KANUNI ZA UTARATIBU WA KUHAMISHA NA KUSIMAMIA MASHAURI YALIYOPANGWA KWA HAKIMU MWENYE MAMLAKA YA NYONGEZA ZA MWAKA 2023
Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Utaratibu Kuhamisha na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa kwa Hakimu mwenye Mamlaka ya Nyongeza za Mwaka 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- KANUNI ZA UTARATIBU WA KUHAMISHA NA KUSIMAMIA MASHAURI YALIYOPANGWA KWA HAKIMU MWENYE MAMLAKA YA NYONGEZA ZA MWAKA 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Utaratibu Kuhamisha na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa kwa Hakimu mwenye Mamlaka ya Nyongeza za Mwaka 2023. These rules govern transferring cases from the High Court to a magistrate and managing those cases. Section 3 defines key terms used in these Rules, unless the context requires otherwise. A case transferred from the High Court to a magistrate must be transferred by a signed and dated transfer order from the Jaji Mfawidhi. Msajili must keep the registers under these regulations and keep the court seal for the magistrate’s court described in Schedule Two.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of KANUNI ZA UTARATIBU WA KUHAMISHA NA KUSIMAMIA MASHAURI YALIYOPANGWA KWA HAKIMU MWENYE MAMLAKA YA NYONGEZA ZA MWAKA 2023
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Utaratibu Kuhamisha na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa kwa Hakimu mwenye Mamlaka ya Nyongeza za Mwaka 2023.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Utaratibu Kuhamisha na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa kwa Hakimu mwenye Mamlaka ya Nyongeza za Mwaka 2023. - 2 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: These rules govern transferring cases from the High Court to a magistrate and managing those cases.
2. Kanuni hizi zitasimamia utaratibu wa kuhamisha mashauri kutoka Mahakama Kuu kwenda kwa hakimu na usimamizi wa mashauri hayo. - 3 Verify source ↗
Tafsiri
AI-assisted research summary: Section 3 defines key terms used in these Rules, unless the context requires otherwise.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Jaji Mfawidhi” ina maana sawa na iliyotolewa chini ya Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama, na inajumuisha Kaimu Jaji Mfawidhi; “hakimu” maana yake ni hakimu mkazi mwenye mamlaka ya nyongeza; na “Msajili” maana yake ni Msajili wa Mahakama Kuu, Naibu Msajili na Kaimu Naibu Msajili. 3 Kanuni Za Utaratibu wa Kuhamisha Na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa Kwa Hakimu Mwenye Mamlaka ya Nyongeza Tangazo la Serikali Na. 23 (Linaendelea.) SHEMU YA PILI USIMAMIZI WA MASHAURI Amri ya kuhamisha shauri - 4 Verify source ↗
Amri ya kuhamisha shauri
AI-assisted research summary: A case transferred from the High Court to a magistrate must be transferred by a signed and dated transfer order from the Jaji Mfawidhi.
4.-(1) Uhamishaji wa shauri lolote kutoka Mahakama Kuu kwenda kwa hakimu utakuwa kwa njia ya amri ya kuhamisha shauri itakayotolewa, kusainiwa na kuwekwa tarehe na Jaji Mfawidhi. (2) Amri ya kuhamisha shauri chini ya kanuni ndogo ya (1) itafanywa- (a) katika shauri la linalosikilizwa na jinai Mahakama Kuu katika mamlaka ya awali, baada ya kumkabidhi mshtakiwa Mahakama Kuu kwa usikilizwaji, na kabla ya kuchukuliwa kwa kiri; na (b) katika mashauri mengine, ya kumbukumbu kukamilika, na kabla Mahakama Kuu haijaanza kusikiliza shauri linalokusudiwa kuhamishwa. baada (3) Amri ya kuhamisha shauri chini ya kanuni hii itaainisha- (a) maelezo ya shauri linalokusudiwa kuhamishwa; (b) jina la hakimu ambaye shauri linahamishiwa kwake; na (c) jina la mahakama ya hakimu mkazi ambapo shauri lililohamishwa litasikilizwa. (4) Amri ya kuhamisha shauri chini ya kanuni hii itashabihiana kwa kadiri inavyowezekana na Fomu A iliyoanishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi. - 5 Verify source ↗
Rejesta na utunzaji
AI-assisted research summary: Msajili must keep the registers under these regulations and keep the court seal for the magistrate’s court described in Schedule Two.
