Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021
This section gives the names and meanings of key terms used in the bylaw on service levy in Igunga District Council.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the names and meanings of key terms used in the bylaw on service levy in Igunga District Council. Halmashauri must levy and collect a 0.3% service levy from taxpayers on gross income from business activities within the council area, with non-commercial institutions excluded. A taxpayer who operates within a council area must pay service tax to the council at the start of each calendar year. Mlipa ushuru lazima awasilishe hesabu za mapato kwa halmashauri ndani ya siku 21 baada ya kipindi cha hesabu kuisha, na alipe ushuru wa huduma ndani ya siku 7 baada ya ushuru kukokotolewa. Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri kwa kazi za ushuru, ikiwemo kukusanya ushuru, kufanya tathmini, na kukagua vitabu, kulingana na masharti ya Sheria Ndogo hii.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021
Showing 11 of 11
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This section gives the names and meanings of key terms used in the bylaw on service levy in Igunga District Council.
2. Sura ya 208 Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo:- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Igunga; “Hesabu” maana yake ni taarifa ya maandishi na au vielelezo vinavyoonesha taarifa za mapato ya mlipa ushuru, kwa lengo la kukokotoa ushuru wa huduma; “Kipindi cha hesabu” maana yake ni kati ya miezi kumi na mbili ya kalenda ya mwaka ambacho mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu zake; “Mamlaka ya Mapato” Maana yake ni Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA; wa “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Igunga pamoja na Afisa yeyote atakayetueuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Mlipa Ushuru” maana yake ni kampuni au taasisi ya kibiashara, inayowajibika kulipa ushuru wa huduma chini ya Sheria Ndogo hii na itahusisha Mkurugenzi, Meneja au Afisa msimamizi wa taasisi ya kibiashara ambaye anapaswa kulipa ushuru wa huduma kwa niaba 1 Sheria Ndogo ya Ushuru Wa Huduma Za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 284 (Linaendelea.) ya taasisi husika; na itahusisha mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara au anayepaswa kuwa na leseni ya biashara kwa mujibu wa Sheria ya Leseni za Biashara; “Mwaka wa hesabu” maana yake ni kipindi miezi kumi na mbili ya kalenda ya mwaka; “Mfanyabiashara” maana yake ni mtu yeyote mwenye leseni ya biashara au anayepaswa kuwa na leseni ya biashara; “Taasisi isiyo ya kibiashara” maana yake ni taasisi isiyo ya kiserikali au mtu ambaye anafanya shughuli za kujitolea kusaidia jamii katika maeneo ya elimu, afya, maji, miundombinu, kuondoa au kupunduza umaskini, kutoa huduma za kidini, au kusaidia watu walioathirika na majanga, bila malipo, au ambaye ana ushahidi wa maandishi kuhusu uamuzi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, kutambua taasisi hiyo au mtu huyo kama taasisi isiyo ya kibiashara au taasisi ya kusaidia; “Taasisi ya kibiashara” maana yake ni Kampuni, taasisi, tawi la kampuni au taasisi au asasi isiyo ya kiserikali, iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni au Sheria ya majina ya kibiashara au ushirika, inayojishughulisha na shughuli za utafiti wa kibiashara, uzalishaji, usambazaji au uuzaji wa bidhaa, mazao au huduma. “ushuru” maana yake ni ushuru wa huduma; “ushuru wa huduma” maana yake ni malipo yanayotolewa kwa Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mtu mwenye leseni ya biashara iliyotolewa chini ya sharia yoyote kwa huduma za umma anazotumia kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni iliyoteuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kukusanya ushuru wa huduma. Utozaji wa Ushuru wa Huduma - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Halmashauri must levy and collect a 0.3% service levy from taxpayers on gross income from business activities within the council area, with non-commercial institutions excluded.
3.- (1) Halmashauri itatoza na kukusanya Ushuru wa Huduma kutoka kwa mlipa ushuru kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu (0.3%) ya mapato 2 Sheria Ndogo ya Ushuru Wa Huduma Za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 284 (Linaendelea.) ghafi ya mlipa ushuru, baada ya kutoa kodi ya ongezeko la thamani na kodi ya mlaji kutokana na shughuli za kibiashara, ziwe za uzalishaji au usambazaji au uuzaji wa bidhaa au mazao au huduma ndani ya eneo la Halmashauri. (2) Kifungu kidogo cha 1 hakitazihusu taasisi zisizo za kibiashara. Wajibu wa kulipa Ushuru - 4 Verify source ↗
Utakuwa ni wajibu wa mlipa ushuru anayefanya
AI-assisted research summary: A taxpayer who operates within a council area must pay service tax to the council at the start of each calendar year.
