PETRO GUNDANGA EDITED 2222222222222222
Appellant failed to prove lawful acquisition or ownership of the disputed land; allocation by village council is mandatory for valid title; evidence presented by appellant was insufficient and unreliable; adverse possession cannot confer title over village land; tribunal had jurisdiction based on claim value.
Source-derived case information.
- Citation
- PETRO GUNDANGA EDITED 2222222222222222
- Parties
- Appellant: Petro Gundanga; Respondent: Petro Kwashema; Respondent: Paulo Bwatata; Respondent: Lucia Gashari
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2020
- Procedural Posture
- Land Appeal / Final Judgment
- Outcome
- appeal dismissed
- Legal Topics
- Burden of Proof, Adverse Possession, Village Land Management, Authority of Village Council, Evidence Assessment
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Petro Gundanga
Appellant
Petro Kwashema
Respondent
Paulo Bwatata
Respondent
Lucia Gashari
Respondent
Procedural Posture
Land Appeal / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the appellant proved ownership of the disputed land
- 2 Whether the village council approval is required for land allocation
- 3 Whether adverse possession applies to village land
Ratio Decidendi
Appellant failed to prove lawful acquisition or ownership of the disputed land; allocation by village council is mandatory for valid title; evidence presented by appellant was insufficient and unreliable; adverse possession cannot confer title over village land; tribunal had jurisdiction based on claim value.
Court Disposition
appeal dismissed
Orders
- Appeal dismissed with costs
- Decision of the District Land and Housing Tribunal affirmed
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MASJALA NDOGO YA MANYARA BABATI RUFAA YA ARDHI NA.6445 YA 2024 (Inatokana na Shauri la Ardhi Na. 86/2020 katika Baraza ia Ardhi na Nyumba ia Mahakama ya Wiiaya Hanang'iiiipo Katesh) PETRO GUNDANGA............................................... MKATA RUFAA VERSUS PETRO KWASHEMA.............................................. 1. MJIBU RUFAA PAULO BWATATA................................................. 2. MJIBU RUFAA LUCIA GASHARI...................................................... 3. MJIBU RUFAA HUKUMU 21st & 20" Agosti, 2024 Kahyoza, J.: Petro Gundanga (mkata rufaa) aliwafungulia madai dhidi ya Petro Kwashema, Paulo Bwatata na Lucia Gashani, (wajibu rufaa) mbele ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wiiaya (Baraza) akidai kuwa wamevamia ardhi yake. Baada ya baraza kuwasikiliza wadaawa liliamua ya kuwa Petro Gundanga hakuthibitisha mdai yake na kufukuza madai hayo kwa gharama. Petro Gundanga hakuridhika na maamuzi, hivyo kukata rufaa katika Mahakama hii akidai; mosi, kuwa baraza halikuzingatia uzito wa ushahidi uliotolewa na hivyo kufikia maamuzi yenye makosa; pili, kuwa baraza lilishindwa kutambua kuwa awali lilikwisha amua kuwa Petro Gundanga ni mmiliki halali wa ardhi hiyo; tatu, kuwa baraza halikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri kwani baraza tayari lilikwisha kusikiliza shauri hilo; nne, kuwa baraza lilishindwa kuzingatia ushahidi wa Petro Gundanga ambao i hakupingwa; na mwisho, kuwa baraza lilikosea kutilia maanani ushahidi usiokuwa wa kweli wa wajibu rufaa. Hoja za rufaa ya Petro Gundanga zilibua kiini kikubwa kimoja na vinii vidogo vingine kama ifuatavyo- 1) je baraza lilikuwa sahihi kuamua kuwa Petro Gundanga alishindwa