MAREJEO NO 5071 OF 2024 WEMA MTENGWA VRS TANZANIA RAILWAY CORPORATION
- Citation
- MAREJEO NO 5071 OF 2024 WEMA MTENGWA VRS TANZANIA RAILWAY CORPORATION
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2024
- Posture
- Labour Reference / Judgment
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2024
- Posture
- Labour Reference / Judgment
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
The CMA lacked jurisdiction to enforce the Deed of Settlement as such enforcement falls within the exclusive mandate of the High Court. The applicant's claims were therefore properly dismissed.
Court disposition
Application dismissed
Orders
- Application is dismissed for lack of merit
- No order as to costs
02
Material facts
Parties
Wema Mtengwa
Applicant Counsel: Sammy KateregaTanzania Railway Corporation
First Respondent Counsel: Stephen KimaroMwanasheria Mkuu wa Serikali
Second Respondent Counsel: Hamimu Nkoleye03
Procedural history
Posture
Labour Reference / Judgment
04
Questions and positions
Legal issues
- 01
Whether the Commission for Mediation and Arbitration (CMA) had jurisdiction to enforce the Deed of Settlement
- 02
Whether the applicant is entitled to a retirement letter and benefits for the period 2007-2013
- 03
Whether the CMA erred in addressing issues outside the applicant's claims
Party arguments
- Applicant
- The CMA failed to properly evaluate evidence, considered irrelevant documents, and addressed issues not raised by the applicant. The applicant seeks a retirement letter and benefits as per the Deed of Settlement, arguing that the employer failed to fulfill agreed terms.
- Respondent
- The respondents argued that the CMA's decision was correct, that the applicant had already received payments, and that the CMA lacked jurisdiction to enforce the Deed of Settlement, which should be enforced by the High Court.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Section 48(3) of the Labour Court Rules, GN No. 106 of 2007
Only the High Court has jurisdiction to enforce settlement agreements made before it.
- 02
Section 89(2) of the Employment and Labour Relations Act, Cap 366 (R.E. 2019)
The CMA lacks jurisdiction to enforce settlement agreements made before the High Court.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
The CMA lacked jurisdiction to enforce the Deed of Settlement as such enforcement falls within the exclusive mandate of the High Court. The applicant's claims were therefore properly dismissed.
Obiter and limits
- Even if the settlement had been made before the CMA, it would still lack enforcement jurisdiction.
Court disposition
Application dismissed
- Application is dismissed for lack of merit
- No order as to costs
Source and reliance status
TANZLII · 1 January 2024
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 1 January 2024
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
DIVISHENI YA KAZI
DAR ES SALAAM MAREJEO NA. 5071 YA MWAKA 2024 KESI KUMBUKUMBU (REFERENCE) NA. 202403111000005071 WEMA MTENGW A.............. .............................. ................. MLETA MAOMBI DHID1 YA TANZANIA RAILWAY CORPORATION...........MJIBU MAOMBI WA KWANZA MWANASHERIA MKUU WA SERI K A LI................. MJIBU MAOMBI WA PILI
