tanzania union of private security employees vs g4s secure solutions t ltd 2021 tzhcld 204 12 julai 2021
- Citation
- tanzania union of private security employees vs g4s secure solutions t ltd 2021 tzhcld 204 12 julai 2021
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2021
- Posture
- Labour Application / Final Judgment
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2021
- Posture
- Labour Application / Final Judgment
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
Applicant failed to demonstrate sufficient cause for delay, did not account for each day, and exhibited negligence in complying with court-ordered timelines. Extension of time cannot be granted in absence of good cause.
Court disposition
Application dismissed
Orders
- Application for extension of time is refused
- Applicant's name amended to Tanzania Union of Private Security Employees as unopposed
02
Material facts
Parties
Tanzania Union of Private Security Employees
Applicant Counsel: Michael MgomboziG4S Secure Solutions (T) Ltd
Respondent Counsel: Moses Kyondo03
Procedural history
Posture
Labour Application / Final Judgment
04
Questions and positions
Legal issues
Whether applicant has shown sufficient cause for extension of time to refile labour dispute
Party arguments
- Applicant
- Applicant argued delay was due to logistical challenges in obtaining signatures from members located in Geita, who were unemployed and difficult to reach, and that all reasonable efforts were made within the time allowed. Applicant also cited the right to be heard and referenced prior court decisions supporting extension of time for procedural defects.
- Respondent
- Respondent argued applicant delayed for 20 days beyond the court-ordered 14 days, failed to account for each day of delay, and exhibited negligence. Respondent cited precedents requiring strict compliance with timelines and asserted that ignorance of law or counsel's mistakes are not valid grounds for extension.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Sebastian Ndaula v Grace Gwamafa, Court of Appeal, Bukoba, Civil Appeal No. 4 of 2014
Applicant must account for each day of delay and show sufficient cause for extension of time.
- 02
Omari Ibrahim v Ndege Commercial Service Ltd, Civil Application No. 83/01 of 2020
Ignorance of law and mistakes of counsel are not sufficient grounds for extension of time.
- 03
Rule 56 of Labour Court Rules, GN No. 106 of 2007
Court has discretion to extend time only upon demonstration of good cause.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
Applicant failed to demonstrate sufficient cause for delay, did not account for each day, and exhibited negligence in complying with court-ordered timelines. Extension of time cannot be granted in absence of good cause.
Obiter and limits
- Right to be heard must be exercised in accordance with procedural rules.
- Court will not encourage laxity by granting extensions for delays caused by negligence.
Court disposition
Application dismissed
- Application for extension of time is refused
- Applicant's name amended to Tanzania Union of Private Security Employees as unopposed
Source and reliance status
TANZLII · 1 January 2021
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 1 January 2021
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA
DIVISHENI YA KAZI
PAR ES SALAAM MAOMBI YA ANUWAI NA. 118 YA 2020
KATI YA
TANZANIA UNION OF PRIVATE SECURITY EMPLOYEES................................................... MUOMBAJI
DHIDI YA G4S SECURE SOLUTIONS (T) LTD......................... MJIBU MAOMBI
