Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 2005
This section says the law is being amended, including the Constitution, the preamble, and Articles 3, 18, 19, 20, 21, 24, 37, and 59.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Act or statute
- Citation
- Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 2005
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section says the law is being amended, including the Constitution, the preamble, and Articles 3, 18, 19, 20, 21, 24, 37, and 59. This section states that amendments are to be made to Articles 66, 74, 78, and 107A. This section lists constitutional amendments, including changes to several articles and the addition of new Articles 110A and 120A. This section gives the Act’s title. Sehemu hii inasema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inabadilishwa kwa namna iliyoelezwa katika Sheria hii.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 2005
Showing 35 of 35
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This section says the law is being amended, including the Constitution, the preamble, and Articles 3, 18, 19, 20, 21, 24, 37, and 59.
1. Jina la Sheria. SEHEMU YA PILI K u f a n y a M a b a d i l i k o k w e n y e K a t i b a Kufanya mabadiliko katika Katiba. Kufanya mabadiliko katika UTANGULIZI. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 3. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 18. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 19. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 20. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 21. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 24. K ufinya mabadiliko katika Ibara ya 37. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 59.
Part
SEHEMU YA PILI
- 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: This section states that amendments are to be made to Articles 66, 74, 78, and 107A.
16. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 66. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 74. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 78. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 107A. 309 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - 25 Verify source ↗
Section 25
AI-assisted research summary: This section lists constitutional amendments, including changes to several articles and the addition of new Articles 110A and 120A.
25. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 109. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 110. Kuongeza Ibara mpya ya 110A. Kufanya mabadiliko katika Sehemu ya Tatu ya Sura ya Tano. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 116. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 118. Kufanya mabadiliko katika Ibara 120. Kuongeza Ibara mpya ya 120A. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 151. 310 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katibci ya 2005 Jam huriya Muungano wa Tanzania Na. 1 ya 2005 N akubali BENJAMIN W. M K A PA , Rais 6 Api ili, 2005 Sheria ya M abadiliko ya K um i na Nne K atika K atiba ya J a m h u ri ya M uungano wa Tanzania. IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SEHEMU YA KWANZA U t a n g u l i z i - 2 Verify source ↗
Masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya
AI-assisted research summary: Sehemu hii inasema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inabadilishwa kwa namna iliyoelezwa katika Sheria hii.
2. Masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977, ambayo katika mafungu yafuatayo ya Sheria hii itaitwa kwa kifupi “Katiba”, yanabadilishwa kwa namna ilivyoelezwa katika vifungu vya Sheria hii. Kufanya mabadilikQ katika Katiba - 3 Verify source ↗
Sehemu ya “UTANGULIZI” katika Katiba inayohusu “MISINGI
AI-assisted research summary: This provision amends the Constitution’s introductory section on basic principles by deleting a full stop at the end of the third paragraph and adding the words “na isiyokuwa na dini”.
3. Sehemu ya “UTANGULIZI” katika Katiba inayohusu “MISINGI YA KATIBA” inafanyiwa mabadiliko kwa kufuta nukta mwishoni mwa aya ya tatu na k u o n g eza m aneno “ na isiy o k u w a na d in i” . - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This section amends Article 3 of the Constitution by inserting the words “isiyokuwa na dini” after the word “kijamaa”.
4. Ibara ya 3 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko katika ibara ndogo ya (1) kwa kuweka maneno “isiyokuwa na dini,” mara baada ya neno “kijamaa”. Kufanya mabadiliko katika Utangulizi Kufanya mabadiliko katika ibara ya 3 311 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kufanya Mabadiliko katika Ibara ya 18 - 5 Verify source ↗
Ibara ya 18 ya Katiba inafutwa na kuandikwa upya kama ifuatavyo
AI-assisted research summary: Section 5 says Article 18 of the Constitution is repealed and rewritten.
5. Ibara ya 18 ya Katiba inafutwa na kuandikwa upya kama ifuatavyo: - 18 Verify source ↗
Kila mtu
AI-assisted research summary: Everyone has the right to hold and express opinions, seek and share information, communicate freely, avoid interference with communications, and receive important public information at all times.
18. Kila mtu: “ U h u'r u wa maoni (a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake; (b) anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi; (c) anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake; na (d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu m atukio m balim bali m uhim u k w a m a is h a n a shughuli za w a n a n ch i na pia kuhusu m asuala muhimu kwa jam ii.” - 6 Verify source ↗
Ibara ya 19 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko
AI-assisted research summary: Section 6 amends Article 19 of the Constitution by replacing subsection (2), inserting a new subsection (3), and renumbering the existing subsection (3) as subsection (4).