kuthibitisha madai yake? a) je baraza halikuzingatia uzito wa ushahidi uliotoiewa? b) je baraza lilitakiwa kufuata uamuzi wake wa awali kama upo wa kuwa ardhi yenye mgogoro ni ya Petro Gundanga? c) je baraza lilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hili? d) je ni kweli kuwa baraza halikuzingatia ushahidi wa Petro Gundanga? e) je ushahidi wa wajibu rufaa ulikuwa si wa kuaminika? Kwa ufupi sana mlolongo wa mgogoro wa ardhi bishaniwa uko hivi; Petro Gundaga alifungua shauri la madai ya ardhi yenye ukubwa wa eka 3 na mipaka kama ifuatavyo, Kaskazini -Samwel Sora, Mashariki - Petro Gundanga, Magharibi- chanzo cha maji na Kusini- Pario la mifugo. Petro Gundanga alidai katika hati yake ya kufungulia shauri ya kuwa ardhi hiyo 2 ilikuwa na thamani ya Tzs. 6,000,000.00 na kuwa ardhi hiyo anaimiliki mwenyewe na kwamba aliiangaikia (processed) mwenyewe na kuanza kuitumia tangu mwaka 1994 yaani " that the disputed land was processed by myself and began to use it since 1994.” aliongeza kuwa wavamizi wa ardhi yaani wajibu rufaa wanadai ya kuwa ardhi hiyo walipewa na bibi yake jambo ambalo siyo sahihi. Wadaawa walishindwa kuleta majibu ya madai hayo, baraza likaamua kesi isikilizwe upande mmoja. Kabla ya kesi kusikilizwa upande mmoja, wajibu rufaa waliomba baraza litengue amri ya kuendesha kesi kwa upande mmoja. Baraza lilitengua amri ya kusikiliza kesi kwa upande mmoja na kuamru kesi isikilizwe pande zote mbili. Kabla wajibu rufaa hawajawasilisha majibu yao, Petro Gundanga aliomba kurekebisha maombi yake. Hata hivyo kabla hajawasilisha marekebisho ya maombi yake mbele ya baraza, wajibu rufaa walikwisha peleka majibu yao. Petro Gundanga alifanyia marekebisho hati yake ya madai. Baada ya kurekebisha hati yake ya maombi, Petro Gundanga alidai kuwa eneo bishaniwa ni halali yake alilipata kwa umiliki mwaka 1994 baada ya kupewa na wazazi wake kwa hati ya tarehe 5.11.1994. Aidha, alieleza kuwa alilipata shamba hilo kupitia ushindi wa Mahakama mwaka 2009 kupitia 3 maombi Na. 111/2009 na shauri dogo la Na. 10/2009. Aliongeza kuwa hoja ya kuwa wadaawa waliuziana mwaka 2017 nikuhalalilisha uvamizi kwani wasingeuziana eneo lake ilihali muda wote lilikuwa mkononi mwake. Aliambatisha hati ya kukabidhiwa. Alidai eneo hilo lilikuwa ndani ya kijiji Mreru ila hakutaja ukubwa wala mipaka ya eneo lake. Wajibu rufaa ambao walikuwa wajibu maombi walikanusha madai ya Petro Gundanga na kueleza kwa pamoja kuwa, eneo la mgogoro hadi mwaka 2017 lilikuwa ni mali halali ya Paulo Bwatata na Lucia Gashani. Mwaka 2017 Paulo Bwatata na Lucia Gashani walimuuzia eka mbili Petro Kwashema. Hivyo eneo analodai Petro Gundanga, eka (2) mbili ni za Petro Kwashema na eka (1) moja ni ya Paulo Bwatata na Lucia Gashani. Walidai kuwa eneo bishaniwa ni sehemu ya eka (8) nane ambazo Paulo Bwatata aligawiwa na halmashauri ya serikali ya Kijiji cha Mureru mwaka 2010. Waliambatisha muhtasari wa kikao cha kijiji. Petro Gundanga alitoa ushahidi wake kwa kueleza kuwa eneo la mgogoro ni kati ya eka (20) alizopewa na mama yake mnamo mwaka 1994 mbele ya Enock Gidamis (Pw2). Petro Gundanga na Enock Gidamis (Pw2) walieleza ya kuwa mwaka 2009 Habonju alivamia eneo la mgogoro. Petro Gundanga alimshtaki Habonju na kumshinda na hivyo baraza la kata 4 likampatia eneo lake ambalo baraza la wilaya lilimkabidhi Petro Gundanga alitoa hati ya kupewa shamba na mama yake, uamuzi wa baraza la kata, uamuzi baraza la wilaya Babati, hati ya dalali ya kukabidhi na