AI-assisted research summary: This section describes the planning area and its boundaries, and says the related table is to be kept by the listed planning and district officials.
3. Mipango ya jumla na kina katika eneo na Jedwali lililoainishwa kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba. itaandaliwa _______ JEDWALI _______ (Limeandaliwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo:- “Unaanzia kwenye barabara kuu ya kijiji cha Katale kwenda kwenye kitovu cha kijiji cha Rubafu kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VU 64 yenye majira - nukta 370380MS, 9883004KZ; baada ya hapo mpaka unafuata gema la mwamba kwa umbali wa kilomita 1.16 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VU 164 yenye majira - nukta 370224MS, 9884157KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 2.067 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VU137 yenye majira - nukta 371543MS, 9885749KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.176 hadi kwenye ufukwe wa ziwa Victoria kwenye majira nukta 371663.9760MS, 9885887.7732KZ; baada ya hapo mpaka unafuata ukingo wa ufukwe wa Amri ya Kupanga Eneo la Kyamalange Tangazo la Serikali na.126 (linaendelea) ziwa Victoria kwa kuelekea Kusini hadi kwenye makutano ya kijito kidogo cha Nyamishasha unapoingia ziwa Victoria kwenye majira - nukta 371836.1755MS, 9882407.9456KZ; baada ya hapo mpaka unafuata kijito cha Nyamishasha Kaskazini - Magharibi hadi kwenye majira - nukta 3708850.9738MS, 9882830.3916KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi kwa umbali wa kilomita 0.49 hadi jirani na barabara kuu ya kijiji cha Katale kwenda kwenye kitovu cha kijiji cha Rubafu kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba VU 64 yenye majira - nukta 370380MS, 9883004KZ hadi ulipoanzia”. Dodoma, 6 February, 2023 ANGELINE S. MABULA Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi