SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI KWENYE MIALO YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI YA MWAKA, 2020
This by-law is named the Kinondoni Municipal Council fishing-landing management by-law and starts to apply after publication in the Government Gazette.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI KWENYE MIALO YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI YA MWAKA, 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is named the Kinondoni Municipal Council fishing-landing management by-law and starts to apply after publication in the Government Gazette. This section says the by-law applies throughout the entire area of Kinondoni Municipal Council. This section defines key terms used in the by-law, including officer, BMU, fishing gear, landing site, director, and agent. Shughuli zote zinazohusiana na rasilimali za uvuvi katika eneo la Halmashauri lazima ziwe chini ya usimamizi wa Halmashauri. This provision sets out the BMU Council structure and the size and responsibilities of its committees.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI KWENYE MIALO YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI YA MWAKA, 2020
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This by-law is named the Kinondoni Municipal Council fishing-landing management by-law and starts to apply after publication in the Government Gazette.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi kwenye Mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya Mwaka, 2020, na itaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii, itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This section says the by-law applies throughout the entire area of Kinondoni Municipal Council.
2. Sheria Ndogo hii, itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama itaelekezwa
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including officer, BMU, fishing gear, landing site, director, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama itaelekezwa vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “BMU” (Beach Management Unit) maana yake ni kikundi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi kwenye mialo; “chombo cha usafiri majini” maana yake ni mtumbwi wa injini, kasi,dau au mashuwa; 1 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kwenye Mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 182 (linaendelea) “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni; “Kamati” maana yake ni Kamati ya BMU; “Kituo” maana yake ni eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya BMU kuendesha shughuli zake na wavuvi kushushia samaki wanapotoka kuvua; “Mjumbe” maana yake Mjumbe wa Kamati ya BMU; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mwalo” maana yake ni sehemu ya kando kando ya bahari ambayo imetengwa kwa ajili ya shughuli za uvuvi na usimamizi wa BMU katika shughuli za uvuvi; “mvuvi halali” maana yake ni mtu yeyote anayemiliki leseni halali ya shughuli za uvuvi; “nyavu” maana yake ni nyavu za makila (gillnets) zenye macho yenye ukubwa wa nchi 5,6 na kuendelea; “ndoano” maana yake ni ndoano za saizi namba 7,8, 9 na 10 tu zinazoruhusiwa kisheria kuopolea samaki; “rasilimali za uvuvi” maana yake ni mazao yote yatokanayo na shughuli za uvuvi; “udhibiti wa ubora wa samaki” maana yake ni uhakiki na uzingatiaji wa ubora wa samaki, vyombo na vifaa vinavyotumika kuvulia na kubebea samaki kabla ya kwenda viwandani kuchakatwa; “Uongozi” maana yake ni uongozi wa BMU katika mwalo 2 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kwenye Mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 182 (linaendelea) husika; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au shirika ambalo litakuwa limepewa mamlaka na Halmashauri kukusanya ushuru na kusimamia Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri; “zana za uvuvi” maana yake ni nyavu za makila zenye macho ya ukubwa wa inchi 5, 6 na kuendelea. Usimamizi wa shughuli za uvuvi. - 4 Verify source ↗
Shughuli zote zinazofanywa na zinazotokana na rasilimali
AI-assisted research summary: Shughuli zote zinazohusiana na rasilimali za uvuvi katika eneo la Halmashauri lazima ziwe chini ya usimamizi wa Halmashauri.
4. Shughuli zote zinazofanywa na zinazotokana na rasilimali za uvuvi zilizo katika eneo la Halmashauri zitafanywa chini ya Usimamizi wa Halmashauri. Muundo wa - 5 Verify source ↗
Kutakuwa na Baraza la BMU ambalo litakuwa na muundo
AI-assisted research summary: This provision sets out the BMU Council structure and the size and responsibilities of its committees.
