SHERIA NDOGO ZA (HIFADHI YA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI, 2020
This section gives the short title of the bylaw as the Moshi District Council Environmental Conservation By-laws, 2020.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO ZA (HIFADHI YA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI, 2020
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the bylaw as the Moshi District Council Environmental Conservation By-laws, 2020. These by-laws apply throughout the whole area of authority of Moshi District Council. This section defines key terms used in the bylaw. Halmashauri must set aside land, manage tree and forest protection, organize tree-planting campaigns, and require local institutions to plant, care for, and promptly report damage to trees. Mtu yeyote haruhusiwi kukata mti au sehemu ya mti bila kibali cha Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO ZA (HIFADHI YA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI, 2020
Showing 23 of 23
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii zitaitwa Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira)
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the bylaw as the Moshi District Council Environmental Conservation By-laws, 2020.
1. Sheria Ndogo hii zitaitwa Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ya Mwaka 2020. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii zitatumika katika eneo lote la Mamlaka ya
AI-assisted research summary: These by-laws apply throughout the whole area of authority of Moshi District Council.
2. Sheria Ndogo hii zitatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo:- “Afisa Mwidhiniwa” Maana yake ni Afisa wa Halmashauri aliyeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. “afisa afya” Maana yake ni Afisa wa Afya aliyeajiriwa na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. “ardhi hatari” Maana yake hi ardhi ambayo ikiendelezwa inaweza kuleta hatari katika maisha au kusababisha uharibifu wa mazingira katika ardhi hiyo au nyingine iliyo karibu. “chukizo” Maana yake ni kitu chochote kinachoweza kuleta madhara au kuhatarisha afya ya binadamu. “chakula” Maana yake ni kitu chochote kinachofaa kuliwa na binadamu. “Halmashauri” Maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. “Mamlaka” Maana yake ni mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. 1 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) Wajibu wa Halmasha- uri katika Mazingira na Vyanzo vya Maji. “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi pamoja na Afisa yoyote wa umma aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Taka hatari” Maana yake ni taka ngumu, miminika na hewa ambazo zina kiwango kibubwa cha kemikali ambazo husababisha sumu na kuathiri maisha ya binadamu pamoja na mazingira kwa ujumla wake. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhakikisha kwamba
AI-assisted research summary: Halmashauri must set aside land, manage tree and forest protection, organize tree-planting campaigns, and require local institutions to plant, care for, and promptly report damage to trees.
4.(1) Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhakikisha kwamba:- (a) inatenga eneo maalum kwa ajili ya kuotesha miche ya miti ambayo itapandwa katika maeneo mbalimbali ndani ya Halamashauri kwa utaratibu utakaopangwa; (b) Inatenga eneo au maeneo kwa ajili ya kupanda miti au kutunza miti iliyokwisha pandwa kama hifadhi ya misitu na hakuna shughuli zozote zitakazo ruhusiwa kufanyika katika eneo au maeneo hayo; (c) inasimamia utunzaji wa miti na misitu iliyomo katika mamlaka yake; (d) inasimamia kampeni za kitaifa, kimkoa na kiwilaya za kupanda miti; (e) inapanga siku moja au zaidi kwa kila mwaka kwa ajili ya kupanda miti na watu wote wanaopaswa kushiriki katika upandaji huo wa miti watatakiwa kushiriki katika zoezi hilo na watalazimika kufanya hivyo; (f) inaweka utaratibu mzuri wa kukomesha aina zote za mifugo kuzurura mitaani ili kuepusha uharibifu wa miti iliyooteshwa. (2) Kila asasi na taasisi zilizomo ndani ya Halmashauri zitahakikisha kwamba:- (a) zinapanda na kutunza miti katika maeneo yaliyo chini ya uangalizi wao. (b) zinashiriki vema katika shughuli za kupanda miti pale wanapotakiwa kufanya hivyo. 2 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) (c) zinatoa taarifa mara moja kwa mamlaka inayohusika pale inapobainika kumetokea uharibifu wa miti katika maeneo yao. Zuio la ukataji miti holela. Upandaji miti. A r d h i hatari. Makosa. - 5 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote kukata mti au sehemu ya mti
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kukata mti au sehemu ya mti bila kibali cha Halmashauri.
5.------(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote kukata mti au sehemu ya mti pasipo kupata kibali cha Halmashauri. (2) Halmashauri itatenga maeneo ya misitu ambayo miti itaruhusiwa kukatwa kwa ajili ya matumizi mbali mbali baada ya kupata kibali cha Halmashauri. - 6 Verify source ↗
Mmiliki yoyote wa ardhi atawajibika kupanda na kuhifadhi miti
AI-assisted research summary: Any land owner must plant and keep at least five trees in their area.
