Download PDF

Tanzania Judgment

TANZLII

obonyo laurence seda dhidi ya prime qualitrate ltd 2022 tzhcld 1112 14 disemba 2022

On this page

Professional case brief

Research organized from the available case record

Source document

01

Holding and result

Applicant failed to prove existence of an employment relationship with respondent as required by law; no documentary or credible evidence was produced to support employment claim.

Court disposition

application dismissed

Orders

  • each party to bear its own costs

02

Material facts

Parties

Obonyo Laurence Seda

Applicant Counsel: Jackson Mhando

Prime Qualitrate Ltd

Respondent

Amounts and remedies

  • Claimed Monthly Salary: TZS 1,450,000

03

Procedural history

  1. Posture

    Labour Revision / Final Judgment

04

Questions and positions

Legal issues

Whether an employment relationship existed between applicant and respondent

Party arguments

Applicant
Applicant argued that the arbitrator erred in law by finding no employment relationship despite respondent admitting applicant worked for them, and by dismissing the dispute when respondent failed to produce ordered documents. Applicant claimed he was not an independent contractor and relied on statutory provisions to support his claim.
Respondent
Respondent argued applicant was not their employee but worked under an arrangement for allowances. Respondent denied being ordered to produce documents and asserted applicant should have produced any relevant evidence.

05

Court’s reasoning

  1. 01

    Section 110(2) Evidence Act [Cap 6, R.E. 2022]

    Burden of proof lies on the party asserting employment relationship

  2. 02

    Section 61 Labour Institutions Act [Cap 300, R.E. 2019]

    Statutory presumptions for employment relationship

06

Ratio, limits and disposition

Ratio decidendi

Applicant failed to prove existence of an employment relationship with respondent as required by law; no documentary or credible evidence was produced to support employment claim.

Court disposition

application dismissed

  • each party to bear its own costs

Source and reliance status

TANZLII · 1 January 2022

This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.

Judgment reading view

Judgment text

The complete available source text.

Source document

TANZLII

Judgment· 1 January 2022

obonyo laurence seda dhidi ya prime qualitrate ltd 2022 tzhcld 1112 14 disemba 2022

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA

DIVISHENI YA KAZI

PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 127 YA 2022 OBONYO LAURENCE SEDA................................MLETA MAOMBI

DHIDI YA PRIME QUALITRATE LTD.................................. MJIBU MAOMBI (Kutokana na Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Kanda ya DSM - Hala) (Kiangi: Muamuzi) Tarehe 21.02.2022 Katika CMA/DSM/ILA/737/19

HUKUMU 03.11 & 14.12.2022 Rwizile, J Haya ni maombi ya marejeo. Mleta maombi ameomba Mahakama kuitisha, kupitia na kutengua tuzo ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Tume) katika Mgogoro Na. CMA/DSM/ILA/737/19 wa tarehe 21.02.2022. Imeelezwa kwamba mleta maombi aliajiriwa na mjibu maombi bila ya mkataba wa maandishi tangu tarehe 20.02.2018. i Aliajiriwa kama Meneja huku akilipwa mshahara wa shilingi 1,450,000/= hadi alipofukuzwa kazi isivyo halali tarehe 15.03.2019. Mleta maombi hakuridhika na umuzi huo, alifungua mgogoro wa kikazi katika Tume akiomba alipwe mshahara wa mwezi mmoja badala ya taarifa ya kuachishwa kazi, madai ya malimbikizo ya mishahara, kiinua mgongo na mshahara wa mwezi mmoja kama malipo ya likizo. Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Tume iliuondoa kwa sababu hapakuwapo mahusiano ya mwajiri na mwajiriwa baina ya mleta maombi na mjibu maombi. Mleta maombi, hakuridhika, akafungua maombi haya ya marejeo. Maombi haya yameambatana na kiapo cha mleta maombi. Sababu za maombi haya ni kama ifuatavyo: - 1. Kuwa muamuzi alikosea kisheria kwa kueleza kuwa hakukuwa na mahusiano ya kiajira wakati mjibu maombi aiikubaii kufanya kazi na mleta maombi.

