Paulo Eliya Msangi and Uzima Eliya Msangi v Augustino Ngaraba Karugwe and Others
The Court held that the preliminary objection about the late filing of the probate cause was not a pure point of law because it would require inquiry into evidence from the Primary Court record, so it was dismissed. On the merits, the Court found that the District Court was wrong to nullify the Primary Court’s...
Source-derived case information.
- Parties
- Complainant / Appellant / Applicant / Plaintiff: PAULO ELIYA MSANGI (ADMINISTRATOR OF THE ESTATE OF ELIYA MSANGI (DECEASED)); Complainant / Appellant / Applicant / Plaintiff: UZIMA ELIYA MSANGI (ADMINISTRATOR OF THE ESTATE OF ELIYA MSANGI (DECEASED)); Respondent / Defendant: AUGUSTINO NGARABA KARUGWE; Respondent / Defendant: WILSON F WANJARA; Respondent / Defendant: EZEKIEL SETH; Respondent / Defendant: JORAM KIBAJI; Respondent / Defendant: WILLIAM SHANGO; Respondent / Defendant: WILFRED M MSENGI; Respondent / Defendant: SPORA JULIUS KIBIRITI; Respondent / Defendant: MAGDALENA KISANGA; Respondent / Defendant: MARY ELIFASI MMBAGA; Respondent / Defendant: JEREMIA EVARESTO NDITIJE; Respondent / Defendant: MIKA E MSANGI; Respondent / Defendant: ESTER MMBAGA; Respondent / Defendant: SETH YOHANA MBWAMBO; Respondent / Defendant: METHEW J FARACAY; Respondent / Defendant: MUSSA E MSANGI; Respondent / Defendant: TUMAINI E MSANGI; Respondent / Defendant: YAKOBO E MSANGI; Respondent / Defendant: LIDIA F WANJARA; Respondent / Defendant: SAYUNI E MSANGI; Respondent / Defendant: ELINGAO E MSANGI; Respondent / Defendant: REHEMA E NDITIJE; Respondent / Defendant: ELI SETH YOHANA; Respondent / Defendant: ENZI E MSANGI; Respondent / Defendant: UPENDO E MSANGI; Respondent / Defendant: SUBIRA E MSANGI; Respondent / Defendant: TUNZO E MSANGI; Respondent / Defendant: HAGAI ELIYA MSANGI; Respondent / Defendant: JOSEPH ELIYA MSANGI
- Jurisdiction
- Tanzania
- Procedural Posture
- Civil Appeal / Appeal From District Court Revision Decision
- Outcome
- appeal allowed in part
- Legal Topics
- Revision, Administration of Estate, Power of Attorney, Locus Standi, Right to Be Heard, Procedural Irregularity
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
PAULO ELIYA MSANGI (ADMINISTRATOR OF THE ESTATE OF ELIYA MSANGI (DECEASED))
Complainant / Appellant / Applicant / Plaintiff
UZIMA ELIYA MSANGI (ADMINISTRATOR OF THE ESTATE OF ELIYA MSANGI (DECEASED))
Complainant / Appellant / Applicant / Plaintiff
AUGUSTINO NGARABA KARUGWE
Respondent / Defendant
WILSON F WANJARA
Respondent / Defendant
EZEKIEL SETH
Respondent / Defendant
JORAM KIBAJI
Respondent / Defendant
WILLIAM SHANGO
Respondent / Defendant
WILFRED M MSENGI
Respondent / Defendant
SPORA JULIUS KIBIRITI
Respondent / Defendant
MAGDALENA KISANGA
Respondent / Defendant
MARY ELIFASI MMBAGA
Respondent / Defendant
JEREMIA EVARESTO NDITIJE
Respondent / Defendant
MIKA E MSANGI
Respondent / Defendant
ESTER MMBAGA
Respondent / Defendant
SETH YOHANA MBWAMBO
Respondent / Defendant
METHEW J FARACAY
Respondent / Defendant
MUSSA E MSANGI
Respondent / Defendant
TUMAINI E MSANGI
Respondent / Defendant
YAKOBO E MSANGI
Respondent / Defendant
LIDIA F WANJARA
Respondent / Defendant
SAYUNI E MSANGI
Respondent / Defendant
ELINGAO E MSANGI
Respondent / Defendant
REHEMA E NDITIJE
Respondent / Defendant
ELI SETH YOHANA
Respondent / Defendant
ENZI E MSANGI
Respondent / Defendant
UPENDO E MSANGI
Respondent / Defendant
SUBIRA E MSANGI
Respondent / Defendant
TUNZO E MSANGI
Respondent / Defendant
HAGAI ELIYA MSANGI
Respondent / Defendant
JOSEPH ELIYA MSANGI
Respondent / Defendant
Procedural Posture
Civil Appeal / Appeal From District Court Revision Decision
Legal Issues
- 1 Whether the District Court erred in nullifying the Primary Court probate proceedings and judgment on the basis of the power of attorney used by the objector’s representative.
- 2 Whether the objection proceedings before the Primary Court were conducted without giving the appellants a fair hearing.
- 3 Whether the revision application was competent despite the estate matter being filed long after the deceased’s death.
Ratio Decidendi
The Court held that the preliminary objection about the late filing of the probate cause was not a pure point of law because it would require inquiry into evidence from the Primary Court record, so it was dismissed. On the merits, the Court found that the District Court was wrong to nullify the Primary Court’s appointment of the administrators on the basis of the power of attorney used by the objector’s representative, because the defect did not prejudice the appellants. However, the Court held that the second objection proceedings concerning the alleged Ikongwe community interests were conducted by Hagai Eliya Msangi without proved authority to represent the 47 community members, thereby...
Court Disposition
appeal allowed in part
Orders
- The District Court’s decision setting aside the appointment of the administrators dated 27/12/2024 was set aside.
- Paul Eliya Msangi and Uzima Eliya Msangi were reinstated as administrators of the estate of Eliya Abraham Msangi @ Nabii Eliya.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
THE JUDICIARY OF TANZANIA IN THE HIGH COURT OF UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AT MOSHI CIVIL APPEAL NO. 000030225 OF 2025 PAULO ELIYA MSANGI (ADMINISTRATOR OF THE ESTATE OF ELIYA MSANGI (DECEASED) .............................. COMPLAINANT / APPELLANT / APPLICANT / PLAINTIFF UZIMA ELIYA MSANGI (ADMINISTRATOR OF THE ESTATE OF ELIYA MSANGI (DECEASED) .............................. COMPLAINANT / APPELLANT / APPLICANT / PLAINTIFF VERSUS AUGUSTINO NGARABA KARUGWE .............................. RESPONDENT / DEFENDANT WILSON F WANJARA .............................. RESPONDENT / DEFENDANT EZEKIEL SETH .............................. RESPONDENT / DEFENDANT JORAM KIBAJI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT WILLIAM SHANGO .............................. RESPONDENT / DEFENDANT WILFRED M MSENGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT SPORA JULIUS KIBIRITI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT MAGDALENA KISANGA .............................. RESPONDENT / DEFENDANT MARY ELIFASI MMBAGA .............................. RESPONDENT / DEFENDANT JEREMIA EVARESTO NDITIJE .............................. RESPONDENT / DEFENDANT MIKA E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT ESTER MMBAGA .............................. RESPONDENT / DEFENDANT SETH YOHANA MBWAMBO .............................. RESPONDENT / DEFENDANT METHEW J FARACAY .............................. RESPONDENT / DEFENDANT Page. 1 MUSSA E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT TUMAINI E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT YAKOBO E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT LIDIA F WANJARA .............................. RESPONDENT / DEFENDANT SAYUNI E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT ELINGAO