AI-assisted research summary: The Director of Urban Planning and the Mafinga Town Director must prepare and keep general and detailed plans for the area in the Schedule.
3. Mipango ya jumla na kina katika eneo la kwenye Jedwali itaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji na Mkurugenzi wa Mji Mafinga. 1 Amri ya Mipango Miji ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Katika Eneo la Mkombwe Na Mjimwema Tangazo la serikali na. 101 (linaendelea) _______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo:- “Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 01 yenye majira - nukta 752217MS, 9082632KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.09 hadi unapokutana na barabara ya TANZAM kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 02 yenye majira - nukta 754360MS, 9084780KZ; baada ya hapo mpaka unafuata barabara ya TANZAM kwa umbali wa kilomita 0.45 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 03 yenye majira - nukta 754485MS, 9085216KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa kufuata barabara ya TANZAM hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 04 yenye - majira nukta 754526MS, 9085343KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi kwa umbali wa kilomita 0.39 hadi unakutana na barabara ya zamani ya Dar es Salaam kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 05 yenye majira - nukta 754210MS, 9085571KZ; baada ya hapo mpaka unafuata barabara ya zamani ya Dar es Salaam kwa umbali wa kilomita 0.49 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 06 yenye majira - nukta 754165MS, 9085084KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 07 yenye majira - nukta 754198MS, 9085063KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 0.23 hadi unapokutana na barabara ya zamani ya Dar es Salaam kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 08 yenye majira - nukta 754184MS, 9084835KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 09 yenye majira - nukta 754207MS, 9084817KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MKM 01 hadi ulipoanzia’’ ANGELINE S. MABULA, Dodoma, 6th February, 2023 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2