maria emirio ngoda vs jamhuri 2024 tzhc 258 16 february 2024
The prosecution failed to prove beyond reasonable doubt that the accused possessed government trophies; the chain of custody was broken; the caution statement was inadmissible; the inventory form was not lawfully prepared; the defense was not considered; conviction and sentence were quashed.
Source-derived case information.
- Citation
- maria emirio ngoda vs jamhuri 2024 tzhc 258 16 february 2024
- Parties
- Applicant: Maria Emirio Ngoda; Respondent: Jamhuri
- Court
- TZHC
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 16 February 2024
- Procedural Posture
- Criminal Appeal / Judgment
- Outcome
- appeal allowed
- Legal Topics
- Possession of Government Trophies, Chain of Custody, Admissibility of Evidence, Right to Legal Representation, Burden of Proof
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Maria Emirio Ngoda
Applicant
Jamhuri
Respondent
Procedural Posture
Criminal Appeal / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the charge of unlawful possession of government trophies was proved beyond reasonable doubt
- 2 Whether the chain of custody of the exhibit was properly established
- 3 Whether the caution statement was admissible
Ratio Decidendi
The prosecution failed to prove beyond reasonable doubt that the accused possessed government trophies; the chain of custody was broken; the caution statement was inadmissible; the inventory form was not lawfully prepared; the defense was not considered; conviction and sentence were quashed.
Court Disposition
appeal allowed
Orders
- conviction quashed
- sentence set aside
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (MASLJALA NDOGO YA IRINGA) ILIYOPO IRINGA. RUFAA JINAI NA. 37116 YA 2023 (Asi/ia Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 28/2022 la Mahakama ya Wi/aya ya Iringa mbete ya Mhe. S.A. Mkasiwa, HMM). MARIA EMIRIO NGODA.......................... MRUFANI DHIDI YA JAMHURI ......................... MRUFANIWA HUKUMU 01 & 16/02/2024 I.C. MUGETA, 3: Mrufani ambaye ni mkulima, mkazi wa Kijiji cha Isakalilo, Wilaya ya Iringa anawakilishwa na mawakili wapatao sita. Uwakilishi huo mzito ni matokeo ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii taarifa kwamba mrufani ametandikwa adhabu ya kifungo cha miaka 22 gerezani kwa kukutwa na hatia ya kumiliki nyara za serikali (vipande 12 vya nyama ya swala) jambo lililoibua maoni na hisia tofautitofauti miongoni mwa wanajamii. Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (Kanda ya Iringa) waliibuka na kutangaza dhamira ya kumsaidia kukata rufaa bure. Katika rufaa hiyo wamewasilisha sababu 13 za rufaa. Hatia ya mrufani ilitokana na mashtaka chini ya fungu la 86(1) na (2), (c)(ii) Sheria ya Uhifadhi Wanyama Pori No. 5/2009, ikisomwa i pamoja na aya ya 14 ya jedwari na kifungu cha 57(1), kifungu cha 60(1) na (2) vya Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uharifu wa Kupangwa [Sura 200 Toleo Rekebu (T.R) la 2022]. Maelezo ya tuhuma kwenye hati ya mashitaka ni kwamba mnamo tarehe 19/11/2022, akiwa eneo la Isakaliio, Wilaya na Mkoa wa Iringa, mrufani alikutwa akimiliki vipande 12 vya nyama ya swala vyenye thamani ya fedha za kitanzania 904,757.01 mall ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kibali