The Budget Act, 2015
This section gives the Act’s title and says it starts to apply on 1 January 2015.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Act or statute
- Citation
- The Budget Act, 2015
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- mul
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the Act’s title and says it starts to apply on 1 January 2015. This law applies in Tanzania Bara (Mainland Tanzania). This section defines key terms used in the Act. Serikali na taasisi za umma lazima zizingatie misingi ya usimamizi mzuri wa fedha; Waziri pia lazima ahakikishe misingi hiyo inazingatiwa katika taarifa zinazoandaliwa kwa Bunge. Serikali inaweza kuacha kuzingatia misingi hiyo tu ikiwa Waziri ataweka sababu, mpango wa utekelezaji na kipindi, na vionyeshwe mbele ya Bunge kwa kupitishwa kabla ya utekelezaji. The Plan and Budget must set budget objectives while considering the listed economic and fiscal criteria.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of The Budget Act, 2015
Showing 78 of 78
- 1
This section gives the Act’s title and says it starts to apply on 1 January 2015.
1. Sheria hii itaitwa Sheria ya Bajeti ya mwaka, 2014 na itaanza kutumika tarehe 1 Januari, 2015. - 2
This law applies in Tanzania Bara (Mainland Tanzania).
2. Sheria hii itatumika Tanzania Bara. Jina na tarehe ya kuanza kutumika Matumizi 55 56 Tafsiri Sura 348 No.11 Budget 2015 - 3
This section defines key terms used in the Act.
3. Katika Sheria hii, isipokuwa pale ambapo muktadha utahitaji vinginevyo- “Mhasibu Mkuu wa Serikali”atakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa katika Sura 348 “Afisa Masuuli” atakuwa na maana kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Sheria ya Fedha ya Umma; Sura 2 Fedha ya Umma; “Sheria ya kuidhinisha matumizi ya fedha” maana yake ni sheria inayohusu matumizi ya fedha za umma kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ajili ya usambazaji wa huduma ndani ya mwaka wa fedha; “bajeti” maana yake ni makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka mzima na yanajumuisha misaada kwa Serikali za mitaa ambayo imewasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuidhinishwa; “mzunguko wa bajeti” maana yake matukio yanayofuatana yanayoonyesha muda wa utakaotumika katika maandalizi ya bajeti kuanzia uandaaji, uidhinishaji, utekelezaji, usimamiaji na utoaji taarifa; “taarifa ya utekelezaji” maana yake ni moja kati ya taarifa nyingi ambazo zinawasilishwa Bungeni na waziri chini ya kifungu cha 51; “mfuko wa dharura” maana kama ilivyotafsiriwa katika Katiba; “Katiba” maana yake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; “kuidhinisha matumizi ya fedha” maana yake ni idhini iliyotolewa na Bunge chini ya Sheria ya kuidhinisha matumiz ya fedha, kuruhusu malipo kufanyika kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina au mfuko wowote wa Serikali ulioanzishwa chini ya sheria yoyote kwa masharti maalum; “wakala wa asasi zilizo nje ya mfumo wa bajeti” maana yake idara zinazoendeshwa nje ya bajeti ya Serikali; “mwaka wa fedha” maana yeke ni, kuhusiana na: (a) Serikali kuu, kipindi cha miezi kumi na mbili kinachoishia tarehe 30 Juni, ya kila mwaka; (b) Serikali za mitaa, ili iliyotafsiriwa kwenye Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa; (c) mamlaka ya umma au taasisi zingine, kipindi kilichobainishwa ndani ya sheria husika au nyaraka zinazohusiana na mamlaka hiyo au taasisi au kipindi kitakachowekwa na mamlaka yenye mamlaka kwa mamlaka hiyo ya umma au taasisi; 56 No.11 Budget 2015 57 “Serikali” maana yake ni Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretariati za mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa; “Waziri” maana yake ni Waziri anayehusika na masuala ya fedha; “miswada ya fedha” maana yake ni Muswada wa Fedha, muswada wa matumizi au muswada mwingine wowote ambao unaweka utaratibu wa masuala ya kifedha; “mwaka wa fedha” maana yake ni, kuhusiana na: (a) Serikali kuu, kipindi cha miezi kumi na mbili kinachoisa tarehe 30 Juni ya kila mwaka; na (b) mamlaka ya umma au taasisi zingine, kipindi kilichobainishwa ndani ya sheria husika au nayaraka zinazohusiana na mamlaka hiyo au taasisi au kipindi kitakachowekwa na mamlaka yenye mamlaka hiyo ya umma au taasisi; “misingi ya usimamizi mzuri wa fedha” maana yake ni misingi ya fedha za umma kama ilivyobainishwa katika Sheria ya fedha za Umma na ile iliyorejewa katika kifungu cha 4 cha Sheria hii; “Mpango na Miongozo ya Bajeti” maana yake ni mwongozo wa mpango na bajeti iliyorejewa katika sheria hii; “mwaka ujao wa fedha” maana yake ni kipindi kinachoanzia tarehe 1 Julai ya mwaka mwingine na kuishia tarehe 30 Juni, ya mwaka unaofuata; “Mlipaji Mkuu wa Serikali” maana yake afisa aliyepewa mamlaka ya kusimamia fedha za umma kwa mafiasa masuuli na ambaye kwa mamlaka yake atazingatia maelekezo ya Waziri, atasimamia fedha za umma katika Wizara na Idara za Serikali na kufanya kazi nyinginezo kama itakavyoainishwa katika kanuni. “Katibu Mkuu” maana yake ni Katibu Mkuu Hazina; “taasisi ya umma” maana yake ni wakala, mamlaka na taasisi zote za umma ikijumuisha mashirika ya umma; “fedha za umma” zinajumuisha: (a) mapato ya umma ya Jamhuri ya Muungano; (b) amana au fedha yoyote ambayo imetunzwa kwa muda au vinginevyo na afisa kwa nafasi yake ya kiofisi, aidha peke yake au kwa pamoja na mtu mwingine, awe afisa au la; 57 58 No.11 Budget 2015 “jumuiya za kiuchumi za kikanda” zinajumuisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Soko la pamoja la Afrika Mashariki na Kusini wa Afrika na Jumuiya nyinginezo za kiuchumi; “sheria ya matumizi ya ziada” maana yake ni sheria yoyote ambayo lengo ambayo ni kuongeza matumizi kwenye matumizi lake yalishaidhinishwa kwenye sheria ya matumizi; Sura 370 “Msajili wa Hazina” maana yake kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Msajili wa Hazina (kazi na mamlaka). SEHEMU YA PILI MUUNDO WA MFUMO WA UCHUMI JUMLA NA BAJETI Misingi ya sera za bajeti
Part
SEHEMU YA PILI
- 4
Serikali na taasisi za umma lazima zizingatie misingi ya usimamizi mzuri wa fedha; Waziri pia lazima ahakikishe misingi hiyo inazingatiwa katika taarifa zinazoandaliwa kwa Bunge. Serikali inaweza kuacha kuzingatia misingi hiyo tu ikiwa Waziri ataweka sababu, mpango wa utekelezaji na kipindi, na vionyeshwe mbele ya Bunge kwa kupitishwa kabla ya utekelezaji.
4.-(1) Serikali na taasisi za umma, katika malengo ya sera zao, itazingatia misingi ya usimamizi mzuri wa fedha. (2) Misingi ya usimamizi mzuri wa fedha itajumuisha- (a) sera ya kukopa ambayo inahakikisha umma kwamba madeni yake yanahimilika; (b) sera za bajeti ambazo zitasaidia kufanikisha na kudumisha kiwango maalum cha tahadhari ili kuwa katika hali nzuri ya kibajeti siku za usoni; (c) kupunguza athari za kibajeti kwa nchi kwa mujibu wa dhamana za mikopo, wajibu katika pensheni na madeni yasiyolipwa; (d) sera ya mishahara inayohimilika, kuvutia, inayoendana na inayohakikisha kuwepo kwa ukubwa wa uchumi, na wafanyakazi wenye tija; (e) sera izinazohakikisha kuwepo kwa mabadiliko ya wastani katika kiwango na uhakika wa viwango vya kodi; (f) mfumo na bajeti ya Taifa yenye kuzingatia uwazi, uwajibikaji na usimamizi mzuri wa uchumi ma sekta binafsi; (g) vipaumbele katika matumizi yenye tija badala ya matumizi yasiyo na tija katika mgawanyo wa rasilimali na (h) kuzingatia dhana ya mgawanyo wa mamlaka kwa kuhakikisha kwamba Bunge tu katika usimamizi wa rasilimali za umma kama ilivyobainishwa na Katiba na sheria nyingine yoyote. linashirikishwa 58 No.11 Budget 2015 59 (3) Waziri atahakikisha kwamba misingi ya usimamizi mzuri wa fedha inazingatiwa wakati wa kuandaa na kutoa taarifa Bungeni juu ya mambo yote yanayotakiwa kutolewa taarifa chini ya Sheria hii. (4) Serikali inaweza kutozingatia misingi ya usimamizi mzuri wa fedha kama Waziri- (a) ataeleza sababu za kutozingatia misingi hiyo ikijumuisha mpango wa utekelezaji na kipindi ambacho Serikali itakuwa haizingatii misingi ya usimamizi mzuri wa fedha; na (b) atawasilisha sababu, mpango wa utekelezaji na kipindi cha kutokuzingatia misingi hiyo mbele ya Bunge kwa ajili ya kupitishwa kabla utekelezaji wa sera ya usimamizi wa fedha. (5) Ukiukwaji wa malengo ya kibajeti utapimwa na kutolewa maelezo katika Mwongozo wa uandaaji Mpango na Bajeti wa mwaka unaofuata. Malengo ya sera za bajeti - 5
The Plan and Budget must set budget objectives while considering the listed economic and fiscal criteria.
5. Mpango na Bajeti utabainisha malengo ya bajeti kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo- (a) kuhamasisha uhimilivu wa uhakika wa uchumi jumla na ukuaji wa uchumi shirikishi usiokuwa na mfumuko wa bei; (b) kuanzisha na kuweka mfumo himilivu wa kibajeti na athari ndogo za deni la Taifa; (c) kuweka wa ukomo wa kibajeti utakaozuia mapungufu katika masuala ya fedha ikiwemo mikopo; (d) kuweka kiwango cha kutosha cha akiba ya Taifa kuwezesha uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi; na (e) kuwa na uhimilivu na uhakika katika masuala ya fedha. Matarajio ya uchumi jumla na bajeti - 6
The budget and macroeconomic planning program for part of the financial year must include specified economic review and forecasting activities.
6. Programu bajeti na uundaji wa uchumi jumla unaotumika kwa ajili ya sehemu ya mwaka wa fedha kama nyenzo ya uandaaji wa mfumo wa uchumi jumla pamoja na mpango na bajeti utahusisha- (a) kutathmini mwenendo wa uchumi wa dunia na athari zake kwenye uchumi wan chi; (b) kuandaa makisio ya muda wa kati ya uchumi jumla na matarajio ya mwaka ujao wa fedha; 59 60 No.11 Budget 2015 (c) kuandaa uchumi jumla wa muda wa kati utakaotumika kwa ajili ya kuandaa mpango na bajeti; (d) kuandaa mahitaji yanaohusu uchumi jumla na matarajio ya bajeti kwenye nayraka za mpango na bajeti ya taifa; na (e) kubainisha majuku ya waziri kutoa matarajio ya uchumi jumla na bajeti kwa kuzingatia muda wa kati. Uratibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa - 7 Verify source ↗
Short title and commencement
Serikali na Taasisi za Umma lazima ziandae bajeti za mwaka kwa kuzingatia mipango ya muda wa kati na muda mrefu, na bajeti hizo ziwezelezwe kwenye mpango wa maendeleo wa taifa.