5.-(1) Kutakuwa na rejesta kadhaa ambamo kutaingizwa maelezo ya mashauri yaliyohamishiwa kwa hakimu. (2) Rejesta chini ya kanuni hii zitatunzwa na Msajili. (3) Kutakuwa na muhuri wa mahakama inayoendeshwa na hakimu kama ulivyoanishwa katika Jedwali la Pili la Kanuni hizi ambao utatunzwa na msajili.
Part
Jedwali la Pili la Kanuni hizi ambao utatunzwa na msajili.
- 6 Verify source ↗
Majukumu ya Msajili
AI-assisted research summary: Msajili lazima ashughulikie mashauri yaliyohamishiwa kwa hakimu kama yangalikuwa Mahakama Kuu, na atekeleze majukumu maalum ya usimamizi wa mashauri na rejesta.
6.-(1) Msajili yote yanayohusiana na mashauri yaliyohamishiwa kwa hakimu atatekeleza majukumu 4 Rejesta na utunzaji Majukumu ya Msajili Kanuni Za Utaratibu wa Kuhamisha Na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa Kwa Hakimu Mwenye Mamlaka ya Nyongeza Tangazo la Serikali Na. 23 (Linaendelea.) kana kwamba mashauri hayo yapo Mahakama Kuu. (2) Bila kuathiri masharti ya jumla ya kanuni ndogo (1), Msajili atatekeleza majukumu yafuatayo: (a) kuandaa ratiba ya mashauri pale inapobidi; (b) kukadiria gharama za mashauri; (c) kutekeleza tuzo na amri; (d) kuandaa takwimu; (e) kuhuisha mashauri katika mfumo wa usimamizi wa mashauri na rejesta; (f) kuidhinisha nyaraka; na (g) kuwa mtunzaji wa mwisho wa kumbukumbu. Usajili baada ya amri ya kuhamisha - 7 Verify source ↗
Usajili baada ya amri ya kuhamisha
AI-assisted research summary: After a transfer order is issued, the Registrar must enter the transferred case information in the register and send the case to a magistrate.
7.-(1) Baada ya kutolewa kwa amri ya kuhamisha shauri, Msajili ataingiza taarifa za shauri lililohamishwa katika rejesta chini ya Kanuni hizi na kusababisha shauri kupelekwa kwa hakimu. (2) Bila kuathiri masharti ya jumla ya kanuni hii, taarifa zitakazoingizwa kwenye rejesta zitajumuisha- (a) namba ya shauri baada ya kuhamishwa; (b) maelezo ya wahusika; (c) namba ya shauri la Mahakama Kuu; (d) namba ya shauri asilia au la ukabidhi; (e) jina la hakimu aliyepangiwa; (f) tarehe ya amri ya kuhamishwa; na (g) uamuzi na tarehe yake. Uchukuaji wa kiri na usikilizwaji - 8 Verify source ↗
Uchukuaji wa kiri na usikilizwaji wa shauri
AI-assisted research summary: Hakimu aliyepangiwa shauri lazima achukue kiri mara baada ya shauri kuhamishwa, kisha asikilize shauri hadi mwisho kwa tarehe itakayopangwa na Msajili au tarehe nyingine baada ya hapo.
8.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi, hakimu ambaye amepangiwa shauri, atachukua kiri mara baada ya shauri kuhamishwa. (2) Baada ya kuchukua kiri chini ya kanuni ndogo ya (1), hakimu atasikiliza shauri hadi mwisho kwa tarehe itakayopangwa na Msajili au tarehe nyingine baada ya hapo. Rufaa na mambo mengine - 9 Verify source ↗
Rufaa na mambo mengine
AI-assisted research summary: Hakimu aliyepewa rufaa au shauri jingine lililohamishwa lazima alipange tarehe bila kuchelewa na asikilize shauri kwa mfululizo hadi limalizike, isipokuwa aiahirishe kwa sababu zilizoandikwa.