wala ieseni halali ya umiliki kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori. Malalamiko yaliyomo kwenye sababu 13 za rufaa ni kwamba mahakama ya chini ilijipotosha kisheria na kimantiki kwa kumtia hatiani na kumpa mrufani adhabu tajwa hapo juu kwa ushah idi ambao hauthibitishi shtaka bila kuacha mashaka ya msingi. Baadhi ya sababu za rufaa zinashabihiana hivyo nitaziunganisha. Muhtasari wake ni kama ifuatavyo: 1. Kwamba, shtaka haiikuthibishwa bila kuacha mashaka ya msingi kwa viie haikuthibishwa kwamba nyama husika n i ya mnyama swaia; 2. Kwamba, maeiezo ya onyo ya mrufani yaiiyopokeiewa kama kieieiezo P3 ni haramu kisheria; 3. Kwamba, nyama anayodaiwa mrufani kukutwa nayo iliharibiwa bi/a kuzingatia utaratibu na fomu iiiyotunza ripoti ya uharibifu huo (inventory form) iiiyotoiewa kama kielelezo P2 iiitayarishwa kinyume cha sheria na iiitolewa mahakamani na shahidi asiyestahiki kufanya hivyo; 4. Kwamba, mnyororo wa utunzaji wa nyama husika (chain o f custody) haukuthibishwa kama itakiwavyo na sheria. 5. Wakati wa usikiiizaji wa shauri kifungu cha 231(l)(a)(b) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai[Sura ya 20 T.R 2022] kiHkiukwa na mheshimiwa Hakimu; 6. Kwamba, mahakama ya chini haikuzingatia ushahidi wa mrufani katika kufikia uamuzi wake. 7. Kwamba, adhabu aiiyopewa mrufani ni kubv/a kuiiko inavyostahiii na iiipotoiewa mheshimiwa Hakimu aiiegemea sana kwenye maeiezo ya historia ya jinai ya mrufani (aggravating factors) ambayo yaiitoiewa na mwendesha mashitaka kiupotoshaji 8. Kwamba, mrufani aiinyimwa uwakiiishi mahakamani kinyume na fungu la 33(l)(a)(b) la Sheria ya Msaada wa Kisheria No. 01/2017. Mawakili wanaomwakilisha mrufani waliongozwa na wakili msomi Barnabas Nyalusi akisaidiwa na wasomi mawakili Moses Ambindwile, Innocent Kibadu, Cosmas Kishamawe, Joshua Chussy and Letitia Petro. Mawakili wa Mrufaniwa waliongozwa na Msomi Wakili wa Serikali Yahya Misango akisaidiwa na wasomi mawakili Majid Matitu na Barton Maya la. Mawakili wote hawa kiia mmoja alisimama kuzungumzia mojawapo ya sababu za rufaa zilizowasilishwa na sababu moja iliyoongezwa wakati wa usikilizaji. Kwa vile sababu hizo nimeziunganisha, sitarudia alichozungumza kila mmoja wao. Hoja muhimu zitazingatiwa wakati wa uchambuzi wa ushahidi ambapo nitarejeiea hoja ya kila mzungumzaji na kumtaja kadri itakavyohitajika. Nimetafakari mambo yanayolalamikiwa nimeridhika kuwa sababu kuu ya rufani ni kwamba shtaka halikuthibitishwa bila kuacha mashaka ya msingi. Sababu nyingine za rufaa, ukiondoa lalamiko la mrufani kutopewa uwa kilishi, zihaunga mkono hoja hiyo kuu. Hivyo, nitahitimisha hukumu hii kwa kujibu hoja hiyo kuu kwa kuzingatia malalamiko madogo yanayoiunga mkono. Nitaanza na lalamiko la uhalali wa kisheria wa maelezo ya onyo ya mrufani. Maelezo ya onyo ya mrufani yalipokelewa mahakamani kama "kielelezo P3". Msomi Hakimu Mkazi Mkuu alitumia maelezo hayo kumtia hatiani mrufani baada ya kuamini yalipokelewa kihalali na alikiri kosa alipoyaandika. Ukurasa wa 11 wa hukumu imeandikwa: "Exhibiti P3 postulated that the accused person was found in possession o f twelve (12) pieces o f m eatoflm pala (sic)". Tafsiri yake ni kwamba "kielelezo P3" kinadhihirisha kwamba mshtakiwa alikutwa na vipande 12 vya