shukrani makwasa bwile vs kings secondary school 2023 tzhcld 1489 15 november 2023
- Citation
- shukrani makwasa bwile vs kings secondary school 2023 tzhcld 1489 15 november 2023
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 15 November 2023
- Posture
- Labour Revision / Judgment
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 15 November 2023
- Posture
- Labour Revision / Judgment
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
The applicant failed to provide sufficient and credible evidence to justify the delay in filing the labour dispute, as the death certificate alone did not establish the necessary relationship or causation, and the arbitrator had jurisdiction to determine the application for extension of time.
Court disposition
Application dismissed
Orders
- The application for revision is dismissed.
- Each party to bear its own costs.
02
Material facts
Parties
Shukrani Makwasa Bwile
Applicant Counsel: Nehemia MungaKings Secondary School
Respondent Counsel: Lembris GodsonAmounts and remedies
- Days of Delay in Filing Dispute: 30
03
Procedural history
Posture
Labour Revision / Judgment
04
Questions and positions
Legal issues
- 01
Whether the applicant provided sufficient cause for delay in filing the labour dispute
- 02
Whether the arbitrator had jurisdiction to determine the application for extension of time
Party arguments
- Applicant
- The applicant argued that the arbitrator erred in law by failing to consider the evidence presented, specifically the death certificate of his aunt who was his guardian, as the reason for delay. He also contended that the arbitrator lacked jurisdiction to determine the application for extension of time, and that the arbitrator wrongly disregarded the role of his guardian in his life.
- Respondent
- The respondent argued that the arbitrator did not err in law, as the death certificate only proved the death of the applicant's aunt and did not establish her as his guardian or that her illness and death prevented timely filing. The respondent further argued that the applicant failed to provide sufficient evidence for each day of delay and that the arbitrator had proper jurisdiction to determine the application for extension of time.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Kanuni ya 31 ya Sheria ya Taasisi za Kazi (Usuluhishi na Uamuzi), T.S. Na. 64/2004; Daudi Haga v. Jenitha Abdan Machanju, Madai ya Masahisho No. 19 of 2006
Extension of time may be granted where sufficient cause for delay is established, and the applicant must account for each day of delay.
- 02
Kanuni ya 15 ya Sheria ya Taasisi za Kazi (Usuluhishi na Uamuzi), T.S. Na. 64/2004; Koba Said Mdoe v R & K Trucking Co. Limited, Labour Revision No. 410 OF 2022
The arbitrator has jurisdiction to determine applications for extension of time under the relevant labour laws.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
The applicant failed to provide sufficient and credible evidence to justify the delay in filing the labour dispute, as the death certificate alone did not establish the necessary relationship or causation, and the arbitrator had jurisdiction to determine the application for extension of time.
Obiter and limits
- There is conflicting High Court authority on the interpretation of the Court of Appeal decision regarding the arbitrator's jurisdiction, but the prevailing view is that the arbitrator retains such jurisdiction.
Court disposition
Application dismissed
- The application for revision is dismissed.
- Each party to bear its own costs.