E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT REHEMA E NDITIJE .............................. RESPONDENT / DEFENDANT ELI SETH YOHANA .............................. RESPONDENT / DEFENDANT ENZI E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT UPENDO E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT SUBIRA E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT TUNZO E MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT HAGAI ELIYA MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT JOSEPH ELIYA MSANGI .............................. RESPONDENT / DEFENDANT JUDGMENT KILIMI, J Baada ya Eliya Abraham Msangi al maarufu kama Nabii Eliya kufariki mwaka 1996, Upendo Eliya Msangi alifika katika Mahakama ya Mwanzo wilaya ya Same kituo cha Kisiwani na kufungua Mirathi kusimamia mali za marehemu mumewe. Shauri lilisajiliwa kama Shauri la Mirathi Nambari 4 la mwaka 2002 na mnamo tarehe 26.09.2002, Upendo hakukidhi vigezo hivyo kupelekea Mahakama kushindwa kumteua kama msimamizi wa mirathi. Ndipo baada ya takribani miaka ishirini na saba, watoto wa marehemu nabii Eliya ambao ni warufani katika shauri hili, Paulo Eliya Msangi pamoja na Uzima Eliya Msangi ambao ni watoto wawili kati ya watoto 48 wa marehemu, walifika Mahakama ya Mwanzo Kisiwani iliyopo wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro Page. 2 na kufanikiwa kuteuliwa kuwa wasimamizi wa Mirathi ya Marehemu Eliya Abraham Msangi. Warufani wote wawili waliteuliwa mnamo tarehe 27/12/2024 kupitia Shauri la Mirathi Na. 6/2024, na walipewa amri ya kuwasilisha orodha ya mali za marehemu katika mahakama hiyo ya mirathi. Mnamo tarehe 10.03.2025, warufani walirudi katika Mahakama ya mirathi ili kuwasilisha orodha ya mali za marehemu. Baada ya orodha ya mali za marehemu kuwasilishwa, mmoja wa ndugu wa marehemu aitwaye Hagai Eliya Msangi alijitambulisha na kuweka pingamizi kwa niaba ya wanajamii 47 wa Ikongwe, aliwasilisha pingamizi dhidi ya orodha hiyo akipinga mali zao kuchanganywa pamoja na mali za marehemu. Mahakama baada ya kusikiliza pande zote mbili, mnamo tarehe 06/06/2025 ilitupilia mbali mapingamizi yote na kutamka kwamba mali zilizokuwa zimeorodheshwa kwenye orodha ya mali za marehemu, zilikuwa ni za Marehemu Eliya Abraham Msangi na kwamba zibaki kwenye orodha ya mali za marehemu kama zilivyoorodheshwa na wasimamamizi wa mirathi. Baada ya uamuzi huo, amri ya mahakama ya mirathi iliwaamuru wasimamizi wawasilishe mgawanyo wa mali za marehemu mahakamani hapo kabla ya tarehe 6.08.2025. Ndipo wajibu rufani wa kwanza hadi wa ishirini na sita (1-26) katika shauri hili walipofika Mahakama ya Wilaya ya Same na kufungua shauri la maombi ya mapitio (Revision). Maombi hayo yalisajiliwa kama Maombi Madogo Namba. 000015786 ya Mwaka 2025 dhidi ya warufani wa kwanza na wa pili pamoja na wajibu rufani wa 27 na 28 katika rufaa hii. Katika maombi hayo, warufani walikuwa ni wajibu maombi wa 1 na wa 2 wakati warufaniwa wa 27 na 28 walikuwa ni wajibu maombi wa 3 na wa 4. Katika maombi hayo Wajibu rufani wa kwanza mpaka wa ishirini na sita walikuwa wanaomba amri zifuatazo dhidi ya wajibu maombi wanne; Kwanza, Mahakama ya Wilaya iweze kuchunguza kumbukumbu za mwenendo wa shauri katika ‘Shauri la Mirathi Na. 06/2024’ lililoamuliwa na Page. 3 Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani tarehe 06/06/2025, ili kujiridhisha kuhusu usahihi, na uhalali wa uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo, pamoja na uhalali wa mwenendo wa shauri hilo. Pili; Kwamba, ilikuwa ni kinyume cha utaratibu kwa Mahakama ya Mirathi kumruhusu Mdaiwa wa 3 kumwakilisha Mjibu maombi wa 4 kwa kutegemea Hati ya Uwakilishi (Power of Attorney) ambayo haikuwa halali. Tatu, Kwamba; ilikuwa si sahihi kwa Mahakama ya Mwanzo kumruhusu mjibu maombi wa 3 kuwawakilisha waombaji kwa kutegemea Hati ya Uwakilishi iliyotolewa na mjibu maombi wa 4 badala ya Hati ya Uwakilishi (Power of Attorney) iliyotolewa na Waombaji wenyewe 26. Nne, Kwamba, `ilikuwa ni ukiukwaji wa haki za msingi na za kikatiba kwa Mahakama ya Mirathi kusikiliza na kuamua suala linalohusu umiliki wa mali za Waombaji bila kuwapa fursa na haki ya kusikilizwa. Hivyo basi; Mahakama iombwe kupitia upya, itengue, ibatilisha, iondoe na kuweka kando uamuzi, amri na mwenendo wote wa Mahakama ya Mwanzo katika ‘Shauri la Mirathi Na. 06/2024. Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mahakama ya Wilaya ya Same mbele ya Mhe. C.A. Chitanda, PRM, tarehe 12 Novemba 2025 ilitoa uamuzi wake ambao ulikubali Maombi ya Revision yaliyowasilishwa na wajibu rufani wa Kwanza hadi wa Ishirini na Sita. Mahakama ilibaini kuwa mtoa hati ya uwakilishi (Power of Attorney) hakutoa sababu yoyote ya msingi ya kumruhusu mwakilishi huyo kuwawakilisha, na hivyo ikaona kuwa Mahakama ya Mwanzo ilikosea kwa kuipokea na kuitumia hati hiyo ya uwakilishi ambayo haikufuata utaratibu na ilikuwa na kasoro za kisheria. Mahakama ya Wilaya iliendelea kubaini kuwa mjibu maombi wa 3 hakuwa na mamlaka ya kisheria (locus standi) ya kuwawakilisha waombaji. Aidha, Mahakama ilieleza kuwa hali hiyo ilifanya mwenendo wote wa shauri uliofanyika kuwa batili na usio na uhalali wa kisheria. Kwa msingi huo, Mahakama ya Wilaya ilitengua, kubatilisha amri pamoja na hukumu ya Mahakama ya mwanzo ya Kisiwani katika Shauri la Mirathi Na. 6/2024. Mahakama hiyo pia iliamuru shauri hilo Page. 4 lirudishwe Mahakama ya mwanzo ya Kisiwani ili lisikilizwe na kuamuliwa upya kwa kuzingatia sheria. Baada ya uamuzi na amri hiyo ya Mahakama ya wilaya, warufani wa kwanza na wa pili wamefika mahakamani hapa wakiwa na sababu zao za rufaa kupinga uamuzi wa mahakama ya wilaya ya Same. Warufani waliwasilisha sababu za rufaa kwa lugha ya kiingereza kama ifuavyo; 1. The District Court of Same at Same erred in law and facts to nullify quash and set aside the proceedings, orders and Judgment of Primary Court of Kisiwani in Probate Cause No. 6 of 2024 in particular the Judgment and Order dated 27th of December 2024 which appointed the Appellants as administrators of the estate of Eliya Msangi (Deceased). 2. The District Court of Same at Same erred in law and facts by failure to hold that the proceedings up to 27th of December 2024 were not tainted with any procedural irregularities or illegalities. 3. The Judgment and Decree of the District Court of Same at Same has the effect of revoking the Appellants as administrators of the estate of the late Eliya Msangi without there being a proper Application for revocation; therefore, the Court erred in law and facts. 4. The District Court of Same at Same erred in law by relying on non existing Statute namely the Powers of Attorney Act Cap 352 R: E 2019 as the basis of its decision. 5. The District Court of Same at Same erred in law and fact for failure to take cognizance the fact that the matter before it was Miscellaneous Application therefore; the decision ought to be Ruling and Drawn Order instead of Judgment and Decree. Page. 5 6.The District Court of Same at Same erred in law for failure to indicate the names of both parties as appeared in Miscellaneous Civil Application No. 000015786 of 2025 Ref No. 202507021000015786 and as reflected in the Documents failed in Court. 