hukumu ya Katesh ya jinai kama kielelezo. Baraza lilipokea nyaraka hizo kwa pamoja kama kielelezo bila kukitaja namba ya kielelezo hicho. Petro Gundanga alikuwa na shahidi mwingine Bw. Muna Gilba (Pw3). Bw. Gilba Muna, alieleza kuwa Petro Gundanga mwaka 1994, Gabriel na mama yake Pwl (Petro Gundanga) walifika kijijini kwa nia ya kuvamia na yeye Bw. Muna Gilba (Pw3) alikuwa mwenyekiti wa kijiji. Bw. Muna Gilba (Pw3) aliwapatia maeneo ya mapori yasiyo kuwa na watu. Baada ya kuwapatia wao waligawana maeneo. Na mwaka huo huo, mama yake na Pwl (Petro Gundanga) alimkabidhi mwanae mbele ya ofisi na Bw. Muna Gilba (Pw3) alikuwa shahidi wa maandishi hayo. Petro Kwashema (Dwl) yeye alidai alifika kijiji cha Mureru mwaka 2006 na kupokelewa na kuishi kwa Bw. Muna Gilba (Pw3). Mwaka 2016 alinunua eneo la eka (1) kutoka kwa Petro Gundanga, kisha kuhamia kwenye eneo lake na kuanza kuishi. Baadae mwaka 2017 alinunua eneo la eka (2) kutoka kwa Lucia Gashani na mme wake Paulo Budata (Bwatata). Alitoa kielelezo cha kunuua eneo la eka 2 kutoka kwa Paulo 5 Bwatata kama elelezo DI. Petro Kwashema aliongeza kuwa mwaka 2018 alilima eneo lake bila shida. Mwaka 2019 Petro Gundanga alimshtaki Petro Kwashema mahakama ya mwanzo na Petro Kwashema kumshinda kesi. Alitoa nakala ya hukumu kama kielelezo D2. Wajibu rufaa waliita James Gejalu (Dw2), ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa kijiji cha Mureru aliyebainisha kuwa waadaawa wote ni wanakijiji chake. James Gejalu (Dw2), alieleza kuwa eneo lenye mgogoro ni mali ya Lucia Paulo kwani kijiji kilimpatia Lucia Paulo eneo hilo. Na kuwa baada ya kuwa wamempatia eneo hilo, Petro Gundanga aliibuka na kudai kuwa eneo ni la kwake. James Gejalu (Dw2)z wakati wa kuhojiwa alieleza kuwa eneo hilo alipewa Lucia mwaka 2010. Alieleza pia kuwa Petro Gundanga alipewa eneo lake mwaka 2004. Alitaja mipaka ya eneo la Lucia Paulo kama Magharibi vyanzo vya maji, Mashariki ni Petro Gundanga, (mleta maombi), Kusini- Palio, na Kaskazini- Samwel Swala. Alidai walimpatia jumla ya eka nane. Daudi Alanjiga (Dw3) alilieleza baraza kuwa Petro Gundanga alihamia kijiji cha Mureru mwaka 1996 na mnamo mwaka 2004 alipewa eneo la ekari 5 na halmashauri ya kijiji. Alitoa muhtasari wa kumpatia eneo la ekari 5 kama kielelezo D3. Aliongeza kuwa mlalamikaji anapakana na eneo jingine 6 ambalo lilikuwa halijapangiwa matumizi. Daudi Alanjiga (Dw3) alieleza kuwa kuna mtu alivamia eneo hilo anaitwa Hamboje, kijiji kilimuondoa. Alitoa muhtasari wa kikao cha tarehe 3.10.2011. Daudi Alanjiga (Dw3) alieleza kuwa Petro Gundanga alivamia eneo la Lucia Paulo mwaka 2015 kijiji kilisuluhisha mwaka 2015 na kumaliza mgogoro huo baadae alifufua kesi na kumshtaki mtu ambaye hana eneo kwenye kijiji. Baadae dalali alienda kutekeleza hukumu, kijiji kiliandika barua ya tarehe 29.10.2018 kwamba hapakuwa na eneo la kukarnbidhi Petro Gundanga. Wakati wa kuhojiwa maswali, Daudi Alanjiga (Dw3) alieleza kuwa wakati wito wa kugawa maeneo, yeye alikuwa Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji hata wakati anatoa ushahidi alikuwa na nafasi hiyo. Musa Mathayo (Dw4) alieleza kuwa mwaka 2019 walibaini kuna mgogoro ambao Petro Gundanga alidai Lucia Paulo ameuza eneo lake kwa Petro Kwashema (Dwl). Walichunguza na kubaini kuwa malalamiko ya Petro Gundanga si ya kweli. Walisuluhisha lakini Petro Gundanga alikataa sululu. Baraza lilikuwa na maoni ya kuwa ushahidi wa wajibu rufaa una mashiko kwani mashahidi wote walionekana kulijua vyema eneo la mgogoro. 