6. Ibara ya 19 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko: (a) kwa kuifuta Ibara ndogo ya (2) na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jam bo la hiari ya mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.” (b) kwa kuongeza Ibara ndogo ya (3) mara tu baada ya Ibara ndogo ya (2) kama ifuatavyo: “(3) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika ibara hii itakuwa chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jam ii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili ya jam ii na umoja wa kitaifa." (c) kwa kuitaja Tbara ndogo ya (3) iliyopo kuwa Ibara ndogo ya (4). - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Kila mtu ana uhuru wa kukutana, kushirikiana, kuzungumza hadharani, na kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika; pia mtu hawezi kulazimishwa kujiunga na chama au shirika lolote, na chama cha siasa hakiwezi kusajiliwa ikiwa katiba au sera yake ina malengo yaliyokatazwa.
7. Ibara >>a 20 ya K a tib a in a fa n y iw a m ab a d ilik o : (a) kwa kuifuta Ibara ndogo ya (1) na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(1) Kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na 312 Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 19 Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 20 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha na kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.” (b) kwa kuifuta Ibara ndogo ya (2) na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(2) Bila ya kujali masharti ya Ibara ndogo ya (1) na ya (4), h aitak u w a h alali kw a cham a ch o ch o te cha siasa kuandikishwa ambachp kutokana na katiba au sera yake- (a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya (1) (11) (hi) imani au kundi lolote la dini; kundi lolote la kikabila, mahali watu watokeapo, rangi au jinsia; eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano; (b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano; (c) (d) (e) k in a k u b a li au k u p ig an ia m atum izi ya nguvu au m apam bano kama n j i a z a kufikia m alengo yake y a kisiasa; kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano; hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia.” (c) kwa k uifuta Ibara n dogo y a (4 ) na kuiandika upya k ama ifuatavyo: “(4) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au shirika lolote au kwa chama chochote cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa ya chama hicho”. - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This section changes Article 21(1) by replacing the words “ya 5” with “ya 47” after the number “39”.
8. Ibara ya 21 inafanyiwa mabadiliko katika Ibara ndogo ya (1) kwa kufuta maneno “ya 5,” yaliyopo kwenye mstari wa kwanza na kisha kuweka maneno “ya 47” mara baada ya tarakimu ya “39”. 313 Kufanya Mabadiliko katika Ibara ya Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 24 Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 37 - 9 Verify source ↗
Ibara ya 24 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko kwa kuifuta Ibara
AI-assisted research summary: Kila mtu ana haki ya kumiliki mali na kupata ulinzi wa mali yake kwa mujibu wa sheria.
9. Ibara ya 24 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko kwa kuifuta Ibara ndogo ya (1) na kuiandika upya kama ifuatavyo: “ Haki ya k u mi l i k i mal' (1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.” - 10 Verify source ↗
Ibara ya 37 inafanyiwa mabadiliko
AI-assisted research summary: This provision amends section 37 and updates how presidential functions are carried out when the President or Vice President is unavailable.
10. Ibara ya 37 inafanyiwa mabadiliko- (a) katika ibara ndogo ya (2) kwa kufuta tarakim u “ (3 )” inayoonekana kwenye mstari wa mwisho na kuweka badala yake tarakimu “(5)”. (b) kwa kufuta maneno ya utangulizi katika ibara ndogo ya (3) na kuandika upya kama ifuatavyo: “(3) Endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano au atashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu nyingine yoyote, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmojawapo ya wafuatao kwa kufuata mpangilio ufuatao, yaani-” (c) kwa kufuta ibara ndogo ya (4 ) na kuandika upya kam a ifuatavyo: “(4) E ndapo Waziri M kuu ndiye atatekeleza kazi n a shughuli za Rais kutokana na sababu kwamba Makamu wa Rais hayupo basi Waziri Mkuu ataacha kutekeleza kazi na shughuli hizo endapo lolote kati ya mambo yafuatayo likitokea mwanzo- (a) Rais atakaporejea katika Jamhuri ya Muungano au atakapopata nafuu kutokana na maradhi na kuanza kutekeleza kazi za Rais; (b) Makamu wa Rais atakaporejea katika Jamhuri ya Muungano.” (d) Kwa kuongeza katika ibara ndogo ya (6) maneno “ au haw ezi k u m u d u k a z i zake” m ara baada ya m aneno “Jam huri y a M uungano yaliyopo katika m an en o ya utangulizi”. 314 r Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: This section amends Article 59 by deleting subsection (2) and replacing it with a new rule on who may be appointed Attorney General.