MAAMUZI Tarehe ya amri ya mwisho: 23/06/2021 Tarehe ya maamuzi: 12/07/2021 M. Mnyukwa, J. Muombaji amefungua maombi haya akiiomba mahakama imuongezee muda wa kuweza kusajili upya shauri la marejeo katika mgogoro wa kazi Na. CMA/DSM/ILA/R.688/17 ulioamuriwa tarehe 29/11/2017. Maombi haya yameambatanishwa na kiapo cha ndugu Charles Basondole, Katibu Mkuu wa muombaji. Mjibu maombi alipinga vikali maombi haya kwa kuleta kiapo kinzani. Katika shauri hili mawasilisho yalifanyika kwa njia ya mdomo. Muombaji aliwakilishwa na ndugu Michael Mgombozi, muwakilishi kutoka i chama cha wafanyakazi TUPSE ilihali mjibu maombi aliwakilishwa na Bw. Moses Kyondo, wakili msomi. Muwakilishi wa muombaji aliiomba Mahakama kiapo cha muombaji kiwe sehemu ya ushahidi wake. Alieleza kuwa, maombi haya yanatokana na amri iliyotolewa na mahakama tarehe 26/02/2020 ambapo ilimruhusu muombaji kuwasilisha maombi upya ndani ya siku 14 kutokana na kasoro zilizoonekana katika shauri la mgogoro wa kazi No. 06/2018. Alieleza kuwa maombi haya yanahusu kuongezewa muda baada ya kutokutekeleza amri ya mahakama katika mgogoro tajwa hapo juu. Muwakilishi huyo aliendelea kueleza kuwa, mgogoro huu ulitokana na makubaliano yaliyofanywa baina ya mleta maombi na mjibu maombi ambao ni wafanyakazi wa kituo cha mgodi wa madini cha mkoani Geita (Geita Gold Mine). Ilielezwa kuwa, mkataba wa biashara baina ya wadaawa ulikoma hivyo
mjibu maombi alikatisha ajira (retrenchment). Kwamba, mnamo tarehe 20/02/2018 mleta maombi (TUPSE) ambaye alikuwa anawakilisha wafanyakazi katika kituo hicho waliingia makubaliano ya kusitisha mkataba kwa wafanyakazi. Alisema kuwa, walikubaliana kwenye mafao yao ya kusitisha ajira mafao ya aina kumi (10) lakini mjibu maombi hakuweza kutekeleza mafao hayo akatekeleza tu matano na kwa upungufu. Kwamba, mapungufu hayo yalibainika 2 tarehe 01/04/2018 baada ya kuwapatia ukomo wa ajira ambapo mleta maombi alifanya juhudi za majadiliano bila mafanikio na mnamo tarehe 11/05/2018 alifungua mgogoro Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Tume). Ilielezwa kuwa, mnamo tarehe 26/06/2018 mgogoro ulikosa suluhu mbele ya Tume na baada ya suluhu kushindikana ulifunguliwa mbele ya mahakama hii tarehe 24/08/2018 ambao uliondolewa na kuruhusiwa kuwasilishwa upya ndani ya siku kumi na nne (14). Kwamba tangu tarehe ruhusa ilipotolewa, 26/02/2010 mleta maombi alichelewa kuwasilisha maombi ndani ya muda uliowekwa kwasababu mleta maombi aliamua kuwasiliana na anaowawakilisha waliopo mkoani Geita. Ilielezwa kuwa, mnamo tarehe 05/03/2020 nyaraka yenye orodha ya wafanyakazi zilitumwa mkoani Geita ili wanachama waweze kusaini na ziwasilishwe mbele ya mahakama hii pamoja na shauri jipya. Muwakilisha alisema kuwa orodha hiyo imeambatanishwa na risiti ya kutuma kwenye kampuni ya SG Transport ambayo ofisi zao
zipo Ubungo. Kwamba nyaraka hizo zilirejeshwa tarehe 26/03/2020 zikiwa tayari zipo nje ya muda uliotolewa na Mahakama. Alisema, tarehe 01/04/2020 maombi haya yaliwasilishwa mbele ya mahakama. 3 Kwamba tangu tarehe 26/02/2020 ambapo ilitolewa amri ya mahakama kufungua shauri jupya mpaka tarehe 01/04/2020 yalipofunguliwa maombi haya, mleta maombi hakuwahi kufanya uzembe wa aina yoyote ile wa kukwamisha mgogoro huu kufunguliwa. Ilielezwa kuwa, mleta maombi alifanya juhudi zote kuhakikisha mgogoro huu unafunguliwa ndani ya muda ila kwakuwa waleta maombi ambao ni wanachama wa TUPSE wanaishi nje ya mkoa wa Dar es salaam huku wengi wakiwa hawana ajira hivyo hawakuweza kupatikana kwa wakati ili waweze kutimiza amri ya mahakama. Iliongezwa kuwa, hali hiyo ilipelekea kuchelewa kufunguliwa kwa mgogoro huu. Bw. Machael Mgombozi aliiomba Mahakama itoe maamuzi ya ■ kuongeza muda ili mleta maombi aweze kuwasilisha mgogoro wa kikazi J mahakamani kwakuwa makubaliano ya mafao waliyokubaliana hayakutekelezwa. Aliongeza kuwa, wanachama wa mleta maombi wanaendelea kuathirika kwenye kituo walichopelekwa na mjibu maombi kwa kutokupewa walichokubaliana kwakuwa wateja wa mleta maombi wanaendelea kuteseka kwa kuwa mjibu maombi alitakiwa kuwasafirisha na kuwarudisha kwao. Aliongeza kuwa makubaliano hayo yameambatanishwa kama kiamatanisho TLIP4. Ili kuyapa nguvu mawasilisho yake mleta maombi alinukuu