Source and reliance status
TANZLII · 15 November 2023
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 15 November 2023
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA
DIVISHENI YA KAZI
DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 231/2023 (Marejeo yanatokana na uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya DSM i/iyoketi Ubungo Tarehe 24 August 2023 katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/UBG/53/2023
BAINA YA SHUKRANI MAKWASA BWILE............................MLETA MAOMBI NA KINGS SECONDARY SCHOOL............................. MJIBU MAOMBI
HUKUMU Tarehe ya mwisho ya Amri: 07/11/23 Tarehe ya Hukumu: 15/11/2023 OPIYO, J Shauri hili la marejeo limefunguliwa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/UBG/53/2023. Ndugu Shukrani Makwasa Bwile ambaye ni Mleta maombi anayeimba Mahakama itoe amri ya kurejea na kisha kutengua uamuzi wenye usajili Na. CMA/DSM/UBG/53/2023 ambao ulitolewa na Tume tarehe 24/8/2023 na Mh. Mvungi-Msuluhishi na amri nyingine yoyote itakayoona inafaa. i Historia fupi ya shauri hili ni kwamba mleta maombi aliwasilisha maombi ya nyongeza ya muda ili mgogoro mama wa kikazi uweze kusikilizwa nje ya muda. Mahusiano ya kiajira yalikoma tarehe 24/03/2023 baada ya mwajiri kusitisha ajira ya mwombaji kwa madai ya utovu wa nidhamu (uzembe). Hata hivyo mgogoro huu uliwasilishwa mbele ya tume tarehe 05/06/2023. Maombi haya baada ya kuwasilishwa mbele ya msuluhishi yaliyatupiliwa mbali kwa mwombaji kukosa sababu ya msingi ya kuchelewa kuleta mgogoro huo wa kazi ndani ya muda. Pamoja na maombi ya faragha, Mleta Maombi aliambatanisha kiapo chake, ambacho kinaeleza mtririko mzima wa mgogoro huu uliopelekea maombi haya kama ilivyoelezwa hapo juu, ambapo Mleta maombi anadai muamuzi alikosea kisheria kataika uamuzi wake kwa kutozingatia vielelezo vilivyotolewa mbele ya Tume juu ya sababu ya uchelewaji wa kufungua shauri ndani ya muda. Pia kwamba alikosea kisheria
kusikiliza na kuamua maombi ya nyongeza ya muda wakati yeye nafasi yake ni ya usuluhishi tu. Mjibu maombi akipinga maombi haya, kiapo cha Stella Bizulu ambaye ni Meneja wa mjibu maombi kiliwasilishwa. Ambapo mjibu maombi anaeleza ya kwamba msuluhishi hakukosea kisheria kufanya maamuzi juu ya maombi ya kuongezewa muda kwani mgogoro husika haukufikia 2 hatua ya kufanya usuluhishi. Mjibu maombi aliongeza kuwa msuluhishi alikataa kutumia kielelezo cha cheti cha kifo kama sababu ya mwombaji kuchelewa kufungua shauri ndani ya muda. Katika kusikiliza maombi haya, Mleta Maombi aliwakilishwa na Bw. Nehemia Munga, Muwakilishi Binafsi na Mjibu maombi aliwakilishwa na Bw. Lembris Godson, Mkuu wa Shule. Akianza na hoja ya kwanza ya kwamba muamuzi alishindwa kutumia vielelezo vya mleta maombi vizuri, Bw. Munga alieleza kwamba msuluhishi alikosea aliposhindwa kuangalia kwa makini vielelezo vilivyotolewa mbele ya Tume, kama vile cheti cha kifo cha shangazi yake. Bw. Munga akiendelea kuwasilisha hoja ya kwanza alieleza ya kwamba mleta maombi alikuwa na cheti cha kifo ambacho ni uthibitisho tosha kwamba shangazi yake aliugua na hatimae alifariki dunia, lakini msuluhishi hakutilia maanani. Hoja ya pili ni kwamba msuluhishi alikosea kisheria kusikiliza na kuamua maombi ya nyongeza ya muda wakati mamlaka yake ni usuluhishi na si kufanya uamuzi. Akiipa nguvu hoja yake alirejea katika kesi ya