nyama ya swala. Mawakiii wa mrufani hawakubaliani na hitimisho hili la mheshimiwa hakimu. Wakili Msomi Innocent Kibadu ndiye alizungumzia lalamiko hili. Hoja yake ni kwamba maelezo:hayo ni haramu kwa vile yaliandikwa nje ya masaa manne yanayotakiwa na fungu la 50(l)(a) la Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai [Sura 20 T.R 2022] na uthibitisho (certification) na uandishi wake uiikiuka fungu la 58(1) la sheria tajwa. Kwamba, ushahidi unaonyesha mrufani alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi saa kumi jioni tarehe 19/11/2019. Maelezo yake yaliandikwa saa mbili asubuhi tarehe 20/11/2022. Wakili wa Serikali, Yahya Misango, alikiri kwamba maelezo hayo yaliandikwa kinyume cha sheria hivyo hayafai kutumika kama ushahidi. Ninakubaliana na hoja ya pande zote mbili kwamba maelezo yaliyoandikwa kinyume cha sheria hayawezi kutumika kumtia hatiani aliyeyaandika kama ilivyoamliwa katika shauri la Mkwavi Njeti dhidi ya Jamhuri, Rufaa Jinai No. 301/ 2015, Mahakama ya Rufani - Iringa (haijaripotiwa) ukurasa wa 7. Hivyo, ninayafuta maelezo hayo kutoka kwenye kumbukumbu za ushahidi wa shauri hili. Kwa uamuzi huu hakuna haja ya kujadili iwapo uthibitisho na uandishj wa maelezo viko sawa. Msomi wakili Moses Am bindwile alijikita katika hoja tatu kuhusu utayarishaji na kupokelewa mahakamani kwa kielelezo P2 ambacho ni orodha ya nyama iliyoharibiwa kwa amri ya mahakama. Mosi, alisema, hakuna ushahidi kuwa nyama husika ni nyama ya swala. Kwa maoni yake, ushahidi wa Mkude MaJeko (PW3) ambaye ni mthaminishaji wa nyara za serikaii kuwa alitambua nyama hiyo ni ya swala kutokana na mbavu (ribs) na misuli (fibres) kuwa minene kuliko ya wa nyama wa kufugwa hautoshi kwa vile wa nyama wa kufugwa wako wengi hivyo alipaswa kumtaja mnyama wa kufugwa ambaye alimtumia kulinganisha hizo mbavu na misuli. Msomi wakili alidai njia sahihi ya kutambua aina za nyama ni kwa kutumia mfumo wa anatomia (anatomy) unaojumuisha uchambuzi wa rangi ya ngozi, muundo (texture) wa nyama, harufu, mafuta katika nyama na muundo (structure) wa mifupa au DNA. Alisisitiza, huku akirejea andiko la Professor Bharama Gupta liitwalo "Speciation of Meat" kwamba PW3 alipoamua kutumia anatomia ya misuli na mifupa alipaswa kumtaja mnyama wa kufungwa anayefanana na swala aliyetumika kufanya ulinganifu. Pili, kwamba wakati amri ya kuharibiwa nyama hiyo ilipotolewa na hakimu na kutayarishwa kwa kielelezo P2 ambayo ni fomu ya orodha ya mali iliyoharibiwa kwa amri ya mahakama, mrufani hakushirikishwa kama inavyotakiwa na Amri Kuu za Polisi (PGO) 229 aya ya 25 na kufafanuliwa katika shauri la Nyamhanga Mwise Muhere dhidi ya Jamhuri, Rufaa Jinai No. 304/2020, Mahakama ya Rufani - Musoma (haijaripotiwa) ukurasa wa 10 - 12. Tatu, kwamba kielelezo hicho sharti kingetolewa na hakimu aliyekiandaa badala ya D.4395 D/Cpl Lubeya (PW2) ambaye ni mpelelezi wa kesi hii. Katika Majibu yake, Majid Matitu aliirejesha mahakama kwenye ukurasa wa 31 wa mwenendo wa shauri ambapo shahidi, ndugu Mkude alizungumzia tofauti ya mbavu na misuli ya wanyama pori na wanyama wa kufugwa kwamba mbavu na misuli ya Wanyama pori ni minene. Pia kwamba nyama ile ilikuwa na ngozi aliyoitambua kwamba ni ya swala. Kwa maarifa yake ya kitaaluma aliyoyapata katika Chuo cha Uhifadhi Wanyama