7 Baraza liliamua kuwa Petro Gundanga ameshindwa kuthibitisha madai yake. Baada ya kupitia Ushahidi nilianza kujibu viini. Je baraza lilikuwa sahihi kuamua kuwa Petro Gundanga alishindwa kuthibitisha madai yake? Rufaa ilisikilizwa kwa njia ya maandishi na hoja za mdomo. Mkata rufaa aliandika hoja zake kwa maandishi zikajibiwa kwa mdomo na wajibu rufaa wa kwanza na wa tatu. Mjibu rufaa wa pili hakufika mahakamani kwani ilielezwa kuwa ni mzee sana. Mkata rufaa alieleza kuwa yeye alikuwa ameishi kwenye eneo hilo tangu mwaka 1994 kwa amani na utulivu. Alibainisha kuwa kesi ya Hemedi Said v Mohamed Mbilu [1984] TLR 113 inasisitiza umuhimu wa nyaraka kama ushahidi wa umiliki. Mbali na hoja za maandishi mashahidi wa Petro Gundanga, mkata rufaa, Bw. Muna Gilba (Pw3) alieleza kuwa Petro Gundanga, Gabriel na mama yake Petro Gundanga walifika kijijini kwa nia ya kuvamia na yeye Bw. Muna Gilba (Pw3) akiwa mwenyekiti wa kijiji aliwapatia maeneo ya mapori yasiyo kuwa na watu. Baada ya kuwapatia wao waligawana maeneo. Kifupi ushahidi wa mkata rufaa ni kuwa alipewa maeneo na uongozi wa kijiji. 8 Ni wazi kuwa, eneo ambalo anadai kupewa lilikuwa eneo la kijiji cha Mureru na alipewa na Bw. Muna Gilba (Pw3) kama mwenyekiti wa kijiji. Hakuna ushahidi wa Bw. Muna Gilba (Pw3) kugawa ardhi kwa Petro Gundanga na wala hakuna shahidi mwingine ambaye alithibitisha ugawaji huo. Pia eneo la kijiji haliwezi kugawiwa na mtu mmoja kama eneo lake na kufanya hivyo bila ushahidi. Halmashauri ya Kijiji ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kugawa eneo na siyo Bw. Muna Gilba (Pw3) kama yeye mwenyewe au kama mwenyekiti wa kijiji. Msimamo wa kisheria kuwa eneo la kijiji haliwezi kugawiwa na mtu bila kuthibitishwa na halmashauri ya kijiji. Kwa kifupi msimamo huo unaeleza kuwa baada ya kijiji kusajiliwa, ni halmashauri ya kijiji chenye jukumu la kusimamia ardhi ya kijiji. That is once the village was registered the management of the village land became the function of the village council'. Naomba kurejea maamuzi katika kesi ya National Agricultural and Food Corporation V Mulbadaw Village Council and Others, [1985] TLR 88 and G.N. 168/75, para 5(2) provides as follows- "(2) subject to availability of arable land, the Village Council shall allot a piece of farmland to every kaya in the village according to need and ability to develop it. The Village Council shall have power to determine the structural pattern of farms in the village and the use thereof " 9 Aidha, mwongozo huo wa "G.N. 168/75" unampatia mwanakijiji jukumu la kupata ardhi kutoka katika kijiji chake kwa ajili ya shughuli za kiuchumi. "Para 7(2) of the Directions aforesaid which provides as follows: (2) Every resident of a village shall have the duty to obtain, and shall be entitled to be allotted, a piece of land in the village on which he shall carry on economic activities, whether on an individual basis or in association with other resident."Msimamo huo ulithibitishwa pia na Mahakama ya Rufani katika kesi ya Metthuselah Paul Nyagwaswa v Christopher Mbote Nyirabu [1985] TLR 103. Katika shauri hili Mahakama ya Rufani aliamua kuwa mtu hawezi kumpatia ardhi mwenzake au kuuza bila halmashauri ya kijiji kuidhinisha ugawaji au uuzaji huo, yaani "the Court found that there was no transferred because the village council did not approve it." Mahakama ya Rufani iliamua kuwa- "rights to land held in a registered village could