Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024
This section gives the Act’s title and says it will start to apply on a date appointed by the Minister by notice in the Government Gazette.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Act or statute
- Citation
- Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the Act’s title and says it will start to apply on a date appointed by the Minister by notice in the Government Gazette. Sheria hii inatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, isipokuwa masuala ya uchaguzi wa Madiwani ambayo yanatumika Tanzania Bara pekee. This section defines key terms used in the Act, including “constituency,” “Constitution,” “member,” “Director of Elections,” “Chairperson,” “President,” “Commission,” “election,” and “Minister.” The provision establishes the Electoral Commission of the United Republic, also called the Independent National Electoral Commission. Kifungu hiki kinaweka muundo wa Tume na utaratibu wa Rais kuwateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024
Showing 27 of 27
- 1 Verify source ↗
2. Matumizi
AI-assisted research summary: This section gives the Act’s title and says it will start to apply on a date appointed by the Minister by notice in the Government Gazette.
1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024 na itaanza kutumika katika tarehe ambayo Waziri atateua kwa notisi katika Gazeti la Serikali. Matumizi Tafsiri - 2 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: Sheria hii inatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, isipokuwa masuala ya uchaguzi wa Madiwani ambayo yanatumika Tanzania Bara pekee.
2. Sheria hii itatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, isipokuwa kwa masuala yanayohusu uchaguzi wa Madiwani, itatumika Tanzania Bara. - 3 Verify source ↗
Tafsiri
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the Act, including “constituency,” “Constitution,” “member,” “Director of Elections,” “Chairperson,” “President,” “Commission,” “election,” and “Minister.”
3. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “jimbo” maana yake ni jimbo la uchaguzi kwa madhumuni 3 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 ya uchaguzi wa Wabunge; Sura ya 2 “Katiba” maana yake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; “Mjumbe” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuwa mjumbe wa Tume kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba; “Mkurugenzi wa Uchaguzi” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 17 na itajumuisha mtu ambaye kwa kipindi hicho atakuwa anatekeleza majukumu yoyote ya ofisi hiyo; “Mwenyekiti” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuongoza Tume na inajumuisha Makamu Mwenyekiti; “Rais” maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; “Tume” maana yake ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba; “uchaguzi” maana yake ni uchaguzi wa Rais, Wabunge na inajumuisha uchaguzi mdogo wa Madiwani na Mbunge au Diwani; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na masuala ya uchaguzi. SEHEMU YA PILI KUANZISHWA, MUUNDO NA MAJUKUMU YA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI Kuanzishwa kwa Tume Muundo wa Tume
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Kuanzishwa kwa Tume
AI-assisted research summary: The provision establishes the Electoral Commission of the United Republic, also called the Independent National Electoral Commission.
4. Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ambayo pia itajulikana kama “Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi”. - 5 Verify source ↗
Muundo wa Tume
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka muundo wa Tume na utaratibu wa Rais kuwateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine.
5.-(1) Tume itakuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine watano watakaoteuliwa na Rais. (2) Rais atateua wajumbe wa Tume kama ifuatavyo: (a) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume majina miongoni kutoka mwa 4 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 yatakayopendekezwa na Kamati ya Usaili kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 74(1)(a) na (b) na (2) ya Katiba na kanuni zitakazotengenezwa chini ya Sheria hii; na (b) Wajumbe wengine wa Tume kutoka miongoni mwa majina yatakayowasilishwa na Kamati ya Usaili baada ya kufanyiwa usaili. (3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais. (4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano. (5) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Katibu na Mtendaji Mkuu wa Tume. - 6 Verify source ↗
Hadhi ya Tume
AI-assisted research summary: Tume lazima iwe huru na isifuate maagizo ya wengine; pia inaweza kumiliki mali, kushtaki au kushtakiwa, na kufanya mambo ya chombo huru.
6.-(1) Tume chombo huru na itakuwa ni kinachojitegemea na uamuzi wake hautaingiliwa na chombo chochote au kulazimika kufuata maagizo ya mtu yeyote au Idara yoyote ya Serikali au maoni ya chama chochote cha siasa. (2) Tume itakuwa ni chombo chenye uwezo wa kumiliki mali na kuwa na nembo na lakiri yake, na kwa jina lake Tume inaweza- (a) kujipatia na kumiliki mali zinazoweza kuhamishika na zisizoweza kuhamishika; (b) kushtaki au kushtakiwa; na (c) kufanya au kutekeleza masuala yoyote ambayo yanaweza kufanywa au kutekelezwa na chombo huru. (3) Pale ambapo Tume imeshtaki au kushtakiwa, itapaswa kumtaarifu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili awe sehemu ya shauri hilo kwa lengo la kukidhi masharti ya Sheria ya Uendeshaji wa Mashauri dhidi ya Serikali. itakuwa Hadhi ya Tume Sura ya 5 Sifa za wajumbe wa Tume - 7 Verify source ↗
Sifa za wajumbe wa Tume
AI-assisted research summary: The Commission’s chairperson or vice chairperson must be a High Court or Court of Appeal judge, or a qualified advocate with at least 15 years’ standing. The other five members must meet listed qualification requirements.
