AI-assisted research summary: The general and detailed plan for the area in the Schedule must be prepared and kept by the Director of Town Planning and the Executive Director of Uyui District Council.
3. Mpango wa jumla na wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui. _________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la Upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji T1 iliyopo katika makutano ya barabara kuu ya Itigi na Singida yenye majira-nukta 596338E, 9392855N; baada ya hapo mpaka utafuata barabara ya Singida hadi alama ya mpaka ya upimaji T2 iliyopo karibu na msitu wa jamii wa Tura yenye majira-nukta 599361E, 9396505N; baada ya hapo mpaka utaelekea Magharibi - Kaskazini katika uelekeo wa W9106’4” kwa umbali wa kilomita 10.1 hadi alama ya mpaka ya upimaji T3 iliyopo katika makutano ya barabara kuu ya Itigi na Mto Tura kwa upande wa Kaskazini yenye majira - nukta 589265E, 9398195N; baada ya hapo mpaka utafuata mto Tura na kukatiza reli ya Itigi katika alama ya mpaka ya upimaji T4 yenye majira-nukta 582487E, 9395353N hadi alama ya mpaka ya upimaji T5 iliyopo katika njia panda ya matawi ya Mto yenye majira-nukta 579746E, 9393554N; baada ya hapo mpaka utafuata tawi la Kusini la mto Tura hadi alama T6 yenye majira-nukta 583565E, 9390520N; baada ya hapo mpaka utaelekea Mashariki-Kusini katika uelekeo wa 1 Tangazo la Serikali na. 704 (linaendelea) Amri ya Kupanga Eneo la Tura E165011’0” kwa umbali wa kilomita 9.6 hadi alama ya mpaka ya upimaji T7 iliyopo pembeni mwa bwawa la Tura yenye majira - nukta 592698E, 9388398N; baada ya hapo mpaka utaelekea Mashariki - Kaskazini katika uelekeo wa E14709’48”N kwa umbali wa kilomita 4.6 hadi alama ya mpaka ya upimaji T8 iliyopo barabara kuu ya Itigi yenye majira-nukta 597127E, 9391416N; baada ya hapo mpaka utafuata barabara Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa N9006’0”W kwa umbali wa kilomita 1.4 hadi ulipoanzia”. Dodoma, 8 Novemba, 2022 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ANGELINE S. MABULA 2