maamuzi mbalimbali ya 4 mahakama pamoja na shauri la marejeo Na. 126/2015 kati ya Christopher Gasper na wenzake watano dhidi ya Tanzania Porty Authority (TPA), pia kesi ya Eliminata Masinda na mwenzake dhidi ya Maswet Masinda na mwenzake, Maombi ya Anuwai Na. 70 ya 2019 mahakama ya rufaa ya Arusha mahakama ilieleza kuwa moja ya sababu za kuongeza muda ni pamoja na kasoro zilizopo katika maamuzi au kumbukumbu za mahakama na kesi nyingine nyingi ambazo mahakama imezingatia. Iliongezwa pia kuwa maombi yaliyopo mbele ya mahakama hii na kwa mujibu wa kanuni ya 56 ya Kanuni za Utendaji Kazi, Mahakama ya Kazi [Tangazo la Serikali Na. 106 la 2007] (itatambulika kama Kanuni za utendaji Kazi wa Mahakama) inaipa mahakama mamlaka ya kuongeza muda ili maombi ya wateja wake yaweze kusikilizwa. Vile vile muwakilishi aliomba Mahakama kupitia kanuni ya 24 (9) ya Kanuni za Utendaji Kazi wa Mahakama ya Kazi [Tangazo la Serikali Na. 106 la 2007] (zitajulikana kama Kanuni za Mahakama ya Kazi) neno Petroliam liondoke katika jina la muombaji na lisomeke Tanzania Union of Private Security Employees. Kwa mawasilisho hayo hapo juu muwakilishi aliiomba mahakama impe muombaji ongezeko la muda. 5 Akijibu hoja za muombaji wakili wa mjibu maombi aliomba kiapo kinzani cha mjibu maombi kiwe sehemu ya mawasilisho yake. Alieleza kuwa, mleta maombi ameshindwa kujikita kwenye hoja za msingi na ameleta hoja mpya
ambazo hazipo kwenye maombi haya. Alisema kuwa, mleta maombi amechelewa kwa siku 20 baada ya kutakiwa na mahakama hii kuleta maombi ndani ya siku 14. Kwamba, uchelewaji wa kufungua maombi umesababishwa kwa kiasi kikubwa na uzembe kwa upande wa muombaji. Ilielezwa kuwa, muombaji ameshindwa kueleza kila siku ya uchelewaji wake katika kiapo chako ikiwa ni kigezo cha mahakama kutoa ruhusu ya kufungua shauri nje ya muda. Alisistiza kuwa muombaji hana sababu ya msingi ya kuchelewa. Aliongeza kuwa uchelewaji wa mleta in maombi umesababishwa na uzembe wa kutofuatilia sheria na amri za Uh. . Rh . b mahakama Pamoja na kutokuwa na bidii kwa upande wa muombaji. Iliendelea kuelezwa kuwa, katika maamuzi ya mahakama ya rufani Sebastian Ndaula dhidi ya Grace Gwamafa, kesi No. 04 ya mwaka 2014, Bukoba, mahakama iliamua kwamba katika maombi ya ruhusa ya kufungua shauri nje ya muda, mleta maombia anatakiwa atoe sababu ya kila siku aliyochelewa jambo ambalo mleta maombi ameshindwa kufanya. Ilifafanuliwa kuwa, amri ya kumtaka mleta maombi alete 6 maombi mapya ilitolewa tarehe 26/02/2020 ambapo ilimtaka alete orodha ya waleta maombi anaowawakilisha. Kwamba, hata hivyo mleta maombi kutokana na kiapo chake ilibidi asubiri mpaka tarehe 05/03/2020 kwaajili ya kutuma nyaraka kwenda Geita ambapo nyaraka hizo zilirejeshwa tarehe 26/03/2020. Alisema, ukiangalia tarehe hizo inaonekana kulikuwa na uzembe
