mwana 20010101015803
The appellant failed to prove legal ownership of the disputed land as there was no evidence of proper transfer of title from the estate of Shabani Lukindo to Idd Shabani Lukindo, and thus any purported sale to the appellant's predecessor was void. The land remains part of the estate of the late Shabani Lukindo, and...
Source-derived case information.
- Citation
- mwana 20010101015803
- Parties
- Appellant: Mwanaidi Nuru Tengeneza (kama msimamizi wa mirathi ya marehemu Nuru Khamis Tengeneza); Respondent 1: Hamis Shabani Ali; Respondent 2: Ramadhani Athumani White; Respondent 3: Musa Ali; Respondent 4: Amosi Magili; Respondent 5: Nasoro Rashid Lukindo Shehe; Respondent 6: Rashid S. Maguku; Respondent 7: Hussein Mkwabi; Respondent 8: Mnyema Daudi; Respondent 9: Masele Hamisi Ali; Respondent 10: Mwajabu Ali; Respondent 11: Ali Mashaka
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2001
- Procedural Posture
- Land Appeal / Judgment
- Outcome
- Appeal dismissed
- Legal Topics
- Ownership Dispute, Succession, Burden of Proof, Adverse Possession, Family Property, Sale of Land
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Mwanaidi Nuru Tengeneza (kama msimamizi wa mirathi ya marehemu Nuru Khamis Tengeneza)
Appellant
Hamis Shabani Ali
Respondent 1
Ramadhani Athumani White
Respondent 2
Musa Ali
Respondent 3
Amosi Magili
Respondent 4
Nasoro Rashid Lukindo Shehe
Respondent 5
Rashid S. Maguku
Respondent 6
Hussein Mkwabi
Respondent 7
Mnyema Daudi
Respondent 8
Masele Hamisi Ali
Respondent 9
Mwajabu Ali
Respondent 10
Ali Mashaka
Respondent 11
Procedural Posture
Land Appeal / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the appellant proved legal ownership of the disputed land
- 2 Whether the sale of the land by Idd Shabani Lukindo to the appellant's predecessor was valid
- 3 Whether the trial tribunal erred in declaring respondent 5 as owner
Ratio Decidendi
The appellant failed to prove legal ownership of the disputed land as there was no evidence of proper transfer of title from the estate of Shabani Lukindo to Idd Shabani Lukindo, and thus any purported sale to the appellant's predecessor was void. The land remains part of the estate of the late Shabani Lukindo, and the appellant's long-term occupation as an invitee does not confer ownership.
Court Disposition
Appeal dismissed
Orders
- Appeal is dismissed for lack of merit
- Each party to bear their own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MASJALA NDOGO YA TABORA ILIYOPO TABORA RUFAA YA ARDHI NA. 27719/2023 (IHyotokana na uamuzi katika Maombi ya Ardhi Na. 84/2020 katika Baraza ia Ardhi na Nyumba ia Wilaya ya Tabora, lililopo Tabora) MWANAIDI NURU TENGENEZA (kama msimamizi wa mirathi ya marehemu Nuru Khamis Tengeneza)....................... MRUFANI DHIDI YA HAMIS SHABANI ALI........................................ MJIBU RUFAA NA. 1 RAMADHANI ATHUMANI© WHITE.................... MJIBU RUFAA NA. 2 MUSA ALI......................................................... MJIBU RUFAA NA. 3 AMOSI MAGILI........... MJIBU RUFAA NA. 4 NASORO RASHID LUKINDO© SHEHE................ MJIBU RUFAA NA. 5 RASHID S. MAGUKU.......................................... MJIBU RUFAA NA. 6 HUSSEIN MKWABI............................................. MJIBU RUFAA NA. 7 MNYEMA DAUDI................................................ MJIBU RUFAA NA. 8 MASELE HAMISI ALI............................. MJIBU RUFAA NA. 9 MWAJABU ALI................................................. MJIBU RUFAA NA. 10 ALI MASHAKA.................................................. MJIBU RUFAA NA. 11 HUKUMU MANGO, J. 1 Mrufani Mwanaidi Nuru Tengeneza (Msimamizi wa Mirathi ya Marehemu Nuru Khamis Tengeneza) aliwasilisha rufaa hii dhidi ya Uamuzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Tabora kwenye shauri la Maombi ya ardhi Na.84 la 2020. Kwenye shauri hilo, Mrufani aliwasilisha madai yake kuhusu umiliki shamba lenye ukubwa wa ekari 27 kwa makadirio lililopo, kijiji cha Mabama ndani ya Halmashauri ya Tabora. Mrufani anadai kuwa eneo hilo ni sehemu ya mirathi ya Marehemu Nuru Hamis Tengeneza na kwamba marehemu Nuru Hamisi Tengeneza alipata umiliki wa eneo hilo kwa kulinunua kutoka Iddi Shabani. Kwa upande wa Wajibu Rufaa ambao walikuwa wajibu Maombi mbele ya Baraza la Wilaya la Ardhi na Nyumba Tabora, walidai eneo linalobishaniwa ni sehemu ya mirathi ya Marehemu Shabani Lukindo. Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, Baraza la Ardhi na Nyumba lilitupilia mbali shauri hilo kwa kukosa mashiko. Mrufani hakuridhika na uamuzi huo hivyo aliwasilisha rufaa yake mbele ya mahakama akiwa na sababu nne za rufaa kama ifuatavyo: - 1. Kwamba, Baraza lilifanya makosa makubwa ya kisheria na kimantiki kwa kumpatia ushindi mjibu rufaa na. 5, kwa kumtangaza kuwa ni mmiliki halali wa ardhi inayobishaniwa (yenye ukubwa wa ekari 27) kwa kuzingatia kwamba baba wa Mrufani alikuwa mwalikwa/mkaribishwaji tu, wakati kinyume chake alikuwa mmiliki halali wa ardhi yenye mgogoro baada ya kununua kutoka kwa Iddi Shaban Lukindo jambo ambalo lilithibitishwa vikali na ushahidi wa PW2 (mtoto wa Iddy Shabani Lukindo) hivyo kufikia hitimisho lisilo sahihi. 2. Kwamba, Baraza lilifanya makosa makubwa kisheria na kimantiki kwa kumuunga mkono mjibu rufaa na. 5 pasipo kuzingatia ushahidi wa Mrufani 2 ambaye baba yake alikuwa akimiliki ardhi yenye mgogoro tangu mwaka 1960 na ardhi tajwa ilikuwa katika umiliki wao hadi kufariki kwake kwa amani bila kusumbuliwa, hata Iddi Shabani Lukindo ameishi hapo kwa zaidi ya miongo minne, hivyo kufikia matokeo yasiyo sahihi; 3. Kwamba, Baraza lilifanya makosa makubwa kisheria na kimantiki kwa kumuunga mkono mjibu rufaa na. 5 bila kuzingatia ushahidi wa mashahidi wa Mrufani PW2, PW3,PW4 ( Mke wa Iddy Shaban Lukindo) na PW5 ambao ulikuwa na mzito ukilinganisha na ushahidi wa DW1 na mashahidi wake wengine; 4. Kwamba, Baraza lilifanya makosa makubwa ya kisheria na kimantiki kwa kumpatia ushindi mjibu rufaa na. 5 kwa kutokuzingatia uzito wa ushahidi. Katika usikilizaji wa shauri mbele ya mahakama hii, Mrufani aliwakilishwa na wakili msomi Hassan Kilingo wakati Mjibu rufaa Na. 5, Nassoro Rashid Lukindo @Salehe akijisimamia mwenyewe. Baada ya mahakama kujiridhisha kwamba Wajibu rufaa na. 1, 2, 3, 4, 6, 7, 8, 9, 10 na 11 walipatiwa wito kupitia chapisho katika gazeti la Mwananchi la tarehe 14 May 2024 katika ukurasa wa 21, usikilizwaji wa shauri hili uliendelea bila uwepo wa wajibu rufaa hao ambao hawakufika Mahakamani licha ya kupatiwa wito wa Mahakama. Katika utetezi wa rufaa hii wakili Kilingo alianza na sababu za rufaa na. 1,3 na 4 kwa pamoja kisha alimalizia