9
There was no valid marriage between appellant and respondent, as respondent was already in a subsisting Christian monogamous marriage with Matrida David, which was never dissolved. Presumption of marriage does not apply where one party is already married. Appellant is not entitled to division of matrimonial property...
Source-derived case information.
- Citation
- 9
- Parties
- Appellant: Rachel Aidan Joseph; Respondent: Godgave Lipawaga
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2024
- Procedural Posture
- Civil Appeal / Final Judgment
- Outcome
- appeal dismissed
- Legal Topics
- Marriage Validity, Presumption of Marriage, Division of Matrimonial Property, Child Maintenance, Parentage Determination
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Rachel Aidan Joseph
Appellant
Godgave Lipawaga
Respondent
Procedural Posture
Civil Appeal / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether there was a valid marriage between appellant and respondent
- 2 Whether presumption of marriage applies
- 3 Whether appellant is entitled to division of matrimonial property
Ratio Decidendi
There was no valid marriage between appellant and respondent, as respondent was already in a subsisting Christian monogamous marriage with Matrida David, which was never dissolved. Presumption of marriage does not apply where one party is already married. Appellant is not entitled to division of matrimonial property or child maintenance under the Law of Marriage Act. Parentage and child maintenance issues fall within the jurisdiction of the Juvenile Court.
Court Disposition
appeal dismissed
Orders
- Judgment of Temeke District Court affirmed
- Appeal dismissed in its entirety
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MASJALA NDOGO, MAHAKAMA KUU KITUO JUMUISHI CHA UTOAJI HAKI TEMEKE RUFAA YA MADAI NA. 2536 YA MWAKA 2024 (Inatokana na Hukumu ya shauri la Ndoa Na. 107 /a mwaka 2023 Mahakama ya Wilaya mbe/e ya Hakimu Mkazi M. X. Sanga ya tarehe 21/12/2023) RACHEL AIDAN JOSEPH................................................................... MLETA RUFAA DHIDI YA GODGAVE LIPAWAGA........................................................................ MJIBU RUFAA HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho: 18/12/2024 Tarehe ya Hukumu:30/12/2024 S.D. MWAIPOPO J, Rufaa hii imefunguliwa na Rachel Aidan Joseph ambaye atarejewa kama Mleta rufaa) dhidi ya Godgave Lipawaga ambaye ni Mjibu rufaa, akipinga hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke, iliyotolewa na Mhe. Hakimu Mkazi M. X. Sanga katika Shauri la Ndoa Na. 107/2023, mnamo tarehe 21/12/2023. Awali mleta Mufaa alifungua shauri la ndoa kv/enye Mahakama ya Wilaya Temeke akiiomba Mahakama hiyo itoe Amri zifuatazo: 1. Kwamba, Mahakama itamke ya kwamba ndoa kati ya Mleta madai na Mjibu madai imevunjika katika hali ambayo haiwezi kurekebishika tena. 2. Kwamba, Mahakama hii itoe amri ya talaka. 3. Kwamba, Mahakama hii itoe amri ya kwamba Mleta madai na Mjibu madai wagawane nusu kwa nusu (50 kwa 50) mali zote za ndoa ambazo zimetajwa kwenye madai 4. Kwamba, Mahakama hii tukufu itoe amri ya kwamba makazi ya mtoto yawe chini ya Mleta maombi 5. Kwamba, Mahakama itoe amri kwa Mjibu madai ya kwamba atoe shilingi 400,000/= kwa ajili ya matunzo ya mtoto kila mwezi 6. Kwamba, Mahakama hii itoe amri kwa Mjibu maombi ya kwamba atoe pesa kwa ajili ya matibabu, elimu, mavazi kwa ajili ya mtoto. 7. Kwamba, Mahakama hii tukufu iweke utaratibu kwa nemna itakavyoona kwa ajili ya Mjibu maombi kumuona mtoto ambaye atakuwa chini ya Mleta maombi 8. Gharama za shauri hili zilipwe na Mjibu Maombi 9. Na nafuu yoyote ile ambayo Mahakama hii itaona inafaa. Mahakama ya Wilaya baada ya kusikiliza pande zote na mashahidi ilitoa uamuzi kama ifuatavyo: 1. Maombi haya yote yameshindwa kuthibitishwa 2. Maombi haya yanatupiliwa mbali kwa kukosa maana 3. Hakuna amri ya gharama. Kufuatia uamuzi huo Mleta rufaa hakuridhika na hivyo aliamua kukata rufaa Mahakama Kuu akiwa na hoja saba kama zifuatazo: - 1. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakarra ya Wilaya ya Temeke, amekosea kisheria na kimantiki kwa kutotamka kuwa Mleta rufaa na mjibu rufaa ni wanemdoa halali na hivyo basi ingezingatia ndoa yao imevunjika kcitika hali isiyorekebishika tena na hivyo kutoa amri ya talaka. 2. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, amekosea kisheria na kimantiki kwa kutozingatia hoja ya Mleta Rufaa kuwa Mleta Rufaa na Mjibu Rufaa kabla ya kufunga ndoa wallishi chini ya Dhan a ya Ndoa kama mke na mume kuanzia Mwaka 2006 mpaka 2009 3. Kwamba Mheshimiwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke ya Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea kisieria na kimantiki kutamka kuwa Mjibu Rufaa na mwanamke anayeitwa Matrida David Mwaigwisa ni wanandoa wakati tayari kuna talaka baina yao na ndoa ilishavunjwa tangu tarehe 2/11/2022 huko Zanzibar na kielelezo cha Hsti ya Kutengua Ndoa ambacho ni kielelezo 'B' kililetwa kama Ushahidi 4. Kwamba Mheshimiwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke ya Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea kisheria na kimantiki kwa kushindwa kutamka kuwa mali zifuatazo ni mali za ndoa na Mleta rufaa akiwa ni mke wa ndoa ana mchango kwenye hizi mali. Mali hizi za ndoa ni Nyumba Moja (1) ina vyumba 4, siting room na vyoo vya nje na fensi, ipo eneo la Killiara Golani, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, fremu 5 za biashara, Vitanda 3 na magodoro 3, Makaoati 3, Tank la Maji la lita 3000, sofa set 2, TV flat Screen 2, jiko la gesi na la umeme, Freezer, subwoofer 2, king'amuzi cha Azam TV na Gari aina ya Rav 4. 5. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea kisheria na Kimantiki kwa kushindwa kutoa amr ya mgawanyo wa mali za ndoa tajwa kwenye sababu ya rufaa na. 3 hapo juu kwa asilimia 50% kwa 50% kw<i kuzingatia mchango wa Mleta Rufaa na Mjibu Rufaa. 6. Kwamba, Mhe. Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, kituo jumuishi cha Mahakama amekosea kisheria na kimantiki kwa kutokutoa amri kwa mjibu rufaa kuhusu kutoa matunzo ya mtoto Goodluck Godgave kwa Tshs. 400,000 kila mwezi kama ambavyo mleta rufaa ameomba. 7. Kwamba, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama amek >sea kisheria na kimantiki kwa kutokutoa amri ya kwamba mjibu rufaa awajibike kutoa pesa kwa ajili ya matibabu e imu, mavazi kwa ajili ya mtoto. Usikilizwaji wa shauri hili uliendelea kwa utaratibu wa uwasilishaji hoja za maandishi. Pande zote mbili ziliwasilisha mawasilisho na kwa amri ya Mahakama wasilisho la nyongeza la mrufani lilipokelewa tarehe 16/12/2024, baada ya nyongeza ya muda kutolewa. Aidha hoja zote za maandishi zilizowasilishwa zimezingatiwa katika uamuzi huu. Wakati wa usikilizaji wa shauri hili pande zote ziliwakilishwa. Mleta rufaa alipata huduma ya msaada wa kisheria kutoka kwa wakili msomi Richard Godlisten Kimaro kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) na Mjibu rufaa aliwakilishwa na wakili msomi Leah Nixon Feruz. Akiwasilisha hoja za maandishi za kuunga mkono rufaa yake, Mleta rufaa aliwasilisha kama ifuatavyo: Akiwasilisha hoja ya 1, 2 na ya 3 kwa pamoja, Mleta rufaa alieleza kuwa, Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, amekosea kisheria na kimantiki kwa: a. kutotamka kuwa Mleta Rufaa na Mjibu Rufaa ni wanandoa halali na hivyo basi ingezingatia kuwa ndoa yao imevunjika katika hali isiyorekebishika tena na hivyo kutoa amri ya talaka. b. kutozingatia hoja ya Mleta Rufaa kuwa Mleta Rufaa na Mjibu Rufaa kabla ya kufunga ndoa wallishi chini ya Dhana ya Ndoa kania mke na mume kuanzia Mwaka 2006 mpaka 2009 c. kutamka kuwa Mjibu Rufaa na mwanamke anayeitwa Matrida David Mwaigwisa ni wanandoa wakati tayari kuna talaka baina yao na ndoa ilishavunjwa tangu tarehe 2/11/2022 huko Zanzibar na kielelezo cha Hati ya Kutengua Ndoa ambacho ni kielelezo 'B' kililetwa kama ushahidi, Mleta rufaa, aliwasilisha kuwa kifungu Na. 160 (1) na (2) cha Sneria ya Ndoa, Sura ya 29, Marejeo ya Mwaka 2019 kimeweka msingi wa kisheria wa masharti/vigezo vya dhana ya ndoa na haki zake, ambapo knampa haki mtu / watu ambao wamekidhi vigezo vya kukaa nyumba moja kama mume na mke, ambao pia hawana ndoa nyingine na ambao wameshi sio chini ya miaka miwili (2) kama mume na mke, hali ya kuaminika kuwa wanayo dhana ya doa hivyo wanastahili haki zote zinazotokana na dhana ya ndoa. Msingi huu umewekwa wazi kupitia shauri la JOHN KIRAKWE dhidi ya IDDI SIKO (1989) TLR 215 Mleta Rufaa kupitia hati yake ya madai aliieleza Mahakama kuwa kabla ya kufungwa kwa ndoa yao na Mjibu rufaa mnamo mwaka 2009, walikuwa wakiishi chini ya dhana ya ndoa kama mke na mume kuanzia mwaka 2006 mpaka Mwaka 2009. Baada ya kuishi kwenye dhana ya ndoa, waliweza kufunga ndoa yao tarehe 20-09-2009 katika kanisa la Romani Katoliki, lakini katika hali ya kushangaza, Mahakama ya Wilaya ya Temeke kupitia uamuzi ilieleza kuwa haitambui ndoa hii kwa sababu Mjibu Rufaa alishakuwa na ndoa nyingine tayari, hivyo ndoa ya Mleta Rufaa ni batili. Aidha, aliitaka itabue kuwa wakati shauri hili likiendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke Mjibu Rufaa aliweka pingamizi kuhusiana ra ndoa hii, ambapo Mleta Rufaa aliweza kutoa utetezi wa pingamizi hilo ambalo lilikosa mashiko kwani Mleta Rufaa aliwasilisha ya kuwa ndoa anayoisema kati ya Mjibu Rufaa na Mtu anayejiita MATRIDA DAVID ilishavunjwa tangu tarehe 7/11/2022 huko Zanzibar. Meta rufaa aliwasilisha kuwa katika Majibu yake ya nyongeza ya Majibu ya Talaka aliwewka kielelezo cha HATI YA KUTENGUA NDOA ambacho ni kielelezo 'B' ambacho kilithibitisha kuwa Serikali ya Wilaya ya Chake Chake Pemba imetengua Ndoa iliyofungwa tarehe 18/09/2021 Hati namba .00358908 katika Wilaya ya Kinondoni kati ya Ndugu GODGAVE LIPAWAGA na ndugu MATRIDA DAVID MWAIGWISA wa vitongoji Chake Chake na kwamba kuanzia leo tarehe 2/11/2022 si mtu na mke wake tena' Akihitimisha hoja hizi tatu za rufaa, Mleta rufaa aliwasilisha kuwa Mahakama ya Wilaya ya Temeke ilitakuwa itambue kuwa Mleta na Mjibu Rufaa walianza kuishi chini ya dhana ya ndoa, na kisha baadae kjfunga ndoa na hivyo basi ndoa ya Mleta rufaa na Mjibu rufaa ni rasmi na inatambulika na haikuwa sahihi kwa Mahakama ya Wilaya kusema kuwa Ndoa ya Mjibu Rufaa na Mleta Rufaa ni batili. Kuhusu sababu ya 4 na ya 5 ya rufaa, Mleta Rufaa aliziwasilisha sababu zote mbili kwa pamoja kwamba; Mheshimiwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke ya Kituo Jumuishi cha Mahakama amekosea kisheria na kimantiki kwa kushindwa; a. kutamka kuwa mali zifuatazo ni mali za ndoa na Mleta