7.-(1) Serikali na Taasisi za Umma zitaandaa bajeti zao za mwaka kwa kuzingatia mpango wa muda wa kati na muda mrefu. (2) Bajeti itakayoandaliwa chini ya kifungu kidogo cha (1) itajielekeza kwenye kutekeleza mpango wa maendeleo wa taifa. (3) Wakati wa kuandaa bajeti chini ya kifungu hiki, Serikali na Taasisi za Umma hazotjumuishwa kwenye bajeti zao, mradi wowote ambao haukuorodheshwa kwenye mpango wa maende wa Taifa. (4) Serikali na Taasisi za Umma zitakahkikisha kwamba- (a) mipango ndiyo iliyoidhinishwa ya maendelo pekee inatekelezwa; (b) mahitaji ya kifedha ya mpango wa maendelo wa taifa yanarandana na kiwango cha ukomo kilichonyeshwa kwenye mpango wa bajeti iliyoelezwa kwenye sheria hii; (c) miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa vipaumbele; (d) utaratibu wa kutekeleza bajeti ya maendeleo na matumizi, unaanzishwa; (e) utaratibu wa kupitia upya mradi wowote mpya wa maendeleo kabla ya kuanza utekelezaji wake, unaanzishwa; (f) miradi ya maendeleo inaidhinishwa na Tume ya Mipgango kabla haijajumuishwa kwenye bajeti; (g) ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kuchangia na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kupitia ubia baina ya sekta binafsi na umma; (h) vigezo vya juibua vyanzo vya mapato ya serikali za mitaa, vinawekwa; (i) upangaji wa madaraja ya serikali za mitaa kwa jaili ya mipango na ugawaji fedha, unafanyika; 60 No.11 Budget 2015 61 (j) muda kwa ajili ya kukandaa na kusambaza mpango na bajeti unawekwa; na (k) vigezo ambavyo kwayo fedha itagawiwa kwa ajili ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo, vinawekwa. SEHEMU YA TATU USIMAMIZI WA MCHAKATO WA BAJETI Majukumu ya Bunge
Part
SEHEMU YA TATU
- 8
Bunge must carry out several budget and fiscal management duties, and it must follow sound public financial management principles when doing so.
8.-(1) Bunge litakuwa na majukumu yafuatayo- (a) kujielekeza kwa makadirio ya awali na mpango wa uchumi jumla na programs; (b) kujadili na kupitia upya mpango na makisio ya bajeti; (c) kusimamia masuala yote ya kibajeti yanayoingia kwenye mamlaka ya Bunge; taarifa (d) kuchambua zingine zilizowasilishwa kwake na kutoa maoni kwa Serikali kuhusu uboreshaji wa usimamizi wa fedha za umma; za kifedha nyaraka na (e) kushauri Serikali kuhusu sheria ya fedha; (f) kutoa ushauri wa jumla kuhusu mwelekeo wa bajeti kwa usuluhishi wake; na (g) kufanya shughuli yoyote inayohusiana na bajeti ambayo sheria yoyote itaitaka kuifanya. (2) Katika kutekeleza majukumu yake, Bunge litazingatia misingi ya usimamizi mzuri wa fedha katika mfumo wa bajeti. Kamati ya Bunge ya Bajeti - 9
The Budget Committee must carry out listed budget oversight tasks, and the Parliamentary Office must provide it with budget, finance, and economic matters.
9.-(1) Kamati ya Bajeti itatekeleza, pamoja na majukumu mengine chini ya Kanuni za Kudumu za Bunge majukumu yafuatayo; (a) kujadili na kufanya mapitio ya Mwongozo wa Mpango na Bajeti pamoja na makadirio ya bajeti na kutoa mapendekezo kwa Bunge; (b) kupitia bajeti ya Serikali na kutoa mapendekezo kwa Bunge; (c) kuchambua makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Ukaguzi wa Taifa, Mahakama na Bunge; (d) kutoa mapendekezo kwa Bunge na Kamati za Bunge za Kudumu kuhusu masuala ya kiujumla ya bajeti; 61 62 No.11 Budget 2015 (e) kufuatilia masuala yote y bajeti yaliyo chini ya mamlaka ya Bunge kupitia Sheria hii au sheria nyingine na kutoa taarifa kwa Bunge; (f) kufuatilia utekelezaji wa Serikali na Taasisi za Umma ili kuhakikisha zinazingatia misingi ya matumizi ya fedha za umma kama ilivyobainishwa kwenye Sheria ya fedha ya Umma na Sheria hii; (g) kupitia taarifa za kifedha za robo mwaka na nyaraka mbalimbali zitakazowasilishwa Bungeni na kutoa mapendekezo jinsi ya kuboresha usimamizi na uwajibikaji wa fedha za umma; (h) kufanya tafiti mara kwa mara kuhusu mwenendo wa utekjelezaji wa bajeti ya Serikali na kutoa mapendekezo kwa Bunge jinsi ya kuboresha; (i) kutekeleza kazi au shughuli nyingine zinazohusu masuala ya bajeti kadri Bunge litakavyoelekeza chini ya Sheria hii au sheria nyingine; na (j) kutekeleza majukumu yoyote yaliyobainishwa chini ya Kanuni za Kudumu ya Bunge, kuhusu usimamizi wa masuala ya bajeti. (2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1), Ofisi ya Bunge itatoa kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti masuala ya bajeti, fedha na kiuchumi. Mamlaka na kazi za Waziri - 10
The Minister must prepare and submit annual revenue and expenditure estimates to Parliament, and carry out several budget-management and transparency duties.
10.-(1) Waziri katika kila mwaka wa fedha ataandaa na kuwasilisha Bungeni- (a) makadirio ya mapato; na (b) makadirio ya matumizi na mahitaji ya fedha ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa mwaka huo. (2) Bila kuathiri ujumla wa kifungu kidogo cha (1), Waziri atakuwa na wajibu wa- (a) kuandaa sera ya uchumi jumla na mpango wa matumizi wa bajeti wa muda wa kati; (b) kudhibiti na kusimamia uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa bajeti, ikijumuisha marekebisho yoyote kwenye bajeti; (c) kuhakikisha kuwa wadau wote wanashirikishwa na kufahamishwa kuhusu maamuzi ya kibajeti katika mpango wa muda wa kati ulioandaliwa na waziri chini ya aya (a); 62 No.11 Budget 2015 63 (d) kutangaza kwa njia zingine zinazofaa, maendeleo ya utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo mwaka; (e) kusimamia na kudhibiti fedha za Serikali, michakato ya kibenki na malipo, matarajio ya upatikanaji wa fedha, deni la umma na mali na madeni ya Serikali; (f) kutangaza na kutekeleza uwazi na usimamizi yakinifu wa mapato, matumizi, mali na madeni ya Serikali. (3) Waziri kwa kutumia kanuni- (a) ataainisha utaratibu wa jinsi, wakati na mahali ambapo umma utashirikishwa katika maandalizi ya bajeti kwa ngazi ya kitaifa; na (b) Kamishna wa Bajeti na Mkaguzi Mkuu wa Ndani watatoa utaratibu wa usimamizi wa bajeti kwa kuhakikisha ushiriki binafsi wa maafisa masuuli katika kazi za kamati za bajeti. Majukumu ya Waziri anayeshughu likia masuala ya Mpango - 11
The Minister responsible for Planning must prepare the National Development Plan, submit it for Cabinet and Parliament approval, coordinate its implementation, and present a report on the state of the national economy to Parliament.
11. Waziri anayeshughulikia masuala ya Mipango atakuwa na jukumu la- (a) kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa; (b) atawasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuidhinishwa; (c) atawasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa ulioidhinishwa kwa ajili ya kuidhinishwa na Bunge; (d) ataratibu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa; na (e) kuwasilisha Bunge taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa. Mamlaka na kazi za Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali - 12
The Secretary General and the Accountant General are responsible to the Minister for implementing this Act, preparing and reviewing budget and public-funds matters, and they may request information from public entities.
12.-(1) Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, kwa madhumuni ya utekelezaji wa masharti ya Sheria hii na sheria ndogo zitakazotengenezwa chini ya sheria hii atawajibika kwa Waziri. (2) Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali atahakikisha kwamba- (a) maandalizi ya makadirio ya matumizi kwa mwaka yanafanyika kwa umakini na wakati kwa ajili ya kuzingatiwa na kuidhinishwa na Waziri kwa kuzingatia idhini la Baraza la Mawaziri kabla ya kuwasilishwa bungeni; 63 64 No.11 Budget 2015 (b) makadirio ya mwaka ya matumizi yanaandaliwa kwa kuzingatia maelekezo ya jumla au mahsusi ya waziri inayoonyesha, kadiri iwezekanayavyo, thamani ya fedha na matumizi bora ya rasilimali za Serikali; (c) mifuko maalum inapitiwa; na iliyopo na inayokusudiwa kuanzishwa (d) mfumo utakaowezesha mifuko maalum kuchangia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali, unaanzishwa. (3) Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, kwa kuzingatia maelekezo ya waziri atadhibiti utoaji wa fedha za umma kwa Serikali na taasisi zingine za umma na atafanya kazi zingine zozote zitakazo bainishwa na waziri. (4) Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali anaweza kuomba taarifa ambayo ni muhimu kwa jili ya kuandaa taarifa yoyote chini ya sheria hii. (5) Maombi chini ya kifungu kidogo cha (4) yatakuwa ya maandishi yanayobainisha masharti na tarehe pamoja na muonekano wa taarifa itakayotolewa na taasisi ya umma ambayo itatakiwa kutii ombi. (6) Afisa yeyote wa umma ambaye, bila sababu madhubuti, atashindwa kutoa taarifa iliyoombwa chini ya kifungu hiki anafanya kosa la kinidhamu na atachukuliwa hatua za kinidhamu ambazi zitalingana na mazingira ya kosa. (7) Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali kwa madhumuni ya kuhakikisha matumizi bora ya fedha za umma kwa taasisi za umma itafanya marejeo ya mapato na matumizi ya taasisi za umma. (8) Katika kufanya marejeo hayo mara kwa mara Katibu Mkuu anaweza kuamuru kiasi chochote cha fedha kuingizwa katika bajeti ya taifa. (9) Waziri anaweza, kupitia kanuni zilizotangazwa kwenye gazeti la Serikali, kubainisha utaratibu wa kufanya marejeo hayo ya mapato na matumizi ya taasisi za umma. Mamlaka na kazi ya Tume ya Mipango. - 13
Tume ya Mipango ina mamlaka ya kutathmini raslimali za taifa, kuishauri Serikali, kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya Serikali, na kutoa mwongozo wa uandaaji wa Mpango wa Taifa.
13. Mamlaka na kazi za Tume ya Mipango zitakuwa- (a) kutathmini hali ya raslimali za taifa kwa maendeleo na kuishauri Serikali juu ya matumizi sahihi ya raslimali hizo; 64 No.11 Budget 2015 65 (b) kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya Serikali kuhusu mipango na usimamizi wa uchumi; (c) kutoa mwongozo wa uandaaji wa Mpango wa Taifa na kufutilia mchakato wa maandalizi wa mipango ya mwaka wa muda mfupi, kati na mrefu. Kamishna wa Bajeti - 14 Verify source ↗
15. National Plan and Budget Guidelines Committee
A Budget Commissioner is established and must carry out budget work under the directions of the Secretary General.
14.-(1) Kutakuwepo na Kamishna wa Bajeti. (2) Kamishna wa Bajeti kwa maelekezo ya Katibu Mkuu atawajibika kuandaa, kutekeleza, kusimamia, kutathmini na kutoa taarifa juu ya bajeti. (3) kamishna wa Bajeti katika kutekeleza majukumu yake atawajibika kwa Katibu Mkuu. (4) Bila kuathiri masharti ya kifungu hiki, Kamishna wa Bajeti atakuwa na jukumu la- (a) kupitia sera za bajeti na kutoa mwongozo kwenye eneo hilo; (b) kuchambua mafungu tofauti ya bajeti wakati wa mchakato wa kuandaa mafungu hayo; (c) kusimamia bajeti ya Serikali na taasisi za umma; (d) kuandaa taarifa za uhamisho wa fedha; (e) kusimamia, kutathmini na kutoa taarifa kuhusu bajeti ya Serikali; (f) kusimamia na kujumuisha mpango wa mtiririko wa fedha wenye kuzingatia utekelezaji na utoaji taarifa; na (g) kutoa ushauri kuhusu miadi ya Serikali yenye kuhitaji rasilimali fedha na taratibu za kibajeti. Kamati ya Kitaifa ya Mpango na bajeti - 15 Verify source ↗
National Plan and Budget Guidelines Committee
Kamati ya kitaifa ya mpango na bajeti ipo; Waziri ataainisha muundo wake kwa kanuni, na kamati itaishauri Serikali na inaweza kuandaa mpango na bajeti na kuomba taarifa zilizoandikwa kutoka serikali na taasisi za umma.
15.-(1) Kutakuwepo na Kamati ya Kitaifa ya mpango wa bajeti. (2) Muundo wa kamati ya kitaifa ya mpango wa bejeti utaainishwa na Waziri kupitia kanuni. (3) Kamati ya kitaifa ya mpango na uchumi itakuwa na jukumu la kuishauri Serikali katika kuandaa Bajeti ya nchi. 65 66 No.11 Budget 2015 (4) Mamlaka na kazi ya kamati ya kitaifa ya mpango na Bajeti yatakuwa: (a) kuandaa mpango na bajeti kwa mujibu wa sheria hii; (b) kuomba taarifa kwa maandishi kutoka Serikalini na taasisi za umma ambazo ni muhimu kwa ajili ya kuandaa Mipango na Miongozo ya Bajeti; Kamishna wa Uchambuzi wa Sera - 16
A Commissioner of Policy Analysis is established and is accountable to the Secretary General; the Commissioner must provide professional policy advice on specified policy and macroeconomic matters.
16.-(1) Kutakuwa na Kamishna wa Uchambuzi wa Sera. (2) katika kutekeleza majukumu yake Kamishna wa Uchambuzi wa Sera atakuwajibika kwa Katibu Mkuu. (3) majukumu ya Kamishna wa Uchambuzi wa Sera yatakuwa ni kutoa ushauri wa kitaalamu wa kisera kuhusiana na- Mamlaka na kazi ya Msajili wa Hazina (a) masuala ya kisera kuhusu bajeti, ukusanyaji wa mapato, mgawanyo wa matumizi, vyanzo vya fedha na mahusiano ya kiuchumi ya kikanda na kimataifa; na (b) masuala ya uchumi jumla kuhusu utungaji wa sera na utekelezaji, usimamizi wa kanzidata na utoaji wa taarifa wa vipindi. - 17
The Treasury Registrar has power to review, approve, supervise, direct, analyze, and sign off on several matters relating to public institutions.
17. Msajili wa Hazina atakuwa na mamlaka na kazi ya- (a) kupitia na kupendekeza au kupitisha mikakati na mipango ya mwaka ya taasisi za umma ambazo ziko chini ya usimamizi wa Msajili wa Hazina kabla ya kuiingiza kwenye mpango wa Maendeleo ya Taifa; (b) kusimamia mifuko ya uwekezaji wa taasisi za umma; (c) kufuatilia na kuhakikisha kwamba ziada, michango na gawio kutoka taasisi za umma zinalipwa kwa wakati; (d) kuelekeza au kupitisha, matumizi au marekebisho ya Kanuni za fedha ili kuhakikisha mapato na matumizi ya taasisi za umma; (e) kusimamia mitaji, ruzuku, fedha za mitaji, akiba au mapato yaliyosalia, yaliyolipwa na shirika na uwekezaji mwingine wa umma; 66 No.11 Budget 2015 67 (f) kuchambua na kuidhinisha muundo wa taasisi,muundo wa mishahara,kada za utumishi katika taasisi za umma; (g) kusimamia fedha zilizopokelewa kutokana na ubinafsishaji wa taasisi za umma, mali na hisa; (h) kufanya mapitio na kusaini mikataba ya utekelezaji ya mashirika ya umma yenye lengo y kuboresha mapato; na Mamlaka na kazi ya Maafisa Masuuli - 18 Verify source ↗
The Commissioner for Policy Analysis
Maafisa Masuuli must ensure budget preparations follow budget guidelines, protect and manage public funds and resources properly, and arrange for revenue collection from the public.
18.(1)-Mamlaka na kazi za Maafisa Masuuli zitakuwa ni kuhakikisha kwamba- (a) mafungu ya bajeti na taasisi za umma zinaandaliwa kwa mujibu wa Miongozo na Miongozo ya Bajeti; (b) fedha za umma na rasilimali za umma zinalindwa na kusimamiwa ipasavyo; na (c) kuna mpangilio mzuri wa kuwezesha kukusanya mapato kutoka kwa umma. (2) Maafisa Masuuli wa Wizara na taasisi za umma wataanzisha kamati za bajeti ambazo muundo wake utaainishwa katika kanuni. Hatua za uandaaji wa bajeti SEHEMU YA NNE UANDAAJI NA UIDHINISHWAJI WA BAJETI
Part
SEHEMU YA NNE
- 19 Verify source ↗
Stages in the budget process
This section lists the steps involved in preparing the annual budget and provides for an advisory committee on revenue sources.
19.-(1) Matayarisho ya Bajeti kwa kila mwaka wa fedha yatahusisha hatua zifuatazo- (a) majumuisho ya mchakato wa mipango ya maendeleo ambayo itakuwa ile mipango ya muda mrefu na muda wa kati; (b) mipango na maamuzi ya sera za kifedha na kiuchumi pamoja na vipaumbele vya ngazi ya kitaifa kwa muda wa kati; (c) Baraza la Mawaziri kuidhinisha Mwongozo wa Mpango wa Bajeti; (d) Bunge kuidhinisha Mwongozo wa Bajeti na Mpango kama msingi wa maamuzi ya kuandaa makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha unaofatia; (e) Baraza la Mawaziri kuidhinisha hatua na vyanzo vya mapato; (f) Bunge kuidhinisha hatua na vyanzo vya mapato; 67 68 No.11 Budget 2015 (g) kuwasilisha makadirio ya bajeti Bungeni kwa ajili ya kupata kibali; (h) kuandaa Muswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali, Muswada wa Sheria ya Fedha na Sheria nyingine zinazohitajika kutungwa kwa ajili ya utekelezaji wa mapendekezo ya Bajeti ya Serikali; (i) kutunga Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali na Sheria ya Fedha; (j) kutekeleza bajeti iliyoidhinishwa; (k) kufanya tathmini na kutoa taarifa za mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali; na (l) kufanya mapitio na kutoa taarifa kuhusu mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu. (2) Kutakuwa na kamati ya kumshauri Waziri kuhusu vyanzo vya mapato katika mwaka wa fedha husika. (3) Muundo wa kamati ya hiyo ya ushauri utaainishwa na Waziri katika kanuni. Mpango wa Maendeleo wa Taifa - 20 Verify source ↗
National Development Plan
The minister responsible for the Planning Commission must prepare and submit the National Development Plan to Parliament.
20. Waziri anayeshughulikia Tume ya Mipango ataandaa na kuwasilisha Bungeni Mpango wa Maendeleo wa Taifa ambao utakuwa msingi wa uandaaji wa bajeti ya Taifa. Mpango na Mwongozo wa Bajeti - 21 Verify source ↗
Plan and Budget Guidelines
The Minister must prepare and submit the Budget Policy and Guidelines to Parliament, including annual timing and required budget details.
21.-(1) Waziri ataandaa na kuwasilisha Bungeni Mpango na Mwongozo wa Bajeti. (2) Mpango na Mwongozo wa Bajeti utawasilishwa Bungeni kila Februari ya kila mwaka, au pale ambapo Bunge halitakuwepo mwezi Februari, kila wiki ya kwanza Bunge litakapokutana. (3) Mpango na Miongozo ya Bajeti utaeleza kwa mapana malengo ya masula ya Uchumi Jumla ambayo yatakuwa msingi wa bajeti kwa kipindi kinachofuata mwaka wa fedha uliopo na mipango ya kati na itazingatia yafuatayo- (a) tathimini ya mwaka wa fedha uliopo na uchumi unaotarajiwa kwa miaka ya fedha mitatu inayofuata; 68 No.11 Budget 2015 69 (b) uchumi jumla na sera za kibajeti kwa kipindi kilichobainishwa chini ya aya (a); (c) malengo ya mapato kwa ujumla, matumizi kwa ujumla, ukopaji wa ndani nan je kwa kipindi kinachofuata mwaka wa fedha na mipango ya kati; (d) jumla ya rasilimali zilizogawanywa kwa ajili miradi ya kisekta au Wizara kwa kipindi kilichobainishwa chini ya aya (a) ilibainisha matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa kila mradi kwa kipindi hicho; (e) vigezo vilivyotumika kugawa rasilimali za umma zilizopo kwa kila mradi; (f) makadirio ya riba na gharama za ulipaji madeni na ulipaji wa madeni kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa bajeti husika na miaka miwili ya fedha inayofuata; (g) mapendekezo ya kugharimia mapungufu yoyote kwa mwaka wa fedha; (h) makusudio kuhusu ukopeshaji na vitu vitakavyosababisha kuongezeka kwa deni ya Taifa kwa mwaka wa fedha; (i) bajeti na hali halisi ya mapato kwa miaka miwili ya fedha iliyotangulia; (j) bajeti na hali halisi ya matumizi kwa miaka miwili ya fedha iliyotangulia kwa kila fungu na Idara muhimu; (k) makadirio ya hali ya kifedha kwa mwaka wa fedha unaohusika na bajeti na miaka miwili inayofuata; (l) malengo ya kisera yanayosimamia maamuzi ya bajeti ya Serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha na maeneno ya kisera ambayo Serikali itazingatia katika mwaka wa fedha. (4) Kamati ya Bunge ya Bajeti kabla ya kumalizika kwa siku saba baada ya kuwasilishwa kwa Mwongozo wa Mpango na Bajeti Bungeni, taarifa yenye mapendekezo ambapo Bunge litayajadili na kupitisha azimio kukubali bila marekebisho au na marekebisho. itawasilisha 69 70 No.11 Budget 2015 Bajeti za taasisi za umma Uwasilishaji wa makadilio ya bajeti (5) Waziri ataitisha na kusambaza Mwongozo wa Mpango na Bajeti ndani ya siku zisizozidi kumi na tano baada ya kuwasilishwa Bungeni. - 22 Verify source ↗
Budget of public entities
Public entities must prepare budget estimates and submit them to the Secretary General for review and approval.
22.-(1) Taasisi za Umma zitatakiwa kuandaa makadirio ya bajeti na kuziwasilisha kwa Katibu Mkuu kwa ajili ya uchambuzi na idhini kwa mujibu wa Sheria hii na kupokea fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa kuzingatia bajeti iliyoidhinishwa. (2) baada ya kupokea makadirio ya bajeti, katibu mkuu anaweza: (a) kuidhinisha makadirio ya bajeti yakiwa na mabadiliko au bila mabadiliko; (b) kukataa makadirio ya bajeti na kutoa sababu za kukataa; (3) Katibu Mkuu anaweza kufanya mabadaliko au kukataa makadirio ya bajeti kwa misingi ya sababu mahsusi zilizotajwa kama zinazoainishwa- (a) makadirio hayaangukii katika majukumu ya msingi ya taasisi za umma husika; (b) makadirio hayo ni ya juu zaidi na hayalingani na mahitaji halisi ya utoaji au upokeaji wa huduma katika soko au (c) hayaendani na hatua za kubana matumizi zilizoainishwa katika Mpango wa Maendeleo ya Taifa. (4) Katibu Mkuu anaweza, kuamuru mapato yaziada ya bajeti yaliyokusanywa na taasisi za umma kuingizwa kwenye Mfuko Mkuu . - 23 Verify source ↗
Submission of budget estimates and related documents for approval
Waziri lazima awasilishe makadirio ya bajeti na nyaraka husika kwa Baraza la Mawaziri na baadaye Bungeni, kisha kuzitangaza na kuzisambaza kwa umma; Serikali pia lazima ihakikishe mfuko wa Bunge na wa Mahakama una fedha za kutosha.
23.-(1) Waziri atatakiwa, ndani ya kipindi kilichowekwa na kubainishwa katika kifungu hiki, kuwasilisha kwa Baraza la Mawaziri kupata kibali cha makadirio ya bajeti na nyaraka nyinginezo zitakazozingatiwa katika makadirio ya bajeti. (2) Endapo Baraza la Mawaziri litakapokuwa limetoa kibali kwa makadirio ya bajeti kwa mujibu wa kifungu kidogo (1), Mawaziri wote watatakiwa kuwa na jukumu la: (a) kuzingatia, kufuata na kusimamia makadilio ya bajeti; (b) kusimamia utekelezaji wa makadirio ya bajeti 70 No.11 Budget 2015 71 (3) Waziri atatakiwa, ndani ya kipindi kilichobainishwa katika Kanuni za Bunge kuwasilisha Bungeni nyaraka zifuatazo- (a) makadirio ya bajeti; (b) nyaraka zinazohusiana na makadirio ya bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti. (4) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1), Serikali itahakikisha kuwa Mfuko wa Bunge na Mfuko wa Mahakama umepewa fedha za kutosha kuwezesha Bunge na Mahakama kutekeleza kazi na majukumu yake kwa ufanisi. (5) Serikali na Bunge . (6) Waziri atatangaza baada ya kuwasilisha Bungeni Makadirio ya bajeti na nyaraka zinazohusiana na makadirio ya bajeti katika Gazeti la Serikali na kuzisambaza kwa umma. (7) Waziri ataandaa mara baada ya kupata idhini ya bunge kuhusu makaririo ya bajeti, kuwasilisha Bungeni Muswadawa Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa makadirio yaliyoidhinishwa. Uwasilishaji wa nyaraka nyingineza bajeti mbele ya Bunge - 24 Verify source ↗
Submission of other budget documents to the National Assembly
Waziri lazima awasilishe nyaraka za bajeti Bungeni kila mwaka wa fedha, pamoja na nyaraka zinazotolewa chini ya Kifungu cha 22.
