Download PDF

Tanzania Judgment

TANZLII

namwima abdallah mohamed na wenzake 9 vs cement distributorsea ltd 2021 tzhcld 400 1 oktoba 2021

On this page

Professional case brief

Research organized from the available case record

Source document

01

Holding and result

The applicants failed to prove an employment relationship with the respondent. Evidence showed they were employees of DYEDO, not the respondent. No contract or documentation established them as employees of the respondent. The arbitrator was correct in dismissing their claims.

Court disposition

Application dismissed

Orders

  • Application is dismissed for lack of merit
  • Decision of the Commission for Mediation and Arbitration is upheld
  • Right of appeal to the Court of Appeal explained

02

Material facts

Parties

Namwima Abdallah Mohamed

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Ramadhan Saidi

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Omary Fundi

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Hamisi Jumanne

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Waziri Asumani

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Omary Hamis

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Yahaya Said

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Mohamed Mpogo

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Bakari Issa

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Waziri Msomi

Applicant Counsel: Michael Mgombozi

Cement Distributors (E.A) Limited

Respondent Counsel: Benson Mwakubuli

03

Procedural history

  1. Posture

    Labour Revision / Judgment

04

Questions and positions

Legal issues

Party arguments

Applicant
Applicants argued they were employees of the respondent, worked at respondent's warehouse, were assigned daily duties, provided with work tools, and entitled to employment benefits. They contended the arbitrator misapplied the law and facts, and that contracts and evidence showed an employment relationship. They sought payment of all dues and benefits claimed.
Respondent
Respondent argued there was no employment relationship; applicants were employees of DYEDO, not the respondent. All contracts and payments were between respondent and DYEDO. Any benefits or work at respondent's premises were under DYEDO's arrangement. The respondent requested dismissal of the application.

05

Court’s reasoning

  1. 01

    Section 61 of the Labour Institutions Act

    Determination of employment relationship requires evidence of contract (written or oral) and compliance with statutory criteria.

  2. 02

    Contract between respondent and DYEDO; general principles of employment law

    Third-party service providers' employees are not employees of the principal unless proven otherwise.

06

Ratio, limits and disposition

Ratio decidendi

The applicants failed to prove an employment relationship with the respondent. Evidence showed they were employees of DYEDO, not the respondent. No contract or documentation established them as employees of the respondent. The arbitrator was correct in dismissing their claims.

Obiter and limits

  • Provision of medical assistance by the respondent does not establish an employment relationship; it may be an act of goodwill.

Court disposition

Application dismissed

  • Application is dismissed for lack of merit
  • Decision of the Commission for Mediation and Arbitration is upheld
  • Right of appeal to the Court of Appeal explained

Source and reliance status

TANZLII · 1 January 2021

This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.

Judgment reading view

Judgment text

The complete available source text.

Source document

TANZLII

Judgment· 1 January 2021

namwima abdallah mohamed na wenzake 9 vs cement distributorsea ltd 2021 tzhcld 400 1 oktoba 2021

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA

DIVISHENI YA KAZI

DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 287 YA 2020

KATI YA NAMWIMA ABDALLAH MOHAMED.................. MLETA MAOMBI WA KWANZA RAMADHAN SAIDI................................................... MLETA MAOMBI WA PILI OMARY FUNDI.........................................................MLETA MAOMBI WA TATU HAMISI JUMANNE................................................... MLETA MAOMBI WA NNE WAZIRI ASUMANI................................................. MLETA MAOMBI WA TANO OMARY HAMIS......................................................... MLETA MAOMBI WA SITA YAHAYA SAID..........................................................MLETA MAOMBI WA SABA MOHAMED MPOGO................................................ MLETA MAOMBI WA NANE BAKARI ISSA..........................................................MLETA MAOMBI WA TISA WAZIRI MSOMI......................................................MLETA MAOMBI WA KUMI

