SHERIA NDOGO ZA (AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI, 2020
This provision gives the title of the by-law: the Kinondoni Municipal Council Health and Environmental Sanitation By-law, 2020.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO ZA (AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI, 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the title of the by-law: the Kinondoni Municipal Council Health and Environmental Sanitation By-law, 2020. This bylaw applies throughout Kinondoni Municipal Council area. This section defines key terms used in the by-laws. House or business owners must keep the surrounding area clean, including grass, waste, undeveloped plots, and rainwater drainage channels. House owners must remove debris from nearby rainwater drains and keep the drain clean and strong at all times.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO ZA (AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI, 2020
Showing 54 of 54
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya (Afya na
AI-assisted research summary: This provision gives the title of the by-law: the Kinondoni Municipal Council Health and Environmental Sanitation By-law, 2020.
1. Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya (Afya na Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni za Mwaka, 2020. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout Kinondoni Municipal Council area.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. 1 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws.
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa pale itakapoelekezwa vinginevyo- “Ada” maana yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya huduma ya uzoaji taka na huduma za usafi; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “Chukizo” au “Kero” maana yake ni kitu chochote ambacho kimejengwa au kuwekwa katika hali ya uchafu na kinaweza kusababisha madhara kwa maisha ya binadamu, adha, mazalia ya wadudu na wanyama hatari au madhara kwenye chakula na vyanzo vya maji; “dampo” maana yake ni eneo maalum lililotengwa na Halmashauri kama eneo maalum mbali na makazi ya watu kwa ajili ya kutupa taka taka za aina yoyote; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa Kinondoni; “Huduma” maana yake ni pamoja na usafishaji, ukusanyaji, uondoshaji na usafirishaji wa taka; “Kaya” maana yake ni baba mama na watoto na ni pamoja na mtu anayeishi peke yake kwa kujitegemea, watu waishio pamoja, mpangaji katika nyumba ya makazi au biashara; “lundo la taka” maana yake ni pamoja na vifaa na zana chakavu, mabaki ya samani ambayo haihusishi mabaki ya vifaa vya ujenzi au wanyama waliokufa; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mmiliki” maana yake ni mmiliki wa nyumba ya makazi au biashara, taasisi, ofisi, nyumba ya biashara, mpangaji, 2 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Sura ya 191 wakala au mtu yeyote mwenye dhamana ya kuishi katika nyumba; “nyumba ya makazi” maana yake ni jengo lolote linalotumiwa kwa kuishi, na inajumuisha pia ardhi inayozunguka nyumba husika. “taka hatari” maana yake ni taka kama ilivyotafsiriwa chini ya kifungu cha 133 (5) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni aina zote za taka zinazozalishwa majumbani, kwenye taasisi, maeneo ya biashara na viwandani lakini hazihusishi maji taka au taka za kimiminika; “taka za majengo ya biashara” maana yake ni taka zote zinazozalishwa kutoka katika majengo ya biashara na viwanda pamoja na taka zitokanazo na utoaji wa huduma mbalimbali taka zinazozalishwa majumbani; lakini hazihusishi “Ukaguzi wa kiafya” maana yake ni ukaguzi utakaofanywa na Halmashauri au Afisa Mwidhiniwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria Ndogo hizi; “Wakala” maana yake ni Kampuni, Taasisi, Kikundi jamii (CBO) au mtu yeyote aliyeteuliwa na Halmashuri kwa ajili ya kutoa huduma ya kuzoa taka katika eneo au sehemu ya eneo la Halmashauri. 3 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) SEHEMU YA PILI USAFI WA MAZINGIRA Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Kila mkazi au mfanyabiashara anayemiliki nyumba au
AI-assisted research summary: House or business owners must keep the surrounding area clean, including grass, waste, undeveloped plots, and rainwater drainage channels.
4. Kila mkazi au mfanyabiashara anayemiliki nyumba au eneo la biashara atahakikisha kwamba anafanya usafi wa mazingira kuzunguka makazi au eneo lake kwa kuhakikisha kwamba- (a) majani yanayozunguka nyumba yake au eneo lake yanalimwa,yanakatwa katika eneo kuanzia mwanzo wa mipaka ya barabara ya mbele ya nyumba yake au eneo lake lote; (b) takataka ngumu zote ikiwa ni pamoja na mifuko ya plastiki zitakusanywa, kuhifadhiwa na kupelekwa katika eneo lililoruhusiwa na Halmashauri; (c) takataka laini zote ambazo zinaweza kuoza zitachimbiwa shimo la taka na kutupwa humo; na (d) nyumba au kiwanja au eneo lolote ambalo halijaendelezwa kuhakikisha linafanyiwa usafi katika eneo hilo mara kwa mara. Usafi wa mifereji ya maji ya mvua. - 5 Verify source ↗
Mmiliki wa nyumba ataondoa uchafu kama vile
AI-assisted research summary: House owners must remove debris from nearby rainwater drains and keep the drain clean and strong at all times.