7. The District Court of Same at Same erred in law for acting on Affidavit sworn by Advocate for the Respondents on substantive matters instead of the Respondents themselves. The Appellants are therefore pray the Court to set aside and quash the Judgment and Decree of the District Court Same at Same dated 12th November, 2025. Rufaa hii ilikubaliwa na pande zote mbili kuendeshwa kwa njia ya maandishi kwa lugha inayoeleweka kwa wadaawa wote ya kiswahili. Katika hatua hiyo, warufani wote wawili hawakuwa na uwakilishi wa kisheria. Kwa upande wa wajibu rufani wa kwanza hadi wa 26, waliwakilishwa na Bw. Erasto Kamani, Wakili Msomi, huku wajibu rufani wa 27 na wa 28 wakijiwakilisha wenyewe pia. Nimeyapitia mawasilisho haya maandishi nitayarejea kadiri hoja husika inapojibiwa katika maamuzi haya. Kwa kuanza na sababu ya kwanza na ya pili, za rufaa ambazo warufani waliziwasilisha kwa pamoja. Kwa kifupi, walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same ilikosea kisheria kufuta na kutengua mwenendo, amri na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani hususani amri ya tarehe 27.12.2024 iliyowateua warufani kuwa wasimamizi wa mirathi ya marehemu. Warufani walieleza zaidi kuwa wajibu rufani hawakupinga uteuzi wao kuwa wasimamizi wa mirathi. Kwa mujibu wao, malalamiko ya wajibu rufani hayakulenga uteuzi huo, bali yalihusu baadhi ya mali ambazo wajibu rufani waliamini kuwa ni mali zao binafsi, lakini ambazo zilijumuishwa katika orodha ya mali za marehemu. Page. 6 Kwa msingi huo, warufani walilalamikia uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Same wa kufuta na kutengua mwenendo, amri na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani ya tarehe 27.12.2024 na 06.06.2025. Walieleza kuwa amri hiyo ya Mahakama ya Wilaya ilisababisha pia kufutwa kwa uteuzi wao kuwa wasimamizi wa mirathi. Kwa mtazamo wa warufani, mwenendo na amri zilizotolewa na Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani hazikuwa na dosari yoyote iliyoweza kuhalalisha Mahakama ya Wilaya kuzifuta na kuzitengua. Katika kuunga mkono hoja yao, warufani walirejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika shauri la Miraji Salimu Nyangasa v. Ramadhani Omary Sewando (As Administrator of the Estate of the Late Hussein Omary Sewando), Civil Appeal No. 686 of 2023 [2024] TZCA 895, wakisisitiza misingi iliyowekwa katika uamuzi huo. Katika sababu ya tatu ya rufaa, warufani walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same ilikosea kisheria kwa kufuta uteuzi wao kuwa wasimamizi wa mirathi bila kuwepo kwa maombi rasmi yaliyolenga kufuta uteuzi huo. Walieleza kuwa hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Same ilienda mbali zaidi kwa kufuta pia uteuzi wao wa kuwa wasimamizi wa mirathi. Kwa mujibu wa warufani, mahakama yenye mamlaka ya kufuta uteuzi wao ilikuwa ni mahakama ileile iliyowateua kuwa wasimamizi wa mirathi, kama ilivyoainishwa katika aya ya 2(c) ya Jedwali la Tano la Sheria ya Mahakama za Mahakimu, Sura ya 11 Toleo la 2023. Kuhusu sababu ya nne ya rufaa, warufani walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same ilikosea kisheria kwa kutegemea sheria ambayo haipo katika orodha ya sheria za Tanzania, ambayo ilitajwa kama ‘The Power of Attorney Act, Cap. 352 R.E. 2019’. Walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same ilishikilia kwamba ili Hati ya Uwakilishi (Power of Attorney) iwe halali, ni lazima izingatie matakwa ya sheria hiyo. Warufani walipinga msimamo huo wakieleza kuwa hakuna sheria hiyo katika sheria za Tanzania. Kwa msingi huo, walidai kuwa uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ulikuwa na dosari ya kisheria na hivyo Page. 7 hauwezi kusimama. Kuhusu sababu ya tano ya rufaa, warufani walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same ilikosea kisheria na kiuhalisia kwa kushindwa kutambua kuwa shauri lililokuwa mbele yake lilikuwa ni maombi madogo. Kwa hiyo, walieleza kuwa uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ulipaswa kuwa katika mfumo wa ‘ Ruling’ na si ‘Judgment’, na amri iliyotokana na uamuzi huo ilipaswa kuwa ‘ Order’ na si ‘Decree’. Walisisitiza kuwa hakukuwa na shauri la msingi mbele ya Mahakama ya Wilaya ambalo lingeweza kutoa msingi wa kutolewa kwa Judgment na Decree. Kwa hiyo, kwa maoni yao, uamuzi uliotokana na maombi ya revision ulipaswa kuitwa Ruling na si Judgment. Kuhusu sababu ya sita ya rufaa, warufani walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same ilikosea kisheria na kimantiki kwa kushindwa kuonyesha majina ya wadaawa wote kwa usahihi kama yalivyoonekana katika nyaraka za mahakama wakati wa kufungua shauri. Walieleza kuwa majina ya wadaawa yaliyoonekana katika maombi ya marejeo yaliyofunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same yalikuwa tofauti na majina yaliyokuwa katika shauri lao. Aidha, walieleza kuwa majina hayo hayakuwa sawa na yale yaliyoonyeshwa katika hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Same.Katika kuunga mkono hoja hiyo, warufani walitegemea uamuzi wa kesi ya Shule ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Mkurugenzi) dhidi ya Hamis Kessy Rajabu, PC Civil Appeal No. 16743 of 2024 [2024] TZHC 10212, hususani ukurasa wa 8, 9 na 10. Kuhusu sababu ya saba na ya mwisho ya rufaa, warufani walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same ilikosea kisheria kwa kutegemea kiapo kilichoapishwa na wakili wa wajibu rufani kuhusu mambo ambayo yalikuwa ndani ya ufahamu binafsi wa wajibu rufani wenyewe. Katika kuunga mkono hoja hiyo, warufani walirejea uamuzi wa kesi ya NCBA Bank Tanzania Limited and Two Others, Miscellaneous Application No. 207 of 2022, ambapo Page. 8 Mahakama ilieleza kwa kina mazingira ambayo wakili anaweza kuapa kiapo kwa niaba ya mteja wake na mazingira ambayo hatakiwi kufanya hivyo. Warufani walieleza kuwa Bw. Erasto Kamani Wakili Msomi wa wajibu rufani, aliapa kuhusu mambo ambayo yalikuwa yanabishaniwa na ambayo yalihitaji ushahidi wa moja kwa moja kutoka kwa wahusika wenyewe. Aidha, walirejea uamuzi wa kesi ya Kellen Rose Rwakatare Kuntu dhidi ya Hamphret Kaulia Kenneth Rwakatare na Wenzake Watatu, Miscellaneous Application No. 89 of 2023. Kwa kumalizia, warufani waliiomba Mahakama hii iruhusu rufaa yao na itengue uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Same wa tarehe 12.11.2025. Aidha, waliomba Mahakama hii irejeshe na kuthibitisha mwenendo, uamuzi, amri na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani ya tarehe 27.12.2024 iliyowateua warufani kuwa wasimamizi wa mirathi. Katika kupinga rufaa hiyo, Bw. Erasto Kamani, Wakili Msomi aliyekuwa akiwawakilisha wajibu rufani wa kwanza hadi wa 26 kwa maandishi, alianza kwa kuibua hoja ya kisheria kuhusu uhalali wa rufaa hiyo. Alidai kuwa rufaa