24.-(1) Pamoja na nyaraka zilizowasilishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 22, Waziri atapaswa kuwasilisha Bungeni nyaraka za bajeti kwa kila mwaka wa fedha- (a) muhtasari wa bajeti unaojumuisha: (i) muhtasari wa sera za kibajeti zinazojumuisha sera za mapato, matumizi, madeni na upungufu wa fedha; (ii) maelezo ya jinsi bajeti inavyohusika na misingi ya wajibu wa kibajeti na malengo ya kibajeti na (iii) maelezo ya Waziri kuhusu makubaliano ya Bunge bajeti na Miongozo ya kwenye Mpango ilivyoshughulikiwa; (iv) mgao wa mapato kwa serikali za mitaa kutoka hisa za Serikali ikiwemo misaada yenye masharti na isiyo na masharti; (b) muundo wa makadirio ya bajeti yanayojumuisha: (i) orodha ya taasisi zote zinazopata fedha kutoka bajeti ya Serikali; 71 72 No.11 Budget 2015 (ii) makadirio yote ya mapato kwa wigo mkubwa wa uchumi; (iii) makadirio yote ya matumizi, mafungu ya miradi, ikibainisha matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo; na (iv) makadirio ya mapungufu ya bajeti au ongekezo kwa mwaka wa fedha na mipango ya kati na mapendekezo ya vyanzo vya fedha; (d) taarifa (c) taarifa kuhusu madeni yatokanayo na bajeti ya Serikali, inayojumuisha makadirio ya deni, riba na gharama zinginezo zinazotakiwa kulipwa na Serikali katika mwaka wa fedha kwa mujibu wa madeni husika; kuhusu madeni za Serikali, na yanayojumuisha makadirioya deni, riba na gharama zinginezo zinazotakiwa kulipwa na Serikali katika mwaka wa fedha kwa mujibu wa madeni husika; kuhusu malipo gharama zitakazolipwa na Serikali ambazo hazikubainishwa katika Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali ambazo zinajumuisha masuala ya kikatiba na mamlaka ya Sheria kufanya malipo hayo na yatakayolipwa (e) taarifa dhamana na Bunge kujadili makadirio ya Bajeti (f) taarifa ya Waziri kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kutekeleza mapendekezo ya Bunge kuhusu bajeti ya Serikali katika mwaka au miaka iliyopita. (2) Waziri atatoa ufafanuzi wa taarifa zitakazowasilishwa pamoja na makadirio ya bajeti na mfumo wa uwasilishwaji utakaotumika. - 25 Verify source ↗
National Assembly to consider budget estimates
Before Parliament debates the budget estimates, the Parliamentary Committee must discuss them and submit recommendations, considering the Minister’s and public’s views. Parliament may amend the Government budget estimates by resolution, but any increase in one spending item must be balanced by cuts elsewhere and reductions must be used to reduce the budget deficit.
25.-(1) Kable ya Bunge kujadili makadirio ya bajeti, Kamati ya Bunge itajadili makadirio hayo na kuwasilisha mapendekezo Bungeni kwa kuzingatia maoni ya Waziri na umma yaliyowasilishwa kabla ya tarehe ya mwisho itakayobainishwa katika Kanuni. (2) Kwa kuzingatia masharti yaliyobainishwa katika Katiba, Bunge linaweza kurekebisha makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa Azimio litakalopitishwa kuhusu Mwongozo wa Mpango wa Bajeti kwa kuhakikisha kwamba- 72 No.11 Budget 2015 73 (a) ongezeko la matumizi katika kasma pendekezwa linawianisha kwa punguzo la matumizi kwenye kasma nyingine;na (b) pendekezo la kupunguza matumizi linatumika kupunguza nakisi ya bajeti. Kuidhinishwa kwa Bajeti ya Taifa na Bunge - 26 Verify source ↗
Approval of the national budget by National Assembly
Bunge must approve the national budget and related finance measures by 30 June each year, and the annual budget is approved by roll-call vote for each MP.
26.-(1) Bunge litaidhinisha ifikapo tarehe 30 Juni kila mwaka, bajeti ya Taifa pamoja na Mpango wa Utekelezaji wa Serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata na kupitisha Muswada wa Kuidhinisha Matumizi ya Fedha za Serikali, Muswada wa Fedha na hati nyingine za kisheria ambazo ni muhimu katika utekelezaji wa bajeti ya Taifa. (2) Bunge litaidhinisha bajeti ya Taifa ya mwaka kwa kupiga kura kwa kuita jina kwa kila mbunge. Matumizi ya Serikali yaliyoidhinish wa - 27 Verify source ↗
28. Where Appropriation Act is not yet in force
The Minister of Finance must make approved budget estimates accurate, clear, and specific, and the Minister must publish and announce them to the public within 30 days after parliamentary approval.
27.-(1) Waziri wa Fedha atahakikisha kuwa matumizi yatakayoidhinishwa katika makadirio ya bajeti katika Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali yanawasilishwa yakiwa- (a) sahihi na zimezingatia masuala muhimu ya kibajeti; na (b) yamebainisha wazi fedha zilizopo katika fungu na miradi. (2) Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali itajumuisha- (a) matumizi ya kawaida kwa kila mradi, ikiainisha kila matumizi husika; na (b) matumizi ya maendeleo kwa kila mradi wa maendeleo, ikiainisha kila matumizi husika. (3) Makadirio ya bajeti yaliyoidhinishwa na Bunge yatachukuliwa kuwa kama yameidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za Serikali na Taasisi za Umma. (4) Fedha zilizoidhinisha kwa matumizi ya Serikali na taasisi za umma, zitatumika kwa kuzingatia madhumuni yaliyoainishwa na katika kiwango kilichowekwa kwa makadirio ya Serikali na taasisi za umma. (5) Waziri katika kipindi cha siku thelathini baada ya Bunge kuidhinisha makadirio ya bajeti, ataboresha, atachapisha na kutangaza kwa umma makadirio ya bajeti. 73 74 No.11 Budget 2015 Wakati ambapo Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali haijaanza kutumika (6) Waziri atahakikisha na kuchukua hatua kuhakikisha makadirio yaliyoidhinishwa yametayarishwa na kutangazwa katika muundo ambao utakuwa wazi na rahisi kueleweka na kupatikana kwa umma. - 28 Verify source ↗
Where Appropriation Act is not yet in force
If the Appropriation Act is not yet in force, the President may authorize spending from the Consolidated Fund to keep government work going, but only up to the stated limit and only until 31 October of the fiscal year or earlier commencement of the Act.
28.-(1) Endapo Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali haijaanza kutumika, Rais anaweza kwa kutumia Warrant iliyosainiwa na resident iliyoelekezwa kwa Waziri, akaruhusu matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali kwa lengo la kuwezesha kazi za Serikali kuendelea mpaka tarehe 31 Oktoba ya mwaka wa fedha husika au kwa kuanza kutumika kwa Sheria hii, chochote kitakachotangulia. (2) Kiasi kitakachoruhusiwa kutumika hakitakiwi kuzidi kiasi kilichoainishwa kwa ajili ya mapendekezo ya shughuli zilizokadiwa kwa mwaka wa fedha au moja ya tatu ya kiasi kilichoainishwa katika Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali. (3) Fedha zilizotumika kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) kitahesabiwa kama sehemu ya fedha zilizoidhinishwa kwa mwaka wa fedha katika Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali inayohusishwa. Mwisho wa Matumizi ya fedha iliyoidhinishw a kwa mwaka wa fedha - 29 Verify source ↗
Appropriations to lapse at the end of financial year
Usiotumika mwishoni mwa mwaka wa fedha huisha, na taasisi za umma lazima zirudishe mabaki ya fedha zilizoidhinishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina na kuwasilisha taarifa husika.
29.-(1) Fedha ambazo hazijatumika kufikia mwisho wa mwaka ambazo ziliidhinishwa matumizi yake yataishia mwaka huo wa fedha. (2) Kwa kuzingatia sheria zingine, endapo mwisho wa mwaka wa fedha taasisi za umma bado ina bakaa ya fedha zilizoidhinishwa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina, fedha hizo zitarudishwa kwenye Mfuko Mkuu wa hazina, taasisi ya umma itaandaa taarifa na kuiwasilisha kwa Kamishna wa Bajeti. (3) Kifungu kidogo cha fedha zilizoidhinishwa kuvuka mwaka wa fedha kama zitakavyoainishwa katika kanuni. (2) hakitatumika kwa (4) Mhasibu Mkuu wa Serikali taarifa zilizowasilishwa kwao kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) na kuziwasilisha kwa Waziri taarifa ya fedha ambazo hazikutumika na kuhifadhiwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina. atazijumuisha 74 No.11 Budget 2015 75 Muda wa matumizi na kibali Kuwasilisha viashiria vya Sera ya Bajeti (5) Waziri wa Fedha atalazimika, kila mwisho wa mwaka wa fedha, kuwasilisha Bungeni taarifa ya fedha ambazo hazikutumika na kuhifadhiwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina na pendekezo la Serikali ya kutumia hizo fedha katika mwaka mwingine wa fedha ili kupata idhini ya Bunge. - 30 Verify source ↗
Duration of appropriations and warrants
Appropriations, warrants, and other statutory authorisations for the year end at the close of the fiscal year, and unspent money issued from the Consolidated Fund must be returned to that fund.
30.-(1) Matumizi yote ya fedha za umma yaliyopitishwa na Bunge kwa ajili ya huduma za mwaka wa fedha na kila kibali na idhini nyingine zilizotolewa na sheria hii kuhusiana na mwaka husika, itaisha na kukoma kuwa na nguvu inapofika mwisho wa mwaka wa fedha. (2) Fedha zote ambazo hazijatumika na ambazo zilitolewa kwenye Mfuko Mkuu zitarejeshwa kwenye Mfuko Mkuu. - 31 Verify source ↗
Submission of budget policy highlights
The Minister must publicly announce budget policy indicators and government revenue measures each financial year after Cabinet approval.
31.-(1) Waziri, katika kila mwaka wa fedha baada ya kupata idhini ya Baraza la Mawaziri, atatangaza kwa umma viashiria vya sera za bajeti pamoja na hatua za kukusanya mapato ya Serikali. (2) Wakati akitoa tangazo hili, atazingatia makubalino ya kikanda na kimataifa ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeingia, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Afrika Mashariki mwaka 1994 na pale ambapo mikataba hiyo inahitaji kutangazwa kwa hatua hizi katika tarehe maalum, Waziri atahakikisha hatua hizi zinatangazwa katika tarehe husika. Kuwasilisha Muswada wa Fedha - 32 Verify source ↗
Submission of the Finance Bill
The Minister must prepare and present the Finance Bill to Parliament, and Parliament’s revenue proposals must follow specified budget and revenue principles.
32.-(1) Waziri ataandaa na kuwasilisha Bungeni, Muswada wa Fedha akiainisha hatua za kuongeza mapato ya Serikali. (2) Katika kuwasilisha Muswada wa Fedha, Bunge litawasilisha mapendekezo yake kuhusu Muswada wa Fedha. (3) Mapendekezo yote yatakayotolewa na Bunge au kuchukuliwa na Bunge katika masuala ya mapato yata- (a) zingatia kwamba kiwango cha mapato kitakachokusanywa kinaendana na misingi ya bajeti iliyoidhinishwa; (b) kuzingatia misingi ya usawa, uhakika na wepesi wa kukusanya; 75 76 No.11 Budget 2015 Kuzuia idhini (c) kuzingatia athari za mapendekezo ya mabadiliko katika mchanganuo wa kodi kwa kuzingatia kodi ya moja kwa moja na kodi inayoingizwa kwenye bidhaa; (d) kuzingatia mwenendo wa mapato ya ndani, kanda na kimataifa; (e) kuzingatia athari katika maendeleo, uwekezaji, kukua kwa uchumi; na (f) kuzingatia kodi na makubaliano mengine ya viwango na majukumu ambayo Jamhuri ya Muungano imechukuwa, ikiwa ni pamoja na kodi na makubaliano ya viwango katika makubaliano ya uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 1994. (4) Mapendekezo yatakayotolewa chini ya kifungu hiki yatazingatia misingi ya usimamizi wa mapato. - 33 Verify source ↗
Withholding of approval
Parliament may withhold or approve budget-related funds and may also rely on audit recommendations from the Controller and Auditor General.
