violeth mathayo mwanila dhidi ya computech ics t ltd 2023 tzhcld 1192 13 machi 2023
- Citation
- violeth mathayo mwanila dhidi ya computech ics t ltd 2023 tzhcld 1192 13 machi 2023
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2023
- Posture
- Labour Revision / Judgment
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2023
- Posture
- Labour Revision / Judgment
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
The dispute had already been dismissed for non-appearance in 2019 and could not be reopened without a proper application for restoration. The mediator lacked jurisdiction to entertain the matter afresh.
Court disposition
Application dismissed
Orders
- The decision of the arbitrator dated 5 September 2022 is set aside as it concerned a matter already determined.
02
Material facts
Parties
Violeth Mathayo Mwanila
Applicant Counsel: Bw. LufasinzaComputech ICS (T) Ltd
Respondent Counsel: Wakili NganongeraAmounts and remedies
- Monthly Salary: TZS 150,000
03
Procedural history
Posture
Labour Revision / Judgment
04
Questions and positions
Legal issues
- 01
Whether the mediator had jurisdiction to entertain a matter previously dismissed for non-appearance
- 02
Whether proper procedure was followed in reopening the labour dispute
- 03
What reliefs are available to the parties
Party arguments
- Applicant
- The mediator had no authority to dismiss the dispute; the matter should have been heard by an arbitrator. The applicant seeks the matter to be remitted for hearing by an arbitrator.
- Respondent
- The application before the mediator was for extension of time, which the mediator had jurisdiction to determine. The dispute had already been dismissed in 2019 for non-appearance, and there was no sufficient cause to reopen it.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Zito Zuberi Kabwe & Others vs. Attorney General, Civil App. No. 365 of 2019
A mediator has jurisdiction to determine applications for extension of time, but cannot reopen a dispute already dismissed for non-appearance without a proper application for restoration.
- 02
Order of CMA/DSM/ILA/754/18 dated 1 April 2019
Once a dispute is dismissed for non-appearance, it cannot be reopened unless an application for restoration is made with sufficient cause shown.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
The dispute had already been dismissed for non-appearance in 2019 and could not be reopened without a proper application for restoration. The mediator lacked jurisdiction to entertain the matter afresh.
Court disposition
Application dismissed
- The decision of the arbitrator dated 5 September 2022 is set aside as it concerned a matter already determined.
Source and reliance status
TANZLII · 1 January 2023
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 1 January 2023
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA
DIVISHENI YA KAZI
ILIYOKETI PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 352 YA 2022 Kutokana na Tuzo ya Tume ya Usu/uhishi na Uamuzi ya mgogoro wa kikazi Na. CMA/DSM/ILA/567/21. VIOLETH MATHAYO MWANILA....................................... MLETA MAOMBI
DHIDI YA COMPUTECH ICS (T) LTD................................................ MJIBU MAOMBI
HUKUMU K.T.R, Mteule, J 27 Februari 2023 & 13 Machi, 2023 Katika maombi haya ya Marejeo, Mleta maombi Violeth Mathayo Mwanila anaomba marejeo dhidi ya uamuzi wa msuluhishi Molele B.L. uliotolewa katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/DSM/ILA/567/21. Mleta maombi alikuwa ameajiriwa na Mjibu Maombi kama mpishi. Aliachishwa kazi tarehe 23/4/2018 akiwa ametumikia nafasi hiyo kwa muda wa miaka 8 kwa mshahara wa TZS. 150,000 kwa mwezi. Kabla ya mgogoro huu, mleta maombi hapo awali alifungua mgogoro CMA/DSM/ILA/74/18 akiwa anawakilishwa na mwakilishi binafsi Makasi Timamu. Shauri likiwa katika hatua ya usuluhishi lilifutwa tarehe 1/4/2019 kutokana na kutokuwepo kwa mleta maombi kutokana na kile alichodai