DHIDI YA CEMENT DISTRIBUTORS (E.A) LIMITED............................ MJIBU MAOMBI

HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho: 17/08/2021 Tareh e ya Hukumu: 01/10/2021 I. ARUFANI, J. Katika maombi haya waleta maombi wanaiomba mahakama ifanye marejeo ya tuzo ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itayojulikana kama Tume) iliotolewa na Mhe. Amos H. Mwamuzi tarehe 27/07/2018 katika mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/TEM/170/94/2017. Katika tuzo hiyo i Tume ilitupilia mbali madai mbalimbali ya waleta maombi yaliyoelekezwa dhidi ya mjibu maombi na kuamua kuwa waleta maombi hawakuwa wafanyakazi wa mjibu maombi. Baada ya kutoridhishwa na tuzo hiyo waleta maombi wamefungua maombi haya mbele ya mahakama hii wakiomba mahakama ipitie tuzo haya kwa kuangalia hoja zifuatazo:- i. Iwapo mwamuzi alikuwa sahihi kutoa uamuzi kuwa waombaji hawakuwa wafanyakazi wa mjibu maombi. ii. Iwapo waombaji wanastahili madai walioelekeza dhidi ya mjibu maombi. Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi. Waleta maombi waliwakilishwa na Bw. Michael Mgombozi, Mwakilishi Binafsi ilihali mjibu maombi aliwakilishwa na Bw. Benson Mwakubuli, Wakili Msomi. Katika hoja ya kwanza Bw. Mgombozi aliieleza mahakama kuwa mwamuzi alijiongoza vibaya na kukosea kutafsiri mahusiano ya kiajira baina ya waleta maombi na mjibu maombi. Alieleza kuwa, kwa mujibu wa nyaraka zilizotolewa mbele ya Tume ni dhahiri kuwa waleta maombi walikuwa wafanyakazi wa mjibu maombi. Kuyapa nguvu mawasilisho yake alirejea kifungu cha 60 (1) (2) cha

Sheria ya Taasisi za Kazi [Sura 300 KM 2019]. Mwakilishi huyo aliomba kifungu hicho kisomeke pamoja 2 na kifungu cha 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini [Sura 366 KM 2019], Bw. Mgombozi aliendelea kueleza kuwa kikundi cha Dar es Salaam Youth Development Organization si kampuni ya kupakia na kupakua mizigo kama ambavyo mjibu maombi amemwaminisha mwamuzi. Alieleza kuwa kikundi hicho tajwa kilianzishwa kwa mahitaji ya wanakikundi kwa ajili ya maendeleo binafsi ya kujikwamua kiuchumi. Maamuzi ya kuwa waleta maombi hawakuwa waajiriwa wa mjibu maombi yalipingwa vikali na ilisisitizwa na mwakilishi wa waombaji kuwa waombaji walikuwa wanapangiwa kazi, kupangiwa majukumu ya kila siku na kupewa vitendea kazi na mjibu maombi kama inavyoonekana Dhahiri katika kielelezo DI. Aliendelea kueleza kuwa mwamuzi alijiongoza vibaya kwa kutozingatia kuwa mwajiri alitoa ushahidi na uthibitisho kuwa waleta maombi walifanya kazi katika ghala lake lililopo kurasini. Aliongeza kuwa waleta maombi wamefanya kazi katika kituo kimoja cha mjibu maombi kwa zaidi ya miaka 10 hivyo mwajiri hakutoa sababu za msingi za kutowatambua. Bw. Mgombozi alieleza kuwa, mwamuzi alishindwa kuzingatia kuwa kitendo cha mwajiri kuunda umoja usio wa mikataba ya kudumu na kuwalazimisha kuwapatia mikataba ya muda maalumu ni 3 kukiuka matakwa ya kifungu cha 36 (a) (ii) na (iii) cha Sheria ya Ajira na mahusiano