Pori - Mwika na Chuo Kikuu cha Sokoine na uzoefu wa shahidi wa miaka minane kazini, alihitimisha wakili Matitu, shahidi ndugu Mkude anapaswa kuaminiwa kwamba nyama ile ni ya swala. Aliomba mahakama izingatie uamuzi katika shauri la William Maganga dhidi ya Jamhuri, Rufaa Jinai No. 104/2020, Mahakama ya Rufani - Tabora (haijaripotiwa) ambapo ilielezwa kwamba kwenye kutumia ushahidi wa wataalamu kwenye masuala ya wanyama, ushahidi wa sayansi ya Wanyama au uzoefu wa shahidi kwenye masuala ya uhifadhi vinaweza kutumika. Kuhusu namna fomu ya orodha ya mali ilivyopatikana, msomi wakili Matitu alisema saini ya mrufani kwenye hat! hiyo inathibitisha kwamba alikuwepo wakati hakimu alipotoa amri ya kuharibiwa kwa nyama na kwamba shahidi D/Cpl. Lubeya alistahili kuitoa orodha hiyo mahakamani kielelezo P2, Nitaanza na utambuzi wa nyama. Wanyama wa kufugwa wanaoliwa ni parnoja na sungura na ng'ombe. Ni hakika nao pia wana mbavu. Wakati mbavu na misuli ya swala ni minene kuliko ya sungura, kamwe haiwezi kuwa minene kuliko ya ng'ombe, Hivyo siyo kweli kwamba mbavu na misuli ya wanyama pori wote ni minene kuliko wanyama wa kufugwa. Swala hawezi kuwa na mbavu nene kuliko ng'ombe. Ninakubaliana na insomi wakili Matitu ni sahihi ndugu Mkude alisema nyama ile ilikuwa na ngozi ambayo aliitambua ni ya swala. Changamoto ya ushahidi huu ni kutoelezea sifa za ngozi ya swala. Mtu yeyote anaweza kusema "hii ni ngozi ya swala". Kwa mtaalamu tunategemea maelezo yanayozingatia taaluma husika badala ya maelezo ya kiujumla. Ndugu Mkude alishindwa katika hilo. Hivyo, ushahidi wake wa unene wa mbavu na kuwepo kwa ngozi, kwa maoni yangu, hautoshi kuthibitisha kwamba nyama ile ilikuwa ya swala pale ambapo hakumtaja mnyama wa kufugwa aliyemtumia kulinganisha mbavu na kueleza sifa za ngozi ya swala kitaaluma kwa lengo la utambuzi. Ushahidi wa kitaalamu unatambulika chini ya kifungu cha 47 cha Sheria ya Ushahidi [Sura 6 T.R 2022]. Hata hivyo, siyo lazima kuuzingatia kama unakiuka uhalisia wa mambo au kanuni na mbinu za utambuzi zinazofahamika. Haya yalisemwa kwenye kesi ya Jamhuri dhidi ya Kerstin Cameron [2003] TLR 84 ukurasa 132 na Yusuph Molo dhidi ya Jamhuri, Rufaa Jinai Na. 343/2017, Mahakama ya Rufani - Iringa (haijaripotiwa) ukurasa wa 13. Ninahamia kwenye hoja ya ujazaji wa orodha ya nyama iliyoharibiwa, kielelezo P2. Katika kesi ya Nyamhanga Mwise Muhere (hapo juu) Mahakama ya Rufani ilisema hivi kuhusu utaratibu wa kujaza fomu ya mali inayoharibiwa kwa amri ya mahakama: "... while PW3 was fully entitled to seek and obtain a disposal order from the primary court magistrate, the inventory form (exhibit P3), which came out cannot be proved against the appellant because he was not given the opportunity to be heard by the primary court magistrate at the time o f making the order to dispose the exhibit Kwa tafsiri rahisi mahakama inasema kwamba fomu ya kuharibu mali ilitayarishwa bila mtuhumiwa kusikilizwa maoni yake na hakimu haiwezi kutumika kama ushahidhi dhidi ya mtuhumiwa huyo. Utaratibu wa mtuhumiwa kuhudhurishwa wakati wa kutolewa amri ya kuharibu kielelezo unapatikana Amri Kuu za Polisi (PGO) 229 aya ya 25 na uiishaelezwa katika kesi ya Mohamed Juma @ Mpakama dhidi ya Jamhuri [2019] 1 T.L.R 514 kwamba mtuhumiwa lazima awepo