marejeo Na. 26/2023 Mahakama Kuu ya Kazi Benjamin Lazaro Iseme na Yepi Markezi Insaat Vs. Sanayi Anomin Surket at Pg 7, ambapo ilirejea 3 kesi ya Barclays Bank (T) Ltd Vs. Ayyan Matesa, Civil Appeal No. 481/2022 ambapo kwa maoni yake ilijadiliwa kwamba katika mashauri ya kufanya uamauzi, msuluhishi anaondolewa kinga kusikiliza mgogoro na hivyo katika shauri letu ambapo msuluhishi alisikiliza mgogoro akiwa anafahamu au kutokufahamu msimamo huo wa sheria ni makosa. Hoja ya tatu ya kwamba msuluhishi alikosea kukubali hoja ya mjibu maombi kwamba mlezi sio mzazi ambaye alimlea mleta maombi tangu chekechea, shule ya msingi, sekondari mpaka chuo, Bw. Munga alieleza kwamba msuluhishi alikosea kumkataa mlezi kuwas sio mzazi. Alifanya makosa makubwa Sana kwa sababu yule alikuwa ni zaidi ya mzazi kwa kazi kubwa yake ya malezi aliyofanya, hivyo kitendo cha kusema ni mtu baki hakumtendea haki mleta maombi. Aliendelea kueleza ya kwamba msuluhishi amekoea kisheria alipokataa cheti cha kifo cha shangazi wa mwombaji. Bw. Munga alieleza cheti hicho kilitolewa na mamlaka inayotambulika kisheria hivyo kitendo cha kukataa cheti ni kudharau mamlaka zilizowekwa kisheria. Kwa hoja hizo anaoomba Mahakama itengue uamuzi wa msuluhishi ili mleta maombi aweze kupata nafasi ya kusikilizwa madai yake mbele ya Tume ya uamuzi na usuluhishi. 4 Kwa upande wa mjibu maombi, akianza na hoja ya kwanza
inayohusiana na cheti cha kifo alichowasilisha mwombaji na kueleza kuwa ni cha shangazi, Bw. Lembris aliwasilisha ya kwamba cheti hicho kinathibitisha kifo cha marehemu, lakini hakithibitishi kuwa marehemu alikuwa mlezi wa mwombaji. Akiendelea kufafanua alieleza ya kwamba kifo cha Nyamisi Magafu Makwasa anayedaiwa kuwa shangazi wa mwombaji hakiwezi kuzuia mgogoro kufunguliwa kwa wakati, Kwani marehemu hakuwa mwombaji na hakuna uthibithisho kuwa alikuwa mlezi wa mwombaji. Kwani Uthibitisho uliowasilishwa ni wa kifo chake tu. Pia Bw. Lembris alisisitiza kuwa hakuna sababu za msingi za kuchelewa kuleta maombi kwani angeweza kumtumia mwakilishi wake kuandaa nyaraka na kumshauri kufungua kwa wakati. Alieleza kuwa msuluhishi hakukataa cheti cha kifo ball alikataa cheti hicho kama ushahidi unaojitosheleza kuthibitisha kwamba mwombaji alilelewa na marehemu aliyetajwa, hivyo kupelekea kukataa cheti hicho kutumika kama sababu ya kuchelewa kupeleka mgogoro huu kwenye Tume. Pia hakuna uthibitisho wowote kwa mwombaji alisafiri kuelekea Geita kwa sababu yoyote ile kwa kutumia usafiri wa umma kwa kuonyesha tiketi au usafiri binafsi ambapo angeweza kuonyesha risiti ya 5 mafuta kuonyesha alikuwa huko au angalau kutaja namba ya gari au kuleta kadi kuthibitisha kuwa kweli ana gari. Akiendelea kupinga sababu hii alieleza kuwa marehemu hakuwahi kutajwa popote na mwombaji kama mmoja wa wazazi,
