YOHANA DAIMA MHENZE
The court upheld the parties' settlement, awarding the Ilangamoto plot to the applicant and confirming other District Court orders, except for the previous exclusive award of the Ilangamoto plot to the respondent, which was revoked.
Source-derived case information.
- Citation
- YOHANA DAIMA MHENZE
- Parties
- Applicant: Yohana Damian Mhanze; Respondent: Ezelina Aron Dugange
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2024
- Procedural Posture
- Divorce Appeal / Judgment
- Outcome
- appeal partly allowed
- Legal Topics
- Division of Matrimonial Property, Divorce, Settlement Agreements
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Yohana Damian Mhanze
Applicant
Ezelina Aron Dugange
Respondent
Procedural Posture
Divorce Appeal / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the District Court erred in awarding the Lyamkena house solely to the respondent without considering it as matrimonial property
- 2 Proper identification and division of immovable matrimonial assets
Ratio Decidendi
The court upheld the parties' settlement, awarding the Ilangamoto plot to the applicant and confirming other District Court orders, except for the previous exclusive award of the Ilangamoto plot to the respondent, which was revoked.
Court Disposition
appeal partly allowed
Orders
- The Ilangamoto plot is awarded to the applicant.
- The District Court's order awarding the Ilangamoto plot exclusively to the respondent is revoked.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (MASUALA NDOGO IRINGA) ILIYOPO IRINGA. (MM) RUFAA TALAKA NA. 5441 YA 2024 (Imetokana na Rufaa ya Talaka Na. 05/2023 ya Mahakama ya Wiiaya ya Njombe mbele ya Mhe. M. Kayombo, HMMr Asifia Shauri la Talaka Na. 14/2023 ya Mahakama ya Mwanzo ya Njombe iliyopo Makambako mbele ya Mhe. L. Gama, HM). YOHANA DAMIAN MHANZE .......... ............................. . MRUFANI DHIDI YA EZELINA ARON DUGANGE ......................... .............. . MRUFANIWA HUKUMU 08 & 08/04/2024 I.C. MUGETA, J: Rufaa hii ina sababu moja tu ya malalamiko dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Wiiaya. Kwamba, mahakama hiyo ilikosea kumpatia mrufaniwa nyumba iliyoko Lyamkena kama mali yake bfla kuzingatia nyumba hiyo ni chumo la ndoa lililotokana na juhudi za wanandoa wote. Mahakama ya Wiiaya iiigawa mali zisizohamishika za wadaawa ambazo ni chumo la ndoa kama ifuatavyo: i. Nyumba mbill ziiizoko Lyamkena moja igawanywe nusu kwa nusu baada ya kufanyiwa tathiminr na nyumba ya pili alipewa mrufaniwa. ii. Viwanja viwili vilivyoko Nzunguni, Dodoma na Lyamkena alipewa mrufani. iii. Kiwanja cha Ilangamoto alipewa mrufaniwa. Page 1 of 3 Rufaa ilipoitwa kusikilizwa Lazaro Hukumu, msomi wakili wa mrufaniwa alisema wadaawa wamekubaliana kumaliza mgogoro baina kwa mrufaniwa kumpa mrufani kiwanja kilichoko Ilangamoto ili asiendelee kudai haki zake katika nyumba ya Lyamkena. Mrufani alikiri makubaliano hayo na wadaawa waliomba niandike hukumu inayozingatia makubaliano hayo. Baada ya kupitia mwenendo wa shauri katika mahakama ya Mwanzo ya Wilaya Njombe iliyopo Makambako na Rufaa ya Mahakama ya Wilaya Njombe, nilibaini utambuzi wa mail zinazobishaniwa hauko thabiti. Hakuna maelezo ya utambuzi wa nyumba wala viwanja vinavyobishaniwa. Mali zote zimetajwa kwa maeneo zilipo pekee. Pia sehemu za Lyamkena au Ilangamoto hazikufafanuliwa zinakopatikana. Ndipo wadaawa walinifahamisha kuwa Lyamkena na Ilangamoto ni sehemu za Mji Mdogo wa Makambako Wilaya ya Njombe. Kwamba eneo ia Lyamkena limeshapimwa lakini Ilangamoto haijapimwa. Walikubali kwamba ni kweli wadaawa wanamiliki nyumba mbili eneo la Lyamkena. Nazo ziko uwanja (Plot) Na. 280, kitalu R na uwanja Na. 191 kitalu X. Walikubaliana pia kuwa nyumba anayolalamikia mrufani ni iliyoko uwanja Na. 2807 kitalu R. Hii ndio mahakama ya Wiiaya imemgawia mrufaniwa pekee na iliyobakia ndiyo imeamriwa wagawane nusu kwa nusu. Page 2 of 3 Kwa kuzingatia matakwa ya wadaawa nimeamua kwamba kiwanja cha Ilangamoto kitakuwa mali ya mrufani. Amri ya Mahakama ya Wilaya ya kukigawa kwa mrufaniwa pekee yake nimeifuta. Amri nyingine za mahakama ya wilaya nimezithibitisha. Nimetafakari yaliyojiri kwenye rufaa hii fikra zimenijia kwamba ni muhimu kwa waamuzi baada ya kutoa amri ya kuvunja ndoa, tuwe tunatoa fursa kwa wadaawa kutoa maoni yao juu ya namna bora ya kugawana mali zao. Mahakama iingilie tu pale ambapo hawawezi kukubaliana na ionyeshwe hivyo kwenye kumbukumbu za shauri. Pengine hili lingefanyika huenda rufaa hii isingeufikia mlango wa Mahakama Kuu. Pia, mali zisizohamishika zitambuliwe kwa alama za utambuzi wake kwa kufafanuliwa kinagaubaga. I.C. MUGETA JAJI 8 / 4/2024 Mahakama: Hukumu hii imesomwa wakiwepo mrufani na Lazaro Hukumu, msomi wakili wa mrufaniwa bila mrufaniwa. Isw. I.C. MUGETA JAJI 8 / 4/2024 Page 3 of 3