11. Ibara ya 59 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko kwa kuifuta ibara ndogo ya (2) na kuiandika upya kama ifuatavyo- “(2) M wanasheria Mkuu wa Serikali atateuliwa kutoka miongoni mwa watumishi wa umma wenye sifa ya kufanyakazi za wakili au watu wenye sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.” Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 59 - 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: This provision amends the Constitution by adding Articles 59A and 59B after Article 59.
12. Katiba inafanyiwa mabadiliko kwa kuongeza Ibara za 59A na 59B mara tu baada ya Ibara ya 59 kama ifuatavyo: “Naibu M wana sheria Mkuu wa Serikali - 59A Verify source ↗
{1) Kutakuwa na Naibu Mwanasheria
AI-assisted research summary: Rais lazima amteue Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka kwa watu wanaostahili chini ya Ibara ya 59(2) na waliokidhi sifa hizo kwa angalau miaka 10 mfululizo.
59A.-{1) Kutakuwa na Naibu Mwanasheria Mkuu w a S erikali atakayeteuliw a n a R a is k utoka m iongoni m wa w atu w enye sifa zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (2) ya Ibara ya 59 na amekuwa na sifa hizo fnfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi. ' • Kuongeza Ibara mpya za 59A na 59B (2) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakuwa msaidizi mkuu katika kutekeleza kazi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali na atafanya kazi nyingine kam a a takavyoelekezw a na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” - 59B Verify source ↗
(1) Kutakuwa na M kurugenzi wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Mashtaka huteuliwa na Rais na anaweza kuendesha na kusimamia mashtaka yote nchini.
59B.-(1) Kutakuwa na M kurugenzi wa Mashtaka ambaye atateuliwa na Rais, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (2) ya Ibara ya 59 na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi. (2) Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa na uwezo wa kufungua, kuendesha na kusimamia mashtaka yote nchini. (3) Mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) yaweza kutekelezw a n a y eye m w enyew e au kwa maelekezo yake na maofisa waliopo chini yake, au wengineo wanaotekeleza kazi hizo kwa maelekezo yake. 315 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: This section amends constitutional rules on the Director of Public Prosecutions and parliamentary membership requirements.
13. ya (1): Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 66 (4) K atika kutekeleza m am laka yake, M kurugenzi wa M ashtaka a takuw a huru, hataingiliwa na mtu yeyote au na mamlaka yeyote na atazingatia mambo yafuatayo- (a) nia ya kutenda haki; (b) kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki; na (c) maslahi ya umma. (5) Mkurugenzi wa Mashtaka atatekeleza mamlaka yake kama ilivyoelekezw a katika sheria yoyote iliyotungwa au itakayotungwa na Bunge.” Ibara ya 66 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko katika ibara ndogo (a) kwa kuifuta aya ya (b) na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(b) W abunge w anaw ake wa id ad i isiyopungua asilimia thelathini ya wabunge wote waliotaj wa katika aya za (a), (c), (d), (e) na (f) wenye sifa zilitajwa katika Ibara ya 67 watakaochaguliwa na vyama vya siasa kwa mujibu wa Ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa kura;” (b) kwa kuifuta aya ya (e) na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais k u to k a m io n g o n i m w a w atu w enye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za Ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa wanawake;” (c).kwa kuongeza aya ya (f) mara baada ya aya ya (e) kama ifuatavyo: “(f) Spika, iwapo hatakuwa amechaguliwa kutoka miongoni mwa Wabunge” 316 * r * Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 74 Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 78 - 14 Verify source ↗
Ibara ya 74 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko
AI-assisted research summary: This section amends Article 74 so that the Chairperson and Vice Chairperson must be a High Court or Court of Appeal judge, or a person qualified as an advocate with at least 15 years of such qualifications.