9.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi, hakimu ambaye amepangiwa shauri la rufaa au shauri lingine lolote, atasikiliza shauri mara baada ya shauri 5 Kanuni Za Utaratibu wa Kuhamisha Na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa Kwa Hakimu Mwenye Mamlaka ya Nyongeza Tangazo la Serikali Na. 23 (Linaendelea.) Kushindwa kumaliza shauri. Kuitisha shauri lilohamishwa Sehemu ya kusikilizia shauri kuhamishwa. (2) Baada ya kupokea amri ya kuhamisha shauri na kumbukumbu ya rufaa au shauri lingine lolote lililotajwa chini ya kanuni ndogo ya (1), hakimu atapanga tarehe bila kuchelewa, na kwa tarehe itakayopangwa, atasikiliza shauri kwa mfululizo hadi kumalizika au, kwa sababu zitakazoandikwa, ataliahirisha hadi tarehe nyingine.
Part
Sehemu ya
- 10 Verify source ↗
Kushindwa kumaliza shauri
AI-assisted research summary: If a judge cannot continue hearing a case, the Chief Resident Judge must reassign it to another judge by signed order. The receiving judge must record the reasons and notify the parties.
10.-(1) Endapo hakimu atashindwa kuendelea na usikilizwaji wa shauri asilia, rufaa au shauri lingine lolote, kwa sababu ya kifo, ugonjwa au sababu yoyote ya msingi, Jaji Mfawidhi, kwa amri atakayoweka saini, atapanga upya shauri kwa hakimu mwingine ili kuendelea na usikilizaji. (2) Hakimu anayepokea shauri chini ya kanuni hii, ataandika sababu za kupokea shauri na kuwajulisha wahusika wa shauri. (3) Amri ya kupangwa upya kwa shauri chini ya kanuni hii itashabihiana kwa kadiri inavyowezekana na Fomu B iliyoanishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi. - 11 Verify source ↗
Kuitisha shauri lililohamishwa
AI-assisted research summary: Jaji Mfawidhi anaweza, kwa sababu za kipekee zilizoandikwa, kuitisha shauri lililohamishiwa kwa hakimu chini ya masharti yaliyotajwa; katika hali hiyo, shauri litaendelea Mahakama Kuu.
11. Jaji Mfawidhi, kwa sababu za kipekee zitakazoandikwa, anaweza kuitisha shauri lililohamishiwa kwa hakimu- (a) iwapo ni shauri haijachukuliwa; na la jinai, kabla ya kiri (b) iwapo ni shauri linguine lolote, kabla ya kuanza kusikilizwa, na katika mazingira hayo, shauri litaendelea Mahakama Kuu. - 12 Verify source ↗
Sehemu ya kusikilizia shauri
AI-assisted research summary: Hakimu anapaswa kusikiliza shauri katika eneo ambako mahakama iliyotajwa kwenye amri ya kuhamisha shauri kawaida huketi, lakini kwa ridhaa ya Jaji Mfawidhi anaweza kusikiliza mahali pengine ndani ya eneo la mamlaka la mahakama hiyo na wahusika lazima wajulishwe.
12.-(1) Hakimu atasikilizia shauri katika eneo ambalo mahakama iliyotajwa katika amri ya kuhamisha shauri kwa kawaida huketi. (2) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), kwa ridhaa ya Jaji Mfawidhi, hakimu anaweza kusikilizia shauri mahali pengine popote ndani ya eneo la mamlaka ya mahakama iliyotajwa katika amri ya uhamishaji na wahusika watajulishwa sehemu hiyo ya kusikilizia shauri. 6 Kanuni Za Utaratibu wa Kuhamisha Na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa Kwa Hakimu Mwenye Mamlaka ya Nyongeza Tangazo la Serikali Na. 23 (Linaendelea.) SEHEMU YA TATU MAOMBI Mahali pa kufungua maombi
Part
SEHEMU YA TATU
- 13 Verify source ↗
Mahali pa kufungua maombi
AI-assisted research summary: Some applications must be filed in the High Court, the Principal Judge must issue a transfer order after registration, and certain cost-taxation and enforcement applications are heard by the Registrar.