walezi au mtegemezi kwenye fomu yake ya taarifa za wafanyakazi kwa mwajiri (fomu hiyo imeambatanishwa kama kings 1 kwenye kiapo cha mjibu maombi). Alidai ya kwamba hakuna uthibitisho wowote kwamba muombaji alikuwa anauguza mtu yoyote akiwemo marehemu huyu. Hakuna kielelezo chochote cha kuthibitisha hilo wala fomu yoyote au risiti ya matibabu. Hivyo ni mtazamo wake ya kwamba mwombaji ameshindwa, kuthibitisha au kueleza kwa kila siku aliyochelewa alikuwa wapi na akifanya nini kama takwa la sheria linavyotaka. Alieleza kwamba Msuluhishi hajakosea kuainisha ushahidi uliotolewa kwenye maombi ya kuongezewa muda, bali alianisha na kuona kuwa hakukuwa na sababu ya msingi na ukweli wa kuongeza muda huo. Akijibu hoja ya pili, Bw. Lembris alieleza kuwa msuluhishi hakukosea kusikiliza maombi ya kuongezewa muda kwani alichokifanya ni utaratibu wa kawaida wa Tume na hata hivyo mgogoro haukufika katika ngazi ya kufanya usuluhishi. Hivyo, maamuzi ya Tume yalifikiwa kwenye ukosefu wa sababu za msingi za kuchelewa kuleta mgogoro mbele ya Tume, 6 kwani mwombaji alishindwa kuthibitisha ukaribu wake na huyo aliyemwita shangazi na matumizi ya kila iitwayo leo aliyochelewa. Hivyo Tume haikukataa kupokea maombi ya mwombaji isipokuwa Tume iliyatupilia mbali maombi hayo kwa kukosa mashiko, kwa sababu mwombaji hakuthibitisha sababu za kuchelewa yenye kueleweka, hivyo alimalizia kwa kusema kuwa, maombi
haya hayana hoja za msingi, na kwa kuwa mwombaji alishindwa kueleza sababu ya kuchelewa Tume ilitoa maamuzi sahihi na kuiomba Mahakama kutupilia mbali maombi haya kwa kukosa mashiko bali mwombaji anataka kuisumbua Mahakama. Pia alieleza kuwa mgogoro wenyewe hauna tija kwa sababu, sababu na taratibu za kufukuzwa kazi zilizingatiwa. Katika mawasilisho ya nyongeza, Bw. Munga, alirudia mawasilisho ya awali nakuongeza kuwa migogoro yote ya Tume inafunguliwa na mlalamikaji mwenyewe na, ni yeye anatakiwa kujaza fomu na kuisaini, mwakilishi anaingia kwenye kutetea hoja tu, hivyo asingeweza kumtumia mwakilishi kufungua kesi. Alieleza pia kuwa sababu za msingi zilikuwepo ambazo ni kifo na wala si vinginevyo. Alisistiza kuwa msuluhishi alikataa cheti cha kifo ndio maana alimnyima mlalamikaji nyongeza ya muda wa kusikiliza mgogoro wake mbele ya Tume. 7 Kuhusu hoja ya usafiri aliotumia, Bw. Munga alieleza kuwa, mleta maombi alikuwa na usafiri wa gari binafsi kutoka Dar es Salaam hadi Geita na kuhusu risiti za kujaza mafuta, alisema vituo vyote vya mafuta zinatumia EFD ambazo hufutika baada ya muda na kwa kuwa mleta maombi alikaa zaidi ya siku ishirini kule Geita risiti hizo zisingeweza kusubiri. Kuhusu kutokuwa na uthibitisho kwenye fomu ya taarifa za mfanyakazi, alieleza kwamba fomu zote zinalenga wazazi na hazina sehemu ya mlezi au mtegemezi hivyo jina la marehemu lisingeweza kuonekana.
Kuhusu ushahidi wa kuuguza mgojwa alisema kwamba ushahidi ni cheti cha kifo, maana kifo kinatokea baada ya mtu kuugua. Suala la kutoonyesha kila siku alikuwa anafanya nini, alisema kwamba alikuwa anauguza kila asubuhi mchana na jioni alikuwa anakwenda hospitali kupeleka chakula na huduma zingine zinaohitajika hospitalini. Baada ya kupitia viapo vya waleta maombi na mawasilisho ya pande zote mbili, Mahakama inaona hoja bishaniwa ni ni kuona kama kuna sababu ya msingi ambayo imetolewa na Mleta Maombi ili Mahakama hii iweze kufanya marejeo dhidi ya uamuzi wa Tume uliotolewa kwenye mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/UBG/53/2023. 8 Katika kujibu hoja bishaniwa, hoja zote zilizoibuliwa katika kiapo zitazingatiwa. Hata hivyo katika kujibu hoja hizo mahakama hii inaona vyema kujibu hoja ya pili kwanza kama ilivyowasilishwa na mleta maombi ambayo katika kiapo chake ni hoja ya tatu, kwani inahusu mamlaka ya msuluhishi katika kuamua maombi ya nyongeza ya muda. Ni wazi ya kwamba suala la muda ni suala la kimamlaka na kwa mujibu wa K. 15 ya Sheria ya Taasisi za Kazi (usuluhishi na uamuzi), T.S Na. 64/2004 msuluhishi anapewa mamlaka kufanya maamuzi katika suala la kimamlaka ikiwepo nyongeza ya muda. Kwa mujibu wa kanuni tajwa ni wazi msuluhishi alikuwa na mamlaka ya kuamua dhidi ya maombi ya nyongeza ya muda. Hivyo, natofautiana na mawasilisho ya mleta maombi hasa kuhusu kesi aliyorejea ya