4. Utakuwa ni wajibu wa mlipa ushuru anayefanya shughuli zake ndani ya eneo la halmashauri, kulipa ushuru wa huduma kwa halmashauri kila mwanzo wa mwaka wa kalenda. - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru lazima awasilishe hesabu za mapato kwa halmashauri ndani ya siku 21 baada ya kipindi cha hesabu kuisha, na alipe ushuru wa huduma ndani ya siku 7 baada ya ushuru kukokotolewa.
5.- Taratibu za kulipa Ushuru wa Huduma (1) Kila mlipa ushuru, atawasilisha hesabu za mapato yake kwa halmashauri ndani ya siku ishirini na moja tangu kuisha kwa kipindi cha hesabu. (2) Mlipa ushuru atapaswa kulipa ushuru wa huduma ndani ya siku saba tangu tarehe ya kukokotolewa kwa ushuru kutokana hesabu sahihi za mapato yake aliyowasilisha. (3) Mlipa Ushuru ambaye atashindwa kuwasilisha hesabu za mapato yake kwa wakati au ambaye kwa maoni ya Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa hesabu zitakazokuwa zimewailishwa na mlipa ushuru zitaonekana kuwa na mapungufu kiasi cha kuathiri ukokotoaji wa ushuru sahihi, atapaswa kulipa ushuru wa huduma kwa viwango vilivyotajwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii pamoja na asilima kumi ya ushuru. (4) Mkurugenzi anaweza kumtaka kwa maandishi mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu mlipa ushuru yeyote anayepaswa kulipa ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumiwa kusaidia kulipwa kwa ushuru. Uwezo wa Afisa Mwidhiniwa - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri kwa kazi za ushuru, ikiwemo kukusanya ushuru, kufanya tathmini, na kukagua vitabu, kulingana na masharti ya Sheria Ndogo hii.
6. Bila kuathiri masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii, Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri kwa nia ya kukusanya ushuru, kufanya tathmini, kufanya ukaguzi wa vitabu au kufanya jambo lolote linalohusu ushuru kwa 3 Sheria Ndogo ya Ushuru Wa Huduma Za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 284 (Linaendelea.) mujibu wa Sheria Ndogo hii. Wakala - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua Wakala kwa mujibu wa Sheria kukusanya ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii.
7. Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua Wakala kwa mujibu wa Sheria kukusanya ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Makosa - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru yeyote anatenda kosa akishindwa kutimiza wajibu wa taarifa, vitabu, malipo, au akitoa taarifa au nyaraka za uongo, au akizuia kazi za Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa, au wakala.
8. Itakuwa ni kosa kwa Mlipa ushuru yeyote: – a) kushindwa kuwasilisha hesabu sahihi za mapato yake; b) kushindwa kulipa ushuru kwa wakati; c) kushindwa kuwasilishwa nyaraka, maelezo au taarifa kwa Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa katika muda uliowekwa; kuwasilishwa inayotakiwa d) kushindwa kutunza kumbukumbu yoyote au nyaraka anazopaswa kutunza kuhusu ushuru; e) kufanya hesabu za uongo kwa kupunguza mapato yake au ushuru isivyo halali; f) kutoa taarifa za uongo kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri wajibu wake au wajibu wa mtu mwingine kuhusu ulipaji wa ushuru; g) kuandaa au kusababisha kuandaliwa au kutengenezwa kwa hesabu au kumbukumbu za uongo ambazo zinaweza kuathiri ukokotoaji wa ushuru; h) kumzuia au kujaribu kumzuia Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hii; i) kuharibu kwa makusudi au kwa uzembe taarifa au mfumo wa taarifa za hesabu; j) kuharibu kwa makusudi au kwa uzembe vitendea kazi vya kukusanyia ushuru; k) kukataa kupokea au kusaini uthibitisho wa kupokea hati, taarifa au notisi chini ya Sheria Ndogo hii, iliyoelekezwa kwake au mtu mwingine ambaye anafanya kazi ofisini mwake au anaishi nyumbani mwake; l) kutenda jambo lolote kinyume na Sheria Ndogo hii. 4 Sheria Ndogo ya Ushuru Wa Huduma Za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 284 (Linaendelea.) Adhabu Kufifilisha kosa - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevunja masharti ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: Anyone who breaches this by-law commits an offence and, if convicted, may have to pay owed tax, a fine up to 300,000 shillings, imprisonment up to 12 months, or both.