mkubwa umefanyika na kusababisha kushindwa kuwasilisha maombi ndani ya wakati. Ilielezwa kuwa, katika maamuzi ya kesi ya Omari Ibrahim dhidi ya Ndege Commercial service Ltd, No. 83/01 ya mwaka 2020 mahakama iliamua kuwa kutokujua sheria na makosa ya wakili hayawezi kuwa sababu ya msingi ya kuongeza muda Kwamba, kwenye suala lililopo mbele ya mahakama hii ■ffhi •% J kumbukumbu zipo bayana kwamba mleta maombi alikuwa mzembe kwenye utaratibu aliouchukua wa kuweza kufungua shauri hivyo kuchelewa kufungua ndani ya muda. Ilielezwa kuwa katika kesi ya Umoja Grage dhidi ya National Bank of Commerce (1997) TLR 109 mahakama ilisema kuwa kutokujua sheria si sababu ya msingi ya kuomba ruhusa ya kuongezwa kwa muda. Aliongeza kuwa, watu wote wanaokuja mahakamani wasiwe na ucheleweshaji usiokuwa na msingi. Alisema kuwa kwenye maamuzi ya 7 Jacob Shija dhidi ya M/S Regent Food and Drinks Ltd na Mwanza City Council, Maombi ya madai No. 140/08 ya mwaka 2017, katika ukurasa wa 8 mahakama ya rufaa ilisema kwamba wenye mashauri lazima wafuate utaratibu wa mahakama wa kufanya mambo yote ndani ya muda na wakishindwa kufanya hivyo waoneshe sababu za kushindwa kufanya hivyo. Iliendelea kuongezwa kuwa, shauri lazima lifike mwisho kama ambavyo iliamuriwa katika kesi ya Barclays Bank Tanzania Ltd dhidi ya Phylisian Hussein Mcheni, maombi ya Rufaa No. 19 ya mwaka 2016. Ilisistizwa kuwa mazingira yaliyopo
katika kesi hii yanaonesha kuwa kulikiwa na uzembe kwamba, mleta maombi ameshindwa kuhesabu kila siku aliyochelewa. Hivyo aliiomba mahakama hii itupilie mbali maombi ya muombaji. A Katika mawasilisho ya nyongeza muwakilishi wa muombaji alieleza kuwa, mleta maombi hajawahi kufanya uzembe kwenye maombi haya na kurudia kama alivyoeleza awali. Aliongeza kuwa si sahihi kujificha kwenye sababu za kiufundi za kutaka shauri limalizike au lifike mwisho wakati mjibu maombi ameshindwa kuhakikisha hili jambo linaafikia mwisho kwa kuwalipa wanachama kwa mujibu wa makubaliano. Iliendelea kuelezwa kuwa katika kesi ya Omari Ibrahim dhidi ya 8 Ndege Commercial (kama ilivyonukuliwa na muombaji) haihusiani na kesi iliyopo mbele ya mahakama hii kwakuwa katika kesi hiyo muombaji alichelewa kwa miezi 10 na siku 27. Aliongeza pia kesi zingine zilizonukuliwa na muwakilishi wa muombaji hazifanani mazingira na kesi iliyopo mbele ya mahakama hii. Hivyo aliomba kuwa iruhusu maombi yake ya ongezo la muda ili haki iweze kutendeka kwa wateja wake. Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili, Mahakama inajiuliza endapo muombaji ametoa sababu za msingi za kuweza kuongezewa muda kusajili upya maombi ya marejeo. VJ Ni matakwa ya kisheria kuwa katika maombi yoyote ya ongezo la muda ni wajibu wa muombaji kutoa sababu za msingi zilizomzuia kuwasilisha maombi yake ndani ya muda uliowekwa kisheria au aliopewa na
mahakama. Haya yameelezwa katika kanuni ya 56 (1) (3) ya Kanuni za utendaji kazi wa mahakama. Katika maombi haya sababu za muombaji za kuchelewa zipo katika aya ya 16 ya kiapo cha muombaji ambapo ameeleza kuwa, alichelewa kutii amri ya mahakama ya kufungua upya mgogoro wake ndani ya siku 14 kwasababu nyaraka ya orodha ya majina ya wateja wa muombaji ilitumwa mkoani Geita tarehe 05/03/2020 kwa ajili ya kusainiwa na 9 wateja wake ambapo ilirejeshwa Dar es Salaam tarehe 26/03/2020 kama inavyoonekana katika kieleleza TUP8 (stakabadhi ya kutuma nyaraka), ikiwa tayari ni nje ya muda uliotolewa na mahakama. Mahakama imezingatia hoja ya wakili wa mjibu maombi kuwa sababu alizowasilisha muwakilishi mbele ya mahakama hii ni tofauti na zile zilizopo katika kiapo cha muombaji. Nimepitia kiapo husika, kama ilivyoelezwa hapo awali ni wazi kuwa sababu aliyowasilisha muwakilishi wa mjibu maombi ni zile zile zilizopo katika kiapo cha muombaji hivyo wakili wa mjibu maombi alijichanganya katika hilo na hoja zake husika katika suala hilo hazina mashiko. Baada ya kupitia hoja aliyotoa muombaji mahakama inajiuliza kama sababu hiyo ni ya msingi kuweza kutoa ongezeko la muda. Kama Ip* ambavyo imeelezwa na pande zote mbili amri ya mahakama ya kusajili ' "d:. d' upya maombi ya marejeo tarajiwa ilitolewa tarehe 26/02/2020. Kumbukumbu zinaonesha maombi haya ya ongezeko la muda yalifunguliwa tarehe
