SHERIA NDOGO YA HIFADHI YA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI ZA MWAKA2022
This section states the short title of the by-law: Ikungi District Council Environmental Conservation By-Law 2022.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA HIFADHI YA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI ZA MWAKA2022
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the by-law: Ikungi District Council Environmental Conservation By-Law 2022. This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, protected area, council, environmental conservation, grazing areas, livestock, forests, and the Executive Director. Mtu anayefuga katika eneo la Halmashauri lazima azingatie masharti ya ufugaji yaliyowekwa na Halmashauri, na baadhi ya vitendo vya usafirishaji, uingizaji, uuzaji na ufugaji wa mifugo ni kosa. Wakulima katika eneo la Halmashauri lazima wafuate masharti ya kilimo, wasiendeshe kilimo katika maeneo yaliyokatazwa, wasiitumie ardhi kinyume cha mpango uliopitishwa, na wasisafishe mashamba kwa kuchoma moto bila kibali maalumu. It is not allowed to commercially excavate sand, gravel, stones, soil, or other construction minerals near homes, protected areas, riversides, or in rivers, dams, or lakes unless there is a special permit from the Council.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA HIFADHI YA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI ZA MWAKA2022
Showing 11 of 11
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya Hifadhi
AI-assisted research summary: This section states the short title of the by-law: Ikungi District Council Environmental Conservation By-Law 2022.
1. Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ya Mwaka 2022. - 2 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, protected area, council, environmental conservation, grazing areas, livestock, forests, and the Executive Director.
2. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utaeleza- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “eneo la hifadhi” maana yake ni maeneo ya milima, mbuga za wanyama, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi, mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji unaozingatia masharti na maelekezo yatakayotolewa na Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; “maeneo ya malisho” maana yake ni sehemu zote ambazo zimetengwa na Halmashauri au Kijiji kuwa maeneo ya malisho ya mifugo; “mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika 1 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Tangazo la Serikali Na. 219 (Linaendelea.) Sura 323 Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mifugo” maana yake ni mifugo yoyote inayofugwa na binadamu; “Misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia kumi na miti, uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia hamsini au zaidi, ya vichaka na miti na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya hifadhi ambayo imetangazwa chini ya Sheria ya Misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na ni pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza kazi za Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii. Masharti kuhusu ufugaji - 3 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayefuga katika eneo
AI-assisted research summary: Mtu anayefuga katika eneo la Halmashauri lazima azingatie masharti ya ufugaji yaliyowekwa na Halmashauri, na baadhi ya vitendo vya usafirishaji, uingizaji, uuzaji na ufugaji wa mifugo ni kosa.
3.-(1) Mtu yeyote anayefuga katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo: (a) kufuga mifugo kwa idadi itakayokuwa imeelekezwa na Halmashau ri (b) kufuga na kulisha mifugo yake katika maeneo ya malisho yaliyopangwa na Halmashauri; (c) kupitisha mifugo yake katika njia zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; (d) kuwa na kadi ya mifugo itakayoonyesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (e) kupeleka mifugo katika majosho kama atakavyoelekezwa na Halmashauri; na (f) kuweka alama kwenye mifugo yake kama itakavyolekezwa na Halmashauri. (2) Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kufanya yafuatayo: (a) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani; (b) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo lingine bila kibali kutoka kwa moja hadi Halmashauri; (c) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (d) kuuza au kununua mifugo katika maeneo 2 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Tangazo la Serikali Na. 219 (Linaendelea.) ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri; (e) kufuga mifugo kwa zaidi ya idadi iliyoelekezwa na Halmashauri; au (f) kuchunga, kulisha au kunywesha maji mifugo katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hiyo. (3) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kukamata yasiyoruhusiwa mifugo inayokutwa katika maeneo kuchungia, kulishia au kunywesha mifugo. (4) Halmashauri inaweza, baada ya kupata Amri ya Mahakama, kuuza kwa njia ya mnada wa hadhara mifugo iliyokamatwa, fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmiliki wa mifugo baada ya kutoa gharama za ukamataji na utunzaji wa mifugo na minada. (5) Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote itakayotokea wakati wa kutekeleza mamlaka yake chini kifungu hiki isipokuwa kama hasara hiyo itasababishwa na uzembe wa Halmashauri. Masharti kuhusu kilimo - 4 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayelima katika eneo
AI-assisted research summary: Wakulima katika eneo la Halmashauri lazima wafuate masharti ya kilimo, wasiendeshe kilimo katika maeneo yaliyokatazwa, wasiitumie ardhi kinyume cha mpango uliopitishwa, na wasisafishe mashamba kwa kuchoma moto bila kibali maalumu.