14. Ibara ya 74 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko: (i) katika ibara ndogo ya (1) kwa kuifuta aya ya (a) na kuiandika upya kama ifuatavyo: (a) Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani au ni mtu mwenye sifa ya kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano; (b) Makamu wa Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa M ahakam a K uu a u M ahakama ya Rufani au ni m tu mwenye sifa ya kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.” - 15 Verify source ↗
Ibara ya 78 inafanyiwa mabadiliko kwa kuifuta ibara ndogo ya
AI-assisted research summary: Ibara hii inabadilisha Ibara ya 78 ili vyama vya siasa vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu, vikifikia angalau asilimia 5 ya kura halali za wabunge, viwasilishe majina ya wanawake kwa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
15. Ibara ya 78 inafanyiwa mabadiliko kwa kuifuta ibara ndogo ya (1) na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(1) Kwa m ad h u m u n iy a uchaguzi wa Wabunge wanawake waliotajwa katika ibara ya 66(1 )(b), vyama vya siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu kwa kufuata utaratibu uliowekwa, na kupata angalau asilimia tano ya kura zote halali za wabunge, vitapendekeza kwa Tume ya Uchaguzi majina ya wanawake kwa kuzingatia uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi wa Wabunge. (2) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), zifuatazo zitahesabiwa kuwa ni kura halali za M bunge aliyepita bila kupingwa katika jim bo la uchaguzi: (a) endapo cham a k im e m sim a m ish a mgombea Urais, kura zilizopigwa katika jimbo kwa mgombea Urais wa chama cha Mbunge huyo; au (b) endapo cham a h a k ik u m sim a m ish a mgombea Urais, asilimia hamsini na moja y a k u ra z a w a tu wote w aliojiandikisha kupiga kura katika jim bo hilo.” 317 V - * Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 107 A Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 109 - 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: This section says subsection (1) of section 107A is repealed and rewritten so that the Court is the final authority for the administration of justice in the United Republic.
16. Ibara ndogo ya (1) ya Ibara ya 107A inafutwa na kuandikwa upya kama ifuatavyo: “(1) Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jam huri y a M uungano itakuwa ni Mahakama”. - 17 Verify source ↗
Ibara ya 109 inafanyiwa mabadiliko kwa
AI-assisted research summary: This provision amends Article 109 to change the High Court judge appointment rules, qualifications, and the Chief Justice’s powers.
17. Ibara ya 109 inafanyiwa mabadiliko kwa:- (a) kufuta ibara ndogo ya (1) na ya (2) na kuandika badala yake ibara ndogo ifuatayo:” “ Majaji vva Mahakama Kuu na utcuzi wao i09.-(l) Kutakuwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu (ambaye katika Ibara zi fuatazo kwenye Katiba hii atataj wa tu kwa kifupi kama “ Jaji K io n g o zi” ) na M ajaji w engine wa M ahakam a K uu w a sio p u n g u a th ela th in i watakaoteuliwa na Rais baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama.” (b) kuzitaja upya ibara ndogo za (3), (4), (5), (6), (7), (8), (9), (10), (11) na (12) kuwa (2), (3), (4), (5), (6), (7), (8), (9), (10) na (11). (c) kuzifuta tarakimu (3) na (4) zilizomo katika mstari wa pili na maneno “kuwakilisha” yaliyomo katika mistari ya saba na kumi na mbili katika ibara ndogo ya (4) kama ilivyotaj wa upya ili ibara ndogo hiyo isomeke kama ifuatavyo: “(4) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi au utekelezaji wa masharti ya ibara ndogo ya (2 ) na y a (3) y a Ibara h ii, inatamkwa rasmi h ap a kwam ba i sipokuwa kama masharti ya K atib a h ii a u ya sh eria nyingine yoyote yameagiza vingine, Jaji Mkuu atakuwa na uwezo wa kutoa kwa Jaji Kiongozi mara kwa mara maagizo au maelekezo kuhusu utendaji wa kazi na shughuli zake kama Mkuu wa M ahakama Kuu; vile vile, Jaji M kuu atakuwa n a uw ezo wa kukasim u k w a Jaji Kiongozi baadhi ya madaraka yake ya uongozi na usimamizi juu ya utekelezaji wa kazi katika 318 