kazini. Aliongeza kuwa mwamuzi alishindwa kutambua mwajiriwa ni nani kama ilivyoelezwa katika vifungu vya 4 na 61 vya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Aliongeza pia kuwa vifungu hivyo tajwa vimetafsiriwa katika kesi ya Mwita Wambura V. Zuri Haji, Marejeo Na. 45 ya 2012. Bw. Mgombozi aliendelea kueleza kuwa kama waleta maombi walikuwa ni wapakiaji na wapakuaji wa mizigo tu wasingestahili aina ya matibabu aliyogharamiwa Omary Mdoe kama inavyoonesha katika kielelezo KI. Katika hoja ya pili alieleza kuwa kwa kuwa kulikuwa na mahusiano ya kiajira baina ya waleta maombi na mjibu maombi hivyo wanaiomba mahakama iagize kuwa walipwe stahili pamoja na mapunjo yote wanayodai kadri ya walivyowasilisha maombi yao. Iliwasilishwa kuwa mwamuzi alikosea kwa kutojiongoza kwamba mwajiri alikiuka kifungu cha 15 (1) na (4) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na kushindwa kutambua kwamba waleta maombi waliajiriwa na mjibu maombi tokea mwaka 1998 na waliachishwa kazi bila sababu zozote za msingi kinyume na vifungu vya 37 na 38 vya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Kwa kuhitimisha hoja zote mwakilishi wa waleta maombi alisisitiza kuwa waleta maombi wanastahili haki zao zote kama walivyoomba 4 Katika fomu ya CMA Fl na kwa mujibu wa kifungu cha 40 (3) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Akijibu hoja za waleta maombi Bw. Mwakubuli alieleza kuwa hakukuwa na mahusiano ya kiajira kati ya

waleta maombi na mjibu maombi hivyo mahakama itupilie mbali maombi yao kwa kuwa mwamuzi alizingatia misingi yote ya kisheria na ushahidi uliotolewa mbele ya Tume. Alieleza kuwa waleta maombi wanajielekeza vibaya kuwa wao ni wafanyakazi wa mjibu maombi kwa kigezo cha kuwa eneo lao la kazi lilikuwa katika ghala la mjibu maombi lililopo Kurasini na walipewa vifaa vya kazi, walijiunga na SACCOS kupitia taasisi ya DYEDO na kupatiwa baadhi ya matibabu wakiwa katika eneo la kazi. Ilielezwa kuwa mjibu maombi alithibitisha kwa kiwango stahiki kupitia mashahidi wake wanne na vielelezo DI, D2 na D3 vinathibitisha pasipo kuacha shaka kuwa waleta maombi walikuwa wafanyakazi wa taasisi ya DYEDO. Kuhusu kifungu cha 61 cha Sheria ya Taasisi za Kazi kilichonukuliwa na waleta maombi, wakili wa mjibu maombi alielezwa kuwa waleta maombi wamepotoka kwa tafsiri yao kwa kuwa hawakidhi vigezo tajwa katika kifungu hicho. Aliendelea kuelezwa kuwa waleta maombi walifanya kazi za uchukuzi kulingana na maelekezo kutoka kwa viongozi wao na si kutoka kwa mjibu maombi. Kuhusiana na matibabu 5 aliyopewa mmoja wa waleta maombi ilielezwa kuwa hoja hiyo pekee haitoshi kuthibitisha mahusiano ya kiajira kati ya waleta maombi na mjibu maombi kwa kuwa matibabu hayo yanaweza kuwa yalifanywa kwa hisani tu. Aliongeza kuwa waleta maombi hawajawahi kulipwa mshahara na mjibu maombi kwa kuwa malipo yalifanyika baina ya

mjibu maombi na DYEDO kama inavyoonesha kwenye kielelezo D6. Katika hoja ya kuwa waleta maombi walipunguzwa kazini baada ya upungufu wa kazi ilielezwa kuwa hoja hiyo haina mashiko kisheria kwa kuwa iliibuliwa na waleta maombi wenyewe wakati mjibu maombi hajasema kama amewahi kuwaachisha kazi waleta maombi. Kuhusu kesi ya Mwita Wambura (supra) alielezwa kuwa haiendani na mazingira yaliyopo katika shauri hili. Bw. Mwakubuli alikiri kuwa mjibu maombi alikuwa na mahusiano ya kuipekee ya huduma ya uchukuzi na taasisi ya DYEDO hivyo kuomba madai ya waleta maombi yatupiliwe mbali. Kuhusu hoja ya pili wakili wa mjibu maombi alielezwa kuwa, kwa kuwa hakukuwa na mahusiano ya kiajira baina ya waleta maombi na mjibu maombi ni wazi kuwa maombi haya hayana mashiko. Aliongeza kuwa, hoja ya kuwa hakukuwa na majadiliano kabla ya kuachishwa kazi haihusiani na shauri hili kwani hakukuwa na uhusiano wa kiajira kati ya 6 pande mbili. Hivyo basi Bw. Mwakubuli aliiomba mahakama itupilie mbali shauri hili na kukazia maamuzi ya Tume. Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili pamoja na kumbukumbu za shauri hili, mahakama imeona ya kuwa itatue hoja mbili zilizoibuliwa na waleta maombi kama ambavyo zimenukuliwa hapo juu. Katika hoja ya kwanza ambayo inahoji endapo mwamuzi alikuwa sahihi kutoa uamuzi kuwa waombaji hawakuwa wafanyakazi mahakama imeona kuwa, kama ilivyoelezwa na pande zote mbili kifungu cha

