hitimisho lake, hakua na jipya zaidi ya kusisitiza wasilisho lake la awali na kwamba yote yaliyosemwa na wakili ni yowe tu dhidi ya hoja nzito na zenye mashiko kwa mrufani. Akasisitiza rufaa ikubaliwe na amri zinazoombwa zikubaliwe na Mahakama hii pamoja na gharama inaporuhusu rufaa hii. Mahakama imesikiliza hoja na mawasilisho ya rufaa hii kutoka pande zote mbili kwa umakini utakiwao na swali la kujiuliza ni moja tu, endapo rufaa hii ina mashiko. Ni takwa la kisheria katika Nchi za Jumuiya ya Madola (common law jjurisdictions) Tanzania ikiwamo kuwa ili mdaawa katika shauri la madai aweze kushinda, basi ni muhimu saana ushahidi wa upande huo unaotaka ushindi uwe ni mzito zaidi kuliko ushahidi wa upande wa pili. Hayo tunayapata katika kifungu cha 110 (1) na (2) cha Sheria yetu ya Ushahidi Sura Na.6 marejeo ya 2019. Aidha kiwango cha kuthibitisha madai hayo ni 7 lazima yawe katika mizania ya ukweli kwamba mtu yeyote wa kawaida katika kupima uzito wa ushahidi wa pande hizo mbili ni lazima kwa kuzingatia ushahidi huo umuaminishe kufikia maamuzi hayohayo (tazama kifungu cha 3(2)(b), cha Sheria yetu ya Ushahidi kwamba mdaawa anayeomba kupewa ushindi lazima athibitishe madai yake katika viwango toshelevu vya ulinganifu wa mizani (pia shauri la Ernest Sebastian Mbele V. Sebastian Mbele and Others [2021] TZCA 168) . Matakwa hayo ya kisheria yalielezwa na mwandishi maarufu Sarkar, katika kitabu chake cha Sheria za Ushaidi Toleo la 18 kilichochapishwa na Lexis Nexis ukurasa wa 1896 (the legendary authors of Sarkar on Sarkar's Laws of Evidence, 18 Edn., M.C. Sarkar, S.C. Sarkar, and P.C. Sarkar, published by Lexis Nexis, katika ukurasa wa 1896) alieleza kwamba wajibu wa kuthibitisha madai ni kwa mdaawa anayeomba kupewa ushindi na si kwa mdaawa anayekana madai hayo. Halikadhalika pia, matakwa hayo yalielezwa katika shauri la ANTHONY M. MASANGA dhidi ya PENINA (MAMA MGESI) & LUCIA (MAMA ANNA), rufaa ya madai Namba .118 ya 2014 Mahakama ya Rufani ya Tanzania (haijaripotiwa). Katika shauri la HEMEDI SAIDI vs MOHAMED MBILU (1984) TLR 113, Mahakama iliamua kwamba 8 mdaawa mwenye ushahidi mzito na wa kuaminika unaothibitisha madai yake katika mizani na viwango toshelevu ndiye anapaswa kupewa ushindi. Ni msimamo wa kisheria pia kwa nyaraka yoyote inapopokelewa kama kielelezo katika kesi, siyo ukamilifu wa ushahidi wake Mahakamani, maana kupokelewa ni jambo moja, uzito wa ushahidi kwa yaliyomo humo ni jambo jingine. Hivyo basi nyaraka inawezapokelewa kama ushahidi kwa kukidhi vigezo vya kimapokezi kama vile kuambatishwa katika hati ya madai, nakala halisi na inatolewa na mtu sahihi (Order VII, Rule 14(1) and 8 (2), Order VII, Rule 18 (1) of the Civil Procedure Code, Cap 33 pamoja na vifungu 61 – 75 vya Sheria ya Ushahidi Sura Na. 6) – Tazama kesi ya Charles Humphrey Richard Simion na Mwenzake dhidi ya Dar es Salaam City Council na Mwenzake, Rufaa ya Madai Na. 303 ya 2021, Mahakama ya Rufani – Dsm. Katika shauri hili, nyaraka zinazofanya maamuzi ni mbili (manunuzi ya 1977 kwa Mrufani na mauziano ya 1983 ambayo yamewekwa katika kumbukumbu mwaka 2023 kwa mrufaniwa). Mrufani anasema alinunua Mwaka 1977 kwa shilingi 500. Muuzaji ni Daudi Zuberi na Mnunuzi ni Laurent Sayida Doto. Ni mauziano ya tarehe 10/10/1977 mbele ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi – Tawi la Migunga – Kishapu. Walioshuhudia ni Cheyo Chalya, 9 Sayida Doto na Pugu Nkuba. Kwa bahati