only be transferred with the approval of the Village Council... the sale to the appellant, for lack of approval, was void and of no effect." Kwa msimamo huo wa kisheria ni wazi kuwa Bw. Muna Gilba (Pw3) alikuwa hana mamlaka ya kumpatia Petro Gundanga, Gabriel na mama yake ardhi bila kibali cha halmashauri ya Kijiji. Hata kama ingekuwa kweli kuwa Bw. Muna Gilba (Pw3) alimgawia Petro Gundanga, Gabriel na io mama yake ardhi, kitendo ambacho hakuna ushahidi wa kukithibitisha, ugawaji huo ni batili kwa kukosa baraka za halmashauri ya kijiji. Hivyo hoja ya kuwa Petro Gundanga alipewa ardhi ya mgogoro na mama yake inakosa msingi kwa sababu mama yake Petro Gundanga hakuwahi kupata ardhi hiyo kihalali, kama alipewa na hivyo hakuwa na ardhi ya kumpatia Petro Gundanga. Aidha, hoja ya kuwa Petro Gundanga alipewa ardhi na Bw. Muna Gilba (Pw3) inakosa msingi wa kisheria kwa sababu Bw. Muna Gilba (Pw3) hakuwa na mamlaka ya kugawa ardhi bali ni halmashauri ya kijiji ndiyo mamlaka ya kugawa ardhi. Mbali na msingi hiyo ya kisheria, pia nilitilia mashaka hati aliyoitoa Petro Gundanga ya kugawiwa ardhi na mama yake mwaka 1994. Hati hiyo inaonekana imetayarishwa siku za hivi karibuni kwa sababu zifuatazo, kwani mwaka 1994 kompyuta zilikuwa sehemu chache. Hati iliyo na zaidi ya miaka 26 ilionekana mpya kabisa. Siyo hilo tu bali hata Petro Gundanga hapo awali hakuwa ameonesha kuwa alipata ardhi hiyo kutoka kwa mama yake na kuweka nyaraka hiyo. Nyaraka hiyo ilitolewa baada ya Petro Gundanga kufanyia marekebisho hati yake ya madai. Nyaraka ya makabidhiano hiyo ilikuwa ya kugushi. ii Kutoka na ushahidi wa Petro Gundanga wa jinsi gani alipata ardhi bishaniwa kuwa dhaifu, kunatoa nafasi kuamini ushahidi wa wajibu rufaa kuwa Petro Gundanga alipewa ardhi na serikali ya kijiji mwaka 2004 na kuwa alipewa ekari 5. Daudi Alanjiga (Dw3) alieleza baraza kuwa Petro Gundanga alihamia kijiji cha Mureru mwaka 1996 na mnamo mwaka 2004 alipewa eneo la ekari 5 na halmashauri ya kijiji. Alitoa muhtasari wa kumpatia eneo la ekari 5 kama kielelezo D3. Hata hivyo muhtasari huo ulikuwa hakuambatishwa kwenye hati ya majibu ya madai. Kwa sababu hiyo nashindwa kutilia maanani kielelezo D3. Pamoja na kutotilia maanani ushahidi wa kielelzo D3 bado ushahidi wa Daudi Alanjiga (Dw3) una nguvu na unathibitisha hoja kuwa Petro Gundanga alipewa eneo mwaka 2004 na ni eneo la ekari 5 na nitofauti na eneo linalobishaniwa. Je inawezekana Petro Gundanga alipata ardhi kwa kuikalia muda mrefu bila kwa amani na utulivu? Petro Gundanga alidai kuwa amekalia eneo ya ardhi yenye mgororo toka mwaka 1994 kwa amani na utulivu had? mgogoro ulipoibuka. Hoja hii ni hafifu kwani hakuna ushahidi kuwa Petro Gundanga alikalia eneo hilo tangu mwaka 1994. Hata kama kuna ushahidi huo, bado sheria iko bayana 12 kuwa hairuhusiwi kuchukua eneo la kijiji kwa kulikalia kwa muda mrefu. Hakuna shaka kuwa eneo la mgogoro lilikuwa sehemu ya ardhi ya kijiji hivyo haiwezekani Petro Gundanga akajipatia ardhi ya kijiji kwa kuikalia kwa muda mrefu. Kifungu 38 cha Sheria ya Ukomo wa Muda [Sura 89] yaani ' Section 38 of the Law ofLimitation Act, [Cap. 89 R.E. 2019]' inabainisha hivyo. Section 38 stipulates that no person shall acquire public land by adverse possession. It states that- 38 (1) Notwithstanding anything contained in this Act- fa) no person shall become entitled to an estate or interest in any public land by adverse possession; Section 2 of the Law of Limitation