33.-(1) Pale ambapo Bunge limeridhika kuwa zipo sababu za kutosha zilizopelekea kushindwa kutekeleza kwa mapendekezo ya ukaguzi uliopita yaliyofanywa na Bunge, Bunge linaweza kuzuia matumizi ya kifungu maalum ndani ya Fungu, kutoka Mfuko Mkuu, kama takavyoona inafaa kwa madhumuni ya kugharamia matumizi ya Fungu hilo. (2) Pale ambapo kwa hiari, Fungu hilo limekuwa kwa mfululizo likishindwa kutekeleza au kujibu hoja za ukaguzi na mapendekezo, Bunge linaweza, kwa mujibu wa taratibu za haraka utakavyoona inafaa, kuzuia fedha hizo kutoka katika Fungu hilo kwa mwaka kulingana na kiasi cha fedha kilichohojiwa kuhusu Fungu hilo. (3) Pale ambapo Bunge limeridhika kuwa kwa hiari na mfululizo Fungu limeshindwa- (a) kuzingatia misingi ya umakini na usimamizi mzuri wa fedha; (b) kuzingatia misingi bora ya uhasibu na usimamizi wa fedha; au (c) kufikia malengo na madhumuni ya bajeti linaweza, pamoja na taratibu nyingine itakavyoona ni za haraka, kuzuia kifungu kimoja au zaidi katika fundu kwa huduma mbalimbali katika Fungu hilo. 76 No.11 Budget 2015 77 (4) Kutokana na kushindwa kwa mfululizo kwa Idara katika seksheni hii ambao unatokana na utendaji mbaya wa Afisa wa Umma, Bunge linaweza, kwa kura ya wachache, na kwa kuzingatia masharti kama itakavyoona inafaa, kuzuia mafano yoyote na mshahara wa Afisa huyo kwa muda itakavyoona inafaa. (5) Pale ambapo Fungu linawasilisha mbele ya Bunge kuonesha kuwa limeyafanyia kazi mapendekezo ya ukaguzi wa hesabu, Bunge linaweza, iwapo sheria ya Fedha haijaidhinishwa, kuidhinisha malipo ya Fungu hilo kwa namna itakavyoona inafaa. (6) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza, katika taarifa yake kwa Bunge, kupendekeza kuzuia matumizi ya kifungu chochote katika seksheni hii. (7) Katika kifungu hii- (a) ‘kuzuia’ ina maana kuzuia, kiasi Fulani au kiasi chote, kwa muda mfupi au moja kwa moja, kifungu kimoja au zaidi ambacho kipo katika makadirio ya mwaka; na (b) fungu, linajumuisha Wizara au Taasisi ya Umma. - 34 Verify source ↗
Government deviation from financial objectives
The Government may deviate from budget objectives only with Parliament’s approval, and the Minister must report such deviations to Parliament.
34.-(1) Serikali inaweza, kwa idhini ya Bunge, kukiuka malengo ya kibajeti kutoka katika Mwongozo wa Mpango na Bajeti kwa muda mfupi pale ambapo ukiukaji huu unatokana na majanga ya asili au tukio linguine jingine ambalo halikutarajiwa kama ilivyobainishwa katika kifungu cha 35. (2) Pale ambapo yapo mabadiliko ya Serikali, Serikali mpya inaweza, kwa idhini ya Bunge, kukiuka malengo ya kibajeti katika Mwongozo wa Mpango wa Bajeti bila ya kukiuka misingi ya bajeti. (3) Waziri atawasilisha bungeni taarifa ya ukiukaji wa malengo ya bajeti, na atajumuisha katika taarifa hiyo- (a) sababu na matokeo ya ukiukaji huo; (b) mapendekezo ya kushughulikia uhamisho huo; (c) muda unaokisiwa wa mabadiliko haya; na (d) hali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na Serikali na iwapo kuna mradi uliosimamishwa, na sababu za kufanya hivyo. Serikali kukiuka malengo ya kibajeti 77 78 No.11 Budget 2015 (4) Waziri atalazimika, ndani ya kipindi cha siku thelathini baada taarifa kusambaza kutangaza kuwasilisha Bungeni, na ya zilizowasilishwa chini ya kifungu kidogo cha (3). Vyanzo vya Mfuko wa Dharura Sura 418 Waziri kusimamia Mfuko wa Dharura - 35 Verify source ↗
36. Minister to administer the Contingency Fund
Mfuko wa Dharura hujumuisha fedha zilizotengwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali, na Bunge linaweza kuidhinisha fedha za kuujaza. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali lazima awasilishe taarifa kuhusu hesabu za Mfuko huo Bungeni.
35.-(1) Mfuko wa Dharura ulioanzishwa utajumuisha fedha zilizotengwa kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali kwa Sheria ya Fedha katika kila mwaka wa fedha. (2) Mfuko wa Dharura utakuwa ni sehemu ya bajeti ya Serikali na Bunge linaweza kuidhinisha fedha itakavyoona inafaa kwa ajili ya kutunisha Mfuko huo. (3) Mfuko wa Dharura utakuwa sehemu ya Bajeti ya mwaka na Bunge, pamoja na viwango vilivyotajwa katika kifungu kidogo cha (2), litaidhinisha fedha nyingine kwa kadri litakavyoona inafaa. (4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi, atatoa taarifa katika Bunge kuhusu hesabu za Mfuko wa Dharura. - 36 Verify source ↗
Minister to administer the Contingency Fund
The Minister administers the Contingency Fund, keeps it in a separate Bank of Tanzania account, and pays it out without delay for expenditures under section 35.
36.-(1) Waziri atasimamia Mfuko wa Dharura. (2) Kiwango cha Kudumu cha Mfuko wa Dharura hakitazidi kiwango kilichoelezwa na Waziri baada ya kuidhinishwa na Bunge. (3) Waziri atatunza Mfuko wa Dharura katika akaunti tofauti, katika Benki Kuu ya Tanzania na- (a) atafanya malipo kwenye akaunti ya mfuko wa dharura kutoka kwenye mfuko wa Serikali kupitia sheria ya kuidhinisha matumizi ya fedha; na (b) atalipa kutoka mfuko wa dharura bila kuchelewa, matumizi yote kwa mujibu wa kifungu cha 35. Matumizi kutoka Mfuko wa Dharura - 37 Verify source ↗
Advances from the Contingency Fund
The Minister may release money from the Contingency Fund for emergencies and unexpected events, and must set criteria for doing so with Parliament’s approval.
37.-(1) Waziri anaweza kutoa fedha kutoka Mfuko wa Dharura pale ambapo, kwa msingi wa vigezo vilivyowekwa na mfumo na taratibu za mwongozo wa uendeshaji zilizotajwa na kuidhinishwa na Bunge pamoja na sheria kuhusiana na kudhibiti majanga akiridhika kuwa ipo dharura na jambo lisilotarajiwa na kusababisha umuhimu wa kufanya matumizi ambayo hayamo katika sheria yoyote maalum. 78 No.11 Budget 2015 79 (2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1), Waziri kwa (a) malipo kuongozwa na Sheria na Kanuni zilizopo, amethibitisha kuwa- kwa hayakukasimiwa sababu hayakutarajiwa na hayawezi kusubiri mpaka mwaka ujao wa fedha bila kuathiri manufaa kwa umma; na katika bajeti (b) tukio halikutegemewa. (3) Pamoja na Kanuni na Sheria husika, kwa madhumuni ya Seksheni hii, tukio lisilotegemewa ni lile ambalo- (a) linatishia kwa kiasi kikubwa uhai na ustawi wa binadamu; (b) linatishia uharibifu mkubwa wa mazingira; na (c) linahusisha kuokoa uharibifu, hasara, ugumu, mateso yanayosababishwa moja kwa moja na tukio hilo. (4) Tukio litachukuliwa kwamba linatishia uhai wa binadamu au ustawi pale tu linapohusisha, kusababisha au linaweza kusababisha- (a) kupotea kwa uhai, ugonjwa wa binadamu au maumivu; (b) kukosa makazi au uharibifu wa mali; (c) kuharibika kwa chakula, maji na makazi. (5) Fedha katika Mfuko wa Dharura zinatunzwa kwa matumizi ya majanga ya asili zinaweza kutumika kumuokoa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameathiriwa na majanga ya asili yaliyotokea nje ya Jamhuri ya Muungano, pale ambapo masharti ya kifungu kidogo cha (1) yamezingatiwa. (6) Mchango wa fedha kwenda katika Fungu, kuhusu majanga ya asili, utatangazwa na Waziri ndani ya siku thelathini baada ya kupokea taarifa. (7) Kwa kuzingatia kifungu kidogo (2), Waziri, kwa mujibu wa kanuni na idhini ya Bunge, ataweka vigezo vya kutoa fedha kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1). Bunge kuidhinisha fedha zilizotumika kutoka Mfuko wa Dharura - 38
Waziri lazima awasilishe taarifa ya kina kwa Bunge ndani ya miezi miwili baada ya malipo kutoka Mfuko wa Dharura na kupata idhini ya Bunge.
38.-(1) Waziri, ndani ya miezi miwili baada ya kufanya malipo kutoka Mfuko wa Dharura atawasilisha Bungeni taarifa ya kina kuhusu malipo yaliyofanyika akizingatia mahitaji ya taarifa yaliyotajwa katika kifungu kidogo cha 37(2) na kupata idhini ya Bunge kuhusu malipo hayo. 79 80 No.11 Budget 2015 (2) Pale ambapo Bunge halikutani katika kipindi kilichotajwa katika kifungu kidogo (1), au halitakutana katika mwisho wa kipindi hicho na Waziri hajaomba idhini ya Bunge kabla ya kipindi hicho kuisha. Waziri ataomba idhini hiyo ndani ya siku kimi na tano baada ya Bunge lijalo kuketi. (3) Mara tu baada ya Bunge kuidhinisha malipo, Waziri atawasilisha Muswada wa Fedha kupelekwa Bungeni kupata idhini ya fedha zilizotolewa ziweze kurudishwa katika Mfuko wa Dharura kwa kiasi kilichotumika. Taarifa za fedha kuhusu Mfuko wa Dharura - 39 Verify source ↗
40. Accruals and investments
The Minister must prepare and submit annual financial statements for the Emergency Fund to the Controller and Auditor General within three months after each financial year ends.
39.-(1) Waziri, ndani ya miezi mitatu baada ya mwisho wa kila mwaka wa fedha, ataandaa na kuwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali taarifa za fedha za mwaka huo kuhusiana na Mfuko wa Dharura. (2) Waziri atajumuisha taarifa zifuatazo katika taarifa za fedha zinazoandaliwa chini ya kifungu kidogo cha (1). (a) tarehe na kiasi cha kila malipo yaliyofanyika kutoka Mfuko wa Dharura; (b) mtu ambaye kwake malipo yamefanyika; (c) madhumuni ya kufanya malipo hayo; (d) iwapo mtu ambaye malipo yamefanyika kwake ametumia fedha hizo kwa madhumuni hayo, taarifa kuhusu hilo; (e) iwapo mtu ambaye malipo yamefanyika kwake, bado hajatumia fedha hizo kwa madhumuni hayo, taarifa kuhusu sababu za kutofanya hivyo; na (f) taarifa ya kuonesha ni kwa namna gani malipo yamezingatia vigezo vya kufanya malipo hayo. Mapato na Uwekezaji - 40 Verify source ↗
Accruals and investments
Only funds approved by Parliament Act, and related interest or other income, may go into the Emergency Fund; those funds are to be placed in the Government Consolidated Fund.
40. Fedha hazitaingia katika Mfuko wa Dharura isipokuwa zile ambazo zimeidhinishwa kwa Sheria ya Bunge pamoja na riba au mapato mengine ambayo yanaweza yakaingizwa katika Mfuko wa Dharura na fedha hizo zitaingizwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali. 80 No.11 Budget 2015 81 Uhamisho wa Fedha - 41
The responsible officer may transfer funds only with the Minister’s approval, and several listed transfers are barred. Some project-fund and intra-vote transfers are allowed only under stated conditions, with quarterly reporting and consultation requirements.
41.-(1) Afisa Masuuli anaweza, baada ya kupata idhini ya Waziri, atahamisha fedha kutoka matumizi yaliyoidhinishwa. (2) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo (1), Afisa Masuuli hatafanya uhamisho wa fedha pale ambapo- (a) Fedha hizo zimeidhinishwa kwa ajili ya yaliyozuiwa kwa matumizi ya shughuli maalum; (b) Fedha hizo zimeidhinishwa kwa ya ofisi nyingine ya Serikali au mtu; (c) fedha zimeidhinishwa kwa matumizi ya uwekezaji to defray matumizi mengine ya maendeleo; (d) uhamisho wa fedha ni kutoka katika mishahara kwenda katika matumizi yasiyo ya mishahara; au (e) uhamisho wa fedha unaweza kusababisha kuvuruga misingi ya bajeti. (3) Afisa Masuuli anaweza kufanya uhamisho wa fedha za miradi kati ya mafungu katika bajeti ya mwaka wa fedha, iwapo- (a) vipo vifungu katika bajeti za miradi ya mafungu ambavyo vinaweza visitumike; (b) maombi ya uhamisho wa fedha yamewasilisha hazina yakitoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu uhamisho wa fedha na Hazina imeidhinisha maombi hayo; na (c) Kiwango cha jumla cha uhamisho wa fedha kulikofanywa kwenda au kutoka katika miradi au mafungu kwa kiwango kisichozidi matumizi yaliyoidhinishwa katika mradi huo au mafungu katika mwaka huo wa fedha. (4) Waziri anaweza, kwa kanuni, kuidhinisha uhamisho wa fedha ndani ya bajeti za mafungu yaliyoidhinishwa na uhamisho wa fedha ndani ya mafungu au miradi. (5) Mamlaka ya Waziri katika uhamisho wa fedha katika bajeti hayatekelezwa- (a) kiwango cha fedha katika mafungu tofauti; (b) kutoka matumizi ya maendeleo kwenda matumizi ya kawaida. Isipokuwa, uhamisho umeidhinishwa kwa bajeti ya nyongeza, na hauzidi kiwango kilichoidhinishwa katika Fungu. 81 82 No.11 Budget 2015 Mapato ya ziada Kuwasilisha bajeti ya nyongeza (6) Afisa Masuuli anaweza kuhamisha fedha za ndani ya Fungu idhini ya Waziri kwa kiwango cha asilimia bila ya kupata kilichoidhinishwa katika kanuni na kutoa taarifa kwa Malipaji Mkuu wa Serikali katika kila robo ya mwaka kuhusu uhamisho huo. (7) Uhamisho wowote wa fedha:- (a) utafanyika kwa kushauriana na Wizara zote zilizoathirika pamoja na Taasisi za Serikali; na (b) utawasilishwa Bungeni na kutolewa taarifa kila robo mwaka. - 42
Revenue collected above the estimated amount must be paid into the Consolidated Fund.
42.-(1) Mapato yote yaliyokusanywa zaidi ya kiwango kilichotajwa katika makadirio kitaingizwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali. (2) Bila kuathiri masharti ya Sheria ya Fedha za Umaa, taarifa ya matumizi ya ziada itakatakatishwa na taarifa ya Afisa Masuuli husika ikielezea sababu na matumizi ya ziada na hatua za kuchukua kuzuia matumizi hayo ya ziada yasitokee. - 43 Verify source ↗
Reallocation of funds
Serikali lazima iwasilishe bajeti ya nyongeza Bungeni kwa idhini katika hali fulani.
43.-(1) Serikali itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa. zilizotumika zimezidi ambazo fedha ya (2) Bajeti ya Nyongeza itahitajika kwa- (a) kuongeza au kupunguza katika idhini mabadiliko ya malengo, au kupata idhini mpya katika sheria ya fedha. (b) kuongeza au kupunguza kiwango cha line item katika makadirio iwapo hayataweza kufikiwa katika mabadiliko ya fedha au mabadiliko ya matumizi yake. (c) kuonesha namna ambayo Mfuko wa Dharura umetumika. (3) Endapo Bunge limeidhinisha matumizi, Sheria ya Fedha itapitishwa kwa kiwango kilichoidhinishwa. (4) Bajeti ya Nyongeza itajumuisha taarifa ya matumizi ya ziada na mapato husika katika kipindi hicho katika kutekeleza misingi ya fedha na Bajeti. 82 No.11 Budget 2015 83 SEHEMU YA TANO UTEKELEZAJI, UFUATILIAJI, TATHMINI NA UTOAJI TAARIFA WA BAJETI Mamlaka ya Matumizi
Part
SEHEMU YA TANO
- 44 Verify source ↗
45. Authorities for expenditure
The Accountant Officer may use funds from the Consolidated Fund as allowed by law, and fund allocations must take implementation, the approved budget, and available funds into account.
44. Mahali ambapo Serikali na taasisi na mashirika ya umma yanakuwa na matumizi yanayotokana na Mfuko Mkuu chini ya Sheria ya Bunge:- (a) Afisa Mhasibu ana mamlaka ya kutumia fedha kadri ya sababu zilizobainishwa katika sheria; na (b) Mgawo wa fedha kwenye mafungu utazingatia utekelezaji, bajeti iliyoidhinishwa na upatikanaji wa fedha. Idhini ya kutumia fedha kutoka Mfuko Mkuu - 45 Verify source ↗
Authorities for expenditure
The Controller and Auditor General must approve the Minister’s use of money from the Consolidated Fund.
45. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, kwa mamlaka aliyopewa, atatoa idhini ya kutumia fedha za Mfuko Mkuu kwa Waziri. (a) Kiasi kinachotakiwa kulipwa katika miezi mitatu inayofuatia kwa ajili ya matumizi ya kisheria; na (b) Kiasi kinachotakiwa kulipwa kwa huduma za mwaka wa fedha chini ya mamlaka ya Sheria ya Matumizi. Utoaji wa malipo Utoaji fedha kutoka Mfuko Mkuu - 46 Verify source ↗
Grants of credit
The Controller and Auditor General must authorize payments from the Government's main fund to the Minister by a document signed by hand.
46. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali atalazimika, kwa hati itakayotolewa kwa mkono wake, kutoa idhini ya kufanya malipo kutoka katikaMfuko Mkuu wa Serikali kwa Waziri- (a) Kiasi kinacho tarajiwa kulipwa katika kipindi cha miezi mitatu kwa ajili ya malipo ya matumizi ya Serikali; na (b) Kiasi kinachotarajiwa kulipwa kwa ajili ya kutoa huduma katika mwaka wa fedha kwa mujibu wa Sheria ya Matumiz ya Serikali. - 47 Verify source ↗
Withdrawal from the Consolidated Fund
Payments from the Consolidated Fund are only allowed as provided by written law and not above the amount appropriated for a service.
47. (1) Malipo hayatafanywa – (a) kutoka kwenye Mfuko Mkuu isipokuwa namna itakavyotolewa na sheria iliyoandikwa; na (b) zaidi ya kiasi ambacho kimetolewa chini ya matumizi kwa huduma yoyote. (2) Kwa kuzingatia vipengele vya sheria inayohusiana na matumizi ya Serikali itatumika kuhusiana na utoaji wa fedha kutoka kwenye Mfuko Mkuu. 83 84 No.11 Budget 2015 Malipo ya fedha kwa mfuko wa Bunge na Mfuko wa Mahakama Kibali cha Mhasibu Mkuu - 48 Verify source ↗
Disbursement of fund to the National Assembly and the Judiciary Fund
The Treasury must pay money every quarter from the General Treasury Fund to the Parliament Fund and the Judiciary Fund.
48. Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 23(1), Hazina italipa katika kila kipindi cha robo mwaka, kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina kwenda katika Mfuko wa Bunge na Mfuko wa Mahakama, kama itakavyo kuwa, fedha zote zilizotolewa na Bunge kugharamia matumizi ya shughuli za Bunge na Mahakama kwa ajili ya robo mwaka huo. - 49 Verify source ↗
Accountant-General’s Warrants
The Accountant-General may authorize accountable officers to spend only within the limits and conditions set by the Treasury warrant, and an accountable officer must not make payments or commitments without a warrant.
49.-(1) Mhasibu Mkuu wa Serikali, kwa kibali alichonacho atawaidhinisha maafisa masuuli kufanya matumizi hadi kufikia kiwango kwa madhumuni na kwa kuzingatia masharti yaliyomo kwenye kibali cha Mlipaji Mkuu wa Serikali. (2) Kibali hakitatolewa na Mhasibu Mkuu wa Serikali mpaka pale kiasi na makusudi ambayo yamesabisha kutolewa yamebainishwa katika kibali kilichotolewa na Mlipaji Mkuu. (3) Kila kibali kitakachotolewa na Mhasibu Mkuu wa Serikali kitazingatia kiwango na masharti ambayo Waziri atayaainisha. (4) Afisa Masuuli anaweza asifanye malipo yoyote au kukubali kulipa kutoka kwenye akaunti au kuingia miadi yoyote au matumizi, isipokuwa imeidhinishwa kwa kibali kufanya hivyo. (5) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo (4) “miadi” maana yake mkataba, makubaliano au mpangilio kwa ajili ya kufanya malipo. Dhana ya miadi - 50 Verify source ↗
Assumption of commitments
Public institutions or agencies must make commitments only under the stated conditions.
50. Taasiri au Mashirika ya Umma itafanya miadi chini ya masharti yafuatayo- (a) Kiasi ambacho kitalipwa chini ya miadi ni sawa na au pungufu ya kiasi kilichopo kwa ajili ya matumizi; (b) Uhalali wa malipo yatakayofanywa chini ya miadi itakuwa imehakikiwa; na (c) Miadi ni kwa mujibu wa matoleo ya fedha ya bajeti ya robo mwaka. Miadi ya miaka mingi - 51 Verify source ↗
Multi-annual commitments
Multi-year commitments must first obtain the Minister’s approval.
51.-(1) Miadi yoyote ya miaka kadhaa itahitaji kwanza kupata kibali cha Waziri. (2) Kupata kwanza kibali cha Waziri kunahitajika kwa ajili ya kuhakikisha kuwa- 84 No.11 Budget 2015 85 Mfumo wa udhibiti wa miadi (a) miadi haisababishi ukomo wa matumizi ya miaka kadhaa chini ya Mwongozo wa Mpango na Bajeti; (b) kiasi ambacho kinatakiwa kulipwa chini ya miadi katika mwaka uliopo wa fedha kinatakiwa kiwe sawa au pungufu kuliko kiasi kilichopo kwa ajili ya matumizi; (c) uhalali wa malipo yatakayofanyika chini ya miadi ini budi yawe yamehakikiwa; na (d) sehemu ya miadi inayotakiwa kulipwa kwa mwaka husika wa bajeti ni sawa na robo ya bajeti iliyotolewa kama ipo. - 52 Verify source ↗
Commitment control system
Serikali, taasisi na mashirika ya umma lazima yadumishe mfumo wa udhibiti wa miadi na yazuie malipo ya bajeti bila miadi ya msingi kuingizwa na namba kutolewa.
52.-(1) Serikali na Taasisi na Mashirika ya Umma yatahitajika- (a) kutunza mifumo ya udhibiti wa miadi ambapo miadi yote inayodhaniwa itaingizwa; na (b) kuzuiwa malipo kufanyika kutoka kwenye bajeti bila ya miadi ya msingi kuwa imeingizwa kwenye mfumo wa udhibiti wa miadi na namba ya miadi kutolewa na mfumo. (2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo (1), miadi yote ambayo haijatekelezwa itajumuishwa kwenye makadirio ya mwaka yakionesha- (a) kuna kiasi cha kutosha kwenye kipengele ili kikidhi miadi ya miaka kadhaa ambayo haijatekelezwa ambayo italipwa chini ya kipengele husika; na (b) ukomo wa matumizi na maoteo ya kibajeti chini ya Mwongozo wa Mpango na Bajeti yanaakisi kikamilifu miadi ya miaka kadhaa. Mikataba ya Miradi ya Maendeleo - 53 Verify source ↗
Report on expenditure commitments
Public institutions and agencies must get the Minister’s approval before signing contracts with financial commitments.
53.-(1) Taasisi na Mashirika ya Umma yatakikiwa kwanza kupata kibali cha Waziri kabla ya kuingia kwenye mikataba yenye mahitaji ya kifedha. (2) Waziri anaweza, ndani ya siku thelathini, kutoa idhini ya kifedha kwa masharti kwamba mkataba unatimiza vigezo vya miadi ya miaka kadhaa na mradi unawezekana kwa maoni ya Waziri. 85 86 No.11 Budget 2015 Taarifa za ndani za mwaka Taarifa ya matumizi ya miadi Taarifa za Utekezaji - 54 Verify source ↗
Development project contracts
Named public finance officials and public bodies must submit or publish monthly or quarterly budget and revenue/expenditure reports within the time set by regulations.
