Sheria Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021
This bylaw is titled the Igunga District Council bylaw on the management and operation of markets and magulio for 2021.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This bylaw is titled the Igunga District Council bylaw on the management and operation of markets and magulio for 2021. Kifungu hiki kinafafanua maneno na taasisi mbalimbali zinazotumiwa katika Sheria Ndogo hii. Halmashauri inaweza kuanzisha na kusimamia masoko na magulio katika eneo lake, na mtu binafsi hapaswi kuanzisha au kuendesha soko au gulio binafsi bila kibali maalum cha maandishi cha Halmashauri ikiwa kibali hicho kinahitajika. Halmashauri ina wajibu wa kutambua, kuanzisha, kuendeleza na kusimamia masoko au magulio, pamoja na kusajili wadau na kukusanya ushuru na ada. Mazao, nguo na bidhaa nyinginezo zinaweza kufanyika kwenye masoko tu kwa idhini ya maandishi ya Halmashauri, baada ya mwombaji kuwasilisha maombi kwa Mkurugenzi.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021
Showing 37 of 37
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This bylaw is titled the Igunga District Council bylaw on the management and operation of markets and magulio for 2021.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021. - 2 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama imeelezwa
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinafafanua maneno na taasisi mbalimbali zinazotumiwa katika Sheria Ndogo hii.
2. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo:- “ada” itakuwa na tafsiri iliyotolewa katika Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga; “Afisa Mwidhiniwa” Maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Dalali” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni au gulioni kwa niaba ya mwenye bidhaa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za soko au gulio; “Halmashauri” Maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Igunga; “Gulio” maana yake ni soko la wazi linalofanyika kwa wakati na siku maalum kwa kibali maalum cha Halmashauri na litajumuisha mnada; “Kamati ya wadau wa Soko” Maana yake ni kamati ya wafanyabiashara iliyoundwa chini ya kifungu cha 15 cha Sheria Ndogo hii; “Kikundi”Maana yake ni kikundi cha ushirika au umoja wa wafanyabiashara uliuosajiliwa na Meneja wa 1 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) soko kwa kuandikishwa katika daftari maalum la wafanyabiashara wa soko; “Kizimba” Maana yake ni meza au nafasi ya kufanyia na kuidhinishwa iliyojengwa biashara Halmashauri katika soko au gulio; au “Makasha” Maana yake ni vifaa maalum vya kubebea, kufungashia au kuhifadhia bidhaa au mazao na yatajumuisha matenga, viroba, magunia, karatasi ngumu, maboksi, masanduku ya mbao na mengine vyenye asili hiyo; “Mfanyabiashara wa sokoni” Maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa au huduma sokoni kwa jumla au rejareja baada ya kusajiliwa katika daftari rasmi la soko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “Meneja wa soko” maana yake ni afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa chini ya Kifungu cha 12 cha Sheria Ndogo hii; “Mkurugenzi “ maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Soko” maana yake ni eneo maalum lililotengwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa kusudi la kuwa soko kwa ajili ya kuuza na kununua bidhaa, huduma au mazao; “wadau wa soko”maana yake ni wafanyabishara binafsi, vyama vya ushirika vikundi vinavofanya shughuli za biashara katika soko vilivyosajiliwa na Halmashauri; au “Wakala” maana yake ni mtu, kikundi kilichosajiliwa chini ya sheria yoyote, taasisi au kampuni iliyopewa kazi ya kutekeleza majukumu ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii; “Ushuru” utakuwa na tafsiri iliyobainishwa katika Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. 2 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) Mamlaka ya usimamizi wa Masoko - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuanzisha na kusimamia masoko na magulio katika eneo lake, na mtu binafsi hapaswi kuanzisha au kuendesha soko au gulio binafsi bila kibali maalum cha maandishi cha Halmashauri ikiwa kibali hicho kinahitajika.