hiyo haikuwa halali kisheria kwa sababu ilitokana na shauri ambalo lenyewe lilikuwa limefunguliwa nje ya muda uliowekwa na sheria. Wakili Kamani alieleza kuwa marehemu, Eliya Abraham Msangi, alifariki mwaka 1996, wakati Shauri la Mirathi Na. 6 la mwaka 2024 lilifunguliwa mwaka 2024 yaani takribani miaka 28 baada ya kifo cha marehemu. Alieleza kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 31(1) ya Probate Rules, G.N. No. 10 ya mwaka 1963, pale ambapo maombi ya usimamizi wa mirathi yanafunguliwa baada ya kupita miaka mitatu tangu kifo cha marehemu, mwombaji anatakiwa kutoa maelezo ya kuchelewa huko kabla ya hati ya usimamizi wa mirathi kutolewa. Kwa mujibu wa Wakili Kamani, hakuna maelezo yoyote ya kuridhisha kuhusu ucheleweshaji huo yaliyotolewa mbele ya Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani kabla ya shauri la mirathi kufunguliwa. Kwa hiyo, alidai kuwa shauri hilo lilianzishwa kinyume na matakwa ya sheria.Katika kuunga mkono hoja hiyo, Wakili Kamani alirejea Page. 9 maamuzi mbalimbali ya mahakama, ikiwa ni pamoja na Songo Nyekaji dhidi ya Majura Songo Nyekaji, Shauri la Mirathi Na. 03 la mwaka 2019, Mahakama Kuu, na Masanja Luponya dhidi ya Eliad Lubinza Mashili, PC Probate Appeal No. 01 of 2020. Katika majibu yao ya nyongeza kujibu hoja tajwa hapo juu, warufani kwanza walipinga kuwepo kwa amri yoyote ya Mahakama hii iliyomruhusu Wakili wa wajibu rufani kuibua na kuwasilisha hoja hiyo ya awali ya kisheria. Walieleza kuwa hoja hiyo iliwasilishwa kinyume na utaratibu kwa kuwa hakukuwa na amri ya Mahakama hii iliyowapa ruhusa wajibu rufani kuiwasilisha katika hatua hiyo ya mwenendo. Katika kuunga mkono hoja hiyo, warufani walirejea uamuzi wa kesi ya Gold Africa Limited dhidi ya Business Registration and Licensing Agency, Miscellaneous Civil Application No. 5 of 2023 [2023] TZHC 17412 aya ya 5. Hata hivyo, pamoja na kupinga namna hoja hiyo ilivyoibuliwa, warufani waliendelea kujibu hoja hiyo kwa madai kwamba haikuwa na mashiko. Walieleza kuwa, katika kuamua suala hilo, Mahakama hii ilikuwa na mamlaka ya kurejea jalada la Mahakama ya Mwanzo. Waliielekeza Mahakama hii hususani katika ukurasa wa 3 wa hukumu ya Mahakama ya Mwanzo, ambao, kwa mujibu wao, unaeleza suala la ucheleweshaji wa kufunguliwa kwa shauri la mirathi. Warufani waliendelea kueleza kuwa maamuzi ya kesi yaliyotajwa na wajibu rufani hayakuwa na mashiko katika mazingira ya shauri hili kwa kuwa yalihusu mazingira tofauti na yale yaliyopo katika shauri hili. Katika kujibu sababu ya kwanza ya rufaa, Wakili Msomi Kamani alieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same haikukosea kufuta na kutengua mwenendo, hukumu na amri zilizotolewa na Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani. Alieleza zaidi kuwa Mahakama ya Wilaya haikufuta hukumu ya Mahakama ya Mwanzo kwa sababu ya ukiukwaji wa taratibu za uteuzi wa wasimamizi wa mirathi, bali kwa sababu ya kupokea na kutumia hati ya uwakilishi (Power of Attorney) ambayo haikukidhi matakwa ya kisheria. Page. 10 Alieleza kuwa kosa jingine lililofanywa na Mahakama ya Mwanzo lilikuwa kumruhusu mjibu rufani wa 27 kuwawakilisha wajibu rufani wa 1 hadi wa 26 wakati hakuwa na mamlaka (locus standi) ya kufanya hivyo. Sababu ya tatu, kwa mujibu wa Wakili Kamani, ilikuwa ni kuwanyima wajibu rufani wa 1 hadi wa 26 haki yao ya kusikilizwa. Alieleza kuwa, kwa kuwa uteuzi wao ulitokana na mwenendo uliokuwa umebatilika, uteuzi huo usingeweza kusimama. Wakili Kamani alisisitiza kuwa ni takwa la kisheria kwamba hati ya uwakilishi ambayo haitaji sababu ya kwa nini mtoa mamlaka ameshindwa kufika mwenyewe mahakamani huwa ni batili, na kwa hiyo mwenendo na shauri lililojengwa juu ya hati hiyo lazima vifutwe. Katika kuunga mkono hoja hiyo, Wakili Msomi alirejea uamuzi wa kesi ya Nurdin Said Mbalije and Others v. Professor Jumanne Abdallah Maghembe (through his Attorney) Twaliib Abdallah Maghembe, Land Appeal No. 62 of 2024. Akiendelea kujibu sababu za rufaa kuhusu hoja kwamba haikuwa sahihi kwa Mahakama ya Wilaya kufuta hukumu ya tarehe 27.12.2024 iliyowateua warufani kuwa wasimamizi wa mirathi kwa madai kwamba malalamiko ya wajibu rufani hayakuhusu uteuzi huo bali yalihusu mali zao kutokujumuishwa katika orodha ya mali za marehemu, Wakili Kamani alieleza kuwa si kweli kwamba wajibu rufani walikuwa wakipinga tu mali zao zisijumuishwe katika orodha ya mali za marehemu. Alieleza zaidi kuwa katika Maombi Na. 15786/2025 yaliyokuwa mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Same, hati ya maombi ya wajibu rufani, hususani aya ndogo (i), (ii) na (iii), iliweka wazi maombi yaliyokuwa yakiombwa na wajibu rufani. Maombi hayo yalifafanuliwa zaidi katika kiapo kilichowasilishwa kuunga mkono maombi hayo, hususani aya ya 4, 5, 6, 10, 11, 12, 13, 14 na 15. Kwa mujibu wa Wakili Kamani, kiini cha maombi hayo kilihusu mwenendo na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani tarehe 27.12.2024 na 06.06.2025. Page. 11 Akiendelea kujibu sababu ya tatu ya rufaa, Wakili Msomi Kamani alieleza kuwa warufani walikuwa wameielewa vibaya hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Same kwa kudhani kwamba Mahakama hiyo ilitoa amri ya kutengua uteuzi wao kuwa wasimamizi wa mirathi, jambo ambalo, kwa mujibu wake si kweli. Alieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ilichofanya ni kufuta mwenendo, hukumu na amri zilizotolewa na Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani baada ya kubaini kwamba Mahakama hiyo ilikiuka sheria zinazohusu uwakilishi kwa njia ya ‘Power of Attorney’, pamoja na kukiuka haki za msingi za binadamu. Wakili Kamani alisisitiza kuwa hakuna mahali ambapo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya alitoa amri ya kutengua usimamizi wa mirathi wa warufani. Badala yake, Mahakama hiyo ilifuta mwenendo, hukumu na amri za Mahakama ya Mwanzo zilizokuwa zimetolewa katika shauri hilo. Katika kujibu sababu ya nne ya rufaa kuhusu madai kwamba Mahakama ya Wilaya iliegemea sheria ambayo haipo katika sheria za Tanzania, Wakili Kamani alieleza kuwa hoja hiyo haikuwa na msingi. Alieleza kuwa katika kufikia uamuzi wake, Mahakama ya Wilaya ya Same ilizingatia maamuzi mbalimbali ya mahakama pamoja na vifungu husika vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuhusu suala la ‘Power of Attorney’, Wakili Kamani alieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ilitegemea uamuzi uliotolewa katika kesi ya Monica Danto Mwansasu (Atupaksiye Tughalaha) vs. Esrael Hosea & Others, Land Revision No. 2 of 2021, ukurasa wa 3 wa uamuzi huo. Wakili Kamani aliendelea kueleza kuwa, katika kufikia hitimisho kwamba wajibu rufani wa 1 hadi wa 26 walinyimwa haki yao ya msingi ya kusikilizwa, Mahakama ya Wilaya ilizingatia matakwa ya Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na uamuzi katika kesi ya Pili Ernest vs. Moshi Musani, Civil Appeal No. 39 of 2019. Wakili Kamani alisisitiza kuwa hakuna mahali ambapo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya alitumia ‘Power of Attorney Act’ licha ya kutaja sheria hiyo katika uamuzi wake. Kwa hiyo, kwa maoni yake hoja hiyo haikuwa na Page. 12 mashiko na ilipaswa kuchukuliwa kuwa ni kosa la kiuandishi tu. Aliomba maneno hayo yaondolewe kwa kuwa hayakuwa na athari yoyote katika msingi wa uamuzi wa Mahakama. Akiijibu sababu ya tano ya rufaa, Wakili Msomi Kamani alieleza kuwa haikuwa kosa kubwa kwa Mahakama ya Wilaya kutumia neno ‘Judgment’ badala ya ‘Ruling’, au ‘Decree’ badala ya ‘Order’. Alieleza kuwa matumizi hayo ya maneno hayakuathiri, kubatilisha wala kuondoa uhalali wa mwenendo wa shauri hilo kwa sababu kiini, maudhui na madhumuni ya uamuzi yalikuwa wazi na yalieleweka. Katika kuunga mkono msimamo huo, Wakili Msomi Kamani alirejea uamuzi wa kesi ya Attorney General vs. Maruti Commissioner Agency (2005) TLR 234. Kuhusu sababu ya sita ya rufaa, ambayo ilihusu kutotajwa kwa baadhi ya wadaawa katika nakala ya uamuzi wa shauri la marejeo Na. 15786/2025, Wakili Kamani alieleza kuwa hilo lilikuwa kosa la kiuandishi ambalo halikuathiri uhalali wa mwenendo wa shauri. Alieleza kuwa, ili rufaa iweze kuwa halali, ni lazima iambatane na nakala ya hukumu au tuzo inayokatwa rufaa, kama ilivyoelezwa katika kesi ya Puma Energy Tanzania Ltd vs. Ruby Roadways Market (T) Ltd, Civil Appeal No. 3 of 2018. Akijibu sababu ya saba ya rufaa, kwamba kiapo kilichowasilishwa kuunga mkono maombi hakikuwa halali kwa sababu kiliapwa na wakili wa waombaji, Wakili Kamani alieleza kuwa hakuna kanuni ya jumla ya kisheria inayomzuia wakili kuapa kwa niaba ya mteja wake. Alieleza kuwa wakili anaweza kuapa kuhusu jambo au mambo aliyoyapata kutoka kwa mteja wake, mradi tu aeleze chanzo cha taarifa hizo na msingi unaomfanya aamini kuwa taarifa hizo ni za kweli. Kwa mujibu wa Wakili Kamani, iwapo wakili ataeleza chanzo cha taarifa zake na msingi wa imani yake, kiapo chake huwa halali kisheria na hakiwezi kubatilishwa kwa msingi huo. Katika kuunga mkono hoja hiyo, alirejea maamuzi ya kesi zifuatazo;Dr. Luis B. Shija vs. Kelly Page. 13 Kamo Lucas, Civil Application No. 209 of 2024, Mahakama ya Rufani ya Tanzania; Re D.J. Rey Father Burette (1959) E.A. 25 uamuzi wa iliyokuwa Court of Appeal for Eastern Africa; na Lalago Cotton Ginnery & Oil Mills Co. Ltd, Civil Application No. 80 of 2002. Kwa kumalizia, Wakili Msomi Kamani aliiomba Mahakama itupilie mbali rufaa kwa kukosa mashiko na itoe amri ya gharama dhidi ya warufani. Kwa upande wa wajibu rufani wa 27 na 28, katika kujibu sababu ya kwanza na ya pili za rufaa, walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ya Same ilikuwa sahihi kisheria kufuta na kutengua mwenendo, hukumu na amri zilizotolewa na Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani. Walieleza kuwa mwenendo na maamuzi ya Mahakama ya Mwanzo yalifutwa na Mahakama ya Wilaya baada ya kubainika kwamba Mahakama ya Mwanzo ilipokea na kutumia hati ya uwakilishi ambayo haikukidhi matakwa ya kisheria. Kwa mujibu wa wajibu rufani hao, matumizi ya hati hiyo ya uwakilishi yalisababisha ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu, hususani kuwanyima wajibu rufani wa 1 hadi wa 26 haki yao ya kusikilizwa. Wajibu rufani wa 27 na 28 waliongeza kuwa hati ya uwakilishi ambayo haielezi sababu za msingi zilizomfanya mtoa mamlaka kushindwa kufika mwenyewe mahakamani kuendesha shauri lake huwa ni batili. Kwa hiyo, walieleza kuwa mwenendo mzima wa shauri unaoendeshwa au ulioendeshwa na mtu kwa kutumia hati hiyo ya uwakilishi huwa batili na unastahili kufutwa. Wajibu rufani hao waliendelea kujibu hoja za rufaa kwa kueleza kuwa malalamiko yao yalihusu Mahakama ya Mwanzo kutumia hati ya uwakilishi yenye dosari, pamoja na kuwanyima wajibu rufani wa 1 hadi wa 26 haki yao ya kusikilizwa. Kuhusu sababu ya tatu ya rufaa, wajibu rufani wa 27 na 28 walieleza kuwa warufani walikuwa wameielewa vibaya hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Same katika Shauri Na. 15786/2025 kwa kudhani kuwa Mahakama hiyo iliwatengua warufani kutoka katika nafasi zao za kuwa wasimamizi wa mirathi. Wajibu rufani hao walipinga hoja hiyo na kueleza Page. 14 kuwa si kweli kwamba Mahakama ya Wilaya ilitoa amri ya kuwatengua warufani kuwa wasimamizi wa mirathi. Badala yake, walieleza kuwa hukumu, mwenendo na amri za Mahakama ya Mwanzo zilifutwa kwa sababu ya matumizi ya hati ya uwakilishi yenye dosari. Katika kujibu sababu ya nne ya rufaa, wajibu rufani wa 27 na 28 walieleza kuwa hoja hiyo haikuwa na mashiko kwa kuwa si kweli kwamba Mahakama ya Wilaya ilitegemea sheria ambayo haipo katika sheria za Tanzania. Walieleza kuwa Mahakama ya Wilaya ilifikia uamuzi wake kwa kuzingatia maamuzi mbalimbali ya mahakama pamoja na vifungu husika vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waliongeza kuwa matumizi ya maneno ‘Power of Attorney Act’ katika uamuzi wa Mahakama ya Wilaya katika Shauri Na. 15786/2025 yalikuwa ni kosa la kiuandishi tu. Kuhusu sababu ya tano ya rufaa, wajibu rufani hao walieleza kuwa matumizi ya neno ‘Judgment’ badala ya ‘Ruling’, na ‘Decree’ badala ya ‘ Order’, hayakuwa na athari ya kufuta au kuondoa uhalali wa mwenendo wa shauri lililokuwa mbele ya Mahakama ya Wilaya. Vivyo hivyo, kuhusu sababu ya sita ya rufaa, walieleza kuwa tofauti au kutokuwepo kwa baadhi ya majina ya wadaawa katika uamuzi wa Mahakama ya Wilaya kulikuwa ni kosa la kiuandishi. Walieleza kuwa, kwa kuusoma uamuzi huo kwa ujumla, ni dhahiri kuwa Mahakama ilifahamu mgogoro uliokuwa mbele yake pamoja na haki na wajibu wa wadaawa ulioamuliwa katika shauri hilo. Katika kusisitiza hoja hiyo, wajibu rufani walirejea uamuzi wa kesi ya Amina Maulidi Ambali & Others vs. Ramadhani Juma, Civil Application No. 173 of 2020 [2020] TZCA 186. Kuhusu sababu ya saba ya rufaa, wajibu rufani wa 27 na 28 walieleza kuwa hoja hiyo pia haikuwa na mashiko kwa kuwa wakili anaruhusiwa kisheria kuapa kiapo kwa niaba ya mteja wake katika mazingira yanayoruhusiwa na sheria. Katika kuunga mkono hoja hiyo, walirejea Page. 15 mamlaka za kisheria zilizowasilishwa na Wakili wa wajibu rufani wa 1 hadi wa 26. Katika mawasilisho yao ya nyongeza, warufani walisisitiza kuwa hoja zao za awali ziendelee kuzingatiwa kwa kuwa hoja zilizotolewa na wajibu rufani hazikuwa na mashiko. Katika nyongeza kuhusu sababu ya kwanza na ya pili za rufaa, warufani walisisitiza kuwa Mahakama ya Wilaya haikupaswa kufuta mwenendo na amri za Mahakama ya Mwanzo hadi kufikia hatua ya uteuzi wa wasimamizi wa mirathi, kwa kuwa taratibu zote za kuomba usimamizi wa mirathi zilikuwa zimefuatwa kabla ya uteuzi wao kufanyika. Kuhusu sababu ya tatu, warufani walisisitiza kuwa kufutwa kwa amri iliyowateua kuwa wasimamizi wa mirathi kulikuwa sawa na kutengua uteuzi wao bila kufuatwa kwa utaratibu kamili wa kisheria wa kuwatengua wasimamizi wa mirathi. Walisisitiza zaidi kuwa uteuzi wao ulifutwa kwa kutegemea sheria ambayo, kwa madai yao haikuwa na uhalali yaani ‘Power of Attorney Act, Cap. 352 R.E. 2019’. Kuhusu sababu zilizobaki za rufaa, warufani walirejea