6. Mmiliki yoyote wa ardhi atawajibika kupanda na kuhifadhi miti isiyopungua mitano katika eneo lake. - 7 Verify source ↗
Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii maeneo ambayo ni vyanzo vya
AI-assisted research summary: This provision says water sources, riverbanks, water wells, springs, and mountain slopes are dangerous land areas.
7. Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii maeneo ambayo ni vyanzo vya maji, pembezoni mwa mito, visima vya maji, chemichemi za maji pamoja na miteremko ya milima ni maeneo ya ardhi hatari. - 8 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa kwa mtu yoyote kufanya shughuli zifuatazo katika
AI-assisted research summary: Mtu yeyote hana ruhusa kufanya shughuli zilizoorodheshwa katika maeneo ya kifungu cha 7 bila kupata kibali cha Halmashauri.
8. Itakuwa ni kosa kwa mtu yoyote kufanya shughuli zifuatazo katika maeneo yaliyoainishwa katika kifungu cha 7 hapo juu bila kupata kibali cha Halmashauri:- (a) kuwasha moto kufanya au kutokufanya jambo lolote ambalo litasababisha moto katika maeneo ya misitu; (b) kuweka, kujenga, kurekebisha, kuondoa au kubomoa aina yoyote ya jengo; (c) kuchimba au kulima maeneo ya barabara au pembezoni mwa barabara kwa madhumuni yoyote yale; (d) kuchepusha maji ya mto au mfereji kutoka katika mkondo wake. Shughuli za kilimo na hifadhi ya Ardhi. - 9 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mkulima kuzingatia kanuni za kilimo
AI-assisted research summary: Kila mkulima lazima azingatie kanuni za kilimo bora, na mtu yeyote anayefanya vitendo vilivyoorodheshwa—kama kulima bila kanuni hizo, kusindika mazao kinyume cha utaratibu, kushindwa kutoa taarifa ya milipuko bila sababu za msingi, au kubadilisha zao bila taratibu za kitaalamu—atakuwa ametenda kosa.
9.(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mkulima kuzingatia kanuni za kilimo bora ili kulinda hifadhi ya ardhi na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo na biashara. (2) Mtu yoyote atakayebainika kufanya yafuatayo atakuwa ametenda kosa:- 3 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) (a) kulima bila kuzingatia kanuni za kilimo bora; (b) kufanya usindikaji wa mazao mbalimbali kinyume na utaratibu; (c) bila sababu za msingi kushindwa kutoa taarifa ya milipuko katika Mamlaka husika kuhusu wadudu, ndege au wanyama waharibifu ikiwa ni pamoja na magonjwa kama vile; kweleakwelea, batobato kali na mnyauko; (d) kubadilisha zao bila kuzingatia taratibu za kitaalamu. - 10 Verify source ↗
(1) Ili kuzuia uharibifu wa na mmomonyoko wa ardhi itakuwa
AI-assisted research summary: Kuchimba udongo, mchanga, au kokoto kwa matumizi yoyote ni marufuku bila kibali cha Halmashauri.
10.-----(1) Ili kuzuia uharibifu wa na mmomonyoko wa ardhi itakuwa ni marufuku kwa mtu yoyote kuchimba udongo, mchanga na kokoto kwa ajili ya matumizi yoyote yale pasipo kupata kibali cha Halmashauri. (2) Mtu yoyote atakayepewa kibali cha kuchimba udongo, mchanga au kokoto ataruhusiwa kufanya shughuli iliyokusudia tu na kwa kiasi kilichoainishwa katika kibali husika. Uharibifu na mmomon- yoko wa ardhi. - 11 Verify source ↗
(1) Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii shughuli zote za mazishi
AI-assisted research summary: Mazishi yanapaswa kufanyika katika maeneo yaliyotengwa na Halmashauri au taasisi husika, baada ya kupata kibali kinachohitajika. Mazishi katika makaburi yaliyofungwa, maeneo ya makazi, au maeneo yasiyoruhusiwa kisheria ni kosa.
11. (1) Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii shughuli zote za mazishi zitafanyika katika maeneo yaliyotengwa na Halmashauri au taasisi mbalimbali baada ya kupata kibali kutoka Halmashauri ili kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli hiyo. Shughuli za mazishi. (2) Mtu yoyote atakayebainika kuhusika katika kufanya shughuli za mazishi katika makaburi yaliyofungwa au katika maeneo ya makazi au maeneo yasiyoruhusiwa kisheria atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. - 12 Verify source ↗
(1) Hakuna mtu yoyote atakayeruhusiwa kukata eneo lolote la
AI-assisted research summary: You must not cut any road area without first getting Council permission and paying the prescribed fee.