3.- (1) Halmashauri ndiyo yenye mamlaka kuanzisha na kusimamia masoko na magulio yote katika eneo la mamlaka ya Halmashauri. (2) Hakuna mtu binafsi atakayeruhusiwa kuanzisha au kuendesha soko au gulio binafsi isipokuwa ikibidi, kwa kibali maalum cha maandishi cha Halmashauri. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri ina wajibu wa kutambua, kuanzisha, kuendeleza na kusimamia masoko au magulio, pamoja na kusajili wadau na kukusanya ushuru na ada.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa:- a) kuona na kutambua maeneo yanayohitaji kuwa na masoko au magulio; b) kuanzisha na kuendeleza masoko au magulio na kuboresha miundombinu yake; c) kusajili wadau wa soko; d) kusimamia usafi wa masoko na magulio; e) kusimamia ufikishaji wa huduma za umeme, maji na huduma nyingine za kijamii katika masoko na gulioni; f) kukusanya ushuru na ada mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa sokoni na gulioni. Kibali cha Minada Ujenzi na ukarabati - 5 Verify source ↗
Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyinginezo
AI-assisted research summary: Mazao, nguo na bidhaa nyinginezo zinaweza kufanyika kwenye masoko tu kwa idhini ya maandishi ya Halmashauri, baada ya mwombaji kuwasilisha maombi kwa Mkurugenzi.
5. Minada ya mazao, nguo na bidhaa nyinginezo zitaruhusiwa kufanyika kwenye masoko kwa idhini ya maandishi ya Halmashauri baada ya mwombaji kuwasilisha maombi yake kwa Mkurugenzi. - 6 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya ujenzi au
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kujenga au kukarabati chumba cha biashara, kibanda, au kizimba katika eneo la soko bila idhini ya maandishi ya Mkurugenzi.
6. Ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya ujenzi au ukarabati wa chumba cha biashara au kibanda au kizimba katika eneo la soko bila idhini ya maandishi ya Mkurugenzi. Maeneo ya kufanyia biashara - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya biashara nje ya
AI-assisted research summary: Anyone is not allowed to carry on business outside the permitted room, cage, or business area.
7. Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya biashara nje ya lililoruhusiwa kufanya chumba, kizimba au eneo biashara hiyo. Mifugo kutoingizwa sokoni Matumizi ya soko kwa muda - 8 Verify source ↗
Hakuna mifugo itakayoruhusiwa kuingia au kuingizwa
AI-assisted research summary: Livestock may not be entered into or brought to the market, except birds and small animals such as rabbits.
8. Hakuna mifugo itakayoruhusiwa kuingia au kuingizwa sokoni isipokuwa jamii ya ndege na wanyama wadogo wadogo kama sungura. - 9 Verify source ↗
(1) Mfanyabiashara ambaye hakusajiliwa katika daftari
AI-assisted research summary: Unregistered market traders may use the market temporarily only after applying for and obtaining a special permit; applications go to the Director on Form 1, and the permit is issued on Form 2.
9.- (1) Mfanyabiashara ambaye hakusajiliwa katika daftari la wafanyabiashara sokoni, anaweza kutumia soko 3 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) kwa muda baada ya kuomba na kupata kibali maalum cha matumizi ya soko kwa muda. (2) Maombi ya kibali cha kutumia soko kwa muda yatawasilishwa kwa Mkurugenzi kwa kutumia fomu Na. 1 iliyobainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (3) Kibali cha kutumia soko kwa muda kitatolewa katika Fomu Na. 2 iliyobainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (1) Hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kupika chakula, kuchoma nyama au kuendesha shughuli za mgahawa au shughuli nyingine yoyote inayohusisha moto ndani ya eneo la soko isipokuwa katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo. (2) Kila mfanyabiashara wa sokoni atapaswa kuchukua tahadhali ya moto kwa kuwa na ndoo ya mchanga au kizimia moto katika eneo lake la biashara. Tahadhari ya moto - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: A market manager must be appointed by the Director and must run and coordinate key market operations.
11. - (1) Kutakuwa na Meneja wa soko atakayeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia shughuli za uendeshaji wa soko. (2) Majukumu ya Meneja wa soko yatajumuisha kazi zifuatazo:- a) Kusimamia ukusanyaji wa ada na ushuru mbalimbali kama ilivyobainishwa katika Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Igunga; b) kuratibu huduma za ulinzi, maji na umeme katika soko; c) kuratibu usajili wa wadau wa soko kwa kuwaandikisha katika daftari la orodha ya wadau wa soko; d) kuratibu usafi na uondoshaji wa taka katika soko; e) kuhakikisha kuwa bidhaa haziuzwi kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kwa shughuli hiyo ndani ya soko; f) kutekeleza majukumu mengine yeyote 4 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) atakayeagizwa na Halmashauri; g) kudhibiti ujenzi holela katika soko; h) kwa idhini ya Mkurugenzi, atasaini kibali cha muda cha kutumia soko; i) kufanya kazi kama atakavyoelekezwa na Mkurugenzi kuhusu shughuli za soko. nyingine Wakala - 12 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua wakala wa kutekeleza majukumu kwa niaba yake chini ya Sheria Ndogo hii.