mawasilisho yao ya awali na kuiomba Mahakama hii izingatie hoja hizo na hatimaye iruhusu rufaa yao kwa kuwa ilikuwa na mashiko. Kuhusu majibu ya wajibu rufani wa 27 na 28, warufani pia walisisitiza kuwa mawasilisho yao ya awali yazingatiwe kama yalivyowasilishwa. Walieleza zaidi kuwa hoja zilizotolewa na wajibu rufani wa 27 na 28 hazikuwa na mashiko. Warufani walieleza kuwa, kwa ujumla, majibu yao dhidi ya hoja zilizotolewa na wajibu rufani wa 27 na 28 yalikuwa sawa na majibu waliyokuwa wameyatoa dhidi ya hoja za wajibu rufani wa 1 hadi wa 26, na waliomba Mahakama iyazingatie ipasavyo katika kuamua rufaa hii. Aidha warufani katika hoja zao za nyongeza walieleza sababu kwa nini waliamua kuwaunganisha warufaniwa wa 27 na 28 wakati kwenye uamuzi Page. 16 wanaoukatia rufaa warufaniwa hao walikuwa ni wajibu maombi wenzao. Warufani walieleza kuwa msimamo wa kisheria kwamba mtu ambaye mlishitakiwa pamoja na mkapoteza pamoja, kama yeye hakuwa tayari kukata rufaa basi aliyeamua kukata rufaa anapaswa kumuweka yule ambaye hajaamua kukata rufaa kama mjibu rufaa. Katika hili ulirejewa uamuzi wa kesi ya TANESCO vs. Mwanza City Council &others, Civil Appeal No.89/2021. Hata hivyo hoja hii haikujibiwa na warufaniwa kwa kuwa iliibuliwa kwenye majibu ya nyongeza ya warufani. Baada ya kupitia kwa umakini rekodi ya shauri hili, sababu za rufaa pamoja na mawasilisho ya pande zote mbili, hoja kuu inayojitokeza kwa ajili ya uamuzi ni kama rufaa hii ina mashiko. Kama nilivyoeleza hapo awali katika historia ya shauri hili, rekodi zinaonyesha kuwa warufani wote wawili waliwasilisha maombi ya kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi ya marehemu baba yao, Eliya Abraham Msangi, maarufu kama Nabii Eliya, mbele ya Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Same, iliyoketi Kisiwani, kupitia Shauri la Mirathi Na. 6/2024. Aidha iweleke wazi katika shauri hili yalitolewa maamuzi mawili kutokana na mapingamizi yaliyopokelewa, uamuzi wa kwanza ulitolewa tarehe 27.12.2024 na wa pili ulitolewa tarehe 6.6.2025. Maombi ya usimamizi wa mirathi yalipata pingamizi kutoka kwa Ndugu Joseph Eliya Msangi, ambaye alitoa hati ya uwakilishi (Power of Attorney) kwa Ndugu Hagai Eliya Msangi ili aweze kumwakilisha katika pingamizi hilo. Baada ya kusikiliza maombi hayo ya uteuzi pamoja na pingamizi zilizowasilishwa, tarehe 27.12.2024 Mahakama ya Mirathi iliyatupilia mbali mapingamizi hayo na kuwateua warufani kuwa wasimamizi wa mirathi. Mahakama hiyo iliwaamuru wasimamizi hao kuwasilisha orodha ya mali za marehemu. Baada ya orodha hiyo kuwasilishwa, Mahakama ya Mirathi ilipokea pingamizi kutoka kwa mmoja wa watoto wa marehemu, HagaiEliya Page. 17 Msangi aliyedai kuwa anawakilisha jamii inayojulikana kama Ikongwe. Alipinga orodha hiyo kwa madai kwamba baadhi ya mali zilizoorodheshwa kama mali za marehemu zilikuwa mali za jamii hiyo ya wana Ikongwe. Baada ya pingamizi hilo kusikilizwa hadi mwisho, tarehe 06.06.2025 Mahakama ya Mirathi ilifikia uamuzi kwamba mali zilizowasilishwa katika orodha hiyo zilithibitika kuwa mali za marehemu. Ndipo wajibu rufani wa 1 hadi wa 26 walipofika Mahakama ya Wilaya ya Same na kufungua Maombi ya Marejeo (Revision) Na. 15786/2025, wakiomba nafuu nilizoziainisha hapo awali. Baada ya Mahakama ya Wilaya kusikiliza pande zote, iliruhusu maombi hayo kwa kufuta hukumu, amri na mwenendo wa Mahakama ya Mirathi na kuamuru shauri hilo lirudishwe katika Mahakama ya Mwanzo ili lisikilizwe na kuamuliwa upya. Uamuzi huo haukuwaridhisha warufani, ambao waliwasilisha rufaa hii kwa misingi ya sababu za rufaa zilizoainishwa hapo awali. Katika rufaa hii, nitaanza na hoja ya kisheria iliyoibuliwa na wajibu rufani wa 1 hadi wa 26 kwamba rufaa hii haikuwa halali kisheria kwa kuwa ilitokana na shauri ambalo lilifunguliwa na kuendeshwa nje ya muda uliowekwa na sheria. Katika kuunga mkono hoja hiyo, wajibu rufani walieleza kuwa Shauri la Mirathi Na. 6/2024 lilifunguliwa takribani miaka 28 baada ya kifo cha marehemu, bila kuwepo kwa sababu iliyotolewa ya kueleza kwa nini maombi hayo yalichelewa kufunguliwa kwa muda wote huo. Kwa upande wao, warufani walijibu kwamba hoja hiyo iliwasilishwa kinyume na utaratibu kwa kuwa hakukuwa na amri ya Mahakama hii iliyowaruhusu wajibu rufani kuiibua. Aidha, walieleza kuwa hoja hiyo haikuwa na mashiko kwa kuwa ukurasa wa 3 wa hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ulieleza sababu za kuchelewa kufunguliwa kwa shauri la mirathi. Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili, kwanza niseme kwamba Wakili Kamani aliwasilisha ombi akieleza kwamba alikusudia kuibua Page. 18 pingamizi hilo katika mawasilisho yake ya majibu ambapo Mahakama hii ilimruhusu kufanya hivyo iwapo angeona inafaa. Hata hivyo, ni kanuni iliyokubalika kwamba pingamizi la kisheria linaweza kuibuliwa wakati wowote wa mwenendo wa shauri, ikiwemo katika hatua ya mawasilisho, iwapo linakidhi vigezo vya kuwa pingamizi la awali la kisheria. Kwa hiyo, sioni kwamba pingamizi liliwasilishwa kinyume na utaratibu. Swali linalofuata ni kama pingamizi lina mashiko. Ni dhahiri kutokana na rekodi ya Mahakama katika shauri hili kwamba marehemu Eliya Abraham Msangi alifariki mwaka 1996, na pia ni jambo lisilopingika kwamba maombi ya usimamizi wa mirathi yake yalifunguliwa mwaka 2024. Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, ukweli huo pekee hauwezi kuifanya hoja hiyo kuwa pingamizi la awali la kisheria linaloweza kuamuliwa bila kurejea ushahidi na ukweli wa shauri. Sababu ni kwamba, ili Mahakama hii iweze kujiridhisha iwapo kulikuwa na maelezo ya kutosha kuhusu kuchelewa kufunguliwa kwa maombi hayo, italazimika kurejea rekodi ya Mahakama ya Mwanzo na kuchunguza kama waombaji waliwasilisha maelezo kuhusu sababu za kutofungua maombi ya usimamizi wa mirathi kwa wakati. Uchunguzi huo utailazimu Mahakama hii kuingia katika ushahidi wa shauri uliokuwa mbele ya Mahakama ya Mwanzo. Hali hiyo ni kinyume na misingi inayotawala pingamizi la awali la kisheria ambalo linapaswa kuamuliwa kwa kuzingatia hoja za kisheria pekee bila kuhitaji uchunguzi wa ushahidi. Kwa hiyo, ingawa ucheleweshaji wa miaka 28 ni jambo linaloweza kuwa na umuhimu katika shauri hili, kwa mazingira yaliyopo hauwezi kwa wenyewe kuunda msingi wa pingamizi la awali la kisheria. Kuhusu maamuzi yaliyorejewa na Wakili Msomi Kamani katika hili, nimeyapitia na nimeona kuwa mazingira ya kesi hizo yanatofautiana na mazingira ya shauri hili. Kwa hiyo hayawezi kutumika moja kwa moja kuunga Page. 19 mkono pingamizi lililoibuliwa hapa. Nasema hivyo kwa sababu, katika maamuzi hayo sheria iliyotumika haitumiki katika mahakama ya mwanzo, na pili katika mahakama ya mwanzo mleta maombi anatakiwa tu kueleza katika fomu ya kuomba mirathi au kutoa maelezo mahakamani endapo mahakama itaona inabidi kufanya hivyo ( rejea kifungu cha 3(2) na (3) cha sheria ya The Primary Courts (Administration Of Estates) (Amendment) Rules, 2025 GN 428 ya 2025. Na ndio maana nasema suala hili linahitaji ushahidi, jambo