5. Mmiliki wa nyumba ataondoa uchafu kama vile mchanga, majani, nyasi au vitu vingine vinavyofanana na hivyo kwenye mfereji wa maji ya mvua unaozunguka au kupita kando ya nyumba yake au eneo la biashara yake, kiwanja chake na kuhakikisha mfereji huo unakuwa msafi na imara siku zote. Uwekaji taa za nje ya nyumba - 6 Verify source ↗
Mmiliki wa nyumba, mpangaji au mfanyabiashara
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba, mpangaji au mfanyabiashara lazima aweke taa zenye mwanga nje ya jengo analotumia na aziwashi wakati wa usiku.
6. Mmiliki wa nyumba, mpangaji au mfanyabiashara ataweka taa zenye mwanga nje ya jengo analoishi au analolitumia kwa shughuli yoyote na atatakiwa kuiwasha wakati wa usiku. Kupaka rangi majengo - 7 Verify source ↗
Mmiliki wa nyumba au mpangaji au mfanyabiashara
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba, mpangaji, au mfanyabiashara lazima apake rangi nyumba yake au majengo anayoyatumia kila yanapochakaa.
7. Mmiliki wa nyumba au mpangaji au mfanyabiashara atahakikisha kwamba anapaka rangi nyumba yake au majengo yote anayoyatumia kila itakapochakaa. 4 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Wajibu wa kuondoa na kudhibiti mazalia ya mbu. - 8 Verify source ↗
Mmiliki wa jengo au mtumiaji wa jengo atahakikisha
AI-assisted research summary: Mmiliki au mtumiaji wa jengo lazima ahakikishe hakuna maji, maji machafu, takataka, au vitu vingine vinavyoweza kuzalisha mazalia ya mbu au wadudu hatari.
8. Mmiliki wa jengo au mtumiaji wa jengo atahakikisha kuwa hakuna mkusanyiko wa maji, maji machafu, takataka au kitu chochote cha majimaji au kigumu ambacho kinaweza kuruhusu kuwepo mazalia ya mbu au wadudu wengine wenye madhara kwa afya ya binadamu. Biashara ya miwa na matunda - 9 Verify source ↗
Mfanyabiashara ya matunda, mboga mboga au miwa,
AI-assisted research summary: Traders of fruits, vegetables, sugarcane, or any product must keep a special container for storing fruit peels or waste.
9. Mfanyabiashara ya matunda, mboga mboga au miwa, au bidhaa yeyote atahakikisha kuwa ana chombo maalumu cha kuhifadhia maganda au mabaki ya matunda. Kupuliza dawa Matengenezo ya magari, pikipiki, mitambo na kuegesha magari mabovu - 10 Verify source ↗
Mtu yeyote haruhusiwi kuendesha biashara ya
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuendesha biashara ya kupuliza dawa au kuuwa wadudu/wanyama waharibifu katika nyumba au mahali popote bila kibali kinachotambuliwa na Serikali na leseni hai kutoka Halmashauri.
10. Mtu yeyote haruhusiwi kuendesha biashara ya kupuliza dawa au biashara ya kuuwa wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila kuwa na kibali kinachotambuliwa na Serikali na awe na leseni hai kutoka Halmashauri. - 11 Verify source ↗
(1) Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo
AI-assisted research summary: Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yanapaswa kufanyika kwenye karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri; mtu yeyote haruhusiwi kutengeneza au kuegesha magari mabovu katika maeneo yaliyopigwa marufuku.
11.-(1) Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yatatakiwa kufanyika kwenye karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. (2) Mtu yeyote haruhusiwi kutengeneza gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo. (3) Mtu yeyote haruhusiwi kuegesha magari mabovu kwenye njia ya miguu, mtaa, uchochoro, mtaro, maeneo ya wazi au barabarani na kusababisha adha kwa wakazi au watumiaji wa njia hiyo. SEHEMU YA TATU UIMARISHAJI WA AFYA Usalama wa maji ya kunywa.
Part
SEHEMU YA TATU
- 12 Verify source ↗
Mkazi yeyote atahakikisha kwamba maji yote
AI-assisted research summary: Kila mkazi lazima ahakikishe maji ya kunywa ni safi na salama kwa kuyachemsha, bila kujali chanzo chake.
12. Mkazi yeyote atahakikisha kwamba maji yote yanayotumika kunywa ni safi na salama kwa kuyachemsha bila kujali yametoka kwenye chanzo gani cha maji. Kutengeneza na kuuza vyakula. - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote haruhusiwi kutengeneza, kuchoma,
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutengeneza, kupika, kuchemsha, kuchoma au kuuza chakula bila kwanza kutimiza masharti ya afya na kupata kibali kutoka kwa Halmashauri au Afisa Mwidhiniwa.
13. Mtu yeyote haruhusiwi kutengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote mahali popote au kwenye nyumba yoyote mpaka awe ametimiza masharti na kanuni za afya na amepata kibali kutoka kwa Halmashauri au kwa Afisa Mwidhiniwa. 5 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Uuzaji vyakula vilivyopikwa. - 14 Verify source ↗
Mtu yeyote anayeendesha biashara ya vyakula vya
AI-assisted research summary: An operator of cooked or fried food businesses must store the food in a clean wooden box covered with glass.