2. Kuwa muamuzi alikosea kisheria kuondoa mgogoro wakati mjibu maombi aiishindwa kufikisha nyaraka muhimu alizoamriwa kuzifikisha mbele ya Tume.

3. Kuwa muamuzi alikosea kisheria kwa kushindwa kupokea ushahidi vizuri uiiofikishwa na mleta maombi. 2 Mleta maombi aliwakilishwa na Bwana Jackson Mhando, Mwakilishi Binafsi. Kabla ya kusikilizwa, Bwana Mhando aliomba kuendelea na hoja mbili tu, nyingine aliziacha. Nazo ni kama hapa chini: - 1. Kuwa muamuzi alikosea kisheria kwa kueleza kuwa hakukuwa na mahusiano ya kiajira wakati mjibu maombi alikubali kufanya kazi na mleta maombi na 2. Kuwa muamuzi alikosea kisheria kuondoa mgogoro wakati mjibu maombi aiishindwa kufikisha nyaraka muhimu aiizoamriwa kuzifikisha mbeie ya Tume. Katika hoja ya kwanza alisema ushahidi wa Omary Mwinyi Shaha Semboni (Mkurugenzi) ulithibitisha kuwa mleta maombi alikuwa akifanya kazi kwa mjibu maombi. Kwa mtazamo wake huo ni uthibitisho tosha kuwa mleta ' •• A . maombi alikuwa na mahusiano ya kiajira na mjibu maombi. Katika kuipa nguvu hoja yake, alirejea kifungu cha 19 cha Sheria ya Ushahidi [Sura ya 6 Marejeo ya Mwaka 2019]. Bwana Mhando aliwasilisha zaidi kuwa, mleta maombi hakuwa "independent contractor" kama muamuzi alivyoeleza kwakuwa hakuna ushahidi wowote uliothibitisha hivyo kinyume na kifungu cha 15(6) cha 3 Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini [Sura ya 366 Marejeo ya Mwaka 2019], kikisomwa na kifungu cha 111 Sheria ya Ushahidi. Katika hoja ya pili Bwana Mhando, alisema kuwa mjibu maombi kwa kitendo cha kushindwa kufikisha nyaraka

alizoamriwa na Tume ni kinyume na kifungu cha 20(5)(e) cha Sheria ya Taasisi za Kazi [Sura ya 300 Marejeo ya Mwaka 2004]. Hivyo akaiomba Mahakama kutengua uamuzi wa Tume na amri itolewe, mleta maombi kulipwa stahiki zake. Katika kujibu hoja, mjibu maombi aliwasilisha kuwa mleta maombi hakuwa mwajiriwa wake bali alikuwa akifanya kazi kwa makubaliano ya kulipwa posho kwakufuata utaratibu. Kwa mtazamo wake muamuzi alikuwa sahihi kueleza kuwa hayakuwepo mahusiano ya kiajira baina ya mleta maombi na mjibu maombi. Katika kujibu hoja ya pili alisema kuwa mjibu maombi hakupewa maelekezo na Tume kufikisha nyaraka kama alivyodai mleta maombi. Kwa maelezo yake kama hizo petty cash au salary slip zingekuwepo, lilikuwa ni jukumu la mleta maombi kuzifikisha mbele ya Tume maana ndie angekuwa na nakala halisi. Mjibu maombi Katika mawasilisho ya nyongeza Bwana Mhando alirudia yale aliyoeleza katika mawasilisho yake ya awali. 4 Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili, Mahakama imeona hoja moja ya kutolea uamuzi: - i. Kama mahusiano ya kiajira baina Mleta Maombi na Mjibu Maombi yamethibitiswa. Katika hoja ya kwanza, Mahakama imepitia kumbukumbu za Tume na kubaini kwa Dwl (Mkurugenzi) alisema, mleta maombi aliwaeleza anajua kazi na hivyo walimuomba ushauri kwasababu ya uzoefu wake. Kwa rahisi ya rejea katika maelezo ya Dwl ni kama ifuatavyo: - "Namfahamu miaiamikaji, tuiikutana aiipita