Act, (supra) defines the public land as follows- "Public land" means any land which is not held, or deemed by the provisions of the Government Leaseholds (Conversion to Rights of Occupancy) Act to be held, under a right of occupancy, or under customary law, or under the pro visions ofsection 5 of the Customary Leaseholds (Enfranchisement) Act; Petro Gundanga hakubainisha kuwa alikuwa anamiliki ardhi ya mgogoro kimila kwani alisema kuwa alipewa na mama yake na ushahidi wa Bw. Muna Gilba (Pw3) unaweka wazi kuwa ni yeye aliyewapatia ardhi Petro Gundanga, Gabriel na mama yake. Hivyo ardhi bishaniwa ilikuwa ni ardhi ya umma yaani"public land' na hiyo sheria hairuhusu kumiliki ardhi hiyo kwa 13 kuikalia kwa muda mrefu. Hivyo, hoja ya Petro Gundanga kuwa aliikalia ardhi hiyo kwa muda mrefu kwa utulivu na amani, na hivyo ni ya kwake inakosa mashiko. Je ushahidi wa wajibu rufaa ulikuwa si wa kuaminika? Petro Gundanga alilalamika kuwa baraza lilikosea kuzingatia ushahidi wa wajibu rufaa ambao ni wa uongo. Ni vyema ifahamike kuwa kwa mjibu wa vifungu Na. 110 na 111 vya Sheria ya Ushahidi [Sura 6 Juzuu ya 2022] mwenye kuleta madai au hoja ndiye mwenye jukumu la kuthibitisha yaani is a trite law that he who alleges must prove". Sections 110 and 111 of the Evidence Act, Cap 6 RE 2002 which provides- "110. Whoever desires any court to give judgment as to any legal right or liability dependent on the existence of facts which he asserts must prove those facts exist 111. The burden of proof in a suit proceeding lies on that person who would fail if no evidence at all were given on either side. Mahakama ya Rufani katika shauri la Anthony M, Masanga vs Penina (mama Mgesi) and Another (Civil Appeal No. 118 of 2014) [2015] TZCA 556 (18 March 2015) ilisisitiza kuwa kwenye mashauri ya madai mwenye jukumu la kudhibitisha jambo ni yule mwenye kuleta hoja au kutaka hukumu itolewe kwa upanda wake yaani "Let's begin by re-emphasizing the 14 ever cherished principle of law that generally, in civil cases, the burden of proof Ues on the party who alleges anything in his favour". Katika shauri hili aliyekuwa na jukumu la kuthibitisha kuwa ardhi ya mgogoro ni yake ni Petro Gundanga na siyo wadaiwa yaani wajibu rufaa. Wadaiwa au wajibu maombi ambao kwa sasa ni wajibu rufaa wangekuwa na jukumu la kupinga ushahidi baada ya Petro Gundanga kutoa ushahidi unathibitisha hoja zake. Mahakama ya Rufani ilisema hayo katika kesi ya Yusufu Selemani Kimaro vs Administrative General & Others (Civil Appeal 266 of 2020) [2022] TZCA 306 (24 May 2022) kwa Kingereza kwamba- ".....Going by the above exposition of the law, it would be insincere if not a misapprehension of the law on the part of Mr, Haifani to complain as he did that the trial Judge had shifted the onus ofproof onto the second respondent. For, in civil cases, the onus of proof does not stand still, rather it keeps on oscillating depending on the evidence led by the parties and a party who wants to win the case is saddled with the duty to ensure that the burden of proof remains within the yard of his adversary. This is so because as per the case of Raghramma v. Chenchamma, A 1964 SC 136, such a shifting of onus is a continuous process in the evaluation of evidence. " Baada ya Petro Gundanga kushindwa kuleta ushahidi wa kina kuthibitisha hoja zake, hata kama wajibu rufaa wasingetoa ushahidi wao 15 bado Petro Gundanga asingeshinda. Hivyo hata kama ushahidi wao usingekuwa wa kweli bado jambo