HUKUMII Tarehe ya amri ya mwisho: 07/ 05/2024 Tarehe ya hukumu: 31/ 05/2024 MLYAMBINA.J. Baada ya kutoridhishwa na Maamuzi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itajulikana kama Tume), Mleta Maombi amewasilisha maombi haya mbele ya Mahakama akijikita katika hoja zifuatazo: i. Kwamba, Muamuzi alishindwa kabisa kuoanisha ushahidi uliotolewa na pande zote mbili hivyo kufikia uamuzi usio sahihi na wa haki. ii. Kwamba, Muamuzi alishindwa kabisa kuona kuwa vielelezo vilivyotolewa na Mlalamikiwa vilikuwa havihusiani na kipindi cha madai na pia kushindwa kuona kuwa uhamisho wa Mleta Maombi na hatimaye kuachishwa kazi isivyo halali ni msingi wa ’’Deed o f Settlement". Kwamba, Muamuzi katoa uamuzi kutokana na hoja ambayo haikuwa sehemu ya madai ya Ml eta Maombi baada ya kutolewa kwa "Certificate of settlement/Non-Settlement" kutoka kwa Msuluhishi yaani fomu CMA F6. Kwamba madai yake yalikuwa "Retirement benefits and letter of retirement" yeye akaongeza hoja na kuitolea uamuzi unaopingwa sasa. Kwamba hoja hiyo ni: "endapo Mlalamikaji a/iajiriwa upya na shirika la TRL 2007 au alihamishiwa kutoka TRC". Mleta Maombi alieleza kuwa hoja tajwa hapo juu ilikuwa imeshatolewa uamuzi na Tume awamu ya kwanza pamoja na Mahakama na haikukatiwa rufaa na Mujibu Maombi. Aliongeza kuwa, kuipenyeza hoja hiyo kinyemela katika Mahakama ya chini ni kosa la kutokuheshimu maamuzi ya Mahakama za juu, hivyo Muamuzi
kujipachika mamlaka ya Marejeo ambayo si yake. Kwamba, Muamuzi alijielekeza vibaya kwa kushindwa kuona kwamba 'Deed of Settlement' haikurudishwa Tume kukaziwa hukumu kama anavyodai bali kama kielelezo cha kuwa Mleta Maombi hakupewa haki yake ya Barua ya kustaafu ili barua hiyo iainishe stahiki zake kwa kipindi cha 2007 hadi 2013 anachodai kutoka kwa Mwajiri wake wa zamani TRL ambaye aiirithiwa na TRC ya sasa ya awamu ya pili. v. Kwamba, Muamuzi ameshindwa kuona kwamba ushahidi na vielelezo vilivyopelekwa mbele yake na mjibu mombi vinaonesha kuwa TRC awamu ya pill inajificha nyuma ya TRC awamu ya kwanza kwa kuleta kumbukumbu za kale ambapo haya ni mashirika mawili kisheria yanayojitegemea yalioanzishwa na sheria tofauti. Hivyo, TRC awamu ya pili ilitegemewa kuleta vielelezo vya TRL kuthibitisha kuwa amelipwa au la ambapo ndiyo madai ya mleta maombi kipincli cha 2007 hadi 2013. Kutokana na hoja ainishwa hapo juu Mleta Maombi anaiomba Mahakama amri zifuatazo: i. Kwamba, Mahakama hii iweze kurejea na kutengua uamuzi wa Tume wa tarehe 25/08/2023 katika Shauri nambari CMA/DSM/ILA/880/19 ill Mleta Maombi aweze kusikilizwa na kuagiza Mwajiri wake ampatie barua ya kustaafu kama alivyoahidi katika Deed aliyotengeneza mwenyewe na ainishe stahiki za Mleta Maombi kwa mjibu wa kanuni za Kampuni zilivyokuwa kama mstaafu kwa sababu Muamuzi alishindwa kutoa uamuzi wa haki. ii. Kwamba, Mahakama
hii tukufu ione kwamba haki ya Mleta Maombi ya utumishi wake kutoka 2007 hadi 2013 ipo na walishakubaliana na Mwajiri wake wa zamani TRL ambaye alirithiwa na TRC awamu ya pili na kuandika makubaliano (Deed of Settlement) halali ambayo yalitekelezwa isipokuwa kipengele X ambacho bado. iii. Kwamba, Mahakama ione ikiwa kuna haki na stahiki nyingine anazostahili kupewa baada ya kunyimwa barua ya kustaafu katika utumishi wake TRL. Kama kuendelea kupokea mishahara tangu tarehe 01/07/2013 hadi 2015 waliandikiana Deed of Settlement kwa sababu Mwajiri alikataa kumrudisha kazini lakini anapinga utekelezaji wa Deed of Settlement. Mleta Maombi alisistiza kuwa anachodai ni kupewa barua ya kustaafu na kuainisha mafao yake. Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya mdomo. Katika kuendesha shauri hili, Mleta Maombi aliwakilishwa na Ndugu Sammy Katerega, Mwakilishi Binafsi, ilihali Mdugu Stephen Kimaro, Wakili wa Serikali na ndugu Hamimu Nkoleye, Wakili wa Serikali Mkuu waliwawakilisha Wajibu Maombi. Bwana Katerega alifanya mawasilisho ya jumla kwa hoja zote zilizoletwa mbele ya Mahakama hii. Alieleza kuwa, malipo ambayo yanadaiwa ni chanzo cha "Deed o f Settlement" iliyotengenezwa na Mwajiri ambayo haijakamilika utekelezwaji wake. Kwamba, Muamuzi baada ya kupokea FOMU Na. 6 aliongeza hoja ambayo siyo mahali pake ya kujielekeza juu ya kama Wema alijariwa au hakuajiriwa. Upande wa Wajibu Maombi