61 cha Sheria ya Taasisi za Kazi kimeeleza mambo mbalimbali ya kuzingatia ili kubaini kama kuna mahusiano ya kiajira baina ya mwajiri na mwajiriwa. Katika shauri hili waleta maombi wanasisitiza kuwa walikuwa na mahusiano ya kiajira na mjibu maombi. Bw. Mgombozi alieleza kuwa waleta maombi walikuwa wakifanya kazi katika ghala ya mjibu maombi iliyopo Kurasini na walikuwa wakipangiwa kazi, kusimamiwa na kupewa vifaa vya kazi na mjibu maombi na kueleza ni viashiria vinavyothibitisha mahusiano yao ya kiajira. Kwa upande wake wakili wa mjibu maombi Bw. Mwakubuli alikiri kuwa ni kweli waleta maombi walikuwa wakifanya kazi katika ghala ya mjibu maombi iliyopo Kurasini lakini akaeleza walikuwa wameajiriwa na 7 kampuni iitwayo Dar es salaam Youth Economic Development Organization (DYEDO). Mahakama imepitia vielezo vilivyotolewa na pande zote mbili na imejiridhisha kuwa waleta maombi hawakuwa waajiriwa wa mjibu maombi. Kwa mujibu wa kielelezo DI kinaonesha wazi kuwa mjibu maombi aliingia makubaliano na kampuni ya DYEDO kwa ajili ya kutoa huduma ya kupakua, kubeba na kupakia saruji na bidhaa zote ziingiazo na kutoka katika maghala ya mjibu maombi yaliyopo eneo la Kurasini (Mabohari ya bodi ya pamba). Katika mkataba huo imeelezwa wazi kuwa waleta maombi hawatatambulika kama wafanyakazi wa mjibu maombi bali watatambulika kama wafanyakazi wa kampuni ya DYEDO. Kwa urahisi wa rejea nanukuu sehemu ya mkataba huo kama ifuatavyo:-

MASHARTI YA MKATABA 2. "Dyedo" itahakikisha kwamba inafuata, inazingatia na kuteke/eza sheria zote za kazi kwa watendaji au wafanyakazi wake na kwamba "kampuni" haitawajibika na madai yoyote yatokanayo na utumishi wao aidha kutoka kwa wafanyakazi wenyewe au Idara/Taasisi zenye mamiaka ya kusimamia sheria kama vile Idara ya Kazi, Mamiaka ya mapato na NSSF/PPF.' Waleta maombi wamesisitiza kuwa walikuwa waajiriwa wa mjibu maombi na kielelezo pekee walichotoa ni hati za matibabu ya mmoja 8 wao (kielelezo KI). Mahakama imeangalia kielelezo hicho na kuona kuwa hakijitoshelezi kuthibitisha kuwa kulikuwa na mahusiano ya ajira baina ya waleta maombi na mjibu maombi. Mahakama inaona kuwa kama ilivyoelezwa na wakili wa mjibu maombi inawezekana matibabu hayo yalitolewa kama hisani tu na si kwa sabubu alikuwa mwajiriwa wa mjibu maombi. Kama alivyoeleza wakili wa mjibu maombi mahusiano yoyote ya ajira huendeshwa kwa makubaliano ya pande mbili. Makubaliano hayo yanayoweza kuwa ya maandishi au ya mdomo. Katika shauri hili waleta maombi wameshindwa kuthibitisha aina yoyote ya mkataba walioingia na mjibu maombi. Mahakama imetafakari maelezo ya mwakilishi wa waleta maombi kuwa ni jukumu la mjibu maombi kutoa mkataba ulioingiwa na pande zote mbili na ikaona kuwa, kama inavyoonekana katika shauri hili mjibu maombi amewasilisha vielelezo mbalimbali vinavyothibitisha kuwa hakukuwa na mahusiano ya

