AI-assisted research summary: Mwombaji lazima azingatie masharti ya kibali cha ujenzi wa bomba la gesi asilia na kuchukua hatua za kiufundi, usalama, na mazingira wakati wa ujenzi.
3. Mwombaji anapewa kibali cha ujenzi kwa ajili ya kujenga bomba la kusambaza gesi asilia lenye urefu wa mita 1500, kipenyo cha milimita 125 na kiwango cha PE 100 SDR 11 HDPE na vifaa vyake kwa ajili ya kupeleka gesi asilia kwenye kiwanda cha nguo cha Urafiki kilichopo manispaa ya Ubungo kwa vigezo na masharti yafuatayo- (a) kuzingatia michoro iliyopitishwa, viwango vya kiufundi, mkuza na njia zilizoainishwa au sheria zozote zinazotumika; (b) kuhakikisha kuwa bomba la gesi asilia na vifaa 1 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Usambazaji Gesi Katika Eneo la Ubungo kwa Kampuni ya Pan African Energy (T) Tangazo la Serikali Na. 725 (Linaendelea.) vyake vinajengwa kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa au sheria; (c) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa bomba na vifaa vyake wakati wa ujenzi unafanyika kadri inavyohitajika ili kuhakikisha kuwa ujenzi, vifaa, uchomeleaji, maunganisho na ujaribuji wa bomba baada ya kukamilika unafanyika kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa; (d) kuhakikisha kuwa bomba pamoja na vifaa vyake vinajengwa kwa kufuata mikuza iliyoidhinishwa kwa madhumuni ya kuepusha au kupunguza mbeleni uwezekano zitakazosababishwa na maendeleo ya viwanda au miji, kupanuliwa kwa njia na kutoharibu mazingira au sehemu za kihistoria; hatari wa za (e) kuhakikisha kuwa hakuna au upo usumbufu mdogo kwa wakazi walio karibu na eneo la ujenzi na usalama kwa umma unapewa kipaumbele. Endapo ulipuzi utafanyika, ufanywe kwa kuzingatia taratibu za kisheria zilizopo na kufanywa na mtu mwenye sifa za kazi ya ulipuzi kwa kuzingatia usalama kwa umma, mifugo, wanyama, majengo, miundo mbinu ya simu, umeme, miundo mbinu ya chini ya ardhi na mali nyingine zilizo karibu na eneo kunako fanyika ulipuzi; na ardhi (f) kuhakikisha kuwa katika kutengeneza njia juhudi za kupunguza uharibifu zinakuwepo kwenye kuzuia mazingira yatakayosababisha kuziba kwa mifereji ya kupitisha maji na mmomonyoko wa udongo. Baada ya ujenzi, ardhi itapaswa kurudishwa katika kadri iliyokuwepo itakavyowezekana; kwa hali (g) kuhakikisha kuwa, bomba linalokatisha reli, barabara, vijito, maziwa, mito na alama za usalama kama vile taa hauathiri vitu ujenzi wa 2 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Usambazaji Gesi Katika Eneo la Ubungo kwa Kampuni ya Pan African Energy (T) Tangazo la Serikali Na. 725 (Linaendelea.) hivi kwa usalama wa umma. Kukatisha kwa bomba kwenye vitu hivi kutazingatia sheria zilizopo na makatazo ya wadhibiti kwenye eneo hili. Kabla ya ujenzi wa bomba unaokatisha maeneo tajwa, ni lazima uwepo utaratibu baina ya Mwombaji na wamiliki wa maeneo (h) kuhakikisha kuwa njia linakopita bomba imepimwa na kuwekewa ambazo zitaendelea kuwepo wakati wote wa ujenzi kwa mujibu wa kibali kilichotolewa na mmili kiwanjia; alama (i) bomba litafuata mkuza ulioanishwa wakati wa upimaji; (j) kuhakikisha kuwa urefu wa mfereji wa bomba ni sahihi kwa kuzingatia eneo, matumizi ya uso wa ardhi, hali ya ardhi na uzito utokanao na barabara na reli. Upana wa mfereji ni lazima uruhusu kuwekwa kwa bomba bila kuharibu rangi yake na kuwezesha kazi ya kupaka rangi na ufungaji wa bomba kufanyika ndani ya mfereji; (k) kuchukua hatua zote stahiki ili kulilinda bomba na vifaa vyake dhidi ya mafuriko, udongo dhaifu, tetemeko la ardhi na hatari nyingine zinazoweza kusababisha bomba kuhama au kupata uzito wa ziada; (l) kuhakikisha kuwa bomba linalazwa umbali wa nchi 12 (milimita 300) kutoka kwenye miundo mbinu mingine iliyo chini ya ardhi ambayo haihusiani na gesi asilia. Endapo haitawezekana kupata umbali huu, bomba lilindwe dhidi ya uharibifu unaoweza kujitokeza kwa kuwa karibu na miundo mbinu mingine. Ni lazima uwepo umbali wa kutosha kutoka kwenye bomba na miundo mbinu mingine ya chini ya ardhi ili kuwezesha bomba kufanyiwa matengenezo na kulilinda dhidi ya uharibifu unaoweza kujitokeza kwa kuwa karibu na miundo mbinu mingine; (m) kuhakikisha kuwa vifaa vinavyotumika kwa ajili 3 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Usambazaji Gesi Katika Eneo la Ubungo kwa Kampuni ya Pan African Energy (T) Tangazo la Serikali Na. 725 (Linaendelea.) ya uchomeleaji ni vya ukubwa na aina sahihi kwa kazi hiyo vitakavyohakikisha uchomeleaji kuendelea mzuri kutumika na usalama wa watu; utakaowezesha bomba (n) kuzingatia viwango vya mazingira, afya na usalama vilivyoainishwanasheria. Afya na vitapaswa usalama wa watu kuzingatiwa na kuhakikisha matumizi ya vifaa vya usalama (PPE) wakati wote kama vile kofia ngumu, miwani na viatu vya usalama na matumizi ya kizima moto; vifaa na (o) kuhakikisha kuwa miundo mbinu yote ya utoaji huduma kwa umma bila kujali kuwa ina dhibiti wana Mamlaka ama la inalindwa dhidi ya uharibifu na kuwaarifu wamiliki wake wawepo eneo la ujenzi wakati wa kujenga; (p) kuhakikisha kuwa eneo la ujenzi limezungushiwa utepe watahadhari; (q) kuweka mifumo ya ulinzi na ufuatiliaji wa bomba ikiwemo mifumo ya kuzuia kutu, valvu za kuondoa mgandamizo, valvu za kujifunga, kipimo cha mgandamizo, mfumo wa kugundua uvujaji wa gesi, mfumo wa kusafisha na kufuatilia unene wa bomba na mifumo ya mawasiliano; (r) kuhakikisha alama mbalimbali kama vile zakuanisha mkuza, bomba na mapumlio zimewekwa eneo lote la bomba; na (s) kuhakikisha kuwa alama zilizowekwa zinakuwa na alama za onyo, taarifa ya tahadhari na namba za simu za dharula Ukomo kwa kibali cha ujenzi