walipinga vikali maombi haya na kueleza kuwa maamuzi ambayo yanaombewa kurejewa tayari yametekelezeka, yameshalipwa na Mwombaji amekiri kwenye kiapo chake kuhusiana na utekelezaji wa Maamuzi hayo. Aliongeza kuwa baadhi ya malipo hayo yamethibitishwa kupitia kielelezo Dl, D2, D3 and D5. Kuhusiana na uhalali wa usahihi wa uamauzi wa CMA, ilielezwa kuwa malalamiko ni kutopewa barua ya kustaafu na mafao ya kustaafu. Ilielezwa kuwa Upande wa Mdaiwa walieleza wakati huo Mleta Maombi alikuwa si mtumishi wa TRL kwani alikuwa amepunguzwa. Hii ilipelekea Mwamuzi kujielekeza kwenye hoja, je kule TRL alikuwa kwenye ajira mpya au amehamishwa? Ikatokea hoja ya kuwepo kwa barua mbili. Moja ya kumpunguza kazi na nyingine ya kumhamisha. Alieleza kuwa, Mleta maombi alianza kwa kupokea barua ya uhamisho. Baadae akapata ya kupunguzwa kazi ambayo ilikuwa inaambatana na malipo. Yeye akapokea barua iliyoambatana na malipo na malipo akapokea na akadai anaendelea na kazi. Hiyo ni mojawapo ya hoja muhimu kwa Mwamuzi ambayo aliitolea maamuzi. Mahakama imezingatia kwa kina mawasilisho ya pande zote mbili. Katika fomu ya kuanzishia lalamiko Tume (CMA FI), Mleta Maombi ameeleza wazi kuwa anadai malipo yake ya kustaafu pamoja na barua ya kustaafu. Pia, katika maelezo yake ya awali mbele ya Tume, Mleta Maombi alifafanua kuwa anadai utekelezaji wa kifungu Namba X cha (Deed of settlement) cha masharti ya
makubaliano ya tarehe 23/03/2015. Lakini hata mbele ya Mahakama hii Mleta Maombi amesisitiza hayo ndiyo madai yake aliyowasilisha mbele ya Tume na ndio kiini cha mgogoro wake uliotakiwa kutatuliwa na Tume. Baada ya kupitia aina ya madai yake, Mahakama inaunga mkono maamuzi bishaniwa. Tume haikuwa na mamlaka ya kutekeleza Makubaliano hayo kwani yalifanywa mbele ya Mahakama Kuu. Huu ndio msimamo uliowekwa na sheria. Utekelezwaji wa Makubaliano husika au maamuzi mengine yoyote ya Mahakama Kuu utafanywa na Mahakama yenyewe kama ambavyo imeelekezwa katika Kifungu cha 48 (3) cha Kanuni za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Na. 106 la mwaka 2007. Naongeza kuwa, hata kama makubaliano hayo yangefanywa mbele ya Tume, Chombo hicho kisingekuwa na mamlaka ya kutekeleza makubaliano hayo kwani jukumu hilo ni la Mahakama kama ambavyo imeelekezwa katika Kifungu cha 89 (2) cha Sherla ya Ajira na Mahusiano Kazini, [Sura Namba 366 Kama Hivyorejewa mwaka 2019]. Pia, Mahakama imezingatia malalamiko ya Mleta Maombi kuwa, Mwamuzi alifanya makosa kutatua hoja ya endapo Mlalamlkaji allajlriwa upya na shirika la TRL 2007 au alihamlshlwa kutoka TRC. Mahakama inakubaliana na Mleta Maombi kuwa Tume ilikua haina sababu ya kujadili tena hoja hiyo kwani tayari ilishaamuriwa na pande zote mbili zikafikia makubaliano. Mleta Maombi anaomba utekelezaji wa sehemu ya makubaliano hayo. Hivyo basi, Mahakama inaona ya kuwa maombi haya hayana mantiki. Ni wazi kuwa Tume haikuwa na mamlaka ya kusikiliza mgogoro huu, hivyo ilikua sahihi kuutupilia mbali. Pia, Mahakama hii inatupilia mbali maombi haya kwakuwa hayana mantiki. Imeamuriwa hivyo. Y. J. MLYAM
JAJI 31/05/2024 Hukumu hii imesomwa na kutolewa leo tarehe 31/05/2024 mbele ya Mleta Maombi, Sammy Kateregga Mwakilishi Binafsi wa Mleta Maombi na Msomi Wakili wa Serikall Mathew Fuko kwa ajili ya Wajibu Maombi\
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.