mbele ya hakimu na apewe fursa ya kusikilizwa. Katika shauri hiii ni kweli mtuhumiwa alitia saini kwenye kilelelezo P2 lakini hakuna ushahidi kwamba alikuwepo mbele ya hakimu au kwamba alisikilizwa maoni yake kuhusu kuharibiwa kwa kielelezo hicho. Mpelelezi D/Cpl. Lubeya alisema aiipeleka nyama kwa hakimu. Hakusema aiipeleka nyama pamoja na mrufani. Hivyo, kuna uwezekano saini yake iliwekwa akiwa sehemu nyingine na hii inajenga mashaka ya msingi kuhusu uhalali wa kielelezo hicho. Kwa upande mwingine, nimeridhishwa na maelezo ya msomi wakilj Matitu kwamba D/Gpl Lubeya, kama mpelelezi wa kesi, alistahili kutoa kielelezo hicho mahakamani hivyo kilipokelewa kihalali ingawa ushahidi wake hauna thamani. Haikuwa lazima kutolewa na hakimu aliyekiandaa kama kungekuwa na ushahidi kuwa taratibu zilizingatiwa. Hoja kuhusu mnyororo wa utunzaji (chain of custody) wa nyama kabla ya kuharibiwa ilizungumziwa na msomi wakili Cosmas Kishamawe. Kwamba, katika ushahidi uliotolewa hakuna mfumo maandishi (paper trail) wa utunzaji wa nyama uliowasilishwa mahakamani kuonyesha jinsi ambavyo mashahidi, Onesphory Kahiga (PW1), G.4395 D/Cpl Lubeya (PW2), Mkude Maleko (PW3), F. 8404 CpI. Owago (PW5) na WP. Agness (PW6) walibadilishana kielelezo hicho hadi amri ya kukiharibu ilipopatikana. Ninakubaliana na majibu ya wakili Misango kwamba mnyororo wa utunzaji kwenye shauri hili ulithibitishwa kwa ushahidi wa mdomo badala ya maandishi. Ninakubaliana naye pia kuna muunganiko wa ushahidi wa mdomo unaonyesha PW1, PW2, PW5 na PW6 walivyopokezana nyama hiyo. Changamoto iliyopo ni kuhusu nani alimkabidhi mthaminishaji (PW3) nyama hiyo. PW3 alisema alipewa na D/Cpl. Lubeya tarehe 19/11/2022. Hii siyo kweli kwa sababu tarehe 19/11/2022, D/Cpl. Lubeya alikuwa hajapangiwa kuanza upelelezi wa shauri hili. Kuthibitisha hilo, katika ushahidi wake ukurasa wa 25 D/Cpl. Lubeya anasema: "On 20/11/2022 I was at my working station (sic) where I was assigned to investigate the m atter..." Tafsiri yake ni kwamba D/Cpi. Lubeya kama mpeleiezi alianza majukumu yake tarehe 20/11/2022. Ushahidi huo unaungwa mkono na mtunza vielelezo (PW5) ambaye katika ukurasa wa 40 wa mwenendo wa shauri alisema: "On 20/11/2022 in the afternoon there was investigator one D/Cpi. Lubeya came where needed (sic) the said exhibit for further investigation" Ushahidi unaonyesha kwa tarehe 19/11/2022 waliokuwa na nyama hiyo ni Onesphory kahiga (PWl), WP. Agness (PW6) na CpI. Owago (PW5) kama waiivyosema wenyewe. Kwa mantiki ya ushahidi uliopo, hakuna namna ndugu Mkude angepokea nyama hiyo kutoka kwa D/Clp. Lubeya siku ya tarehe 19/11/2022 kama anavyodai katika ushahidi wake. Kwa msingi huo nyama aliyochunguza kutoka kwa D/Cpl. Lubeya tarehe 19/11/2022 siyo nyama inayobishaniwa katika shauri hili. Ninakubaliana na wakiii Kishamawe kwamba mnyororo wa utunzaji nyama hiyo ulikatika. Hali hii inaieta shaka kwenye ushahidi wa mrufaniwa. Kwa upande wake msomi wakiii Barnabas Nyalusi aiitolea maelezo hoja kuwa utetezi wa mrufani haukuzingatiwa na mahakama ya chini. Ushahidi ambao haukuzingatiwa, alisema wakiii Nyalusi, ni madai ya 12 mrufani kuwa ndoo iliyokuwa na nyama haikuwa yake bali ilikuwa mali ya Kibuna Fute. Katika majibu yake Wakili wa Serikali, Yahya Misango alisema mrufani alikiri kosa