na sababu ya pili. Katika sababu ya 1, 3, na 4, wakili alieleza kwamba Baraza la Ardhi na Nyumba la Tabora lilikosea kisheria na kimantiki kwa kumtangaza mjibu rufaa kuwa mmiliki wa eneo linalobishaniwa la ekari 27 na kutamka kuwa baba wa mrufani alikuwa ni mkaribishwaji tu. Alifafanua kwamba baba wa Mrufani alinunua ardhi husika 3 kutoka kwa Idd Shabani Lukindo. Wakili msomi alisisitiza kwamba, maelezo ya mrufani kuhusu ununuzi huo yanaungwa mkono na mashahidi PW2, PW3, PW4 na PW5. PW2, Mohamed Idd Shaban Lukindo ni mtoto wa mmliki wa ardhi ambaye alimuuzia baba wa mrufani. Wakili ameeleza zaidi kwamba, kwa mujibu wa maelezo ya PW2 hakuna ndugu yoyote wa Shabani Lukindo aliyedai eneo husika kwa sababu wanajua shamba husika limeuzwa. Wakili aliongelea pia ushahidi uliotolewa na PW4 Halima Musa Matambo ambaye alikuwa Mke wa Idd Shabani Lukindo. Shahidi huyu ameeleza kwamba, mjibu maombi na. 5 aliomba mashamba kwa baba yake mkubwa, Idd Shabani Lukindo. Akaoneshwa eneo ambalo halijauzwa akalima miaka miwili kisha akaondoka. Alisema kuwa eneo lenye mgogoro liliuzwa na mumewe kwa Mzee Nuru. Mjibu Maombi hakumuuliza maswali ya dodoso yaliyotikisa ushahidi huo. PW3, Omari Mrisho Mnazi, uk. 33 na 34 anaeleza eneo linalobishaniwa kwanza liliazimwa na mzee Nuru baadaye aliuziwa na shimeji yake (Iddi Shabani Lukindo). Manunuzi hayo yalithibitishwa na Mzee Nuru pamoja na Mzee Iddi. Wakili alikiri kuwa upo ushahidi wa DW4 uk. 57 mtoto wa Shabani Lukindo unaokinzana na ushahidi wa PW2. Akasema, shahidi huyu hana taarifa sahihi kwa kuwa hakuwahi anafuatilia mambo ya mashamba. Alisema kuwa mara ya mwisho alifika Mabamba mwaka 1989. Hakuwahi kuhudhuria hata vikao vya familia. Kuhusiana nani aaminiwe na mahakama aliiongoza mahakama kuangalia uamuzi wa Mahakama kwenye kesi ya Hemed Said Mbilu. 4 Kwa kuhitimisha wakili wa Mrufani aliieleza mahakama kuwa Mjibu maombi na. 5, hakuwahi kuleta kesi kinzani, ni jambo la kushangaza Baraza lilimtamka kama mmiliki wa eneo husika bila kuwa na kesi kinzani. Aliomba Mahakama ichambue upya ushahidi uliopo na kufanya maamuzi. Kuhusu madai ya Mzee Nuru kuwa amekaribishwa kwenye ardhi husika, wakili Kilingo alisema ni jambo ambalo ushahidi unaonyesha kuwa alikaribishwa kwa muda baadae akauziwa. Jambo la kuwa hakuna maandishi yanayothibitisha mauziano, mauziano kwenye shauri hili yalikuwa ni ya mdomo na yamethibitishwa na Mashahidi waliotoa ushahidi, PW2, PW3 na PW4. Katika kuipa uzito hoja yake, alijielekeza katika Uamuzi wa mahakama katika shauri la Joachim Ndelembi vs Maulid M. Mshindo na wenzake wawili Civil Appeal No. 106 of 2020 CAT AT DSM. Mrufani alitoa vielelezo Pl na P3 ambavyo Mwenyekiti hakuzingatia ushahidi uliotolewa kuhusiana na umiliki wa mzee Nuru kwenye eneo husika, vielelzo vyote viliongeza uzito wa ushhahidi wa Mrufani na Mrufani hakuwahi sumbuliwa kwenye eneo husika kwa miaka Zaidi ya 40. Pia DW2, Kabona Hamis Kabona anasema baba yake Rashidi hakuwahi kulima kwenye eneo linalobishaniwa, ushahidi wake ulikuwa ni wa kusikia. Wakili alisema DW3 Rashidi Salum Maguku, ushahidi wake usiaminiwe kwasababu ni moja wa walalamikiwa. Alikuwa miongoni mwa wadaiwa ambao hawakufika mbele ya Baraza ball alikuja kama shahidi, alikuwa mvamizi. Kisha aliomba rufaa ikubaliwe kwa gharama. 