12.-----(1) Hakuna mtu yoyote atakayeruhusiwa kukata eneo lolote la barabara pasipo kwanza kupata kibali cha Halmashauri na kulipa ada iliyowekwa kisheria. (2) Mmiliki yoyote wa ardhi atakuwa ametenda kosa endapo ataruhusu ardhi anayomiliki kwa nia ya kuchimbwa ili kupata udongo, mchanga au kokoto pasipo kupata kibali cha Halmashauri. (3) Itakuwa ni ukiukwaji wa Sheria hii endapo mtu yoyote atabainika kutumia ardhi kwa matumizi ambayo ni kinyume Shughuli hatarishi kwa hifadhi ya mazingira. 4 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) na masharti ya matumizi ya kiwanja alichopewa kisheria au eneo hilo. - 4 Verify source ↗
(a) Ili kuepuka uharibifu unaoweza kujitokeza maeneo ya vituo
AI-assisted research summary: It is an offence to repair vehicles or do vehicle-related work in bus stations, on roads, or in other open public areas.
4.(a) Ili kuepuka uharibifu unaoweza kujitokeza maeneo ya vituo vya mabasi, barabarani na maeneo mengine ya wazi itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kutengeneza magari au shughuli yoyote inayohusiana na gari katika maeneo hayo; (b) Mtu yoyote atakayepatikana na hatia kwa kuvunja Sheria Ndogo hii pamoja na adhabu nyingine atakayopewa pia atalazimika kulipa fidia kutokana na uharibifu aliousababisha. - 13 Verify source ↗
Ili kuepuka madhara ambayo binadamu anaweza kupata kutokana
AI-assisted research summary: Anyone is prohibited from carrying out activities that may produce smoke or dirty air in residential areas, open areas, or on roads.
13. Ili kuepuka madhara ambayo binadamu anaweza kupata kutokana na hewa chafu ni marufuku mtu yoyote kufanya shughuli yoyote inayoweza kuzalisha moshi na hewa chafu katika maeneo ya makazi, maeneo ya wazi na barabarani. - 14 Verify source ↗
Mmiliki yeyote wa kiwanda atahakikisha kuwa
AI-assisted research summary: Mmiliki wa kiwanda lazima akague mashine mara kwa mara; mmiliki wa gari lazima ahakikishe magari yanayosafirisha vifaa vya ujenzi au taka hizo yamefunikwa; na mabomba ya moshi/hewa chafu yafungiwe vifaa maalum kupunguza madhara kwa viumbe hai na mazingira.
14. Mmiliki yeyote wa kiwanda atahakikisha kuwa:- (a) anakagua mashine zake mara kwa mara ili kuona kuwa zinafanya kazi vizuri ili kuzuia moshi na hewa chafu; (b) Mmiliki wa gari ahakikishe gari yeyote inayobeba vifaa vya ujenzi au taka itokanayo na vifaa vya ujenzi kama mchanga, kokoto na pumba za mbao inakuwa katika hali ya kufunikwa; na (c) Mabomba ya kutolea moshi na hewa chafu yanafungwa vifaa maalum ili kuepuka au kupunguza madhara kwa viumbe hai na mazingira. - 15 Verify source ↗
Shughuli zote za gereji pamoja na mashine za kusaga na za mbao
AI-assisted research summary: Shughuli za gereji na mashine za kusaga na za mbao zinapaswa kufanyika tu katika maeneo yaliyotengwa.
15. Shughuli zote za gereji pamoja na mashine za kusaga na za mbao zitafanyika tu katika maeneo yaliyotengwa kwa kazi hiyo ili kuepusha kelele na uzalishaji wa hewa chafu katika maeneo ya makazi. Udhibiti wa uchafuzi wa hewa. Wajibu wa Wamiliki wa viwanda. Shughuli za gereji na endeshaji wa mashine za kusaga. 5 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) - 16 Verify source ↗
Ni marufuku kupitisha magari na pikipiki itoayo kelele katika
AI-assisted research summary: Ni marufuku kupitisha magari na pikipiki zenye kelele katika maeneo ya utulivu.
16. Ni marufuku kupitisha magari na pikipiki itoayo kelele katika maeneo yanayohitaji utulivu, hasa katikati ya mji na katika mahospitali; ofisi na taasisi mbalimbali. Marufuku ya kelele () - 17 Verify source ↗
Kila mkazi wa Halmashauri atahakikisha kwamba nyumba yake
AI-assisted research summary: Kila mkazi wa Halmashauri lazima ahakikishe nyumba yake ina milango na madirisha ya kutosha, mfumo mzuri wa kupitisha moshi, na kuta pamoja na paa vilivyo nadhifu.