5. Kutakuwa na Baraza la BMU ambalo litakuwa na muundo BMU ufuatao: (1) Kutakuwa na Kamati Tendaji yenye wajumbe kumi na tano, wakiwemo Mwenyekiti, Katibu, Mweka hazina, mtunza bohari, mzee maarufu pamoja na wajumbe kumi. Kamati hii itakuwa na jukumu la kusimamia shughuli zote za kikundi. (2) Kutakuwa na Kamati ya Fedha na mipango ambayo itakuwa na wajumbe watano ambao ni Mwenyekiti, Katibu na wajumbe watatu. (3) Kamati iliyoanzishwa chini ya kifungu kidogo cha (2), itakuwa na wajibu wa kupanga mipango ya kuendesha shughuli za kikundi pamoja na kusaidia kukusanya mapato yatokanayo na shughuli za uvuvi kwa idhini ya Halmashauri (4) Kutakuwa na Kamati ya doria ambayo itakuwa na wajumbe watano wakiwemo Mwenyekiti na Katibu, itawajibika kufanya doria kwa kusaidia Halmashauri katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (5) Kutakuwa na Kamati ya Takwimu na taarifa ambayo itakuwa na wajumbe watano wakiwemo Mwenyekiti na Katibu na itakuwa na wajibu wa kukusanya takwimu za mazao mbalimbali ya uvuvi kwa kushirkiana na Halmashauri. - 6 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote ambaye anajishughulisha na masuala ya
AI-assisted research summary: Watu wanaojihusisha na uvuvi lazima wawe na leseni ya uvuvi, na mvuvi anayesafiri kuvua nje ya eneo la BMU lazima apewe kibali kwa madhumuni hayo.
6.-(1) Mtu yeyote ambaye anajishughulisha na masuala ya 3 Leseni za uvuvi Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kwenye Mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 182 (linaendelea) mvuvi atatakiwa kuwa na leseni ya uvuvi. (2) Kila mvuvi atakayesafiri kwenda kuvua nje ya eneo lililo chini ya BMU atatakiwa kupewa kibali kwa madhumuni hayo. Usajili wa wavuvi - 7 Verify source ↗
Kutakuwa na orodha ya wavuvi wote katika BMU
AI-assisted research summary: Wavuvi wote katika BMU wanapaswa kuwa kwenye orodha, na kila mvuvi asajiliwe kabla ya kuanza kazi.
7. Kutakuwa na orodha ya wavuvi wote katika BMU ambapo kila mvuvi atasajiliwa kabla ya kuanza kazi akionyesha kuwa yeye ni mmiliki wa chombo cha uvuvi au ni mwajiriwa katika chombo cha uvuvi. Maegesho ya mitumbwi - 8 Verify source ↗
Mitumbwi yote ya kukusanyia samaki au kusafirisha
AI-assisted research summary: Boats used to collect fish or carry cargo or passengers must be parked 10 meters away from the fence.
8. Mitumbwi yote ya kukusanyia samaki au kusafirisha mizigo au abiria itaegeshwa umbali wa mita kumi kutoka kwenye uzio. Kuhudhuria Vikao Vyoo vya umaa - 9 Verify source ↗
Kila mvuvi au mwanachama wa BMU atalazimika
AI-assisted research summary: Kila mvuvi au mwanachama wa BMU lazima ahudhurie vikao vya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wavuvi au Kamati ya Mazingira vinapoitishwa.
9. Kila mvuvi au mwanachama wa BMU atalazimika kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wavuvi au Kamati ya Mazingira pale vikao vitakapoitishwa na Kamati hizo. - 10 Verify source ↗
Kutakuwa na vyoo vya umma vitakavyo jengwa na
AI-assisted research summary: The council must build and manage public toilets in landing sites, and they must operate under health-law procedures.
10. Kutakuwa na vyoo vya umma vitakavyo jengwa na kusimamiwa na Halmashauri katika maeneo ya mwalo na vitaendeshwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Sheria za Afya. Uhakiki wa ubora wa samaki - 11 Verify source ↗
Magari yote yatakayobeba samaki yatakuwa ni magari
AI-assisted research summary: Vehicles carrying fish must be special vehicles with a permit from the fish quality and standards supervising officer, and they must be free of dust or rust and have doors made from acceptable materials.