14. Mtu yeyote anayeendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa atahakikisha kwamba vyakula hivyo vinahifadhiwa kwenye sanduku lililotengenezwa kwa mbao safi na kuwekwa kioo kuzuia inzi, vumbi na wadudu waletao madhara kwa afya ya binadamu. Usalama wa vyakula. Uzuiaji wa shughuli mbalimbali wakati wa magonjwa ya mlipuko Ukamataji wa vyombo vilivyotumika kuhifadhia chakula - 15 Verify source ↗
Mtu yeyote haruhusiwi kuuza vyakula visivyopikwa
AI-assisted research summary: Any person must not sell uncooked food while it is placed on the ground, and food must be placed on a table.
15. Mtu yeyote haruhusiwi kuuza vyakula visivyopikwa vikiwa vimewekwa chini, vyakula vyote vitatakiwa kuwekwa juu ya meza. - 16 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa anaweza kutoa amri ya kuzuia
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuzuia shughuli fulani, ikiwemo utengenezaji wa vyakula, pombe, mijumuiko, sherehe na mikusanyiko, ikiwa ana sababu ya kuamini shughuli hiyo inaweza kueneza magonjwa ya mlipuko na kuathiri maisha ya binadamu.
16. Afisa Mwidhiniwa anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli yoyote isifanyike kama vile utengenezaji wa vyakula, pombe, mijumuiko, sherehe na mikusanyiko yoyote kwa kutangaza kwa njia ya kipaza sauti, maandishi au kupitia vyombo vya habari endapo atakuwa na sababu ya kuamini kwamba shughuli hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuleta athari kwa maisha ya binadamu. - 17 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kukamata
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kukamata vyakula, vyombo au vifaa vinavyotumika baada ya amri ya kuzuia uuzaji wa vyakula wakati wa magonjwa ya mlipuko.
17.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kukamata vyakula, vyombo au vifaa vingine vyovyote vitakavyokuwa vinatumika mara baada ya kutolewa amri ya zuio la kutofanyika kwa shughuli ya uuzaji wa vyakula wakati wa magonjwa ya mlipuko. (2) Endapo vyakula vitakavyokamatwa vitakuwa ni vile ambavyo vinaharibika kwa haraka Halmashauri itaharibu vyakula hivyo. (3) Endapo vyakula vitakavyokamatwa vitakuwa haviharibiki kwa haraka Halmashauri itakuwa na jukumu la kuvihifadhi hadi mwisho wa amri ya zuio na Halmashauri haitahusika na gharama zozote zitakazotokea isipokuwa kama uharibifu huo utakuwa umesababishwa kwa uzembe wa Halmashauri au Afisa wa Halmashauri. Maduka ya nyama - 18 Verify source ↗
(1) Mmiliki yeyote wa duka la kuuzia nyama
AI-assisted research summary: Butcher shop owners must keep the shop in the specified hygienic condition, and meat sellers must wear white clothing and be medically examined every six months.
18.-(1) Mmiliki yeyote wa duka la kuuzia nyama atahakikisha kwamba duka lake- (a) ni jengo la kudumu lililosakafiwa kwa marumaru nyeupe hadi urefu wa mita 6 kutoka usawa wa sakafu; (b) lina maji safi, na misumeno ya kukatia nyama; (c) lina milango ya vioo na jokofu la kuhifadhia nyama 6 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Kuchinja na kuuza nyama mahali pasiporuhusiwa Uendeshaji wa biashara ya Nyumba za kulala wageni na Hosteli Mahitaji ya nyumba za wageni, migahawa na hosteli na sehemu za mizani; na (d) lina pipa la kuhifadhia taka taka. (2) Muuzaji yeyote wa nyama atatakiwa kuvaa vazi jeupe pamoja na aproni nyeupe,viatu vya kufunika na sharti awe anapimwa afya kila baada ya miezi sita. - 19 Verify source ↗
Mtu yeyote haruhusiwi kuchinja au kuuza nyama ya
AI-assisted research summary: Anyone must not slaughter or sell any meat except in slaughterhouses, butcher shops, or places permitted by the Council.
19. Mtu yeyote haruhusiwi kuchinja au kuuza nyama ya aina yoyote katika maeneo yasiyokuwa machinjio au maduka ya nyama au katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri. - 20 Verify source ↗
(1) Mmiliki wa nyumba za kulala wageni, hosteli au
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba za kulala wageni, hosteli au nyumba za biashara lazima apate kibali cha Halmashauri kabla ya kuanza biashara.
20.-(1) Mmiliki wa nyumba za kulala wageni, hosteli au nyumba za biashara atahakikisha anapata kibali kutoka Halmashauri kabla ya kuanza biashara. (2) Endapo mmiliki hajakidhi masharti ya kiafya Halmashauri inaweza kuzuia kibali cha kuendesha biashara ya nyumba za kulala wageni, hosteli, au nyumba za biashara mpaka hapo mmiliki atakapokuwa amekidhi masharti yaliyotolewa na Halmashauri. - 21 Verify source ↗
Kibali cha kuendesha biashara ya nyumba ya kulala
AI-assisted research summary: Halmashauri itatoa kibali cha kuendesha nyumba ya kulala wageni, mgahawa au hosteli baada ya kujiridhisha kuwa majengo yanakidhi masharti fulani ya usalama, usafi na vifaa.