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mahakama Kuu na Mahakama nyinginezo zote za ngazi ya chini yake, na kila inapohitajika, J a ji M kuu anaw eza k u te k e le z a yeye mwenye we moja k w a m o ja madaraka yake yoyote aliyoyakasimu kwa Jaji Kiongozi.” (d) kufuta tarakimu ya “(9 )” na ya “(8)” zilizopo katika mstari wa kwanza na wa tatu na neno “mitano” lililomo katika mstari wa tano wa ibara ndogo ya (6) kama ilivyoitwa upya ili sasa isomeke kama ifuatavyo: “(6) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo y a (8) ya Ibara hii, m tu aw eza tu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa ana sifa maalum, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (7) ya Ibara hii, na awe mtu am baye am ekuw a na m o jaw ap o ya sifa maalum kwa muda usiopungua miaka kumi.” (e) kufuta tarakimu ya “(7)”, “(9)” na ya “(11)” zilizopo katika mstari wa kwanza na wa pili wa ibara ndogo ya (7) kama ilivyotajwa upya na kuweka badala yake tarakimu “(6)”, (8)” na ya “(10)”; (f) kuifuta ibara ndogo ya (7) kama ilivyotajw a upya na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(7) kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara ndogo za (6), (8) na (10) ya Djara hii, sifa maalumu maana yake ni mtu aliye na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na mamlaka ya ithibati Tanzania na- (a) amekuwa hakimu; (b) amefanya kazi katika utumishi wa umma akiwa na sifa za kufanya kazi ya u w a k ilia u ni w akili wa kujitegem ea; (c) ana sifa ya kusajiliwa kuwa wakili, na, amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.” (g) kuifuta ibara ndogo ya (8) kama ilivyotajwa upya na kuiandika upya kama ifuatavyo: Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “(8) Iwapo Rais atatosheka kwam ba ijapokuwa mtu mwenye sifa mojawapo ya hizo sifa maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwa muda usiopungua miaka kumi, lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu na kuna sababu za kum fanya mtu huyo astahili kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutengua lile sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka kumi na baada ya kushauriana na Tume ya U tum ishi wa Mahakama, Rais aweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.” (h) kuifuta tarakimu “(11)” iliyomo katika mstari wa pili wa ibara ndogo ya (11) kama ilivyoitwa upya na kuiweka badala yake tarakimu “(10)”; (i) kuifuta aya ya (b) ya ibara ndogo ya (10) kama ilivyoitwa upya na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(b) kwa madhumuni ya kumteua Kaimu Jaji kwa m ujibu w arn asharti ya ibara h ii ndogo, Rais anaweza kutengua lile sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka kumi kwa sababu kama zile zilizotajwa katika ibara ndogo ya (8) ya Ibara hii”. - 18 Verify source ↗
Ibara ya 110 inafanyiwa mabadiliko kama ifuatavyo
AI-assisted research summary: Jaji wa Mahakama Kuu anaweza kustaafu baada ya kufikisha miaka 55, isipokuwa kama Rais ataamuru asistaafu.
18. Ibara ya 110 inafanyiwa mabadiliko kama ifuatavyo: (a) Kwa kuifuta ibara ndogo ya (2) na kuiandika upya kama ifuatavyo: “(2) Jaji yeyote wa Mahakama Kuu anaweza kustaafu kazi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wakati wowote baada ya kutim iza umri wa m iaka ham sini na tano, isipokuwa kama Rais ataagiza kwamba asistaafu, na iwapo Rais ataagiza hivyo, basi huyo Jaji atakayehusika na m aagizo hayo ya Rais hatakuwa na haki ya kustaafu mpaka upite kwanza muda wowote utakaotajwa na Rais kwa ajili hiyo.” 320 K u f a n y a mabadiliko k a t i k a Ibara ya 110 \ » . • Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (b) kwa kuzifuta ibara ndogo za (5), (6), (7), (8) na (9). - 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: This provision says the Constitution is being amended by adding a new article.
19. Katiba inafanyiwa mabadiliko kwa kuongeza Ibara mpya ya Kuongeza ya - 10A Verify source ↗
Section 10A
AI-assisted research summary: Utaratibu wa kumwondoa Jaji wa Mahakama Kuu unaanza na uchunguzi wa Tume iliyo teuliwa na Rais, na Rais anaweza kumsimamisha kazi Jaji wakati wa uchunguzi.