12. Halmashauri inaweza kumteua wakala ambaye atawajibika katika kutekeleza majukumu kwa niaba ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Kamati ya Wadau wa soko - 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: Wadau wanapaswa kuunda Kamati ya Wadau wa soko chini ya Sheria Ndogo hii.
13. - (1) Kutakuwa na Kamati ya Wadau wa soko ambayo itaundwa na wadau kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Wajumbe wa Kamati ya Wadau wa soko watapatikana kwa njia ya kidemokrasia na watakuwa ni Mwenyekiti na Katibu kutoka kila kikundi cha wafanyabiashara kilichosajiliwa na ambacho wanachama wake wanafanya biashara soko na wajumbe wengine watano katika watakaochaguliwa wa wafanyabiashara wote katika soko. mkutano na Vikao vya kamati ya wadau wa soko - 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: Meneja wa soko husimamia uchaguzi wa wajumbe watano; pia ndiye katibu wa kikao cha kila mwezi cha Kamati ya wadau wa soko.
14. - (3) Meneja wa soko ndiye atakayesimamia uchaguzi wa wajumbe watano watakaochaguliwa katika mkutano wa wafanyabiashara wote. (1) Kutakuwa na kikao cha Kamati ya wadau wa soko kitakachofanyika mara moja kila mwezi ambapo Meneja wa soko atakuwa katibu wa kikao na Mwenyekiti atachaguliwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya wadau wa soko. (2) Kamati ya wadau inaweza kukutana kwa jinsi itakavyoona inafaa nje ya vikao vya lazima kwa ajili ya kutekeleza maazimio yaliyoainishwa katika kikao cha kamati ya wadau wa soko au kupata ufumbuzi wa jambo la dharula. Usajili wa wadau - 15 Verify source ↗
Section 15
AI-assisted research summary: Market stakeholders must be registered by the market manager, and market brokers must be registered as traders.
15. (1) Wadau wote watasajiliwa na Meneja wa soko kwa 5 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) - lengo la kuwatambua na kuwaorodhesha kwenye rejista maalum. taarifa (2) Rejista ya wadau wa soko itaonesha muhimu kuhusu mdau ikiwa ni pamoja na:- a) tarehe ya usajili; b) jina la mdau; c) jinsia; d) aina ya biashara anayoifanya sokoni; e) kikundi chake kama mdau ni mfanyabiashara binafsi na ni mwanachama wa kikundi; f) aina ya Mdau, kama ni kikundi, ushirika au mfanyabiashara binafsi; na g) taarifa nyingine muhimu kwa kadri zitakavyohitajika. (3) Kila dalali katika soko au gulio atasajiliwa kama mfanyabiashara. (4) Wajumbe wa kamati ya wadau watawajibika pamoja na mambo mengine, kumpa ushirikiano meneja wa na kuwatambua wafanyabiashara waliopo katika vikundi vyao. katika soko Kazi za Kamati ya wadau wa soko - 16 Verify source ↗
Kazi za Kamati ya Wadau wa soko zitakuwa ni
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa soko lazima ihamasishe nidhamu, ulipaji wa ushuru na ada, maendeleo ya biashara sokoni, usafi na usalama, na itekeleze kazi nyingine itakazoelekezwa na Meneja wa soko.
16. Kazi za Kamati ya Wadau wa soko zitakuwa ni:- a) kuhimiza au kuhamasisha nidhamu katika shughuli za soko; b) kuhamasisha wadau wote wa soko kulipa ushuru na ada kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; c) kukuza na kuendeleza mfumo wa biashara sokoni; d) kuhakikisha kila eneo la mdau linakuwa safi na salama muda wote; e) kutekeleza kazi zingine watakazoelekezwa na Meneja wa soko kulingana na Sheria Ndogo hii. Kuundwa kamati Ndogo - 17 Verify source ↗
Kamati ya Wadau wa soko itaunda kamati ndogo
AI-assisted research summary: Kamati ya Wadau wa soko itaunda kamati ndogo za wajumbe watatu.