5 Mjibu Rufaa namba 5 aliomba awasilishe majibu yake kwa maandishi, baada ya upande wa Mrufani kutokuwa na pingamizi, mahakama hii ilidhinisha afanye hivyo. Katika mawasilisho yake, mjibu rufaa Na. 5 alieleza kwa ujumla kwamba ushahidi wa mrufani ulikuwa unakinzana kwa kuangalia ushahidi wa PW1 aliyedai kuwa mauziano yalifanyika miaka ya 1950 na PW2 aliyedai kuwa mauziano yalifanyika miaka ya 1990 na alisisitiza kuwa hakuna sehemu yoyote katika Uamuzi wa Baraza alipotangazwa kuwa yeye ndiye mmiliki wa ardhi yenye mgogoro bali Baraza lilielekeza ardhi hiyo ni mali familia ya mzee Shabani Lukindo. Aliendelea kueleza kuwa Wakati mrufani anafungua madai haya katika baraza la ardhi la wilaya eneo hilo bado mrithi alikuwa yupo hai bi Mwashamba shabani lukindo ambaye ndiye mrithi pekee aliyekuwa amebaki, ambaye ni shangazi yake Mrufani na. 5, akasema hakuweza kudai eneo la ardhi yenye mgogoro kwa sababu hakuwa mrithi na kwamba wakati madai haya yanaendelea terehe 08/11/2023 Bi Mwashamba akawa amefariki, hivyo kwa sababu eneo hilo kulikuwa na shauri linaendelea katika baraza la ardhi la wilaya ya Tabora hakuweza kuomba chochote juu ya ardhi hiyo ya mgogoro hadi shauri litakapomalizika, shauri ndio msingi wa rufaa hii. Mrufaniwa alihitimisha kwa kusema kuwa ana maslahi na eneo hilo kwa na amejenga kwenye shamba la mgogoro kwa sababu; (1) baba yake Rashidi Shabani Lukindo anahusika katika shamba hilo kurithi mali ya baba yake mzazi (2) mgao wake bado hajapewa (3) kwa kutambua ukweli kuwa eneo hilo halijauzwa. Mrufaniwa aliomba mahakama hii itupilie mbali rufaa hii. 6 Baada ya kusikiliza hoja za pande zote kama ambvyo ziliwasilishwa na wadaawa kwa njia yam mdomo na kwa njia ya maandishi, mahakama hii itaanza kufanya uchambuzi katika sababu ya rufaa namba 1, 2 na 4 kwa pamoja na kisha namba 3 peke yake. Katika sababu ya rufaa namba 1, 2 na 4, sababu hizi zimejikita katika hoja kwamba Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya lilikosea kisheria na kiushahidi kuamuru kwamba mjibu rufaa namba 5 ni mmiliki halali wa ardhi yenye mgogoro, yenye ukubwa wa ekeri TJ, pasipo kuzingatia kwamba ushahidi wa mrufani pamoja na mashahidi wake PW2, PW3, PW4 na PW5 ulikuwa mzito zaidi kuliko ushahidi wa mjibu rufaa namba 5. Baada ya kupitia kumbukumbu zilizopo katika mahakama hii, nimebaini kwamba Baraza la Wilaya la ardhi halikumtamka Mjibu rufaa Na. 5 wala mjibu rufaa yeyote kuwa mmiliki wa eneo linalobishaniwa. Baraza liliona Mrufani ameshindwa kuthibitisha umiliki wake juu ya ardhi bushaniwa na kwamba ushahidi uliopo unaonesha kwamba eneo linalobishaniwa ni sehemu ya mirathi ya Marehemu, Shabani Lukindo. Kwa urahisi wa rejea sehemu ya uamuzi wa baraza inanakiliwa kama ifuatavyo:- "Hivyo kutokana na uchambuzi huo ni wazi Mieta Maombi ameshindwa kudhibitisha madai yake ya umiliki juu ya ardhi ya mgogoro, uk. 15.................Mwisho maombi haya yanatupiiiwa kwa kukosa mashiko. Kwa kuwa ardhi ya mgogoro inamiiikiwa pamoja na watoto wa Lukindo senior, hivyo warithi wao wafuate utaratibu kisheria Hi kuweza kumiliki kihalali ardhi hiyo, uk. 16." 