rufaa akiwa ni mke wa ndoa ana mchango wake kwenye mali hizo. Mali hizi za ndoa ni Nyumba Moja (1) ina vyumba 4, siting room na vyco vya nje na fensi, ipo eneo la Killiara Golani, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, fremu 5 za biashara, Vitanda 3 na magodoro 3, Makabati 3, Tank la Maji la lita 3000, sofa set 2, TV flat Screen 2, jiko la gesi na la umeme, Freezer, subwoofer 2, king'amuzi cha Azam FV na Gari aina ya Rav 4. b. kutoa amri ya mgawanyo wa mali za ndoa tajwa kwenye sababu ya rufaa na. 3 hapo juu kwa asilimia 50% kwa 50% kwa kuzingatia mchango wa Mleta Rufaa na Mjibu Rufaa. Mleta rufaa aliwasilis kuwa Mahakama katika suala la kuamua rrali za ndoa huongozwa na kifungu Na. 114 (2) (b) ya Sheria ya Ndoa, Sura ya 29, Marejeo ya Mwaka 2019 katika kujiridhisha juu ya mchango wa wanandoa kwenye kutafuta machumo na kuendeleza machumo hayo ya ndoa kwa pamoja. Alirejea ukurasa wa 2 aya ya 3 ya nakala ya hukumu ya Mahakama ambapo aliieleza Mahakama namna ambavyo alivyotoa Ushahidi wake kuhusiana na mali walizochuma hususani nyumba moja iliyoko Kimara Suka mtaa wa Golan ambayo walianza kuijenga kuanzia mwaka 2012 ambapo kiwanja kilinunuliwa mwaka 2011, gari aina ya RAV 4, vyombo vya ndani kuanzia Dar es Salaam hadi pemba. Akisisitizia hoja hii, Mleta rufaa alirejea misimamo ya kisheria iliyowekwa kwenye kesi za Gabriel Nimrod Kurwijila dhidi ya Theresia Hassani Malongo, Civil Appeal No. 102 of 2018 (tanzlii) na Yesse Mrisho dhidi ya Sania Abdul, Civil Appeal No. 147 of 2016 (Haijaripotiwa), ambapo Mahakama ilieleza kuwa: tafsiri ya mali ya chumo la ndoa kuwa ni mali iliyopatikana ndani ya ndoa au kabla ya ndoa na kuendelezwa kwenye ndoa na wadaawa wote au mmoja. Aidha, alirejea shauri la Bi. Hawa Mohamed dhidi ya Ally Seif [3 9831 TLR 32, ambapo Mahakama ilieleza kuwa ustawi wa familia ni sehemu muhimu ya shughuli za uchumi wa familia na hivyo ni sahihi kuchukua mchango wa mume au mke katika kustawishia familia kama mchango uliosaidia kupatikana kwa mali (au uchumi) wa familia. Meshauri mengineyo yaliyorejewa kusisitizia msimamo huu ni pamoja na Mariamu Tumbo dhidi ya Harold Tumbo [19831 TLR 293 na Gabriel N mrod Kurwijila vs Theresia Hassani Malongo, Civil appeal no. 102 of 2018 (unreported), Cleophas M. Malitabaro v Sophia Washusha, Civil Application No.13 2011 (Court of Appeal of Tanzania) Hivyo, kwa kuzingatia mashauri tajwa, mleta rufaa aliwasilisha kuwa Mahakama ya Wilaya ya Temeke ilikosea kwa kutozingatia uwepo wa mali hizo za ndoa ambazo Mleta Rufaa ana mchango wake na kitendo cha kusema kuwa hakukuwa na ndoa balna ya Mleta rufaa na Mjibu rufaa, kimeathiri haki na mchango wa Mleta Rufaa kupata asilimia yake 50 kwenye mali za ndoa tajwa hapo juu. Kuhusu sababu ya 5 na ya 6 ya Rufaa, Mleta Rufaa aliziwasilisha kwa pamoja, ambapo alieleza kuwa; Mheshimiwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama, amekosea kisheria na kimantiki kwa kutokutoa: a. amri kwa Mjibu Rufaa kuhusu kutoa matunzo ya mtoto Goodluck Godsave kwa Tshs. 400,000/kila mwezi kama ambavyo Mleta Rufaa ameomba b. amri ya kwamba Mjibu Rufaa awajibike kutoa pesa kwa ajili ya matibabu, elimu, mavazi kwa ajili ya mtoto. Mleta rufaa aliwasilisha kuwa sababu hizi za rufaa zina mashiko kwani uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke katika kipengele cha hjduma ya mtoto kina mapungufu na hivyo Mahakama Kuu ikiangalie kwa jicho la pekee katika kulinda ustawi wa mtoto GOODLUCK kwani kitendo cha Hakimu wa Mahakama ya Wilaya kutolizungumzia hili kwa kutokutaja kiwango cha pesa ni kuweka ustawi na maslahi ya mtoto mastakani. Alirejea kifungu cha Sheria cha 129(1) cha Sheria ya Ndoa, Sura ya 29, Marejeo ya Mwaka 2019 na kifungu Na. 4(2) na 37 (4) cha Sheria ya Mtoto Sura ya 13, Marejeo ya Mwaka 2019 vinavyoweka wajibu kwa baba kutunza mtoto na maslahi ya mtoto kuangaliwa katika kila jambo linalofanywa Aliwasilisha zaidi kuwa Mahakama ya Wilaya ilitakiwa kuzingatia kuwa Mjibu Rufaa ni mwajiriwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JVVTZ) , hivyo basi kwa mwezi Mjibu Rufaa anapata Mshahara parroja na marupuru mengine hivyo ana uwezo wa kumhudumia mtoto. Mahakeima ya Wilaya ya Temeke kutokutaja kiwango cha pesa cha matunzo ni kuweka hatarini suala ya matunzo ya mtoto. Hakimu alitakiwa kutaja kiwango cha pesa ya matunzo kwa kuongozwa na vifungu vifungu vya 44(b) na 44(d) vya Sheria ya Mtoto, Sura ya 29, Marejeo ya Mwaka 2019, ambavyo vimesitiza kuwa kabla ya kutoa amri ya kutunza mtoto basi Mahakama iangalie uwezo wa mtoaji pamoja na gharama za maisha za maeneo husika. Aidha, aliwasillisha kuwa Mahakama ya Wilaya haikuwashirikisha ustawi wa jamii katika suala hili la matunzo ya watoto kwa mujibu wa Kifungu No. 45 (1) na (2) cha Sheria ya Mtoto, Sura ya 13, Marejeo ya Mwaka 2019. Akihitimisha hoja hii, Mleta rufaa aliiomba Mahakama iyaangalie upya maamuzi ya Mahakama ya wilaya katika kipengele cha matunzo kwakuwa kiwango cha pesa cha matunzo kwa mwezi kilipaswa kutajwa kwa kuangalia kipato cha Mjibu Rufaa ili kurahisisha utekelezaji. Hivyo, aliomba rufaa yake ikubaliwe na Hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Wilaya ya Temeke, Kituo Jumuishi cha Mahakama katika Shauri la Ndoa Na. 107 la Mwaka 2023 Hukumu tarehe 21-12-2023 mbele ya Mheshimiwa Hakimu Mkazi