17. Kamati ya Wadau wa soko itaunda kamati ndogo ambazo zitakuwa na wajumbe watatu kutoka miongoni mwa wajumbe wa kamati ya wadau kama ifuatavyo:- a) Kamati ndogo ya Miundombinu na Usafi; b) Kamati ndogo ya Fedha, Biashara na Utawala; 6 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) na c) Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama. Saa za kazi - 18 Verify source ↗
Section 18
AI-assisted research summary: The market must stay open every day during the stated hours, and the council may close it for maintenance or another necessary reason after giving notice.
18. - (1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. (2) Halmashauri baada ya kutoa inaweza kufunga soko kwa ajili ya matengenezo au kwa sababu nyingine yoyote pale itakapoonekana kuna ulazima wa kufanya hivyo. taarifa Udhibiti wa Bidhamu - 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: Marufuku kufanya vitendo fulani ndani ya soko au gulio, na wafanyabiashara wanaweza kuitwa, kuamriwa kurekebisha hali, au kuzuiliwa kuendelea na shughuli ikiwa hawatii.
19. - (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya mambo yafuatayo katika soko au gulio:- a) kubandika au kubandua tangazo lolote bila ya idhini ya Meneja wa soko katika eneo la soko au Afisa Mwidhiniwa katika gulio; b) kuweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko au gulio; c) kufanya shughuli za siasa ndani ya soko au gulio; d) kuharibu miundombinu ya soko au gulio; e) kufaya ujenzi au ukarabati bila kibali cha Mkurugenzi; f) kutumia lugha ya matusi, kufanya vurugu au ugomvi; g) kufanya shughuli yeyote kwenye eneo ambalo haliruhusiwi au halijatengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; h) kutupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; i) kuwasha moto maeneo yasiyoruhusiwa; j) kufunga chumba cha biashara kwa madai ya kukitumia kama stoo au matumizi mengine yasiyoainishwa katika mkataba au leseni; k) kuendelea na biashara baada ya muda wa kazi. (2) Mfanyabiashara ambaye atakosa nidhamu, licha kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria anaweza kuitwa na Meneja wa soko au Afisa Mwidhiniwa katika gulio kwa vyovyote itakavyokuwa, na baada ya kupewa nafasi ya kujitetea, Meneja au Afisa 7 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) anaweza kumtaka mtu Mwidhiniwa huyo kurekebisha hali aliyoisababisha ambayo haitakiwi. (3) Mfanyabiashara ambaye atakaidi amri ya Meneja au Afisa Mwidhiniwa anaweza kuzuiliwa kuendelea na shughuli zake sokoni, gulioni au mnadani. Usafi wa soko au gulio - 20 Verify source ↗
Section 20
AI-assisted research summary: Market traders must keep their area clean, have a covered waste container, join the scheduled weekly general cleaning, and follow health rules.
20. - (1) Kila mfanyabiashara anayefanya shughuli za biashara katika soko au gulio atawajibika kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote, na anatakiwa awe na chombo maalum chenye mishikio na mfuniko kwa ajili ya kuhifadhia taka. (2) Meneja wa soko kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko watapanga siku, namna na muda maalum mara moja kwa juma kwa ajili ya kufanya usafi wa jumla katika eneo lote la soko. (3) Kila mfanyabiashara katika eneo atatakiwa kushiriki katika usafi wa utakaofanyika katika siku itakayopangwa. la biashara jumla (4) Kila mfanyabiashara katika soko au gulio atatakiwa kufuata kanuni za afya. Ufungaji wa bidhaa ziletwazo sokoni - 21 Verify source ↗
Section 21
AI-assisted research summary: Bidhaa zinazoletwa sokoni au gulioni lazima zifungashwe kwenye makasha maalumu ya kusafirishia bidhaa, na bidhaa zilizoharibika au zilizoisha muda wa matumizi haziruhusiwi kuletwa au kuingizwa sokoni au gulioni.
21. - (1) Bidhaa zote ziletwazo sokoni au gulioni zitatakiwa kufungashwa kwenye makasha maalumu ya kusafirishia bidhaa. (2) Mazao au bidhaa zilizoharibika au zilizoisha muda wa matumizi haziruhusiwi kuletwa au kuingizwa sokoni au gulioni. (3) Endapo italazimika kufungasha bidhaa kwa kutumia majani wakati wa kusafirisha, majani hayo yatabaki ndani ya chombo kilichotumika kusafirishia bidhaa hiyo na mwenye bidhaa au msafirishaji atawajibika kuhakikisha majani hayo yanasafirishwa na kutupwa katika dampo la Halmashauri kwa gharama zake. Ulipaji wa ada au ushuru - 22 Verify source ↗
Section 22
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itoeza ada au ushuru kwenye masoko na magulio, na kila mfanyabiashara lazima alipe ada au ushuru unaostahili.