21. Kibali cha kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni, mgahawa na hosteli kitatolewa baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa katika majengo hayo kuna- (a) mwanga na hewa ya kutosha; (b) nafasi na vifaa (samani ) za kutosha; (c) mfumo wa uondoshaji wa maji taka na taka ngumu wa kuaminika; (d) usafi wa jumla wa jengo na vifaa vyake; (e) vyoo na mabafu kwa jinsia zote na watu wenye ulemavu; (f) vifaa vya zima moto; (g) tanki la kuhifadhia maji safi; na (h) vyoo na bafu vilivyosakafiwa kwa marumaru na kuta zake zimewekwa marumaru kiasi cha mita sita kutoka usawa wa sakafu. Upimaji wa afya - 22 Verify source ↗
(1) Mmiliki wa hoteli, mgahawa, baa, duka la nyama,
AI-assisted research summary: Wamiliki wa baadhi ya biashara za chakula na malazi lazima wahakikishe wafanyakazi wao wote wanapimwa afya kila baada ya miezi sita na kulipa ada ya Tsh 5,000; watengenezaji wa chakula kwa ajili ya kuuza pia lazima wapimwe afya na kulipa ada hiyo hiyo.
22.-(1) Mmiliki wa hoteli, mgahawa, baa, duka la nyama, sehemu za kuokea mikate, nyumba za kulala wageni na duka la pombe atahakikisha kuwa wafanyakazi wake wote 7 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) wamepimwa afya kila baada ya miezi sita na watalipa ada ya upimaji wa afya kiasi cha shilingi elfu tano (Tsh.5,000/=). (2) Mtu yeyote anayetengeneza chakula kwa ajili ya kuuza atalazimika kupimwa afya kila baada ya miezi sita na atalipa ada ya upimaji wa afya kiasi cha shilingi elfu tano (Tsh.5,000/=). (3) Mmiliki yeyote atakayeruhusu mtoa huduma yeyote kufanya kazi bila kupimwa afya yake kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1), atakuwa ametenda kosa. Uwezo wa kukagua
Part
sehemu za kuokea mikate, nyumba za kulala wageni na duka
- 23 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia
AI-assisted research summary: A health officer may enter any building at any time to inspect compliance with this bylaw.
23. Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika jengo lolote wakati wowote kukagua utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Kufungwa kwa jengo la biashara lisilokidhi masharti ya afya Ada ya ukaguzi wa afya - 24 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuagiza
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kuamuru kufungwa kwa biashara iliyo katika ukiukaji au ambayo haijakaguliwa, kwa mujibu wa masharti ya Sheria Ndogo hii.
24. Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuagiza ambalo limekiuka kufungwa kwa biashara yoyote halijakaguliwa au masharti ya Sheria Ndogo hii. lililokaguliwa na kukutwa jengo au - 25 Verify source ↗
Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya ambayo
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge an annual health inspection fee before an applicant is given a business license.
25. Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya ambayo italipwa kwa mwaka kabla ya mwombaji kupewa leseni ya biashara kama vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. vitakuwa viwango ambayo vyake Muda wa kulipa ada - 26 Verify source ↗
(1) Ada ya ukaguzi wa afya italipwa kila mwanzo wa
AI-assisted research summary: Ada ya ukaguzi wa afya hulipwa mwanzoni mwa mwaka wa fedha wa Halmashauri, yaani mwezi Julai.
26.-(1) Ada ya ukaguzi wa afya italipwa kila mwanzo wa mwaka wa fedha wa Halmashauri yaani mwezi Julai. (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kulipa ada katika kipindi cha miezi miwili baada ya mwaka wa fedha kuanza atawajibika kulipa kiwango hicho pamoja na adhabu ya asilimia hamsini ya kiwango atakachokuwa anadaiwa. 8 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) SEHEMU YA NNE UZOAJI TAKA Ada ya uzoaji taka
Part
SEHEMU YA NNE
- 27 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kutoka kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ichukue ada ya uzoaji taka kutoka kwa kila kaya au jengo la biashara, na ada ya kila mwezi italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa mwishoni mwa mwezi husika.
27.-(1) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kutoka kwa kila kaya au jengo la biashara kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. (2) Ada ya kila mwezi italipwa kila mwisho wa mwezi ndani ya mwezi husika na italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa ambaye atatoa stakabadhi ya malipo atakayolipwa na atajaza katika rejista ya wazalishaji taka. (3) Iwapo mzalishaji wa taka atashindwa kulipia gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo Halmashauri itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. Uanzishwaji wa Vikundi Jamii (CBOs) - 28 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhamasisha
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ihamasishe uundaji na utambuzi wa Vikundi Jamii ili viweze kushughulikia udhibiti wa taka ngumu na usafi wa mazingira, baada ya kuingia mkataba na Halmashauri.
28. Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhamasisha uundaji wa Vikundi Jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Wajibu wa kuwa na pipa la taka - 29 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa nyumba au
AI-assisted research summary: House owners, tenants, and businesspeople must keep solid waste in a strong covered container before the Council collects it for disposal.
29. Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa nyumba au mpangaji au mfanyabiashara kuhakikisha kuwa ana chombo imara chenye mfuniko kwa ajili ya kuhifadhia taka ngumu kabla hazijachukuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kwenda kutupwa. Kutupa taka katika sehemu maalum - 30 Verify source ↗
Mkazi yeyote atahakikisha kwamba anatupa uchafu au
AI-assisted research summary: Any resident must put waste into special containers in designated places, and is prohibited from throwing waste carelessly.