01/04/2020 ikiwa ni takribani baada ya siku 34 tokea siku ya amri ya mahakama ambayo ilitolewa tarehe 26/02/2020. Kwa hesabu hiyo ni wazi kuwa muombaji alichelewa kwa takribani siku 20 kutii amri ya mahakama. 10 Maamuzi mbalimbali ya mahakama yamesisitiza kuwa katika maombi ya ongezo la muda ni jukumu la muombaji kutoa sababu na kuthibitisha kwa kila siku aliyochelewa kama ilivyoamuriwa katika kesi ya Sebastian Ndaula dhidi ya Grace Gwamafa (kama ilivyonukuliwa na wakili wa mjibu maombi). Katika shauri hili tokea amri ya mahakama imetolewa tarehe 26/02/2020 ilimchukua muombaji takribani siku nane (8) kutuma nyaraka za orodha ya majina ili iweze kusainiwa na wateja wake. Na hata wateja wake baada ya kusaini waliirejesha nyaraka hiyo baada ya siku 19 ambapo ilikua tarehe 26/03/2020 kama inavyoonesha katika kielelezo TUP8 (stakabadhi ya kurudisha nyaraka). Muombaji pia baada ya kurejeshewa nyaraka hiyo husika, alitumia takribani siku sita (6) kuwasilisha maombi yake mbele ya mahakama hii. Kwa mchanganuo huo hapo juu inaonesha wazi kuwa muombaji alifanya uzembe katika kushughulikia shauri hili. Katika kila hatua aliyokuwa anachukua alikuwa anaonesha uzembe wa hali ya juu wa kutokujali muda aliopewa na mahakama. Muombaji alijua wazi kuwa wateja wake wanaishi mkoani Geita na hawako sehemu moja lakini akachukua siku 8 kuwatumia nyaraka hiyo ilihali akijua wazi muda aliopewa na
mahakama ni siku kumi na nne tu. Lakini hata hivyo muombaji pia ameonesha ya kuwa alishindwa kuwasisitiza wateja wake li juu ya uharaka wa kutii muda wa mahakama na kuwaruhusu kutumia muda wa siku 19 kusaini nyaraka hiyo. Mahakama imezingatia sababu ya muwakilishi wa muombaji kuwa wateja wake hawana ajira na hawakuweza kupatikana kwa wakati, lakini hata hivyo muombaji ameonesha uzembe wa kutokuwa na mahusiano mazuri na wateja wake. Ni maoni ya mahakama kuwa endapo muombaji angekuwa na bidi ya kutafuta wateja wake na akawa na mawasiliano mazuri nao basi wangeweza kupatikana kwa siku hata 3 na kuwa tayari wamekamilisha zoezi la kuweka sahihi katika nyaraka husika. 5' ' s' ■, , Z' Ni rai ya mahakama kuwa ukomo wa muda umewekwa ili kuzuia wadaawa wasiwe wazembe na wasije mahakamani kwa muda wanaojipangia wao wenyewe. Hivyo basi endapo mahakama itaweka mazoea ya kuruhusu ongezeko la muda katika mazingira ya uzembe kama yaliyopo katika kesi hii itapoteza maana ya kuweka sheria hizo. Mahakama pia imezingatia hoja ya haki ya kusikilizwa kama alivyowasilisha muwakilishi wa muombaji. Ni kweli sheria za nchi zinasisitiza haki ya kusikilizwa kabla ya kutolea maamuzi jambo lolote lile, lakini hata hivyo haki hiyo inatakiwa itolewe kwa kufuata taratibu zilizowekwa kama ambavyo wakili wa mjibu maombi amewasilisha. 12 Katika shauri hili muombaji ameshindwa kufuata taratibu za msingi ili haki
ya kusikilizwa iweze kutolewa. Aidha mahakama pia imeridhia maombi ya muwakilishi wa muombaji ya kutoa neno Petrolman katika jina la muombaji kwa kuwa maombi haya hayajapingwa na mjibu maombi na hata hivyo jina hilo pia halipo katika kumbukumbu za Tume ambako ndipo mgogoro huu ulipoanzia. Hivyo basi jina la muombaji litasomeka kama Tanzania Union of Private Security Employees kama ilivyoombwa. % % w Hivyo basiz kutokana na majadiliano hapo juu ni wazi kuwa & K. muombaji ameshindwa kutoa sababu za msingi za kuipa mamlaka mahakama ya kumuongezea muda wa kuwasilisha maombi yake nje ya muda aliokuwa ameamuriwa tarehe 26/02/2020. Kwa sababu hiyo, mahakama inaliona shauri hili halina mantiki na inalitupilia mbali. Imeamuriwa hivyo. M. MNYUKWA
JAJI 06/07/2021 13
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.