13.-(1) Maombi yanayotokana na mashauri yaliyohamishiwa kwa hakimu, yanayofunguliwa kabla au baada ya shauri lililohamishwa kuamuliwa, yatafunguliwa katika Mahakama Kuu. (2) Baada ya kusajiliwa kwa maombi yaliyofunguliwa chini ya kanuni ndogo ya (1), Jaji Mfawidhi atatoa amri ya kuhamisha maombi inayoshabihiana kwa kadiri inavyowezekana na Fomu C iliyoanishwa katika Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi. (3) Bila kujali masharti ya Kanuni hizi na kwa kuzingatia masharti ya Sheria nyingine yoyote, maombi ya ukadiriaji gharama na utekelezaji wa maamuzi yanayotokana na utekelezaji wa mamlaka ya nyongeza yatasikilizwa na Msajili. (4) Kanuni hii haitamzuia hakimu kuamua na kutekeleza malipo ya gharama zilizoamriwa kulipwa wakati shauri linaendelea. Usikilizwaji wa maombi - 14 Verify source ↗
Usikilizwaji wa maombi
AI-assisted research summary: Applications arising from a case decided by a magistrate must be heard by that same magistrate or another magistrate assigned to hear them.
14. Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi au sheria nyingine yoyote, maombi yanayotokana na shauri lolote lililoamuliwa na hakimu yatasikilizwa na hakimu aliyeamua shauri husika au hakimu mwingine yeyote atakayepangiwa. SEHEMU YA NNE MASHARTI MENGINEYO Mahali pa kuwasilisha indhari ya rufaa Sura ya 141
Part
SEHEMU YA NNE
- 15 Verify source ↗
Mahali pa kuwasilisha indhari ya rufaa
AI-assisted research summary: Notice of appeal against a subordinate court decision is to be filed in the High Court, subject to the Appellate Authority Act or any other law.
15. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Mamlaka ya Rufaa au sheria nyingine yoyote, indhari ya rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya chini inayotekeleza mamlaka ya nyongeza, itawasilishwa Mahakama Kuu. Kutolewa kwa kumbukumbu ya rufaa, nakala ya mwenendo na uthibitisho wa ucheleweshwaji Sura ya 141 Gharama - 16 Verify source ↗
Kutolewa kwa kumbukumbu ya rufaa, nakala ya mwenendo na
AI-assisted research summary: Msajili lazima aandae, atoe na apeleke kumbukumbu ya rufaa, nakala ya mwenendo na uthibitisho wa ucheleweshwaji kwa masuala yanayotokana na uamuzi wa hakimu.
16. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Mamlaka ya Rufaa au sheria nyingine yoyote, msajili ataandaa, kutoa na kupeleka kumbukumbu ya rufaa, nakala ya mwenendo na uthibitisho wa ucheleweshwaji kwa masuala yanayotokana na uamuzi wa hakimu. - 17 Verify source ↗
Gharama
AI-assisted research summary: Mahakama Kuu itagharamia uendeshaji wa mashauri mbele ya hakimu, kwa kuzingatia masharti ya sheria yoyote.
17. Kwa kuzingatia masharti ya sheria yoyote, uendeshaji wa mashauri mbele ya hakimu utagharimiwa na Mahakama Kuu. 7 Kanuni Za Utaratibu wa Kuhamisha Na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa Kwa Hakimu Mwenye Mamlaka ya Nyongeza Tangazo la Serikali Na. 23 (Linaendelea.) FOMU A _______ JEDWALI LA KWANZA ______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(4), 10(3) na 3(2) (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 4(4)) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA INAYOKETI…………………… AMRI YA KUHAMISHA SHAURI Shauri la Kikao cha Jinai/Rufaa ya Jinai /Rufaa ya Madai/Rufaa ya Ardhi/Maombi ya Mapitio/ (au shauri jingine lolote) Na……la Mwaka 20.… (weka aina na namba ya shauri la Mahakama Kuu litakalohamishiwa kwa hakimu mkazi mwenye mamlaka ya nyongeza) Shauri asilia la ukabidhi/Shauri la Jinai/Shauri la Madai (au Shauri lolote la awali) Na…...la Mwaka
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 20 Verify source ↗
(ingiza aina na namba ya shauri la mahakama ya chini iliyopelekea shauri la Mahakama Kuu
AI-assisted research summary: This provision contains template forms for transferring a case, reassigning a case, and transferring an application to a resident magistrate with extended jurisdiction.