7 Kwa mujibu wa maelezo hapo juu hakuna mahali ambapo Baraza lilitannka moja kwa moja kuwa Mjibu rufaa na. 5 ndiye mmiliki bali eneo hilo limetamkwa kuwa mali ya marehemu Shabani Lukindo ambaye ni babu wa mjibu rufaa na. 5. Maamuzi hayo ya Baraza nayaona kuwa ni sahihi kwakuwa kumbukumbu za mahakama zinaonesha kuwa shamba linalobishaniwa ni mali ya Marehemu Shabani Lukindo, ambaye baada ya kufariki shamba hilo lilikuwa likitumiwa na familia yake, watoto wake aliowaacha, ambao ni Iddi Shabani Lukindo (anayedaiwa kumuuzia baba wa Mrufaniwa), Rashid Shabani Lukindo (baba wa Mjibu rufaa na. 5), Chausiku Shabani Lukindo na Mwashamba Shabani Lukindo ambao kwa sasa wote ni marehemu. Watoto wa marehemu Shabani Lukindo hawakugawa mirathi ya marehemu baba yao bali waliendelea kutumia maeneo hayo kama wanafamilia. Ushahidi wa namna hiyo unaonekana wazi kwenye maelezo ya mashahidi Mbalimbali akiwemo shahidi wa pili wa Mrufani (PW2) Mohamed Idd Shaban Lukindo. Shahidi huyu ameeleza wazi kwamba shamba husika lilikuwa mali ya marehemu babu yake, Shabani Lukindo. Ninanukuu ushahidi wa Mohamed Idd Shabani Lukindo kama unavyoonekana kwenye ukurasa wa 29 wa mwenendo wa shauri uliochapwa; "Eneo la mgogoro lilikuwa la babu yetu-Shabani Lukingo. Baada ya babu kufariki watoto wake wane akiwemo baba yangu Idd Shabani ndio wakarithi shamba hilo. Msimamizi wa mirathi ahkuwa ni baba yangu. Shangazi yetu Chiku Shabani Lukindo aliolewa na Nuru. Rashid Shaban 8 alikuwa babamdogo (baba wa Nassoro), yeye alikuwepo maeneo ya Itumba. Eneo hilo hawakuligawana. Baba alilitumia na ndugu zake wote ambao ni Chiku Shaban Rashid Shaban, na Mwashamba Shaban. Waiikuwa kitu kimoja." Ushahidi unathibitisha wazi kwamba eneo husika halikugawiwa kwa warithi bali waliendelea kulitumia wote kama familia moja. Hivyo uamuzi wa Baraza ambao umelitamka eneo hilo kuwa sehemu ya mirathi ya marehemu Shabani Lukindo uko sahihi. Nimeona pia upo ushahidi unaoashiria kwamba shamba husika liliuzwa na Marehemu Idd Shaban Lukindo. Kwa mujibu wa Mrufani na mashahidi wake takriban wote, Marehemu Idd Shaban Lukindo alimuuzia eneo linalobishaniwa Marehemu Nuru Hamisi Tengeneza. Nimejiuliza iwapo mauziano hayo yanauhalali wowote kisheria. Ni msimamo wa kisheria kwamba mauziano yanakuwa sahihi iwapo muuzaji anamiliki ki ha la I i eneo au kitu anachouza. Mahakama ya rufani ya Tanzania kwenye kesi ya Farah Mohamed dhidi ya Fatuma Abdallah (1999) TLR 205, iliamua kama ifuatavyo; "He who has no legal title to the land cannot pass good title over the same to another." Kwa tafsiri isiyo rasmi maneno haya yanamaanisha yule ambaye hana umiliki haiaii wa ardhi hawezi kuhamisha miliki kwenda kwa mtu mwingine." 9 Kwa mujibu Mrufani, baba yake alinunua shamba husika kutoka kwa Idd Shabani Lukindo ambaye alikuwa ni mtoto wa marehemu Shabani Lukindo. Bahati mbaya hakuna ushahidi wowote unaoonesha namna gani umiliki wa shamba husika ulihama kutoka kwa marehemu Shabani Lukindo kwenda kwa mwanaye, Idd Shaban Lukindo. Kwakuwa ushahidi unaonesha kwamba shamba hilo lilikuwa mali ya marehemu Shaban Lukindo wakati wa kifo chake, basi njia ambayo ingeweza kuhamisha umiliki wa eneo husika kutoka kwa Shaban Lukindo kwenda kwa Idd Shaban Lukindo ilikuwa ni kugawiwa kama sehemu ya mirathi au vinginevyo kupitia msimamizi wa mirathi ya marehemu Shabani Lukindo. Kwa mujibu wa shahidi Mohamed Idd Shabani Lukindo, baada ya babu yake, Shabani Lukindo kufa, eneo linalobishaniwa lilibaki kuwa mali ya watoto wanne wa marehemu Shabani Lukindo na wamekuwa wakilitumia pamoja. Hakuna ushahidi wa mgawanyo wa mirathi