AI-assisted research summary: The general and detailed plan for the area in the Table must be prepared and kept by the Director of Urban Planning and the Executive Director of Uyui District Council.
3. Mpango wa jumla na wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui. ________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la Upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji M1 iliyopo katika makutano ya barabara ya Mbiti na Mto Mabama yenye majira - nukta 48985E, 9437256N; baada ya hapo mpaka utaelekea Magharibi katika uelekeo wa 11207’28”W kwa umbali wa kilomita 1.8 hadi alama ya mpaka ya upimaji M2 iliyopo barabara ya Maswanywa yenye majira-nukta 447129E, 9437267N; baada ya hapo mpaka utaendelea kuelekea Magharibi hadi katika alama ya mpaka ya upimaji M3 iliyopo barabara ya Maswanywa kwenye majira - nukta 444186E, 9436951N; baada ya hapo mpaka utafuata barabara ya Maswanywa - Magharibi kuelekea Kusini katika uelekeo wa 9206’8”S kwa umbali wa kilomita 1.7 hadi katika alama ya mpaka M4 iliyopo barabara kuu ya Kigoma katika majira-nukta 444355E,9435276N; baada ya hapo mpaka utaelekea kufuata barabara ya Mwigerezi na kukatiza reli katika alama ya mpaka ya upimaji M5 yenye majira - nukta 445272E, 1 Tanagzo la serekali na. 703 (linaendelea) Amri ya Kupanga Eneo la Mabama 9434028N na kwenda kukutana na barabara ya Uturu kwenye alama ya upimaji M6 yenye majira - nukta 445331E, 9433233N; baada ya hapo mpaka utaelekea Kusini - Mashariki katika uelekeo wa S8502’50”E kwa umbali wa kilomita 1.06 hadi katika alama ya mpaka ya upimaji M7 iliyopo barabara ya Idete yenye majira - nukta 446425E, 9432794N; baada ya hapo mpaka utafuata uelekeo wa Kusini - Mashariki hadi Mto mabama kwenye alama ya mpaka ya upimaji M8 yenye majira - nukta 450307E, 9431956N; baada ya hapo mpaka utafuata mto Mabama kuelekea Kaskazini na kukatiza reli ya Kigoma katika alama ya mpaka ya upimaji M9 yenye majira - nukta 450424E, 9433845N; baada ya hapo mpaka utaendelea kufuata mto mabama na kukatiza barabara kuu ya Kigoma katika alama ya mpaka ya upimaji M10 yenye majira - nukta 450019E, 9435729N kwenda hadi ulipoanzia” ANGELINE S. MABULA Dodoma, 8 Novemba, 2022 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2