54.-(1) Mhasibu Mkuu wa Serikali ndani ya muda uliobainishwa kwenye Kanuni atatakiwa, atawasilisha kwa Katibu Mkuu, taarifa ya Serikali na taasisi na mashirika ya umma kuhusiana na mapato na matumizi halisi kwa mwezi uliopita na kiasi ambacho kinatarajiwa kukusanywa au kutumika katika mwezi huo na Serikali. (2) Taasisi na mashirika ya umma, mifuko maalum, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itatoa taarifa kwa Mlipaji Mkuu kuhusu mapato na matumizi katika kila robo mwaka. (3) Kamishna wa Bajeti kwa kushirikiana na Kamishna wa uchambuzi wa sera, ndani ya muda utakaoelezwa na kanuni watachapisha taarifa utekelezaji wa bajeti ya robo mwaka. (4) Maafisa Wahasibu, ndani ya muda utakaoelezwa kwenye kanuni atawasilisha taarifa ya utekelezaji ya robo mwaka kwa Katibu Mkuu Hazina. - 55
The responsible officer must prepare and submit a quarterly report to the Secretary General about actual and estimated appointments and the financial status of the department or fund.
55.-(1) Afisa masuuli atalazimika kuandaa na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu taarifa ya robo mwaka ya miadi halisi na miadi ya makisio na hali ya kifedha ya kasma au mfuko, kutegemea shughuli za kasma au Mfuko na utekelezaji wa bajeti ya kasma ya Mfuko. - 56 Verify source ↗
57. Quarterly statements of the Government
The Minister must submit execution reports to Parliament: first within three months after presenting the budget, then quarterly, and again within six months after the annual budget is approved and at each financial year end.
56.-(1) Waziri, ndani ya miezi mitatu baada ya kuwasilisha bajeti kwenye Bunge na katika kila robo mwaka baada ya hapo atawasilisha kwenye Bunge, kwa mtiririko na kwa ujumla taarifa ya utekelezaji. (2) Endapo Bunge halipo kwenye vikao vyake na katika tarehe zilizobainishwa kwenye kifungu kidogo (1), taarifa ya utekelezaji itawasilishwa katika Bunge katika siku ya pili, mara tu baada ya kuanza kwa Bunge. (3) Taarifa ya Utekelezaji- (a) itaonesha kipindi cha mapitio, na jinsi ambavyo malengo na shabaha katika Mwongozo wa Mpango na Bajeti yamefikiwa; na (b) kubainisha kiasi kifuatacho na kuvilinganisha na shabaha zinazoendana katika kipindi cha mapitio- 86 No.11 Budget 2015 87 (i) mapato halisi katika kipindi husika na ikilinganishwa wa matarajio; (ii) matumizi halisi kwa fungu, yakitofautishwa baina ya matumizi ya maendeleo na matumizi ya kawaida kwa kipindi hicho; na (iii) mikopo halisi kwa kipindi hicho, na kwa mwaka wa fedha hadi mwisho wa mwaka wa fedha. (4) Ambapo malengo na shabaha hayajafikiwa, taarifa ya kisheria itataja- (a) sababu za kwa nini malengo na shabaha hazikufikiwa; (b) hatua za marekebisho zinachukuliwa kuhakikisha kuwa malengo na shabaha ambayo hayakufikiwa yatafikiwa katika robo ijayo; na (c) Mapendekezo yoyote ya maamuzi ya kisera ya Serikali ambayo yanaweza kuathiri kwa kiwango kikubwa malengo na shabaha katika taarifa ya matarajio ya bajeti au utekelezaji wa kibajeti na kiuchumi kwa ujumla katika nchi. (5) Mhasibu Mkuu wa Serikali, ataandaa taarifa ya kila mwezi ya Mfuko Mkuu ambayo itahusisha mapato halisina ridhaa za matumizi zilizotolewa na kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu ili kutumika katika maandalizi ya taarifa mbalimbali. (6)Waziri atalazimika, ndani ya miezi sita baada ya Bunge kuidhiniha Bajeti ya mwaka na kila mwisho wa mwaka wa fedha, kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa ajili ya kujadiliwa. Taarifa za Serikali za robo mwaka - 57 Verify source ↗
Quarterly statements of the Government
The Government Accountant General and a responsible officer must prepare and submit specified financial reports, including a quarterly government revenue/expenditure statement and transfer-of-funds reports.
57.-(1) Mhasibu Mkuu wa Serikali ataandaa taarifa ya mapato na matumizi halisi kwa ujumla wake ya Serikali na Taasisi na Mashirika ya Umma na kuwasilisha kwa Waziri ambaye atawasilisha kwenye Bunge mwezi mmoja baada ya mwisho wa kila robo mwaka. (2) Afisa Masuuli ataandaa na kuwasilisha kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali taarifa za uhamisho wa fedha uliofanyika ndani ya Mafungu husika. 87 88 No.11 Budget 2015 Misingi ya usimamizi wa mapato SEHEMU VI USIMAMIZI WA MAPATO
Part
SEHEMU VI
- 58
Government revenue from domestic and foreign sources must be paid into the Consolidated Fund, and anyone authorized to collect revenue must collect, account for, and report it efficiently while taking precautions against leakage.
58.- Sehemu ya Mapato ya Bajeti itazingatia misingi ifuatayo- (a) mapato yote ya Serikali kutoka vyanzo vya ndani na nje yataingizwa Mfuko Mkuu wa Hazina; (b) yeyote aliyepewa mamlaka ya kukusanya mapato ya Serikali atawajibika katika ukusanyaji wa mapato wenye ufanisi, na utunzaji hesabu na utoaji taarifa kwa kuzingatia sheria husika na kuchukua tahadhari ili kuzuia ufujaji wa mapato ya Serikali;na (c) mapato yote ya Serikali yataingizwa kwenye Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Fedha za Serikali. Majukumu ya ukusanyaji mapato na usimamizi - 59 Verify source ↗
Principles for management of revenues
The Minister must set a process for receiving parliamentary comments and recommendations on next year’s budget estimates, and the Secretary General must carry out several revenue-management duties.
59.-(1) Waziri ataweka utaratibu wa kupokea maoni na mapendekezo kuhusu makadirio ya bajeti kwa mwaka ujao wa fedha kutoka kwa Bunge ambayo yatawasilishwa kwa Waziri si zaidi ya tarehe 15 Februari. (2) Majukumu ya Katibu Mkuu kuhusiana na ukusanyaji na usimamizi wa mapato yatakuwa ni- (a) kusimamia na kuweka misingi ya mipango na utafiti wa vyanzo vya mapato vya sasa na fursa ya mapato zaidi zilizopo; (b) kuanzisha mfumo ambao utaweka muda maalum wa kupokea mapendekezo ya hatua za mapato; (c) kuandaa hatua za mapato kwa bajeti ya Serikali; (d) kutafuta rasilimali ikiwa pamoja na misaada kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na kujumuisha fedha hizo kwenye michakato ya mipango, bajeti na utoaji taarifa na uwajibikaji kama inavyoelezwa na sheria hii. (e) kuboresha na kusimamia uwazi, ufanisi na namna inayofaa ya usimamizi wa mapato; 88 No.11 Budget 2015 89 SEHEMU YA SABA USIMAMIZI WA VIFUNGU VIDOGO VYA NJE YA MFUMO WA BAJETI YA SERIKALI Usimamizi wa kibajeti na kifedha za serikali za mitaa
Part
SEHEMU YA SABA
- 60
Waziri husimamia masuala ya bajeti na fedha ya mamlaka za Serikali za Mitaa, na baadhi ya taasisi zinahitaji idhini yake kabla ya kuanzishwa au kusimamiwa.
60.-(1) Waziri atasimamia masuala ya kibajeti na kifedha ya mamlaka ya Serikali za Mitaa. (2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1), bajeti inayopendekezwa na bajeti zilizoidhinishwa kwa pamoja zitawasilishwa kwa Waziri kwenye dhamana ya mamlaka ya serikali za mitaa kwa kuzingatia muda maalum. (3) Uanzishwaji na usimamizi wa asasi zinazofanya kazi nje ya mfumo wa bajeti na mifuko maalum ya serikali za mitaa kutahitaji idhini ya Waziri wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Mamlaka ya Waziri kusamehe kodi, ada na tozo - 61
Waziri anaweza kusamehe kodi, ada au tozo za Serikali kwa kufuata vigezo vya sheria yoyote, lakini lazima aweke kumbukumbu za kila msamaha na sababu zake na awaarifu Bunge kila robo mwaka.
61. Waziri anaweza kusamehe kodi, ada au tozo zilizowekwa na Serikali kwa mujibu wa vigezo kwenye sheria yoyote, ili mradi atatunza kumbukumbu ya kila msahama pamoja na sababu za kutoa msamaha husika na kutoa taarifa Bungeni katika kipindi cha kila robo mwaka. Usimamizi wa kibajeti na kifedha na wa asasi nyingine za Serikali - 62 Verify source ↗
Budgetary and financial management of local government authority
Certain extra-budgetary institutions and special funds must submit proposed and approved budgets to the Minister and the responsible Minister; loans for those bodies need the Minister’s prior approval where the body has legal capacity.
62.-(1) Waziri mwenye dhamana usimamizi wa kibajeti na kifedha na asasi zilizo nje ya mfumo wa bajeti na Mifuko Maalum inayojumuishwa ndani ya Serikali Kuu na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. (2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1)- (a) bajeti inayopendekezwa na bajeti iliyoidhinishwa ya asasi zilizo nje ya mfumo wa bajeti na Mifuko inatakiwa kuwasilishwa kwa Waziri na Waziri mwenye dhamana kwa kuzingatia muda maalum ulioelezwa kwenye Kanuni; (b) mikopo kwa ajili ya asasi zilizo nje ya mfumo wa bajeti na Mifuko maalum itahitaji kupata kwanza kibali cha Waziri, endapo asasi hiyo iliyo nje mfumo wa bajeti ina uwezo huo kisheria. 89 90 No.11 Budget 2015 SEHEMU YA NANE MASHARTI YA JUMLA Kanuni maelekezo na
Part
SEHEMU YA NANE
- 63
Waziri anaweza kutunga kanuni za kusaidia utekelezaji wa Sheria hii, na kanuni hizo zinaweza kuweka maelezo ya taarifa, muda wa kuwasilisha taarifa kabla ya kuwasilishwa Bungeni, na vigezo vingine vya utekelezaji.
63.-(1) Waziri anaweza kutunga kanuni zinazohitajika kuwezesha utekelezaji wa masharti ya Sheria hii. (2) Bila kuathiri masharti kifungu kidogo (1), kanuni zitakazotungwa zibaainisha- (a) yaliyomo na aina mbalimbali ya taarifa zinazohitajika na Sheria hii; (b) muda wa kufuata kuwasilisha taarifa kabla ya kuwasilisha Bungeni; (c) vigezo ambavyo Bunge litatumia kuamua endapo hoja za ukaguzi zimezingatiwa; na (d) kanuni au vigezo vitakavyotumika kubainisha mgao wa fungu haukuzingatia sheria hii. Kuongeza kipindi muda uliowekwa cha - 64
Bunge may extend the time for submitting required information or documents by resolution.
64. Bunge linaweza kuongeza muda wa kuwasilisha taarifa au nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa Sheria hii au muda uliowekwa kikatiba kupitia azimio. Uwajibishaji wa mamlaka iliyoshindwa kutekeleza matakwa ya Sheria - 65
Waziri must explain failures to comply with the Act and take corrective action for public institutions that breach financial procedures or make unauthorized expenditure.
65.-(1) Serikali na taasisi za umma zitakaposhindwa kutekeleza masharti ya Sheria hii, Waziri atalazimika kutoa maelezo na mazingira yaliyosababisha kushindwa kutekeleza masharti husika. (2) Endapo inapothibitika kwamba afisa wa umma kwa kusudia au kwa uzembe amesababisha Serikali au taasisi ya umma kushindwa kutekeleza masharti ya Sheria hii, Afisa huyo atakuwa ametenda kosa la kinidhamu na atachukuliwa hatua za kinidhamu na atawajibishwa yeye mwenyewe. (3) Waziri atachukua hatua za kurekebisha taasisi ya umma pale inaposhindwa kufuata taratibu za kifedha au matumizi za ziada au matumizi ambayo hayajaidhinishwa. (4) Hatua za kurekebisha zinazoainishwa katika kifungu kidogo cha (3) zitajumuisha: 90 No.11 Budget 2015 91 (a) kuwasilisha na kuidhinisha Mpango kazi; (b) kupunguza kiasi cha bajeti iliyotumika zaidi ya iliyoidhinishwa katika mwaka unaofuata wa fedha; (c) kuweka sharti la Waziri kuomba kibali kabla ya kufanya matumizi; na (d) kusitisha mamlaka ya Afisa Masuuli katika usimamizi wa fedha. Hatua za urekebishaji dhidi ya Serikali na Taasisi za Umma - 66 Verify source ↗
Regulations, instructions and directions
The Minister may take corrective measures against listed public entities if they fail to follow financial procedures or face financial difficulties.
