AI-assisted research summary: Mipango ya Jumla na ya Kina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inapaswa kuandaliwa na kuhifadhiwa na Mkurugenzi wa Mipango miji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
3. Mipango ya Jumla na ya Kina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali itaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipango miji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. 1 Tangazo La Seriakali Na. 84 (Linaendelea) Amri ya Kupanga Eneo la Mkata _______ JEDWALI ________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: - “Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba NP90 yenye majira - nukta 408635MS, 9351289KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi katika uelekeo wa mto Mligazi hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba NP31 yenye majira - nukta 425570MS, 9342537KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi kwa umbali wa kilomita 2.8 katika uelekeo wa 223º 46’ 58’’ hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VTB292 yenye majira - nukta 427657MS, 9344805KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi kwa umbali wa kilomita 8.8 katika uelekeo wa 287º 32’ 18’’ hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VTB117 yenye majira - nukta 436284MS, 9342073KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 1.3 katika uelekeo wa 193º 27’ 30’’ hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VTB 455 yenye majira - nukta 433653MS, 9347816KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 5 katika uelekeo wa 325º 16’ 06’’ hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VTB 296 yenye majira - nukta 433609MS, 9347899KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 8.11 katika uelekeo wa 19º 25’ 22’’ hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VTB 125 yenye majira - nukta 436360MS, 9355701KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini- Magharibi kwa kufuata uelekeo wa mto Mkula hadi unapokutana na mto Kwale; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini-Mashariki kwa kufuata uelekeo wa mto Kwale hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba NP1 yenye majira - nukta 423649MS, 9364312KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 3.7 katika uelekeo wa 151º 17’ 54’’ hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira - nukta 421847MS, 9367636KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 4.8 katika uelekeo wa 203º 28’ 55’’ hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira – nukta 414820MS, 9363172KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 6.92 katika uelekeo wa 31º 45’ 09’’ hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VTB102 yenye majira – nukta 416088MS, 9357151KZ; hadi ulipoanzia”. ANGELINE S. MABULA, Dodoma 6 February, 2023 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2