AI-assisted research summary: Mpango wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unatakiwa kuandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
3. Mpango wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. 1 Amri ya Mpango wa Urasimishaji wa Eneo la Ikola Na Mchangani Tangazo La Serikali Na. 678 (Linaendelea.) ________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la Upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Unaanzia katika alama ya mpaka ya upimaji namba RV3 yenye majira - nukta 212088.70E, 9254581.87N kwenye makutano ya mto Kafisha na Ziwa Tanganyika; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini- Magharibi kwa kufuata mto Kafisha hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P1 yenye majira - nukta 212672.58E, 9255232.34N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Mashariki kwa kufuata barabara ya Isengule - Ikola kwa umbali wa kilomita 0.672 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P2 yenye majira - nukta 213238.42E, 9254897.46N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Mashariki kwa kufuata barabara ya Ikola – Mpanda kupitia njia ya Kaburiwazi umbali wa kilomita 0.490 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P3 yenye majira - nukta 213666.40E, 9255043.86N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Mashariki katika uelekeo wa S17°18'43''E kwa umbali wa kilomita 1.43 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P4 yenye majira - nukta 214480.43E, 9253715.60N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Magharibi katika uelekeo wa S74°28'37'' kwa umbali wa kilomita 0.349 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P5 yenye majira - nukta 214153.76E, 9253624.86N (iliyopo katika barabara ya Ikola – Karema); baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Mashariki kufuata barabara ya Ikola – Karema kwa umbali wa kilomita 0.736 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P6 yenye majira - nukta 214355.80E, 9252947.68N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Magharibi katika uelekeo wa S87°36'52''W kwa umbali wa kilomita 1.01 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba P7 yenye majira - nukta 213338.78E, 9252905.31N (iliyopo katika mwambao wa Ziwa Tanganyika); baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi kufuata mwambao wa Ziwa Tanganyika hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba RV2 yenye majira - nukta 213135.09E, 9253693.81N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi kwa kufuata mwambao wa Ziwa Tanganyika hadi ulipoanzia. Dodoma, 8 Novemba, 2022 ANGELINE S. MABULA, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2