AI-assisted research summary: Mpango wa jumla na wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.
3. Mpango wa jumla na wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui. 1 Tangazo la Serikali na. 705 (linaendelea) Amri ya Kupanga Eneo la Kigwa ________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la Upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Unaanzia katika alama ya mpaka K1 iliyopo katika makutano ya barabara kuu ya Tabora - Itigi na Magiri yenye majira - nukta 511661E, 9435296N;baada ya hapo mpaka utafuata uelekeo wa Kaskazini kupitia barabara ya Magiri ya juu katika uelekeo wa N170011’20” kwa umbali wa kilomita 1.5 hadi alama ya mpaka K2 iliyopo katika makazi ya Magiri ya juu kwenye majira-nukta 511785E, 9436805N; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki katika uelekeo wa E174011’36” kwa umbali wa kilomita 4.4 kupitia barabara ya Kigwarubhuga hadi alama ya mpaka K4 iliyopo bonde la Mpunga lililopo Mashariki mwa makazi ya Kigwa katika majira-nukta 516156E, 9437040N kwa kukatiza alama ya mpaka K3 iliyopo katika makutano ya barabara ya Isikizya na Kigwarubhuga yenye majira - nukta 514607E, 9436825N; baada ya hapo mpaka utafuata uelekeo wa bonde kuelekea Kusini pembezoni mwa msitu wa Kigwarubhaga katika uelekeo wa S6504’20” kwa umbali wa kilomita 2.5 hadi alama ya mpaka K5 iliyopo barabara kuu ya Tabora - Itigi yenye majira - nukta 516721E, 9434629N na kuendeleo katika uelekeo wa Kusini sambamba na bonde mpaka kaatika alama ya mpaka K6 iliyopo barabara ya Goweko kwenye majira - nukta 516118E, 9432204N; baada ya hapo mpaka utaelekea Magharibi katika uelekeo wa W165011’0” kwa umbali wa kilomita 3.3 hadi alama ya mpaka K7 iliyopo barabara ya Igalula katika majira-nukta 512792E, 9431814N; baada ya hapo mpaka utaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa N9706’28” kwa umbali wa kilomita 3.5 hadi ulipoanzia” ANGELINE S. MABULA Dodoma, 8 Novemba., 2022 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2