M.X. Sanga ifutwe na itupiliwe Mbali na nafuu zhgine ambazo Mahakama hii tukufu ingeona inafaa kuzitoa. Akiwasilisha hoja za kupinga rufaa, Mjibu rufaa alieleza kama ifuatavyo: Kuhusiana na sababu ya kwanza ya rufaa, Mjibu rufaa alieleza kuwa ni dhahiri kuwa Mleta Rufaa si mke wa ndoa wa Mjibu Rufaa na hana ushahidi wowote kuthibitisha kuwa yeye ni mke halali wa Mjibu Rufaa. Alirejea kifungu cha 99 cha Sheria ya Ndoa Toleo la 2019 sura namba 29, amoacho kinawapa haki wanandoa kufungua madai ya talaka pale ndoa itakapofikia kwenye migogoro isiyoweza kusuluhishwa au kurekebishika. Mjibu rufaa aliwasilisha kuwa Mjibu Rufaa hajawahi kuoa mke wa pili kama sheria inavyokataza, kwa kuthibitisha hoja hii Mjibu Rufaa katika ushahidi wake aliithibitishia Mahakama kupitia cheti cha ndoa namba 00358908 (kielelezo P7) kilichotolewa na Mleta Rufaa (SMI) mwenyewe katika ushahidi wake ambacho kinaonyesha ndoa iliyofungwa kati ya Mjibu Rufaa (Godgave Lipawaga) na Matrida David katika Kanisa la Katoliki Parokia ya Maria Mtakatifu - Kimara na si kati ya Mleta Rufaa na Mjibu Rufaa jambo ambalo alieleza lina dosari kisheria. Pia, wakati Mleta Rufaa (SMI) anatoa Ushahidi wake alieleza kuwa Mjibu Rufaa ni mume wake kwa nooa ya kimila ambapo walioana tangu mwaka 2009 huko morogoro, Mleta Rufaa alipopewa nafasi ya kutoa vielelezo vyake alitoa cheti cha ndoa (kielelezo P7) chenye majina ya Mjibu Rufaa na Matrida David cha mwaka 2001 akithibitisha ndoa ya kikristo na si ya kimila na kwa cheti kisicho chake kama alivyoshuhudia Mahakamani kuwa mwaka 2009 aliolewa na Mjibu Rufaa kimila jambo ambalo aliidanganya Mahakama. Mjibu rufaa al rejea Kifungu cha 9(2) cha Sheria ya Ndoa akieleza kuwa Ndoa ya mke rr moja ni siyo ndoa ya wake wengi na kwamba Mjibu rufaa ameshindwa kuithibitishia Mahakama kuwa aliwahi kufunga ndoa na mjibu rufaa kwa kuwa Mleta Rufaa alikiri Mahakamani kuwa ndoa yake ilifungwa rrwaka 2009 ukilinganisha ndoa kati ya Mjibu Rufaa na Matrida David ilifungwa mwaka 2001, hivyo basi ndoa ya Mleta Rufaa kama anavycjaribu kuishawishi Mahakama ndoa hiyo haijawahi kutokea, hairuhusiwi na haitambuliki katika misingi ya kisheria. Mjibu rufaa aliiomba Mahakama ipuuzie sababu hii ya Mleta Rufaa. Akiwasilisha kuhusu sababu ya pili ya rufaa, Mjibu rufaa alieleza kuwa katika kesi hii sheria haimpi haki Mleta Rufaa kuegemea katika Dhena ya ndoa (Presumption of Marriage) ukizingatia kuna ndoa halali iliyofungwa toka mwaka 2001 kati ya Mjibu Rufaa na Matrida Da/id na haikuwahi kuvunjwa. Iko wazi katika kifungu namba 160 (1) na (2) cha Sheria ya Ndoa 2019 kuwa, kifungu hiki kililenga kutumika kwa watu ambao hawakuwahi kuoana kabisa lakini wameishi pamoja kwa muda usiopungua miaka miwili kama mume na mke na si kama Mleta Rufaa aliyeingia katika ndoa ya Mjibu Rufaa na Matrida David. Mjibu alire ea pia kifungu cha 15(4) cha sheria ya ndoa kinachokataza wanandoa kjfunga au kuingia kwenye ndoa nyingine wakati wameoana. Mjibu rufaa alirejea pia kesi ya Yohanne Amani Lyewe v. Theodory M vaya Rufaa ya Madai Na. 22, 2017 kusisitizia hoja hii. Ni uelewa wa Mjibu Rufaa kwamba, kwakuwa Mleta Rufaa aliishi na Mjibu Rufaa toka mwaka 2009 kipindi ambacho Mjibu Rufaa alikuwa ana ndoa yake halali iliyofungwa kati yake na Matrida David mwaka 2001, kwa misingi hiyo dhana ya ndoa haiwezi kutumika kwa Mleta Rufaa kama kigezo cha kumhalalisha Mleta Rufaa awe mke wa ndoa wa Mjibu Rufaa ukizingatia kuna ndoa halali kati ya Mjibu Rufaa na Matrida David ambayo pia haijavunjwa. Hivyo ni maombi ya Mjibu Rufaa kuwa Mahakama isikubaliane na hoja ya Mleta Rufaa kwamba Mleta Rufaa na Mjibu Rufaa ni wanandoa kwasababu waliishi katika dhana ya ndoa jambo ambalo si sahihi na haliruhusiwi kisheria. Kuhusiana na sababu ya tatu ya rufaa, Mjibu rufaa alieleza kuwa Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya ndoa ya Mwaka 2019 kinakataza ndoa yoyote iliyofungwa kikristo kanisani kubadilishwa kutoka kuoa mke mmoja na kuoa wake wengi. Kwa kifungu hicho, Mjibu Rufaa hajawahi kuvunja sheria kwa kufunga ndoa nyingine wala kuitengua ndoa yake kwasababu anatambua yeye kama mkristo haruhusiwi kufunga ndoa nyingine haci kifo kitakapowatenganisha. Mjibu rufaa aliwasilisha zaidi kuwa ni kweli Mahakama ndiyo yenye jukumu au mamlaka ya kuvunja ndoa kama ilivyoandikwa katika kifungu namba 110 (a) cha sheria ya Ndoa Hata hivyo, ndoa iliyofungwa kati ya Mjibu Rufaa na Matrida David haijawahi kuvunjwa na Mahakama za (Tanzania) tangu ilipofungwa mwaka 2001 katika Kanisa la Katoliki lililopo Kimara Dar es Salaam, *Xidha aliwasilisha kuwa Mleta Rufaa katika ushahidi wake aliwasilisha kielelezo P7 Mahakamani ambacho ni Hati ya Kutengua ndoa ikiwa ni ya kigushi (forged) kwasababu zifuatazo; Moja, Kielelezo hicho kilionyesha ndoa kati ya Mjibu Rufaa na Matrida David imetenguliwa na serikali ya Wilaya ya chake chake na sio Mahakamani Dar es Salaam mahali ndoa ilipofungwa.Pili, kielelezo hicho kinaonyesha ndoa ilifungwa tarehe 18/09/2021 na sio mwaka 2001 kama Mleta Rufaa alivyotoa kielelezo chake na ushahidi wake Mahakamani. Tatu, Kielelezo hicho hakikuwa na sahihi ya Matrida David ambaye ndiye mke halali wa Mjibu Rufaa jambo ambalo linatia shaka ya uhalali wa kielelezo hicho kilichotolewa Mahakamani na Mleta Rufaa akidai ndoa kati ya Mjibu Madai na Mleta