7.-(1) Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Tume atapaswa kuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya 5 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 Sura ya 357 Rufani au kuwa na sifa ya kuwa Wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano. (2) Wajumbe wengine watano watakuwa na sifa zifuatazo: (a) awe raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Tanzania; (b) awe mtu mwaminifu na mwadilifu; (c) awe na uzoefu katika uongozi, utawala au masuala ya uchaguzi; na (d) awe mtu anayeweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Muda wa utumishi wa wajumbe - 8 Verify source ↗
Muda wa utumishi wa wajumbe
AI-assisted research summary: Mjumbe wa Tume hutumikia kwa miaka mitano, na anaweza kuacha wadhifa au kuondolewa chini ya hali fulani.
8.-(1) Mjumbe wa Tume atashika nafasi ya madaraka kwa kipindi cha miaka mitano. (2) Mjumbe wa Tume atakoma kuwa Mjumbe endapo litatokea lolote kati ya mambo yafuatayo: (a) ukimalizika muda wa miaka mitano tangu alipoteuliwa; (b) ikiwa atafariki; (c) endapo atajiuzulu; (d) ikiwa litatokea jambo asingekuwa Mjumbe wa Tume, asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume; au lolote ambalo, kama lingemfanya Sura ya 398 (e) ikiwa ataondolewa madarakani na Rais. (3) Rais anaweza kumuondoa madarakani mjumbe wa Tume kutokana na- (a) mjumbe kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya maradhi au sababu nyingine yoyote; (b) tabia mbaya inayoathiri maadili ya kazi ya mjumbe wa Tume au inayokiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; au (c) kupoteza sifa ya kuteuliwa kuwa mjumbe. (4) Endapo suala la kumuondoa Mjumbe wa Tume litajitokeza, Rais anaweza kuunda Kamati itakayofanya uchunguzi na kumshauri ipasavyo. (5) Kamati iliyorejewa chini ya kifungu kidogo cha (4) itajumuisha wajumbe wafuatao: (a) Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye atakuwa Mwenyekiti; 6 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 (b) Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; (c) Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma; (d) Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Zanzibar; (e) wajumbe wawili wenye uzoefu wa masuala ya uchaguzi, mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine kutoka Tanzania Zanzibar; na (f) Mjumbe mmoja kadri Rais atakavyoona inafaa kwa kuzingatia jinsia. (5), (6) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi atateua mtumishi wa umma mwandamizi kuwa Katibu wa Kamati. (7) Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Uchunguzi itajiwekea utaratibu wa kujiendesha. Kamati ya Usaili - 9 Verify source ↗
Kamati ya Usaili
AI-assisted research summary: The President must convene an Interview Committee when Commission members need to be appointed, and the Committee must run the selection process and report names to the President.
9.-(1) Wakati wowote inapobidi kuteuliwa mjumbe au wajumbe wa Tume, Rais ataitisha Kamati ya Usaili. (2) Kamati itakayoitishwa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni Mwenyekiti; (b) Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti; (c) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; na (d) mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais kwa kuzingatia jinsia. (3) Katibu wa Kamati ya Usaili atakuwa afisa mwandamizi katika utumishi wa umma atakayeteuliwa na Rais. (4) Wajumbe wa Kamati ya Usaili wataapa mbele ya Rais kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao. (5) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kuundwa, Kamati ya Usaili itatoa tangazo kwa umma kupitia magazeti angalau mawili yenye wigo mpana wa usambazwaji nchini na vyombo vingine vya habari kuwaalika wananchi wenye nia ya kuomba kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume kuwasilisha maombi yao kwenye 7 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 Kamati. (6) Kamati ya Usaili mara baada ya kupokea na kuchambua maombi ya watu walioomba kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume, itafanya usaili na kupendekeza kwa Rais majina ya watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume. (7) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (6) na kifungu cha 5(2), utaratibu wa kusimamia- (a) mchakato wa upatikanaji wa majina yatakayopendekezwa kwa ajili ya uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti; na (b) mchakato wa usaili wa wajumbe wengine wa Tume, utakuwa kama utakavyoainishwa katika kanuni. (8) Kamati ya Usaili itawasilisha kwa Rais majina manne zaidi ya idadi ya nafasi zinazohitajika kujazwa. (9) Muda wa Kamati ya Usaili utakoma mara baada ya Rais kuteua wajumbe wa Tume. Majukumu ya Tume - 10 Verify source ↗
Majukumu ya Tume
AI-assisted research summary: The Commission is responsible for managing and coordinating voter registration and several elections, and it may delegate its duties or parts of them to specified Commission staff.
