SHERIA NDOGO YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPIMBWE YA MWAKA, 2020
This provision states the short title of the by-law: the Mpimbwe District Council Health and Environment By-Law, 2020.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPIMBWE YA MWAKA, 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision states the short title of the by-law: the Mpimbwe District Council Health and Environment By-Law, 2020. Sehemu hii inaweka maana ya maneno muhimu yanayotumika katika Sheria Ndogo hii, kama Afisa Mwidhiniwa, chakula, Halmashauri, kaya, mkazi, Mkurugenzi, taka, taka ngumu na Wakala. Wamiliki na wakazi lazima waweke maeneo yao safi, waondoe uchafu kwenye mifereji iliyo karibu na nyumba au biashara, na washiriki kwenye usafi wa mazingira siku ya mwisho ya Jumamosi ya mwezi au siku nyingine itakayopangwa na Halmashauri. Owners of houses or business premises must put a lit light outside the building and turn it on at night. Mmiliki wa nyumba, kiwanja, au eneo la biashara lazima ahakikishe eneo lake halina maji yaliyotuama, maji machafu, taka, au vitu vingine vinavyoweza kuwa mazalia ya mbu au wadudu wengine hatari kwa afya ya binadamu.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPIMBWE YA MWAKA, 2020
Showing 25 of 25
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Afya na
AI-assisted research summary: This provision states the short title of the by-law: the Mpimbwe District Council Health and Environment By-Law, 2020.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Afya na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ya Mwaka, 2020. Tafsiri - 2 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaweka maana ya maneno muhimu yanayotumika katika Sheria Ndogo hii, kama Afisa Mwidhiniwa, chakula, Halmashauri, kaya, mkazi, Mkurugenzi, taka, taka ngumu na Wakala.
2. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo:- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa dawa, hii ni pamoja na- (a) kitu chochote kinachotumika katika matengenezo ya chakula; (b) kitu chochote kinachoongeza ladha ya chakula; au (c) kitu chochote kinachobadili rangi ya chakula. “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe; “kaya” maana yake ni familia inayojumuisha baba, mama, mtoto au watoto na mtu mwingine yeyote anayeishi na familia hiyo au watu wanaokaa katika nyumba moja na kuishi kama familia au mtu yeyote anayeishi peke yake katika chumba au nyumba; Sura 191 “maji taka” maana yake ni ile iliyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi katika eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au 1 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri au anafanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “taka” maana yake ni ile iliyoanishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni ile iliyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni, taasisi au shirika aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Sura ya 191 Sura ya 191 - 3 Verify source ↗
(1) Kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara
AI-assisted research summary: Wamiliki na wakazi lazima waweke maeneo yao safi, waondoe uchafu kwenye mifereji iliyo karibu na nyumba au biashara, na washiriki kwenye usafi wa mazingira siku ya mwisho ya Jumamosi ya mwezi au siku nyingine itakayopangwa na Halmashauri.
3.- (1) Kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba anafanya usafi wa mazingira yanayozunguka makazi au eneo lake hadi mwanzo wa mipaka ya barabara ya mbele ya nyumba yake. Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira (2) Kila mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuondoa uchafu kama vile mchanga, majani, nyasi au vitu vingine vinavyofanana na hivyo kwenye mifereji ya kupitisha maji inayozunguka au kupita kando ya nyumba, kiwanja au eneo la biashara yake. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), na (2), kila mkazi atakuwa na wajibu wa kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira katika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi au katika siku itakayopangwa na Halmashauri. (4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu hiki atakuwa ametenda kosa. - 4 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba au eneo la biashara atakuwa na
AI-assisted research summary: Owners of houses or business premises must put a lit light outside the building and turn it on at night.
4.-(1) Kila mmiliki wa nyumba au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuweka taa yenye mwanga nje ya jengo analoishi au analolitumia kwa shughuli za biashara na atatakiwa kuiwasha wakati wa usiku. Uwekaji taa za nje ya nyumba 2 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) (2) Mtu yeyote ambaye, bila sababu za msingi atakiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. Wajibu wa kuondoa na kudhibiti mazalia ya mbu - 5 Verify source ↗
(1) Mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara atakuwa na
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba, kiwanja, au eneo la biashara lazima ahakikishe eneo lake halina maji yaliyotuama, maji machafu, taka, au vitu vingine vinavyoweza kuwa mazalia ya mbu au wadudu wengine hatari kwa afya ya binadamu.