22. - (1) Halmashauri itatoza ada au ushuru kwenye masoko na magulio kwa huduma na shughuli mbalimbali kama zilivyobainishwa katika Sheria Ndogo ya Ada 8 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. (2) Kila mfanyabiashara atatakiwa kulipa ada au ushuru stahiki kwa Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii na kwa viwango vilivyotajwa katika Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. (3) Meneja wa soko au Afisa Mwidhiniwa atakuwa msimamizi mkuu wa ukusanyaji wa mapato ya sokoni, na kwa upande wa gulio Afisa Mwidhiniwa atasimamia kazi hiyo. Ada ya kupangisha Eneo - 23 Verify source ↗
Section 23
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweka ada ya kupanga eneo la biashara kwa mfanyabiashara ambaye hajasajiliwa kufanya biashara katika eneo la soko.
23. - (1) Halmashauri itatoza ada ya kupanga eneo la biashara ambayo italipwa na mfanyabiashara yeyote asiyesajiliwa kufanya biashara katika eneo la soko. (2) Ada kupanga eneo italipwa kwa Halmashuri kwa kuzingatia viwango vilivyotajwa katika Sheria Ndogo Ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Huduma ya usafi, ulinzi, maji na umeme - 24 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara
AI-assisted research summary: Kila mfanyabiashara lazima alipe gharama za ulinzi, usafi, maji na umeme kila mwezi, kwa kufuata utaratibu utakaowekwa na Halmashauri.
24. Kila mfanyabiashara atawajibika kugharamia huduma za ulinzi, usafi, maji na umeme kulingana na mahitaji yake kila mwezi kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na Halmashauri. katika soko Barua, hati kutoka Halmashauri - 25 Verify source ↗
Section 25
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuandika barua au hati kwa watu au umoja wa watu kuhusu usimamizi wa soko au gulio, au kudai fedha inayostahili kulipwa; mpokeaji wa barua au hati lazima asaini sehemu iliyoelekezwa kama uthibitisho wa kufikishwa.
25. - (1) Halmashauri inaweza kuandika barua au hati, kwa mtu yeyote au umoja wa watu kwa lengo kutoa taarifa, wito au maelekezo kuhusiana na uendeshaji na usimamizi wa soko au gulio, au kudai fedha ambayo inapaswa kulipwa na mhusika kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Barua au hati itakayoandikwa na Halmashuri kwenda kwa mtu yeyote au umoja wa watu unaotambulika sokoni au gulioni itakapokelewa na mhusika au mfanyakazi wake au mtu ambaye ameachiwa ofisi au mtu mzima anayeishi nyumbani mwa mhusika au kiongozi wa umoja husika. (3) Mtu atakayepokea barua au hati kutoka Halmashuri atapaswa kusaini sehemu atakayoelekezwa kusaini na mtu atakayemkabidhi barua au hati husika kwa 9 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) Makosa na Adhabu kufililisha kosa ajili ya kuthibitisha kufikishwa kwa barua au hati iliyopelekwa. - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya
AI-assisted research summary: Anyone who acts against the by-law’s requirements commits an offence and may be fined, imprisoned, or both.
26. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki mbili au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi kumi na mbili au adhabu zote mbili, faini na kifungo kwa pamoja. - 26 Verify source ↗
Bila kujali masharti ya Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kumtoza mtu aliyekiri kosa kiasi kisichozidi shilingi 200,000, akitimiza masharti yaliyotajwa.
26. Bila kujali masharti ya Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mtu atakiri kutenda kosa na kuwa tayari kutimiza wajibu wake na kujaza Fomu Na. 3 iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii 10 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) JEDWALI LA KWANZA Fomu Na. 1 MAOMBI YA KIBALI CHA KUTUMIA SOKO KWA MUDA (Kifungu cha 10(2)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This line is a form field for the applicant’s name.
1. Jina la Mwombaji……………………………………………………………………………… - 2 Verify source ↗
Anuani ya
AI-assisted research summary: Kichwa hiki kinahusu anuani ya mwombaji.