4.-(1) Mtu yeyote anayelima katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo: (a) taratibu za kilimo kwa kuzingatia kalenda ya kilimo ya Halmashauri na kwa kuzingatia Sheria zinazosimamia masuala ya ardhi na mazingira; (b) kutolima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa au maziwa au kufanya jambo lolote litakaloharibu hifadhi ya mazingira; (c) kutotumia ardhi kinyume na matumizi kama ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri; na (d) kutosafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto, isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri. (2) Kibali cha kusafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto kitakuwa cha maandishi na kitaonyesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma moto. (3) Muda unaoruhusiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hii ni kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne kamili asubuhi na saa kumi na mbili jioni hadi saa 3 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Tangazo la Serikali Na. 219 (Linaendelea.) moja kamili usiku. (4) Itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kufanya yafuatayo: (a) kutozingatia kalenda ya kilimo ya Halmashauri; (b) kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa au maziwa au kufanya jambo lolote litakaloharibu hifadhi ya mazingira; (c) kutumia ardhi kinyume na mpango wa matumizi wa ardhi ulioidhinishwa na Halmashauri; au (d) kusafisha shamba kwa njia ya kuchoma moto bila ya kuwa na kibali au nje ya muda ulioruhusiwa chini ya Sheria Ndogo hii. - 5 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchimba mchanga,
AI-assisted research summary: It is not allowed to commercially excavate sand, gravel, stones, soil, or other construction minerals near homes, protected areas, riversides, or in rivers, dams, or lakes unless there is a special permit from the Council.
5.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuchimba mchanga, kokoto, mawe, udongo au madini yoyote ya ujenzi kwa madhumuni ya kibiashara karibu na makazi ya watu, maeneo ya hifadhi, kandokando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa kibali maalumu cha Halmashauri. (2) Mtu atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. Uchimbaji wa mchanga Uhifadhi wa vyanzo vya maji - 6 Verify source ↗
(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakuwa
AI-assisted research summary: Watu wote katika eneo la Halmashauri lazima wafanye hatua za kulinda vyanzo vya maji na hawaruhusiwi kufanya shughuli zinazoharibu maeneo ya hifadhi au ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji.
6.-(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakuwa na wajibu wa- (a) kupanda miti isiyonyonya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Halmashauri; (b) kutoishi katika eneo la hifadhi au chanzo cha maji ndani ya mita sitini; (c) kutolima, kutokata miti, kutochunga mifugo au kutofanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote eneo lililotangazwa kuwa eneo la hifadhi au chanzo cha maji; (d) kutoelekeza mabomba ya maji machafu au kujisaidia kupuliza dawa za kuua wadudu kwenye mito, mabwawa, maziwa, visima, mifereji, chemchem au sehemu yoyote ambayo ni chanzo cha maji; (e) kutojimilikisha eneo ambalo ni chanzo cha maji cha umma; 4 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Tangazo la Serikali Na. 219 (Linaendelea.) (f) kutojenga choo cha shimo au jalala la kutupia taka umbali wa chini ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji; na (g) kutofanya shughuli yoyote ya kibinadamu ndani ya mita sitini kutoka chanzo cha maji. (2) Mtu atakayekiuka masharti ya kifungu hiki atakuwa ametenda kosa. Uhifadhi wa misitu - 7 Verify source ↗
(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakuwa
AI-assisted research summary: Watu wote katika eneo la Halmashauri lazima wasikate miti, wasichome misitu, na wasivune miti bila kibali kinachohitajika; uchomaji wa mkaa unahitaji kibali maalum na maeneo yaliyotengwa.