5.-(1) Mmiliki wa nyumba, kiwanja au eneo la biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa katika eneo lake hakuna mkusanyiko wa maji, maji machafu, takataka au kitu chochote cha majimaji au kigumu ambacho kinaweza kuruhusu kuwepo kwa mazalia ya mbu au wadudu wengine wenye madhara kwa afya ya binadamu. (2) Mtu yeyote ambaye bila sababu za msingi, atakiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa. Upulizaji dawa - 6 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayeendesha biashara ya kupuliza dawa ya
AI-assisted research summary: An operator of pesticide/pest-control spraying business in a council area must have a government-recognized professional certificate and a valid council licence, be supervised by a Health Officer during spraying, and issue a certificate signed by the Health Officer after spraying.
6.-(1) Mtu yeyote anayeendesha biashara ya kupuliza dawa ya kuuwa wadudu au wanyama waharibifu katika eneo la Halmashauri atatakiwa:- (a) kuwa na cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali na leseni hai kutoka Halmashauri; (b) kusimamiwa na Afisa Afya wakati wa kupuliza; na (c) kutoa cheti baada ya kupuliza dawa kilichosainiwa na Afisa afya. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1), atakuwa ametenda kosa. Matenge- nezo na maegesho ya magari, pikipiki na mitambo - 7 Verify source ↗
(1) Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yatatakiwa
AI-assisted research summary: Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yanapaswa kufanywa kwenye karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri; mtu yeyote haruhusiwi kutengeneza au kuegesha gari bovu katika maeneo yaliyopigwa marufuku, na ukiukaji ni kosa.
7.- (1) Matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yatatakiwa kufanyika kwenye karakana, gereji au maeneo yaliyoruhusiwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. (2) Mtu yeyote hataruhusiwa:- (a) kutengeneza gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo; au (b) kuegesha gari bovu kwenye njia ya miguu, mtaa, uchochoro, mtaro, maeneo ya wazi au barabarani. 3 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) U t e n g e - nezaji, na u u z a j i vyakula Machinjio na maduka ya nyama (3) Mtu yeyote atakayekiuka, bila sababu za msingi, masharti ya kifungu kidogo cha (2), atakuwa ametenda kosa. - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au
AI-assisted research summary: Mtu anayeshughulika na chakula katika eneo la Halmashauri lazima azingatie masharti ya afya na awe na kibali cha Afisa Afya wa Halmashauri.
8. Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa- (a) kutimiza masharti na kanuni za afya; na (b) kuwa na kibali kutoka kwa Afisa Afya wa Halmashauri. - 9 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuchinja mifugo nje ya machinjio, kuuza nyama nje ya maduka ya nyama au maeneo yasiyoruhusiwa, kuuza nyama ambayo haijakaguliwa, au kusafirisha nyama ya biashara kutoka machinjioni bila gari maalumu lililoidhinishwa. Wamiliki wa maduka ya nyama lazima waweke duka katika hali na vifaa vilivyoorodheshwa.
9.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa; (a) kuchinja mifugo katika maeneo yasiyokuwa machinjio; (b) kuuza nyama ya aina yoyote katika maeneo yasiyokuwa maduka ya nyama au katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (c) kuuza nyama isiyokaguliwa na mtaalamu wa mifugo au mtaalamu wa afya; na (d) kusafirisha nyama kwa madhumuni ya biashara toka machinjioni bila kutumia gari maalumu la kusafirishia nyama lililoidhinishwa na Halmashauri. (2) Kila mmiliki wa duka la kuuza nyama atatakiwa kuhakikisha yafuatayo:- (a) duka lake ni jengo la kudumu lililosakafiwa kwa marumaru nyeupe hadi urefu wa futi sita kutoka usawa wa sakafu; (b) duka lake lina maji safi, misumeno ya kukatia nyama na vyuma vya kutundikia nyama; (c) duka lake lina kabati la vioo na jokofu la kuhifadhia nyama na mizani ya kupimia nyama;(d) duka lake lina pipa au kifaa cha kuhifadhia takataka; (e) muuzaji ana vazi jeupe pamoja na aproni nyeupe na kofia nyeupe; (f) muuzaji anapima afya kila baada ya miezi sita; na(g) duka lake lina karo la maji machafu. 4 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) Uendeshaji wa biashara ya hoteli na hosteli (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) na (2), atakuwa ametenda kosa. - 10 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni, hosteli, shule,
AI-assisted research summary: Before starting business, owners of the listed premises must have the building inspected by a Health Officer and obtain a council permit.