mbaya wote hao (Muuzaji na mashuhuda) hakuna hata mmoja aliyefika Barazani kutoa ushahidi wake ili kuunga mkono hoja ya Mrufani. Ila kwa Mrufaniwa, Shahidi SM1, SM2, SM3 na SM4 wameunga mkono bayana kuwa Mrufaniwa alinunua eneo hilo kutoka kwa SM2; na huyo SM2 alieleza namna alivyolipata eneo hilo mwaka 1975 na hatimae alipoamua kuliuza lote Mwaka 1983. Hata hivyo kutokana na usumbufu wa mara kwa mara kutoka kwa Mrufani dhidi ya Mrufaniwa na yeye kuhusishwa kama shahidi kuhusiana na eneo hilohilo, mwaka 2023 tena baada ya ushauri aliamua kuweka mauziano hayo katika maandishi baada ya kutofanyika hivyo mwaka 1983. Nimepitia ushahidi uiliomo katika nyaraka zote mbili, kwa hakika hupati shaka ya kuamini ushahidi mmoja na kuupuuzia ushahidi mwingine. Kwanza ushahidi wa Mrufaniwa umeungwa mkono na muuzaji wake na kuelezea ni kwanini baada ya mauziano ya mdomo ya mwaka 1983 ameamua kuyaweka katika maandishi sasa ili kulinda masilahi ya Mrufaniwa kwa siku za usoni kutokana na mgogoro wao usioisha. Ushahidi huu unaungwa mkono na ushahidi wa Mrufaniwa mwenyewe (SM1), SM3 (jirani wa SM1) na SM4 (ndugu wa Wadaawa). Ushahidi wa Mrufani pamoja na uwepo wa nyaraka hiyo ya mwaka 1977, imekosa nguvu kutokana na kutokuwapo kwa shuhuda 10 wa mauziano hayo aliyefika Barazani kuelezea zoezi hilo la uuzaji na ununuzi hivyo ni ushahidi ambao haujaungwa mkono na shahidi yoyote yule. Mbili hata hiyo karatasi yenyewe ya mauziano na maandishi yaliyomo, inaonekana kuwa ni mpya zaidi kimuonekano kuliko hata karatasi (M1) ya mwaka 2023. Yaani karatasi ya mauziano ya mwaka 1977, haionyeshi hata ukongwe huo bali ni kama imeandikwa jana tu. Hivyo pamoja na kupokelewa kwake haikua kete ya ushindi au turufu ya ushindi maana pekee haikua ushahidi kamilifu ya umiliki wa eneo hilo. Hata hivyo, hasemi mara baada ya manunuzi ya eneo hilo mwaka 1977, ni nani alikua analitumia na kwa shughuli gani, na kwa nini mgogoro huo uibuke miaka ya 2016/2018 kama kweli eneo hilo ni lake kwa kipindi chonde hicho. Vinginevyo, hoja ya umiliki wa eneo husika bila tatizi (adverse possession) bado inaegeme zaidi kwa mrufaniwa kwa kua na utumiaji endelevu na usio na mawaa kwa zaidi ya kipindi cha miaka 12. Isitoshe ni msimamo wa kisheria sasa kuwa suala la umiliki wa ardhi pamoja na kuwa ni kesi ya madai, kiwango chake cha uthibitishaji siyo tu unapaswa kuwa katika mizania ya ulinganifu ya ukweli, bali uwe umethibitika ipasavyo ili kutoleta sintofahamu. Kuna paswa kuwapo na ushahidi wa uhakika, tosherezi na usioleta mashaka yoyote katika historia ya umiliki wake. Katika shauri hili, Mrufaniwa anaeleza ni vipi, amekua akilitumia eneo 11 hilo tokea 1983 na kwamba mzozo umeanza pale tu Mrufani aliporejea hapo kijijini baada ya shughuli za uchungaji kuisha. Kwa hakika, Mahakama hii imeridhika pasipo kuacha shaka kuwa ushahidi wa Mrufaniwa siyo tu ulikua ni mzito, bali wa uhakika, wa kuaminika na usio na chembe ya shaka hata kidogo dhidi ya Mrufani. Kwa sababu nilizoeleza hapo juu, Mahakama hii inatupilia mbali rufaa hii kwa sababu haina mashiko na maamuzi ya Baraza la chini yanaendelea kusimama kama yaliyoamriwa. Kutokana na shauri hili kuhusisha ndugu, kila upande utabeba gharama zake. Haki ya rufaa kwa hoja za kisheria inatamkwa kwa upande usioridhika. Hukumu hii imetolewa leo na kusainiwa hapa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Shinyanga tarehe 6 Desemba 2024. F.H. Mahimbali Jaji. 12