17. Kila mkazi wa Halmashauri atahakikisha kwamba nyumba yake inakuwa na:- (a) milango na madirisha ya kutosha ili kuruhusu hewa na mwanga; (b) mfumo bora wa kupitisha moshi kutoka jikoni na maeneo mengineyo yanayotoa au kuzalisha moshi; (c) Kuta na paa zilizo katika hali nadhifu. Ujenzi wa nyumba bora. - 18 Verify source ↗
(a)Itakuwa ni wajibu wa mmiliki, mpangaji wa nyumba kufagia
AI-assisted research summary: Wamiliki na wapangaji wa nyumba lazima wafagie, waondoe uchafu, na waweke safi maeneo yao; kamati na halmashauri zinaweza kusimamia usafi na kushughulikia taka.
18.(a)Itakuwa ni wajibu wa mmiliki, mpangaji wa nyumba kufagia na kuondoa uchafu au marundo ya uchafu na kuweka safi eneo lote la nyumba yake Wajibu wa kutunza usafi (b) Vichochoro vyote vitatunzwa na wenye nyumba husika na kila mwenye nyumba au mpangaji atawajibika kutunza eneo lake yaani hatua za upande wake baada ya vigingi vinavyotenganisha viwanja katika uchochoro. (c) Halmashauri au mtu yeyote aliyeteuliwa kuwa wakala atakuwa na uwezo wa kukusanya, kuhifadhi, kusafirisha na kutupa taka za majumbani na biashara kwa kutoza ada kama ilivyoainishwa katika Jedwali la kwanza. (d) Kamati za maendeleo za mitaa na kata zitakuwa na uwezo chini ya Sheria Ndogo hizi kusimamia usafi kwenye maeneo yao kwa kukomesha utupaji taka ovyo na usafishaji wa vichochoro. (e) Kamati za maendeleo za kata na mitaa zitakuwa na uwezo wa kuunda vikosi kazi vya kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kushirikiana na kamati za afya za kata au mtaa. - 19 Verify source ↗
Mtu yoyote atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa
AI-assisted research summary: Anyone who breaches these by-laws commits an offence and may be fined up to Tsh. 300,000 or imprisoned for up to 12 months, or both.
19. Mtu yoyote atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na iwapo atapatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu (Tsh. 300,000/=) au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili (12) jela au yote kwa pamoja. Adhabu. 6 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) Kufililisha kosa. - 20 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufililisha kosa iwapo mkosaji
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufililisha kosa ikiwa mkosaji akikiri kwa maandishi, ajaze fomu maalum na alipe faini isiyozidi Tsh. 200,000.
20. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufililisha kosa iwapo mkosaji atakiri kwa maandishi kwa kujaza fomu maalum itakayoambatishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipia faini kiasi kisichozidi shilingi laki mbili (Tsh. 200,000). JEDWALI LA KWANZA _______ (Limetungwa chini ya kifungu cha 18(c)) _______ SEHEMU “A” ADA ZA UZOAJI TAKA NGUMU Na.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 21 Verify source ↗
Section 21
AI-assisted research summary: This section lists different business types and the levy charged for each one, with amounts shown per week or per month.
21. AINA YA BIASHARA Maeneo ya Kaya Tea room Café Restaurant Nyumba za wageni Dispensary(normal refuse) Health centre(normal refuse) Viwanda vidogo/garage Hotel: vyumba 01 – 10 Hotel: vyumba 11 – 20 Hotel: vyumba 21 – 30 Hotel: vyumba 31 – 40 Hotel: vyumba 41 – 50 Hotel: vyumba 51 – 60 Maduka ya dawa muhimu Bucha Masoko kwa chumba(stals) Magenge Wauza vyakula mitaani Magari ya mizigo (cargo) Biashara ndogondogo Saloon/vinyozi Vituo vya mafuta Wauza mikaa Maduka ya jumla 7 TOZO 500/= kwa wiki 5000/=kwa wiki 500/= kwa wiki 1,000/= kwa wiki 5,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 7,000/= kwa mwezi 2,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 15,000/= kwa mwezi 20,000/=kwa mwezi 25,000/=kwa mwezi 30,000/= kwa mwezi 35,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 500 /=kwa wiki 500/=kwa wiki 500/=kwa wiki 15,000/= kwa mwezi 500/= kwa wiki 2,000/= kwa wiki 20,000/= kwa wiki 1,000/= kwa wiki 10,000/= kwa mwezi Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) - 55 Verify source ↗
Section 55
AI-assisted research summary: This section lists local fees and charges for various businesses and services, plus a voluntary compound-offence payment of Tsh 200,000.