kama inayoonekana katika ukurasa wa 54 wa mwenendo wa shauri. Kwa maoni yake ushahidi wa mtuhumiwa anayekiri mwenyewe ni ushahidi bora zaidi kumtia hatiani kama ilivyoelezwa kwenye shauri la Nyerere Nyague dhidi ya Jamhuri, Rufaa Jinai No, 67/2010, Mahakama ya Rufani - Arusha (haijaripotiwa) ukurasa wa 14 kwamba ungamo linalofanyjka mahakamani lina nguvu kuliko uthibitisho mwingineo. Nitaanza kwa kuchunguza iwapo utetezi wa mrufani ulizingatiwa na kumaiizia na iwapo alikiri kosa. Hukumu ya mahakama ya chini ina kurasa 24 bila kujumuisha kurasa 4 za mwisho zinazobeba adhabu na mchakato wake. Kwenye ukurasa wa 8 mheshimiwa hakimu ametoa muhtasari wa ushahidi wa utetezi wa mrufani. Imeandikwa hivi kwa sehemu: '7/7 her defence DW1 one Maria Emirio Ngoda who was also the accused in this case told this court that, it was true that she was found at the alleged place with the plastic bucket covered with a Hd" 13 Kwa ufupi tafsiri yake ni kwamba mrufani alikiri kukutwa kwenye eneo husika akiwa na ndoo ya plastic iliyofunikwa. Baada ya kufanya uchambuzi wa ushahidi katika ukurasa wa 12 Msomi Hakimu Mkazi Mkuu alihitimisha: "... DW1 who is also the accused person in this case conceded that she was found in possession o f the said twelve (12) pieces ofimpala, " Tafsiri yake ni kwamba mrufani alikiri kukutwa na nyama ya swala vipande 12. Hii siyo kweli mrufani hakukiri sehemu yoyote isipokuwa kwenye maelezo yake ya onyo ambayo nimeyafutilia mbali. Mheshimiwa hakimu atakuwa alipotoshwa na maelezo hayo ambayo ni haramu. Utetezi wa mrufani unapatikana katika ukurasa wa 52 - 54 wa mwenendo wa shauri. Katika ukurasa wa 52 - 53 alisema: "It is true that I was found at the alleged place seating (sic) where nearby me there was a plastic bucket covered with a lid. I found the said bucket with a woman when I arrived at the said area. ... Thereafter the said woman departed and told me she was going to her home to take money as she had forgotten. After about 15 minutes I saw people coming accompanied by chairman o f the street (sic). The chairman stated that they were suspicious with what contained in 14 the bucket. They told me to open. I denied and told them that the bucket was not mine. It was belonged (sic) to Kibuna Fute." Tafsiri fupi ya ushahidi huo ni kwamba mrufani anakubali kukutwa eneo la tukio lakini ndoo inayodaiwa kukutwa na nyama si yake bali ni ya Kibuna Fute aliyemkuta katika eneo hilo na ndoo hiyo kabla hajaondoka kwa madai kwamba anaenda kuchukua hela zake alizozisahau nyumbani. Baada ya kama dakika 15 watu walioambatana na mwenyekiti walifika na walipomtaka afunue ndoo hiyo alikataa kwa vile si mali yake. Ushahidi huo ni wa msingi sana katika utetezi wa mrufani. Nimepitia hukumu yote ya mahakama ya chini hakuna sehemu ambapo ushahidi huu umezingatiwa hivyo lalamiko kwamba utetezi wake ulipuuzwa na Hakimu Mkazi Mkuu lina mantiki. Pia, licha ya kupuuzwa kwa utetezi huo, kwa maoni yangu hauonyeshi kukiri kwa mrufani kinyume na hitimisho la mheshimiwa hakimu. Kukutwa katika eneo la tukio na kuwa mmiliki wa ndoo yenye nyama ni vitu viwili tofauti. Hakika, kama mheshimiwa hakimu angeelekeza akili yake kwenye utetezi huu angeona kwamba mashtaka hayakuthibitishwa. Kwa utetezi wa mrufani, umiliki haukuthibitishwa. 