30. Mkazi yeyote atahakikisha kwamba anatupa uchafu au taka katika vyombo maalum vilivyowekwa kwa ajili ya kutunzia taka katika maeneo maalum yaliyotengwa. Marufuku kutupa taka hovyo Uhifadhi maji taka Kutiririsha maji taka - 31 Verify source ↗
Mtu yeyote haruhusiwi kutupa taka, uchafu wowote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutupa taka au uchafu mahali popote isipokuwa maeneo yaliyotengwa kwa shughuli hiyo.
31. Mtu yeyote haruhusiwi kutupa taka, uchafu wowote takataka mahali popote ambapo au kuacha kuwepo hapajatengwa kwa shughuli hiyo. - 32 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba anatakiwa kuhakikisha kuwa
AI-assisted research summary: Kila mmiliki wa nyumba lazima ahakikishe ana karo la kuhifadhi maji taka na ayatoe maji taka tanki likijaa.
32. Kila mmiliki wa nyumba anatakiwa kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhi maji taka na atawajibika kunyonya maji taka pale karo linapojaa. - 33 Verify source ↗
Mtu yeyote haruhusiwi kutiririsha au kuelekeza maji
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutiririsha au kuelekeza maji kutoka maeneo ya vyoo, bafu, au baada ya kufua na kuosha vyombo kwenda sehemu isiyotengwa kuhifadhi maji taka.
33. Mtu yeyote haruhusiwi kutiririsha au kuelekeza maji 9 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) kutoka vyooni, bafuni, karoni, baada ya kufua au kuosha vyombo kwenda sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhi maji taka. Taka za viwanda - 34 Verify source ↗
(1) Kiwanda chochote hakiruhusiwi kutoa au
AI-assisted research summary: Kiwanda hakipaswi kutoa uchafu, maji machafu, au harufu mbaya inayosababisha kero kwa wakazi; mmiliki wa kiwanda lazima ahakikishe takataka na moshi vinavyoweza kuleta kero havimfikii mtu wala kusababisha madhara.
34.-(1) Kiwanda chochote hakiruhusiwi kutoa au kusababisha kutoa uchafu wa aina yoyote, maji machafu au harufu mbaya na kusababisha kero kwa wakazi wa eneo la Halmashauri. (2) Mmiliki wa kiwanda atahakikisha kuwa taka kama vile vumbi, maganda, moshi na takataka nyingine zinazoweza kuleta kero au adha kwa ujumla haziwafikii wala hazileti madhara kwa binadamu na viumbe hai wengine. - 35 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuteua Kampuni, kikundi,
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua kampuni, kikundi, kikundi cha jamii au mtu binafsi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii.
35. Halmashauri inaweza kuteua Kampuni, kikundi, kikundi cha jamii au mtu binafsi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Uteuzi wa Wakala SEHEMU YA TANO UJENZI NA MATUMIZI YA VYOO Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia
Part
SEHEMU YA TANO
- 36 Verify source ↗
Mmiliki wa nyumba au mpangaji atahakikisha
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba au mpangaji lazima ahakikishe nyumba ina choo safi, imara na kinachotumika kwa wakati wote.
36. Mmiliki wa nyumba au mpangaji atahakikisha kwamba nyumba yake ina choo safi, imara na madhubuti kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo na kuhakikisha kinatumika wakati wote. Umbali wa kujenga choo Vyoo vya umma - 37 Verify source ↗
Choo kinatakiwa kijengwe umbali wa zaidi ya mita
AI-assisted research summary: Toileti ijengwe zaidi ya mita 60 kutoka chanzo chochote cha maji.
37. Choo kinatakiwa kijengwe umbali wa zaidi ya mita sitini (60) kutoka chanzo chochote cha maji. - 38 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kumruhusu mtu binafsi,
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuruhusu watu binafsi, vikundi au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo inayoona yanahitajika.
38.-(1) Halmashauri inaweza kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo ambayo Halmashauri itaona kuwa kuna haja ya kufanya hivyo. (2) Mtu binafsi, kikundi au taasisi ambaye amejenga choo cha umma katika eneo lake binafsi atalipia ushuru wa kuendesha biashara hiyo kulingana na mwongozo au makubaliano au mkataba kati yake na Halmashauri. (3) Vyoo hivyo vitamilikiwa na Halmashauri au kwa ubia na wajenzi na vitakuwa ni vya kulipia kama itakavyokuwa imeelekezwa na Halmashauri katika mkataba wake na 10 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) mawakala watakaopewa kusimamia vyoo hivyo. Vyoo vya muda katika mikusanyiko - 39 Verify source ↗
Mtu, kikundi au taasisi yenye lengo la kukutanisha
AI-assisted research summary: Mtu, kikundi, au taasisi inayokusanya watu kwa ujenzi, sherehe, au mkusanyiko wa muda mfupi lazima ijenge vyoo vya muda ikiwa eneo hilo halina choo cha kudumu, chini ya idhini na usimamizi wa Halmashauri.
