AI-assisted research summary: Mpango wa jumla na wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unatakiwa kuandaliwa na kuhifadhiwa na Mkurugenzi wa Mipangomiji pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
3. Mpango wa jumla na wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge. ________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la Upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Unaanzia kwenye alama ya mpaka I1 iliyopo katika bonde la Mpunga kupita barabara ya Mbeya kwenye majira-nukta 470592E, 9357661N; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi-Kaskazini sambamba na bonde katika uelekeo wa W8005’20”N kwa umbali wa kilomita 1.3 hadi alama ya mpaka I2 iliyopo barabara ya Mpanda katika majira-nukta 469268E, 9358567N; baada ya hapo mpaka utaelekea Kaskazini-Magharibi katika uelekeo wa N10507’0”W kwa umbali wa kilomita 0.4 hadi alama ya mpaka I3 iliyopo barabara ya zamani ya Mpanda katika majira-nukta 469220E 9359010N; baada ya hapo mpaka unanyooka kwa umbali wa kilomita 2.9 hadi katika alama ya mpaka I4 iliyopo barabara ya Mihamakumi katika majira-nukta 468676E, 9361894N; baada ya hapo mpaka 1 Tagazo la seriakli na. 716 (linaendelea) Amri ya Kupanga Eneo la Ipole unanyooka kwa umbali wa kilomita 1.06 hadi katika alama ya mpaka I5 iliyopo barabara ya Makazi na Kaskazini-Magharibi mwa eneo la Makazi yenye majira-nukta 468400E, 9362947N; baada ya hapo mpaka utaelekea Mashariki-Kaskazini katika uelekeo wa E9506’20” kwa umbali wa kilomita 3.1 hadi katika alama ya mpaka I6 iliyopo barabara ya Tabora-Mpanda katika majira-nukta 471529E, 9364387N; baada ya hapo mpaka utaelekea Kusini-Mashariki katika uelekeo wa S9006’0” kwa umbali wa kilomita 3.5 hadi alama ya mpaka I7 iliyopo barabara ya Kabanga katika majira-nukta 473152E, 9360918N; baada ya hapo mpaka utaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa S9506’20” kwa umbali wa kilomita 1.6 hadi katika alama ya mpaka I8 iliyopo barabara ya zamani ya Kabanga yenye majira-nuta 471697E, 9359341N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini-Magharibi kwa umbali wa kilomita 1.7 hadi ulipoanzia”. Dodoma, ANGELINE S. MABULA 8 Novemba, 2022 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2