kiajira kati yake na waleta maombi. Vielelezo hivyo ni pamoja na DI na D2 (ambavyo ni mikataba ya kazi na maombi ya kuendela na mkataba) vinavyoonyesha makubaliano ya kazi yalikuwa baina ya mjibu maombi na DYEDO na si waleta maombi. Mahakama imeona hakuna nyaraka yoyote inayothibitisha kuwa waleta maombi walikuwa waajiriwa wa mjibu maombi. Hata katika 9 nyaraka zao zilizowasilishwa mbele ya Tume zimeonyesha waleta maombi walijitambulisha kama wafanyakazi wa kampuni ya DYEDO na hiyo inaonekana katika barua kutoka chama cha wafanyakazi CHODAWU (kielelezo D3). Lakini hata malipo ya waleta maombi yalikuwa yakifanywa kupitia taasisi yao na sio kwao mmoja mmoja kama wafanyakazi, kama inavyooneshwa katika hati za malipo (kielezo D6). Mahakama imejaribu kupitia vifungu mbalimbali vya sheria na mashauri yaliyonukuliwa na mwakilishi wa waleta maombi katika mawasilisho yake lakini ikaona hakuna kufungu chochote wala uamuzi wowote wa mahakama unaounga mkono hoja za waleta maombi kuwa walikuwa waajiriwa wa mleta maombi. Hivyo basi kutokana na ufafanuzi huo hapo juu ni wazi kuwa ushahidi uliotolewa mbele ya Tume uliweza kuthibitisha kuwa waleta maombi hawakuwa waajiriwa wa mjibu maombi hivyo Mwamuzi alikuwa sahihi kuamua kuwa waleta maombi hawakuwa waajiriwa wa mjibu maombi. Baada ya kuona kuwa majibu ya hoja ya kwanza ni kuwa waleta maombi hawakuwa wameajiriwa wa mjibu maombi ni wazi kuwa

jibu la hoja ya pili ya iwapo waleta maombi wanastahili kulipwa madai waliyoyaelekeza dhidi ya mjibu maombi hayastahili kulipwa kwa waleta maombi kwa sababu hawakuwa wafanyakazi wa mjibu maombi. Hivyo 10 basi, ni maamuzi ya mahakama hii kuwa mwamuzi alikuwa sahihi kutupilia mbali madai ya waleta maombi kwani hawakuwa waajiriwa wa mjibu maombi. Kwa kueleza hivyo shauri hili linatupiliwa mbali kwa kukosa mashiko. Inaamriwa hivyo. Imesainiwa hapa Dar es salaam leo tarehe 01 mwezi Oktoba, Mahakama: Hukumu hii imesomwa leo tarehe 01 mwezi wa Oktoba, 2021 akiwepo Bw. Michael Mgombozi, Mwakilishi Binafsi wa Waleta Maombi na Mjibu Maombi akiwa hayupo. Haki ya kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani imeelezwa. li

Source wording is retained. Consult the source document for its original formatting and pagination.

Authorities

Authorities used by the court

Cases, legislation, regulations, and constitutional provisions identified in the available record.

Mwita Wambura v. Zuri Haji, Revision No. 45 of 2012

Case cited

Labour Institutions Act [Cap 300 R.E. 2019]

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Employment and Labour Relations Act [Cap 366 R.E. 2019]

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Case-aware research

Ask AI about this case

The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.

About this LexChat collection

This page organizes the available case record for research. Verify quotations, current status, and subsequent treatment against the source document. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.

Legal information, not legal advice. Research summaries do not replace the judgment.