20.... (ingiza aina na namba ya shauri la mahakama ya chini iliyopelekea shauri la Mahakama Kuu linalohamishwa) ya Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya Hakimu Mkazi ya……..inayoketi………. (weka jina na mahali inapoketi mahakama ya chini iliyosikiliza shauri la Mahakama Kuu linalohamishwa) ………………………. JAMHURI/MRUFANI/MWOMBAJI DHIDI YA ……………………...MSHTAKIWA/MJIBU MAOMBI (weka maelezo ya wahusika katika shauri la Mahakama Kuu linalohamishwa) AMRI YA KUHAMISHA (chini ya kifungu cha…. cha…….) (weka kifungu cha Sheria kinachoruhusu kuhamisha shauri kwenda kwa hakimu mkazi mwenye mamlaka ya nyongeza) (au shauri Inaamriwa kuwa Shauri la Kikao cha Jinai/Rufaa ya Jinai/Rufaa ya Madai/Rufaa ya Ardhi/Maombi ya Mapitio baina ya………………na…………………. linalotokana na uamuzi wa …………. (weka jina la hakimu ambaye uamuzi wake unapingwa) katika…………… (weka maelezo ya shauri asilia) la………………. (weka maelezo ya mahakama asilia) linahamishwa kwenda kusikilizwa na kuamuliwa na ………………………., hakimu mkazi mwenye mamlaka ya nyongeza. lolote) Na………… la Mwaka 20…… lingine Inaamriwa pia kwamba usikilizwaji wa shauri tajwa utafanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya ……….………. ……………………….. Jaji Mfawidhi Tarehe……….mwezi………………mwaka 20.… 8 Kanuni Za Utaratibu wa Kuhamisha Na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa Kwa Hakimu Mwenye Mamlaka ya Nyongeza Tangazo la Serikali Na. 23 (Linaendelea.) (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 10(3)) FOMU B JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA INAYOKETI…………………… AMRI YA KUPANGWA UPYA KWA SHAURI Shauri la Kikao cha Jinai katika Mamlaka ya Nyongeza/Rufaa ya Jinai/Rufaa ya Madai/Rufaa ya Ardhi/Maombi ya mapitio (au shauri lingine lolote) Na……la Mwaka 20.……... (weka namba ya shauri la mamlaka ya nyongeza) Shauri asilia la ukabidhi/Shauri la Jinai/Shauri la Madai (au shauri lingine lolote asilia) Na…… la mwaka 20.... (weka aina na namba ya shauri la mahakama ya chini iliyopelekea shauri la Mahakama Kuu linalohamishwa) la Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya Hakimu Mkazi ya……..inayoketi………. (weka jina na mahali inapoketi mahakama ya chini iliyosikiliza shauri la Mahakama Kuu linalohamishwa). ………………………. JAMHURI/MRUFANI/MWOMBAJI DHIDI YA ……………………...MSHTAKIWA/MJIBU MAOMBI (weka maelezo ya wahusika wa shauri linalopangwa upya) AMRI YA KUPANGWA UPYA KWA SHAURI (Chini ya kifungu cha……. cha…….) (weka kifungu cha Sheria kinachoruhusu kupangwa upya kwa shauri kwa hakimu mkazi mwenye mamlaka ya nyongeza) Inaamriwa kuwa Shauri la Kikao cha Jinai la Mamlaka ya Nyongeza/Rufaa ya Jinai/Rufaa ya Madai/Rufaa ya Ardhi/Maombi ya Mapitio/ (au shauri lingine lolote) Na…… la mwaka 20…… baina ya…………………na……….…….hapo awali mbele ya……………………...(weka jina la hakimu wa awali ambaye hakuweza kumaliza usikilizwaji) limepangwa upya kwa ajili ya kusikilizwa na ………………………., hakimu mkazi mwenye mamlaka ya nyongeza. Inaamriwa pia kwamba usikilizwaji wa shauri tajwa utafanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya ……….