39. Mtu, kikundi au taasisi yenye lengo la kukutanisha watu kwa madhumuni ya ujenzi, sherehe au sehemu yoyote ambayo itakutanisha watu kwa muda maalum na endapo eneo hilo hakuna choo cha kudumu, atatakiwa kujenga vyoo kwa matumizi ya wakati huo kwa idhini na usimamizi wa Halmashauri. Vyoo katika majengo ya biashara - 40 Verify source ↗
Kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa kujenga
AI-assisted research summary: Mmiliki wa jengo la biashara lazima ajenge vyoo 2 au 3 vinavyokubalika kwa matumizi ya wateja wa jinsia zote na watu wenye ulemavu.
40. Kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa kujenga vyoo viwili au vitatu vyenye viwango vinavyokubalika chini ya Sheria Ndogo hii kwa ajili ya matumizi ya wateja wake wa jinsia zote pamoja na watu wenye ulemavu. Ilani ya kujenga choo - 43 Verify source ↗
Section 43
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa must issue notice when a house lacks a toilet, has a full toilet, or has a toilet unfit for human use, and the council may stop the house or building from being used until the problem is fixed.
43.- Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo, choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu, Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani ya siku thelathini (30) kwa mmiliki wa nyumba au mpangaji akiainisha masharti ya kurekebisha hali hiyo kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii. Bila kuathiri masharti ya kifungu cha 41 Halmashauri inaweza kuamuru nyumba au jengo hilo lisitumike kwa shughuli za makazi au biashara hadi hapo hali hiyo itakaporekebishwa. (1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa ilani ya (7) kwa mmiliki wa nyumba, siku saba mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote anayehusika akimtaka kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne la Sheria Ndogo hii. kuondoa hiyo kero (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani aliyopewa ndani ya muda ulioainishwa kwenye ilani atakuwa ametenda kosa. Halmashauri kuteua mkaguzi - 44 Verify source ↗
Section 44
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua mtu yeyote kuwa mkaguzi kwa ajili ya ukaguzi wa usafi.
44. Halmashauri inaweza kumteua mtu yeyote kuwa mkaguzi kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa usafi 11 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Mamlaka ya kutoa adhabu ya papo kwa papo - 45 Verify source ↗
Section 45
AI-assisted research summary: Mkaguzi ana mamlaka ya kutoa adhabu ya papo kwa papo kwa mtu anayekutwa akichafua mazingira kwa kutupa takataka mahali palipokatazwa, ndani ya eneo la Halmashauri na kwa kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii.
45. katika eneo la Halmashauri. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii, Mkaguzi atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu ya papo kwa papo kwa mtu yeyote atakayekutwa amechafua mazingira kwa kutupa takataka mahali popote pasiporuhusiwa ilimradi kuwa adhabu hiyo izingatie masharti ya Sheria Ndogo hii. Makosa - 46 Verify source ↗
Section 46
AI-assisted research summary: This section makes it an offence for any person to obstruct an Authorized Officer or to carry out listed unsanitary acts such as dumping waste, discharging dirty water, washing vehicles in water sources, opening workshops in residential areas, or storing food improperly.
46. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atamzuia au kujaribu kumzuia Afisa Mwidhiniwa asitekeleze wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii; (b) atamshawishi mtu au kundi la watu kumzuia Afisa Mwidhiniwa asitekeleze wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii; (c) atamwaga takataka barabarani, kwenye mtaro wa maji ya mvua, uchochoroni, au mahali popote hadharani au katika eneo lolote lisiloruhusiwa; (d) ataendesha biashara ya pombe ndani ya nyumba ya makazi; (e) atatiririsha maji machafu barabarani au katika eneo la nyumba ya jirani; (f) ataosha magari, kufua, kunywesha mifugo na kukoroga dawa za mimea ndani ya mito, mabwawa, lambo au kisima chanzo ndani kinachotumika ya binadamu; kwa matumizi au ya (g) atafanya matengenezo na mitambo, ya magari, pikipiki kuendesha shughuli za viwanda katika maeneo ya wazi, makazi, barabarani, uchochoroni, au katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli hizo bila kuzingatia taratibu za 12 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) mipango miji; (h) ataanzisha au kufungua karakana katika majengo au majumba au maeneo ya makazi; (i) ataenda haja ndogo au kubwa hovyo barabarani, uchochoroni, upenuni au mahali popote ambapo siyo chooni; au (j) atashindwa kuhifadhi chakula kwenye kabati safi lililofunikwa na lenye kioo. Adhabu - 49 Verify source ↗
Section 49
AI-assisted research summary: Anyone who breaches these by-laws commits an offence and may be fined up to Tsh 300,000 or imprisoned for up to 12 months, or both.
49. Tangazo la Serikali namba 202 la mwaka, 2002 Tangazo la Serikali namba 353 la mwaka, 2001 atakuwa Mtu yeyote ambaye atakiuka masharti ya Sheria Ndogo hii ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi (300,000/-) au kifungo shilingi kisichozidi miezi kumi na mbili (12) au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. laki tatu Sheria Ndogo hii inafuta Sheria ndogo ya (Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni za Mwaka, 2002. Sheria Ndogo hii inafuta Sheria Ndogo ya Sheria Ndogo ya Ada ya Usimamizi na Uchukuaji Taka ya Halmashauri ya Manispaa Kinondoni ya Mwaka 2000 (The Kinondoni Municipal Council (Waste Management and Refuse Collection Fees By-Laws) pamoja na marekebisho yake yote za Mwaka, 2000. 13 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) __________ JEDWALI LA KWANZA __________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 25) __________ Ada ya Ukaguzi wa Afya Na. Aina ya biashara Ada kwa mwaka Tsh.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Maduka ya pombe ya jumla na rejareja
AI-assisted research summary: This provision mentions wholesale and retail liquor shops and an amount of 5,000/=.