10.-(1) Kwa kuzingatia matakwa ya Ibara za 74(6), 75 na 78 za Katiba, Tume itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano na uchaguzi wa Madiwani kwa Tanzania Bara; (b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge na uchaguzi wa Madiwani kwa Tanzania Bara; (c) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa serikali za vijiji, mitaa na vitongoji Tanzania Bara kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa katika Sheria itakayotungwa na Bunge; (d) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge; (e) kuteua na kuwatangaza Wabunge Wanawake wa Viti Maalumu katika Jamhuri ya Muungano na Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu kwa Tanzania Bara; (f) kuandaa na kusimamia Kanuni za Maadili ya 8 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 Sura ya 298 Maadili katika utendaji kwa wajumbe Sura ya 398 Vikao vya Tume Uchaguzi; (g) kutoa elimu ya mpiga kura nchini; (h) kuratibu na kusimamia taasisi na asasi zinazotoa elimu ya mpiga kura; (i) kualika na kusajili waangalizi wa uchaguzi; (j) kuajiri au kuteua watumishi na watendaji wa Tume kwa kadri itakavyohitajika kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Utumishi wa Umma na masharti mengine yatakayowekwa na Tume; na (k) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama sheria yalivyoainishwa kwenye Katiba au nyingine yoyote. (2) Tume inaweza kukasimu majukumu au sehemu ya majukumu yake kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, mtumishi au mtendaji mwingine wa Tume. - 11 Verify source ↗
Maadili katika utendaji kwa wajumbe
AI-assisted research summary: Kila Mjumbe wa Tume lazima azingatie Sheria ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma na kanuni za maadili zitakazotungwa chini ya Sheria hii.
11. Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu ya Tume, kila Mjumbe wa Tume atalazimika kuzingatia Sheria ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma na Kanuni za Maadili zitakazoandaliwa chini ya Sheria hii. - 12 Verify source ↗
Vikao vya Tume
AI-assisted research summary: The Commission must hold at least four ordinary meetings a year, and it may hold special meetings when needed.
12.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 74(7) ya rasmi kuhusu Katiba, Tume itafanya uamuzi wake utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao. (2) Tume itakuwa na vikao vya kawaida visivyopungua vinne kwa mwaka. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (2), Tume inaweza kufanya vikao maalumu muda wowote itakapoonekana kuwa ni lazima kufanya hivyo. (4) Tume itafanya vikao vyake katika sehemu na muda utakaopangwa na Tume. (5) Mwenyekiti atahakikisha kuwa kila mjumbe wa Tume anapewa taarifa ya kikao mapema kabla ya kikao hicho kufanyika. (6) Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, Mwenyekiti ataongoza vikao vyote vya Tume na endapo Mwenyekiti hatakuwepo, Makamu Mwenyekiti ataongoza, au ikiwa wote wawili hawapo, wajumbe waliopo wanaweza kumchagua mjumbe mmoja miongoni mwao atakayekuwa 9 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 mwenyekiti wa muda wa kikao husika. Akidi katika vikao vya Tume Uamuzi wa Tume - 13 Verify source ↗
Akidi katika vikao vya Tume
AI-assisted research summary: A Commission meeting has a quorum only if at least four members are present.
13. Akidi ya kikao chochote cha Tume itakuwa si chini ya wajumbe wanne. - 14 Verify source ↗
Uamuzi wa Tume
AI-assisted research summary: Maamuzi ya kikao cha Tume hupitishwa kwa kuungwa mkono na wajumbe wengi, na mwenyekiti au mwenyekiti wa muda anaweza kutumia kura ya turufu endapo kura zinalingana.