Rufaa imetenguliwa. Mwisho, Mleta Rufaa (SMI) wakati akitoa ushahidi wake Mahakamani alikiri kuwa kielelezo "P7" (Hati ya kutengua ndoa na cheti cha ndoa) alichokileta Mahakamani kilikuwa ni cha kugushi alipoulizwa maswali na wakili wa Mjibu Rufaa. Kutokana na sababu hizo, Mjibu rufaa Mjibu rufaa aliomba Mahakama isiweke uzito kwenye Kielelezo P7 kilichotolewa kama Ushahidi na Mleta rufaa kwa kuwa Mleta Rufaa aliidanganya Mahakama kwakuleta Hati ya Kutengua Ndoa (kielelezo P7) ambayo imegushiwa. Kuhusiana na sababu ya 4 na 5 ya rufaa, Mjibu Maombi aliwasilisha kuwa Kifungu cha 114 (1) cha Sheria ya Ndoa kinaweka utaratibu wa kugawa mali za wanandoa baada ya kutoa amri ya kuvunja ndoa au kutoa amri ya mauzo ya mali na magawanyo ya mapato Ni mtizamo wa mjibu rufaa kuwa kifungu hicho kinawahusu wanandoa pekee na si vinginevyo, kwakuwa Mjibu Rufaa hakuwahi kufunga nd Da na Mleta Rufaa hivyo basi Mleta Rufaa hastahili kupata mgawanyo wa mali kwasababu Mleta Rufaa hakuithibitishia Mahakama uhalali wa yeye kuwa mke halali wa Mjibu Rufaa isipokuwa Mleta Rufaa alijaribu kuidanzjanya Mahakama kwa kutoa vielelezo (P7) visivyo sahihi/vya uongo, hivyo basi Mjibu Rufaa anaiomba Mahakama isikubaliane na hoja ya Mleta Rufaa kuhusu mgawanyo wa mali ukizingatia Mleta Rufaa na Mjibu Rufaa sio wanandoa. Akiwasilisha kwenye hoja ya 6 na 7 ya rufaa, Mjibu rufaa alieleza kuwa Iko wazi katika kifungu cha 129 cha sheria ya ndoa kinachosema Mjibu Rufaa anatakiwa kuwa na wajibu wa matunzo kwa watoto wake aliowazaa na si vinginevyo, kutokana na kielelezo D2 ambayo ni (Ripoti ya utaca wa uhalali wa wazazi kwa mtoto / Parentage Test Report - DNA Profiling) kilichotolewa Mahakamani na Mjibu Rufaa kinatosha kuth bitisha kuwa Goodluck hakuwa mtoto wa Mjibu Rufaa jambo lililowekwa wazi katika kielelezo hiki, hivyo basi madai ya matunzo ya mtoto aayana mashiko na Mleta Rufaa hastahili kudai matunzo ya mtoto dhidi ya Mjibu Rufaa. Mjibu Rufaa aliomba Rufaa hii itupiliwe mbali kwa gharama. Akiwasilisha hoja za nyongeza Mleta rufaa alisisitizia hoja zake za msingi. Kwa ajili ya kuepeuka kurudia kuandika hoja zilezile sitazirudia hoja hizo ila zitazingatiwa kikamilifu katika uchambuzi wa maamuzi haya. Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, swali la msingi arribalo Mahakama hii imejiuliza ni endapo, rufaa hii ina msingi. Katika kushughulikia rufaa hii, Mahakama imejiongoza katika misingi ifuatayo - Moja, Mahakama hii ikiwa ni ya kwanza ya rufaa inayo mamlaka na uwezo wa kutathimini ushahidi uliotolewa kwenye Mahakama iliyosikiliza shauri na kufikia uamuzi wa haki, rejea shauri la: Kaimu said vs. Republic, Criminal Appeal no 391 of 2019, Hassan Mohammed Mfaume vs Republic (1981) TLR 167, Rashid Abiki Nguwa vs Ramadhani Hassan Kuteya and another, Civil Appeal No. 421 of 2021 na Malkit Singh Bansal vs Harbansa Kaur Bansal civil appeal no. 000020211 of 2024 HCT Temeke Pili, ni wajibu wa mleta shauri mahakamani kuthibitisha shauri lake kwa mujibu wa kifungu cha 110 cha Sheria ya Ushahidi na upande wenye ushahidi mzito ndio unaoshinda kesi. Tatu, Mahakama inayo uwezo wa kusikiliza hoja moja moja za rufaa au kuziunganisha ili mradi hoja zote zijibiwe; Kuhusiana na sababu ya kwanza na ya pili ya rufaa, mleta rufaa amewasilisha kuwa Mahakama ya Wilaya ya Temeke imekosea kisheria na kimantiki kwa kutotamka kuwa mleta rufaa na mjibu rufaa ni warandoa halali na hivyo basi ingezingatia kwa ndoa yao imevunjika katika hali isiyorekebishika tena na hivyo kutoa amri ya talaka. Vilevile mletci rufaa amewasilisha kuwa mleta rufaa na mjibu rufaa kabla ya kufunga ndoa waliishi chini ya dhana ya ndoa kama mke na mume kuanzia 2006 mpaka 2009 upande wa mjibu rufaa umepinga hoja hizi kwa kuwasilisha kuwa mleta rufaa si mke wa ndoa wa mjibu rufaa na dhana ya ndoa haiwezi kutumika kwake kama anavyodai kwani mjibu rufaa ana mke arrbaye alimuoa kabla ya kuwa na mahusiano na mleta rufaa. Katika kushughulikia hoja hizi niimepitia sheria ya ndoa ya 1973 na kuona kuwa, Sheria ya Ndoa Sura ya 29 Toleo la 2019 inaainisha aina tatu za ufungaji ndoa chini ya kifungu cha 25 cha Sheria ya Ndoa, yaani; ndoa za kidini (civil), ndoa za kiislamu na kimila. Aidha kifungu cha 9 (1) kimetoa tafsiri ya ndoa kuwa ni muungano wa hiyari baina yam me na mke unaotarajiwa kudumu katika kipindi cha Maisha yao. Na kifungu ha 9 (2) kimeweka msisitizo kuwa ndoa ya mme mmoja na mke mmoja haiwezi kwa ndoa ya wake wengi vilevile sheria hii katika kifungu cha 160 limeweka dhana ya ndoa pale inapotokea kwa mwananrke na mwanaume wamekaa pamoja kama mke na mume kwa kipindi kisichopungua miaka miwili. Katika rufaa hii mleta rufaa ameeleza kuwa alikuwa mke wa mjibu rufaa tangu kipindi cha 2006 hadi 2009 walipokaa pamoja na kupitia hukumu ya Mahakama ya Wilaya imeelezwa kuwa, Mleta rufaa alifunga ndoa ya kimila na Mjibu rufaa na aliwasilisha Mahakamani cheti cha ndoa. Baada ya kupitia rekodi ya shauri hili, Mahakama imegundua kuwa, ni ukweli usiopingika kuwa mleta rufaa na mjibu rufaa waliwahi kuishi pamoja Zanzibar hata hivyo katika mawasilisho yake na wakati wa kutoa ushahidi, mleta rufaa alieleza Mahakama kwa aliwahi kufunga ndoa na Mjibu rufaa na aliwasilisha cheti cha ndoa ambacho kina majina ya mjibu rufaa na mwanamke mwingine aitwaye Matrida David Mwaigisa, akidai