1. Maduka ya pombe ya jumla na rejareja 5,000/= - 3 Verify source ↗
Nyumba za wageni (Guest House) na Hoteli
AI-assisted research summary: The provision mentions guest houses and hotels and lists an amount of 10,000/=.
3. Nyumba za wageni (Guest House) na Hoteli 10,000/= - 4 Verify source ↗
Kumbi za starehe au mikutano
AI-assisted research summary: The text names “Kumbi za starehe au mikutano” and states 10,000/=.
4. Kumbi za starehe au mikutano 10,000/= - 5 Verify source ↗
Majengo mengine ya biashara
AI-assisted research summary: This schedule sets a Tshs 5,000 fee for “majengo mengine ya biashara” (other business premises).
5. Majengo mengine ya biashara 5,000/= 14 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Na 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 ________________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 27(1)) _______________ Ada ya Uzoaji Taka Aina ya jengo Kiwango kwa Tshs (a) Eneo la makazi (kaya) (kwa mwezi) (b) Mabalozi (kila ubalozi) (kwa mwezi) (a) 3,000-30,000 (b) 500,000/= Mahali panapouzwa barafu ( kwa 50,000/= mwezi) Mgahawa (kwa mwezi) 5000-30,000/= Nyumba ya wageni ( kwa mwezi) Zahanati (kwa mwezi) Kituo cha afya (kwa mwezi) Maabara Kliniki (a) Taka ngumu za Viwandani (taka zisizohatarishi) (kwa tripu/safari moja) (b) Taka hatarishi za viwandani (kwa kila tani) Hospitali ( kwa mwezi) Maduka ya jumla ( kila mwezi) 30,000/= 20,000/= 50,000/= 30,000-50,000/= 30,000-50,000/= (a) 500,000/= (b) 200,000/= 300,000/= 30,000/= Maduka ya rejareja ( chakula na 10,000-20,000/= 25,000/= 30,000/= 40,000/= bidhaa nyingine) (kila mwezi) Shule ya binafsi ya kutwa (kila mwezi) Shule ya binafsi ya bweni (kila mwezi) 15 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 Taasisi (kwa mwezi) Kituo cha kutwa cha kutunzia watoto 14,000/= ( kila mwezi) Duka la jumla vyakula (kila mwezi) Duka la pombe (kila mwezi) Butcher (kila mwezi) Duka la dawa (kila mwezi) Soko ( kwa safari) 20,000/= 50,000/= 20,000/= 20,000/= 250,000/= Magenge ( kila mwezi) 5,000-20,000/= Mama lishe/ baba lishe ( kwa siku) Daladala – ushuru kwa mwezi Biashara ndogo ndogo. Sekta isiyo rasmi (kwa mwezi) Dobi kwa siku 5,000/= 30,000/= 2,000/= 2,000/= Fundi seremala (kwa mwezi) 5,000- 60,000/= Fundi viatu ( kwa mwezi) 2,000-10,000/= Supermarket ( kwa mwezi) 250,000/= Meza ndani ya soko – kwa mwezi Ada ya kutupa taka kizimbani – kwa mwezi Ada ya kutupa taka kutoka kwenye mkokoteni ndani ya kizimba – kwa mwezi Ukarabati wa vifaa vya umeme kama televisheni Fundi cherehani aliesajiliwa (kila mwezi) 4,000/= 4,000/= 4,000/= 6,000/= 5,000-20,000/= Saluni iliyosajiliwa (kila mwezi) 5,000-20,000/= 16 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Kituo cha Petrol (kila mwezi) Kituo cha mafuta ya taa (kila mwezi) 250,000/= 10,000/= Stoo ya Mkaa (kila safari) 20,000-250,000/= 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44
Part
JEDWALI LA PILI
- 45 Verify source ↗
Ofisi
AI-assisted research summary: Hii ni jedwali la ada/gharama mbalimbali kwa aina za ofisi, malazi, magari na idadi ya wafanyakazi.
45. Ofisi Ghala ( kila mwezi) Hoteli (kila mwezi) Nyumba ya wageni ( kila mwezi) Ada ya magari ya kubebea taka (kwa mwaka) Magari ya maji taka (kwa mwaka) Kijiko – wheel loader (kwa masaa 8) Kuzoa taka kwa trip moja Magari makubwa ya kushusha na kupakia abiria ndani ya soko Wafanyakazi 01-10 (kila mwezi) Wafanyakazi 11-20 (kila mwezi) Wafanyakazi 21-30 (kila mwezi) Wafanyakazi 31-50 (kila mwezi) Wafanyakazi 51-100 (kila mwezi) Wafanyakazi 101 na kuendelea (kila mwezi) 50,000/= 250,000/= 40,000/= 250,000/= 250,000/= 600,000/= 250,000/= 20,000/= 20,000/= 40,000/= 50,000/= 70,000/= 100,000/= 200,000/= 20,000/= 250,000/= 250,000/= - 49 Verify source ↗
Biashara ya kufyatua na kuuza tofali (kwa kila
AI-assisted research summary: This provision names brick-making and brick-selling business and mentions a monthly amount of 5,000–50,000/=.