7.-(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atakuwa na wajibu wa- (a) kutokata miti katika maeneo ya misitu iliyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka katika Mamlaka husika; (b) kutochoma moto misitu kwa namna yoyote ile katika eneo la Halmashauri; (c) kutovuna miti isipokuwa kwa kibali maalum cha Halmashauri; au (d) kutovuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe malum. (2) Uchomaji wa mkaa utafanyika kwa kibali maalum cha Halmashauri katika maeneo yaliyotengwa mahsusi kwa ajili hiyo. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) na (2) atakuwa ametenda kosa. Utupaji wa taka - 8 Verify source ↗
(1) Kila mtu katika eneo
AI-assisted research summary: Everyone in the council area must have waste-holding facilities and a clean, safe toilet.
8.-(1) Kila mtu katika eneo la Halmashauri atatakiwa kufanya yafuatayo- Wajibu wa jumla (a) kuwa na shimo au chombo maalum cha kuhifadhi taka ngumu na laini; na (b) kuwa na choo safi na salama. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. - 9 Verify source ↗
(1) Wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au
AI-assisted research summary: Wakazi wa maeneo yaliyoharibiwa na uoto au mazingira lazima wayarejeshe kwa kupanda miti na wasiharibu zaidi; pia wakazi wa eneo lenye moto unaotishia watu, mali au mazingira lazima washiriki kuzima moto kwa maelekezo ya Halmashauri.
9.-(1) Wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira yameharibiwa watakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa wanalirudisha katika hali yake ya kawaida eneo hilo kwa kupanda miti na kuendelea kutoharibu mazingira ili kuwezesha uoto au mazingira yarudi katika hali yake ya kawaida kwa kadri 5 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Tangazo la Serikali Na. 219 (Linaendelea.) watakavyoelekezwa na Halmashauri. (2) Wakazi wa eneo ambalo moto utatokea unaotishia maisha ya watu, mali au mazingira watakuwa na wajibu wa kushiriki kuzima moto huo kwa kadri watakavyoelekezwa na Halmashauri. (3) Mtu yeyote atakayeshindwa, bila sababu za msingi, kutekeleza maelekezo ya Halmashauri chini ya kifungu kidogo cha (1) na cha (2) atakuwa ametenda kosa. Uwezo wa Afisa Mwidhiniwa - 10 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kuingia eneo, nyumba au jengo lolote kati ya saa 12 asubuhi na saa 12 jioni ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii.
10. Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika eneo, nyumba au jengo lolote kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa madhumuni ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Adhabu - 11 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa
AI-assisted research summary: Anyone convicted of an offence under these by-laws may be fined, jailed for up to 12 months, or both. The Director may also compound an offence if the accused admits it and pays up to TZS 200,000 using the prescribed form.
11.-(1) Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hii atahukumiwa adhabu ya kulipa faini tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili au vyote kwa pamoja. isiyozidi shilingi laki (2) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (1), Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa lolote endapo mtuhumiwa atakiri kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa kumtoza kiasi kisichozidi shilingi laki mbili baada ya kujaza fomu iliyoainishwa katika Jedwali. 6 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Tangazo la Serikali Na. 219 (Linaendelea.) ______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 11(2)) _______ HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi …………..….....................…………………………….nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele ya …………………………………….... ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Ikungi kuwa tarehe …..… ya Mwezi …...…. Mwaka …........… nilitenda kosa la kukiuka kifungu cha …… cha Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ya mwaka 2022. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri niko tayari kulipa kiasi cha shilingi .............................. na kutimiza wajibu wangu badala ya kushtakiwa Mahakamani. Nathibitisha kwamba maelezo hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu Leo Tarehe………………… Mwezi…………………Mwaka..................... Jina...................................................................................... Saini........................................................................................ Mbele ya: Jina: …………………………………………… Cheo: …………………………………………. Saini: ………………………………………….. 7 Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Tangazo la Serikali Na. 219 (Linaendelea.) Nembo na muhuri wa Halmashauri ya Wilaya ya IKUNGI umebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa Azimio lililopitishwa na mkutano wa Baraza la madiwani ulioitishwa Tarehe 22/1/2021 na ubandikwaji huo kushuhudiwa na:- JUSTICE L. KIJAZI, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya , Wilaya ya Ikungi ALLY J. MWANGA, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya IKUNGI L.S NAKUBALI, Dodoma, 9 Machi, 2022 UMMY A MWALIMU Waziri wa Nchi-OR-TAMISEMI 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA HIFADHI YA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI ZA MWAKA2022
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in