hilo lisingemsadia Petro Gundanga kushinda kwani kwa sababu yeye ndiye alikuwa na jukumu la kuthibitisha madai yake. Hata hivyo, ukilinganisha ushahidi wa pande zote mbili, ushahidi wa wajibu maombi ulikuwa mzito. Wajibu maombi walileta ushahidi wa ambaye alikuwa kiongozi wakati wa kugawa maeneo na walileta muhtasari wa Mkutano wa kijiji ambacho ndicho chombo chenye mamlaka ya rnwisho ya kugawa ardhi. Hivyo ushahidi wa wajibu rufaa ulikuwa mzito kuliko wa Petro Gundanga. Hoja ya kuwa baraza lilizingatia ushahidi wa uongo wa wajibu rufaa haina msingi. Je baraza lilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hili? Petro Gundanga hakueleza jinsi gani baraza halikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hili. Hakuna ubishi kuwa shauri linalojadiliwa ni juu ya mgogoro wa ardhi ambao mahala sahihi ni baraza la ardhi. Nimeangalia suala la mamlaka ya baraza kwa kuzingatia thamani ya madai na kuona kuwa Petro Gudanga alidai thamani ya shamba ni Tzs. 6,000,000/= na kiwango cha kusikiliza mashauri ya baraza kwa wakati huo kilikuwa kuanzia zaidi ya milioni tatu. Kifungu cha 15 cha Sheria ya Mahakama za Migogoro ya Ardhi 16 yaani "the Land Disputes Courts Act, [Cap.216 R.E. 2Z77^/kinabainisha kwa Kingereza kuwa- 15. Notwithstanding the provisions of section 10 of the Ward Tribunals Act, the jurisdiction of the Tribunal shall in all proceedings of a civil nature relating to land be limited to the disputed land or property valued at three million shillings. Kwa sababu hiyo, naona hoja ya kuwa Mahakama haina mamlaka haina msingi wowote. Je Baraza lilishindwa kuzingatia ushahidi wa mkata rufaa? Petro Gundanga alilalamika kuwa baraza halikuzingatia ushahidi wote. Katika hoja zake za maandishi, Petro Gundanga alieleza kuwa Sheria inatambua umiliki wa ardhi kwa njia ya urithi au kutoa kwa familia na inahitaji mahakama kuzitambua nyaraka kama hati ya kupewa shamba kama ushahidi halali wa umiliki. Alieleza kuwa katika kesi ya Amratial Damodar Maltaser & Another t/a Zanzibar Silk Stores v A.H. Jaraiwalla t/a Zanziba Hotel [1980] TLR 31, Mahakama ya Rufani ilisema kwamba mahakama za chini zinapaswa kuzingatia ushahidi wote uliowasilishwa mbele yao kabla ya kutoa uamuzi. Aiiendelea kuwa baraza lilitakiwa kuzingatia nyaraka zote za umiliki zilizowasilishwa na mrufani, pamoja na ushahidi mwingine ulitolewa. 17 Nilipata fursa ya kusoma uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi pamoja na kutoona mahala ambapo suala la kuzingatia ushahidi kabla ya kutoa uamuzi limeongelewa, maelekezo ya kuzingatia Ushahidi na nyaraka ndiyo msingi wa kutoa maamuzi katika kesi. Ni lazima kabla ya kutoa uamuzi kuzingatia ushahidi na nyaraka za pade zote mbili. Nimepitia hukumu na kubaini kuwa baraza lilipitia ushahidi wa pande zote mbili japo kwa ufupi. Baraza lilipitia ushahidi wa Petro Gundanga, mkata rufaa kuona ni hafifu. Ni vyema ieleweke kuwa kupitia ushahidi ni jambo jingine na kubaini kuwa ushahidi ni mzito na hivyo kuutumia kutoa uamuzi ni suala jingine. Baraza lilieleza kuwa- "Dw3 ametoa muhtasari wa Kijiji wa tarehe 3.10.2011 na makubaliano ya kati ya Kijiji na Rwl kuonyesha kwamba hataingiiia tana hiio, vielelezo D4 na D5, Dw3 anasema hata hivyo Rwl aliingilia mpaka wa Lucia na tarehe 20.01.2015 Serikaii ya Kijiji ilishurutisha. Rwl akaamua kufungua katika baraza ia ardhi akimdai mtu ambaye hana eneo pale kijijini. Na kwamba mieta maombi aiishinda na kukabidhiwa eneo ia Kijiji kiiiandika