………. ……………………….. Jaji Mfawidhi Tarehe……….mwezi………………mwaka 20.…. 9 Kanuni Za Utaratibu wa Kuhamisha Na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa Kwa Hakimu Mwenye Mamlaka ya Nyongeza Tangazo la Serikali Na. 23 (Linaendelea.) FOMU C (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 13(2)) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA INAYOKETI…………………… AMRI YA KUHAMISHA SHAURI LA MAOMBI Maombi ya Jinai/Madai Na……la Mwaka 20.… (weka namba ya shauri la maombi la Mahakama Kuu litakalohamishiwa kwa hakimu mkazi mwenye mamlaka ya nyongeza) Yanayotokana na Shauri la Kikao cha Jinai/Rufaa ya Jinai/Rufaa ya Madai/Rufaa ya Ardhi (au Shauri lolote linalohamishika) Na…...la Mwaka 20.... (weka aina na namba ya shauri la mahakama ya chini iliyopelekea shauri la Mahakama Kuu linalohamishwa) ya Mahakama Kuu/Mahakama ya Hakimu Mkazi ya……..inayoketi……….(weka jina na mahali inapoketi mahakama ya chini iliyosikiliza shauri la Mahakama Kuu linalohamishwa). ………………………. MWOMBAJI DHIDI YA ……………………...MJIBU MAOMBI (weka maelezo ya wahusika katika maombi litakalohamishwa) AMRI YA KUHAMISHA (Chini ya kanuni ya 13(2) ya Kanuni za Utaratibu Kuhamisha na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa kwa Hakimu mwenye Mamlaka ya Nyongeza za Mwaka 2022.) ya Jinai/Madai kuwa Maombi Inaamriwa - 20 Verify source ↗
…baina
AI-assisted research summary: This provision is a transfer form for moving a case to be heard by a resident magistrate with additional jurisdiction.
20.…baina ya………………na…………………. Yanayotokana na Shauri la Kikao cha Jinai/Rufaa ya Jinai/Rufaa ya Madai/Rufaa ya Ardhi (au Shauri lolote linalohamishika) Na…...la Mwaka 20.... (weka aina na namba ya shauri la mahakama ya chini iliyopelekea shauri la Mahakama Kuu Mkazi linalohamishwa) ya................……..inayoketi……….......(weka jina na mahali inapoketi mahakama ya chini iliyosikiliza shauri la Mahakama Kuu linalohamishwa) linahamishwa kwenda kusikilizwa na ………………………., hakimu mkazi mwenye mamlaka ya nyongeza. Na……la Mwaka Kuu/Mahakama Mahakama Hakimu ya ya Inaamriwa pia kwamba usikilizwaji wa shauri tajwa utafanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya ……….………. ……………………….. Jaji Mfawidhi Tarehe……….mwezi………………mwaka 20.…. 10 Kanuni Za Utaratibu wa Kuhamisha Na Kusimamia Mashauri Yaliyopangwa Kwa Hakimu Mwenye Mamlaka ya Nyongeza Tangazo la Serikali Na. 23 (Linaendelea.) _________ JEDWALI LA PILI __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(3)) MUHURI WA MAHAKAMA Dar es Salaam, 9 Januari, 2023 IBRAHIM HAMIS JUMA, Jaji Mkuu 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
KANUNI ZA UTARATIBU WA KUHAMISHA NA KUSIMAMIA MASHAURI YALIYOPANGWA KWA HAKIMU MWENYE MAMLAKA YA NYONGEZA ZA MWAKA 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in