AI-assisted research summary: The town planning and Mafinga town directors must prepare and keep the area’s general and detailed plans in the table.
3. Mipango ya jumla na kina katika eneo la itaandaliwa na kuhifadhiwa kwa kwenye Jedwali Mkurugenzi wa Mipango miji na Mkurugenzi wa Mji wa Mafinga. 1 Amri ya Mipango Miji ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Katika Eneo la Mifugo Na Luganga Tangazo la Serikali na. 231 (Linaendelea.) _______ JEDWALI ________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Mpaka naanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba LGG 01 kwenye makutano ya barabara kuu ya Mafinga–Mgololo kwenye mto mdogo wa Ruaha yenye majira - nukta 756320MS, 9074399KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi kwa kufuata barabara kuu ya Mafinga - Mgololo kwa umbali wa kilomita 6.35 hadi kwenye majira - nukta 754911.656MS, 9079175.344KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 1.40 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MTG 04 yenye majira - nukta 756397MS, 9079129KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 0.36 hadi unapokutana na mkondo kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MTG 05 yenye majira – nukta 756354.098MS, 9079484.518KZ; baada ya hapo mpaka unafuata mkondo wa mto Mselefyuko kwa ukielekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 0.80 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MFG 01 yenye majira - nukta 756508.525MS, 9080190.370KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.84 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MFG 02 yenye majira – nukta 757348.679MS, 9080126.287KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 2.06 hadi unapokutana na mkondo wa mto Mselefyuko kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MFG 03 yenye majira – nukta 758009.865MS, 9082077.302KZ; baada ya hapo mpaka unafuata mkondo wa mto Mselefyuko kwa upande wa Mashariki kwa umbali wa kilomita 4.96 hadi kwenye unapokutana na mto mdogo wa Ruaha kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MFG 04 yenye majira – nukta 761547.807MS, 9080389.326KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa kufuata mto mdogo wa Ruaha kwa umbali wa kilomita 10.01 hadi ulipoanzia’’ Dodoma, 6 Februari, 2023 BANGELINE S. MABULA, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2