15 Mashahidi waliokuwa kwenye eneo la tukio ni Onesphory Kahiga (PW1) na Maisha Modestus Kiuko. Onesphory ni askari mkamataji na Maisha ni mwenyekiti wa mtaa wa Isakalilo. Kwenye ushahidi wake (ukurasa wa 18 wa mwenendo) kuhusu umiliki wa ndoo Onesphory alisema: "... we saw the accused with a bucket o f m eat" Kwa upande wake Maisha Kiuko (ukurasa wa 37 wa mwenendo) alisema: "Maria ngoda had a bucket on her fron t" Ushahidi wa wawili hawa unakinzana kuhusu ilipokuwa ndoo. Onesphory anasema mrufani aliibeba na Maisha anasema ilikuwa mbele yake. Kwa vile Onesphory kama askari mkamataji katika shauri ana maslahi ya kulinda ushahidi wake unapaswa kuungwa mkono na uungwaji mkono huo haupo kwa sababu shahidi huru ndugu Maisha alielezea hadithi tofauti na yake. Yeye anasema ndoo ilikuwa mbele ya mrufani. Ushahidi wa ndugu Maisha unarandana na wa mrufani kwamba ndoo ilikuwa pembeni yake. Hivyo, nimeridhika kuwa upande wa mashtaka haukuthibitisha kuwa mrufani alikutwa amebeba ndoo hiyo. Kwa kuzingatia utetezi wake na ushahidi wa mwenyekiti wa mtaa, hakuna sababu ya kutomwamini kwamba ndoo hiyo haikuwa ya kwake. 16 Mheshiwa Hakimu Mkazi Mkuu aliuelewa vibaya (misapprehend) ushahidi na kufikia hitimisho potofu. Hebu tutazame kilichoko ukurasa wa 54 wa mwenendo ambako wakili Misango anadai kuna kiri ya mrufani. Imeandikwa: "Kibuna Fute is not my relative. She is not my dose friend. I was found with Kibuna and a bucket while drinking intoxicating liquor (sic). I did a mistake to agree to take care o f the said bucket. She told me that, I should take care for the said bucket so that she will come back, she w ill give me Tshs. 1,500/=." Kwa maoni yangu anachokiri mrufani ni kwamba ndoo hiyo ilikuwepo lakini haikuwa yake. Ni mali ya Kibuna Fute. Katika ushahidi wake alisema Mwenyekiti anamfahamu Kibuna Fute na aliwapeleka kwake ila hawakumkuta. Ushahidi huu haukupingwa na unapaswa kuaminiwa. Upande wa mashitaka ulipaswa kuthibitisha bila kuacha shaka ya msingi kwamba ndoo hiyo na nyama yake ilikuwa ni mali ya mrufani. Ushahidi huo haupo. Kwa haya niliyoeleza, nimeridhika kuwa mrufani alitiwa hatiani kimakosa. Baada ya kufikia hitimisho hilo, itakuwa kwa manufaa ya kitaaluma kujielekeza katika kujadili malalamiko yaliyobakia. Malalamiko hayo yanahusu kutozingatiwa kwa kifungu cha 231(l)(a)(b) cha Sheria 17 ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai [Sura ya 20 T.R 2022], adhabu aliyopewa kuwa kinyume cha sheria na kunyimwa uwakilishi wa sheria. Kwa madhumuni ya shauri hili nitaishia hapa. Hayo mengine yanaweza kusubiri nafasi na muda mwingine utakaofaa. Mwisho, natamka kwamba, shtaka dhidi ya mrufani halikuthibitishwa. Ushahidi dhidi yake una mashaka ya msingi. Kwa sababu hiyo ninatoa amri kwamba rufaa hii imeshinda. Hatia ya mrufani nimeibatilisha na adhabu anayoitumikia nimeifuta. Wanaomshikilia gerezani sharti wamwachilie mara moja isipokuwa kama wana amri nyingine halali isiyotokana na shauri hili ya kuendelea kumshikilia. Na iwe hivyo 16 / 02/2024 Mahakama: Hukumu hii imesomwa kwenye mahakama ya wazi wakiwepo Majid Matitu na Barton Mayage, Wakili wa Serikali, Letitia Petro Ntagazwa, Innocent Kibadu na Cosmas Kishamawe, Mawakili wa Utetezi pa moja na Mrufani. Imesainiwa: I.C. MUGETA JAJI 16 / 02/2024 18