kwa warithi hao wanne mgao ambao pengine ungempa ummiliki Idd Shabani Lukindo na kumpa mamlaka ya kuuza eneo husika. Kuna maelezo kwamba Idd Shaban Lukindo ndio alikuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Shabani Lukindo. Hata hivyo maelezo haya hayajathibitishwa na ushahidi wowte ule kama vile ni lini, wapi na nani alimteua Idd Shaban Lukindo kuwa msimamizi wa mirathi ya Marehemu Shabani Lukindo. Zaidi ya kukosekana kwa ushahidi juu ya madai kwamba Iddi Shabani alikuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Shabani Lukindo, hakuna ushahidi wowte unaoonesha kugawiwa kwa mirathi ya Shabani Lukindo. Ushahidi unaonesha watoto wa marehemu Shabani Lukindo waliendelea kutumia mali zilizoachwa na marehemu baba yao kwa pamoja kama wanafamilia. 10 Hivyo basi kisheria, ingawa watoto na ndugu wa karibu wa Idd Shabani Lukindo wanaonesha kutokuwa na shaka kuhusu mauzo ya shamba husika kulikofanywa na baba yao, mauziano hayo ni batili. Iwapo mfufani anamadai yoyote yanayotokana na mauziano hayo anayodai kuwepo, basi anaweza kuelekeza madai yake kwenye mirathi ya marehemu Idd Shabani Lukindo. Hivyo sababu ya 1,3 na ya 4 na rufaa inatupiliwa mbali kwa kukosa mashiko. Sababu ya 2 ya rufaa na yenyewe haina mashiko kwakuwa hakuna ubishi kwamba baba wa Mrufani ambaye ni shemeji wa marehemu Idd Shabani Lukindo alikaribishwa kutumia eneo linalobishaniwa na alilitumia kwa muda mrefu. Ni kanuni iliyokubalika kisheria kwamba mara zote aliyealikwa au aliyeidhinishwa kukaa kwenye ardhi daima atabaki kuwa mwalikwa au mwenye idhini ya kutumia ardhi husika na sio mmliki. Aliyealikwa au aliyepewa idhini ya kutumia eneo la ardhi hawezi kudai umiliki ardhi hiyo kwa namna yoyote ile hata umiliki unaotokana na uvamizi, "adverse possesion" . Msimamo huu wa kisheria hauathiriwi na muda ambao mwalikwa ameutumia kwenye ardhi hiyo. Kwa kuwa hakuna ushahidi kwamba baba wa Mrufani alinunua shamba hilo kihalali bali kuna ushahidi kwamba alianza kutumia shamba hilo kwa kukaribishwa tu, hoja hii pia inakosa mashiko. Kabla ya kumaliza, naona kuna umuhimu wa kukumbusha warithi wa mali zinazotokana na mirathi kugawana mali hizo mara tu mmiliki wa awali anapofariki ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Nasema hivyo kwasababu, mgogoro kama huu ulio kwenye rufaa hii usingekuwepo iwapo warithi wa ii marehemu Shabani Lukindo wangegawana mirathi ya marehemu wao mara tu baada ya kifo chake. Kuachwa kwa mali za mirathi bila kugawiwa kunaweza kusababisha migogoro baina ya warithi au kwa jamii kwa ujumla wake. Kwa mujibu wa PW2, sio Idd Shabani Lukindo pekee alieuza eneo linaloloachwa na marehemu Shabani Lukindo bali warithi wengine wa Mzee Lukindo nao wameuza sehemu ya eneo lililoachwa na baba yao ingawa mauziano hayo hayajasababisha mgogoro wowote kwa sasa. Kwa kifupi, namuona Mrufani kuwa ni sehemu ya waathirika wa matendo ya warithi wa marehemu Shabani Lukindo yanayotokana na kutogawanywa kwa mirathi ya marehemu kwa muda muda mrefu. Baada ya kusema hayo. r ha kwa kusema kwamba rufaa hii inatupiliwa mbali kwa kukosa mashiko. Kwa kuzingatia ukweli kwamba Mrufani ni muathirika wa vitendo vya familia ya Shaban Lukindo, basi Mahakama hii haitoi gharama kwa upande wowote, kila upande ubebe gharama zake wenyewe. Imetolewa mbele yangu leo tarehe 03 mwezi Aprili, 2025 12