AI-assisted research summary: This section defines several terms used in the Order, including cargo documents, consignee, consignor, charges, cargo consolidation and deconsolidation, and shipping agent.
3. Katika Amri hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “hati ndogo ya mzigo majini” maana yake ni nyaraka iliyotolewa na ya usafirishaji ya mzigo mkusanyaji mzigo kwa mtumaji wa mzigo ikionesha hati ya mzigo uliokusanywa ikiwa na taarifa za uzito wa mzigo, vipimo, maelezo ya mzigo na idadi, jina la mtumaji na mpokeaji, jina la meli, bandari iliyopakia mizogo na bandari itakayoshusha mzigo na namba ya hati ya mzigo majini; “hati ya kukabidhi” maana yake ni nyaraka inayotolewa na mtawanyaji wa mzigo, kwa niaba ya mkusanyaji wa mzigo, kwa mtu ikiidhinisha mwendeshaji wa aliyetajwa 1 Amri ya Tozo Za Wakusanyaji Na Watawanyaji wa Mizigo Tangazo la Serikali Na. 269 (Linaendelea.) Sura ya 415 TS. Na. 7 la 2020 TS. Na. 3 37 la 2018 bandari au bandari kavu kukabidhi mzigo ulio katika hati ndogo ya mzigo majini kwa mtu aliyetajwa; “mpokeaji wa mzigo” maana yake ni mtu ambaye anatumiwa mzigo uliopokelewa kubebwa kwenye meli na ambaye ametajwa hivyo kwenye hati ndogo ya mzigo majini; “mtumaji” maana yake ni mtumaji wa mzigo aliyetajwa katika hati ndogo ya mzigo majini ambaye anawajibika kuanzisha mchakato wa kusafirisha, na ambaye anawajibika kulipia gharama za usafirishaji au kuingia mkataba na msafirishaji kuhusu namna gharama za usafirishaji zitakavyolipwa; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania; “Shirika” maana yake Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania lilioanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria; “tozo” maana yake ni gharama au bei pamoja na vigezo na masharti yanayotumiwa na mtoa huduma anayedhibitiwa; “ukusanyaji wa mizigo” maana yake ni kuunganisha mizigo miwili au zaidi kutoka kwa watumaji wa mzigo na kufanya mzigo mmoja kwa ajili ya usafirishaji katika meli, au katika kasha moja na unaweza kujumuisha uratibu wa kazi za upokeaji mizigo, kuhifadhi, kuipanga, kuiandaa kwa kutumwa, kuiwekea utambulisho katika na ukusanyaji wa mizigo; itakavyolazimu alama kama “utawanyaji wa mizigo” maana yake kutenganisha mzigo ulio katika hati ya mzigo majini katika mizigo miwili au zaidi kwa mujibu wa hati ndogo za mzigo majini kwa ajili ya kukabidhi kwa wapokeaji na unaweza kuhusisha uratibu wa kazi ya kuhifadhi mzigo, kufungua mzigo na kupanga kama itakavyolazimu katika kutenganisha na kukabidhi mzigo kwa wamiliki; “wakala wa meli” maana yake ni kampuni 2 Amri ya Tozo Za Wakusanyaji Na Watawanyaji wa Mizigo Tangazo la Serikali Na. 269 (Linaendelea.) inayojihusisha na utoaji wa huduma za uwakala wa meli katika bandari za bahari kwa mujibu wa Sheria. SEHEMU YA PILI TOZO NA MASHARTI YANAYOTUMIWA Tozo zilizoidhinishwa