site yetu 1 ya Muhimbiii na kujiieza anafahamu hizo kazi na tuiimueieza hatuna kazi Ha baadae tuiimuomba ushauri sababu ya uzoefu wake." Kwa maelezo haya inaonyesha wazi kuwa mleta maombi aliwahi kuombwa ushauri na mjibu maombi. Kwa maelezo ya mjibu maombi inabainisha kuwa mleta maombi hakuwa mfanyakazi wake. Pamoja na maelezo hayo % Jr * mleta maombi ameeleza kuwa alikuwa mwajiriwa. Kifungu cha 61 cha Sheria ya Taasisi za Kazi [sura ya 300 marejeo ya mwaka 2019] kinaelezea dhana zinazothibitishwa mahusiano ya kiajira. Dhana hizo moja au zote kwa pamoja zinatakiwa kuthibitiswa na mwajiriwa kuwa na mahusiano ya kiajira kati yake na mwajiri. Dhana hizo ni: - 5 (a) kama kwa mfano anafanya kazi ya kila siku chini ya mwajiri (b) kama ni mwajiri anaye mpagia masaa ya kazi au mudu wa kufanyakazi (c) anafanya kazi katika taasisi, basi awe ni sehemu ya taasisi hiyo (d) awe amefanya kazi kwa angalau masaa arobaini na tano kwa mwezi katika miezi mitatu ya mwisho (e) awe anamtegemea mwajiri wake kiuchumi (f) awe anapatiwa vifaa vya kufanyia kazi na mwajiri wake (g) awe anamfanyia kazi mwajiri huyo tu Mjibu maombi (mwajiri) ameeleza kuwa hakuwahi kumwajiri mleta maombi. Hivyo jukumu la kuthibitisha kuwa alikuwa ni mwajiriwa ni la mleta maombi. Kifungu cha 110(2) cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 marejeo ya mwaka 2022, kinaweza kutumika. Mmleta maombi amedai alikuwa ameajiriwa na Mjibu

maombi. Hivyo anawajibika kuleta ushahidi kuthibitisha hilo. Katika mahojiano mbele ya Tume, mleta maombi alisema, kwa rahisi ya rejea kama ifuatavyo: - "S/J - Mkataba wako ni wa muda gani? Sikumbuki" 6 Lakini hata hivyo katika kupitia kumbukumbu za Tume hakukuwa na kielelezo chochote kinachothibitisha kama mleta maombi aliwahi kuwa mfanyakazi wa mjibu maombi. Hakuleta kielelezo chochote au hata mashahidi huru kufanya hivyo. Ameshindwa hata kufikisha kielelezo chochote kinachoonyesha ni jinsi gani alikuwa akilipwa mshahara. Pia hata mshahara wake unalipwa kwa namna gani. Kwa kitendo cha mleta maombi kushindwa kuthibitisha mahusiano ya kiajira baina yake na mjibu maombi; imeifanya Mahakama kuamini kuwa mleta maombi hakuwa mwajiriwa wa mjibu maombi kama alivyoeleza. Hivyo Mahakama inaona maombi haya hayana msingi. Yanafukuzwa. Kila upande utalipa gharama zake. 7

Source wording is retained. Consult the source document for its original formatting and pagination.

Authorities

Authorities used by the court

Cases, legislation, regulations, and constitutional provisions identified in the available record.

Evidence Act [Cap 6, R.E. 2022]

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Labour Institutions Act [Cap 300, R.E. 2019]

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Employment and Labour Relations Act [Cap 366, R.E. 2019]

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Case-aware research

Ask AI about this case

The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.

About this LexChat collection

This page organizes the available case record for research. Verify quotations, current status, and subsequent treatment against the source document. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.

Legal information, not legal advice. Research summaries do not replace the judgment.