AI-assisted research summary: A general and detailed plan for the area in the Schedule must be prepared and kept by the Director of Urban Planning and the Executive Director of Nsimbo District Council.
3. Mpango wa jumla na wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo. ________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la Upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji P1 yenye majira ya nukta 297771.957E, 9270000.000N inayopatikana Mto Kabenga; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Magharibi katika uelekeo wa S 64o 33’ 43” W hadi alama ya mpaka ya upimaji P2 yenye majira ya nukta 294615.234E, 9268612.948N kwa umbali wa kilomita 0.527; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Mashariki katika uelekeo wa S 15o 56’ 14” E hadi alama ya mpaka ya upimaji P3 yenye majira ya nukta 294689.714E, 9268352.127N kwa umbali wa kilomita 0.271; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Magharibi katika uelekeo wa S76o 15’ 22” W hadi alama ya mpaka ya upimaji P4 yenye majira ya nukta 294340.297E, 9268266.666N kwa umbali wa kilomita 0.359; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi katika uelekeo wa N 15o 37’ 17” W hadi alama ya mpaka ya upimaji P5 yenye majira ya nukta 294313.288E, 9268363.261N kwa umbali wa Tangazo la Serikali na 693 (linaendelea) Amri ya Kupanga Eneo la Sitalike kilomita 0.100; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Magharibi katika uelekeo wa S 65o 17’ 29” W ukikatiza Barabara ya Mpanda/Sumbawanga hadi alama ya mpaka ya upimaji P6 kwa umbali wa kilomita 2.287; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Mashariki ukikatiza Mto Katuma katika uelekeo wa S 72o 07’ 22” E hadi alama ya mpaka ya upimaji P7 inayopatikana Darajani yenye majira ya nukta 294715.00E, 9266731.000N kwa umbali wa kilomita 2.655; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini sambamba na Mpaka wa Mbuga ya Taifa ya Katavi katika uelekeo wa S 04o 47’ 31” W hadi alama ya mpaka ya upimaji WK 60 yenye majira ya nukta 294182.000E, 9260373.000N kwa umbali wa kilomita 6.380; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki sambamba na Mpaka wa Mbuga ya Taifa ya Katavi katika uelekeo wa N 88o 30’ 01” E hadi alama ya mpaka ya upimaji WK 45 katika Barabara ya Mpanda – Mpimbwe yenye majira ya nukta 308277.000E, 9260742.000N kwa umbali wa kilomita 14.099; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi katika uelekeo wa N 19o 56’ 05” W hadi alama ya mpaka ya upimaji WK 301 yenye majira ya nukta 307070.000E, 9264070.000N kwa umbali wa kilomita 3.540 sambamba na Barabara ya Mpanda – Mpimbwe na Msitu wa Hifadhi Msaginia; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi katika uelekeo wa N 74o 41’ 50” W hadi alama ya mpaka ya upimaji WL 655 yenye majira ya nukta 298423.000E, 9266436.000N kwa umbali wa kilomita 8.964 sambamba na Msitu wa Hifadhi Msaginia; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi katika uelekeo wa N 10o 21’ 08” W hadi alama ya mpaka ya upimaji P1 yenye majira ya nukta 297771.957E, 9270000.000N kwa umbali kilomita 3.621, ulipoanzia”. ANGELINE S. MABULA Dodoma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na 8 Novemba, 2022 Maendeleo ya Makazi 2