kuwa waliachana kwenye ndoa yao ambapo aliwasilisha Hati ya kutengua ndoa iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katika kupitia rekodi ya Mahakama ya Wilaya na kufanya uchambuzi wake, Mahakama imeona kuwa, Bi Matrida David Mwaigisa alitoa ushahidi wake Mahakamani kama SU2 akiunga mkono upande wa Mjibu rufaa kwa kupinga vikali hoja ya yeye na mjibu rufaa kuachana na alieleza kuwa walioana kama m<e na mume mwaka 2001 kwa ndoa ya kikristo katika Kanisa Katoliki la Mwenge na kwamba vyeti hivyo viliwasilishwa kwa mwajiri wake hata hivyo mwaka 2014 yeye na Mjibu rufaa walikosa kuelewana akaamua kwenda kujipumzisha kwao, isipokuwa hawajawahi kuachana kwa talaka Mahakamani. Ushahidi huu wa Bi Matrida ulithibitishwa na ushah di wa Mjibu rufaa. Mahakama imeona kuwa hakuna shahidi yeyote wa Mleta rufaa aliyepinga ushahidi huu wa Mleta rufaa. Aidha, ushahidi wa Mleta rufaa wa kuhusiana na ndoa baina ya Mjibu rufaa na Bi Matrida kutenguliwa na Hati ya kutengua ndoa iliyotolewa na Taasisi ya Serikali ya Mapinduzi, haukutolewa au kuthibitishwa na shahidi yeyote kutoka Taasisi husika iliyotoa Hati ya kutengua ndoa na hivyo unabaki kuwa ni ushahidi hafifu na kinachobaki kusimama ni ndoa ya kikristo bcina ya Mjibu rufaa na Bi. Matrida ambaye walifunga nae ndoa husika. Kwa mujibu wa Kifungu cha 10(b) cha Sheria ya Ndoa ya kikristo ni ndoa ya mke mmoja na kwa mujibu wa kifungu cha cha 15 (I) cha sheria hiyo, hakuna mwanaume anayeruhusiwa kuoa akiwa kwenye ndoa ya mke mmoja. Hivyo hoja ya kwamba kumekuwa na ndoa baina ya Bi Recho, Mleta rufaa na Mjibu rufaa haina mashiko, kwakuwa ndoa ya awali iliyofungwa baina ya Mjibu rufaa na Bi Matrida ni ndoa ya mke mmcja na haijawahi kutenguliwa na hivyo bado ipo hai. Pili hoja ya kufungwa kwa ndoa ya kimila hata kama ingeweza kuthibitishwa haiwezi kusimama endapo tayari kulikuwa na ndoa ya kikristo baina ya Mjibu rufaa na Bi Matrida iliyofungwa tangu mwaka 2001 na haijawahi kuvunjwa. Aidha kwa mujibu wa rekodi na Ushahidi, Mleta rufaa hakuweza kuthibitishia Mahakama kuwa yeye ni mke halali wa mjibu wa rufaa na Mjibu rufaa ameweza kuthibitishia Mahakama kuwa hajawah kuoa mke wa pili kama sheria inavyokataza na katika ushahidi wake alithibitishia Mahakama kupitia cheti cha ndoa namba 00358908 (kielelezo P7) kilichotolewa na Mleta rufaa (SMI) mwenyewe katika ushahidi wake ambacho kinaonesha ndoa iliyofungwa kati ya mjibu rufaa Gcdgave Lipawaga na Bi Matrida David katika Kanisa Katoliki Parokia ya Maria Mtakatifu Kimara na si ushahidi wa ndoa kati ya Mleta rufaa na mjibu rufaa. Ninakubaliana na hoja za mjibu rufaa kwa mujibu wa kifungu 9(2) cha Sheria ya Ndoa sura ya 29 Marejeo 2019 kuwa: A monogamous marriage is a union between one man and one woman to the exclusion of all others. Kwamba ndoa ya mke mmoja ni muungano kati ya mwanaume na mwanamke mmoja tu haihusishi watu wengine. Kwakuwa ndoa ya mjibu rufaa ilikuwa ni ya kikristo ilikuwa ni ya mke mmoja na ilifungwa mwaka 2001 na haijawahi kutenguliwa na Mahakama yeyote. Hoja ya uwepo wa ndoa baina ya mleta rufaa na mjibu rufaa iliyofungwa 2009 ni hoja isiyo na msingi na ndoa hiyo haijawahi kutokea na haitambuliki kisheria au katika misingi ya kisheria. Hivyo, baada ya uchambuzi wangu ninakubaliana na msimamo wa Mahakama ya Wilaya kwenye eneo hili na ninakubaliana na kesi ya Paschal Simon Maginga (1978) LRT kwamba mkristu ambaye hajaacha imani yake au kutaliki mke wake wa ndoa anakosa uwezo wa kuoa mke mwingine. Rejea pia shauri la Yohanne Amani Lyewe dhidi ya Theodory Mwaya rufaa ya madai Na. 22 ya mwaka 2017. Kwakuwa kwa mujibu wa hoja ya kwanza ya rufaa, Mahakama hii ineona kuwa hakukuwa na ndoa yoyote baina ya Mleta rufaa na Mjibu rufaei, basi Mahakama inaona kwamba hakukuwa na ndoa yoyote mbele yake ya kuivunja na inakubaliana na Mahakama ya Wilaya kwenye eneo hi i kwa kutokutoa talaka. Hivyo hoja hii ya kwanza ya rufaa inashindwa. Kuhusiana na hoja ya pili ya rufaa kwamba; Mahakama ya Wile ya ya Temeke ilikosea kisheria na kimantiki kwa kutokuzingatia hoja ya Mleta rufaa kuwa Mleta rufaa na Mjibu rufaa kabla ya kufunga ndoa waliishi chini ya dhana ya ndoa kama Mke na Mume kuanzia mwaka 2006 mpaka 2009. Kifungu cha 160 cha sheria ya ndoa kinatoa au kuweka utaratibu wa dhana ya uwepo wa ndoa inapothibitika kuwa mwanaume na mwanamke wameishi pamoja kwenye mazingira ya kupewa hadhi ya mke na mime na hivyo kuchukuliwa kama mke na mume. Nikirudi kwenye kesi iliyopo mbele ya Mahakama hii, mleta rufaa ameeleza kuwa aliishi na mjibu rufaa kama mke na mume kuanzia mwaka 2006 hadi 2009, kabla ya kufungwa kwa ndoa yao mwaka 2009 na alirejea shauri la John Kirakwe dhidi ya Iddi Siko (1989) TLR 215. Hoja hii ya mleta rufaa imepingwa vikali na mjibu rufaa kwa maelezo kwamba dhana ya ndoa haiwezi kutumika katika mazingira ya shauri hili ambapo tayari kulikuwa na ndoa ambayo haijavunjwa. Baada ya kupitia rekodi zinazohusiana na rufaa hii, sheria na Ushahidi, ninakubaliana na hoja za Mjibu rufaa kuwa kwa kuwa kuna ndoa halali ambayo ilifungwa baina ya mjibu rufaa na bi Matrida (SU2) na haiiawahi kuvunjwa na Mahakama, hivyo dhana ya ndoa chini ya kifungu cha 160 cha Sheria ya ndoa haiwezi kutumika kwa upande wa Mleta rufaa na Mjibu rufaa. Kifungu hiki kililenga kutumika kwa watu ambao hawakuwahi kuoana kabisa