AI-assisted research summary: General and detailed plans for the specified area must be prepared and kept by the Town Planning Director and the Executive Director of Chemba District Council.
3. Mipango ya jumla na kina ya eneo lililoainishwa katika itaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba. Jedwali 1 Tangazo la Seriakali na. 88 (linaendelea) Amri ya Kupanga Eneo la Chandama _______ JEDWALI _______ (Limeandaliwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo:- “Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba CM1 yenye majira – nukta 181791.235MS, 9433171.882KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki katika uelekeo wa KZ78004’37.45’’MS kwa umbali wa kilomita 12.09 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba CM2 yenye majira – nukta 193623.627MS, 9430673.459KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki kwa kukatiza barabara ya Mrijo Juu - Songolo katika uelekeo wa KS22007’34.08’’MS kwa umbali wa kilomita 3.68 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba CM3 yenye majira - nukta 192233.802MS, 9427255.206KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa KS66020’44.00’ kwa umbali wa kilomita 4.81 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba CM4 yenye majira – nukta 187822.770MS, 9425323.080KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS61018’58.51’’MG kwa umbali wa kilomita 1.51 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba CM5 yenye majira – nukta 186491.814MS, 9426051.266KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi katika uelekeo wa KS82001’20.23’’MG kwa umbali wa kilomita 5.37 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba SY6 yenye majira – nukta 181167.989MS, 9426797.370MG; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi katika uelekeo wa MG6022’01.20’’ kwa umbali wa kilomita 2.18 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba CM7 yenye majira – nukta 180925.154MS, 9428973.611KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ9025’37.77’’MG kwa umbali wa kilomita 1.3 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba CM8 yenye majira – nukta 181149.753MS, 9430326.323KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi katika uelekeo wa KZ10013’55.73’’MG kwa umbali wa kilomita 2.07 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba CM9 yenye majira – nukta 181518.325MS, 9432368.189KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi katika uelekeo wa KZ18045’21.42’’MG kwa umbali wa kilomita 8.48 hadi ulipoanzia.” Dodoma, 6 Februari, 2023 ANGELINE S. MABULA, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2