ambalo linasababisha pingamizi hili lisiwe pingamizi la kisheria kwani linahitaji ushahidi.Kwa msingi huo, naona pingamizi hilo halikukidhi vigezo vya pingamizi la awali la kisheria na hivyo ninalitupilia mbali. Nikirejea kwenye sababu za rufaa zilizowasilishwa, nitaanza kwa kujibu sababu ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne, ya tano na ya saba kwa pamoja kwa kuwa zote kwa kiasi kikubwa zinahusu suala moja yaani kama Mahakama ya Wilaya ya Same katika Maombi ya Marejeo Na. 15786/2025, ilikosea kubatilisha, kufuta na kutengua mwenendo wa Mahakama ya Mwanzo katika Shauri la Mirathi Na. 6/2024 na kuamuru shauri hilo lirudishwe kwa ajili ya kusikilizwa upya. Sababu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ilikuwa kwamba Mahakama ya Mwanzo ilikosea kupokea na kutumia hati ya uwakilishi (Power of Attorney), na kwamba mjibu maombi wa 3 hakuwa na mamlaka ya kisheria ya kuwawakilisha waombaji. Kwa msingi huo, Mahakama ya Wilaya ilifuta na kubatilisha amri pamoja na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani katika Shauri la Mirathi Na. 6/2024 na kuamuru shauri hilo lirudishwe Mahakama ya Mwanzo ya Kisiwani ili lisikilizwe na kuamuliwa upya kwa kuzingatia sheria. Nimepitia kwa umakini mwenendo wa Mahakama ya Mirathi na nimejiridhisha kwamba ni kweli Ndugu Joseph Eliya Msangi ambaye alikuwa mpingaji katika maombi ya uteuzi wa wasimamizi wa mirathi alimpa Ndugu Page. 20 Hagai Eliya Msangi mamlaka ya kumwakilisha katika pingamizi hilo kupitia Hati ya Uwakilishi. Sababu kuu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya katika maombi ya marejeo ilikuwa kwamba hati hiyo ya uwakilishi haikutaja sababu iliyomfanya mpingaji kushindwa kufika mwenyewe mahakamani kusikiliza na kuendesha pingamizi lake. Kwa maneno mengine, Mahakama ya Wilaya iliona kwamba kwa kuwa sababu hiyo haikutajwa katika hati ya uwakilishi, hati hiyo haikuwa halali. Kutokana na mtazamo huo, Mahakama ya Wilaya ilihitimisha kwamba mjibu maombi wa 3 hakuwa na ‘locus standi’ ya kumwakilisha mpingaji huyo na pia ikafikia hitimisho kwamba waombaji wa marejeo walinyimwa haki yao ya kusikilizwa. Baada ya kulichunguza suala hilo kwa umakini, sishawishiki na hitimisho la Mahakama ya Wilaya kwamba hati ya uwakilishi ilikuwa batili kwa sababu hiyo pekee. Ninasema hivyo kwa sababu Mahakama za Mwanzo hazipaswi kuongozwa na misingi ya technicalities zinazoweza kuzuia uamuzi wa haki kufikiwa, hususani pale ambapo hakuna upande ulioonyesha kwamba umeathirika au kupewa madhara kutokana na kasoro hiyo. Nayasema haya kwa sababu, kwanza, ukiangalia ukurasa wa 9 wa mwenendo wa mahakama ya mwanzo na nukuu; “MBELE YA M.A. CHANDE Waleta maombi- wapo Mleta pingamizi -hayupo MAHAKAMA - Shauri limekuja kwa kusikiliza utetezi Hagai Eliya Msangi - Mh. Mimi nina hati ya uwakilishi kutoka kwa mleta pingamizi naomba kuiwakilisha. Ameniteuwa niendelee na hili shauri. Waleta maombi - Hatuna pingamizi MAHAKAMA Mahakama imepokea hati ya uwakilishi ya mleta pingamizi kumteuwa Hagai Eliya Page. 21 msangi, kwahiyo kwa sasa Hagai Eliya Msangi atasimama kama mleta pingamizi kwa niaba ya Joseph Eliya Msangi. Mleta pingamizi - nipo tayari kwa utetezi na nina mashahidi wanne Waleta maombi -tupo tayari kusikiliza.” Kutokana na nukuu hapo juu pamoja na mleta ombi la kumuwakilisha hakuna pingamizi lilitolewa na upande ambao ungeathirika na ombi hilo kuhusu maombi yaliyokuwa mbele ya mahakama ya mirathi. Hata hivyo, kwanza, ni muhimu pia kutofautisha kati ya suala la nani anaweza kuwakilisha mwingine katika shauri na suala la nani ana haki ya kupinga mwenendo wa shauri hilo. Mtu anaweza, katika mazingira yanayoruhusiwa na sheria, kuanzisha au kuendesha shauri kwa kutumia mwakilishi. Hata hivyo, ili mtu aweze kuhoji uhalali wa mwenendo huo kwa njia ya Revision, ni lazima aonyeshe maslahi ya kisheria yanayotambulika katika shauri hilo na namna ambavyo amepata madhara kutokana na mwenendo unaolalamikiwa. Katika mazingira ya shauri hili, sijaona namna matumizi ya Power of Attorney yalivyowabagua au kuwaathiri moja kwa moja wajibu rufani kiasi cha kuwapa msingi wa kuomba kufutwa kwa mwenendo mzima wa Mahakama ya Mwanzo. Pili katika mazingira ya kesi iliyokuwa mahakama ya mwanzo kwa wakati huo yalikuwa ni maombi ya uteuzi wa usimamizi wa mirathi, nimeangalia mapingamizi yaliyowekwa na wapingaji, kwa maoni yangu Page. 22 hayakuathiri, kubatilisha wala kuondoa uhalali wa mwenendo wa shauri hilo kwa sababu maudhui na madhumuni ya uamuzi wa mahakama ya mwanzo wa tarehe 20/12/2024 ulikuwa bayana na kuwashauri kuwa mapingamizi yao yaliletwa kabla ya wakati ( premature) ndio maana wakashauriwa kuleta mapingamizi baada ya uteuzi wa wasimamizi wa mirathi. Hivyo kwa muktadha niliosema hapo juu hata kama utaratibu haukuwa sawa mazingira ya kesi hii niliyoyasema hayakuathiri mdaawa yeyote na haki iliyokusudiwa ilipatikana. ( angalia kesi ya Stanley Murithi Mwaura vs Republic Criminal Appeal No. 144/2019 [2021] TZCA 688 ( TanzLII). Hivyo basi, katika shauri hili, sijaona namna warufani walivyopata madhara au kuwaathirika (prejudiced) kutokana na hati hiyo ya uwakilishi. Zaidi ya hayo, hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba matumizi ya hati hiyo yaliathiri kwa namna yoyote haki zao za msingi au uwezo wao wa kuwasilisha na kutetea maombi yao mbele ya Mahakama ya Mwanzo. Kwa hiyo, kwa maoni yangu, Mahakama ya Wilaya ilikosea kisheria kuhitimisha kwamba hati ya uwakilishi ilikuwa batili kwa sababu tu haikutaja sababu iliyomfanya mtoa mamlaka kushindwa kufika mwenyewe mahakamani. Ni kutokana na sababu hizo natengua uamuzi wa mahakama ya wilaya wa kufuta uteuzi wa wasimamizi wa mirathi uliotolewa na mahakama ya mwanzo tarehe 27/12/2024, hivyo basi maamuzi hayo ni halali na walioteuliwa wanaendelea kuwa wasimamizi wa mirathi ya Marehemu Eliya Abraham Msangi @ Nabii Eliya. Jambo jingine la kujadili, Mahakama ya wilaya iliendelea na kusema kuwa warufaniwa 1 mpaka wa 26 walikosa haki zao, katika hili nimezingatia pia sababu zilizotolewa katika maombi ya Revision yaliyokuwa mbele ya Page. 23 Mahakama ya Wilaya. Ni ukweli usiopingika kwamba anayelalamika kunyimwa haki ya kusikilizwa anapaswa kuonyesha namna haki hiyo ilivyokiukwa na namna alivyopata madhara kutokana na ukiukwaji huo. Nimesoma kiapo kilichopelekwa na wajibu rufani kwenye maombi ya Revision mahakama ya wilaya (Probate Revision no.15786 of 2025) ambapo, paragraph ya 9, 10, 11, 12, 13 na 14 ziko bayana kuwa wasimamizi wa mirathi walikuwa wameingilia mali zao, na wakasema katika mahakama hiyo kuwa walioenda kuweka pingamizi ya mali hizo ambazo ni zao, wao hawakuwapa mamlaka kuwawalikisha, hivyo haki yao ya kusikilizwa ilipokonywa. Nimepitia kumbukumbu za mahakama, nimeoni hili ni kweli kabisa; nayasema haya kwa sababu, kama nilivyosema hapo juu mapingamizi haya ya mali za marehemu ndio yaliyopelekea uamuzi wa pili kutolewa na mahakama ya mwanzo mnamo tarehe 6/6/2025. Ukipitia mwanzo wa mwenendo wa mapingamizi hayo yaliyoanzia