lakini wameishi pamoja kwa muda usiopungua miaka miwili kama mme na mke na si kama wapenzi au kwa namna ambayo Mleta rufaa aliingia katika ndoa ya Mjibu rufaa na Bi Matrida David (SU2). Hivyo, ninakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Wilaya kwamba chini ya kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Ndoa, mwanaume aliye katika ndoa ya mke mmoja ambayo haijavunjwa hataweza kuoa au kuingia kwenye ndoa ny ngine. uamuzi huu pia ulielezwa katika kesi ya Yohanne Amani Lyeme dhidi ya Theodory Mwaya ambapo Mahakama ilieleza kuwa katika mazingira hayo, dhana ya ndoa haiwezi kutumika. Pia katika kesi ya Francis Leo vs. Paschal Simon Maganga (1978) LRT Mahakama Kuu ilieleza kuwa Mkristu ambaye hajaacha imani yake au kutoa talaka kwa mkewe hana uwezo wa kuoa mwanamke mwingine na hivyo hawezi kutumia dhana ya ndoa chini ya kifungu cha 160 cha sheria ya ndoa. Hivyo ninakubaliana na Mjibu rufaa na Mahakama ya Wilaya kuwa kwakuwa Mleta rufaa aliishi na Mjibu rufaa toka mwaka 2006 hadi 2009 kipindi ambacho mjibu rufaa alikuwa na ndoa yake halali iliyofungwa kati yake na Bi Matrida David (SU2) mwaka 2001, katika misingi hiyo dhana ya ndoa haiwezi kutumika kwa Mleta rufaa kama kigezo cha kumuhalalisha Mleta rufaa kuwa mke wa ndoa wa Mjibu rufaa. Pili katika mazingira hayo, Melta rufaa atabakia kuwa alikuwa ni mpenzi wa Mjibu rufaa. Mahakama ya Wilaya ambayo ninakubaliana nayo kwenye uamuzi wake, ikirejea shauri la Anthony Isidori Ndongo dhidi ya Tundondeshe Nasoni Mwakijuna rufaa ya ndoa na 10/2020 imeeleza katika kesi hiyo kuwa: Mahakama inapojiridhisha kwamba pande za kesi hazikuwa na uwezo wa kuoa basi dhana ya ndoa haiwezi kusimama kwa upande wao haijalishi wameishi kwa muda mrefu kiasi gani. Hivyo kutokana na yaliyoelezwa hapo juu kwa mujibu wa sheria, ushahidi na hoja za pande zote za kesi, Mahakama inaona kuwa Mahakama ya Wilaya ilikuwa sahihi kutokubaliana na uwepo wa dhana ya ndoa baina ya Mleta rufaa na Mjibu rufaa na hivyo kutoa uamuzi kuwa hawakuwa wanandoa kisheria. Kuhusu sababu ya tatu ya rufaa, kwamba Mahakama ilikosea kisheria na kimantiki kwa kutamka kuwa mjibu rufaa na mwanamke aitwaye Matrida David Mwaigawisa ni wanandoa wakati tayari kuna talaka baina yao na ndoa ilishavunjwa tangu tarehe 2/11/2022 huko Zanzibar na kielelezo cha Hati ya Kutengua ndoa, kielelezo B kililetwa kama ushahidi. 1 «r Katika kushughulikia hoja hii nimepitia mwenendo na hukumu ya Mahakama ya Wilaya na kuona kuwa Mleta rufaa alitoa Cheti cha kutengua ndoa baina ya Mjibu rufaa na Bi Matrida David ambacho kilipokelewa kama kielelezo P7 nyaraka hiyo inaonesha kuwa ndoa ya Mjibu rufaa na Bi. Matrida ilivunjwa tangu tarehe 2/11/2022 Zanzibar na Serikali ya Wilaya ya Chake Chake Pemba na imetengua ndoa hiyo iliyofungwa tarehe 18/9/2021 kwa Hati Namba 0035908. Hoja hii pia imepingwa na Mjibu rufaa ambaye ameeleza kuwa ndoa husika haijawahi kuvunjwa na Mahakama tangu ilipofungwa mwaka 2001. Katika kushughulikia rufaa hii ninaongozwa na kifungu cha 110 (a) cha Sheria ya Ndoa ambayo kinaipa Mahakama jukumu au mamlaka ya kuvunja ndoa baada ya kujiridhisha na ushahidi wa pande zote za kesi. Aidha, ninakubaliana na hoja za Mleta rufaa kuwa kwa Mahakama ndiyo chombo kilichopewa mamlaka ya kuvunja ndoa kwa mujibu wa kifungu cha 110(a) cha Sheria ya ndoa. Hata hivyo, tofauti na tafsiri ya kifungu hiki, cheti kilichowasilishwa na Mleta rufaa kinaonesha ndoa hiyo ilivunjwa na Serikali ya Wilaya ya Chake Chake Pemba mnamo tarehe 2/11/2C22 na kuwa ndoa hiyo ilifungwa mnamo mwaka 2021. Maelezo haya yanatofautiana na ushahidi wa Mjibu rufaa na Bi Matrida (SU2) ambao walieleza mbele ya Mahakama kuwa ndoa yao ilifungwa mwaka 2001 na si 2021 na hawajawahi kuachana. Hivyo Hati ya kutengua ndoa inakinzana na ushahidi wa Mleta rufaa ulitolewa kwenye Mahakama ya Wilaya na kuacha mashaka mengi ya kuiwezesha Mahakama kukiamini cheti hicho na kukipa uzito katika hoja ya utenguzi wa ndoa husika baina ya Mjibu rufaa na Bi. Matrida. Aidha nimepitia pia mwenendo wa Mahakama ya Wilaya na ninakubaliana na mjibu rufaa kuwa, wakati mleta rufaa (SMI) akitoa ushahidi wake alikiri kuwa kielelezo P7 ambacho ni Hati ya kutengua ndoa na cheti cha ndoa, alicholeta yeye Mahakamani kilikuwa ni cha kugushi. Vilevile hakuna Afisa wa kutoka Ofisi ya Serikali ya Chake Chake Pemba aliyeitwa kuthibitisha uhalali wa Cheti/Hati cha utenguzi hata kama ingekuwa na mamlaka ya kutengua ndoa husika. Hivyo hoja hii ya tatu ya rufaa inashindwa kwa misingi hiyo. Kuhusu hoja ya 4 na ya 5 ambazo nitazishughulikia kwa pamoja, Mleta rufaa ameeleza kuwa Mahakama ya Wilaya ilikosea kisheria na kimantiki kwa kushindwa kutamka kuwa mali zifuatazo ni mali za ndoa na mleta rufaa akiwa ni mke wa ndoa ana mchango wake kwenye hizo mal yaani nyumba, fremu 5 za biashara, Vitanda 3, Magodoro 3, Makabati 3, Tenki la maji lita 3000, Sofa seti, TV flat screen, Jiko la Gesi na umeme, freezer, subwoofer 2, Kin'gamuzi cha Azam TV na gari aina ya Rav 4 na kwamba Mahakama ilikosea kisheria na kimantiki kwa kushindwa kutoa amri ya mgawanyo wa mali za ndoa tajwa kwa asilimia 50% kwa 50% kwa kuzingatia mchango wa mleta rufaa na mjibu rufaa. Akiwasilisha hoja hizo Mleta rufaa ameeleza kuwa Mahakama inapaswa kuzingatia kifungu cha 114 2(b) cha Sheria ya ndoa katika kugawa mali za wanandoa zilizopatikana katika ndoa, kwa kuzingatia mchango wa kila mwanandoa. Mleta rufaa alirejea pia shauri la Gabriel Nimrod Kuwijila dhidi ya Theresia Hassan Makungo, Civil appeal No. 102/2018 tanzilii, Yesse Mrisho dhidi ya Sania Abdul civil appeal no. 147/2016 (unreported), Bi hawa Mohamed dhidi ya Ally Seif (1983) TLR 32, Mariam Tumbo dhidi ya Harold Tumbo 19831 TLR 293. Mleta rufaa ameeleza kuwa kitendo cha kusema kuwa hakuna ndoa kimeathiri mchango wake wa kupata asilimia 50 kwenye mali za ndoa tajwa. Aidha, akipinga hoja hiyo, Mjibu rufaa amerejea kifungu cha 114 (1) cha Sheria ya Ndoa akieleza kuwa kinawahusu wanandoa pekee na si vinginevyo na hakiwezi kutumika kwenye kesi hii kwa kuwa mleta ru"'aa na mjibu rufaa hawakuwa wanandoa. Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, Mahakama inakubaliana kyvanza na pande zote mbili kuhusiana na tafsiri ya kifungu cha 114 cha Sheria ya Ndoa ambacho kinaipa mamlaka Mahakama kugawa mali za wanandoa baada ya kutoa amri ya talaka au utengano kwa kuzingatia vigezo tajwa kwenye kifungu husika, hususani mchango wa wanandoa katika machumo ya ndoa. Hata hivyo kwa kuzingatia hoja za Mjibu rufaa, ninakubaliana naye kuwa, kifungu hiki kinawahusu wanandoa ambao wametalikiana na siyo mahusiano ya kimapenzi yaliyokuwepo baina ya Mleta rufaa na mjibu rufaa ambayo Mahakama imethibitisha kuwa hayakuwa ni ndoei wala kuitwa au kurejewa kama ni ya dhana ya ndoa. Pia ninakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Wilaya kuwa kwakuwa hawakuwa wanandoa basi hawakuchuma mali pamoja kama wanandoa na hivyo suala la upatikanaji au umiliki wa mali linapaswa liangaliwe katika muktadha wa sheria nyinginezo husika. Hivyo hakuna amri ambayo Mahakama ya Wilaya ingeweza kutoa ya mgawo wa asilimia 50 kwa 50 baina yao au asilimia yeyote ile na katika misingi hii ninakubaliana na Mahakama ya Wilaya kuwa Mleta rufaa anaweza endapo akitaka kudai mali zake kwenye shauri la kawaida la madai. Rejea kesi ya Coi. Vs. Grace Crispian rufaa ya madai no. 3/2021 iliyorejewa kwenye hukumu ya Mahakama ya Wilaya. Kuhusu hoja ya sita na ya saba ya rufaa, mleta rufaa ameeleza kuwa Mahakama ya Wilaya imekosea kisheria na kimantiki kwa kutokutoa anri ya Mjibu rufaa kuhusu kutoa matunzo ya mtoto Goodluck Godgave ya shilingi 400,000 kila mwezi kama ambavyo Mleta rufaa ameomba na pia Mjibu rufaa awajibike kutoa pesa ya matibabu, elimu, mavazi, kwa ajili ya Mtoto. Mleta rufaa akiunga mkono hoja zake amerejea kifungu cha 129 (1) cha Sheria ya Ndoa akieleza kuwa mjibu rufaa ana wajibu wa kutunza mtoto hivyo Mahakama ya Wilaya ilipaswa kutaja viwango vya pesa ya matunzo kwa mujibu wa kifungu cha 41(2) na 37 (4) cha Sheria ya Mtoto sura ya 13 Toleo la Mwaka 2019 pamoja na Vifungu 44 (b) na 44 (d) vya Sheria ya Mtoto kwakuwa baba ni mwajiriwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na ana kipato cha mshahara na marupurupu. Pia Mleta rufaa amerejea kifungu cha 45 (1) na (2) cha Sheria ya Mtoto akieleza kuwa Mahakama ilipaswa kuwashirikisha ustawi wa jamii katika sjala la matunzo ya mtoto hivyo suala la matunzo liangaliwe upya. Akijibu hoja za kupinga rufaa mjibu rufaa amerejea kifungu cha 129(1) cha sheria ya ndoa akikitafsiri kuwa kinahusu wajibu wa mwanaurre kwa Watoto aliowazaa na si vinginevyo na kwamba kwa mujibu wa kielelezo D2 ambayo ni ripoti ya utata wa uhalali wa wazazi kwa mtoto/ parentage Test Report DNA profiling, kimethibitisha kuwa Goodluck hakuwa mtoto wa mjibu rufaa hivyo mleta rufaa hastaili kudai matunzo ya mtoto dhidi ya Mjibu rufaa. Katika kushughulikia hoja hii nimeipitia rekodi za Mahakama ya Wilaya na kuona kuwa ilikataa hoja hii ya matunzo ya mtoto kwakuwa suala h Io lipo katika mamlaka ya Mahakama ya Watoto (Juvenile Court), hivyo Mahakama hiyo ilifungwa mikono kuamulia jambo hilo. Lakini pia Mahakama haikutolea uamuzi juu ya utata wa mzazi wa mtoto (parentage) kwakuwa kwa mujibu wa kifungu cha 35 cha Sheria ya Mtoto sura ya 13 RE 2019 na kifungu cha 98(1), mamlaka hiyo ipo kwenye Mahakama ya Watoto. Kwakuwa Mahakama hii na Mahakama za Wilaya zote zimeona kuwa hakukuwa na ndoa baina ya mleta rufaa na mjibu rufaa basi suala la matunzo ya mtoto haliwezi kuletwa chini cha kifungu cha 129 cha Sieria ya ndoa ambayo inasimamia masuala yote na nafuu zote zitokanazo na masuala ya ndoa au dhana ya ndoa. Kwa muktadha huu ninakubaliana na Mahakama ya Wilaya kuwa suala hili linaangukia kwenye mamlaka ya Mahakama ya Watoto pamoja na masuala mengineyo ya mazazi ambayo mleta rufaa mwenyewe hajayawasilisha katika Mahakama hii, licha ya kuwa yalijadiliwa na Mahakama ya Wilaya, na kama ambavyo yameibuliwa na Mjibu rufaa, kwa kadri ambavyo mleta rufaa yeye mwenyewe ataona inafaa. Kwa kuzingatia hoja za pande zote za kesi, sheria na ushahidi kama ulivyorekodiwa kwenye mwenendo wa Mahakama ya Wilaya, Mahakama hii inaona kuwa Mleta rufaa ameshindwa kuthibitisha hoja zake za rufaa kwa mujibu wa Kifungu cha 110 cha Sheria ya Ushahidi hivyo hoja zote za rufaa I ‘ * zinakataliwa kwa kukosa mashiko na Hukumu ya Mahakama ya Wilaya inathibitishwa na rufaa hii inatupiliwa mbali kwa ujumla wake. Kila upande ubebe gharama zake. Imeamriwa hivyo. Haki ya rufaa imeelezwa kikamilifu. Imetolewa Temeke Leo Tarehe 30 Disemba 2024 S.D. MWAIPOPO JAJI 30/12/2024