Mahakama ya Rufani ambayo ni kesi ya Ayyan Matessa's (supra) iliyorejewa katika kesi ya Yapi Merkezi (supra) kwa sababu katika kesi hiyo ya rufani muamuzi alisikiliza usuluhishi wa upande mmoja na kutoa uamuzi na siyo maombi ya nyongeza ya muda. Na ndio sababu Mahakama ya rufani ilisema msuluhishi hana malaka ya kutoa uamuzi wa namna hiyo. Kesi hiyo haikumuondolea Muamuzi mamlaka ya kusikiliza maombi ya kuongeza muda kama yanavyotolewa na kifungu cha sharia iliyorejelewa hapo juu. Kwa msingi huo kesi hiyo haina maudhui sawa na maombi haya, kwa maoni yangu thabiti. 9 Najua kuwa katika ngazi ya mahakama hii kuna kesi kuna ukinzani juu ya tafsiri ya maamuzi katika kesi hiyo ya mahakama ya rufani. Rengo mmoja unaeleza kuwa kesi hiyo iliiondolea muamuzi mamlaka ya kutoa maamuzi ikiwemo ya maombi ya kuongeza muda sawa na msimamo katika kesi ya Yapi Merkezi (supra) iliyorejelewa na mwakilishi binafsi hapo juu. Lakini ijulikane kwamba mahakama hii haifungwi na maamuzi yake, bali yana nguvu ya ushawishi mkubwa kiasi kwamba haitakiwi kutofautiana nayo kwa sababu nyepesi nyepesi kama ilivyoonwa na Msomi Mwenzangu, Mh. Jaji Mansoor katika kesi ya David David Mbunda dhidi ya Stanley Joachim Mmanyi Misc. Land Appeal No. 80 ya 2013, Mahakama Kuu, Division ya Ardhi, DSM. Katika kesi hiyo Mh. Mansoor, J. alikiri kuwa anajua kuwa habanwi na maamuzi ya jaji mwenzake, lakini pia anajua kanuni kuwa
kwa ajili ya uthabiti wa sheria si ruhusa kwa jaji kutofautiana na maamuzi ya mwenzake kirahisi rahisi tu. Bahati nzuri mimi nimekwisha kuelezea sababu zangu za kutofautiana na mrengo huo, nikiungana na msimamo unaosema kuwa msuluhishi bado ana mamlaka ya kuamua juu ya maombi ya kuongezewa muda kwa kuwa kesi ya Matesa ya Mahakama ya rufani haikuondoa mamlaka hayo katika kesi ya Koba Said Mdoe v R & K Trucking Co. Limited, Labour Revision No. 410 OF 2022, HC, io Labour Division. Hivyo, sihitaji kurudia maoni yangu hayo hapa, itoshe kusema kuwa maoni yangu thabiti ni kuwa ana hayo mamlaka. Sababu hii inakosa mashiko kwa sababu zilizoelezewa hapo juu. Katika kujibu hoja ya kwanza, mleta maombi ameeleza kwenye kiapo chake ya kwamba sababu ya kuchelewa kufungua maombi haya ni ugonjwa wa shangazi yake uliopelekea kifo chake. Lakini kielelezo hich hakikuzingatiwa na muamuzi. Kwa upande wa Mjibu Maombi alieleza Mleta Maombi ameshindwa kuelezea ni jinsi gani ugonjwa wa shangazi yake na kifo vilivyomkwamisha kufungua shauri ndani ya muda. Kutokana na ubishi huo, mahakama hii inaona hoja ya msingi kati ya wadaawa ni kama mwobombaji alikuwa na sababu ya msingi ya kuchelewa, ukilinganisha na vielelzo alivyowasilisha Tume. Katika utatuzi wa hoja hii Kanuni ya 31 ya Sheria ya Taasisi za Kazi (Usuluhishi na Uamuzi), T.S. Na. 64/2004, inaeleza ya kwamba tume inaweza kutoa nyongeza ya muda