10.-(1) Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni, hosteli, shule, kituo cha kutolea huduma za afya au nyumba ya biashara kabla ya kuanza biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha- (a) jengo lake limekaguliwa na Afisa Afya; na (b) amepata kibali cha Halmashauri cha kufanya shughuli husika. (2) Kibali cha kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni, hosteli, shule, kituo cha kutolea huduma za afya au nyumba ya biashara kitatolewa baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa mahitaji yafuatayo yamezingatiwa:- (a) jengo lina mwanga na hewa ya kutosha; (b) jengo lina nafasi na vifaa vya kutosha; (c) jengo kwa imara; (d) jengo lina mfumo imara wa uondoshaji wa maji taka, miminika na taka ngumu; (e) usafi wa jumla wa jengo na vifaa vyake; (f) jengo lina vyoo na mabafu ya kutosha kwa jinsia zote; (g) jengo lina vifaa vya kuzimia moto; (h) tanki la kuhifadhia maji safi; (i) vyoo na bafu vimesakafiwa kwa vigae au marumaru na kuta zake zimewekwa vigae kiasi cha futi sita toka usawa wa sakafu; na (j) kwa nyumba za kulala wageni na hosteli, uwepo wa vyandarua. (3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu cha (1), atakuwa ametenda kosa. (4) Bila kuathiri masharti ya kifungu cha (3), wakati wowote Halmashauri ikijiridhisha kuwa mmiliki hajakidhi masharti ya afya inaweza kuzuia utoaji wa huduma husika mpaka hapo mmiliki atakapokuwa amekidhi masharti ya kiafya yaliyotolewa na Halmashauri. 5 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) - 11 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa hoteli, mgahawa, baa, bucha, sehemu za
AI-assisted research summary: Wamiliki wa hoteli, migahawa, baa, bucha, sehemu za kuokea mikate, nyumba za kulala wageni, grosari, na watengenezaji wa chakula kwa ajili ya kuuza lazima wahakikishe wahudumu wao wanapimwa afya kila baada ya miezi sita.
11.-(1) Kila mmiliki wa hoteli, mgahawa, baa, bucha, sehemu za kuokea mikate, nyumba ya kulala wageni na grosari au mtu yeyote anayetengeneza chakula kwa ajili ya kuuza atatakiwa kuhakikisha mhudumu wake amepima afya kila baada ya miezi sita. Upimaji wa afya (2) Mmiliki yeyote atakayebainika kuruhusu mhudumu kufanya kazi bila kupimwa afya yake atatakiwa kulipa faini ya kiasi cha shilingi elfu hamsini na kuhakikisha mhudumu huyo anapimwa afya. (3) Ada ya upimaji wa afya itakuwa shilingi elfu sita. - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya kabla ya kutoa
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge a health inspection fee before issuing or renewing a business license.
12.-(1) Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya kabla ya kutoa au kuhuisha leseni ya biashara. (2) Viwango vya ada ya ukaguzi wa afya vitakuwa kama vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. - 13 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must set aside a waste dumping area, provide special waste bins, and collect waste for a fee; anyone who dumps or leaves waste in places not designated for that purpose commits an offence.
13.(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa:- (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupia taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. (2) Mtu yeyote atakayetupa taka au uchafu wowote au kuacha takataka au uchafu kwenye nyumba, uchochoro, kiwanja, mfereji wa maji ya mvua, barabara au mahali popote pasipotengwa kwa shughuli hiyo atakuwa ametenda kosa. U kagu z i wa afya Eneo la k u t u p a taka - 14 Verify source ↗
Halmashauri itahamasisha uundaji wa Vikundi Jamii na
AI-assisted research summary: Halmashauri must encourage and recognize community groups so they can be enabled to carry out solid waste control and environmental cleanliness activities in streets, after contracting with Halmashauri.