katika ukurasa wa 27 wa mwenendo uliochapwa; unaonyesha mpingaji Hagai Elia Msangi akionyesha kuwa anawawakilisha wenzake, na hapa kwa wepesi wa rejea nanukuu:- “12/05/2025 MBELE YA M.A.CHANDE-HAKIMU MKAZI Wasimamizi wa Mirathi- wapo Mleta pingamizi-yupo M.A. CHANDE-HAKIMU 12/05/2025” MAHAKAMA Shauri limekuja kwa ajili ya kusikiliza pingamizi Page. 24 Mleta pingamizi Nipo tayari na nina vielelezo sitakuwa na shahidi Wasimamizi wa Mirathi Tupo tayari SHAURI LINAANZA PINGAMIZI JINA: HAGAI ELIYA MSANGI UMRI: 36 DINI: MKIRISTO KABILA: MPARE KAZI: AFISA MAGEREZA MAKAZI: GEREZA LA KARANGA Ameapa na kusema katika pingamizi hili mimi na wenzangu ambao nimeorodhesha hapo na pingamizi. Tunapinga mali zetu kuchanganywa na mali za marehemu, zile mali zilikuwa pamoja ( co-owned) na sio za marehemu pekee yake. Nina vielelezo kadhaa juu ya Hilo. Kikao cha tisa cha 1982 kinaeleza juu ya umiliki wa mali. Mpingamizi: naomba kutoa muhtasari wa kikao hicho kama kielelezo Mahakama: muhtasari utolewe upande wa pili kama pingamizi. Pingamizi 1: sina pingamizi Pingamizi 2: haya mheshimiwa sio mazungumzo ya mwisho ya marehemu sina pingamizi, nitaleta ushahidi wa kupinga. Mahakama: kielelezo kinapokelewa Kama W-01. M.A. CHANDE-HAKIMU 12/05/2025” Page. 25 Baada ya hayo yaliyonakilwa, katika ukurasa uliofuata wa 29 na 30, shahidi huyu aliendelea kutoa vielelezo vingine vilipokelewa kama W-02 na W-03, vielelezo hivi vyote vinahusu wanajumuiya ya Ikongwe ambao miongoni mwao ndio hao walioomba mapitio mahakama ya wilaya wakieleza kwamba wao hawakuwatuma wajibu maombi wa wa 3 na wa 4 ambao katika rufaa hii ni wajibu rufaa wa 27 na 28, kwamba hawakuwatuma kuwawakilisha wanajumuiya hao . Nimeangalia pia hati iliyopokelewa katika mahakama ya mirathi mnamo tarehe 14.4.2025 ambayo inaonyesha mpeleka mapingamizi akiwa anawawakilisha wanajumuya na katika kiambatanisho cha hati hiyo, kuna sahihi za wanaowakilishwa. Hata hivyo barua au hati hiyo ya mapingamizi na ambayo ndio msingi wa uwakilishi wa wanajumuiya hao wa Ikongwe ikiwemo warufaniwa wa 1-26 haikutolewa mahakamani kama ushahidi ili kuthibitisha kuwa kweli walipata mamlaka hayo toka wanajumuiya ya Ikongwe. Mahakama ya mirathi katika uamuzi wake, iliona kuwa jambo hili lilikuwa sio la msingi sana lakini kwa mazingira ya kesi hii pamoja na warufaniwa wote 1-26 kukana kuwapatia mamlaka mrufaniwa wa 27 na 28 kama wawakilishi wao, ninaona lilikuwa na umuhimu. Hivyo Haikuwa sahihi kwa mahakama ya mwanzo kusema katika ule ukurasa wake wa 2 wa uamuzi kuwa Hagai Eliya Msangi alikuwa mleta pingamizi kwa niaba ya wanajamii 47 wa Ikongwe wakati kulikuwa hakuna ushahidi wa kiuhalali ulioingizwa kwenye kumbukumbu za mahakama kama ndugu huyo alikuwa anawawakilisha wanajumuiya hao. Nikutokana na sababu hizo tajwa hapo, nimefikia maamuzi ya kuona kuwa katika mapingamizi yaliyowekwa mara tu baada ya kuteuliwa wasimamizi wa mirathi kama nilivyoelezwa hapo juu, na yaliyowasilishwa na Bwana Hagai Eliya Msangi bila kuwa na mamlaka ya kuwawakilisha hao wanajamii 47 wa Ikongwe, ninaona kuwa kwa mkutadha huo basi ni kweli walikosa haki ya kusikilizwa jambo ambalo linaathiri mwenendo wote wa Page. 26 mahakama ya mwanzo kuanzia mnamo tarehe 12/05/2025 ilipoanza kusikiliza mapingamizi yaliyowasilishwamara baada ya orodha ya mali za marehemu kuwasilishwa katika mahakama ya mirathi na wasimamizi wa mirathi, ambapo maamuzi yake yalitolewa mnamo tarehe 6/6/2025. ( Angalia kesi ya Margwe Error & Others vs Moshi Bahalulu (Civil Appeal No. 111 of 2014) [2015] TZCA 282 (25 February 2015), ECO-TECH (Zanzibar) Limited vs Government of Zanzibar, ZNZ Civil Application No. 1 of 2007 (unreported), Mbeya-Rukwa Auto Parts & Transport Limited vs Jestina George Mwakyoma- Civil Appeal No. 45 of 2000 (unreported), D. P. P. vs Sabina Tesha & Others [1992] T. L. R. 237, Dishon John Mtaita vs D. P. P.- Criminal Appeal No. 132 of 2004 (unreported) kutaja chache. Hivyo basi kutoka na misamamo tajwa ya kisheria mwenendo wote wa kesi wa mapingamizi ya pili baada ya uteuzi unakuwa batili na kufutwa, pia maamuzi ya mahakama ya Mwanzo ya tarehe 6/6/2025 yanafutwa kabisa. Kuhusu hoja ya sita kwamba majina ya wadaawa yalikuwa yamekosewa au kutofautiana na majina yaliyokuwa katika shauri la awali, nimeipitia rekodi na kuona kwamba hoja hiyo haina mashiko. Ni kweli kwamba hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Same iliyopo katika mfumo wa ECMS inaonyesha majina ya wadaawa kama Augustino Ngaraba Karugwe vs. Paulo Eliya Msangi. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa na Wakili Kamani pamoja na wajibu rufani wa 27 na 28, nimeona kuwa tofauti hiyo ya majina inatokana na namna taarifa zilivyozalishwa katika mfumo wa ECMS ambazo hazina msimbo wa kuonyesha majina yote ya wadaawa katika kesi. Nimezingatia zaidi nyaraka zilizoambatanishwa katika shauri hilo ambazo ziko kwenye mfumo was ECMS na nimeona kwamba zinaonyesha kwa uwazi majina ya wahusika waliowasilisha na kushiriki katika Maombi ya Marejeo yaliyokuwa mbele ya Mahakama ya Wilaya. Page. 27 Kwa hiyo, kwa kuzingatia nyaraka na mwenendo mzima wa shauri, tofauti hiyo ya majina katika kichwa cha hukumu haiwezi kwa yenyewe kubatilisha uamuzi wa Mahakama ya Wilaya iwapo wahusika, kwani mgogoro uliokuwa mbele ya Mahakama na haki na wajibu wa pande hizo vilikuwa vinaeleweka. Mwisho kwa haya niliyojadili hapo nahitimisha kuwa uteuzi wa wasimamizi wa mirathi uliotolewa na mahakama ya mwanzo tarehe 27/12/2024, ni halali na walioteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi ya Marehemu Eliya Abraham Msangi @ Nabii Eliya, ambao ni Paul Eliya Msangi na Uzima Eliya Msangi wanarejeshwa katika majukumu yao ya usimamizi wa mirathi. Pili mwenendo wote wa kesi wa mapingamizi baada ya uteuzi wao unaoanzia tarehe 12/05/2025 unakuwa batili na kufutwa, pia maamuzi ya mahakama ya Mwanzo ya tarehe 6/6/2025 yanafutwa kabisa. Badala yake natoa amri, jalada la mahakama lilirudishwe katika mahakama ya Mwanzo Kisiwani kwa ajili ya kuendelea na usimamizi wa mirathi, na endapo kuna ndugu au mtu yoyote anapinga uteuzi wa wasimamizi wa mirathi, basi arudi katika mahakama hiyo hiyo ya mirathi kupinga uteuzi wao na wala si kwenda mahakama ya juu, kwani hiyo ndio mamlaka ya kutengua uteuzi wao, na hii ni kama ilivyobainishwa katika kanuni ya tisa ya kanuni za uendeshaji wa mirathi katika mahakama za mwanzo ( The Primary Courts (Administration Of Estates) Rules GN. No. 49 of 1971. Aidha wapingaji wa mgawanyo wa mali ya marehemu kama wapo wawasilishe mapingamizi upya katika mahakama ya mwanzo hiyo kwa kusingazitia misingi ya uwakilishi iliyopo kwa mujibu wa sheria. Na endapo hayo maombi tajwa hapo juu yatafikishwa mahakamani yasikilizwe na Mheshimiwa Hakimu mwingine. Hivyo rufaa hii imefaulu kwa kiasi kama nilivyoelezea hapo juu, kutokana na kuwa kesi hii ina asili ya mirathi, natoa amri kila upande ubebe Page. 28 gharama zake. Dated at MOSHI this 31st of August 2026 . A. P KILIMI JUDGE OF THE HIGH COURT Page. 29