barua ya tarehe 29.10.2018 kueieza kuwa hakuna ardhi ya kukabidhi kwa Rwl kama daiaii wa baraza aiivyokuwa ametuhumiwa, kieieiezo D6 ni hiyo barua. Dw4 Mussa Mathayo anasema Lucia aiipata mgogoro na Rwl iakini ukweii ni kwamba Lucia aiipewa eneo na Serikaiiya Kijiji cha Mureru mwaka 2010. Na kwamba ni kweii Lucia aiiuza eneo ia eka mbili kwa Petro 18 Kwashema. Ni ushahidi huo wa mteta maombi na mashahidi wake na wajibu maombi na mashahidi wake na ajumbe wa baraza hi/i Bw. Joseph Mduma na Bi. Bertha Mkuti wametoa maoni yao kwamba baada ya kusikiiiza pande zote mbiii wanaona ushahidi wa wajibu maombi una mashiko kwa sababu mashahidi wao wote wanne wameonyesha kuiifahamu vizuri eneo ienye mgogoro na kutoa vieieiezo kuonyesha Serikaii ya Kijiji iiivyogawa eneo kwa Lucia na mieta maombi. Na kwamba vyote vimethibitisha kwamba eneo ienye mgogoro la ukubwa wa eka tatu siyo ma/i ya rn/eta maombi" Maelezo hayo ya baraza yanabainisha ukweli kuwa baraza lilizingatia ushahidi wote na kubani kuwa Petro Gundanga hana ushahidi wa msingi. Hivyo sioni msingi wa Petro Gundanga kulalamika kuwa ushahidi wake haukuzingatiwa. Hata kama kulikuwa na upungufu Mahakama hii imeuziba kwa kupitia upya ushahidi. Jukumu la mahakama ya kwanza ya rufaa, kama ilivyokuwa kwa Mahakama hii ni kupitia upya ushahidi na ikibidi inaweza kufikia uamuzi wa kwake tofauti na wa baraza, yaani "it is settled law that a first appeal is in theform of a rehearing. The first appellate court has a duty to reevaluate the enter evidence in an objective manner and arrive at its own findings of fact, if necessary". Baada ya kupitia ushahidi kama nilivyoonesha hapo juu bado ushahidi wa upande wa wajibu rufaa ni mzito kuliko ushahidi wa Petro Gundanga, mkata rufaa. Kwa kuwa nimepitia 19 upya ushahidi ulioko kwenye kumbukumbu, hata kama baraza halikupitia ushahidi wa huo, hakuna madhara. Je baraza lilitakiwa kufuata uamuzi wake wa awali kama upo wa kuwa ardhi yenye mgogoro ni ya Petro Gundanga? Petro Gundanga alilalamika kuwa baraza lilishindwa kuzingatia uamuzi wa awali wa kuwa eneo linalogombaniwa lilikwisha tolewa hukumu kuwa ni mali yake. Hi kuthibitisha kuwa eneo la mgogoro ni mali yake, Petro Gundanga alitoa nakala ya hukumu ya baraza la kata kesi ambayo ilikuwa kati yake na Habonju Gishumghoda. Aidha, alitoa pia nakala ya hati ya utekelezaji wa uamuzi huo kutoka baraza la ardhi na nyumba la Waliya. Ni wazi kuwa wajibu maombi hawakuwa sehemu ya kesi hiyo na hivyo maamuzi hayo hayawabani kwa namba yoyote ile. Hivyo baraza lisingetumia uamuzi katika shauri baina ya Petro Gundanga na Habonju Gishumghoda katika kutoa maamuzi katika shauri baina ya Petro Gundanga na Petro Kwashema, Paulo Bwatata na Lucia Gashani, (wajibu rufaa). Kama Baraza lingefanya hivyo lingekuwa limewanyima haki ya kusikilizwa wajibu rufaa. Hivyo, hoja hiyo nayo haina msingi. Mwisho, nimebaini baraza lilikuwa sahihi kuamua kuwa Petro Gundanga hakuthibitisha madai yake. Hivyo, Petro Gundanga alikata 20 rufaa bila sababu za msingi. Ninatupa rufaa yake kwa gharama na kukubaliana na uamuzi wa baraza ya kuwa Petro Gundanga alishindwa kuthibitisha madai yake kuwa eneo lenye mgogoro ni lake. Imeamuriwa hivyo leo 26 siku ya Agosti, 2024. R. Kahyoza JAJI MAHAKAMA: Hukumu imesomwa mbele ya Petro Gundanga, mkata rufaa, Petro Kwaslema, mjibu rufaa wa kwanza na Lucia Gashari, mjibu rufaa wa tatu na bila ya kuwepo mjibu rufaa wa pili. Bi. Fatina (RMA) yupo. R. Kahyoza JAJI 26/08/2024 21