14. Halmashauri itahamasisha uundaji wa Vikundi Jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Vikundi vya wazoa taka - 15 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa gari la abiria litakaloingia katika eneo la
AI-assisted research summary: Vehicle owners entering the council area must have a waste container and make sure passengers put litter in it.
15.-(1) Kila mmiliki wa gari la abiria litakaloingia katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhi taka na kuhakikisha kwamba kila abiria anatupa taka kwenye chombo hicho. Magari ya abiria kuwa na 6 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) vyombo vya kuhifadhia takataka Uhifadhi maji taka (2) Endapo abiria atatupa takataka nje ya chombo cha usafiri, mmiliki au dereva au kondakta atawajibika kulipa kiasi cha shilingi elfu hamsini chini ya utaratibu wa kufifilisha kosa au kushtakiwa mahakamani. - 16 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara
AI-assisted research summary: Owners of houses, factories, or business premises must keep wastewater storage facilities, empty them when full, and must not discharge wastewater into roads, rivers, water sources, open areas, storm drains, or other unapproved places.
16.-(1) Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa analo karo la kuhifadhi maji taka; (b) kunyonya maji taka pale karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhia maji taka. (2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1), atakuwa ametenda kosa. Ada ya u t o z a j i taka - 17 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kila mwezi kutoka
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge a monthly waste collection fee from specified local users, and the fee must be paid by the 30th of each month to the authorized officer.
17.-(1) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kila mwezi kutoka kwa kila kaya, wamilliki wa nyumba za biashara, taasisi na kampuni zilizopo ndani ya eneo la Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. (2) Ada ya kila mwezi italipwa kila tarehe 30 ya kila mwezi ndani ya mwezi husika na italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa ambaye atatoa stakabadhi ya malipo yatakayolipwa na atajaza katika rejista ya wazalishaji taka. (3) Endapo mzalishaji wa taka atashindwa kulipia gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo, Halmashauri itamtaka kulipa deni hilo na adhabu ya asilimia hamsini ya ada anayostahili kulipa. (4) Endapo mzalishaji taka atashindwa kulipa gharama ya huduma kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3), itachukuliwa kuwa ametenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii. 7 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea)
Part
Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii.
- 18 Verify source ↗
Kila mmiliki wa jengo la makazi au la biashara atakuwa na wajibu
AI-assisted research summary: Owners of residential or commercial buildings must make sure their building has a clean, sturdy, and durable toilet that is used at all times.
18. Kila mmiliki wa jengo la makazi au la biashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba jengo lake lina choo safi, imara na madhubuti na kuhakikisha kuwa kinatumika wakati wote. - 19 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kujenga vyoo vya umma au kumruhusu
AI-assisted research summary: The council may build public toilets or allow others to build them for paid service in places it considers necessary.
19.(1) Halmashauri inaweza kujenga vyoo vya umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya umma vitakavyotoa huduma kwa malipo katika maeneo ambayo Halmashauri itaona kuwa kuna haja ya kufanya hivyo. W a j i b u wa kuwa na choo na kukitumia Vyoo vya umma - 20 Verify source ↗
(1) Mtu, kikundi au taasisi yenye lengo la kukutanisha watu kwa
AI-assisted research summary: Watu, vikundi au taasisi zinazokusanya watu kwa muda katika eneo lisilo na choo cha kudumu lazima zijenge vyoo vya muda kwa idhini na usimamizi wa Halmashauri.
20.(1) Mtu, kikundi au taasisi yenye lengo la kukutanisha watu kwa muda maalum katika eneo ambalo halina choo cha kudumu itatakiwa kujenga vyoo kwa matumizi ya wakati huo kwa idhini na usimamizi wa Halmashauri. Vyoo vya m u d a k a t i k a m k u s a - nyiko (2) Mtu, kikundi au taasisi itakayokiuka masharti ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa imetenda kosa. - 21 Verify source ↗
(1) Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba
AI-assisted research summary: If a health inspection finds a house has no toilet, a full toilet, or an unsuitable toilet, the authorized officer must give the owner 30 days’ notice to fix it.