55. Maduka ya vyakula (Super Markets) Maduka ya Hardware Maduka ya rejareja Maabara Furniture/carpentry Video show Battery charge Refregerate services Welding Posho mills Pombe shop Ushonaji nguo Wachoraji Soda (whole sale) Studio Spare parts Mafuta ya taa mitaani Karakana Bakeries Kuuza magazeti Computer services Godowns Stores Uuzaji samaki Mabasi express/taxi (michomoko) Night club Makanisa Miskiti Maduka makubwa ya dawa (pharmacy) Grocery Baa Waosha magari Viwanda(taka Nzito) kwa tani Hospitali vitanda 1 – 10 vitanda 11 – 20 vitanda 21 – 30 vitanda 31 – 40 8 15,000/= kwa mwezi 20,000/=kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 3,000/= kwa wiki 5,000/= kwa wiki 3,000/= kwa wiki 1,000/= kwa wiki 2,000/= kwa wiki 2,500/= kwa wiki 7,000/= kwa mwezi 3,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 1,000/= kwa wiki 10,000/= kwa mwezi 3,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 1,000/= kwa wiki 5,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 1,000/=kwa wiki 3,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 3,000/= kwa mwezi 2,000/= kwa mwezi 2,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 3,000/= kwa mwezi 3,000/= kwa mwezi 15,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 2,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa wiki 5,000/= kwa mwezi 8,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 15,000/= kwa mwezi Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) vitanda 41 – 50 vitanda 51 – 60 vitanda 61 – 70 vitanda 62 – 81 vitanda 81 – 90 vitanda 91 – 100 vitanda 101 na kuendelea 56 Magari yaliyobeba watalii kuingia mbuga za wanyama au maeneo ya utalii; (a) magari madogo (b) magari makubwa 17,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 25,000/= kwa mwezi 30,000/= kwa mwezi 35,000/= kwa mwezi 50,000/= kwa mwezi 60,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa siku 10,000/= kwa siku SEHEMU “B” ADA ZA UNYONYAJI WA MAJI TAKA S/N AINA YA BIASHARA Nyumba ya kuishi 01 Taasisi 02 Viwanda 03 Kukodi gari nje ya Wilaya 04 KIASI KWA SAFARI MOJA(Trip) 15,000.00 30,000.00 100,000.00 150,000.00 SEHEMU “C” ADA YA UKAGUZI Na. Aina Hotel i Mgahawa au baa ii Nyumba za kulala wageni iii Viwanda iv Biashara nyinginezo v Ukaguzi wa dharura vi kiasi 50,000 kwa mwaka 30,000 kwa mwaka 30,000 kwa mwaka 100,000 kwa mwaka 10,000 kwa mwaka 15,000 kwa mwaka SEHEMU “D” ADA YA KUPULIZIA DAWA ZA WADUDU (i) Ada ya kupulizia dawa ya wadudu (fumigation) ambayo itafanywa na Halmashauri Shs. 3,000/= kwa mita za mraba za eneo (per square meter) (ii) Ada ya usimamizi wa kunyunyizia dawa ya wadudu unaofanywa na watu binafsi shs. 3,000/= kwa kazi. 9 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) SEHEMU “E” ADA YA MAGARI YA KUMWAGA TAKA DAMPO kiasi 5,000 kwa tripu 10,000 kwa tripu Gari ujazo wa tani moja Gari ujazo wa tani zaidi ya moja Na. Aina a b JEDWALI LA PILI _______ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 20) _______ HATI YA KUFILILISHA KOSA Mimi ........................................................................ nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya........................................................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwamba tarehe ..........ya mwezi ................... Mwaka................. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha …….. cha Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Wilaya ya Moshi ya Mwaka 2019. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri niko tayari kulipa kiasi cha shilingi laki mbili badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe ......................ya Mwezi ................................Mwaka ….............… Jina: ...................................................... Saini: .................................................... Mbele ya:- Jina……............................................... Cheo: ................................................... Saini: ................................................... Tarehe: ............................................... 10 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi TANGAZO LA SERIKALI NA 186 (Linaendelea) Nembo ya Hlmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanuyika mnamo tarehe 26/01/2018 mbele ya:- ERASTO N. KIWALE Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe L.S NYANSONGO M. SERENGETI Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe NAKUBALI Dodoma MH. SELEMANI S. JAFFO (MB) 8 Feburuary, 2020 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO ZA (HIFADHI YA MAZINGIRA) ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI, 2020
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in