2. Anuani ya Mwombaji……………………………………………………………………………… - 3 Verify source ↗
Matumizi
AI-assisted research summary: Kichwa cha kifungu ni “Matumizi yanayokusudiwa.”
3. Matumizi yanayokusudiwa………………………………………………………………………… - 4 Verify source ↗
Eneo maalum la soko linalokusudiwa kutumiwa (Kama ni muhimu
AI-assisted research summary: Kichwa cha sehemu kinataja eneo maalum la soko linalokusudiwa kutumiwa.
4. Eneo maalum la soko linalokusudiwa kutumiwa (Kama ni muhimu kutaja)…………………….... ……………………………………………………………………………………………… - 5 Verify source ↗
Muda ninaokusudia kutumia eneo la
AI-assisted research summary: Section heading about the time you intend to use a market area.
5. Muda ninaokusudia kutumia eneo la soko………………………………………..………………. - 6 Verify source ↗
Nathibitisha kwamba maelezo niliyotoa ni kweli tupu na niko tayari kuzingatia masharti
AI-assisted research summary: The applicant declares that the information provided is true and that they are ready to comply with the permit conditions if the permit is granted.
6. Nathibitisha kwamba maelezo niliyotoa ni kweli tupu na niko tayari kuzingatia masharti ya kibali endapo nitapewa kibali hicho. Jina la Mwombaji………………………………………………………………………………… Saini …………………………………………………………………...…………………… Tarehe……………………………………………………………………………………… 11 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) KIBALI CHA KUTUMIA SOKO KWA MUDA (Kifungu cha 10(3) Fomu Na. 2 - 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This section asks for the applicant’s name.
1. Jina la Mwombaji………………………………………………………………………………… - 2 Verify source ↗
Anuani ya
AI-assisted research summary: This section is titled “Applicant’s address.”
2. Anuani ya Mwombaji……………………………………………………………………………. - 3 Verify source ↗
Eneo ambalo kibali hicho
AI-assisted research summary: Hii inataja eneo ambalo kibali hicho kitatumika.
3. Eneo ambalo kibali hicho kitatumika………………………….………….…………………….. - 4 Verify source ↗
Muda wa kibali ni kuanzia tarehe ……………………………… hadi
AI-assisted research summary: Kibali kinaanza tarehe iliyojazwa na kuisha tarehe iliyojazwa.
4. Muda wa kibali ni kuanzia tarehe ……………………………… hadi tarehe…………….……. - 5 Verify source ↗
Masharti ya kutumia kibali
AI-assisted research summary: This section is a form for stating permit conditions and for confessing an offence under the Igunga market bylaw.
5. Masharti ya kutumia kibali: a) ………………………………………………………………………………………… b) ……………………………………………………………………………….……… c) ……………………………………………………………………………….……… d) ……………………………………………………………………………………..… e) ………………………………………………………………………………..……… Kimetolewa leo tarehe………………….mwezi………………mwaka……………………………… Jina……………………………………………………………. Saini………………………………………………………….... Cheo…………………………………………………………... 12 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) (Imeundwa chini ya kifungu cha 28) KUFILILISHA KOSA Fomu Na. 3 Mimi…………………………………………….…………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwamba Tarehe ………Mwezi………...Mwaka………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha………………. cha Sheria Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri, niko tayari kulipa kiasi ninachodaiwa pamoja na faini na kutekeleza wajibu niliopewa na Sheria Ndogo hii. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI KWELI NA NINAYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe………………. ya Mwezi………………..………. Mwaka………………… Jina…………………………………………Saini……………………………………… Mbele ya: Jina………………………………………...Cheo……………………………………. Saini………………………………………Tarehe…………………………………… 13 Sheria Ndogo ya Usimamizi Na Uendeshaji Wa Masoko Na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 286 (Linaendelea.) Nembo na Muhuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga vimebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 30/4/2020 na ubandikaji huo kushuhudiwa na:- REVOCATUS L. K. KUULI, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Igunga PETER ONESMO MALODA, Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya, Igunga L.S NAKUBALI, Dodoma, SELEMANI SAID JAFO (MB.), 22 Februari, 2021 Waziri wa Nchi -OR- Tamisemi 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usimamizi na Uendeshaji wa Masoko na Magulio ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ya mwaka 2021
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in