49. Biashara ya kufyatua na kuuza tofali (kwa kila 5,000-50,000/= mwezi) - 51 Verify source ↗
Biashara za matunda (kwa kila siku)
AI-assisted research summary: Section 51 lists a daily charge for fruit businesses of 5,000–50,000/=.
51. Biashara za matunda (kwa kila siku) 5,000-50,000/= 17 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) - 52 Verify source ↗
Biashara ya mchanga, kokoto na kifusi
AI-assisted research summary: The section heading refers to sand, gravel, and rubble business and shows an amount range of 5,000–50,000/=.
52. Biashara ya mchanga, kokoto na kifusi 5,000-50,000/= __________ JEDWALI LA TATU __________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 41) __________ ILANI YA KUJENGA CHOO Ilani hii imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha (41) cha Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya mwaka, 2020. SEHEMU ‘A’ Ndugu…………………...............wa Mtaa/……………Kata ya………………… Unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika Tarehe……mwezi………..mwaka…. Katika nyumba yako ya Biashara/kuishi/kutolea Huduma*/ Namba………… iliyopo eneo la ………………katika Kitongoji/Mtaa*……….Kijiji cha……………Kata ya…………. Imekuwa haina choo/ choo kimejaa/kimeharibika* hivyo unaamriwa kutekeleza mambo yafuatayo; (1) ………………………………………………………………………………… (2) ………………………………………………………………………………… (3) ………………………………………………………………………………… (4) ………………………………………………………………………………… SEHEMU ‘B’ Unapewa muda wa siku thelathini (30) tu tangu siku ya kupokea ilani hii kutekeleza maelekezo yote yaliyoelezwa katika sehemu ‘A’ ya Ilani hii, SEHEMU ‘C’ Ukaguzi wa kuthibitisha utekelezaji wa maelekezo uliyopewa utafanyika tarehe……………….endepo utashindwa kutekeleza maelekezo ndani ya muda uliopewa Halmashauri itakuchukulia hatua kali za kisheria bila kukupa taarifa nyingine. ……………………………….. AFISA MWIDHINIWA IMETOLEWA NA; IMEPOKELEWA NA; Jina;……………………………….…. Jina;…………………………………. Saini………………………………… saini……………………………….... Wadhifa……………………...……... wadhifa…………………………….. Tarehe………………………..…….. Tarehe……………………………... *Futa lisilotakiwa. 18 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) __________ JEDWALI LA NNE __________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 43(1)) __________ ILANI YA KUONDOA KERO Ilani hii imetolewa kwa mujibu wa Kifungu cha (43)(1) cha Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya mwaka 2020. SEHEMU ‘A’ Ndugu…………………...............wa Mtaa/ ……………Kata ya………………… Unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika Tarehe……mwezi………..mwaka…. Katika ya Biashara/kuishi/kutolea Huduma/kiwanja* la………………………………………………………………………….kumekutwa machukizo/kero/uchafu*; kama ifuatavyo; nyumba yako iliyopo eneo 1) ……………………………………………………………………… 2) ……………………………………………………………………… 3) ……………………………………………………………………… 4) ……………………………………………………………………… SEHEMU ‘B’ Kwa ilani hii unaamriwa kurekebisha/kuondoa/kusafisha* kwa;
Part
JEDWALI LA NNE
- 4 Verify source ↗
………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: You must carry out everything listed in Section B within 7 days after receiving the notice.
4. ……………………………………………………………………… SEHEMU ‘C’ Unapewa muda wa siku saba (7) tangu siku ya kupokea ilani hii, unatakiwa kutekeleza yote yaliyoelezwa katika sehemu ‘B’ ya Ilani hii, kushindwa kwako kutekeleza ndani ya muda uliopewa Halmashauri italazimika kukuchukulia hatua kali za kisheria bila kulazimika kukupa taarifa nyingine. ………………………………….. AFISA MWIDHINIWA IMETOLEWA NA; IMEPOKELEWA NA; Jina;………………………. Jina;…………………………………. Saini……………………… saini……………………………….... Wadhifa…………………... wadhifa…………………………….. Tarehe…………………….. Tarehe……………………………... *Futa lisilohusika 19 Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo la Serikali Na. 183 (linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imebandikwa kwenye Sheria ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika kikao cha baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kilichofanyika tarehe 20 Desemba, 2018 na kushuhudiwa. Lakiri hiyo ilibandikwa mbele ya:- ………………………..………….. ARON T. KAGURUMJULI, Mkurugenzi wa Halmashauri Halmashauri ya Kinondoni L.S L.S ………………………..………….. BENJAMINI K. SITTA, Mstahiki Meya wa Halmashauri Halmashauri ya Kinondoni NAKUBALI, Dodoma 8 Februari, 2020 ……….……..…………… SELEMANI SAID JAFO (MB.), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 20
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO ZA (AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI, 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in