panapokuwa na sababu ya msingi ya kuchalewa. Kutokana na kifungu tajwa, Tume ina mamlaka ya kisheria kuongeza muda wowote chini ya Kanuni hii, ikiwa Mwombaji ametoa sababu ya msingi ya uchelewaji. Mwombaji katika shauri hili kama inavyoonyesha katika CMA Form No. 1 anakiri kwamba mgogoro ulitokea tarehe 05/04/2023 na aliuwasilisha Tume tarehe 5/06/2023 ii ilimchukua siku zaid ya sitini kupeleka shauri Tume ikiwa na maana kwamba alichelewa kwa muda wa mwezi (1) kwani tarehe ya mwisho kufungua ilikuwa tarehe 05/05/2023, kwa mujibu wa Kanuni 10 (1) ya Sheria ya Taasisi za Kazi (Usuluhishi na Uamuzi), T.S Na. 64/2004 inayoelekeza ufunguaji wa migogoro inayohusiana na uachishwaji kazi ufanyike ndani ya siku 30 tangu uachishwaji kazi ulipofanyika. Kwa kuanza na hoja ya ugonjwa iliyoplelekea kifo kama ilivyoibuliwa na mleta maombi, ni wazi ugonjwa huweza kuwa sababu ya nyongeza ya muda kama ilivyojadiliwa katika kesi ya Fredrick Mdimu dhidi ya Cultural Heritage Ltd, Marejeo Na. 19 of 2011, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyoketi Dar Es Salaam, ilielezwa ya kwamba: - "Ugonjwa ni Sababu inayokubalika katika kucheiewa kufungua shauri ndani ya mda. Lakini sababu hii iazima ithibitishwe na kisiwe kisingizio. Kama mwombaji alikuwa anatabiwa hospital! ni kwanini hakutoa had ya taarifa ya matibabu Hi kuunga mkono hoja hiyo?" Katika maombi haya, ugongwa unaowekwa mbele na hatimae kifo ni
cha ayedaiwa kuwa shangazi na mlezi wa mleta maombi toka alipoachishwa kazi. Ni dhahiri kuwa uthibitisho wa cheti cha kifo pekee kilichowasilishwa ma mwombaji sio kielelezo cha kuthibitisha kiasi cha ushiriki katika kuuguza mgonjwa huyu ambaye kisheria ni mtu baki kwa 12 mwombaji. Kwani cheti hicho pekee hakithibitishi kama marehemu alikuwa ni shangazi wa muombaji na pia mlezi wake. Hata kama angekuwa na ukaribu huo, muombaji pia hakueleza mpaka alipofungua mgogoro, mgonjwa alianza kuumwa lini na kama aliendelea kuumwa na yeye aliendelea kuuguza kwa siku zote hadi umauti na baada ya kifo kutakiwa kukaa kwa siku zote hizo bila kuchukua hatua kwenye suala kubwa kama kufukuzwa kazi. Katika KF. 110 cha Sheria ya Ushahidi, mtoa hoja anatakiwa kuthibitisha. Alichotakiwa kuthibitisha ni ukaribu wake na marehemu pamoja na uhusika wake katika kumuuguza na ushiriki katika kifo. Sasa cheti cha kifo, tena cha mtu ambaye hata uhusiano wa kindugu wenyewe haukuthibitishwa haithibitishi yote hayo yalioyotakiwa kuthibitishwa, kama alivyolisemea kwa sahihi ndugu Lembris. Pia katika Kesi ya Daudi Hag a v. Jenitha Abdan Machanju, Madai ya Masahisho No. 19 of 2006, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, iliyoketi Tabora (Haijaripotiwa), ambapo ilielezwa ya kwamba; "Mtu yeyote anaeomba nyongeza ya muda anatakiwa aithibitishie Mahakama kila siku ya ucheiewaji Hi kuiwezesha Mahakama kutumia mamlaka
yake." 13 Kutokana na msimamo huo wa kisheria katika kesi tajwa ni wazi uchelewaji wa mwezi mmoja ni mkubwa hasa pale ambapo Muombaji ameshindwa kueleza kifasaha matumizi ya kila siku yake baada ya kuachishwa kazi. Katika msingi huu, ni wazi muamuzi alichambua vizuri ushahidi na si kweli kwamba hakuzingati ushahidi wa muombaji. Katika mazingira haya natupilia mbali maombi haya na kushikilia uamuzi wa Tume. Kila upande utajigharamia gharama zake katika shauli hili. M. P. OPIYO,
JUDGE 15/11/2023
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.