11. Magari yote yatakayobeba samaki yatakuwa ni magari maalum yenye kibali cha kusafirisha samaki kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa udhibiti wa ubora wa samaki na viwango ambayo yatakuwa na sifa zifuatazo:- (a) hayatatakiwa kuwa na vumbi au kutu; na (b) yatatakiwa kuwa na milango iliyotengenezwa kwa kutumia vifaa vinavyo kubalika katika viwango vya ubora. 4 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kwenye Mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 182 (linaendelea) Makosa - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya shughuli au vitendo vilivyokatazwa vya uvuvi, mazingira, mauzo ya samaki, au kuzuia maafisa wa usimamizi.
12. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo- a. atafanya shughuli za uvuvi bila kibali maalum kutoka Halmashauri; b. atavua samaki kwa kutumia sumu, mabomu, kemikali au nyavu zisizoruhusiwa au kuvua samaki katika maeneo yasiyoruhusiwa; c. atavua samaki kwa kutumia mitego ya mtando (Ring nets) katika maeneo yenye maji madogo chini ya kina cha mita arobaini (40m); d. atachafua mazingira kwa kutupa takataka au kujisaidia katika maeneo ya fukwe, bandari au masoko; e. atavuna au kukata miti ya mikoko bila kibali maalum; f. atajisaidia baharini, mtoni na bwawani au kutotumia vyoo vilivyotengezwa katika maeneo ya makambi; g. atavua pweza chini ya uzito wa gramu 500; h. atafanya shughuli za uvuvi katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mazalia ya samaki na viumbe wengine wa baharini,mtoni na mabwawa; i. atauza au kukausha samaki katika maeneo machafu, au mchangani; j. atauza au kununua samaki katika maji au baharini au sehemu nyingine yeyote isiyotengwa kama soko la samaki; k. atamzuia Afisa yeyote wa Halmashauri, au mjumbe 5 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kwenye Mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 182 (linaendelea) wa BMU kutekeleza majukumu yake halali ya usimamizi. Adhabu Kufifilisha kosa
Part
sehemu nyingine yeyote isiyotengwa kama soko la
- 13 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye atakiuka masharti ya Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Anyone who violates these bylaws commits an offence and, if convicted, may be fined up to TZS 300,000, imprisoned for up to 12 months, or both.
13. Mtu yeyote ambaye atakiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au adhabu zote kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 14 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging a fine of at least 50,000 shillings if the offender admits the offence voluntarily and completes the specified form.
14. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza faini ya kiasi kisichopungua shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari yake mwenyewe na kujaza fomu maalum iliyoainishwa kwenye Jedwali la Sheria Ndogo hii. 6 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kwenye Mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 182 (linaendelea) _________ JEDWALI __________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 14) __________ KUFIFILISHA KOSA Mimi ………………………………………………wa S. L. P……………….………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya…………………………………………...ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kwamba tarehe……ya Mwezi…...Mwaka………nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha …………. cha Sheria Ndogo za Udhibiti na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi kwenye Mialo za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni za mwaka 2020. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri, niko tayari kulipa kiasi cha shilingi elfu hamsini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KWA KADIRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe……………. ya mwezi……………mwaka…………………… Jina…………………………….…………………………... Saini……………………........ Mbele ya: Jina…………………………….………………. Saini…………………………………….…........ Wadhifa………………………………………… Tarehe…………………………………………… 7 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kwenye Mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 182 (linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kilichofanyika tarehe 20 mwezi 12 mwaka 2018 na kushuhudiwa. Lakiri hiyo ikibandikwa mbele ya:- ………………………..………….. ARON T. KAGURUMJULI, Mkurugenzi wa Halmashauri Halmashauri ya Kinondoni L.S ………………………..………….. BENJAMINI K. SITTA, Mstahiki Meya wa Halmashauri Halmashauri ya Kinondoni NAKUBALI, Dodoma 8 Februari, 2020 ……….……..…………………….. SELEMANI SAID JAFO (MB.), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI KWENYE MIALO YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI YA MWAKA, 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in