9. Mtu yeyote atakayevunja masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa ushuru anaodaiwa na faini isiyozidi shilingi laki tatu au atatumikia kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 10 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mhusika shilingi laki mbili, ikiwa anakiri kosa, yuko tayari kujaza fomu maalum, na kulipa ushuru anaodaiwa.
10. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ushuru anaodaiwa. JEDWALI LA KWANZA (Limeundwa chini ya Kifungu cha 5(3)) VIWANGO VYA USHURU WA HUDUMA KWA ASIYEWASILISHA TAARIFA YA MAPATO NA. Ada ya Leseni ya Biashara(TSh.) Ushuru wa Huduma kwa Mwaka (TSh) 1 2
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: This section lists value ranges and corresponding amounts in a fee or rate table.
12. 5,000 – 7,999 8,000 – 9,999 10,000 – 19,999 20,000 – 29,999 30,000 – 39,999 40,000 – 49,999 50,000 – 59,999 60,000 – 69,999 70,000 – 79,999 80,000 – 89,999 90,000 – 99,999 100,000 -119,999 5 20,000.00 30,000.00 40,000.00 50,000.00 60,000.00 80,000.00 200,000.00 250,000.00 300,000.00 350,000.00 400,000.00 500,000.00 Sheria Ndogo ya Ushuru Wa Huduma Za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 284 (Linaendelea.) 600,000.00 650,000.00 700,000.00 750,000.00 800,000.00 850,000.00 1,700,000.00 950,000.00 1,100,000.00 1,200,000.00 1,300,000.00 1,400,000.00 1,500,000.00 1,600,000.00 1,700,000.00 1,800,000.00 1,900,000.00 2,000,000.00 2,200,000.00 2,400,000.00 2,600,000.00 - 33 Verify source ↗
Section 33
AI-assisted research summary: This text provides a form for admitting an offence and agreeing to pay the service levy owed plus a fine.
33. 120,000 – 139,999 140,000 – 159,999 160,000 – 189,999 190,000 – 219,999 220,000 – 239,999 240,000 – 269,999 270,000 – 300,000 300,001 – 350,000 350,001 – 400,000 400,001 – 450,000 450,001 – 500,000 500,001 – 550,000 550,001 – 600,000 600,001 – 650,000 650,001 – 700,000 700,001 – 750,000 750,001 – 800,000 800,001 – 850,000 850,001 – 900,000 900,001 – 950,000 950,001 - 1,000,000 6 Sheria Ndogo ya Ushuru Wa Huduma Za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 284 (Linaendelea.) JEDWALI LA PILI (Limetungwa chini ya kifungu cha 10) KUFILILISHA KOSA Mimi…………………………………………..………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, kwamba mnamo tarehe ………mwezi………. Mwaka………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha………………. cha Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Niko tayari kulipa kiasi cha Ushuru wa Huduma ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI KWELI NA NINAYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe………………………………. ya Mwezi…………………. Mwaka………………… Jina…………………………………………Saini……………………………………… Mbele ya: Jina………………………………………...Cheo……………………………………. Saini………………………………………Tarehe…………………………………… 7 Sheria Ndogo ya Ushuru Wa Huduma Za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 284 (Linaendelea.) Nembo na Muhuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga vimebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 30/4/2020 na ubandikaji huo kushuhudiwa na:- REVOCATUS L. K. KUULI, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Igunga PETER ONESMO MALODA, Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya, Igunga L.S NAKUBALI, Dodoma, SELEMANI SAID JAFO (MB.), 22 Februari, 2021 Waziri wa Nchi -OR- Tamisemi 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in