10A. 110A mara tu baada ya Ibara ya 110 kama ifuatavyo: “Utaratibu wa kushughu- likia nidhamu ya Majaji wa Mahakama Kuu 110A-(1) U taratibu w a kushughulikia nidhamu ya Majaji, kwa sababu mbali na zile zilizoainishw a k a tik a ib ara ndogo y a (2), utakuwa kama utakavyoelekezwa na Sheria itakayotungwa na Bunge. (2) Jaji wa M ahakam a K uu aw eza tu kuondolewa katika m adaraka ya kazi kw a sababu y a kushindwa kutekeleza kazi yake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kw a sababu ya tabia m baya mayoathiri maadili ya kazi ya Jaji au sheria ya maadili ya viongozi wa umma; na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya Ibara hii. (3) Iwapo R ais anaona kuwa suala la kumwondoa Jaji kazini lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:- (a) Rais anaweza baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kumsimamisha kazi Jaji huyo; (b) Rais atateuaTume ambayo itakuwa na M w en y ek iti na W ajum be wengine wasiopungua wawili. Na huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya W ajumbe wengine w a Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni M ajaji wa M ahakam a K uu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola; 321 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (c)T u m e h iyo i tachunguza s hauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu m aelezo ya shauri lolote na itamshauri Rais kama huyo Jaji anayehusika a o n d o le w e k a z in i kwa m ujibu wa m asharti ya Ibara hii kw a sababu ya k u sh in d w a k u fa n y a k a z i k u to k a n a na m a ra d h i au s a b a b u n y in g in e yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya. (4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri R ais kw am ba Jaji am baye hab ari zake zim echunguzw a n a h iy o Tume aondolew e kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na m aradhi au sab ab u nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini Jaji huyo anayehusika na utumishi wa Jaji huyo utakuwa umekoma. (5) Ikiwa suala la kumwondoa Jaji kazini lim epelekw a kw enye T u m e kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo y a ( 3 ) ya Ibara hii, R a is anaw eza kumsimamisha kazi Jaji huyo anayehusika, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi Jaji huyo, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatiiika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba Jaji huyo asiondolewe kazini. (6) Mashsrti ya Ibara hii yatatumika bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (11) ya Ibar3 ya 109 ya Katiba hii.” Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - 20 Verify source ↗
Section 20
AI-assisted research summary: This section amends the Constitution by deleting the text of Part Three of Chapter Five and rewriting it as stated.
20. Katiba inafanyiwa mabadiliko kwa kuyafuta maelezo ya Sehemu ya Tatu ya Sura ya Tano na kuyaandika upya kam a ifuatavyo: “SEHEMU YATATU TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA Kufanya mabadiliko katika Sehemu ya Tatu ya Sura ya Tano - 112 Verify source ↗
( 1) Kutakuwa na Jum e ya Ushauri wa Uteuzi wa Majaji
AI-assisted research summary: A Judicial Service Commission is established for appointing judges and serving magistrates, with specified members and appointment rules.
112.-( 1) Kutakuwa na Jum e ya Ushauri wa Uteuzi wa Majaji na Ajira ya Mahakimu wa Mahakama za Tanzania Bara ambayo katika Katiba hii itaitwa “Tume ya Utumishi wa M ahakama”. Tume ya Utumishi wa Mahakama (2) Wajumbe wa Tume hiyo watakuwa: Jaji Mkuu ambaye atakuwa Mwenyekiti; (a) (b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali; (c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa atakayeteuliwa kwa ajili hiyo na Rais baada ya kushauriana na Jaji Mkuu; Jaji Kiongozi; na (d) (e) Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Rais. (3) Mtu hataweza kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume kwa mujibu wa masharti ya aya ya (e) ya ibara ndogo ya (2) ya Ibara hii ikiwa mtu huyo ni Mbunge au ni mtu mwenye madaraka ya ain a n y in g in e yoyote i liyotajw a kwa a jili hiyo n a sheria iliyotungwa na Bunge.” (4) K atika kutekeleza m ajukum u yake, Tum e yaw eza kukasimu kazi zake kwa Kamati mbalimbali zitakazoundwa kwa mujibu wa Sheria itakayotungwa na Bunge. - 113 Verify source ↗
(1) Majukumu ya Tume yatakuwa ni
AI-assisted research summary: Tume must advise the President on judicial appointments, discipline, and pay, recruit magistrates, and form committees; the President holds appointment and discipline powers for judges and registrars, and Parliament may set implementation conditions.