14.-(1) Uamuzi wa kikao chochote cha Tume utafikiwa kwa kuungwa mkono na Wajumbe walio wengi. uamuzi kufikiwa (2) Pale ambapo katika kikao chochote cha Tume italazimu kura, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au mwenyekiti wa muda atakayekuwa anaongoza kikao atakuwa na kura ya turufu zaidi ya kura yake ya kawaida inapotokea kulingana kwa kura zilizopigwa. kupigiwa kwa Posho na stahili za wajumbe wa Tume - 15 Verify source ↗
Posho na stahili za wajumbe wa Tume
AI-assisted research summary: Wajumbe wa Tume wana haki ya kulipwa posho, stahili nyingine, na kiinua mgongo baada ya kumaliza muda wao wa ujumbe.
15.-(1) Wajumbe wa Tume watalipwa posho na stahili nyingine kwa mujibu wa Sheria, kanuni, taratibu na miongozo itakayotolewa na mamlaka husika. (2) Wajumbe wa Tume watalipwa kiinua mgongo baada ya kumaliza muda wa ujumbe wa Tume. Uhusiano kati ya Tume na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar - 16 Verify source ↗
Uhusiano kati ya Tume na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
AI-assisted research summary: Tume must regularly consult the Zanzibar Electoral Commission while carrying out its duties.
16. Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 74(13) ya Katiba, katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania Zanzibar. SEHEMU YA TATU SEKRETARIETI YA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI Mkurugenzi wa Uchaguzi
Part
SEHEMU YA TATU
- 17 Verify source ↗
Mkurugenzi wa Uchaguzi
AI-assisted research summary: Section 17 says there must be a Director of Elections, appointed by the President after recommendation from the Commission.
17.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume. (2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo: Sura ya 357 (a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Tanzania; (b) awe ni mtu mwaminifu na mwadilifu; (c) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria; na (d) awe afisa mwandamizi katika utumishi wa umma. 10 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 Maadili ya utendaji kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Sura ya 398 - 18 Verify source ↗
Maadili ya utendaji kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Uchaguzi lazima aape mbele ya Rais kabla ya kuanza kazi na azingatie sheria na kanuni za maadili za viongozi wa umma.
18. Mkurugenzi wa Uchaguzi ataapa mbele ya Rais kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake na atalazimika kuzingatia Sheria ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma na Kanuni za Maadili zitakazoandaliwa chini ya Sheria hii. Majukumu ya Mkurugenzi wa Uchaguzi - 19 Verify source ↗
Majukumu ya Mkurugenzi wa Uchaguzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Uchaguzi ndiye mtendaji mkuu wa Tume na lazima atekeleze majukumu yake ya kila siku na majukumu mengine yaliyoorodheshwa.
19.-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Mtendaji Mkuu na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Tume. (2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Afisa Masuuli wa Tume na atatekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu za fedha. (3) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yafuatayo: (a) kuandaa na kuratibu vikao vya Tume; (b) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura; (c) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi; (d) kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Tume katika kutekeleza majukumu yake; (e) kuandaa bajeti na kalenda ya shughuli za Tume; (f) kuweka kumbukumbu za vikao vya Tume; (g) kutayarisha nyaraka mbalimbali za Tume; (h) kushirikiana na taasisi za ndani na nje ya nchi ambazo zinafanya kazi zinazohusu uchaguzi, demokrasia na utawala bora; (i) kusimamia miongozo kwa watendaji wa uchaguzi kama kutekeleza majukumu yao katika itakavyoagizwa na Tume; (j) kusimamia rasilimali watu na mali za Tume; (k) kufanya tafiti zinazohusiana na uchaguzi; na (l) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama atakavyoagizwa na Tume kwa mujibu wa Sheria hii. (4) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni watumishi wa sifa kwa kadri umma au watu wengine wenye itakavyohitajika. Watumishi na watendaji wa - 20 Verify source ↗
Watumishi na watendaji wa Tume
AI-assisted research summary: Watu walioajiriwa, kuteuliwa au kuazimwa na Tume wanachukuliwa kuwa watumishi wa Tume na wanapaswa kuzingatia sheria husika wakati wanatekeleza majukumu ya Tume.
20.-(1) Kwa madhumuni ya Sheria hii, mtumishi 11 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 Tume Sheria Na. 1 ya 2024 aliyeajiriwa, aliyeteuliwa au aliyeazimwa na Tume, kwa kipindi chote atakachokuwa anatekeleza majukumu ya Tume, atachukuliwa kuwa ni mtumishi wa Tume na atatakiwa kuzingatia Katiba, Sheria hii, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na sheria nyingine yoyote inayohusu utekelezaji wa majukumu ya Tume. (2) Mtu yeyote aliyeajiriwa kwa madhumuni ya kutekeleza majukumu ya Tume, ikiwa hajaajiriwa katika utumishi wa umma, atapokea malipo yanayostahili kwa kazi hiyo kadri Tume itakavyoona inafaa kuidhinisha. Fedha za uendeshaji wa Tume Gharama kulipwa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali SEHEMU YA NNE MASHARTI YA FEDHA
Part
SEHEMU YA NNE
- 21 Verify source ↗
Fedha za uendeshaji wa Tume
AI-assisted research summary: The Commission’s operating funds come from the Government budget.