21.-(1) Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo, choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu, Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani ya siku thelathini kwa mmiliki wa nyumba akiainisha masharti ya kurekebisha hali hiyo. Ilani ya k u j e n g a choo (2) Mmiliki wa nyumba atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1), atakuwa ametenda kosa. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Halmashauri inaweza kuamuru nyumba au jengo hilo lisitumike kwa shughuli za makazi au biashara hadi hapo hali hiyo itakapokuwa imerekebishwa. - 22 Verify source ↗
(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua
AI-assisted research summary: If the inspecting officer finds a nuisance in the area inspected, the officer must give a seven-day notice requiring removal of the nuisance. Anyone who fails to comply with the notice within the stated time commits an offence.
22.-(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa ilani ya siku saba kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote anayehusika akimtaka kuondoa kero hiyo. Ilani ya kuondoa kero (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani aliyopewa ndani ya muda ulioainishwa kwenye ilani atakuwa ametenda kosa. 8 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) Uteuzi wa Wakala Adhabu - 23 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuteua kampuni au kikundi cha jamii
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua kampuni au kikundi cha jamii kutekeleza majukumu yake, lakini si majukumu mahsusi ya Mkurugenzi, Afisa Mwidhiniwa, na Afisa Afya.
23. Halmashauri inaweza kuteua kampuni au kikundi cha jamii kutekeleza majukumu yake isipokuwa majukumu mahsusi ya Mkurugenzi, Afisa Mwidhiniwa na Afisa Afya chini ya Sheria Ndogo hii. - 24 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria
AI-assisted research summary: Anyone convicted of any offense under this by-law may be fined up to 50,000 shillings, imprisoned for up to 12 months, or both.
24. Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria Ndogo hii atahukumiwa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 25 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii shilingi 30,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu ya Jedwali la Tatu.
25. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi elfu thelathini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiyari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii. ________ JEDWALI LA KWANZA ________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 12 (2)) ________ ADA YA UKAGUZI WA AFYA ADA KWA MWAKA AINA YA BIASHARA Baa na maduka ya vinywaji (groceries) Migahawa, baba na mama lishe Nyumba za kulala wageni (guest house) na hosteli Kumbi za starehe na mikutano Maduka Gereji Majengo mengine ya biashara 1 2 3 4 5 6 7 15,000 5,000 15,000 20,000 10,000 15,000 10,000 9 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) JEDWALI LA PILI _______ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 17(1)) _______ ADA YA UZOAJI TAKA ENEO KIWANGO KWA MWEZI Nyumba za kulala wageni 1 2 Maduka 3 Mgahawa, baba,mama lishe Hoteli,baa, na maduka ya vinywaji (groceries) 4 5 Vibanda au meza za biashara 6 Wachoma chipsi, kuku na nyama 7 8 9 10 Wauza mbao au karakana za kuranda mbao 11 Ofisi ya taasisi 12 Mashine za kusaga na kukoboa Saluni Gereji Fundi seremala, samani 2000 2000 2000 2000 2000 2000 2000 2000 2000 2000 2000 2000 10 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) _______ JEDWALI LA TATU ________ (Limetungwa chini ya kifungu cha 25) ________ HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi……………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, kuwa Tarehe ………Mwezi………. Mwaka………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha………………. cha Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ya Mwaka 2020. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri, niko tayari kulipa kiasi cha shilingi elfu thelathini (30000/=) na kutekeleza wajibu wangu badala ya kushitakiwa mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI KWELI NA NINAYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe………………………………. ya Mwezi…………………. Mwaka………………… Jina…………………………………………Saini……………………………… Mbele ya:- Jina………………………………………...Cheo……………………………………. Saini………………………………………Tarehe…………………………………… 11 Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe TANGAZO LA SERIKALI NA 185 (Linaendelea) Nembo ya Hlmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanuyika mnamo tarehe 26/01/2018 mbele ya:- ERASTO N. KIWALE Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe L.S NYANSONGO M. SERENGETI Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe NAKUBALI Dodoma MH. SELEMANI S. JAFFO (MB) 8 Feburuary, 2020 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPIMBWE YA MWAKA, 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in