113.-(1) Majukumu ya Tume yatakuwa ni- (a) kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu; (b) kumshauri Rais kuhusu masuala ya nidhamu ya majaji; (c) kumshauri Rais kuhusu mishahara na maslahi ya majaji; (d) (e) (f) kumshauri Rais kuhusu uteuzi na nidhamu kwa ajili ya Msaj ili wa Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu; kuajiri mahakimu na kusimamia nidhamu yao; kuunda kamati mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake. 323 Majukumu na madaraka ya Tume Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2) Madaraka ya uteuzi, kudhibiti nidhamu na ya kuwaondoa kazini majaji yatakuwa mikononi mwa Rais kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii. (3) Madaraka ya uteuzi, kuwathibitisha kazini, kudhibiti nidhamu na ya kuwaondoa kazini Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu yatakuwa mikononi mwa Rais. (4) Madaraka ya kuajiri, kuwathibitisha kazini, kudhibiti nidhamu na kuw aondoa kazini mahakimu w a mahakama z a Tanzania B ara yatakuwa mikononi mwa Tume iliyotajwa katika Ibara ya 112. (5) B unge linaweza kutunga sheria itakayow eka m asharti y a utekelezaji wa majukumu ya Tume. Uanachama katika vyama vya siasa. - 113A Verify source ↗
Section 113A
AI-assisted research summary: Hakimu na maafisa fulani wa mahakama hawaruhusiwi kujiunga na chama cha siasa, lakini wanahifadhiwa haki ya kupiga kura.
113A. Itakuwa ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu, Msajili wa Mahakama ya ngazi yoyote, hakimu wa ngazi yoyote kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika Ibara ya 5 ya Katiba hii.” - 21 Verify source ↗
(1) Ibara ya 116 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko
AI-assisted research summary: This provision changes Article 116 of the Constitution by deleting subsection (1) and renumbering subsections (2) and (3) as subsections (1) and (2).
21.-(1) Ibara ya 116 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko: (a) kwa kufuta ibara ndogo ya (1); na (b) kuzitaja ibara ndogo za (2) na (3) kuwa ibara ndogo za (1) na (2). - 22 Verify source ↗
Section 22
AI-assisted research summary: This provision amends Article 118 and replaces its text with new wording about judges of the Court of Appeal and their appointment.
22. Ibara ya 118 ya Katiba inafanyiwa mabadiliko: (a) kwa kuifuta Ibara hiyo na kuiandika upya kama ifuatavyo: “Majaji wa Mahakama ya Rufani na uteuzi wao. - 118 Verify source ↗
(1) K utakuw a n a Jaji M kuu wa
AI-assisted research summary: The President appoints the Chief Justice and other Court of Appeal judges, and may appoint acting judicial officers in stated situations.
118.-(1) K utakuw a n a Jaji M kuu wa M ahakama (ambaye katik a Ibara zifuatazo kwenye Katiba atatajwa tu kwa kifupi kama “Jaji Mkuu”) na Majaji wengine wa Rufani wasiopungua wanne, isipokuwa kwamba kikao maalum cha Mahakama nzima kitak '•milika kam a k itak u w a na M ajaji wa Cufani wasiopungua watano. 324 Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 1 1 6 Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 1 1 8 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuwa Jaji wa Rufani n a atakuwa ndiye Kiongozi wa M ahakam a ya R ufani na p ia M kuu wa Mahakama kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 116 ya Katiba na atashika madaraka ya Jaji Mkuu mpaka atakapotimiza umri wa kustaafu kama Jaji wa Rufani, isipokuwa kama: (a) atajiuzulu; au (b) kiti chake kitakuwa wazi kutokana na maradhi au kifo; (c) atavuliwa wadhifa wa Jaji Mkuu na Rais. (3) Majaji wengine wa Rufani watateuliwa na Rais, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu w enye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano zilivyoainishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sh e ria z in a z o tu m ik a Z a n z ib a r na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano. (4) Iwapo itatokea kwamba:- (a) Kiti cha Jaji Mkuu kitakuwa wazi; au (b) Jaji Mkuu hayupo Tanzania; au (c) Jaji Mkuu atashindwa kutekeleza kazi yake kwa sababu yoyote, na, Rais ataona kuwa kwa muda wa tukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua Kaimu Jaji Mkuu, basi Rais anaweza kumteua Kaimu Jaji Mkuu kutoka miongoni mwa Majaji wa Rufani. Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (5) Kaimu Jaji Mkuu atatekeleza kazi za Jaji Mkuu mpaka atakapoteuliwa Jaji Mkuu m w ingine au m paka Ja ji M kuu am baye alikuwa hayupo Tanzania au alikuwa hamudu kazi zake atakaporejea kazini. (6) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji wa Rufani kitakuwa wazi au endapo Jaji wa Rufani yeyote atateuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu au kama Jaji wa Rufani atashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, au Jaji Mkuu atamshauri Rais kuwa kazi za Mahakama ya Rufani ilivyo wakati huo zahitaji ateuliwe Kaimu Jaji wa Rufani, basi Rais aweza, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kumteua Kaimu Jaji wa Rufani kutoka miongoni mwa watu ambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Rufani kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya Ibara hii. (7) Mtu yeyote atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Rufani ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji w a Rufani kwa muda w ow ote utakaotajwa wakati wa kuteuliwa kwake, au, endapo muda haukutajwa, mpaka uteuzi wake utakapofutwa na Rais, lakini bila ya kujali kwamba muda wake wa kazi umemalizika au kwamba uteuzi wake u m efutwa, mtu huyo anaweza kuendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Rufani mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe shughuli nyingine yoyote i nayohusika na rufaa au am bayo m ash au ri m en g in e alikw ishaanza kuyasikiliza k abla ya muda wake wa kazi haujamalizika au uteuzi wake haujafutwa. y o y o te (8) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (1) ya Ibara hii na Ibara ya 119 ya Katiba h ii, inatam kw a rasm i hapa kw am ba mtu aliyeteuliwa kuwa K aim u Jaji wa Rufani atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Rufani na atatekeleza kazi zote za Jaji wa Rufani na Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba idadi ya Majaji iliyotajwa katika Ibara ya 122 ya Katiba hii, haitaathirika kwa sababu tu mmoja au zaidi ya Majaji wa Rufani katika kikao chochote ni Kaimu Jaji wa Rufani. (9) Ofisi ya Jaji wa Rufani haitafutw a wakati yupo mtu aliyeshika madaraka ya kiti cha Jaji wa Rufani.”; (b) kufuta maneno “ya Tanzania” popote yalipo katika Ibara ya - 23 Verify source ↗
Section 23
AI-assisted research summary: This section says Section 120 is repealed and rewritten with new wording.
23. Ibara ya 120 inafutwa na kuandikwa upya kama ifuatavyo:- “ Muda wa Utumishi wa Majaji wa Rufani - 120 Verify source ↗
(1) Kila Jaji wa Rufani atalazimika
AI-assisted research summary: Jaji wa Rufani lazima aache kazi akiwa na miaka 65, lakini anaweza kustaafu kuanzia miaka 60 isipokuwa Rais aagize vinginevyo.
120.-(1) Kila Jaji wa Rufani atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini na tano, lakini masharti ya Ibara hii ndogo yatatumika bila kuathiri masharti yafuatayo katika ibara hii. Kufanya mabadiliko katika Ibara ya 120 (2) Jaji yeyote wa Rufani aweza kustaafu kazi ya Ujaji wa Rufani wakati wowote baada ya kutimiza umri wa miaka sitini, isipokuwa kama R ais a taagiza k wamba a sistaafu, n a iwapo Rais ataagiza hivyo, basi huyo Jaji wa Rufani atakayehusika na maagizo hayo ya Rais hatakuwa na haki ya kustaafu mpaka upite kwanza muda wowote utakaotajwa na Rais kwa ajili hiyo. (3) Iwapo Rais ataona kuwa kwa ajili ya m a n u fa a y a u m m a in a fa a Jaji wa Rufani aliyetim iza um ri wa m iak a sitini n a tano aendelee kufanya kazi, na Jaji huyo wa Rufani anakubali kwa maandishi kuendelea kufanya kazi, basi Rais aweza kuagiza kuwa Jaji huyo wa Rufani aendelee kufanya kazi kwa muda wowote utakaotajwa na Rais. (4) Bila ya kujali kwamba Jaji wa Rufani ametimiza umri ambao analazimika kuacha kazi kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii, mtu anayefanya kazi ya Jaji w a Rufani aw eza 327 Na. 1 Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya 2005 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (b) kufuta na kuandika upya maneno: “Jaji Mkuu” maana yake ni Jaji Mkuu aliyetajwa, kuteuliwa na ambaye majukumu yake yameelekezwa katika Ibara ya 118 ya Katiba.” (c) Kufuta maneno “Idara ya” katika tafsiri ya maneno “Jaji Mkuu wa Zanzibar” na vile vile katika ibara ndogo ya (2) ya Ibara ya 4 ya Katiba.” Umepitishwa na Bunge tarehe 7 Februari, 2005 D am ia n S. F o k a , Katibu wa Bunge 329
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Sheria hii itaitwa Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika
AI-assisted research summary: This section gives the Act’s title.
1. Sheria hii itaitwa Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 2005. Jina la Sheria SEHEMU YA PILI K u f a n y a M a b a d i l i k o k a t i k a K a t i b a
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria ya Mabadiliko ya Kumi na Nne Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka, 2005
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in