kuwa alikuwa Dodoma kumwangalia mama yake aliyekuwa mgonjwa huku akimwacha mwakilishi binafsi i aliyekataliwa na Tume kuendelea kumwakilisha na hatimaye shauri kufutwa. Kutokana na maelezo aliyotoa Mleta maombi CMA, aliporudi, alipeleka shauri kulifungua Mahakama ya mwanzo ya Kariakoo Ilala ambapo alirudishwa akafungue mgogoro wake Tume. Ndipo Mleta maombi alifungua mgogoro Na. CMA/DSM/ILA/567/2021 ambao ulipangwa kwa Mhe. Molel, Msuluhishi akiwa ameambatanisha na maombi ya kuomba kuongezewa muda. Maombi hayo yaliendelea kusikilizwa na Mhe Molel ambaye alikataa kuongeza muda na kutupilia mbali maombi ya mleta maombi. Katika mawasilisho yake, mwakilishi wa mleta maombi alikuja na
Hoja zifuatazo: - 1) Endapo kulikuwa na sababu ya Tume kumwondoa mwakilishi wa awali wa mleta maombi 2) Endapo taratibu zilifuatwa kwa Mhe. Molel kuondoa mgogoro wa mleta maombi 3) Nini nafuu ya pande zote Alianza na hoja ya pili kwa kueleza kwamba hakukuwa na sababu ya Mhe. Msuluhishi kuondoa mgogoro kwani yeye ni msuluhishi hana mamlaka ya kuamua mgogoro. Alirejea kesi ya Marejeo No. (9) ya 2022 kati ya Suzana Mwanyawa dhidi ya Cardinal Rugambwa Hospital, ukurasa wa 8 ambapo Mahakama hii iliamua kuwa 2 Msuluhishi hana mamlaka ya kuamua mgogoro. Hivyo ni maoni ya Bw. Lufasinza kuwa mleta maombi anaomba marejeo yarudishwe yakasikilizwe na Muamuzi na siyo Msuluhishi. Kuhusu hoja ya tatu ya nafuu, mleta maombi anaomba shauri likaamuliwe na Arbitrator. Tunaomba kuwasilisha. Kwa upande wake Wakili Nganongera akianza na hoja ya pili endapo utaratibu ulifuatwa kuondoa mgogoro wa mleta maombi, aliwasilisha kwamba Maombi Na. CMA/DSM/ILA/567/2021 yalikuwa yanaiomba Tume mgogoro wa kazi kufunguliwa nje ya muda. Akirejea kesi ya Zito Zuberi Kabwe na Wenzake vs. Attorney General, Civil App. No. 365 of 2019, ukurasa wa 9 alinukuu maamuzi ya Mahakama kwamba "the Court has discretion to extend time but the discretion must be exercised judiciously" Aliendelea kueleza kwamba Shauri lililokuwa mbele ya Mhe. Molel lilikuwa ni la kuongezewa muda na siyo la kufukuzwa kazi na hivyo
linaanza kusikilizwa na Mediator na ana mamlaka ya kuamua suala la muda. Alisema Kesi ya Suzana ni tofauti kwa sababu ilikuwa inazungumzia kuondolewa kwa mgogoro ambao haukuwa nje ya muda. Wakili aliendelea kuongeza kuwa kurudisha mgogoro huu Tume haikuwa sahihi kwani ulishatolewa maamuzi kuwa umetupiliwa mbali tangu 2019. Kwa maoni yake Mgogoro unarejeshwa pale tu ambapo 3 kuna sababu ya msingi na katika shauri hili hakuna sababu ya msingi. Hivyo aliomba maombi yatupiliwe mbali. Baada ya kuangalia hoja za wadaawa, nimeona ni muhimu nianze na kile alichosema Wakili wa mjibu maombi kuwa shauri halikutakiwa kurudishwa CMA kwani lilishatolewa uamuzi tangu 2019. Hoja hii haikujibiwa na mwakilishi wa mleta maombi. Baada ya kuzingatia maelezo ya Mleta maombi kwamba alikuwa na shauri lililoondolewa kutokana na kukosa uendeshaji, na kutokana na kumbukumbu za CMA, ni kweli, kulikuwa na mgogoro Na. CMA/DSM/ILA/754/18 uliowahi kutupiliwa mbali na Mhe Mahindi, Msuluhishi katika order yake ya tarehe 1 April 2019. Kwa mujibu wa amri hii, mgogoro ulitupwa kwa kukosa uendeshaji kutokana na Mleta maombi kutokuwepo. Nakubaliana na wakili wa Mjibu maombi kwamba mgogoro haukutakiwa kurudishwa tena CMA. Kwa maoni yangu, hata msuluhishi hakuwa na mamlaka ya kusikiliza mgogoro ambao ulishatupwa kutokana na kukosa kuendeshwa. Kilichotakiwa kufanyika ni mleta maombi kufungua maombi ya kuomba
mgogoro uliotupwa akiwa hayupo urudishwe huku akitoa sababu zilizomfanya ashindwe kufika Tume na kusababisha mgogoro huo kutupwa. 4 Kutokana na maoni haya, sioni sababu ya kuendelea na hoja nyingine kwani hii inatosha kumaliza shauri. Kwa sababu hii, natengua uamuzi wa Muamuzi wa Tarehe 5 Septemba 2022 kwani ulihusu shauri ambalo lilishaamuliwa awali. Imeamuliwa hivyo Imetolewa Dar es Salaam leo tarehe 13 Machi 2023 5
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.