66.-(1) Waziri atachukua hatua za kurekebisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Taasisi iliyopo nje ya bajeti ya Serikali na mfuko maalum ikiwemo Serikali, taasisi ya umma, pale Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Taasisi iliyopo nje ya bajeti ya Serikali na mfuko maalum itakaposhindwa kufuata taratibu za kifedha au matatizo ya kifedha. (2) Hatua za kurekebisha zitajumuisha- (a) Kuwasilisha Mpango wa Utekelezaji; (b) Kuweka sharti la Waziri kuomba kibali kabla ya kufanya maamuzi; (c) Kupunguza au kusimamisha uhamishaji wa fedha za bajeti; au (d) Kuteua msimamizi wa fedha ambaye atakuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi. Hatua dhidi taasisi za umma - 67 Verify source ↗
Indemnity of public officers
Public officers and certain public bodies are exempt from administrative or criminal action for good-faith acts or omissions done while carrying out assigned duties under this Act.
67. Afisa wa umma aliyepo Serikalini, taasisi ya umma,Taasisi iliyopo nje ya bajeti ya Serikali na mfuko maalum hatachukuliwa hatua mwenyewe za kiutawala au za makosa ya jinai kwa kufanya au kuacha kufanya kwa nia nzuri wakati wa utekelezaji au alipotakiwa kutekelezaji wajibu aliopewa au wakati wa utekelezaji wake wa majukumu aliyopewa kwa mujibu wa Sheria hii na nafasi yake ya kazi. Kuingia kwa dharura kwa mafias wa mamlaka - 68 Verify source ↗
Overriding effect of the Act
This provision says the Act overrides other laws on specified budget-related matters.
68. Sheria hii itakuwa na masharti ya mamlaka ya juu dhidi ya sheria nyingine katika masuala yoyoyte yanayohusu- (a) bajeti ya taifa, bajeti ya taasisi za umma, mamlaka za serikali za mitaa au wakala nje ya bajeti; 91 92 No.11 Budget 2015 Masharti Mpito ya (b) usimamizi wa mchakato wa bajeti; (c) utekelezaji, ufuatiliaji. Tathimini na utoaji wa taarifa wa bajeti; (d) usimamizi wa mapato na matumizi ya bajeti; na (e) kusimamia taasisi za umma na wakala nje ya bajeti. - 69 Verify source ↗
Transitional provisions
This section sets transitional budget rules for votes/funds, including when they start operating, what they may cover before the annual Appropriation Act begins, and a 25% cap where section 64 has not been complied with.
69.-(1) Sheria hii itakapoanza kutumika, fungu husika kwa ajili ya mafungu mbalimbali ambazo bado hazijawasilishwa kwa kuzingatia taarifa au utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi zitaanza kutumika siku baada ya makadirio kuwasilishwa Bungeni. (2) Mafunguyataomba kiasi kinachotakiwa kwa ajili ya kukidhi matumizi muhimu ya shughuli za Serikali na taasisi za umma kabla ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa mwaka huo. (3) Bunge litaweka ukomo wa kiasi kitakachoidhinishwa kwa fungu husika kwa asilimia ishirini na tano au chini ya kiasi chote kilichopo katika makadirio ya mwaka endapo anayeomba vote hajatekeleza masharti ya kifungu cha 64. (4) Katika kifungu hiki, “shughuli za Serikali” zitamaanisha huduma zozote zinazotolewa na kazi zinazofanywa na fungu ikiwa huduma hizo ni za kawaida au sio za kawaida. SEHEMU YA TISA MAREKEBISHO YATOKANAYO MAREKEBISHO YA SHERIA YA BUNGE (UTAWALA) (SURA YA 115)
Part
SEHEMU YA TISA
- 70 Verify source ↗
71. Addition of section 18A
This section must be read together with the Administration Act, and that Act is referred to here as the “main Act.”
70. Sehemu hii itasomwa pamoja na Sheria ya Bunge (Utawala), ambapo itarejewa kama “Sheria kuu”. - 71 Verify source ↗
Addition of section 18A
This provision amends the law by adding a new section 18A after section 18.
71. Sheria Kuu inafanyiwa marekebisho yafuatayo- Tafsiri Sura ya 115 Kuongezwa kwa kifungu cha 18A. 92 No.11 Budget 2015 93 (a) Kuongeza kifungu kipya cha 18A. mara baada ya kifungu cha 18 kama ifuatavyo: “Kuanzishwa kwa Ofisi ya Bunge ya Bajeti - 18 Verify source ↗
The Commissioner for Policy Analysis
Kuna Ofisi ya Bunge ya Bajeti ndani ya huduma za Bunge, na Ofisi hiyo lazima ifanye uchambuzi na kazi za ushauri, uandaaji wa taarifa, na uchunguzi wa masuala ya bajeti na uchumi kwa Bunge na Kamati zake.
18.A (1) Kutakuwa na Ofisi ya Bunge ya Bajeti ndani ya huduma za Bunge, ambayo itakuwa na watumishi watakaoteuliwa na Tume ya Huduma za Bunge kwa kuzingatia ujuzi, kuanzishwa kwa Ofisi ya Bunge utaalamu na uzoefu katika masuala ya fedha, uchumi na sera za umma. (2) Ofisi ya Bunge ya Bajeti itafanya uchambuzi wa kina na kwa wakati kuhusu bajeti ya Serikali kwa Bunge na Kamati zake. (3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa kifungu kidogo cha (2), Ofisi ya Bunge ya Bajeti itatekeleza yafuatayo: (a) kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu taarifa zinazohusu bajeti, fedha na kiuchumi kwa Kamati za Kudumu za Bunge; (b) kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Bunge na Kamati zake za kudumu katika kutekeleza majukumu yake; (c) kuliwezesha Bunge kuhakikisha utekelezaji wa Sheria hii; (d) kuandaa taarifa kuhusu maoteo na mapendekezo ya masuala ya kibajeti kwa Bunge na Kamati zake za Kudumu; (e) kutoa taarifa zinazohusu Bajeti kwa Kamati za Kudumu za Bunge katika maeneo yao ya kiutawala; (f) kuwasilisha taarifa kuhusu maoteo ya kiuchumi, maoteo ya kibajeti na jinsi ya kupunguza nakisi ya bajeti. 93 94 No.11 Budget 2015 (g) kubainisha na kutoa mapendekezo kuhusu Miswada ya Sheria na hati za kisheria ambazo zinahusu ongezeko au punguzo la mapato na bajeti ya Serikali; (h) kuandaa tafiti kuhusu masuala mahsus kama vile vihatiarishi vya kifedha na mMashirika na taasisi za umma na pia masuala ya sera ya fedha; vinavyosababishwa (i) kutoa ushauri wa jumla kwa Bunge na Kamati zake za Kudumu za Bunge kuhusu bajeti ya Serikali na uchumi wa Taifa; (j) kuandaa uchambuzi wa masuala mahsusi, pamoja na vihatarishi vya kifedha na Serikali na sera za Serikali na shughuli zake na kushauri Bunge na Kamati zake za Kudumu; vinavyosababishwa (k) kupitia mapendekezo ya Bajeti ya Serikali na mwelekeo wa uchumi na kulishauri Bunge; (l) kuanzisha na kukuza uhusiano na na asasi nyingine ya HAZINA kitaifa na kimataifa maslahi katika masuala ya Bajeti na masuala ya Kijamii na Kiuchumi kama ambavyo zinafaa kwa ajili ya itaona utekelezaji wa majukumu yake kwa ufanisi; (m) kuhakikisha taarifa na nyaraka nyinginezo zinazoandaliwa na Ofisi ya Bunge ya Bajeti zinaandaliwa, kuchapidhwa na kusamazwa; 94 No.11 Budget 2015 95 (n) kutoa taarifa kwa Kamati za Bunge kuhusu Muswada za Kudumu wowote wa Sheria uliowasilishwa Bungeni ambao unahusu masuala ya kiuchumi na kifedha, kwa kufanya reja kwenye misingi ya kibajeti na malengo ya kifedha yaliyobainishwa kwenye Mwongozo wa Mpango na Bajet; na (o) kupendekeza kwa kamati ya Bunge ya Bajeti mfumo mbadala wa mapato kwa mwaka husika wa fedha. (4) Katika kutekeleza majukumu yake, Ofisi ya Bunge ya Bajeti itazingatia misingi ya kushirikisha Umma katika masuala ya kibajeti. ” ; (b) kufuta vifungu vya 28na 29 na kuweka badala yake yafuatavyo: “Makadirio na mapato - 29 Verify source ↗
Appropriations to lapse at the end of financial year
The Secretary must prepare Parliament’s annual revenue and expenditure estimates and send them to the Parliamentary Service Commission for review and approval.
29.-(1) Katibu ataandaa kila mwaka, makadirio ya mapato na matumizi ya Bunge na kuyasafirisha kwenye Tume ya Huduma za Bunge kwa mapitio na kuridhia. (2) Katibu atawasilisha kwenye kikao cha mashauriano kitakacho jumuisha Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, Waziri mwenye dhamana na masuala ya mipango na kamati ya Bunge ya Bajeti madadirio yaliyoidhinishwa chini ya kifungu kidogo cha (1) kwa kupitishwa. (3) Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha atawasilisha Bungeni makadirio ya mapato kwa kuidhinishwa. ”; na na matumizi ya Bunge 95 96 No.11 Budget 2015 (c) kurekebisha vifungu vya 31 hadi 41 ili visomeke kama vifungu vya 30 hadi 40 MAREKEBISHO YA SHERIA YA UKAGUZI YA UMMA (SURA YA 418) Tafsiri - 72 Verify source ↗
73. Amendment of section 44
This section is to be read together with the Public Audit Act, referred to here as the principal Act, and it amends section 44.
72. Sehemu hii itasomwa pamoja na Sheria ya Ukaguzi wa Umma hapa ikirejewa kama “Sheria kuu”. Marekebisho ya kifungu cha 44 - 73 Verify source ↗
Amendment of section 44
This provision amends section 44(2) by replacing specified words with “Kamati ya Bunge ya Bajeti”.
73. Sheria kuu irekebishwe kwenye sehemu 44(2), kwa kufuta maneno “Kamati ya Hesabu za Serikali marekebisho ya kifungu cha 44 na badala yake kuweka maeneo “Kamati ya Bunge ya Bajeti”. MAREKEBISHO YA SHERIA YA UTAWALA WA MAHAKAMA (SURA YA 237) Tafsiri - 74 Verify source ↗
75. Amendment of section 39
This section is to be read together with the Administration of Courts Act, which is referred to as the principal Act.
74. Sehemu hii itasomwa pamoja na Sheria ya Utawala wa Mahakama ambapo itarejewa kama Tafsiri “Sheria kuu”. Marekebisho ya kifungu cha 44 - 75 Verify source ↗
Amendment of section 39
This section amends the principal law by deleting section 59 and replacing it with a new section on the Court’s estimates of revenue and expenditure.
75. Sheria kuu inarekebishwa kwa kufuta kifungu cha 59 na kuandika kifungu kipya kifuatacho: “Makadirio ya mapato na matumizi ya Mahakama - 59 Verify source ↗
Principles for management of revenues
The Chief Registrar of the Court must prepare annual revenue and expenditure estimates, submit them for approval, and pass the approved estimates through the budget process for parliamentary consideration and approval.
59.-(1) Mtawala Mkuu wa Mahakama, kila mwaka wa fedha ataandaa makadirio ya na mapato na matumizi kuyawasilisha kwenye Tume kwa mapito na kuridhiwa. ya mahakama (2) Mtawala Mkuu wa Mahakama atawasilisha makadirio yaliyoridhiwa chini ya kifungu kidogo cha (1) kwa Kamati ya Bunge ya bajeti kwa kujadiliwa na kupitishwa kwenye kikao cha mashauriano kati ya Waziri mwenye dhamana na masuala ya Fedha, Waziri mwenye chamana ya masuala ya mipango. 96 Na.11 Budget 2015 97 (3) Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha atawasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya mahakama kwa ajili ya kupitishwa. ” Imepitishwa na Bunge tarehe 28 Machi, 2015 THOMAS D. KASHILILLA Katibu wa Bunge 97
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
The Budget Act, 2015
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign inLexChat organizes source-backed legal information for research. Verify amendments, commencement, and current legal force with the official publisher before relying on it.