21. Fedha za uendeshaji wa shughuli za Tume zitatoka katika bajeti ya Serikali. vinavyohitajika - 22 Verify source ↗
Gharama kulipwa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali
AI-assisted research summary: Certain election-related costs are charged to and paid from the Consolidated Fund of the Government.
22. Gharama zote- (a) zilizotumika katika kuandaa daftari, kutoa kadi ya mpiga kura na kufanya mambo mengine au vitu vingine kwa madhumuni ya kutekeleza masharti ya Sheria hii; na Tume, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na mtu mwingine kutekeleza majukumu ya uchaguzi; (b) zilizotumiwa aliyeajiriwa kufanywa yeyote (c) zilizotumika kwa ajili ya malipo ya maafisa walioainishwa katika kifungu cha 20(2); na (d) zilizotumika kwa ajili ya malipo kwa afisa yeyote wa umma kuhusu shughuli rasmi zinazohusu au zinazotokana na uchaguzi, zitatozwa na kulipwa kutoka kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali. Hesabu na ukaguzi Sura ya 348 - 23 Verify source ↗
Hesabu na ukaguzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Uchaguzi lazima atunze vitabu vya hesabu na kumbukumbu za shughuli za Tume na aandike taarifa ya hesabu ya mwaka; hesabu za Tume zitakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
23.-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatunza vitabu vya hesabu na kumbukumbu nyingine zinazohusu shughuli za Tume na kuandaa taarifa ya hesabu ya mwaka kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma. (2) Hesabu za Tume zitakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. 12 Na. 2 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 Taarifa ya mwaka - 24 Verify source ↗
Taarifa ya mwaka
AI-assisted research summary: Tume lazima iandae na kuwasilisha taarifa ya mwaka ndani ya miezi mitatu baada ya mwaka wa fedha kuisha, na taarifa hiyo ipelekwe kwa Waziri kwa ajili ya kuiwasilisha Bungeni.
24.-(1) Ndani ya miezi mitatu baada ya kuisha kwa mwaka wa fedha, Tume itaandaa taarifa ya mwaka kuhusiana na mwaka wa fedha uliopita na kuwasilisha taarifa hiyo kwa Waziri ambaye ataiwasilisha Bungeni. (2) Taarifa ya mwaka itajumuisha- (a) maelezo ya kina kuhusu utendaji wa Tume kwa mwaka husika; (b) nakala ya hesabu za Tume zilizokaguliwa pamoja na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; na (c) taarifa nyingine yoyote ambayo Tume itahitajika kutoa chini ya Sheria hii. SEHEMU YA TANO MASHARTI MENGINEYO Muundo wa Utumishi wa Sekretarieti ya Tume
Part
SEHEMU YA TANO
- 25 Verify source ↗
Muundo wa Utumishi wa Sekretarieti ya Tume
AI-assisted research summary: Tume lazima, baada ya kushauriana na Waziri mwenye dhamana na masuala ya utumishi, iandae Muundo wa Utumishi wa Sekretarieti ya Tume.
25. Tume kwa kushauriana na Waziri mwenye dhamana na masuala ya utumishi, itaandaa Muundo wa Utumishi wa Sekretarieti ya Tume. Kanuni na miongozo Masharti ya mpito - 26 Verify source ↗
Kanuni na miongozo
AI-assisted research summary: Tume inaweza kutengeneza kanuni na miongozo na kutoa maelekezo ili kuboresha utekelezaji wa majukumu yake.
26. Tume inaweza kutengeneza kanuni na miongozo na kutoa maelekezo kwa ajili ya utekelezaji bora wa majukumu yake. - 27 Verify source ↗
Masharti ya mpito
AI-assisted research summary: Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe wa Tume ataendelea kushika madaraka yake baada ya Sheria kuanza kutumika hadi uanachama wake utakapoisha.
27. Mara baada ya kuanza kutumika kwa Sheria hii, mtu yeyote ambaye ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe wa Tume ataendelea kushika madaraka hayo hadi pale ujumbe wake utakapokoma. Imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 2 Februari, 2024. NENELWA JOYCE MWIHAMBI Katibu wa Bunge 13
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in